Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Urusi na Ukraine: Nato inahitajika sasa kuliko wakati wowote- Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden, amefanya mkutano na waandishi wa habari pamoja na Waziri Mkuu wa Uswidi Magdalena Andersson na Rais wa Finland Sauli Niinistö.
Moja kwa moja
Wanachama wapya wanaojiunga na Nato sio tishio – Biden
Rais wa Marekani Joe Biden, amefanya mkutano na waandishi wa habari pamoja na Waziri Mkuu wa Uswidi Magdalena Andersson na Rais wa Finland Sauli Niinistö.
Anazihakikishia nchi hizo mbili maombi yao ya Nato yana "ufadhili kamili na kamili" wa Marekani.
Anasema ripoti zimeenda kwa Bunge la Uingereza leo ili baraza la juu la wanasiasa, Seneti, liweze kuelekea kuziidhinisha.
Anasisitiza hali ya kujihami ya Nato: "Wanachama wapya wanaojiunga na Nato sio tishio kwa taifa lolote, haijawahi kuwa tishio," anasema.
"Nato itaimarishwa kwa muda wote" na Uswidi na Finland zikijiunga, anasema.
Anongeza pia ‘nchi hizo mbili zina taasisi imara za kidemokrasia, wanajeshi wenye nguvu, uchumi imara na uwazi na hisia kali za kimaadili za kile ambacho ni sawa’.
"Wanakidhi kila mahitaji ya Nato," anasema Joe Biden.
Taarifa zaidi kuhusu Ukraine:
- Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- Mzozo wa Ukraine: Fahamu uhusiano wa kihistoria kati ya Ukraine na Urusi
- Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- Mzozo wa Ukraine: Fahamu kwanini baadhi ya mataifa yenye uwezo mkubwa yamesalia kimya
Gavana Sonko aliyetimuliwa Nairobi azuiwa kuwania ugavana Mombasa
Mahakama imezuia kwa muda Tume ya Uchaguzi nchini Kenya kumuidhinisha gavana wa zamani wa Nairobi mwenye utata kuwania wadhifa sawia na huo katika mji wa pwani wa Mombasa.
Mahakama Kuu mjini Mombasa imeamuru Tume Huru ya Uchaguzi kutoshughulia karatasi za uteuzi za Mike Sonko kwa ajili ya uchaguzi wa Agosti 9 kabla ya kesi inayomkabili kuamuliwa.
Mashiriki matatu ya kijamii ambayo yamemshtaki Sonko yanataka aondolewe katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa ugavana wa Mombasa kwa sababu aliondolewa katika wadhifa wake kama gavana wa Naorobi kwa kukiuka katiba.
Wanasema kwa vile alibainika kuwa hafai kushikilia wadhifa huo, basi hafai kushikilia wadhifa wowote wa umma.
Bw.Sonkoa liondolewa ofisini kupitia kura ya kutokuwa na Imani naye mwezi Disemba 2020 kwa utovu wa nidhamu na matumizi mabaya ya mamlaka.
- Gavana wa Sonko wa Nairobi aondolewa madarakani
- Marekani yampiga marufuku aliyekuwa gavana wa jiji la Nairobi Mike Mbuvi Sonko na famila yake kuingia nchini humo
Bobi Wine na mtoto wa Museveni wajibizana kwenye mtandao wa Twitter
Ama kweli maisha ni sanaa ya maigizo, baada viongozi wawili wa Uganda walioangaziwa katika mchoro wa katuni wakijibizana kufanya hivyo kiuhalisia.
"Kiatu hiki ni saizi yangu-usikaribie," mchoro unamuashiria kiongozi wa upinzani Bobi Wine akisema.
"Tulia Kaka! Sio kosa langu, ipo kwenye jeni yangu, "mwana mkubwa wa rais wa sasa wa Uganda alijibu katika mchoro huo wa katuni unaomuashiria.
Wahusika katika mchoro huo wa katuni wanajadiliana ni mguu wa nani utatoshea kwenye kiatu cha kiongozi wa Uganda aliyehudumu kwa muda mrefu Rais Yoweri Museveni, ambaye sasa ana umri wa miaka 77.
Mchoro huo ulishirikishwa kwenye mtandao wa Twitter na mwanawe rais Museveni Jenerali Kainerugaba.
