Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Onyo la Marekani kwa Waafrika: msinunue kitu chochote kutoka Urusi isipokuwa nafaka na mbolea
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield alifanya ziara katika nchi za Afrika, na miongoni mwa mambo mengine, amewaonya Waafrika wasinunue chochote kutoka Urusi isipokuwa nafaka na mbolea, akiwatishia vikwazo iwapo watafanya hivyo.
Moja kwa moja
Urusi na Ukraine-Zaporizhzhia: Roketi za Urusi zaharibu sehemu ya kiwanda cha nyuklia, Ukraine yasema
Shirika la nyuklia la Ukraine linasema kuwa roketi za Urusi zimeharibu sehemu yam tambo kubwa wa nyuklia unaodhibitiwa na Urusi, lakini mionzi ya nyuklia haikuvuja.
Enerhoatom limesema kuwa kitengo cha nitrojeni-oksijeni na mtambo wa nishati ya juu vimeharibiwakatika kiwanda cha Zaporizhzhia - ambacho ni kiwanda kikubwa zaidi cha Ulaya- kilichopo kusini mwa Ukraine.Maafisa wa eneo hilo walioteuliwa na Urusi waliilaumu Ukraine kwa kufanya mashambulio awali.
Ukraine pia imevishutumu vikosi vya Urusi kwa kufyatua makombora katika maeneo ya raia kutoka kwenye eneo hilo kwa kutumia "mkakati wa ugaidi".
"Kila siku tukiamka tunaona wamepiga maeneo ya makazi ya watu tu ," mkazi wa eneo hilo ambaye ni mfanyabiashara aliiambia BBC.
Urusi na Ukraine: Mengi zaidi:
- MOJA KWA MOJA:Biden amuonya Putin: ''Madikteta watagharamika
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Uchaguzi Kenya 2022 kwa picha: siku ya mwisho ya kampeni za uchaguzi Kenya
Ni siku ya mwisho ya kampeni za uchaguzi wa urais nchini Kenya. Wagombea wakuu wa urais Raila Odinga, na Naibu Rais William Ruto watafanya mikutano yao ya mwisho ya hadhara ya kampeni katika maeneo tofauti ya jiji la Nairobi kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika Jumanne wiki ijayo. Hizi ni baadhi ya picha kutoka kwenye kampeni za Urais za Raila Amollo Odinga na William Ruto:
Kampeni za mwisho za uchaguzi mkuu zimekuwa zikiendelea pia katika maeneo mengine ya nchi katika siku ya kwanza ya kampeni ikiwa ni pamoja na Pwani ya Kenya na Rift Valley
Uchaguzi Kenya 2022: Diamond Platnumz atumbuiza kampeni za mwisho za Azimio La Umoja
Muungano wa Azimio la Umoja – umemualika mwanamuziki maarufu wa Tanzania Diamond Platnumz kutumbuiza katika mkutano wake wa mwisho wa kampeni katika uwanja wamichezo wa Kasarani Jumamosi, tarehe August 6, 2022.
Raila Odinga-ameongoza kampeni yake ya mwisho katika uwanja wa Kasarani huku Naibu Rais William Ruto akifanya kampeni zake katika eneo tofauti mjini Nairobi wakati kampeni zikifikia ukingoni Jumamosi hii.
Mikutano ya kampeni ya Jumamosi inakamilisha kampeni za kisiasa za wagombea wote wa uchaguzi kulingana na sheria na muda wa mwisho na sheria za Tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC)
Kabla ya kuelekea Nairobi Diamond ambaye alikuwa ameambatana na mwanaye Tiffa alituma ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram:
Uchaguzi Mkuu Kenya 2022: Wagombea wa uchaguzi wadhatiti kusaka kura katika siku ya mwisho ya kampeni
Ni siku ya mwishi ya kampeni za uchaguzi wa urais nchini Kenya. Wagombea wakuu wa urais Raila Odinga, na Naibu Rais William Ruto watafanya mikutano yao ya mwisho ya hadhara ya kampeni katika maeneo tofauti ya jiji la Nairobi kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika Jumanne wiki ijayo.
Uchaguzi huu unatarajiwa kuwa wa mchuoano mkali kuwahi kushuhudiwa kwa miaka nchini Kenya.
Wagombea wote wamewatolea witi wafuasi wao kujitokeza kwa wingikwenye mikutano yao ya mwisho ya kampeni, kabla ya uchaguzi wa Jumanne. Kiongozi wa zamani wa upinzani Raila Odinga, ambaye anaungwa mkono na Rais Uhuru Kenyatta, anawania kiti cha urais kwa mara ya tano, huku ikiwa ni mara ya kwanza kwa mpinzani wake William Ruto, ambaye alichaguliwa pamoja na Rais Uhuru Kenyatta, lakini kwa sasa wametengana.
