Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Uhuru: Unga wa mahindi utauzwa kwa Ksh.100

Katika hotuba ya kitaifa kwa nchi, Uhuru alisema kuwa pakiti ya kilo 2 ya unga wa mahindi sasa itauzwa kwa Sh100 kote nchini.

Moja kwa moja

  1. Na kufikia hapo ndio tunakamilisha matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo, majaaliwa ya Mungu tukutane tena hapo kesho.

  2. Zaidi ya 100 wafariki katika mapigano ya kikabila Sudan - mamlaka

    Mamlaka katika jimbo la Blue Nile kusini-mashariki mwa Sudan wanasema watu 105 sasa wamethibitishwa kufariki katika siku za mapigano ya kikabila kuhusu upatikanaji wa ardhi.

    Waziri wa afya wa jimbo ameliambia shirika la habari la Ufaransa kuwa hali sasa ni shwari lakini kuna changamoto kubwa ya kutafutia hifadhi waliokimbia makazi yao.

    Umoja wa Mataifa unasema watu 15,000 wamelazimika kuyahama makazi yao huko Blue Nile na wengi wapo katika makazi ya muda shuleni.

    Ilisema kote Sudan, zaidi ya watu milioni 14 sasa wanahitaji msaada wa kuokoa maisha, lakini kulikuwa na upungufu mkubwa wa misaada.

    Vurugu za Blue Nile zimesababisha maandamano ya mitaani katika miji kote Sudan, mawili kati ya hayo yaliweka marufuku ya kutotoka nje mapema wiki hii.

    Soma zaidi:

  3. Habari za hivi punde, Uhuru: Unga wa mahindi utauzwa kwa Ksh.100

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametangaza ruzuku ya chakula kwa unga wa mahindi.

    Katika hotuba ya kitaifa kwa nchi, Uhuru alisema kuwa pakiti ya kilo 2 ya unga wa mahindi sasa itauzwa kwa Sh100 kote nchini.

    Hatua hii inafuatia makubaliano kati ya serikali na wasagaji mahindi waliosajiliwa na wizara ya Kilimo.

    Hatua hizo zilizochukuliwa ili kupunguza gharama ya chakula hiki kikuu ni pamoja na kusimamishwa kwa ushuru wa maendeleo ya reli kwa mahindi yote yanayoagizwa kutoka nje.

    Pia alisitisha ada ya kuagiza kutoka nchi za nje kwa mahindi yote yanayoagizwa kutoka nchi za kigeni na kinachotokea sasa ni kwamba hatua hiyo inapunguza gharama ya pakiti ya kilo 2 ya unga wa mahindi kutoka Sh.205 ya sasa hadi Sh100 iliyotangazwa rasmi.

    ‘’Mpango huu wa ruzuku ya takriban Sh.105 kwa pakiti ya kilo 2 ya unga wa mahindi unakusudiwa kupunguza gharama ya maisha kwa kaya zilizo hatarini tunapotafuta suluhu la kudumu la kupanda kwa bei ya unga kila uchaguzi,’’ Uhuru alisema.

    Rais aliwashukuru wasagaji kwa kuelewa na kuona haja ya kukubali mpango huo na kuhakikisha Wakenya wanaishi kulingana na uwezo wao.

    Kiongozi huyo wa nchi aliwaonya viongozi dhidi ya kuingiza siasa za kupanda kwa gharama ya maisha bila kutoa suluhu ni sawa na kukejeli machungu ya wanyonge, watu wale wale wanaotafuta kuwapigia kura.

    ‘’Wito wangu kwa wenye kujihusisha na siasa ni kutekeleza uwajibikaji wa kiraia. Ninawaalika wote kujiunga na jamii sio ya waombolezaji au walalamikaji hata wakati unahudumu serikalini lakini ninawaomba nyote muungane na jamii ya watoa suluhu kwani hapa ndipo penye mustakabali wa nchi yetu,’’ Uhuru alisema.