Bobi Wine alimkosoa kwa kufikiria"Uganda ni moja ya mali ya baba yako ndio uwe mrithi"
Jenerali Kainerugaba, 47, amepanda madaraka kwa kasi katika jeshi la Uganda na kuna dhana kwamba anaandaliwa kuwa rais siku moja.
Amewahi kupinga dhana hiyo akisema kwamba Uganda sio"ufalme wa kisiasa"ambapo baba yake atamkabidhi hatamu za uongozi
Mwavuli unaovuja na kuuzwa zaidi ya dola elfu moja wazua mjadala China
Seti ya mwavuli inayotarajiwa kuuzwa nchini China na chapa maarufu za magharibi za Gucci na Adidas kwa yuan 11,100 sawa na dola 1,651 (£1,329) imezua mjadala mtandaoni huku ukidaiwa kuwa hauna uwezo wa kujikinga na mvua.
Ukosoaji wa bidhaa hizo ambayo makampuni hayo wameita ni "mwavuli wa jua" umevuma kwenye mtandao wa kijamii wa China Weibo.
Hatua hii imekuja baada ya tovuti ya Gucci kusema "haiwezi kuzuia maji na inakusudiwa kulinda jua au matumizi ya mapambo".
Mwavuli huu ni sehemu ya toleo la pamoja la kampuni hizo mbili ambalo limetangazwa mtandaoni kabla ya kutolewa mwezi ujao.
Mtumiaji mmoja wa mtandao huo amenukuliwa akisema "Maadamu mimi ni maskini, hawataweza kunihadaa ili nilipe hii," alisema.
Msemaji wa Gucci aliliambia gazeti la Beijing la Caijing kwamba bidhaa hiyo "haipendekezwi kutumika kama mwavuli wa kila siku".
Toleo hilo la mwamvuli linatarajiwa kutolewa tarehe 7 Juni kama sehemu ya bidhaa mpya ya chapa ya kifahari ya Gucci na kampuni kubwa ya mavazi ya michezo Adidas.
Mwamuzi mwanamke kutoka Rwanda Salima Mukansanga kuchezesha kombe la Dunia Qatar 2022
Mwamuzi kutoka Rwanda, Salima Mukansanga ametajwa kuwa mmoja wa waamuzi watatu wa kike watakaochezesha Fainali za Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.
Waamuzi wanamke hawajawahi kushiriki katika mashindano ya wanaume, kwa hivyo hii itakuwa ya kwanza kwenye mashindano mnamo Novemba.
Mukansanga amekuwa mwanamke wa kwanza kuchukua jukumu la mechi ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanaume mapema mwaka huu
Kuna maafisa wengine kadhaa wa Kiafrika waliotajwa kwenda Qatar, akiwemo Janny Sikazwe, ambaye alivuma kwa kumaliza mechi sekunde 13 mapema katika mchezo wa Kombe la Mataifa ya Afrika mwezi Januari.
Mapema leo kamati ya Waamuzi ya FIFA ilitangaza orodha yenye majina ya wasimamizi wa mechi waliochaguliwa kwa ajili ya Kombe la Dunia la FIFA Qatar 2022™.
Waamuzi 36, waamuzi wasaidizi 69 na maafisa 24 wa mechi za video wamechaguliwa kwa ushirikiano wa karibu na mashirikisho sita, kulingana na ubora wao na uchezaji uliotolewa kwenye mashindano ya FIFA na pia katika mashindano mengine ya kimataifa na ya nyumbani katika miaka ya hivi karibuni.
FIFA yaifungia Kenya kushiriki katika shughuli zote za soka
Shirikisho la kandanda duniani, Fifa, limeitaka serikali ya Kenya kufuta uamuzi wa kulivunja Shirikisho la Soka la Kenya na kuweka kamati ya muda la sivyo nchi itasitishwa kujihusisha na shughuli zote za soka kwa muda usiojulikana.
Katika barua iliyotumwa kwa katibu mkuu wa shirikisho lililovunjwa Barry Otieno, Fifa iliitaka serikali: "kubatilisha uamuzi wa Katibu wa Baraza la Mawaziri wa tarehe 11 Novemba 2021 kuteua kamati ya muda badala ya Kamati Tendaji iliyochaguliwa ya FKF."
