Ukraine yaripoti kupigwa na mashambulio ya makombora ya masafa kusini na mashariki
Gari lililoubeba mwili wa Waziri mkuu wa zamani wa Japan Shinzo Abe limewasili nyumbani kwake katika mji mkuu wa Tokyo.
Moja kwa moja
Habari za hivi punde, Nyumba ya Waziri mkuu wa Sri Lanka Ranil Wickremesinghe yachomwa moto
Nyumba ya Waziri mkuu wa Sri Lanka Ranil Wickremesinghe imechomwa moto katika ghasia za waandamanaji.
Kipindi cha saa moja iliyopita hali ya ghasia baina ya waandamanaji na polisi imekuwa ikiendela kuongezeka nje ya makazi ya Wickremesinghe katika mji mkuu Colombo.
Ruka X ujumbe, 1Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Ruka X ujumbe, 2Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Unaweza pia kusoma:
Urusi na Ukraine: Ukraine yaripoti kupigwa na msahambulio ya makombora ya masafa kusini na mashariki

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Jengo la ghorofa linaloungua baada ya kupigwa na kombora la Warusi katika Siversk,mashariki mwa Ukraine Mashambulio ya makombora ya masafa ya Urusi na roketi vimesababisha uharibifu mkubwa kote mashariki na kusini mwa Ukraine, maafisa wa majimbo hayo wanasema.
Raia wanne wameuawa katika shambulio lililofanyika katika mji wa Siversk, uliopo katika jimbo la Donetsk region, gavana wa eneo Pavlo Kyrylenko amesema.
Maeneo ya raia ya Druzhkivka,katika jimbo hilo, pia yalipigwa. Duka la bidhaa za jumla liliharibiwa na shimo refu linaonekana kando yake.
BBC haikuweza kudhibitisha taarifa za mashambulio ya hivi karibuni.
Vikosi vya ardhini vya Urusi havionekani kusonga mbele katika kipindi cha saa 24 katika jaribio lao la kuyachukua maeneo mengine ya jimbo la Donetsk..

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Shimo linaloaminiwa kuwa limetokana na kombora lililopiga katika eneo la Druzhkivka Maafisa wa Ukraine pia waliripoti kuwa makombora ya Urusi yalipiga katika maeneo ya Kharkiv, kaskazini, Mykolaiv kusini na Kryvyi Rih, mji wa kaskazini mashariki waMykolaiv.
UrUvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine: Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Mkenya Angella Okutoyi ashinda kwa mara ya kwanza taji la tenis la Wimbledon

Maelezo ya picha, Angella Okutoyi, ni Mkenya wa kwanza kushinda mashindano ya Wimbledon Historia imeandikwa katika shindano la tenis la Wimbledon wanawake baada ya Mkenya Angella Okutoyi kutoka Kenya akishirikiana na Mholanzi Marie Nijkamp kuwa mshindi kwa mara ya kwanza katika Wimbledon. Bi Angella amekuwa mshindi wa kwanza wa Kenya kushinda taji hilo.
Shirikisho la kimataifa la mchezo wa Tenisi ITF limetuma ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter kuhusu ushindi wa Bi Angella:
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Akiwa na umri wa miaka 18, Angella Okutoyi kutoka nchini Kenya na mchezaji mwenza anaonekana kuwa ndiye nyota wa baadaye wa tenisi wa Afrika. Lakini njia ya kufikia mafanikio ya juu imekuwa ngumu kwake kutokana na kukabiliwa na njaa na huzuni katika maisha yake.Akizungumza ya na BBC Idhaa ya Kiswahili awali alisema kuwa amedhamiria kutumia ugumu huu kusukuma mbele mafanikio yake kwenye tenisi katika siku zijazo:
Tazama jinsi waandamanaji walivyovamia ofisi ya Rais mjini Colombo
Picha ya video inaoonyesha waandamanaji wakichukua udhibiti wa ofisi ya rais mjini Colombo:
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Unaweza pia kusoma:
- Sri Lanka: Waandamanaji wavamia makazi ya Rais Gotabaya Rajapaksa
Kwa picha: Jinsi Waislamu washerehekea siku kuu Eid al-Adha
Waislamu kote dunia wanasherehekea siku ya Eid al-Adha. Waislamu wamekusanyika katika Misikiti na viwanja mbali mbali duniani kuanzia asubuhi kwa ajili ya sala ya Eid al-Adha.
Leo, ni siku ya kumi ya mwezi wa Arafat, ambayo ni siku inayosherehekewa na Waislamu wote Duniani.Siku hii inasherehekewa katika maadhimisho ambayo mtume Mohammad alitoa hmafundisho yake ya mwisho katika Mlima Arafat karibu na Mecca karibu na mwisho wa maisha yake.
Hizi ni baadhi ya picha za Idd- al -Adha kutoka baadhi ya maeneo mbali mbali duniani.