    Soma zaidi:

  4. Raila Odinga: Hakuna mfisadi atakayesalimika

    Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga anasema hakuna atakayesalimika katika kampeni ya kupambana na ufisadi ambayo anaahidi kutekeleza iwapo atachaguliwa kuwa rais katika uchaguzi wa mwezi ujao.

    Bw Odinga anafanya jaribio la tano na la mwisho kwenye wadhifa wa juu nchini humo.

    Waziri mkuu wa zamani mwenye umri wa miaka 77 aliniambia kuwa kwa umri wake, hataki kugombea tena lakini bado atakuwa na mengi ya kufanya hata kama hatachaguliwa.

    ‘’Nimekuwa nje ya siasa tendaji, lakini Umoja wa Afrika uliniteua kama mwakilishi wa Juu wa Miundombinu na imenifanya kuwa na shughuli nyingi,’’ alisema.

    Iwapo atashinda, Bw Odinga anasema ataangazia kupambana na ufisadi.

    Rais wa Kenya amesema nchi hiyo inapoteza zaidi ya $16m (£13m) kwa siku kutokana na ufisadi.

    ‘’Hakuna aliye muhimu kulko wengine.’’

    Nikibainika kuwa mfisadi wanapaswa kunishughulikia,” alisema, akitoa mfano wa Korea Kusini ambapo Rais Park Geun-hye alishtakiwa na kufungwa jela kwa takriban miaka mitano kwa ufisadi.

    Kuhusu uchumi, Bw Odinga anasema ataanzisha hatua za kubana matumizi na kutafuta kupanga upya deni la nje ili kuhakikisha nchi haileti ulipaji.

    Soma zaidi:

  5. Vijana wa Ghana wenye hasira wamfukuza mbunge na kumrushia maji

    Vijana wenye hasira nchini Ghana katika eneo la Suame wamemfuata mbunge, huku wakimpigia makofi, kumtusi na kumrushia maji.

    Kiongozi wa wengi, Osei Kyei Mensah-Bonsu alikuwa katika eneo hilo kuzungumza na watu juu ya mahitaji yao ikiwa ni pamoja na miundombinu duni.

    Wiki iliyopita baadhi ya wakazi waliweka vizuizi barabarani kupinga hali ya barabara hizo.

    Wakati kikundi cha mafundi wachanga kilipogundua kuwa Bw Mensah-Bonsu alikuwa katika eneo hilo walielekea moja kwa moja kwenye eneo la tukio na kuanza kusema kwa kelele ‘’ondoka, ondoka!’’.

    Polisi walifika baadaye kutuliza ghasia.

    Vijana hao walisema walimfukuza Bw Mensah-Bonsu, kwa sababu licha ya kuwawakilisha bungeni, hatimizi ahadi zake za kurekebisha barabara.

    Bw Mensah-Bonsu alisema hana wasiwasi kuhusu tukio hilo kwa sababu vijana wangefanya vivyo hivyo kwa afisa yeyote wa serikali, na sio yeye pekee.

  6. Mshukiwa wa wizi wa Kenya akamatwa kwa mganga wa kienyeji

    Mwanamke wa kenya ambaye anadaiwa kuiba pesa kutoka kwenye nyumba ya afisa wa serikali ambako alikuwa akifanya kazi kama mfanyakazi wa nyumbani, amekamatwa katika kaburi la mganga wa kienyeji leo, polisi imesema

    Polisi imesema kuwa mshukiwa huyo alikamatwa pamoja na mume wake katika “nyumba ya mganga wa kienyeji anayefahamika ” karibu na mji wa Nairobi , “aambako alikuwa ameenda kuomba alindwe ” ili asikamatwe.

