Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: Uongozi mpya wa wanawake katika kaunti za Machakos na Nakuru
Kwa mara ya kwanza nchini Kenya, kaunti mbili zimepata uongozi wa wanawake pekee katika nyadhifa za juu kwa kuchaguliwa.
Moja kwa moja
Mume wa zamani wa Britney Spears, akutwa na hatia kwa kuvamia harusi ya mwimbaji huyo
Mume wa kwanza wa nyota wa Pop Britney Spears amekutwa na hatia ya kwa kosa la kutumia nguvu na kuingia bila ruhusa baada ya kujitokeza bila kualikwa kwenye harusi ya mwimbaji huyo wa Marekani mwezi Juni. Jason Alexander, 40, alikubali mashtaka.
Jaji alimhukumu kifungo cha siku 64 - muda ambao tayari amehudumu. Alidhibitiwa na watu wa ulinzi baada ya kufunga lango laukumbi wa harusi ya Spears na mpenzi wake wa muda mrefu, Sam Asghari.
Alexander alimuoa nyota huyo wa pop ambaye alikuwa rafiki yake wa utotoni, mwaka2004. Lakini ndoa hiyo ilidumu kwa saa 55 tu na kuvunjika.
Spears, 40, na Asghari, 28, walifunga ndoa katika sherehe ya faragha nyumbani kwa mwimbaji huyo katika jimbo la Ventura Juni 9. Lakini maandalizi yalitatizwa na kuwasili kwa Alexander.
Muda mfupi kabla aliongea moja kwa moja kupitia Instagram live ambapo alisema alikuwa huko "kuvunja" harusi.
Video yake ilimwonyesha akitembea nyumbani kwa Spears akimtafuta, na kisha kwenda kwenye jumba la kifahari. Alidai Spears alikuwa amemwalika, akisema: "Yeye ni mke wangu wa kwanza, mke wangu wa pekee." Alexander alikamatwa na kupelekwa kizuizini katika eneo hilo.
Unaweza pia kusoma:
- Britney Spears atangaza kuchumbiwa na Sam Asghari
- Britney Spears asherehekea uhuru kutoka kwa mkataba wa usimamizi wa babake
- Britney Spears: Jaji atoa uamuzi wa baba yake Britney kugawana nguvu ya umiliki wa fedha za binti yake
Nani kuibuka kidedea Dabi ya Kariakoo: Simba au Yanga?
Wapenzi wa kandanda nchini Tanzania jioni ya leo watashuhudia pambano la watani wa jadi kati ya Simba na Yanga, mchezo utakaopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Mchezo huu wa dabi ni wa ngao ya jamii ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara kwa msimu wa 2022/ 2023.
Kila timu inaingia uwanjani ikiwa imefanya usajili bora wa vikosi vyao na wote wakiwa wametoka kwenye maandalizi bora ya kabla ya kuanza kwa msimu mpya.
Yanga wanaingia katika mchezo huu wakiwa na nyota wao kadhaa wa msimu uliopita akiwemo mfungaji wa bao pakee katika mchezo wa ngao ya msimu ulipita Fiston Mayele, Feisal Salum, Khalid Aucho na sajili mpya za kina Stephane Aziz Ki, Bernad Morrison na wengine wengi.
Kwa upande wa Simba wao watacheza mchezo huu wakiwa na Kocha mpya anayekutana na Yanga kwa mara ya kwanza ambaye ni kocha Zoran Manojlović lakini pia Wapo nyota wa msimu uliopita kama Pape Ousmane Sakho beki kisiki Henoc Inonga Baka, Shomary Kapombe na wengine wengi.
Unaweza pia kusoma:
- Yanga yapaa kileleni ligi ya Tanzania
- Simba na Yanga: Nani kuibuka mbabe mchezo wa watani wa jadi leo?
Matokeo ya Uchaguzi Kenya 2022: Aliyekuwa Kamishna wa IEBC atuma ujumbe wa mshikamano kwa familia ya msimamizi aliyetoweka
Aliyekuwa Kamishna Huru wa Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Roselyn Akombe ametuma ujumbe wa mshikamano kwa familia ya Msimamizi wa Uchaguzi wa Embakasi Mashariki ambaye aliripotiwa kutoweka Ijumaa usiku.
Akombe alikimbilia New York na kujiuzulu katika marudio ya uchaguzi wa marudio ya urais wa 2017, akisema alihisi hayuko salama, na kwamba hana uwezo wa kufanya uchaguzi wa kuaminika.
Unaweza kusoma pia:
- Je kamishna wa IEBC Roselyn Akombe Kwamboka ni nani?
- Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: William Ruto, Raila Odinga wachuana vikali
- Matokeo ya Uchaguzi Kenya 2022: Vigogo wa Raila Odinga na Uhuru Kenyatta waliolambishwa sakafu
Matokeo ya uchaguzi Mkuu Kenya 2022: Shule zote nchini Kenya sasa zitafunguliwa Alhamisi wiki ijayo
Shule zote nchini Kenya sasa zitafunguliwa Alhamisi na wala sio Jumatatu kama ilivyotangazwa awali na serikali.
Waziri wa Elimu George Magoha alisema amelazimika kufanya mabadiliko hayo kutokana na shughuli inayoendelea nchini humo yakujumlisha kura na hatimaye kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa urais.
"Kwa hivyo nawasilisha uamuzi wa serikali ya Kenya kuhusu kuahirishwa kwa kufunguliwa tena kwa shule na taasisi zote za elimu ya msingi kutoka Jumatatu Agosti 15 hadi Alhamisi, Agosti 18," alisema katika taarifa yake iliyotumwa kwa vyombo vya habari muda mchache uliopita.
"Niliagiza kufungwa mapema kwa Vyuo vyote vya Elimu ya Msingi ili kutoa nafasi ya maandalizi na uendeshaji wa kutosha wa Uchaguzi Mkuu. Tulieleza kuwa tutafungua tena tarehe 11 Agosti 2022 lakini hilo haliwezekani kwa sasa," alisema.Magoha alisema wizara imefahamishwa kuwa huenda mchakato wa kujumlisha kura bado utakuwa unaendelea kufikia tarehe iliyotajwa.
Waziri huyo aliomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza kwa wazazi na kusema mawasiliano yake yanafuta mawasiliano yoyote yaliyofanywa mapema kuhusu shule zaelimu ya msingi nchini Kenya.
Shule kawaida hutumiwa kama vituo vya kupigia kura na kujumlisha kila mwaka wa uchaguzi.
Notisi ya gazeti la serikali ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC ilionyesha kuwa takribanshule 250 zitatumika kama vituo vya kuhesabia kura.
Matokeo ya Uchaguzi Kenya 2022: Matokeo kutoka maeneo 49 kati ya 292 yamepokewa
Matokeo kutoka maeneo 49 kati ya 292 - ikiwemo ughaibuni na magereza - yamepokewa, kuthibitishwa na kutangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).
Maafisa wa Uchaguzi 291 wa maeneo bunge wamefika katika kituo cha kitaifa cha kuhesabu kura Bomas mjini Nairobi ambapo wamewasilisha nakala halisi za Fomu 34A kwa msimamizi wa uchaguzi Wafula Chebukati.
IEBC imeripoti kuwa mmoja wa maafisa wake wa uchaguzi ametoweka.
Imelazimu naibu wa afisa huyo kutoka Embakasi Mashariki jijini Nairobi aliyepotea, kupokea jukumu.
Kuna maeneo 292 nchini Kenya yanayojumuisha diapora (Wakenya wanaoishi nje ya nchi) na magereza.
IEBC itatangaza matokeo ya urais baada tu ya kupokea na kuthibitisha matokeo na nakala halisi za fomu 34 A kutoka vituo vyote 46,229 vilivyowekwa kwenye gazeti rasmi la serikali.
Matokeo rasmi yanapaswa kutangazwa ndani ya siku saba baada ya siku ya kupiga kura.
Unaweza pia kusoma:
- Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: William Ruto, Raila Odinga wachuana vikali
- Matokeo ya Uchaguzi Kenya 2022: Vigogo wa Raila Odinga na Uhuru Kenyatta waliolambishwa sakafu
Matokeo ya Uchaguzi Kenya 2022: Viongozi waliothibitishwa kutoka Muungano wa Azimio La Umoja wakutana
Viongozi wapya waliothibitishwa ushindikatika uchaguzi mkuu Kenya kutoka Muungano wa Azimio La Umoja – wa mgombea urais Raila Odinga -wamekutana hii leo katika mji mkuu Nairobi.
Viongozi hao walionekana kumiminika katika jumba la mikutano KICC Nairobi Jumamosi mchana katika hafla ya kutambuana na kutoa pongezi kwa waliotangazwa ushindi katika uchaguzi mkuu nchini.
Ni mara ya kwanza mkutano wa Azimio unafanyika tangu wakenya kupiga kura Jumanne.
Baadhi ya viongozi katika hafla hiyo wamekuwa wakizungumza kwa matumaini ushindi waAzimio cha mgombea urais Raila Odinga licha ya kukiri pia kushindwa kwa baadhi ya viongozi wakuu waliokuweko.