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Mamia ya mahujaji wa kiislamu wakiendelea kutupa mawe kwa jiwe la shetani Macca 
Maelezo ya picha, Mahujaji wakielekea katika Arfa jana 
Chanzo cha picha, BBC/SHIRAAZ MOHAMED
Maelezo ya picha, Waumini wa Kiislamu wakisali katika siku kuu ya Idd nchini Madagascar 
Chanzo cha picha, BBC/SHIRAAZ MOHAMED
Maelezo ya picha, wanawake wakipika chakula kwa ajili ya sherehe ya Idd Kagame kuwania muhula wa nne kama rais wa Rwanda

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa Rwanda, Paul Kagame,amesema atagombea tena urais katika uchaguzi wa mwaka 2024.
Katika mahojiano na televisheni ya Ufaransa, Bwana Kagame mwenye umri wa miaka 64 amesema kuwa "anaangalia uwezekano wa kugombea kwa miaka mingine 20".
"Uchaguzi ni kuhusu watu kuchagua," aliongeza.
Katika mwaka 2015 Bw Kagame alibadilisha katiba na hivyo kumruhusu kubakia mamlakani hadi mwaka 2034.
Katika uchaguzi wa mwishii miaka mitano iliyopita, takwimu rasmi zilionyesha kuwa alishinda kwa 99%ya kura – jambo ambalo wengi nje ya nchi hiyo walilipinga kuwa lisilowezekana.
Rais Kagame alitetea vikali rekodi ya haki za binadamuya Rwanda katika Mkutano wa Jumuiya ya Madola uliofanyika mwezi Juni mjini Kigali.
Unaweza pia kusoma:
- Paul Kagame ashinda asilimia 98.78 ya kura
- 'Mpango wa Uingereza wa kuwapeleka wahamiaji Rwanda 'ni kinyume cha Mungu' - Welby
- Wake wa marais: Mfahamu Bi Jeanette Nyiramongi Kagame mke wa rais wa Rwanda Paul Kagame
Kinyang’anyiro cha kumrithi Waziri mkuu wa Uingereza: Ni yapi mapya?