Hatua hii imekuja ikiwa ni muda mfupi baada ya Rais wa Fifa Gianni Infantino kutangaza kusimamishwa kwa muda usiojulikana kwa shughuli zote za kandanda wakati wa Mkutano wake na waandishi wa habari.
"Bila ya kuathiri uchunguzi wowote wa mamlaka ya kitaifa au vyombo vingine vya mahakama, Baraza la Fifa pia liliamua kusimamisha Shirikisho la Soka la Kenya na Chama cha Soka cha Zimbabwe mara moja kutokana na kuingiliwa isivyofaa na mtu wa tatu," Infantino alisema.
Katibu wa Baraza la Mawaziri la Michezo nchini Kenya, Amina Mohamed, Novemba 11 mwaka jana alivunja Shirikisho la Soka la Kenya lililoongozwa na Nick Mwendwa na kuweka Kamati ya Uangalizi.
Amina alimteua Jaji Mstaafu Aaron Ringera kuongoza kamati ya muda, huku mwanahabari Lindah Oguttu akitawazwa kuwa mkuu wa sekretarieti hiyo.
Katibu Mkuu wa Fifa, Fatma Samoura aliiandikia mamlaka ya Kenya mara mbili baada ya kuvunjwa kwa shirikisho hilo, akiiomba serikali, angalau, kurejesha sekretarieti ya chombo hicho wakati wakiendelea kutafuta suluhu.
Rais wa zamani wa Marekani George W Bush alaani uvamizi wa Putin wa 'Iraq' badala ya Ukraine
Rais wa zamani wa Marekani George W Bush alilaani kwa bahati mbaya uvamizi wa Vladmir Putin wa "Iraq", kabla ya kujisahihisha kwa kusema anazungumzia Ukraine.
Bw Bush alizungumza hayo alipokuwa akihutubia katika hafla moja huko Dallas, Texas, ambapo alikuwa akizungumzia umuhimu wa uchaguzi wa haki.
Alisema, "uamuzi wa mtu mmoja kuanzisha uvamizi usio na msingi na wa kikatili kabisa wa Iraq... namaanisha Ukraine".
Katika hotuba hiyo alimaanisha kukemea uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine wakati wa hotuba yake huko Dallas siku ya Jumatano.
Badala yake, huku akiukosoa mfumo wa kisiasa wa Russia, alisema: “Matokeo yake ni kutokuwepo kwa cheki na mizani nchini Urusi, na uamuzi wa mtu mmoja kuanzisha uvamizi usio na msingi na wa kikatili kabisa wa Iraq.
Bw Bush alikuwa rais wakati wa uvamizi ulioongozwa na Marekani nchini Iraq mwaka 2003 kutokana na madai ya silaha za maangamizi ambazo hazikupatikana kamwe.
Matamshi ya Bush yalienea haraka kwenye mitandao ya kijamii, na kukusanya maoni zaidi ya milioni tatu kwenye Twitter pekee baada ya video hiyo kutumwa kwenye Twitter na ripota wa Dallas News.
Rais huyo wa zamani wa Marekani pia alimlinganisha kiongozi wa Ukrania Volodymyr Zelenskiy na kiongozi wa wakati wa vita wa Uingereza Winston Churchill, huku akimlaani Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa kuanzisha uvamizi wa Ukraine mwezi Februari.
Taarifa zaidi kuhusu Ukraine:
- Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- Mzozo wa Ukraine: Fahamu uhusiano wa kihistoria kati ya Ukraine na Urusi
- Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- Mzozo wa Ukraine: Fahamu kwanini baadhi ya mataifa yenye uwezo mkubwa yamesalia kimya
Ajiunga na chuo kikuu akiwa na umri wa miaka 69
Raia mmoja wa Ethiopia na baba wa watoto 11 amekuwa maarufu kwenye mitandao ya kijamii nchini humo baada ya kujiunga na chuo kikuu akiwa na umri wa miaka 69.
Akiwa yatima katika umri mdogo, Tadesse Ghichile, hakuweza kuendelea na elimu rasmi baada ya kumaliza shule ya sekondari.
