Ukraine yawaua zaidi ya wanajeshi 1000 wa Urusi waliojaribu kuvuka mto kuingia Ukraine

Jeshi la Urusi lilipata hasara kubwa na wanajeshi wengi walijaribu kutoroka na kuogelea hadi ufuo mwingine lakini wanajeshi wa Ukraine mara moja waliwafyatulia risasi, iliongeza.

Moja kwa moja

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo, tukutane tena hapo kesho majaaliwa

  2. Zelensky anasema anaweza kuzungumzana Putin- ila pasiwe na waamuzi

    zelensky

    Chanzo cha picha, EPA

    Rais wa Urusi Volodymyr Zelensky yuko tayari kuzungumza moja kwa moja na Rais wa Urusi Vradmir Putin, ila "pasiwepo na mtu mwingine yeyote wa kuwapatanisha", rai swa Ukraine ameiambia televisheni ya Italia , channel Rai 1.

    Zelensky amesema anaweza kuzungumza tu na Putin, "kwa masharti ya mazungumzo, sio kwa kulazimishwa ".

    Amesema "hatua ya kwanza ya wazi " ya kufanya mazungumzo inaweza kuwa wakati Urusi itakapoondoa vikosi vyake kutoka Ukraine.

    Aliongeza kuwa ana kesi zaidi za '' ukatili wa wazi '' uliofanywa na warusi ambao ulionekana. kama ule uliofanyika katika Bucha , Borodyanka au Mariupol, jambo ambalo haliwezi kuvumiliwa katika mazungumzo yoyote na Warusi.

    Ukraine na Urusi bado hazijafanya mazungumzo ya ana kwa ana tangu tarehe 29 machi na mpatanishi mkuu wa Moscow, Vladimir Medinsky, amekuwa akisema kuwa mazungumzo yalifanyika kwa njia isiyo ya ana kwa ana.

  3. Umoja wa Mataifa: Raia zaidi ya 3,000 wameuawa katika vita vya Ukraine

    Getty

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limekuwa likiendelea kuhesabu idadi ya raia wanaouawa tangu uvamizi wa Urusi ulipoanza nchini Ukraine.

    Kulingana na baraza hilo, watu 3,496 wamekwishauawa kufikia tarehe 10 Mei na wengine 3,760 wamejeruhiwa tangu uvamizi wa Ukraine uanze. Miongoni mwao ni watoto na vijana wadogo.

    Wengi wao wameripotiwa kuuawa katika mashambulio ya makombora, mashambulio ya maroketi na yale ya anga.

    Raia

    Chanzo cha picha, EPA

    Wataalamu wa Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa wanaamini idadi kamili ya watu waliouawa na kujeruhiwa ni kubwa zaidi kuliko idadi rasmi inayotolewa. Hii ni kwasababu data kutoka maeneo ya vita hazijakamilika na ripoti nyingi zinahitaji kuthibitishwa.

  4. Ukraine yadai kuizamisha meli ya Urusi karibu na kisiwa cha Snake

    .

    Chanzo cha picha, Reuters/maxar

    Maelezo ya picha, Kisiwa cha Snake Island

    Kama tulivyoripoti hapo awali, meli nyingine ya Urusi imezama karibu na Kisiwa cha Zmiinyi (Snake) katika shambulio dhahiri la makombora la Ukrain.

    Sasa, mkuu wa ujasusi wa Ukraine, Kirill Budanov, anasema wanajeshi wa nchi hiyo watapigania kisiwa hicho "mradi tu", akiongeza kuwa watakiteka tena kutoka kwa Warusi.

    Kisiwa cha Snake ni eneo muhimu kimkakati kwa Ukraine na Urusi, kwa vile kinaruhusu ufikiaji wa Bahari Nyeusi kwa njia za biashara zilizo wazi, uagizaji wa silaha na kwa suala la uwezo wa Urusi pia kutekeleza kutua kwa majini kwa busara.

    "Mtu yeyote anayedhibiti kisiwa hicho anaweza kuzuia harakati za meli za raia katika pande zote kuelekea kusini mwa Ukraine wakati wowote," Budanov alisema.

