Urusi na Ukraine: 'Jiandaeni kwa vita vya muda mrefu ' uvamizi wa Ukraine ukiingia siku ya 100
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anasema kuwa vikosi vya Urusi vimeteka 20% ya eneo la nchi yake, wakati uvamizi wa Moscow ukifikia siku 100.
Moja kwa moja
Mume wa Osinachi akana kumuua mwimbaji huyo wa injili.

Mahakama kuu ya Abuja nchini Nigeria imeamuru kuwa mume wa marehemu aliyekuwa mwimbaji wa muziki wa Injili, Osinachi azuiliwe gerezani.
Peter Nwachukwu anashtakiwa kwa “kumshambulia mke wake akijua kwamba huenda madhara ya kifo yangetokea.
Mashtaka 23 yanayohusishwa na unyanyasaji wa nyumbani na mauaji ambayo yanaambatana na adhabu ya kifo yamefunguliwa dhidi yake.
Mashtaka hayo pia yalitaja unyanyasaji wa kihisia, lugha chafu na kisaikolojia. Alifikishwa mahakamani siku ya Ijumaa na kukana mashtaka hayo.
Polisi walimkamata Nwachukwu baada ya mkewe, nyota wa muziki wa injili nchini Nigeria kufariki katika hospitali ya Abuja. Tangu wakati huo amekuwa kizuizini huku polisi wakisema wanachunguza chanzo cha kifo chake.
Ripoti za awali zilidai Osinachi mweneye umri wa miaka 42 alikuwa anaugua saratani ya koo, lakini familia yake ilikanusha hilo, kwa madai kuwa alikuwa mwathirika wa unyanyasaji wa nyumbani. Walimshutumu mumewe kwa kumfanyia unyanyasaji na kusababisha kifo chake
Osinachi Nwachukwu,Mwimbaji wa Injili aliyejizolea umaarufu duniani kupitia wimbo wa injili Ekwueme, ambao umetazamwa mara milioni 71 kwenye mtandao wa YouTube ameacha watoto wanne.
- Mama yake Osinachi azungumza kwa mara ya kwanza
- Osinachi Nwachukwu: Mume wa mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Nigeria akamatwa baada kifo chake
Rais wa Senegal azungumza na Putin kuhusu athari ya vita kwa Afrika

Chanzo cha picha, AFP
Rais wa Senegal na mkuu wa Umoja wa Afrika, Macky Sall, amemwambia rais wa Urusi kwamba azingatie athari za uhaba wa chakula kwa bara la Afrika zinaosababishwa na mzozo wa Ukraine, shirika la habari la AFP limeripoti.
Marais hao wawili wamekutana katika mji wa kusini mwa Urusi wa Sochi. AFP inamnukuu Rais Sall akisema kwamba Rais Vladimir Putin atalazimika "kufahamu kwamba nchi zetu, hata kama ziko mbali na mzozo huo, pia ni waathirika katika ngazi ya uchumi" kutokana na mzozo huo.
Aliongeza kuwa umuhimu wa chakula unapaswa kuwa "nje" ya vikwazo vya Magharibi kwa Urusi. Kabla ya mzozo huo, zaidi ya 40% ya ngano inayotumiwa barani Afrika ilitoka Ukraine au Urusi.
Kabla ya kuondoka Senegal, ofisi ya rais Sall ilisema ziara hiyo ililenga kukomboa akiba ya nafaka na mbolea ambayo kwa sasa imezuiwa katika bandari za Ukraine.
Nchi za Afrika zinaathirika haswa kutokana na kupanda kwa bei kunakosababishwa na vita Hapo awali, shirika la habari la Reuters lilinukuu Kremlin ikisema kwamba Putin atatoa maelezo "ya kina" kuhusu kile kinachotokea kwa nafaka ya Ukraine.
Katika hotuba yake kwa umma baada ya mkutano huo, iliyonukuliwa na AFP, Putin alisema Urusi "siku zote iko upande wa Afrika".
- Urusi na Ukraine: Kitakachotokea iwapo Vradmir Putin atatangaza rasmi vita dhidi ya Ukraine
- Urusi na Ukraine: Hatuwezi kuruhusu nguvu ya kikatili itawale ulimwengu - Zelensky
- Mzozo wa UKraine: Umoja wa Ulaya wagawanyika juu ya msimamo vikwazo kwa Urusi
Siri ya Kuishi Muda Mrefu: Pata mke wa pili- Utafiti

