Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Urusi na Ukraine: Mapigano yanaendelea mashariki mwa Ukraine

Maelezo zaidi sasa kutoka Severodonetsk - jiji lililozingirwa huku Urusi ikijaribu kuliteka eneo lote la mashariki mwa Ukraine la Luhansk.

Moja kwa moja

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu mubashara kwa leo, jiunge nasi tena hapo kesho majaaliwa

  2. Uingereza: Mwanamke afungwa jela kwa kumuua mtoto aliyetakiwa kumlea

    Mwanamke mmoja nchini Uingereza amehukumiwa kifungocha miaka 18 jela kwa kumuua mtoto mchanga wa kiume.

    Laura Castle alimuua Leiland-James Corkill aliyekuwa na umri wa miezi 13 mwezi Januari 2021.

    Katika kesi dhidi yake, alikiri kosa la kuua bila kukusudia, lakini mahakama ilimpata na hatia ya kuua kwa kukusudia.

    Mume wake, Scott Castle, aliondolewa shitaka la kuua au kusababishakifo cha mtoto huyo mchanga.

    Laura, mwenye umri wa miaka 38, alifungwa kifungo cha maisha lakini anaweza kufungwa miaka walau 18.

    MhakamaniBi Laura aliangua kilio wakati alipokuwa akisomewa hukumu yake , lakini alilia zaidi ujumbe wa mama mzazi wa mtoto ulipokuwa ukisomwa ambaye alimuita "myama".

    Leiland-James alitolewa kwa laura na mume wake Scott in tarehe 8 Agosti , 2020 alipokuw ana umri wa miezi minane. Wakati alipozaliwa alipelekwa kwenye kituo cha kulelea watoto wachanga kilichopo Cumbria, kaskazini-magharibi mwa Uingereza

    Mahakama ilisikiliza ujumbe wa mume wake ambao mkewe alimtumia alipokuwa kazini akimkosoa mtotoLeiland-James, huku akimuita majina mabaya, akielezea pia jinsi ’’alivyompiga sana".

    Baadaye usiku majira ya saa mbili na dakika 15 laura alipiga simu kwa polisi akisema mtoto Leiland amepoteza fahamu baada ya kuanguka kutoka kwenye kiti, na kwamba alikuwa anapumua vibaya.

    Mtoto Leiland-james alifariki siku iliyofuata.

  3. Madaktari waonya juu ya upasuaji wa kupunguza uzito nje ya nchi

    Madaktari katika nchi ya Scotaland wameonya wale wanaokwenda kufanyiwa upasuaji wa kupunguza uzito nje ya nchi kuwa sio salama kutokana na kushindwa kufuatiliwa na wataalamu wa kiafya baada ya upasuaji.

    Kampuni moja nchini Scotland inasema kwamba husaidia wagonjwa kukabiliana na unene kupita kiasi kwa kuwasafirisha hadi Uturuki kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji.

    Lakini madaktari wa upasuaji nchini humo wanasema huduma ya afya sasa zimekuwa msaada pale upasuaji unapokwenda tofauti.

    Daktari wa upasuaji wa Chuo cha Edinburgh, De Beaux alisema kuwa katika bodi ya huduma ya afya, mwaka jana kulikuwa na rufaa 33 za haraka kwa ajili ya usaidizi wa kimatibabu kwa watu waliopata upasuaji wa kupunguza uzito nje ya nchi na kufanyika vibaya.

    "Katika miezi mitatu iliyopita tumekuwa na wagonjwa wawili ambao wameshuka kwenye ndege na kulazwa hospitalini na bado wako hospitalini," alifafanua.

    Mmoja wa madktari kutoka Midlothian Dr Becky Harley, anasema ameona ongezeko la idadi ya wagonjwa wanaorudi kutoka kwa upasuaji nje ya nchi na kuhitaji ushauri wa ziada wa lishe na kisaikolojia.

    "Inaonekana wakati wagonjwa wanapata upasuaji huu nje ya nchi, mara nyingi watarudi na hakuna ufuatiliaji huo hivyo inaweza kusababisha hatari kwa wagonjwa."Utafiti wa 2021 ulioongozwa na Chuo Kikuu cha Glasgow uligundua kuwa wagonjwa nchini Scotland wanaofanyiwa tathmini ya upasuaji wa kupunguza uzito ni watu wazima na wanye uzito mkubwa kuliko wastani wa kimataifa.

