Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tanzania: Askari polisi auawa katika vurugu baina ya jeshi la polisi na wananchi Loliondo
Askari Polisi mmoja ameuwa katika eneo la Loliondi Kaskazini mwa Tanzania kufuatia vurugu zinazoendelea kati ya Jeshi la Polisi na wananchi wa Loliondo ambao wamekuwa wakipinga kuondolewa kwenye baadhi ya makazi yao.
Moja kwa moja
Urusi na Ukraine: Paspoti za kwanza za Urusi zatolewa kwenye maeneo yaliyotwaliwa Ukraine
Paspati za kwanza za Urusi zilizotolewa kwa wakazi wa majimbo ya Ukraine yaliyotekwa ya Kherson na Zaporizhzhia zimekabidhiwa kwa wahusika, maafisa waliowekwa uongozini na Moscow-wamesema.
Zaidi ya watu 20 katika jimbo la Kherson wamepokea paspoti za Urusi, limesema shirika la habari la Interfax, likinukuu huduma za habari vya "utawala wa kijeshi- na kiraia" uliowekwa na Urusi.
"Leo paspoti za kwanza zilitolewa katika Kherson kwa watu ambao walikuwa wa kwanza kutuma maombi ya kuwa rai awa Urusi ," alisema afisa wa habari,akiongeza kuwa hii inakuja katika siku ya maadhimisho ya Russia Day, ambayo huadhimishwa tarehe 12 Juni.
Afisa wa utawala unaoungwa mkono na Moscow katika jimbo la Ukraine la Zaporizhzhia, Vladimir Rogov aliliambia shirika la habari la taifa kwamba idadi ya wakazi isiojulikana wamepata pia paspoti za Urusi katika sherehe iliyofanyika Melitopol.
"Kwetu sisi, hili ni tukio muhimu na la kihistoria. Hatua inayofuata katika njia ya kurejea nyumbani Urusi," alisema.
Mapema leo Rais Vladimir Putin alisaini sheria inayorahisisha maombi ya uraia kwa wakazi wa majimbo ya Ukraine na Zaporizhzhia na Kherson.
Urusi yaishambulia Ukraine: Mengi zaidi
- MOJA KWA MOJA:Biden amuonya Putin: ''Madikteta watagharamika
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukrain
Aurelien Tchouameni: Real Madrid yasaini mkataba na kiungo wa kati kutoka Monaco
Real Madrid imesaini mkataba wa miaka sita na kiungo wa kati Mfaransa Aurelien Tchouameni ambaye anatoka katika klabu ya Monaco.
Klabu zote zimetangaza mkataba huo na Real Madrid inasema itafanya hafla ya kumtambulisha kijana huyo mwenye umri wa miaka 22 Jumanne baada ya kumfanyia vipimo cya matibabu.
Tchouameni alicheza michezo 35 ya Ligi 1 katika klabu ya Monaco msimu uliopita, akichangia magoli matatu na kusaidia kufungwa kwa magoli mawili
Alicheza mechi 11 katika Ufaransa tangu alipocheza mchezo wa kimataifa mwezi Septemba.
Mkataba huo unaripotiwa kuwa wa thamani ya Euro milioni 80 (sawa na pauni milioni 68.3 pamoja na Euro milioni 20 (pauni milioni17) za nyongeza.
Tchouameni pia amekuwa akihusishwa na klabu za Liverpool, Manchester United na Paris St-Germain.
Taarifa zilisema kuwa Tchouameni alikuwa amekubali makubaliano na klabu ya Primia Ligi ya Liverpool.
Taarifa zaidi za soka
- Tetesi za soka Ulaya Jumamosi tarehe 11.06.2022: Milinkovic-Savic, Pogba, Zidane, Kounde, Jesus, Marquinhos
Mkataba wa wahamiaji wa Uingereza: Mahakama yaruhusu kuondoka kwa ndege za wahamiaji kuelekea Rwanda
Ndege ya kuwapeleka Rwanda iliyopangwa kuwasafirisha wahamiaji nchini Uingereza Jumanne wiki ijayo imeruhusiwa na Mahakama Kuu kuendelea na mpango huo.
Wanaharakati walishindwa katika azama yao ya mwanzo ya kuzuwia kupelekwa kwa wahamiaji hao nchini Rwanda, lakini wamethibitisha kuwa wataipelekeka kesi yao katika Mahakama ya rufaa.
Chini ya sera, baadhi ya wale wanaoingia nchini Uingereza kinyume cha sheria watasafirishwa kwa ndege hadi nchini Rwanda ambako wataweza kuomba uhamiaji wakiwa kule.
Takriban watu 31 wamekwisha ambiwa kuwa wanaweza kuwa katika ndege ya kwanza itakayoelekea Rwanda.
Kutakuwa na tathmini kamili ya kisheria, ambapo Mahakama ya juu itasikiliza hoja za kupinga sera hiyo nzima, kabla ya mwisho wa mwei Julai.