  5. Rais wa Milki za Kiarabu Sheikh Khalifa amefariki akiwa na umri wa miaka 73

    REUTERS

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Wadhifa Sheikh Khalifa bin Zayed al-Nahyan kwa kiasi kikubwa haukuwa na mamlaka

    Mmoja wa watu wa familia tajiri zaidi za kifalme duniani, Rais wa Sheikh Khalifa bin Zayed al-Nahyan wa Milki za kiarabu (UAE) amefariki akiwa na umri wa miaka 73.

    Sheikh Khalifa alikuwa rais wa Milki za Kiarabu (UAE) tangu mwaka 2004, lakini wadhifa wake kwa kiasi kikubwa haukuwa na mamlaka tangu alipopata maradhi ya kiharusi mwaka 2014.

    Kaka yake, Mohamed bin Zayed al-Nahyan, sasa ndiye anayeongoza masuala ya kitaifa.

    Familia ya al-Nahyan inaaminiwa kuwa na utajiri wa thamani ya dola bilioni 150(£123bn).

    Pamoja na kuwa Rais wa UAE, Sheikh Khalifa alikuwa mtawala wa Abu Dhabi, mji mkuu wenye utajiri wa mafuta wa milki saba zinazounda Muungano wa nchi za kiarabu

    Taarifa ya kifo chake ilitangazwa katika Shirika rasmi la habari la WAM.

    Wizara ya masuala ya rais ilitangaza siku 40 za maombolezo na kuperurushwa kwa bendera nusu mlingotikuanzia Ijumaa, na kazi zimeahirishwa katika sekta za umma na za kibinafsikwa muda wa siku tatu.

    Sheikh Khalifa alichukua mamlaka kama rais wa pili wa UAE mwezi Novemba 2004 , akimrithi baba yake kama mtawala wa 16 wa Abu Dhabi.

  6. Habari za hivi punde, Picha ya vifaru vya Urusi vilivyoshambuliwa na kuharibiwa na Ukraine wakati wa jaribio la kuvuka mto

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Mtaalamu wa masuala ya usalama na mhudumu wa zamani wa Uingereza Justin Crump anasema juhudi za Urusi "zimeshindwa pakubwa". Lakini anasema madai ya Ukraine ya kuwaangamiza zaidi ya wanaume 1,000 huenda sio kweli.

    Akizungumza na BBC, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la usalama la Sibylline Ltd anakadiria kuwa zaidi ya Warusi 140-180 waliuawa.

    Anaeleza kuwa magari 70 au 80 yaliripotiwa kuharibiwa katika shambulio la Ukraine.

  7. Udongo kutoka mwezini kukuza mimea

    Udongo

    Chanzo cha picha, UF/IFAS

    Maelezo ya picha, Wanasayansi walifurahi kwamba udongo wa mwezi unaweza kuchipuza mbegu( kulia) hatakama ukuaji wake ulidumaa

    Wanasayansi wamepanda mimea kwenye udongo wa mwezini kwa mara ya kwanza , ikiwa ni hatua muhimu kuelekea kuishi kwa muda mrefu mwezini iwezekanavyo.

    Watafiti walitumia sampuli ndogo za vumbi iliyokusanywa wakati wa safari yaApolo kati yam waka 1969-1972 Apollo kupanda aina mboga za jamii ya kabeji.

    Walishangaa sana kwamba, mbegu zilianza mbegu zilianza kutoka baada ya siku mbili.

    "Siwezi kukwambia jinsi tulivyoshangaa ," alisema Anna-Lisa Paul, Profesa katika Chuo kikuu cha Florida ambaye ni mwandishi mwenza wa matokeo ya utafiti.

    "Kila mmea-uwe ni wa sampuli ya mwezi au unaodhibitiwa- ilionekana sawa hadiilipofika siku ya sita baadaye."

    Baada yah apo, tofauti zilijitokeza. Mimea iliyopandwa katika udongo wa mwezini ilianza kuonyesha kunyong’onyea, ikaanza kukua kwa kurora zaidi na kuishia kudumaa.