Chanzo cha picha, UK Parliament
Maelezo ya picha, Waziri wa zamani wa usawa nchini Uingereza Kemi Badenoch amekuwa wa nne kuwania kiti cha Johnson Zimekuwa ni siku chache za heka heka katika siasa za Uingereza tangu tangazo la kujiuzuru kwa Bw Boris Johnson siku ya Alhamisi.
Haya ni yale ambayo yamekuwa yakifanyika kwa ufupi:
·Wabunge wanajitokeza katika mapambano ya kuwa kiongozi wa chama cha Conservative na Waziri mkuu
·Waziri wa zamani wa usawa Kemi Badenoch amekuwa mbunge wa hivi karibuni wa Conservative kuingia katika kinyang’anyiro hicho
·Rishi Sunak ametangaza azma yake Ijumaa mchana, pamoja kuanzisha kampeni yake ya rasmialiyoiita- Ready for Rish
·Tom Tugendhat, mweneykiti wa kamati ya mambo yanje na Mwanasheria mkuu Suella Braverman pia wamewasilisha majina yao kuwania kiti hicho
·Mwana kampeni ya Brexit Steve Baker amesema ataunga mkono azma yaMwanasheria Mkuu Suella Braverman ya kuwania kiti hicho
·Wengine wanaotajwa kuwa wanaangalia uwezekano wa kuwania wadhifa wa Boris Johnson ni pamoja na Waziri wa zamani wa afya Sajid Javid, ambaye kwa sasa ni Waziri wa ulinzi Ben Wallace, na Waziri wa zamani wa mambo ya nje Jeremy Hunt
·Muda uliopangwa kwa ajili ya uchaguzi wakiongozi wa chama cha Conservative unatarajiwa kuthibitishwa wiki ijayo na Waziri mkuu mpya anatarajiwa kuchukua wadhifa huo mwezi Septemba.
Unaweza pia kusoma:
- Nani atachukua nafasi ya Boris Johnson?
- Boris Johnson: Urusi yashangilia masaibu ya Johnson huku maoni yakitolewa kote duniani kuhusu tangazo lake
- Mvutano kuhusu Waziri Mkuu Uingereza: Je Boris Johnson yupo katika hatihati ya kuanguka?
- Kujiuzulu kwa Boris Johnson: Kipi kinafanyika sasa?
Urusi na Ukraine: Makombora ya Urusi yapiga katika jimbo la Donetsk

Chanzo cha picha, Pavel Kirilenko
Jumamosi hii majira ya asubuhi, vikosi vya Urusi vimeshambulia makazi kadhaa katika jimbo laDonetsk - gavana wa jimbo hilo Pavel Kirilenko amesema.
Matokeo yake, kumekuwa na majeruhi wengi, na walau mtu mmoja ametambuliwa kufa.
Miundo mbinu ya raia miongoni mwake hospitari, kasri la utamaduni, kituo cha leri na majengo ya makazi ya watu vimeharibiwa.
"Warusi wanawashambulia rai ana wataendelea kuwapiga risasi na makombora! Njia inayofaa kwa sasa ni kuwaokoa!" Kirilenko aliandika.
Wakati huo huo katika jimbo la Kharkiv, vikosi vya Urusi vimefanya shambulio la kombora kwenye makazi ya watu, amesema mkuu wa jimbo la Kharkiv ,Oleg Sinegubov.
"wapendwa wakazi wa Kharkiv, mjizuia kukaa kweney mitaa ya jiji iwezekavyo. Muwe waangalifu, makae sehemu salama!" - Sinegubov aliandika kwenye chaneli yake ya Telegram.
Huduma za uokozi ziko katika eneo la tukio na hakuna ripoti za majeruhi.

Chanzo cha picha, EPA
Unaweza pia kusoma:
- Mzozo wa Ukraine: Fahamu uhusiano wa kihistoria kati ya Ukraine na Urusi
- Mzozo wa Ukraine: Fahamu kwanini baadhi ya mataifa yenye uwezo mkubwa yamesalia kimya
- Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
Elon Musk ataka kusitisha mkataba wa dola bilioni 44 wa kununua Twitter