Sasa, anahudhuria masomo ya Chuo Kikuu cha Jimma kilichopo sehemu ya magharibi ya nchi ambako anatarajia kuhitimu na shahada ya matibabu.
Tadesse Ghichile ni mkulima. Asipokuwa shambani, hufanya kazi kwenye mgahawa katika kijiji chake ili kutunza familia yake.
Lakini alipata muda wa kufanya na kufaulu mtihani wa kitaifa wa kuingia chuo kikuu.
Miaka 10 iliyopita ndipo alipoamua kurudi katika elimu yake rasmi ambayo aliiacha akiwa darasa la nane kufuatia kifo cha wazazi wake.
Kwa muda mrefu alikuwa amepata ugumu kurudi shuleni haswa baada ya kuanzisha familia. Lakini mara tu aliporudi, alidhamiria kumaliza hadi mwisho.
Sasa, amejiandikisha katika moja ya chuo kikuu kikubwa zaidi nchini humo. Aliiambia BBC kuwa amekuwa na uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa wanafunzi wenzake katika miaka michache iliyopita na kwamba anatazamia kile kitakachotokea mbeleni.
Mshukiwa wa mauji ya Rwanda Munyarugarama athibitishwa kufa
Mahakma ya Umoja wa mataifa imetangaza kifo cha mshukiwa mwingine wa mauaji ya kimbari ya Rwanda, ambaye ni miongoni mwa washukiwa watano ambao bado wanasakwa.
Mahakama hiyo imesema kwamba iligundua kuwa Phénéas Munyarugarama alifariki mwaka 2002 mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo
Katika taarifa iliyotolewa Jumatano , mahakama hiyo ilisema kuwa iliweza kubaini kifo chake ’’baada ya uchunguzi wa kina na wenye changamoto’’, na kwamba alikufa kifo cha kawaida tarehe 28 Februari 2002”.
Munyarugarama, ambaye ni kamanda wa zamani wa jeshi, amekuwa akishitakiwa mashitaka manane yakiwemo mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya binadamu.
"Kwa waathiriwa na manusura wa uhalifu uliotekelezwa na Munyarugarama katika eneo la Bugesera, tunamatumaini matokeo haya yanafunga kesi ,"mwendesha mashitaka Serge Brammertz amesema katika taarifa.
Tangazo la hivi karibuni linafuatia tangazo lingine la mahakama la wiki iliyopita la kuthibitisha kifo cha mshukiwa Protais Mpiranyi ambaye pia alikuwa miongoni mwa washukiwa wakuu wanaosakwa na mahakama kwa mauaji ya Rwanda.
Takriban watu laki 800,000 waliuliwa kikatili na Wahutu wenye itikadi nchini Rwanda , katika kipindi cha siku 100 katika mwaka 1994.
Walikuwa wakiwalengawatu wa jamii ya Watutsi walio wachache pamoja na wapinzani wao kisiasa, bila kujali asili asili yao.
Mwanafunzi wa kidato cha kwanza apeleka kuku shuleni kama malipo ya karo ya $480
Mwanafunzi anayejiunga na kidato cha kwanza katika shule ya upili ya Kangaru kaunti ya Embu nchini Kenya aliwasili shuleni hapo akiandamana na mamake huku akiwa amebeba kuku kama njia yake ya kulipa karo ya shule ya upili.
Kulingana na tovuti ya the Citizen nchini Kenya, Lawrence Murimi, 14, alipata alama 313 katika mitihani yake ya KCPE na kusema alipewa jogoo huyo na mjombake.
Akizungumza Jumatano baada ya kusafiri kilomita 5 hadi shuleni akiwa na mamake, Lawrence aliyekuwa akitokwa na machozi alisema walirudishwa nyumbani kuchukua Ksh.48,000{$480} zinazohitajika kwa ajili ya karo ya shule.
"Nilimwambia mama yangu kwamba ni kuku niliopewa pekee ndiye ambaye tunaweza kumpeleka shuleni baada ya kujaribu kugonga milango yote ili kutafuta msaada bila mafanikio," alisimulia nje ya lango la shule.
Aliongeza kuwa kuku huyo alikuwa na thamani ya Ksh.1,000 ikiwa ni fedha kidogo ikilinganishwa karo ninayofaa kulipa katika shule hiyo ili kusajiliwa.