Katika uamuzi wake, Jaji Swift alikubali kuwa kuna "mausla ya maslahi ya umma" kwa Waziri wa mambo ya ndani Priti Patel ili kuweza kutekeleza sera zake.
Bi Patel aliusifu uamuzi wa mahakama na akasema kuwa serikali itaendelea na mipango yake, huku Waziri mkuu Boris Johnson akielezea uamuzi huo kama"taarifa iliyopokelewa".
Hatahivyo, wanaharakati waliopeleka kesi hiyo mahakamani, walielezea hofu yao kuhusu maslahi ya watu waliopangiwa "kupelekwa kwa lazima" nchini Rwanda.
Unaweza pia kusoma
- Wahamiaji Rwanda: Uingereza inaweza kutuma watu wa kwanza 'ndani ya wiki kadhaa'
- Mkataba wa wahamiaji wa Uingereza: Je, Rwanda ni nchi ya usalama au hofu?
- Wahamiaji Rwanda: Uingereza inaweza kutuma watu wa kwanza 'ndani ya wiki kadha
Urusi na Ukraine: Wanajeshi10,000 wa Ukraine waliuawa, Kyiv yasema
Ukraine inasema wanajeshi wake 10,000 wameuawa katia vita tangu ulipoanza uvamizi wa Urusi mwishoni mwa mwezi wa Februari.
Mshauri wa rais Oleksiy Arestovych alitoa maelezo katika mahojiano kwenye mitandao ya kijamii, wakati aliulizwa jinsi makundi mengi ya Ukraine yalivyopoteza maeneo katika siku za mwanzo 100 za kivita – hadi kufikia tarehe 3 Juni.
Ukraine inasema inapoteza takriban wanajeshi 100 katika mapigano ya kila siku, huku mamia zaidi wakijeruhiwa.
Arestovych alisema kupoteza kwa Urusi kulikuwa kukubwa zaidi. Serikali ya Ukraine inasema kuwa zaidi ya wanajeshi wake 30,000 wa Urusi waliuawa. Makadirio yaujasusi wa Uingereza –kwa zaidi yawanajeshi 15,000.
Gharama ya vita vyote vya Afghanstan kuanzia 1979 hadi 1989 jeshi la Usovieti lilipoteza maisha ya wanajeshi wake 15,000.
Maafisa nchini Urusi hawajatoa idadi yoyote rasmi za vifo vya wanajeshi wake nchini Ukraine tangu Machi 25, wakati waliposema wanajeshi 1,351 na maafisa walikufa.
Idhaa ya Kirusi ya BBC BBC imethibitisha vifo vya wanajeshi 3,502 wa Urusi– lakini waliobainika ni wale waliotajwa majina na kuzikwa katika makaburi.
Urusi yaishambulia Ukraine: Mengi zaidi
- MOJA KWA MOJA:Biden amuonya Putin: ''Madikteta watagharamika
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukrain
Justin Bieber afichua uso wake uliopooza baada tamasha lake kufutwa
Muimbaji Justin Bieber amefichua kuwa anaumwa amepooza uso baada ya kufutwa kwa onyesho lake wiki hii.
Bieber mwenye umri wa miaka 28 alisema katika video ya Instagram kwamba hali yake inatokana nahali ya kiafya ya Ramsay Hunt syndrome.
"Kama unavyoweza kuona jicho hili haliwezi kufunga. Siwezi hata kutabasamu kwa upande huu wa uso…Kwahiyo nimepooza upande huu kabisa ," alisema.
Ramsay Hunt syndrome ni mlipuko wa maambukizi ya virusi vinavyoathiri neva za masikio, wanasema wataalamu wa afya.
Mapema wiki hii, Onyesho ladunia la Bieber- Bieber's Justice World Tour – ambalo lilianza Februari- alitangaza kuwa maonyesho matatu yataahirishwa.
Pia alitabasamu na kukonyeza macho, kuwaonyesha wafuasi wake milioni 240 jinsi upande wake wa kulia wa uso usivyoweza kutingisika.
"Inatokana na virusi hivi ambavyo hushambulia neva na kusababisha uso wangu kupooza ," alisema mwimbaji huyo mzaliwa wa Canada katika video ya dakika tatu, iliyoonyesha uso wake.
Aliwaomba mashabiki wake kuwa wavumilivu, na alisema kuhusu matamasha yake yajayo kwamba "kimwili, bila shaka, hana uwezo wa kuyafanya".
Tanzania: Askari polisi auawa katika vurugu baina ya jeshi la polisi na wananchi Loliondo
Askari Polisi mmoja ameuwa katika eneo la Loliondi Kaskazini mwa Tanzania kufuatia vurugu zinazoendelea kati ya Jeshi la Polisi na wananchi wa Loliondo ambao wamekuwa wakipinga kuondolewa kwenye baadhi ya makazi yao.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mogella alithibitisha kifo cha askari mmoja na kueleza kuwa aliuawawa kwa kupigwa na silaa ya jadi aina ya mshale wakati akitekeleza majukumu yake.