    Lakini wale waliohusika wanasema ni mafanikio- na yenye athari za kidunia.

  8. Kilichofanyika katika mto Siversky Donets Ukraine

    .

    Chanzo cha picha, reuters

    Kama ambavyo tumekuwa tukiripoti, Urusi inaaminika kupoteza kikosi kizima cha wanajeshi wake katika jaribio lililofeli la kuvuka mto wa Siversky Donets.

    Mto huo unapita katika mikoa ya Donetsk na Luhansk mashariki mwa Ukraine - ambayo hivi karibuni imekuwa ikilengwa kijeshi ya Urusi.

    Licha ya hasara kwenye kivuko cha mto Siversky Donets, vikosi vya Moscow vinaonekana kupata mafanikio makubwa katika eneo hilo:

    Wizara ya Ulinzi ya Uingereza inasema Urusi imekuwa ikielekeza nguvu zake nyingi za kijeshi katika maeneo ya Izyum na Severodonetsk, miji miwili iliyo karibu na eneo la kivuko cha maafa ya wanajeshi wa Urusi .

    Mkuu wa utawala wa kijeshi wa mkoa wa Luhansk Serhiy Haidai anasema wanajeshi wa Urusi wamevamia Rubizhne na maeneo mengine mawili nje kidogo ya Severodonetsk katika jaribio la kuizingira miji hiyo.

    Vikosi vya Urusi vina uwezekano wa kuanzisha shambulio katika eneo la Severodonetsk katika siku zijazo, Taasisi ya Utafiti wa Vita ilisema katika uchambuzi wake wa vita.

    MoD anasema vikosi vya Urusi vimeondoka Kharkiv, kaskazini, na kuna uwezekano wa kupeleka tena wanajeshi wake katika mto Siversky Donets kuchukua nafasi iliowachwa na wanajeshi waliouawa.

  9. Habari za hivi punde, Ukraine yawaua wanajeshi 1000 wa Urusi waliojaribu kuvuka mto kuingia Ukraine

    Ukraine Airborne forces

    Chanzo cha picha, Ukraine Airborne forces

    Maelezo ya picha, Ukraine Airborne forces

    Urusi ilianzisha jaribio lake la kuvuka mto tarehe 8 Mei, ikisafirisha wanajeshi wake na silaha ikiwa mizinga, magari na kivita , kulingana na huduma ya habari ya Kiukreni ya InformNapalm.

    Mara tu walipovuka, vikosi vya Ukraine viliharibu daraja la pantoni ndani ya maji, na wanajeshi wa Urusi "waliingia kwenye mtego", ilisema.

    Jeshi la Urusi lilipata hasara kubwa na wanajeshi wengi walijaribu kutoroka na kuogelea hadi ufuo mwingine lakini wanajeshi wa Ukraine mara moja waliwafyatulia risasi, iliongeza.

    Ilisema kwamba kifaru kilichokuwa kikivuka daraja hilo kiliharibiwa katika daraja hilo baada ya kufayatuliwa risasi huku wanajeshi wengi wakifa maji..

    Zaidi ya vitengo 70 vya vifaa vya kijeshi vya Urusi vilipotea kutokana na shambulio hilo na Ukraine inadai zaidi ya wanajeshi 1,000 wangeweza kuuawa.

  10. Miss Rwanda: Kesi ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya muandaaji yawekwa faraghani

    Ishimwe Dieudonné

    Chanzo cha picha, MISSRWANDA

    Maelezo ya picha, Ishimwe Dieudonné

    Mahakama ya mwanzo mjini Kigali imeamua kuendesha kesi dhidi ya mwandaaji wa shindano la urembo la Rwanda -Miss Rwanda faraghani ili kuwalinda mashahidi, amesema jaji.

    Dieudonné Ishimwe, al maarufu Prince Kid, anashutumiwa ubakaji, kuwa na upendeleo kwa misingi ya ngono , na unyanyasaji dhidi ya wasichana wanaowania taji la urembo.