    Wapelelezi walimpata mshukiwa huyo akiwa amewekwa kwenye karai iliyokuwa na damu ya ndege waliokufa, Imesema taarifa ya Idara ya upelelezi wa makosa ya jinai (DCI)

    “Alipowatambua wapelelezi, mganga huy wa kienyeji mzee alitangazaaliongea maneno yasiyo na mwisho ili kuwafaya waondoke, lakini hilo halikuwazuia wapelelezi kutekeleza mpango wao wa kumkamata mshukiwa ambaye alikuwa amefunga macho yake ,” taarifa iliongeza.

    DCI pia ilituma ujumbe wa Twitter wenye picha za vifaa vinavyodaiwa kutumiwa na mganga wa kienyeji.

  7. Gachagua na Karua wapambana katika mdahalo wa wagombea wenza Kenya

    Mdahalo wa wagombea wenza katika uchaguzi wa Kenya ulifanyika jana usiku na kutazamwa na Wakenya kote nchini kwa hamu kubwa. Mjadala huo uliofanywa kwa ngazi mbili uliwahusisha wagombea wanne wanaowania nafasi ya naibu rais kwa matumaini ya kuwashawishi wapiga kura kuwaunga mkono.

    Mgombea mwenza wa muungano wa Kenya Kwanza, Rigathi Gachagua aliitumia mdahalo huo kuanzisha mashambulizi makali dhidi ya familia ya kwanza na Rais Uhuru Kenyatta haswa, kwa kuanzisha kile alichokiita "kutekwa kwa serikali."

    Akijitokeza wakati wa safu ya pili ya mijadala hiyo na mwenzake wa Azimio Martha Karua, Bw Gachagua alimkabili Rais Kenyatta ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la muungano wa Azimio, akimshutumu kwa kueneza ufisadi na kuwa mpangaji mkuu wa ‘mradi’ wa Raila Odinga-Martha Karua. .”

    "Kuna utekaji nyara wa serikali unaofanywa na magenge ya ufisadi...makundi ya wahalifu ambayo yanapora rasilimali zetu kila siku," Bw Gachagua alidai.

    Alimshutumu Bi Karua kwa kuondoka kutoka utawala wa aliyekuwa rais Mwai Kibaki alipomhitaji zaidi.

    Lakini Bi Karua alisema kujiuzulu kwake kutoka kwa serikali ya Bw Kibaki ni jambo la kawaida lakini hiyo haimaanishi kuwa alimdharau Mkuu wa Nchi.

    Badala yake alimshutumu bosi wa Bw Gachagua - Dkt Ruto kwa kukosa kufanya jambo la heshima kwa kujiuzulu ikiwa anahisi serikali ya Rais Kenyatta haifanyi ipasavyo.

    Lakini Bw Gachagua alibainisha kuwa Dkt Ruto alikataa kutosheleza matamanio ya Rais Kenyatta kung’atuka serikalini na hakuwa na uwezo wa kumfukuza kwa vile nafasi hiyo ni ya kuchaguliwa na si ya uteuzi kama ilivyokuwa siku za nyuma.

    Bw Gachagua alidokeza kuwa wadhifa wa Naibu wa rais haufai kuteuliwa bali unapaswa kusalia kuwa wa kuchaguliwa hivyo hivyo kulindwa kikatiba jinsi ilivyo sasa.

    Karua alitangaza ushirikiano wake na mgombeaji wa urais wa Azimio la Umoja Raila Odinga kama unatakaofanikisha vita dhidi ya ufisadi nchini Kenya

    Taarifa zaidi :

    • Uchaguzi Kenya 2022:Nani yuko kwenye kinyang'anyiro cha kuiongoza Kenya ?
    • Viongozi wanawake Kenya wamekuwa na mchango gani katika siasa za nchi hiyo?
    • Uchaguzi Kenya 2022:Utaratibu wa kupiga kura Kenya