Akitoa taarifa ya hali inayoendelea Loliondo alisema kuwa kila kitu kipo salama na askari waliopo katika eneo hilo wapo maalum kwaajili ya kusimamia zoezi la uwekaji mipaka.
Hata hivyo, watetezi wa haki za kibinadamu wamekemea vikali kile walichoeleza kuwa wananchi wanaumizwa kwa kupigwa risasi na mabomu ya machozi ili kuweza kuwaondoa kwa nguvu kwenye maeneo ambayo wamekuwa wakiisha miaka na mikaka.
Onesmo Ole Ngurumwa, Mkurugenzi wa Kituo cha Haki za Binadamu anasema kuwa suluhu ya mgogoro ulioibuka si vita bali ni pande zote mbili kukweti na kuzungumza.
Alisema, “ Tayari tumempoteza askari mmoja, lakini raia wengi wamejeruhiwa. Je hii ina faida gani? Tunamuomba Rais Samia Suluhu aingilie kati kumaliza mzozo huu kwa kuhakikisha pande zote mbili zinakaa mezani na kukubaliana.”
Kwa upande mwingine, Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, TAMWA, kimeitaka serikali ya Tanzania kuangalia njia bora ya kumaliza mgogoro huo badala ya kutumia nguvu kupambana na wananchi
Jana, baadhi ya raia waliieleza BBC kuwa wamekuwa wakishuhudia magari mengi ya jeshi la polisi na lile la jeshi la polisi yakizunguka katika maeneo mbalimbali ya Loliondo ambapo baadaye walianza kupiga mabomu ya machozi na milio ya risasa kusikika.
Hata hivyo taarifa zilizokuwa zikisambazwa mitandaoni zinaeleza kuwa wananchi waliomizwa na askari wengi ni wale ambao wanatakiwa kuondoka kwenye eneo ambalo linadaiwa kuwa linamilikiwa na mwekezaji kutoka Falme za Kiarabu.
Unaweza pia kusoma:
- Kassim Majaliwa: Waziri mkuu wa Tanzania apuuzilia mbali ghasia za Loliondo
- Tanzania yakanusha tuhuma za kukandamiza haki za Wamaasai
Jaji mkuu wa Kenya ataka Rais Uhuru Kenyata ang’olewe madarakani kwa kukiuka sheria
Jaji mkuu wa Kenya Martha Koome anataka mahakama ya rufaa kutangaza kwamba Rais Uhuru Kenyata amekiuka katiba ya nchi hiyo kwa kushindwa kuwateuwa majaji sita katika ya majaji 40 walioteuliwa na Tume ya huduma za mahakama (JSC) miaka mitatu iliyopita .
Bi Koome pia anataka mahakama itangaze kwamba suluhu ya madai ya kukiuka ni kuondolewa ofisini kwa Rais. Katika rufaa dhidi ya uamuazi wa Mahakama ya juu zaidi Bw Uhuru Kenyatta aliagizwa kuwateuwa majaji sita na iwapo atashindwa kufanya hivyo Jaji mkuu achukue jukumu la kutekeleza hilo. Bi Koome amekataa hata hivyo kufanya kazi ya rais .
Badala yake, amependekeza kutangazwa kwamba Rais amekiuka kipengele cha 3(1) na cha 166(1)(b) cha katiba au maagizo.
Mapigano makali yanaendelea katika mji muhimu wa mashariki mwa Ukraine wa Severodonetsk – Wizara ya ulinzi ya Uingereza
Mapigano makali ya mtaa kwa mtaa yanaendela katikamji muhimu wa Ukraine Severodonetsk na pande zote mbili Ukraine na Urusi zinauwezekano mkubwa wa kuwa na idadi kubwa ya waathiriwa, imesema Wizara ya ulinzi ya Uingereza katika taarifa zake za hii punde za ujasusi.
Hatahivyo, vikosi vya Urusi vimeweza kupata mafanikio ya kusonga mbele katika mji wa kusini, imesema wizara ya ulinzi ya Uingereza.
Iliongeza kuwa Urusi inafyatua makombora mengi ya ardhini nay a anga, katika jaribio la kuyazidi uwezo majeshi ya Ukraine.
Wizara ya ulinzi ya Uingereza inasema inapungukiwa na makombora ya kisasa na imeamua kutumia mfumo wa kuzuwia makombora mazito dhidi ya maeneo yanayolengwa nchini Ukraine ambayo kwa kawaida yametengezwa kwa ajili ya kuangamiza mifumo inayobeba ndege kwa kutumia mitambo ya ufyatuzi wa nyuklia.
Urusi yaishambulia Ukraine: Mengi zaidi
- MOJA KWA MOJA:Biden amuonya Putin: ''Madikteta watagharamika
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukrain
Hujambo tena na karibu kwa matangazo yetu mubashara ya leo tarehe 11.06 .2022