Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Matokeo ya Uchaguzi Kenya 2022: Kamati ya makabidhiano Kenya yakutana

Bw Kinyua alisema kuwa jukumu la kamati hiyo litaanza mara tu baada ya mshindi wa urais kutangazwa.

Moja kwa moja

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo, tukutane tena hapo kesho majaaliwa

  2. Kundi la Islamic State (IS) limedai kuhusika na shambulio la gereza mashariki mwa DRC

    Kundi la Islamic State (IS) limedai kuhusika na shambulio la Jumanne katika gereza mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambapo mamia ya wafungwa walitoroka.

    Zaidi ya wafungwa 800 walitoroka kutoka gereza la Kakwanguru kufuatia shambulio hilo. Jeshi la Congo limesema kwamba limefanikiwa kuwakamata upya zaidi ya wafungwa 100 kufikia sasa.

    IS limedai kupitia ujumbe kwenye mtandao wa Telegram kuhusika na uvamizi huo siku ya Jumanne katika gereza Kakwanguru la Butembo.

    Zaidi ya wafungwa 800 walitoroka kutoka gereza la.

    Jeshi mjini Butembo linasema limefanikiwa kuwakamata upya wafungwa wapatao 250.

    Hapo jana jeshi liliwaonyesha wafungwa 166 mbele ya waandishi Habari. Hii ikiwa ni idadi ya ziada baada ya kukamatwa wafungwa wengine 86 waliotoroka kwa usaidizi wa raia.

    Kapteni Anthony Mwalushayi ameiambia BBC kwamba washambuliaji walikadiriwa kuwa 80 na waliwashinda nguvu maafisa 15 waliokuwa zamu gerezani mwendo wa saa nane usiku Jumanne.

  3. Matokeo ya Uchaguzi Kenya 2022: Wakazi wa Kijiji cha Naibu wa rais William Ruto wafurika barabara kungoja matokeo

    Wakazi wa kijiji cha Kosachei katika kaunti ya Uasin Gishu anakotoka naibu wa rais William Ruto na mgombeaji wa urais kwa tiketi ya chama cha UDA wanasubiri matokeo ya uchaguzi kwa hamuna kulalamikia muda mrefu ambao wamengoja kuyapata kutoka kwa Tume huru ya uchaguzi na Mipaka IEBC .

    Wameitaka IEBC kuchukua kuongeza juhudi za kuyatoa matokeo hayo kwa haraka ili waendelee na shughuli zao za kawaida .

    Wengi wameniambia kuwa wana matumaini kwamba Rutoataibuka na endapo hatoshinda basi basi wako tayari kumuunga mkono mshindi .

    Kumekuwa na zogo katika kituo cha kitaifa cha kujumlisha kura jijini Nairobi kuhusu matokeo yanayoletwa na wasimamizi wa vituop vya kupigia kura hatua ambayo imelaumiwa pia kwa njia ya kujikokota ya kuwasilisha matokeo ya mwisho .

    Unaweza pia kusoma:

    • Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: William Ruto, Raila Odinga wachuana vikali
    • Matokeo ya Uchaguzi Kenya 2022: Vigogo wa Raila Odinga na Uhuru Kenyatta waliolambishwa sakafu
  4. Matokeo ya Uchaguzi Kenya 2022: Kamati ya makabidhiano Kenya yakutana

    Serikali inayoondoka madarakani imeanza maandalizi ya kuikabidhi madaraka serikali ijayo, huku Tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC) ikiendelea na mchakato wa kujumlisha kura .

    Joseph Kinyua, Mkuu wa huduma za umma aliongoza mkutano wa kamati inayosimamia makabidhiano ya mamlaka mapema Ijumaa akisema kuwa wako tayari kufanikisha makabidhiano ya mamlaka kwa mujibu wa sheria.