    Bw Ishimwe alitarajiwa kukubali au kukana mashitaka katika kesi ya kutaka dhamana hii leo, lakini mara kesi hiyo ilipoanza mwendesha mashitaka aliomba kesi iendeshwe faraghani.

    Mwendesha mashitaka alielezea sababu za kesi hiyo kuendeshwa faraghani kuwa ni za kimaadili na kuwalinda mashahidi.

    Bw Ishimwe alipinga, akiomba kuwa kesi iendeshwe wazi“ ili umma ufuatilie na kujua matokeo ya kesi ”.

    Jaji aliamua kuiweka kesi faraghani , na waandishi wa habari na umma waliagizwa kutoka mara moja ndani ya chumba cha mahakama.

    Kesi hii ni moja ya voisa vinavyozungumziwa zaidi na Wanyarwanda katika mitandao ya kijamii.

    Wiki iliyopita, Waziri wa utamaduni aliahirisha shindano la Miss Rwanda, wakati mshindi wa taji hilo wa mwaka 2017 Elsa Iradukunda alipokamatwa kuhusiana na kesi ya Bw Ishimwe.

  11. Uamuzi wa mahakama: "Wanaume hawapaswi kutukanwa kwa vipara vyao’’

    Upara

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mahakama nchini Uingereza imeamua kuwa ni kinyume cha sheria kwa wanaume kutukanwa baada ya mwanaume mmoja kuwasilisha kesi mahakamani dhidi ya muajiri wa kampuni aliyoifanyia kazi zamani.

    Tony Finn, mwenye ummri wa miaka 64, alifanya kazi kwa miaka 24 kama fundi wa umeme katika eneo la West Yorkshire nchini Uingereza, kabla ya kufukuzwa kazi mwezi Mei, 2021.

    Alidai kuwa Jamie King, mmoja wa wakurugenzi wakuu wa kampuni, alikuwa akimtusi kwa kuwa na upara, alipokuwa akielezea mzozo uliotokea mwaka 2019.

    "Nilifunika vifaa kwa ajili ya kuvikarabati. Baada ya muda mfupi , niliona vifaa vikifunuliwa, na nikabaini kuwa Jamie King alikuwa amefanya hivyo . " Aliiambia mahakama katika Finn.

    Alisema kwamba kwasababu King alikuwa ni kijana mwenye nguvu, vitisho vyake vilisababisha hofu na hofu kwa maisha yake.

    Jaji Jonathan Brain aliombwa kuamua kuhusu kosa la kumtusi mtu kwa kuwa na upara, na kulielezea kama "unyanyasaji wa kingono."

    Unaweza pia kusoma:

    • Utafiti: Upara na nywele za kijivu ni ishara za magonjwa ya moyo
    • Njia za kuwasaidia wanaume kukabiliana na upara
  12. Seneta wa Marekani achelewesha msaada wa $40bn kwenda Ukraine

    mm

    Chanzo cha picha, Reuters

    Mjini Washington, kumekuwa na jitihada za kutuma kwa haraka $40bn (£32.7bn) kama msaada kwa Ukraine kupitia Congress.

    Democrats na Republican Seneti waliungana ikiwa ni ishara ya nadra ya umoja kwani wote walikubaliana juu ya hitaji la kutuma haraka msaada mkubwa zaidi katika miongo kadhaa - kwa Kyiv.

    Lakini seneta mmoja, Rand Paul wa Republican kutoka Kentucky, alijaribu kuchelewesha siku ya Alhamisi.

    Paul, ambaye kihistoria amepinga matumizi ya fedha katika misaada ya kigeni, alikataa kuunga mkono pendekezo hilo ambalo lilihitaji kuungwa mkono kwa kauli moja.

    Anadai sheria ibadilishwe ili kumtaka afisa kusimamia matumizi katika mzozo huo.

    "Ikiwa Seneta Paul ataendelea na madai yake... atafanikiwa kuchelewesha msaada pekee unaohitajika sana Ukraine," Kiongozi wa wengi Seneti Chuck Schumer alisema.