Chanzo cha picha, Getty Images
Utafiti kutoka chuo kikuu cha Sheffield nchini Uingereza unapendekeza kuwa siri ya kuishi maisha marefu kunahusishwa na kuwa mke wa pili au zaidi.
Watafiti kutoka chuo hicho waliwachunguza wanaume wenye umri zaidi ya miaka 60 kutoka nchi 140 zinazotumia ndoa za mitala na wakagundua kwamba waliishi wastani wa asilimia 12 zaidi ya wanaume kutoka mataifa 49 yenye mke mmoja, kwa mujibu wa ripoti kutoka gazeti la Times of India.
Matokeo ya utafiti yaliwasilishwa wiki iliyopita katika mkutano wa kila mwaka wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ekolojia huko Ithaca, New York,
Watafiti waliangalia utafiti wa awali juu ya wanawake kujibu kwa nini wanaume wenye mitala huishi kwa muda mrefu.
Pia Wanasayansi wanaamini kuwa wanawake ambao wamekoma hedhi wanaishi kwa muda mrefu zaidi kuliko mamalia wengine kwa sababu kadiri wanavyoishi ndivyo wajukuu wengi zaidi wanavyolazimika kuwajali.
Kutunza wajukuu, inaonekana, kunawapa wanawake sababu ya kuishi muda mrefu baada ya kushindwa tena kuzaliana.
Kupenda wajukuu, hata hivyo, hakuna faida sawa za kuongeza maisha kwa wanaume kwani wanaume wanaweza kuzaliana katika miaka ya 60, 70 na 80. Hivyo watafiti wanasema, kwamba wanaume wenye wake wengi hupata aina fulani ya athari za baba, wakimaanisha, kadiri wanavyokuwa na wake wengi, ndivyo wanavyozaa watoto zaidi.
Kuzaa watoto huwapa sababu ya kuendelea kuishi muda mrefu zaidi kuliko wanaume wenye mke mmoja ambao mara nyingi huacha kuzaa watoto katika umri wa mapema zaidi, watafiti walihitimisha.
- Ndoa ya mitara: 'Sisi ndugu wanne tulioa mke mmoja'
- Wanawake wa Kiislamu nchini India wapinga ndoa za wake wengi
- Unaujua uzuri wa kumuoa mkeo zaidi ya mara moja?
Tume ya uchaguzi Kenya yajibu kuhusu madai ya kuhamishwa kwa wapiga kura

Chanzo cha picha, AFP/GETYY
Tume ya uchaguzi nchini Kenya (IEBC) imejitetea kuhusu kuhamishwa kwa orodha ya wapiga kura kabla ya uchaguzi wa urais kufanyika Agosti.
Tume ya uchaguzi imekiri kwamba kumekuwa na uhamishaji wa maeneo ya wapiga kura kinyume cha sheria, lakini imesema kuwa uchunguzi kuhusu suala hilo unafanyika.
Katika kipindi chote cha mwezi Mei, wapiga kura kote nchini wamekuwa wakithibitisha maelezo yao katika tume hiyo , shughuli iliyomalizika tarehe 2 Juni. Hatahivyo baadhi ya wapiga kura wamekuwa wakilalamika kuwa majina yao yamehamishiwa kwenye maeneo mapya ya kupigia kura bila idhini yao.
Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati, anawalaumu maafisa wa usajiri katika majimbo 290 ya uchaguzi, na kaunti 47 kwa kufanya makosa ana akawaonya kuwa tume hiyo itachukua hatua dhidi wale wote waliohusika.
Unaweza pia kusoma:
- Uchaguzi wa Kenya 2022: Je ahadi za serikali ya Jubilee kwa Wakenya zimetimizwa?
- Uchaguzi Kenya 2022: Habari potofu zinazosambaa mtandaoni
- Uchaguzi Kenya 2022: Kwa nini uchaguzi wa Kenya mwaka huu ni muhimu?
Habari za hivi punde, Meli za Urusi huko Pasifiki kuanza mazoezi ya wiki nzima -kunani?
Jeshi la Urusi la Pacific Fleet limezindua mfululizo wa mazoezi ya wiki moja huku meli zaidi ya 40 na hadi ndege 20 zikishiriki, mashirika ya habari ya Urusi yalinukuu wizara ya ulinzi ikisema.
Taarifa ya wizara hiyo ilisema mazoezi hayo, yanayofanyika kuanzia tarehe 3 hadi 10 Juni, yatahusisha, miongoni mwa mambo mengine, "vikundi vya meli vitashiriki katika shughuli za utafutaji wa manowari za [adui]".
Watu wasiojulikana 'waiba makaburi' Msumbiji