    Bw Kinyua alikuwa akizungumza katika jengo la Harambee House akiambatana na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo ambao ni pamoja na Mwanasheria mkuu Paul Kihara, Mkuu wa majeshi Robert Kibochi, Inspekta Mkuu wa Polisi Hilary Mutyambai, Katibu wa kudumu wa wizara ya mambo ya ndani Karanja Kibicho na Katibu wa kudumu wa wizara ya mambo ya nje Macharia Kamau.

    Bw Kinyua alisema kuwa jukumu la kamati hiyo litaanza mara tu baada ya mshindi wa urais kutangazwa.

    Unaweza pia kusoma:

    • Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: William Ruto, Raila Odinga wachuana vikali
    • Matokeo ya Uchaguzi Kenya 2022: Vigogo wa Raila Odinga na Uhuru Kenyatta waliolambishwa sakafu
  5. Johnson & Johnson kutumia wanga wa mahindi badala ya ulanga kutengeneza poda

    Johnson & Johnson (J&J) itaacha kutengeneza na kuuza poda yake ya watoto iliyotengenezwa kwa ulanga kote duniani mwaka ujao.

    Taarifa hii inakuja zaidi ya miaka miwili baada ya kampuni hiyo kubwa ya huduma ya afya kusitisha mauzo ya bidhaa zake nchini Marekani.

    J&J inakabiliwa na maelfu ya mashitaka kutoka kwa wanawake waliodai kuwa poda ya ulanga ilikuwa na madini ya asbestona iliwasababisha wapate saratani ya mvuko wa mayai ya uzazi. Lakini kampuni hiyo ilirejelea ilisisitiza tena kwamba miongo ya utafiti wake inaonyesha kuwa bidhaa ni salama kutumiwa.

    "Kama sehemu ya tathmini ya maeneo mengine ya dunia, tumefanya uamuzi wa kibiashara wa wa kubadilisha poda ya watoto iliyokuwa ikitengenezwa kwa kutumia ulanga na kuwa ya wanga wa mahindi ,"ilisema katika taarifa yake.

    Kampuni hiyo iliongeza kuwa poda ya watoto iliyotengenezwa kwa kutumia wanga wa mahindi tayari iliuzwa katika nchi mbali mbali duniani.

  6. Mbunge mteule aliyeshutumiwa kwa mauaji ajisalimisha Kenya

    Mbunge mteule nchini Kenya, Dismas Barasa, amejisalimisha kwa polisi baada ya kutafutwa kwa siku tatu baada ya kufyatua risasi na kumuua msaidizi wa mpinzani.

    Polisi wanamchukulia Bw Barasa kama mshukiwa wa kisa kilichotokea katika kituo cha kupigia kura siku ya kupiga kura.

    Kwa sasa anasaidia mamlaka katika uchunguzi, polisi wamesema.

    Eneo bunge la Bw Barasa la Kimilili liko magharibi mwa Kenya karibu na mpaka na Uganda.

    Wakili wake alituma maombi ya dhamana siku ya Alhamisi akisubiri kukamatwa kwake.

  7. Uchaguzi Kenya 2022: Wakenya wasubiri matokeo kwa siku ya tatu

      • Author, Richard Kagoe
      • Nafasi, BBC Africa, Nairobi

    Wakenya bado wanasubiri matokeo ya uchaguzi wa urais baada upigaji kura siku ya Jumanne ambao ulikuwa na idadi ndogo ya waliojitokeza kupiga kura.

    Tume ya uchaguzi inathibitisha fomu za matokeo katika kituo cha kitaifa cha kuhesabia kura katika mji mkuu, Nairobi Kituo hiki ni msururu wa shughuli kama mawakala kutoka kote nchini kuwasilisha kwa mkono karatasi halisi ya matokeo ili kuthibitishwa Matokeo ya muda yanaonesha ushindani mkali kati ya vinara William Ruto na Raila Odinga.

    Waangalizi wameipongeza tume ya uchaguzi kwa zoezi zuri la upigaji kura. Tume ya uchaguzi ina siku saba baada ya siku ya uchaguzi kutangaza matokeo.

    • Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: William Ruto, Raila Odinga wachuana vikali
    • Matokeo ya Uchaguzi Kenya 2022: Vigogo wa Raila Odinga na Uhuru Kenyatta waliolambishwa sakafu
  8. Waangalizi wa EAC walivyoridhishwa na mchakato wa kura Kenya

    Ujumbe wa Waangalizi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) nchini Kenya umeipongeza Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kwa kutekeleza zoezi la upigaji kura lililokamilika Jumanne.

    Katika hotuba kwa wanahabari Alhamisi jijini Nairobi, ujumbe wa waangalizi ulisema kwamba polisi pia walikuwa katika nafasi ya kuhakikisha wapiga kura wanalindwa wakati wa zoezi hilo katika vituo vya kupigia kura.

    Kiongozi wa ujumbe huo Jakaya Kikwete (Rais wa zamani wa Tanzania) alisema kuwa polisi hawakuingilia zoezi la upigaji kura.

    ‘”Ujumbe unaipongeza IEBC kwa kutumia vyema teknolojia katika usajili wa wapigakura, kuwatambua wapigakura na uwasilishaji wa matokeo,” Bw Kikwete alisema.

    Alisema teknolojia hiyo imeongeza ufanisi na kuongeza uwazi nchini, tofauti na chaguzi zilizopita.

    Hata hivyo, Bw Kikwetre alisema kulikuwa na matukio machache yanayohusiana na utambulisho wa wapigakura na kitengo cha KIEMS, akiomba tume kuzingatia masuala hayo na kutatua siku zijazo.

    "Tunapendekeza kwamba matatizo yanayohusiana na vifaa vya KIEMS yatambuliwe na hatua muhimu za kurekebisha zichukuliwe kwa utendakazi bora katika siku zijazo."

    • Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: William Ruto, Raila Odinga wachuana vikali
    • Matokeo ya Uchaguzi Kenya 2022: Kwa nini hesabu inachukua muda mrefu
  9. Hatimaye Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Kenya yaanza kutiririsha matokeo ya urais

    Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) hatimaye ilianza kutiririsha matokeo ya urais yaliyothibitishwa mwishoni mwa siku Alhamisi kwa ajili ya kutangaza matokeo ya mwisho.

    Uchaguzi huu umekuwa tofauti na nyakati zilizopita kwasababu Tume ya IEBC, haijatangaza matokeo moja kwa moja kadiri wanavoyapokea.

    Hatua hii imeonekana kama njia ya kujaribu kwendana na uamuzi wa Mahakama ya Juu Zaidi wa mwaka 2017, ikiwa ni pamoja na kutojumlisha papo hapo kura zote na kutoa matokea moja kwa moja kwa umma, badala yake jukumu hilo limeachwa mikononi mwa vyombo vya Habari.

    Pia kuna hatua zingine zilizofanyiwa maboresho kama vile kifungu cha 138 (3)(c) cha katiba.

    Kinachofanyika, Tume hiyo inatumia fomu za 34A zenye matokeo ya urais kutoka kwenye vituo vya kupiga kura 46,229 kote nchini humo.

    Ilivyokuwa wakati wa miaka ya nyuma ni kwamba fomu 34A zilikuwa ndio matokeo ya mwisho na tume hiyo haikuwa na nguvu ya chochote baada ya hapo.

    Aidha, fomu 34A zilizoidhinishwa zinapatikana kwenye tovuti ya Tume ya IEBC na hapo wananchi wanaweza kujijumlishia wenyewe matokeo yao.

    Hatua hii huenda ikasababisha wasiwasi miongoni mwa wananchi wanaofuatilia kwa karibu kujua viongozi wao wajao hasa kutokana na mwendo wa pole wa zoezi hilo kwa jumla lakini mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati, amesihi wananchi kutokuwa na hofu na matokeo tofauti yanayotolewa na vyombo vya Habari.