    Kufuatia mdahalo wa wagombea wenza wa urais nchini Kenya, Wakenya wameonyesha msisimuko mkubwa wa kutaka kujua maoni ya wenzao kuhusu ni nani aliyeng'ara kwenye mchuano huo uliowapatia fursa wagombea kueleza sera zao na jinsi watakavyoweza kutatua matatizo yanayoikabili nchi. Mitandao ya kijamii hususan Twitter imefurika maoni ya Wakenya kuhusu mdahalo huo:

    Baadhi kama Justice Sila Owiti na Ruth Wachela walihoji ni nani anayefaa kuwa naibu rais wa Kenya :

  8. Mmoja wa mapadre waliotekwa Nigeria apigwa risasi na kuuawa

    Mmoja wa makasisi wa Kikatoliki wawili waliotekwa nyara na watu wenye silaha katika jimbo la kaskazini mwa Nigeria la Kaduna amepigwa risasi na kuuawa na watekani wake baada ya kupokea kikombozi. Padre mwingine ambaye pia alikuwa ametekwa na watu hao aliachiliwa jana.

    Taarifa ya kanisa Katoliki imesema kuwa mwili wa Padre John Mark Cheitnum uligundulika Jumanne. Ilielezea mauaji hayo kama ''ya kutisha'' Mwenyekiti wa shirikisho la Wakristo wa Nigeria katika jimbo la Kaduna ameiambia BBC kuwa watekaji walikuwa wamepokea kikombozi.

    Halafu walioongoza wale walioleta pesa za kikombozi mahala ambapo mwili wa mhanga ulikuwa.

    Lakini watekaji hao walimuachilia Padre Donatus Cleopas. Haijajulikana wazi ni kwanini mmoja wa mapadre hao aliuliwa na watekaji wake. Makasisi hao walitekwa kwa mtutu wa bunduki walipokuwa katika makazi ya mapadre katika kijiji cha Yadin Garu siku ya Ijumaa.

    Tangu mwezi Mei, takriban makumi kadhaa ya makasisi wa Kikristo – wengi wao wakiwa ni Wakatoliki - wametekwa na watu wenye silaha kote Nigeria . Takriban watatu kati yao waliawa na watekaji wao .

    Watu wanaoachiliwa na watekaji nchini Nigeria mara nyingi huachiliwa baada ya kulipiwa kikombozi. Nigeria inahangaishwa na wimbi la ghasia za magenge yenye silaha. Serikali ya Rais Muhammadu Buhari inakabiliwa na ukosoaji kwa kushindwa kukabiliana na ukosefu mkubwa wa usalama - licha ya kusambaza maelfu ya wanajeshi kukabiliana nao.

  9. Marekani : Mashirika ya ujasusi yaonya juu ya uingiliaji wa Urusi wa mtandao wakati wa uchaguzi

    Mkurugenzi wa shirika la ujasusi la Marekani FBI Christopher Wray na mkuu wa Shirika la usalama wa taifa nchini humo pamoja na kituo cha usimamizi wa mtandao Jenerali Paul Nakasone, wamesema kuwa Urusi inaweza kuingilia katika uchaguzi wa awali urais unaotarajiwa kufanyika Novemba, imesema ripoti ya New York Times.

    "Nina uhakika kabisa Warusi wanaweza kuingilia katika uchaguzi ," Ray alisema katika mkutano wa usalama wa mtandao mjini New York, wanaweza kuanzisha vita Ukrainehuku wakati huo huo wakijaribu kushawishi mchakato wa siasa za ndani ya Marekani.

    Moscow imekanusha hili, lakini ujasusi wote wa Marekani, pamoja na mwendesha mashitaka maalum aliyefanya uchunguzi anasema Urusi iliingilia kati uchaguzi wa urais wa mwaka 2016, ambapo Donald Trump alichaguliwa kama rais.