Chanzo cha picha, AFP
Wakaazi wa mji wa Beira katika jimbo la kati la Msumbiji la Sofala wametaka ulinzi wa makaburi ya eneo hilo huku kukiwa na ripoti za uharibifu wa makaburi. Katika makaburi ya Mangalane, zaidi ya makaburi 50 yameharibiwa katika muda wa mwezi mmoja uliopita.
Wahalifu hao wanaiba misalaba ya shaba na vitu vingine vya chuma. Kiongozi wa kimila anayehusika na makaburi hayo, Fernando Jaime, alisema vitendo vya unajisi vimekuwa vikifanyika mchana kweupe.
"Wanachukua misalaba na vitu vingine vya watu waliokufa wanavyovikuta kando ya kaburi. Wanaweka vitu hivi pamoja na kuviuza kwa chakavu," aliambia vyombo vya habari vya ndani.
Carlos Cassicussa mkazi wa kitongoji cha Mungassa alisema hali hiyo inatokana na kuporomoka kwa maadili. “Hii tabia ni mbayakwa kweli, wizara ya mambo ya ndani ichukue hatua waje makaburini hata saa sita mchana,” alisema.
Urusi imefanikiwa katika vita mashariki mwa Ukraine, lakini imewagharimu pakubwa - Uingereza
Urusi sasa inapata "mafanikio ya kimbinu" katika eneo la mashariki la Donbas nchini Ukraine, lakini mafanikio hayo yamekuwa kwa "gharama kubwa ya rasilimali", Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema katika waraka wake hivi punde la kijasusi.
Maswali yanasalia kuhusu uamuzi wa Moscow wa kuelekeza zaidi "nguvu na mashambulizi" yake kwenye sehemu moja ya kampeni nzima ya vita ya Ukraine. Ukirudi nyuma katika siku 100 tangu Urusi kuvamia jirani yake, Mod inakumbusha mpango wa awali wa Vladimir Putin ulikuwa ni- kunyakua mji mkuu wa Kyiv na kupindua serikali ya Ukraine - umeshindwa.
Hata hivyo, asilimia 90% ya mji wa Luhansk - sehemu ya mkoa wa Donbas - sasa inadhibitiwa na Urusi, chapisho hilo lilisema. Na kuna uwezekano Putin atakuwa na udhibiti kamili wa eneo hilo katika muda wa wiki mbili zijazo.

Chanzo cha picha, g
Lebron James awa mchezaji wa kwanza bilionea akicheza ligi ya NBA

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Lebron James LeBron James– Nyota mara 18 wa mpira wa vikapu nchini Marekani NBA na bingwa mara 4 wa NBA, mbali na kuwa mshindi wa medali ya dhahabu mara 2 kwenye Olimpiki – amepiga hatua nyingine muhimu, wakati huu akifanya kitu ambacho hakuna mchezaji mwingine wa NBA amewahi kufanya.
Baada ya mwaka mwingine mbaya wa mapato– ya jumla ya dola milioni 121.2 mwaka jana–Forbes inakadiria kuwa James amekuwa bilionea rasmi, huku akiendelea kushiriki katika mchezo huo.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 37 ana utajiri wa dola bilioni 1, kulingana na hesabu ya Forbes. James, ambaye amekosa mechi za mchujo kwa mara ya nne pekee katika misimu wake wa 19, ndiye mchezaji wa kwanza wa NBA aliye hai kuingia katika orodha ya mabilionea. (Michael Jordan, bilionea mwingine pekee wa mpira wa vikapu, hakufikia ubilionea hadi 2014 - zaidi ya muongo mmoja baada ya kustaafu, kufuatia hatua yake ya kuwekeza katika timu ya mpira wa vikapu ya Charlotte Hornets.)
Tazama Video inayomuonyesha mwanamke aliyeweka rehani maisha yake kwa sababu ya maji India

Chanzo cha picha, ANI
Maelezo ya picha, Mwanamke ahatarisha maisha yake ili kupata maji India Video hiyo inamwonyesha mwanamke huyo akiteremka katika kisimani kirefu bila kamba ili kwenda kuchota maji.
Watu katika kijiji cha Ghusiya wamelazimika kuchukua hatua hizo kali baada ya visima na madimbwi kukauka.
Maeneo mengine kadhaa kote India yanakabiliwa na shida kama hiyo ya maji.
Video zinazoonyesha raia wa India wakihatarisha maisha yao ili kupata maji husambazwa mara kwa mara. Mnamo Aprili, video kama hiyo ilionyesha mwanamke akishuka kwenye kisima katika jimbo la Maharashtra kupata maji.
Ripoti ya kimataifa ya 2019 ilikuwa imeitaja India kuwa moja kati ya nchi 17 ambapo "matatizo ya maji yalikuwa juu".
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Wananchi wengi wa India kwenye mitandao ya kijamii waliguswa na video ya waliyoiita ni ya "kuvunja moyo" na kuwataka maafisa kusaidia kijiji hicho haraka.
India ndio mchimbaji mkubwa zaidi wa maji ya ardhini duniani - wengi bado wanategemea maji hayo kwa usambazaji wao wa kila siku wa maji.Lakini karibu theluthi mbili ya wilaya za nchi hiyo zinatishiwa na kushuka kwa kiwango cha maji chini ya ardhi, Benki ya Dunia inasema.India inakadiriwa kukabiliwa na matatizo makubwa ya maji ifikapo mwaka 2050, huku miji 30 ikisemekana kuwa katika maeneo yenye hatari kubwa zaidi.
Platinum Jubilee: Malkia ajiondoa katika ibada kuu ya Kanisa la St Paul leo

