Urusi na Ukraine: Ndege ya kijeshi ya Ukraine yadunguliwa karibu na Odesa- Urusi
Urusi inasema kuwa vikosi vyake vimedungua ndege ya kijeshi ya Ukraine iliyokuwa inasafirisha silaha na zana za kivita karibu bandari ya Bahari nyekundu ya Odesa.
Moja kwa moja
Urusi na Ukraine: Mbinu isiyo ya kawaida inatumiwa katika mashambulizi ya helikopta za Urusi

Chanzo cha picha, Russian Ministry of Defence
Maelezo ya picha, Helikopta ya Urusi aina ya Ka-52 ‘Alligator’ Kuna mbinu ya kushangaza na isiyo ya kawaida ambayo imekuwa ikitumiwa mara kwa mara na marubani wa helikopta za kijeshi za Urusi zinazofanya mashambulizi nchini Ukraine.
Helikopta aina ya Ka-52 'Alligator' inaweza kutumia roketi zisizoongozwa kushambulia maeneo yanayolengwa ardhini. Hizi ni ni silaha za kufyatuliwa kuchoma na kusahau ambazo zinaweza kupiga eneo fulani kubwa bila kujali kubainisha usahihi wa eneo halisi linalolengwa.
Katika video kadhaa zilizotolewa na wizara ya ulinzi ya Urusi, mara nyingi unaweza kuona kutoka kwa ncha ya rubani kwamba rubani huvuta pua la ndege na kuisongesha mbele kabla ya kufyatua roketi zao.

Chanzo cha picha, Russian Ministry of Defence
Maelezo ya picha, Helikopta ya Urusi aina ya Ka-52 ‘Alligator’ ikifyatua makombora Je ni ni kwanini huenda marubani wanafanya hili?
Kwa kuvuta ncha ya mbele ya ndege(au pua) katika kona hii, maroketi hurushwa angani.
Kona hiyo ya juu huwapatia umbali mkubwa, badala ya uwezo wa usahihi wa maeneo wanayoyalenga. Ni karubu na kutumia silaha kama kombora la anga .
Lakini eneo kubwa linamaanisha helikopta iko mbali na kadri zinapokuwa mbali ndivyo uwezekano wa kuwa nje yae neo linalolengwa na shambuliola vikosi vya pinzani.
Kwahiyo kwa ufupi, mbinu hii huenda ni ya kujilinda.
Unaweza pia kusoma:
- Je Putin atabonyeza mtambo wa nyuklia?
- Putin aamuru kikosi cha nyuklia cha Urusi kuwa tayari
- Swift ni nini na kwa nini kupigwa marufuku Urusi ni muhimu sana?
Urusi na Ukraine: Helikopta ya Urusi iliyodunguliwa ikiwa na wahudumu yaopolewa kwenye hifadhi ya Kyiv

Chanzo cha picha, National Guard of Ukraine
Wapiga mbizi wa kikosi cha walinzi wa taifa wa Ukraine wameinua kutoka chini ya maji ya Kyiv helikopta ya Urusi chapa MI-35M, iliyodunguliwa katika siku ya wanza ya vita.
Kama ilivyoelezwa na Walinzi wa taifa, hii ni helikopta ya tatu ambayo waokoaji waliitoa kutoka katika hifadhi ya kyiv: Ya kwanza ilitolewa hadi kwenye nchi kavu mapema mwezi Aprili, na ya pili mapema wiki hii.
Mara hii, kulingana na shirika hilo, wapigambizi walibaini miili ya marubani wawili wa Urusi katika helikopta iliyoopolewa-miili yao ilipelekwa kwenye ufukwe.

Chanzo cha picha, National Guard of Ukraine

Chanzo cha picha, National Guard of Ukraine

Chanzo cha picha, National Guard of Ukraine
Unaweza pia kusoma:
- Je Putin atabonyeza mtambo wa nyuklia?
- Putin aamuru kikosi cha nyuklia cha Urusi kuwa tayari
- Swift ni nini na kwa nini kupigwa marufuku Urusi ni muhimu sana?
Tanzania yatenga ardhi maalumu kwa ajili ya wawekezaji