    Unaweza pia kusoma:

    Urusi yaishambulia Ukraine: Mengi zaidi

    • MOJA KWA MOJA:Biden amuonya Putin: ''Madikteta watagharamika
    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  10. Urusi inapanga kunyakua maeneo zaidi ya Ukraine kupitia"mbinu" iliyotumia kunyakua Crimea, Marekani inasema.

    Akiashiria ujasusi wa Marekani, msemaji wa Baraza la Kitaifa la Usalama John Kirby alisema Urusi tayari inaweka msingi wa unyakuzi huo.

    Maeneo yanayokaliwa nchini Ukraine huenda yakafanya kura "bandia" ya maoni kuhusu kuiunga na Urusi ifikapo Septemba,alisema.

    Urusi ilinyakua jimbo la Crimea kutoka kwa Ukraine 2014 kufuatia kura ya maoni iliyoonekana na wengu kuwa haramu.

    "Tunataka kuweka wazi kwa watu wa Marekani," Bw. Kirby aliwaambia waandishi wa habari. "Hakuna anayedanganyika naye. [Rais wa Urusi Vladimir Putin] anatumia mbinu aliyotumia mwaka 2014"

    Aliishutumu Urusi kwa kuweka maafisa wasio halali wanaounga mkono hatua yake ya kuendesha mikoa inayokalia kimabavu nchini Ukraine, kwa lengo la kuandaa kura ya maoni ili maeneo hayo yaweze kuwa sehemu ya Urusi

    Matokeo ya kura hiyo yanaweza kutumiwa na Urusi "kujaribu kudai kunyakuliwa kwa eneo huru la Ukraine",Bw. Kirby alisema.

    Urusi tayari imeweka maafisa wake wa kikanda katika maeneo inayokalia nchini Ukraine.

    Crimea ilinyakuliwa na Urusi mwaka 2014 baada ya kura ya maoni iliyoandaliwa kwa haraka - iliyochukuliwa kuwa haramu na jumuiya ya kimataifa, ambapo wapiga kura walichagua kujiunga na Urusi.

    Baadhi ya wafuasi wa Kyiv walisusia kura na kampeni haikuwa huru na haki.

    Kura kama hizo zilizopigwa katika maeneo mengine ya Ukraine zingeshuhudia hali kama hiyo huku upinzani wowowte wa kujiunga na Urusi ukikandamizwa kwa kiasi kikubwa.

    Bwana Kirby alisema "anafichua" njama ya Urusi "na ulimwengu unajua kwamba unyakuzi wowote unaodaiwa ni wa kimakusudi, kinyume cha sharia na haramu", na kuahidi kungekuwa na jibu la haraka kutoka kwa Marekani na washirika wake.

    Maeneo yanayolengwa kunyakuliwa ni pamoja na Kherson, Zaporizhzhia, Donetsk na Luhansk,alisema.

    Unaweza pia kusoma:

    Urusi yaishambulia Ukraine: Mengi zaidi

    • MOJA KWA MOJA:Biden amuonya Putin: ''Madikteta watagharamika
    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  11. Wimbi la joto: Rekodi ya joto yashuka huku joto kali likiichoma Ulaya

    Wazima moto kote Ulaya wamekuwa wakikabiliana na viwango vya juu vya joto huku visa vya moto wa nyikani vikiongezeka

    Rekodi za juu za viwango vya joto vimeshuka na wazima moto wanakabiliwa na visa moto mpya unachoma maeneo mengi ya Ulaya Magharibi kufuatia wimbi kubwa la joto.

    Kwa kawaida Uingereza, ambayo imezowea kuwa na viwango visivyo vibaya sana vya hali ya hewa, sasa imeshuhudia viwango vya joto vikipanda kwa zaidi ya nyuzijoto 40 (104F) kwa mara ya kwanza.

    Ujerumani imeshuhudia siku yenye joto zaidi yam waka hadi sasa huku viwango vya vifo vikiongezeka nchini Ureno baada ya siku kadhaa za joto la kupindukia.