Mamake mwanafunzi huyo alisema baada ya kupokea barua ya ksajiliwa kwa mwanawe, alianza kuzunguka afisi zote kutafuta msaada lakini hakufanikiwa.
Alisema mwanawe alilazimika kwenda shule ya upili na daftari alizokuwa akitumia katika darasa la nane.
Mama huyo kutoka mtaa wa Majengo huko Embu sasa anawaomba wasamaria wema kumsaidia mwanawe.
Urusi inasema zaidi ya wapiganaji wa Ukraine zaidi ya 900 wamepelekwa katika kambi ya jela
Zaidi ya wapiganaji 900 wa Ukraine ambao walikuwa wamekwama katika kiwanda cha chuma wa Azovstal katika Mariupol wamepelekwa katika kambi ya gereza katika eneo linalodhibitiwa na Warusi, imesema Moscow .
Urusi iliwaamrisha wanajeshi pale kujisalimisha kama sehemu ya mkataba uliofikiwa na pande zote, kama njia ya kuyaokoa maisha yao. Inaripotiwa kuwa kulikuwa na uhaba wa chakula na maji katika kiwanda hicho kwa wiki kadhaa.
Msemaji wa Wizara ya mambo yan je ya Urusi , Maria Zakharova, alisema Jumatano kwamba wanajeshi 959 walikuwa wamejisalimisha kwa Urusi tangu Jumanne . Kati ya wanajeshi hayo 521, walikuwa wanatibiwa majeraha na waliosalia wamepelekwa katika kambi ya zamani ya jela katika mji wa Olenivka katika eneo linalodhibitiwa lililopo katika jimbo la Donetsk.
Wizara ya ulinzi katika Kyiv ilisema kuwa inamatumaini kuwa kutakuwa na "utaratibu wa kubadilishana …kuwahamisha mashujaa hawa wa Ukraine haraka iwezekanavyo", kulingana na Shirika la habari la AFP.
Hatma yao imesalia kuwa haijulikani , huku msemaji wa serikali ya Urusi Dmitry Peskov akikataa kusema iwapo watachukuliwa kama wahalifu au wafungwa wa kisiasa.
Wizara ya ulinzi ya Ukraine iliahidi kufanya "kila liwezekanalo" kuwaokoa wale ambao bado wamejificha kwenye mitandao ya mahandaki chini ya kiwanda cha chuma, lakini ilikiri kuwa hakuna njia nyingine ya kijeshi iliyopo ya kukwepa.
Taarifa zaidi kuhusu Ukraine:
- Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- Mzozo wa Ukraine: Fahamu uhusiano wa kihistoria kati ya Ukraine na Urusi
- Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- Mzozo wa Ukraine: Fahamu kwanini baadhi ya mataifa yenye uwezo mkubwa yamesalia
Rais Zelensky: Urusi inatumia silaha 'dhaifu'
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anasema kuwa hatua ya Urusi kutumia "silaha zisizo na nguvu" katika uvamizi wake dhidi ya nchi yake ni ishara ya kushindwa kwao.
Hatua hiyo Inafuatia madai ya afisa mmoja wa Urusi kwamba teknolojia - yenye uwezo wa kuangusha ndege zisizo na rubani - ilikuwa "ikisambazwa sana" kwenye uwanja wa vita.
Warusi wanamtafuta "wunder-waffe" Zelensky alidai kwa dhihaka. Ilikuwa ni marejeleo ya uwindaji wa silaha ya ajabu ambayo ingegeuza wimbi la Vita vya dunia vya pili wajati Wanazi walipokuwa wakishindwa katika uwanja wa vita.
Wakati huohuo bwana Zelensky amesema uvamizi wa Urusi dhidi ya nchi yake ulikuwa ni kosa la "kubwa’’ baada ya Urusi kudai ushindi wa kimkakati huko Mariupol.
Akizungumza kutoka Kyiv wakati wa hotuba yake ya kila siku ya televisheni, Zelensky alisema uvamizi huo umethibitika kuwa "umeshindwa kabisa" na kudai kuwa vikosi vya Moscow vimekosa makombora ya kushambulia wanajeshi wake.