    Upasuaji wa kupunguza uzito hutolewa katika nchi kadhaa za Ulaya, zikiwemo Poland na Uturuki.

    • Gharama za kitambi ni sawa na za uvutaji
    • Utafiti: Unene wahusishwa na aina 11 za saratani
    • Je unajua madhara ya njia za mkato katika kutafuta kupunguza unene wa mwili wako?
  4. Habari za hivi punde, Vita vimeongezeka kwa kiwango cha juu Donbas – Waziri wa Ukraine

    Naibu waziri wa ulinzi wa Ukraine anasema mapigano ya Donbas yamefikia kiwango cha juu zaidi, huku Warusi wakivamia maeneo ya Ukraine katika maeneo kadhaa kwa wakati mmoja.

    "Kuanzia leo, mvamizi aemfanya mashambulio makali katika eneo la makabiliano huko Donetsk. Adui anatumia silaha za roketi, angana mizinga’’ Hanna Maliar anasema

    "Hali ni ngumu na kuna dalili ya kuwa mbaya zaidi. Adui ametumia rasilimali zote kuteka eneo letu na kuzingira vikosi vyetu. Mapigano yamefikia kiwango cha juu zaidi. Adui anashambulia maeneo yetu kutoka sehemu tofauti kwa wakati mmoja. Tuko katika harakati za mapambano ya muda mrefu."

    Hapo awali, mamlaka huko Donbas ilisema Warusi walishambulia zaidi ya makazi 40 katika harakati zao za kuiteka miji ya kimkakati ya Severodonetsk na Lysychansk, shirika la habari la AFP linaripoti.

  5. Visa vinavyoshukiwa kuwa ni vya maradhi ya monkeypox vyabainika Morocco na Sudan

    Morocco na Sudan zinachunguza visa vinavyoshukiwa vya ugonjwa wamonkeypox, imesema taasisi hiyo ya afya barani.

    Hii inakuja baada ya milipuko ya virusi kubainika hivi karibuni barani Ulaya, Australia na Mashariki ya Kati.

    Monkeypox kwa kawaida huhusiana na safari za kuelekea katika maeneo ya kati na magharibi mwa Afrika, karibu na misitu ya kitropiki, lakini baadhi ya visa vipya havina uhusiano wowote na safari.

    Wakati wa mazungumzo na waandishi wa habari Dkt Ahmed Ogwell, naibu mkurugenzi wa Taasisi ya udhibiti wa magonjwa (CDC) alithibitisha kuwa hapakuwa na uhusiano wa moja kwa moja na safari za kuelekea maeneo yanayohusishwa na Monkeypox.

    Alisema kuwa bara la Afrika hadi sasa limeripoti visa1,405 na vifo 62 vinavyohusiana na monkeypox- mwaka huu-kikiwa ni kiwango cha 4.4%

    Watu hawa wenye Monkeypox walipatikana katika nchi nne ambako maradhi haya nadra yalipatikana : Cameroon, Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Nigeria.

    Dkt Ogwell amesema kuwa nchi zote za Kiafrika zimeshauriwa kuongeza kiwango chake cha ufuatiliaji na upimani wa ugonjwawa Monkeypox.

    Monkeypox, ambayo ni maambukizi ambayo sio makali sana, yanaweza kusambaa wakati mtu anakaribianana mtu mwenye maambukizi.

    Dalili za mwanzo ni pamoja na homa, maumivu ya kichwa, uvimbe, maumivu ya mgongo. Maumivu ya misuli- na upele unaweza kujitokeza wakati homa inapojitokeza.

    Inadhaniwa kuwa inasambaa kwa panya, na kindi.

    Kunawa mikono ni muhimu sana kwani ni ugonjwa unaosambaa kwa kusalimiana ” Dkt Ogwell alisema.

    Pia ameshauri watu kuepuka kuwagusa Wanyama wanaoonekana kuumwa na wale wanaofahamika kubeba virusi vya maambukizi.

    Chanjo ya tetekuwanga inatolewa Afrika, Dkt Ogwell amesema.