Mitaa ya mji wa Nairobi, ambapo kampeni zote za mwisho zitafanyika imejaa mabango ya wagombea wakuu hao wawili n ani jambo la kawaida kuona mara kwa mara magari yenye vipaza sauti vikubwa yakisikika kupiga miziki au nyimbo za kampeni.
Hadi sasakwa ujumla kampeni zimekuwa za amani, licha ya kuwepo kwa malumbano ya mara kwa mara ya wagombea wakuuna pia Rais Uhuru Kenyatta.
Unaweza pia kusoma:
- Uchaguzi Kenya 2022: Je wanamuziki wana ushawishi gani katika siasa za Kenya
- Uchaguzi Kenya 2022:Nani yuko kwenye kinyang'anyiro cha kuiongoza Kenya ?
- Uchaguzi Kenya 2022:Mfahamu mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya
Israel-Gaza: Israel yawakamata wanamgambo 19 baada ya mashambulio ya Gaza
Israel inasema imewakamata wajumbe 19 wa kikundi cha Jihadi cha Wapalestina katika uvamizi iliyofanywa katika kote katika eneo la West Bank , baada ya kufanya mashambulizi dhidi ya maeneo yaliyolengwa kwenye Ukanda wa Gaza.
Watu kumi wameuawa kastika shambulio la anga, mkiwemo mtoto na kiongozi waPIJ Tayseer Jabari.
Israel inasema kwamba shambulio hilo lilifuatia "tisho la moja kwa moja" kutoka kwa kikundi hicho.
Roketi kadhaa zilifyatuliwa kutoka Gaza kuelekea Israel Usiku, nyingi kati yake zilizuiwa, limesema jeshi la Israel.
Ghasia za hivi karibuni ni mashambulio mabaya zaidi baina ya Israeli na Gaza kuwahi kushuhudiwa kwa kipindi cha mwaka mzima .
Vita vya siku 11 mwezi Mei, 2021 vilisababisha vifo vya Wapalestina zaidi ya 200 na Waisraeli wapatao 12 kabla ya kufikia makubaliano ya usitishaji wa mapigano.
Unaweza pia kusoma:
- Israel-Gaza: Raia wa Palestina na wanamgambo wauawa huku mapigano yakizuka
- Israel-Gaza:Mashambulizi ya angani yatekelezwa na Israel huko Gaza
Onyo la Marekani kwa Afrika: msinunue kitu chochote kutoka Urusi isipokuwa nafaka na mbolea
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield alifanya ziara katika nchi za Afrika, na miongoni mwa mambo mengine, amewaonya Waafrika wasinunue chochote kutoka Urusi isipokuwa nafaka na mbolea, akiwatishia vikwazo iwapo watafanya hivyo.
“Urusi ina mtazamo kwamba vikwazo dhid ya bidhaa za chakula na na kilimo vimepelekea ongezeko la bei ambalo nchi zinakabiliana nalo. Ninataka kusema kwamba hatuna vikwazo kwa vidhaa zozote za kilimo kutoka Urusi. Urusi inaweza kuuza nje bidhaa za kilimo, nan chi nyingine zinaweza kuzinunua, ikiwa ni pamoja na mbolea na ngano ," alisema katika mkutano na waandishi wa habari mjini Kampala, Uganda
“Kuhusu vikwazo dhidi ya Urusi,” Linda Thomas-Greenfield aliendelea kusema kuwa, “kwa mfano,kuhusu mafuta, iwapo nchi itaamua kushirikiana na Urusi, katika maeneo ambayo yamewekewa vikwazo, basi zinatakuwa zimekiuka vikwazo, na katika baadhi ya matukio pia itakuwa imekiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa. Na tunaonya nchi zisikiuke vikwazo ."
Nchi nyingi za Afrika zinapendelea kutoegemea upande wowote katika vita vya Ukraine na Urusi. Sababu mara nyingine huelezewa kuwa ni kutokana uhusiano uliopo baina ya Afrika na chi za Magharibi ambazo nyingi ni wakoloni wa zamani wa mataifa ya Afrika, na wakati huo huo wasomiwengi wa Afrika waliosomea Urusi ambao wasingependa kujiuhusisha na vita dhidi.Wakati huo, baadhi ya nchi za Afrika ni wanunuzi wakuu wa bidhaa kutoka Ukraine ambazo kwa sasa zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.
Urusi na Ukraine: Mengi zaidi:
- MOJA KWA MOJA:Biden amuonya Putin: ''Madikteta watagharamika
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mubashara ya leo, tarehe 06.08.2022