  13. Mkenya anayepambana na ukeketaji ametangazwa kuwa muuguzi bora zaidi duniani

    Dubai

    Chanzo cha picha, Dubai Media

    Muuguzi wa Kenya ameshinda tuzo ya kwanza kuwahi kuepo ya uuguzi duniani ambayo ina zawadi ya $250,000.

    Anna Qabale Duba, ambaye anafanya kazi katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Marsabit kaskazini mwa Kenya, alitunukiwa kwa kujitolea kutokomeza mila potofu kama vile ya ukeketaji katika jamii yake.

    Bi Duba pia ameanzisha taasisi - Qabale Duba Foundation - inayolenga kuwawezesha wasichana wadogo.

    "Kupitia shirika langu, nimejenga shule ya kipekee kijijini kwangu inayofundisha watoto na wazazi wao, kwa sababu kwangu elimu ni muhimu kwa maisha bora ya baadaye," Bi Duba alisema katika hotuba yake.

    Zaidi ya wauguzi 24,000 kutoka nchi 184 waliwasilisha maombi yao.

    Aliadhimishwa huko Dubai katika sherehe iliyofanyika katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wauguzi.

    • 'Mashujaa' wa vita vya ukeketaji Tanzania
    • Miss Tanzania apambana na ukeketaji nchini Tanzania
  14. Mwanafunzi wa Nigeria auawa kufuatia madai ya kukashifu uislamu

    w

    Chanzo cha picha, UGC

    Ghasia zimezuka katika chuo cha elimu ya juu katika mji wa Sokoto kaskazini mwa Nigeria baada ya mwanafunzi wa kike wa Kikristo kudaiwa kutoa matamshi ya kashfa dhidi ya Uislamu.

    Eneo hilo lina Waislamu wengi.

    Wanafunzi wa Kiislamu katika Chuo cha Elimu cha Shehu Shagari wanaripotiwa kumuua msichana huyo na kuuchoma moto mwili wake.

    Kisha wakaingia kwenye msako wa kuharibu mali yakiwemo magari.

    Msemaji wa polisi katika jimbo la Sokoto aliambia BBC kuwa vikosi vya usalama viliingilia kati kurejesha hali ya utulivu na uchunguzi unaendelea.

    Mamlaka imekifunga chuo hicho kwa muda usiojulikana na kuwaamuru wanafunzi kurudi nyumbani mara moja.

    Kiongozi mkuu wa kidini wa Kiislamu nchini Nigeria, Sultan wa Sokoto, Sa'ad Abubakar, amelaani mauaji ya mwanafunzi huyo wa Kikristo na kuomba utulivu.

  15. Afrika Kusini inayataka mashirika kununua chanjo za Covid-19 zinazotengenezwa Afrika

    mm

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ameyataka mashirika ya kimataifa na mashirika ya wafadhili kununua chanjo za Covid kutoka kwa wazalishaji wa Kiafrika.

    Rais Ramaphosa amesema hili "litahakikisha uwezo unaoendelea katika bara unadumishwa", alipokuwa akizungumza na mkutano wa kilele wa kimataifa kuhusu Covid , Alhamisi.

    “Mashirika ya kimataifa ambayo yamechangiwa fedha nyingi kwa ajili ya kununua na kupata chanjo kwa nchi zinazoendelea kiuchumi, hayanunui chanjo kutoka kwa watengenezaji chanjo barani Afrika, hata kwa zile chanjo ambazo zimewekwa kwa nchi za Afrika,” alisema.

    Taarifa hii inakuja wakati mtengenezaji wa chanjo nchini Afrika Kusini anatoa angalizo la kusimamisha uzalishaji wa chanjo kwa kukosa watu wanaoagiza.

    Aspen Pharmacare hivi majuzi ilisema kwamba inaweza kulazimika kusitisha uzalishaji katika kiwanda chake cha Afrika Kusini baada ya kukumbwa na uhitaji mdogo.

    Kampuni ilijadili mkataba wa kutoa leseni mwezi Novemba ili kufunga na kuuza chanjo ya Johnson & Johnson ili kusambazwa barani Afrika.

    Ilionekana kama nyongeza ya uzalishaji na usambazaji wa chanjo barani Afrika.