    “Chanjo iliyopo ya tetekuwanga itapewa kipaumbele kwa wahudumua wa afya na maeneo yaliyothibitishwa kuwa na virusi hivyo,” alisema.

    Unaweza pia kusoma:

    • Ufahamu ugonjwa hatari wa Monkeypox
    • Monkeypox: Ugonjwa huu unaweza kuwa janga?
  6. Urusi yakana kuzuia mauzo ya nafaka kutoka Ukraine

    Urusi imekanusha madai ya Marekani na Umoja wa Ulaya kwamba inazuia mauzo ya nafaka kutoka Ukraine, na kuzishutumu nchi za Magharibi kwa kuunda hali hiyo kwa kuweka vikwazo.

    Wakulima wa Ukraine wana tani milioni 20 za nafaka ambazo hawawezi kuziuza katika masoko ya kimataifa kutokana na uvamizi unaoendelea.

    "Hatukubali kabisa shutuma hizi. Kinyume chake, tunalaumu nchi za Magharibi kwa kuchukua hatua ambazo zimesababisha hili," msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov aliwaambia waandishi wa habari.

    Moscow ilizitaka nchi za Magharibi kuondoa vikwazo ambavyo inasema vinazuia mauzo ya nafaka kutoka Ukraine.

    Mkuu wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen alisema mapema wiki hii Urusi ilikuwa ikitumia "njaa na nafaka kutawala", huku Ukraine ikiishutumu Urusi kwa kuiba mamia ya maelfu ya tani za nafaka katika maeneo ambayo majeshi yao yameteka.

  7. Hatuwezi kumruhusu Putin kushinda vita hivi - Kansela wa Ujerumani

    Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amekuwa akitoa hotuba ya nusu saa yenye maswali na majibu mafupi katika siku ya mwisho ya Kongamano la Kiuchumi la Dunia huko Davos.

    Analaani uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, lakini hataji ukosoaji unaotolewa dhidi ya serikali yake kwa kuchelewa sana kupeleka silaha nzito kwa Ukraine.

    "Nguvu kubwa ya kinyuklia inatenda kana kwamba ina haki ya kuchora upya mipaka," anasema.

    "Putin anataka kurejea kwa utaratibu wa ulimwengu ambao nguvu huamuru kile kilicho sawa, ambacho uhuru, uamuzi na uhuru sio wa kila mtu.

    "Hatuwezi kumruhusu Putin kushinda vita hivi," anasema, na kuongeza "hakutakuwa na amani iliyoamriwa".

    Scholz amekuwa akishtumiwa nchini Ujerumani na nje ya taifa hilo. Wakosoaji wanasema anaonekana kusitasita kuiunga mkono Ukraine kijeshi.

    Lakini katika hotuba yake, anasema Ujerumani inakamilisha kile kinachojulikana kama "Zeitenwende" au hatua ya kubadilisha sera ya kigeni, kwa kusambaza silaha kwenye eneo la vita kwa mara ya kwanza, kutumia € 100bn ($ 107bn, £ 85bn) kwa jeshi lake na kupunguza utegemezi wake kwa nishati ya Kirusi.

  8. Habari za hivi punde, Wanajeshi wa Urusi wauzingira mji wa Severodonetsk Ukraine

    Maelezo zaidi sasa kutoka Severodonetsk - jiji lililozingirwa huku Urusi ikijaribu kupata eneo lote la mashariki mwa Ukraine la Luhansk.

    Jiji hilo limekuwa chini ya "mashambulizi ya wa mara kwa mara" kwa wiki moja na nusu iliyopita, kulingana na mkuu wa utawala wa ndani wa kijeshi na kiraia.

    Takriban 90% ya nyumba zimeharibiwa na mapigano, Oleksandr Stryuk anakiambia kituo cha redio cha NV cha Ukraine.

    Takriban watu 12,000-13,000 bado wanafikiriwa kuwa katika jiji hilo, Stryuk anasema - wengi wao wakihifadhwai katika vyumba vya chini ya ardhi.

  9. Naibu rais wa Kenya William Ruto amuomba msamaha Rais Kenyatta

    Naibu Rais wa Kenya William Ruto amemwomba Rais Uhuru Kenyatta msamaha baada ya wawili hao kutofautiana pindiu tu baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa 2018.