Chanzo cha picha, Getty Images
Tanzania imetenga zaidi ya ekari laki tano kwaajili ya wawekezaji ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya kukaribisha wawekezaji na kufungua milango ya biashara kimataifa.
Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi nchini Tanzania Angelina Mabula, ardhi imeandaliwa kutoka katika halmashauri 26 na juhudi za upangaji na uendelezaji zimeanza katika baadhi ya maeneo hayo yaliyo tengwa ambayo pia baadhi yanasubiri kutwaliwa na kulipa fidia.
Kauli ya waziri huyo inakuja kipindi ambacho Tanzania bado inakabiliwa na migogoro mikubwa ya ardhi katika maeneo mbali mbali ikiwemo Ngorongoro na Loliondo.
Waziri Angelina Mabula amesisitiza kuwa migogoro yote hiyo inashughulikiwa kwa kasi na wizara yake na tayari wana mipango ya kuanzisha kliniki ya ardhi katika ngazi za mikoa nchini Tanzania.
Urusi na Ukraine: Taarifa za vyombo vya habari kuhusu mashambulio Svyatogorsk Lavra Ukraine
Katika eneo la Svyatogorsk (jimbo la Donetsk), baada ya mashambulio ya makombora, mnara wa Kanisa la Kiothodox la Ukraine lililopo Svyatogorsk Lavra uliwaka moto, zinasema taarifa za vyombo vya habari.
Mnara wa kanisa unaangaliwa kama kielelezomuhimu cha usanifu wa mbao. Ulijengwa katika mwaka 1912.
Ruka Instagram ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa Instagram ujumbe
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Unaweza pia kusoma:
- Je Putin atabonyeza mtambo wa nyuklia?
- Putin aamuru kikosi cha nyuklia cha Urusi kuwa tayari
- Swift ni nini na kwa nini kupigwa marufuku Urusi ni muhimu sana?
Urusi na Ukraine: Urusi yaendelea kusonga mbele maeneo ya mashariki – Jeshi la Ukraine lathibitisha

Chanzo cha picha, Getty Images
Vikosi vya Ukraine vimetuma taarifa zake za hivi karibuni ikielezea hali ya mambo inasema:
- Juhudi kuu za vikosi vya Urusi zimeelekezwa juu ya maeno ya Severodonetsk na Bakhmut yaliyoko mashariki mwa nchi
- Wanavamia Severodonetsk, kwa usaidizi wa mizinga ya makombora. Mapigano yanaendelea katika mji.
- Vikosi vya Urusi vilirudi nyuma baada ya kushindwa kwa majaribio ya kusonga mbele kuelekea katika mji wa Bakhmut, hadi kusini-magharibi katika mji wa Severodonetsk
- Katika jimbo la Donetsk , Urusi inapiga makombora katika ngome za wanajeshi katika eneo lote kwa kutumia vifaru na ndege za kivita, lakini kasi ya kusonga mbele kwa Warusi katika eneo hilo ni ya chini, kwasababu jeshi limechoka na ari ni ya chini.
- Katika eneo la Lyman, Warusi wanajaribu kuchukua udhibiti wa ukanda wa kushoto wamto Seversky Donets.
BBC haijaweza kuthibitisha taarifa hizi kwa vyanzo huru vya habari

Unaweza pia kusoma:
- Je Putin atabonyeza mtambo wa nyuklia?
- Putin aamuru kikosi cha nyuklia cha Urusi kuwa tayari
- Swift ni nini na kwa nini kupigwa marufuku Urusi ni muhimu sana?
Urusi na Ukraine: Ndege ya kijeshi ya Ukraine yadunguliwa karibu na Odesa- Urusi

Chanzo cha picha, Gett
Urusi inasema kuwa vikosi vyake vimedungua ndege ya kijeshi ya Ukraine iliyokuwa inasafirisha silaha na zana za kivita karibu bandari ya Bahari nyekundu ya Odesa.
Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema katika taarifa zake kuhusu vita za siku ya Jumamosi kwamba ndege hiyo ilikuwa ikisafirisha silaha na zana za kivita.
Imesema pia kwamba shambulio la kombora katika kanda hiyo lilipiga eneo ambalo ni "kituo cha mamluki wa kigeni". Awali maafisa wa Ukraine waliripoti kuwa kiwanda cha kilimo kimepigwa na kombora katika eneo la bandari ya Odesa.
Wizara ya ulinzi Urusi ilisema pia kuwa makombora ya Urusi yalipiga kituo cha mafunzo ya makombora katika jimbo la Sumy nchini Ukraine ambako waalimu wa kigeni walikuwa wakitoa mafunzo kwa vikosi vya Ukraine.
BBC haijaweza kuthibitisha taarifa hizi kwa vyanzo huru.
Unaweza pia kusoma:
- Je Putin atabonyeza mtambo wa nyuklia?
- Putin aamuru kikosi cha nyuklia cha Urusi kuwa tayari
- Swift ni nini na kwa nini kupigwa marufuku Urusi ni muhimu sana?
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya mubashara leo Jumamosi tarehe 04.06.2022