    Lakini, bara bado lina kiwango cha chini cha chanjo hata wakati linakabiliwa na wimbi jipya la virusi.

    Kati ya Waafrika sita, mmoja ndio amepata dozi mbili za chanjo ya virusi vya corona, huku wengi wakisita kuchapwa.

    Siku ya Alhamisi, Bw Ramaphosa alisema nchi yake bado inatetea msamaha wa haki miliki ili kuboresha ufikiaji wa kimataifa wa chanjo.

    • Afrika Kusini imesema 'imeadhibiwa' kwa kugundua virusi vipya vya corona aina ya Omicron
    • Virusi vya corona: Nchi sita Afrika kuanzisha uzalishaji wa chanjo ya mRNA
  16. Wazazi nchini India wanamshtaki mtoto wao kwa kutowapatia mjukuu

    w

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Wazazi wawili nchini India wanamshtaki mtoto wao wa kiume kwa kutowapatia mjukuu.

    Wanandoa katika jimbo la kaskazini mwa India la Uttarakhand wameshtaki mtoto wao wa pekee wa kiume na mke wake kwa kutowapatia mjukuu baada ya miaka sita ya ndoa.

    Sanjeev 61 na Sadhana Prasad 57, wanasema walitumia akiba yao kumlea mtoto wao wa kiume, kulipia mafunzo ya urubani wake pamoja na harusi ya kifahari.

    Wanadai fidia ya takriban $650,000 (£525,000) kama hakuna mjukuu anayezaliwa ndani ya mwaka mmoja.

    Mtoto wao na mkewe hawajasema chochote kuhusiana suala hilo.

    Kesi hiyo isiyo ya kawaida sana iliwasilishwa kwa misingi ya "unyanyasaji wa kiakili".

    Bw Prasad alisema ametumia akiba yake yote kwa mtoto wake, na kumpeleka Marekani mwaka wa 2006 kwa mafunzo ya urubani kwa gharama ya $65,000.

    Alirejea India mwaka wa 2007, lakini alipoteza kazi yake na familia yake ikalazimika kumsaidia kifedha kwa zaidi ya miaka miwili, gazeti la Times of India linaripoti.

    Shrey Sagar, 35, hatimaye alipata kazi kama rubani. Wazazi wake wanasema waliandaa doa yake na Shubhangi Sinha, ambaye sasa ana umri wa miaka 31, mwaka wa 2016, kwa matumaini kwamba watapata "mjukuu wa kucheza naye" wakati wa kustaafu kwao.

    Wazazi hao wanasema walilipia sherehe ya harusi katika hoteli ya nyota tano, gari la kifahari la thamani ya dola 80,000 na fungate nje ya nchi.

    “Mwanangu amekuwa kwenye ndoa kwa miaka sita lakini bado hawajapanga kupata mtoto,” Bw Prasad alisema.

    "Angalau ikiwa tuna mjukuu wa kukaa naye, maumivu yetu yatavumilika." Wakili wa wanandoa hao, AK Srivastava, aliambia The National kwamba wenzi hao walikuwa wamedai pesa hizo "kwa sababu ya ukatili wa kiakili".

    "Ni ndoto ya kila mzazi kuwa babu na nyanya. Walikuwa wamesubiri kwa miaka mingi kuwa babu na nyanya." Ombi la wanandoa hao, lililowasilishwa Haridwar, linatarajiwa kusikilizwa na mahakama tarehe 17 Mei.

  17. UK- Putin anajidhalilisha mbele ya dunia

    w

    Chanzo cha picha, PA Media

    Vikwazo vya kimataifa dhidi ya Urusi vinapaswa kuondolewa tu wakati wanajeshi wake wote wameondoka Ukraine, waziri wa mambo ya nje wa Uingereza amesema.

    Liz Truss aliuambia mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa G7 nchini Ujerumani kwamba Rais wa Urusi Vladimir Putin lazima akabiliane na kushindwa jambo linalozuia uchokozi zaidi.

    "Putin anajidhalilisha katika jukwaa la dunia," alisema, akiongeza kwamba lazima anyimwe manufaa yoyote kutokana na uvamizi wake nchini Ukraine.