Akihotubia mkusanyiko huo, mgombea mwenza wa Odinga, Martha Karuaameeleza kwamba ni lazima walinde utaratibu unaoendelea katika ukumbi wa Bomas ambao ndio kituo kikuu cha kuhesabia kuranchini, kuhakikisha “hauingiliwi na kwamba fomu sahihi zinatoa matokeo…’
Ameeleza matumaini yake kwamba muungano huo utakuwa na uwingi bungeni kwa namna matokeo yanavyoendelea kutitirika.
Kadhalika Martha amekiri kuwa wapinzani wao wanaelekea kuwa na ushawishi katika bunge la Seneti.
Unaweza pia kusoma:
- Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: William Ruto, Raila Odinga wachuana vikali
- Matokeo ya Uchaguzi Kenya 2022: Vigogo wa Raila Odinga na Uhuru Kenyatta waliolambishwa sakafu
Takribani Polisi watano wauawa Mashariki ya DR Congo
Kwa mujibu wa wakazi wa Butembo, polisi walipelekwa majira ya asubuhi ya leo kurudisha amani na utulivu katika viunga vya mji ambapo baadhi ya waandamanaji wenye hasira waliwageukia polisi.
Mapema leo msemaji wa jeshi aliiambia BBC kuwa idadi ya waliouawani maafisa 5, magari yalichomwa moto na kwamba silaha 8 zilipatikana kutoka kwa washambuliaji.
Wapiganaji wa eneo hilo wanaojulikana kama Mai Mai Baraka wanalaumiwa kwa tukio la leo.
Tukio la leo linajiri siku chache baada ya Allied Democratic Forces, kundi katili lililojihami na linalofungamana na kundi la Jihadi la Islamic State, kushambulia gereza kuu la Kakwangura huko Butembo.
Kundi la IS lilidai kuhusika na tukio hilo la gerezani likisema lilifanywa kuwaachilia huru makumi ya wafungwa Waislamu.
Waasi wa ADF walitoka Uganda, lakini kwa miaka 27 iliyopita mashambulizi yao mengi yamekuwa yakilenga raia mashariki mwa DRC.
Vyombo vya usalama vya eneo hilo vinasema kuwa ADF walisaidiwa na makundi ya wenyejiyenye silaha walipovamia gereza hilo.
Roger Moya, naibu meya wa Butembo alisema takriban watu 250 waliotoroka wamekamatwa tena na vikosi vya usalama hadi kufikia sasa. Lakini zaidi yawafungwa 800 waliotoroka wakati wa uvunjaji wa gereza bado wako huru.
Unaweza pia kusoma:
- ADF: Lifahamu kundi la waasi kutoka Uganda linaloshirikiana na Islamic State
- Majeshi ya Uganda, DRC yanasema kambi za ADF ziliharibiwa
Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022:Uongozi mpya wa wanawake katika kaunti mbali mbali
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Grace Kuria
- Nafasi, BBC News
Kwa mara ya kwanza nchini Kenya, kaunti mbili zimepata uongozi wa wanawake pekee katika nyadhifa za juu kwa kuchaguliwa.
Wavinya Ndeti ametangazwa rasmi muda mfupi uliopita kama gavana mteule wa Machakos na Tume ya uchaguzi na Mipaka (IEBC) katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 uliofanyika Jumanne wiki hii.
Agnes Kavindu Muthama pia ametangazwa kama seneta mteule, baada ya kubakia na kiti chake, huku Joyce Kamene Kasimbi akiwa mbuge mteule wa kiti cha uwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Machakos.
Katika Kaunti ya Nakuru county, Susan Kihika Ijuamaa alitangazwa na IEBCkama gavana mteule
Tabitha Karanja pia amatangazwa kama seneta mteule wa Nakuru, huku Liza Chelule akiwa mbunge mteule wa kiti cha wawakilishi wanawake.
Wanawake wamekuwa wakipongezwa kwa udhubutu wao wa kuwania viti vya juu katika uchaguzi wa mwaka huu.
Hadi sasa, Anne Waiguru ametangazwa kuwa gavana wa Kaunti ya Kirinyaga , Gladys Wanga Gavana wa Kaunti ya Homabay , Kawira Mwangaza wa Kaunti ya Meru na Fatuma Achani, Kaunti ya Kwale
Wanawake zaidi wanaendelea kujinyakulia viti katika uchaguzi kadri matokeo yanavyoendelea kutangazwa.
Naibu rais Wiliam Ruto ametuma ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter akiwapongeza wanawake kwa kuchaguliwa kuchukua nyadhifa za juu za uongozi:
Unaweza pia kusoma:
- Matokeo ya Uchaguzi Kenya 2022: Wanawake waliong’ara katika uchaguzi
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mubashara ya leo Jumamosi tarehe 13.08.2022