    Tofauti kati ya Rais Kenyatta na naibu wake zimekuwa wazi.

    Rais haungi mkono azma ya Bw Ruto ya kuwania urais katika uchaguzi wa Agosti na badala yake anamuunga mkono kinara wa upinzani Raila Odinga.

    Wakati wa mkutano wa kila mwaka wa maombi ya Alhamisi ulioandaliwa na bunge, Bw Ruto alimwomba rais msamaha.

    "Pia najua kuwa kuhudumu kama naibu wa rais huenda sikufikia matarajio ya bosi wangu, Rais Kenyatta na ninaomba unisamehe," alisema.

    Aliendelea kumtakia rais kustaafu kwa amani.

    Bw Kenyatta anamaliza muhula wake wa pili na wa mwisho mwaka huu.

    Rais hana mamlaka ya kumtimua naibu wake - anaweza kuondolewa tu madarakani iwapo atapigiwa kura bungeni au kutukuwa na uwezo.

    Hii hapa video ya wakati Bw Ruto alipotoa matamshi hayo kama ilivyorushwa na NTV Kenya;

  10. Polisi wa Nigeria wanamkamata mlaghai wa mtandaoni anayesakwa

    Kitengo cha uhalifu wa mtandaoni nchini Nigeria kimemkamata mwanamume mwenye umri wa miaka 37 anayedaiwa kuwa mkuu wa kundi la kimataifa la uhalifu wa mtandaoni.

    Kundi hilo lilizindua kampeni kadhaa za kilaghai na miradi ya maelewano ya barua pepe za biashara inayolenga makampuni na waathiriwa binafsi, kulingana na taarifa ya Interpol.

    Raia huyo wa Nigeria alikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Murtala Mohammed mjini Lagos katika operesheni - iliyopewa jina la Delilah - iliyohusisha mabara manne, ilisema.

    "Natumai matokeo ya Operesheni Delilah yatasalia kama ukumbusho kwa wahalifu wa mtandao kote ulimwenguni kwamba vyombo vya sheria vitaendelea kuwafuatilia, na kwamba kukamatwa huku kutaleta faraja kwa wahasiriwa wa kampeni zinazodaiwa za mshukiwa," alisema Inspekta Jenerali Msaidizi wa Nigeria.

    Garba Baba Umar. Interpol ilisema kumekuwa na ongezeko la aina nyingi za uhalifu wa mtandao katika miaka ya hivi karibuni.

    Soma:

  11. Djimi Traore: Fainali ya Ligi ya Mabingwa 'inaweza kuamua Ballon d'Or'

    Matokeo ya mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa kati ya Liverpool na Real Madrid yanaweza kuamua mshini wa mwaka huu wa tuzo ya Ballon d'Or, kulingana na mlinzi wa zamani wa Reds Djimi Traore.

    Mchezaji huyo ambaye alikuwa beki wa kushoto wakati klabu hiyo ya Anfield ilipotwaa kombe mwaka wa 2005 anadhani mshambuliaji wa Senegal Sadio Mane yuko katika kinyang'anyiro cha kuwania tuzo hiyo - lakini anasema anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa mshambuliaji wa Real na Ufaransa Karim Benzema.

    Benzema, 34, amefung amabao 15 Ulaya msimu huu na kuwezesha miamba hao wa Uhispania kukutana na goals in Europe this Liverpool mjini Paris Jumamosi hii.

    Mane alikuwa kiungo muhimu katika ushindi wa kwanza wa Senegal wa taji la Kombe la mataifa ya Afrika mwezi Februari na kusaidia Teranga Lions kufuzu kwa Kombe la Dunia 2022, Huku nyota huyo wa miaka 30- akishindia klabu yake makombe mawili ya nyumba msimu huu.

    "Nadhani Karim Benzema yuko katika hali nzuri maishani mwake - anafanya vyema," Traore aliiambia BBC Michezo Afrika.

    "Nadhani mshindi wa Ligi ya Mabingwa, zawadi ya mtu binafsi itakuwa kama kushinda Ballon d'Or. Hivi sasa inaonekana itakuwa kati ya Benzema na Mane."

    Walioteuliwa kuwania tuzo ya Ballon d'Or mwaka huu watatangazwa tarehe 12 Agosti, huku mshindi akitangazwa katika hafla itakayofanyika Paris mnamo Oktoba 17.