    Visa vya moto mbaya unaoibuka nyikani vimeyakumba maeno yote ya bara la Ulaya. Shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa (WMO) limeonya kuwa kutakuwa hali mbaya zaidi ziku zijazo.

    Mawimbi ya joto yamekuja mara kwa mara na kwa kiwango cha juu zaidi, na kudumu kwa muda mrefu kwasababu ya mabadiliko ya tabia nchi yanayosababishwa na binadamu.

    "Siku zijazo aina hizi za mawimbi ya joto zitakuwa jambo la kawaida, na tutashuhudia hata mawimbi mabaya zaidi," alisema mkuu wa WMO Peterri Taalas.

    Unaweza pia kusoma:

    • Joto kali laua 238 na kusababisha moto mkubwa katika nchi za Mediterania
    • Je binadamu ni wa kulaumiwa kwa hali mbaya ya hewa?
  12. Jeshi la Polisi Tanzania kuchunguzwa, Rais atangaza kamati maalumu akimuapisha IGP mpya

      • Author, Yusuph Mazimu
      • Nafasi, BBC Swahili

    Rais Samia Suluhu amemuapisha Mkuu mpya wa jeshi la Polisi Tanzania Camillus Wambura aliyechukua nafasi ya Simon Sirro aliyeteuliwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe. Akimuapisha Wambura na viongozi wengine, Rais Samia ametangaza kuunda kamati ya watu 12 pamoja na mambo mengine kuangalia utendaji wake.

    Mbali na kamati hiyo itakayoongozwa na Jaji Mstaafu Mohamed Chande Othman na Balozi mstaafu Ombeni Sefue.Pia ameunda sekretarieti ya watu 5 kwa mantiki ya kusaidia ufanisi wa Jeshi hilo na majeshi mengine.

    Rais amesema ameunda kamati hiyo 'kunishauri njia bora ya kuleta mabadiliko ya utendaji wenye matokeo bora kwenye vyombo vya haki jinai, wakianza na Jeshi la Polisi'.

    Kamati hiyo itakuwa na kazi ya kuchunguza na kuangalia masuala ya utendaji wake, mifumo na miundo ambayo itasaidia kuboresha utendaji wake.

    Ameongeza pia yatafanyika mabadiliko mengine makubwa zaidi kwenye jeshi hilo na majeshi mengine ili kuboresha ufanisi wake.

    Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko katika uongozi wa juu wa jeshi la Polisi.

    Hapo awali Wambura alikuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai.

    Mabadiliko hayo yaliyofanywa mapema alfajiri ya jumatano ambapo yamezua mawazo mseto baina ya wanaharakati na watumiaji wa mitandao ya kijami.

    Simon Sirro aliteuliwa kuwa mkuu wa Jeshi la polisi mwaka 2017 chini ya uongozi wa Hayati John Pombe Magufuli akichukua nafasi ya Ernest Mangu.

    Mbali na mabadiliko hayo Rais Samia pia amempandisha cheo Kamishna Msaidizi wa Polisi(ACP) Ramadhan Hamisi Kingai na kumteua kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) akichukua nafasi ya Camilius Wambura ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP).

    Pia amemteua Kamishina wa Polisi (CP) Hamad Khamis Hamad kuwa kamishna wa polisi Zanzibar akichukua nafasi ya Kamishna wa polisi Awadgi Juma Haji aliyeteuliwa kuwa mkurugenzi wa operesheni makao makuu.

    Teuzi zilizofanywa na rais Samia zimezua maoni mbali mbali hasa katika mitandao ya kijamii ikiwamo kutoka kwa viongozi wa upinzani na wanaharakati nchini humo

    Uteuzi huo umeanza rasmi Julai 19, 2022 na wote walioteuliwa wanatarajiwa kuapishwa leo Julai 20 saa tano asubuhi katika Ikulu ya Chamwino, Dodoma.

  13. Natumai Hujambo.Karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja leo