    Pia alitoa wito kwa Ukraine kuongeza upatikanaji wa zana za kijeshi za Nato.

    Mawaziri wa mambo ya nje wa G7 watakutana tena siku ya Ijumaa na wenzao wa Ukraine na Moldova.

    Unaweza pia kusoma

  18. Uhispania inapanga kuanzisha likizo ya hedhi kwa wafanyakazi wanawake

    w

    Uhispania inapanga kuanzisha likizo ya matibabu kwa wanawake wanaougua maumivu makali wakati wa hedhi, ripoti za vyombo vya habari zinaeleza.

    Rasimu ya mswada inasema wanawake wanaweza kuwa na siku tatu za likizo kwa mwezi - kuongezwa hadi tano katika baadhi ya mazingira.

    Lakini wanasiasa walionya kwamba rasimu hiyo - iliyovujishwa kwa vyombo vya habari vya Uhispania - ilikuwa bado inafanyiwa kazi.

    Ikiwa itapitishwa, itakuwa ni haki ya kwanza kama hiyo ya kisheria barani Ulaya. Ni nchi chache tu ulimwenguni ambazo zina sheria kama hiyo.

    Sheria ya Uhispania ni sehemu ya mageuzi mapana zaidi ya afya ya uzazi ambayo yatajumuisha mabadiliko ya sheria za uavyaji mimba nchini humo.

    Vyombo vya habari ambavyo vimeona sehemu za sheria hiyo vinaripoti kwamba inapaswa kuwasilishwa kwa baraza la mawaziri mapema wiki ijayo.

    Likizo ya siku tatu ya ugonjwa kwa vipindi vyenye uchungu itaruhusiwa kwa barua ya daktari, rasimu inasema, ambayo inaweza kuendelea hadi tano kwa msingi wa muda kwa maumivu makali au ya kutoweza.

    Lakini haitarajiwi kutumika kwa wale wanaopata usumbufu mdogo.

    Ni sehemu ya mbinu pana ya kutibu hedhi kama hali ya afya, inaripoti El País, ambayo pia inajumuisha kukomesha VAT kwa baadhi ya bidhaa za usafi - kile kinachojulikana kama "kodi ya pedi" - na bidhaa za usafi bila malipo kupatikana katika vituo vya umma. kama shule na magereza.

    • Hedhi:Ni zipi dhana za kupotosha kuhusu hedhi?
    • Ukomo wa hedhi una athari gani mwilini na utawezaje kukabiliana nazo?
  19. Urusi: Tutachukua hatua ikiwa Finland itajiunga na NATO

    W

    Chanzo cha picha, EPA

    Urusi imesema italazimika kuchukua "hatua za kulipiza kisasi" kutokana na hatua ya jirani yake Finland kujiunga na Nato.

    Taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Urusi imesema hatua hiyo itaharibu pakubwa uhusiano wa nchi hizo mbili, pamoja na usalama na uthabiti kaskazini mwa Ulaya.

    Hapo awali, rais wa Finland na Waziri Mkuu walitoa wito kwa nchi hiyo kuomba uanachama wa Nato "bila kuchelewa".

    Kauli hiyo inakuja huku kukiwa na ongezeko la uungwaji mkono wa umma kwa wanachama wa Nato kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

    Finland inashiriki mpaka wa kilomita 1,300 (maili 810) na Urusi. Hadi sasa, imesalia nje ya Nato ili kuzuia kuchukiza jirani yake wa mashariki.

    Finland itatangaza rasmi uamuzi wake Jumapili baada ya kuzingatiwa na bunge na viongozi wengine wakuu wa kisiasa.

    Uswidi imesema itatangaza uamuzi kama huo siku hiyo hiyo.

    Katibu Mkuu wa Nato Jens Stoltenberg amesema anatarajia mchakato wa kuipa Sweden na uanachama wa Finland kutokea "haraka kabisa".

    Unaweza pia kusoma

  20. Hujambo, karibu katika taarifa zetu za moja kwa moja leo 13.05.2022