    Waandalizi wa Soka ya Ufaransa wameamua kuwa zawadi hiyo sasa itaamuliwa kutokana na uchezaji wake katika msimu mmoja badala ya mwaka wa kalenda, ambao ulikuwa muundo wa awali.

    Pambano la Jumamosi kati ya Real Madrid na Liverpool mjini Paris ni mechi ya marudiano ya fainali ya Ligi ya Mabingwa 2018, wakati Wahispania hao waliibuka washindi 3-1 na kutwaa taji lao la 13 la Uropa.

    Soma zaidi:

  12. Vita vinaweza kusababisha mdororo mkubwa wa kiuchumi duniani -Benki ya Dunia

    Mkuu wa Benki ya Dunia ameonya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine unaweza kusababisha mdororo wa kiuchumi duniani - huku bei za vyakula, nishati na mbolea zikipanda.

    David Malpass anasema nchi nyingi za Ulaya bado zinategemea sana Urusi kwa mafuta na gesi. Anasema hatua za Urusi kupunguza usambazaji wa gesi zinaweza kusababisha "kupungua kwa kiasi kikubwa" katika eneo hilo.

    Anaongeza bei ya juu ya nishati tayari ina uzito kwa Ujerumani, moja ya nchi zenye uchumi mkubwa zaidi duniani.

    Urusi na Ukraine ni baadhi ya wazalishaji wakubwa wa mbolea na chakula, na Malpass, akizungumza nchini Marekani jana, alisema nchi zinazoendelea tayari zimeathiriwa na uhaba.

    Maelezo zaidi:

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
    • SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
  13. Watoto wachanga 11 wafariki kwa moto katika hospitali Senegal

    Watoto 11 waliozaliwa wamefariki kwenye moto uliotokea katika hospitali moja iliyopo mji wa Tivaouane, magharibi mwa Senegal, rais wa nchi hiyo alisema siku ya Jumatano.

    Rais Macky Sall alisema "kujifunza kwa uchungu na kufadhaika kuhusu vifo vya watoto 11 wachanga katika moto uliotokea kwenye idara ya watoto wachanga ya Hospitali ya Mame Abdou Aziz Sy Dabakh huko Tivaouane".

    "Kwa mama zao na familia zao, ninawapa pole sana," Sall alisema kupitia ukurasa wake wa Twitter.

    Tivaouane iko karibu 120km (maili 75) mashariki mwa mji mkuu, Dakar.

    Moto huo ulisababishwa na "Shoti ya umeme", mwanasiasa wa eneo hilo Diop Sy alinukuliwa akisema.

    Hospitali hiyo inasemekana ilizinduliwa hivi karibuni.

  14. Urusi yashambulia miji 40 katika mikoa ya Donbas na Luhansk

    Vikosi vya Urusi vimeshambulia zaidi ya miji 40 katika maeneo ya mashariki huko Donbas na Luhansk, jeshi la Ukraine lilisema.

    "Wavamizi walifyatua risasi katika miji zaidi ya 40 katika mkoa wa Donetsk na Luhansk, na kuharibu maeneo 47 ya raia, pamoja na nyumba 38 na shule.

    Kutokana na shambulio hilo raia watano walikufa na 12 walijeruhiwa," Kikosi Kazi cha Pamoja cha Ukraine kilisema

    Katika mwezi uliopita, Urusi imefunza mwelekeo wake wa kuchukua udhibiti kamili wa eneo la Donbas.

    Urusi imetuma maelfu ya wanajeshi katika eneo hilo, na kushambulia kutoka pande tatu katika jaribio la kuzingira vikosi vya Ukraine vinavyoshikilia katika miji ya Severodonetsk na Lysychansk.

    Kuanguka kwao kungeacha jimbo lote la Luhansk chini ya udhibiti wa Urusi, lengo kuu la vita vya Kremlin.

    Siku ya Jumapili, Gavana wa Luhansk Serhiy Gaidai alikuwa ameishutumu Urusi kwa kutumia "mbinu ya dunia iliyoungua" katika juhudi zake za kukamata Severodonetsk.

    Bw Gaidai alionya kuwa vikosi vya Urusi vimeharibu daraja lote isipokuwa moja katika mto Donets na kusema kuwa jiji hilo liko katika hatari ya kukatwa.