Zelensky pia aliwakashifu viongozi wa Urusi, ambao alisema waliogopa kukiri "kwamba makosa makubwa yalifanywa katika ngazi ya juu zaidi ya kijeshi na serikali" wakati wa vita.
Kiongozi huyo wa Ukraine alishutumu maafisa wa Moscow kwa kuwalazimisha askari vijana wasio na uzoefu kwenye mstari wa mbele na kuwatupa "katika vita kama chakula cha mizinga".
Maoni yake yanajiri baada ya mwanajeshi wa Urusi mwenye umri wa miaka 21 kukiri kosa la kumuua raia asiye na silaha, katika kesi ya kwanza ya uhalifu wa kivita nchini Ukraine tangu vita kuanza.
Taarifa zaidi kuhusu Ukraine:
- Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- Mzozo wa Ukraine: Fahamu uhusiano wa kihistoria kati ya Ukraine na Urusi
- Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- Mzozo wa Ukraine: Fahamu kwanini baadhi ya mataifa yenye uwezo mkubwa yamesalia kimya
"Mlango" wagundulika katika sayari ya Mars
Likionekana kama umbo la mraba, na mkato laini unaoonekana katika mwamba mkali, umbo la kijiolojia lililotengenezwa katika sayari ya Mars limeibua maswali kwa siku kadhaa.
Baadhi wamebaini kuwa ni umbo la "mlango" na wengine wameibuka na nadharia kuhusu iwapo ’’mlango’’ huu uliopo nje ya dunia unaweza kubuni "njia " ya kuingia katika sayari jirani.
Lakini kile kilichoonyeshwa ni picha iliyopigwa na roboti ya udadisi, ambayo imekuwa ikituma taarifa kuhusu sayari ya Mars kutoka duniani tangu mwaka 2012, ina maelezo zaidi ya kimantiki.
Kulingana na NASA, ni suala la kimtazamo.
NASA ilitambua picha kama sehemu ya msururu wa "Sol 3466" ambao ulichapishwa katika picha nyingi katika wavuti wa mpango wa uvumbuzi wa roboti
Baada ya kuchapishwa, baadhi ya watu mtandaoni walianza kuzungumzia nadharia kuhusu umbo lake na jinsi umbo hivyo lilivyo na muonekano wa ‘’mlango’’ au "njia"
Katika picha hii unaweza kuona mkusanyiko wa picha za misururu ya 3466 na jinsi umbo linavyoonekana kwenye mwamba wa Jezero , ambalo limevumbuliwa na roboti yenye udadisi katika wiki za hivi karibuni.
Mzozo kati ya Ukraine na Urusi kusababisha baa la njaa duniani - UN
Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine huenda ukasababisha baa la njaa kote duniani katika kipindi cha miezi michache ijayo, Umoja wa Mataifa umeonya.
Atibu mkuu wa Umoja huo Antonio Guterres alisema kwamba vita hivyo vimesababisha ukosefu a usalama wa chakula katika mataifa masikini kutokana na kupanda kwa bei za vyakula.
Dunia huenda ikakabiliwa na kiangazi kitakachochukua muda mrefu iwapo bidhaa za Ukraine hazitaimarishwa kwa kiwango cha kabla ya vita, aliongezea.
Mzozo huo umekata usambazaji wa bidhaa kutoka katika bandari za Ukraine, kama vile mafuta ya kupikia pamoja na nafaka kama vile mahindi na ngano.
Hali hiyo imepunguza usambaza wa bidhaa hizo hali iliofanya bei kupanda.Bei za vyakula duniani zinakaribia kupanda kwa asilimia 30 ikilinganishwa na mwaka uliopita , kulingana na Umoja wa Mataifa.
Akizungumza mjini New York siku ya Jumatano, bwana Guterres alisema kwamba mzozo huo unatishia kuwawacha bila chakula mamilioni ya watu na kusababisha utapiamlo, baa la njaa na kiangazi.
Taarifa zaidi kuhusu Ukraine:
- Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- Mzozo wa Ukraine: Fahamu uhusiano wa kihistoria kati ya Ukraine na Urusi
- Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- Mzozo wa Ukraine: Fahamu kwanini baadhi ya mataifa yenye uwezo mkubwa yamesalia
Hujambo na karibu tena katika matangazo yetu mubashara leo tarehe 19.05.2022