Chanzo cha picha, Getty Images
Elon Musk anataka kuacha azma yake ya kununua mtandao wa kijamii wa Twitter kwa dola 44 (£36bn), akidai kuwa kumekuwa na uvunjaji wa mara nyingi wa makubaliano.
Tangazo hilo ni mabadiliko ya hivi karibuni katika sakata inayoendeelea baada ya mtu huyu tajiri zaidi duniani kuamua kununua Twitter mwezi Aprili.
Bw Musk amesema ameamua kujiondoa kwasababu Twitter ilishindwa kutoa taarifa za kutosha kuhusu idadi ya akaunti gushi na ambazo hazitumiwi.
Twitter inasema inapanga kuchukua hatua ya kisheria kutekeleza makubaliano.
"Bodi ya Twitter Board imejitolea kuzuwia uhamishaji wa fedha kuhusu bei na masharti yaliyofikiwa kati yake na Bw Musk,"Mwenyekiti wa Twitter Bret Taylor aliandikakwenye ujumbe wake wa Twitter, hatua inayoashiria uwezekano wa makabiliano ya muda mrefu ya kisheria baina ya pande hizo mbili.
Makubaliano ya makubwa ya awali yalijumuisha dola bilioni 1 (£830m) bila kuvunjwa.
Mzozo kuhusu akaunti gushi
Mwezi Mei, Bw Musk alisema mkataba ulikuwa "umezuiwa kwa muda" kwasababu alikuwa anasubiri data kuhusu akaunti feki na zisizotumiwa za Twitter.
Mfanyabiashara huyo bilionea alikuwa ameomba ushahidi wa kuthibitisha maelezo ya kampuni kwamba akaunti gushi na zile zisizotumiwa ni sawa na 5% ya watumiaji wa mtandao huo kwa ujumla.
Katika barua iliyowasilishwa na taasisi za usalama za Marekani na tume ya ubadilishaji wa pesa, wakili wa Bw Musk alisema kuwa Twitter ilishindwa au ilikataa kutoa taarifa hizi.
Unaweza pia kusoma:
- Elon Musk atishia kujiondoa kwa mkataba wa Twitter
- Twitter: Je ni kwanini Elon Musk amedhamiria kuchukua udhibiti wa Twitter
- Elon Musk na Twitter: Sababu sita zilizomfanya bilionea huyu kujipata mashakani mtandaoni
Mauji ya Shinzo Abe: Mwili wa Waziri mkuu wa zamani wa Japan warejeshwa nyumbani

Chanzo cha picha, Getty Images
Gari lililoubeba mwili wa Waziri mkuu wa zamani wa Japan Shinzo Abe limewasili nyumbani kwake katika mji mkuu wa Tokyo.
Abe alipigwa risasi na kuuawa alipokuwa akizungumza katika mkutano wa kampeni ya kisiasa Ijuamaa kusini mwa mji wa Nara.
Polisi wanaochukuza mauaji yake wanasema mshukiwa aliyefyatua risasi aliwaambia maafisa kwamba alikuwa na chuki dhidi ya ‘’shirika maalum’’
Yamagami aliamini Shinzo Abe alikuwa sehemu ya kundi hilo, ndiyo maana alimpiga risasi, wanaongeza.
Alipoulizwa na mjumbe wa vyombo vya habari vya Japan kama nia ya mpiga risasi huyo ilikuwa kumuua Abe, polisi wanasema tu kwamba Yamagami alikiri kumpiga risasi Waziri Mkuu huyo wa zamani.
Waziri mkuu wa sasa Fumio Kishida anatarajiwa kutembele eneo la tukio leo mchana.
Kulingana na taarifa za vyombo vya habari nchini humo, kutakuwa na mkesha siku ya Jumatatu na mazishi ya Bw Abe yatafanyika Jumanne.
Abe walikuwa Waziri mkuu aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi nchini Japan na kifo chake ambacho kimetokea akiwa na umri wa miaka 67, kimewashtua wengi katika nchi hiyo ambako visa vya uhalifu wa bunduki ni nadra sana.
Aliawa alipokuwa akifanya kampeni kwa ajili ya chama chake katika uchaguzi wa bunge wa Jumapili.
Unaweza pia kusoma:
- Kifo cha Shinzo Abe:Mauaji ya kushtua yanayoweza kuibadilisha Japan milele
- Shinzo Abe: Waziri Mkuu wa zamani wa Japan auawa kwa kupigwa risasi katika hafla ya kampeni
- Shinzo Abe: Mfahamu Waziri Mkuu aliyehudumu kwa kipindi kirefu zaidi Japan
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mubashara ya leo tarehe 09.07.2022