Maelezo ya picha, Malkia Elizabeth wa pili Malkia hatohudhuria ibada ya Ijumaa ya Jubilee katika Kanisa Kuu la St Paul baada ya kutojisikia vyema wakati akitazama gwaride la Alhamisi kwenye kasri la Buckingham.
Uamuzi huo ulifanywa kwa "kusitasita" baada ya kuzingatia "safari na shughuli zinazohitajika", ikulu ilisema.
Hatahivyo alishiriki katika hafla ya kuwasha taa Alhamisi jioni.
Siku nne za sherehe za kuadhimisha utawala wa miaka 70 wa Malkia zilianza mapema.
Mfalme huyo mwenye umri wa miaka 96 alionekana mara mbili kwenye Jumba la Buckingham, akiwa amezungukwa na washiriki wengine wakuu wa familia ya kifalme, walipokuwa wakitazama gwaride la kijeshi na kuwapungia mkono maelfu ya watu waliokusanyika kwenye The Mall.
Saa chache baada ya sherehe hiyo, ikulu ilithibitisha kuwa hatohudhuria ibada ya Ijumaa, lakini akasema "angependa kuwashukuru wale wote waliofanya siku ya Alhmisi kua yenye kukmbukumbu nyingi".
Vita vya Ukraine: Makubaliano ya Magharibi dhidi ya Urusi yataendelea kwa muda gani?

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Viongozi wa mataifa ya Ulaya pamoja na rais wa Marekani Joe Biden Huku majeshi ya Urusi yakipiga hatua polepole katika eneo la Donbas mashariki na wataalam wa kijeshi wakizungumzia vita virefu vya mvutano, je, nyufa zimeanza kuonekana katika uungaji mkono wa nchi za Magharibi kwa Ukraine?
Akiongoza mapigano kutoka kwenye kumbi nyeupe zinazometa za Kremlin, Vladimir Putin anafanya nini kuhusu mijadala inayozunguka Magharibi kuhusu njia bora ya kuiunga mkono Ukraine, na ni kwa kiwango gani Urusi inapaswa kuadhibiwa?
Katika kona moja, anaona serikali za Uingereza, Poland na Baltic zikitoa wito wa kushindwa kwake.
"Tunahitaji kuhakikisha kuwa Urusi inafukuzwa kutoka Ukraine na Waukraine," Waziri wa Mambo ya nje Liz Truss alisema wiki iliyopita.
"Hakuwezi kuwa na maelewano yoyote juu ya eneo la Ukraine."
Lakini katika kona nyingine, Bw Putin anaona viongozi wa Ufaransa, Ujerumani na Italia wakitoa wito wa kuweko kwa mbinu tofauti ya kukabiliana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Urusi inashambulia mji wa Severodonetsk kutoka pande zote - Gavana

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Mwanajeshi wa Urusi Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anasema kuwa vikosi vya Urusi vimeteka 20% ya eneo la nchi yake, wakati uvamizi wa Moscow ukikaribia siku kufikia siku 100.
Akiwahutubia wabunge wa Luxembourg, aliongeza kuwa eneo la makabiliano limepanuka na kufikia kilomita zaidi ya kilomita 1,000 (maili 621).
"Makundi yote ya kijeshi ya Urusi yaliyo tayari kupigana yanahusika katika uvamizi huu," aliwaambia wabunge kupitia kanda ya video.
Vikosi vya Urusi vimekuwa vikizidisha mashambulizi kwenye mji wa Severodonetsk katika eneo la Donbas mashariki.
Maafisa wa ulinzi wa Uingereza wanasema Urusi imeteka sehemu kubwa ya jiji hilo na inapata "mafanikio ya ndani, yanayowezeshwa na mkusanyiko mkubwa wa mizinga".
Severodonetsk ni mji wa mashariki kabisa chini ya udhibiti wa Ukraine na gavana wa eneo hilo Serhiy Haidai alisema Urusi ilikuwa inajaribu kuvunja ngome ya ulinzi katika mji huo "kutoka pande zote".
Natumai hujambo