    Maelezo zaidi:

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
    • SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
  15. Mapigano DR Congo: Maelfu ya raia waliokimbia makazi yao "wanahitaji chakula haraka"

    Takriban watu 80,000 wamekimbia makazi yao katika jimbo la Kivu Kaskazini kutokana na mapigano ya hivi karibuni na yanayoendelea kati ya jeshi na waasi wa M23, Umoja wa Mataifa unasema.

    Mapigano yalianza katika eneo la Rutshuru kabla ya kuenea chini mapema wiki hii hadi kilomita 20 kutoka Goma, mji mkuu wa jimbo hilo.

    Mapigano siku ya Jumanne yalisababisha kuondoka kwa makazi katika eneo la Kibumba takriban raia 10,000 waliokimbilia katika mazingira ya Goma, ofisi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kibinadamu, OCHA, ilisema katika taarifa yake.

    Wengine wengi wamekimbia eneo hilo hilo kutokana na mapigano makali ya Jumatano; chanzo cha mashirika ya kiraia kimeiambia BBC Idhaa ya Maziwa Makuu.

    Takriban watu 80,000, wengi wao wakiwa wakimbizi wa ndani, wamekimbilia katika maeneo yaliyoboreshwa, makanisa, na shule, na wengi wao "wanahitaji chakula na msingi muhimu", inasema OCHA.

    Mashirika ya kibinadamu yanahofia hali mbaya zaidi kwa wakimbizi ikiwa uhasama utaendelea. Katika taarifa ya Jumatano jioni, msemaji wa gavana wa jimbo hilo Jenerali Sylvain Ekenge alisema "wanakabiliwa na hali hii ya wasiwasi".

    "Gavana wa kijeshi wa jimbo la Kivu Kaskazini anatoa wito kwa wakazi kuwa watulivu na waangalifu, na wasiache hofu," Jenerali Ekenge aliongeza.

    Waasi wa M23 wanaripotiwa kudhibiti baadhi ya maeneo katika umbali wa Km 25 kutoka Goma, lakini Jenerali Ekenge alisema mashambulizi ya waasi yamerejeshwa nyuma.

  16. ‘Jeshi la Putin limeanza kupata mafanikio fulani katika eneo la Donbass’

    Jeshi la Vladimir Putin limeanza kuonyesha mafanikio fulani - Vikosi vya Urusi vinapiga hatua katika eneo la Donbass.

    Katika siku chache zilizopita, wameteka miji na vijiji kadhaa, na kuwalazimu Waukraine kurudi kwenye nafasi zao kwa ulinzi.

    Urusi inapata mafanikio haya, shukrani hii kwa faida ya nambari tu, silaha, mizinga na ndege.

    Asubuhi, gavana wa mkoa wa Luhansk alisema katika mahojiano kwamba "kuna wanajeshi wengi wa Urusi wanaopinga Vikosi vya Wanajeshi." Kulingana na Rais Volodymyr Zelensky, kuna Warusi saba kwa askari mmoja wa Kiukreni katika eneo hilo.Malengo ya Urusi sasa ni miji ya Severodonetsk na Lysychansk.

    Lazima kuwe na vikosi vingi vya Kiukreni, vilivyoimarishwa na tayari kwa vita virefu. Walakini, wanakabiliwa na tishio kwamba wanaweza kutengwa na wengine na kukandamizwa kwa faida ya nambari.Hilo likitokea, Ukraine inaweza kupoteza baadhi ya wanajeshi wake bora.

    Lakini si kila kitu kinapotea kwa Waukraine. Wana msaada mkubwa wa kijeshi wa kimataifa katika uwezo wao - zote mbili zinazotolewa na Wanajeshi na wale walio barabarani.

    Nyingi za silaha hizi ni za juu zaidi kuliko zile zinazotumika sasa huko Donbass.Swali ni ikiwa Vikosi vya Wanajeshi vitakuwa na wakati wa kutumia vizuri faida hii ya kiteknolojia kabla ya jeshi la Urusi kuwakandamiza.

    Maelezo zaidi:

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
    • SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
  17. Hujambo na karibu katika matangazo ya moja kwa moja leo Alhamisi 26.05.2022.