    Hata hivyo, Bwana Chebukati ameonyesha kuwa maafisa wa Tume ya IEBC wenye jukumu la kuwasilisha fomu 34A, wanatarajiwa kuanza kuziwasilisha ana kwa ana kuanzia hii leo asubuhi.

    “Tunaendesha uchaguzi huu kwa kufuata sheria. Maafisa husika wa IEBC watakapowasilisha fomu 34A na 34B, tutaanza mchakato wa uthibitishaji na kuwapa taarifa Wakenya kuhusu kile kinachoendelea,” alisema katika moja ya mikutano yake.

    Soma zaidi:

  10. Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Kenya ataka wananchi wasiwe na wasiwasi juu ya tofauti za kura za urais kutoka vyombo tofauti vya habari

    Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati ametuliza umma huku akiwataka Wakenya kutokuwa na wasiwasi kuhusu tofauti za kura za urais kutoka vyombo tofauti vya habari.

    Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati ametuliza umma na kuwataka Wakenya kutokuwa na wasiwasi kuhusu tofauti za kura za urais kutoka vyombo tofauti vya habari.

    ‘’Vyombo vya habari vinajumlisha matokeo kwa madhumuni ya kuripoti. Kusiwe na wasiwasi kuhusu tofauti hizo. Chanzo cha matokeo hayo ni sawa...kutoka kwa tovuti yetu ya umma,’’ chabukati alisema.

    Pia aliwaonya wagombea dhidi ya kutangaza ushindi kwa kutumia matokeo yao ambayo hayajathibitishwa, akibainisha kuwa hiyo ni kazi ya IEBC.

    ‘’Pia tuliruhusu watahiniwa kufanya hesabu zao wenyewe. Hii ni kwa matumizi yao wenyewe na kusaidia mawakala wao katika kuhakiki matokeo.’’

    Soma zaidi:

  11. Mawakala wa William Ruto wazozana na maafisa wa IEBC

    Ghadhabu zilipanda katika kituo cha kitaifa cha kuhesabia kura cha Bomas of Kenya usiku wa Alhamisi wakati tume ya uchaguzi ilipoanza kuhakiki matokeo ya uchaguzi wa urais.

    Maafisa wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) walitatizika kudumisha utulivu baada ya Chama cha United Democratic Alliance (UDA) kudai kuwa fomu 34A ambazo hazijaidhinishwa zilikuwa zikiingizwa kinyemela katika ukumbi huo.

    Mawakala wa mgombea urais William Ruto walizozana na maafisa wa uchaguzi kuhusu fomu zinazotiliwa shaka, na kuzua taharuki ambayo ilifanya makamishna wa IEBC kuingilia kati. Katibu Mkuu wa UDA, Veronica Maina, walitishia kujiondoa katika mchakato wa kupokea na kukusanya fomu 34A na 34B.

    Bi Maina aliwashirikisha maafisa wa bodi ya kura kwenye dawati la kuhakiki ubora kabla ya mawakala wengine wa UDA kujiunga nao kwa dakika 10.

    Mawakala wa UDA pia walikuwa wamelalamikia idadi ya watu walioruhusiwa kwenye madawati manne yaliyowekwa kwa ajili ya uhakiki na uchukuaji fomu.

    Mkuu wa masuala ya ushirika wa IEBC Tabitha Mutemi baadaye aliamuru maajenti ambao hawakuidhinishwa katika ukumbi huo kuondoka.

    Huku hayo yakijiri tume ya IEBC imesema kuwa wameanzisha mchakato wa uhakiki wa ngazi nne, kuashiria kuwa huenda tangazo la matokeo ya mwisho likafanywa wikendi.

    Kamishena wa tume hiyo Prof Abdi Guliye alisema tume imeunda madawati manne kwa ajili ya uhakiki wa matokeo kutoka katika majimbo 291 ya uchaguzi yakiwemo magereza na kure zilizopigwa nje ya nchi.

  12. Karibu katika matangazo ya moja kwa moja leo Ijumaa 12.08.2022