Vita vya Ukraine: Kiongozi wa Ukraine aweka masharti kwa ajili ya mkataba na Urusi

Mpango wowote wa amani na Urusi utategemea kurudi nyuma kwenye maeneo vilipokuwa vikosi vya Urusi kabla ya uvamizi, Rais wa Ukraine anasema

Moja kwa moja

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo, tukutane tena hapo kesho majaaliwa.

  2. Vikosi vya Taliban vinawalazimisha wanawake kufunika nyuso zao

    taliban

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Wanawake waliovalia burka wakipokea msaada wa chakula katika Kandahar mwezi uliopita

    Wanawake wa Afghanstan watalazimika kufunika nyuso zao vilemba vya Kiislamu kwa mara ya kwanza baada ya miongo chini ya sheria iliyoidinishwa na wanamgambowa Taliban wanaotawala nchi hiyo.

    Mwanamke yeyote anayekataa kutekeleza na kupuuza onyo rasmi kwa wanaume wa familia yake anaweza kushuhudia mlezi wake wa kiume akifungwa jela kwa siku tatu.

    Talibani walitekeleza kwanza uvaaji wa burka zinazofunika mwili mzima mzima wakati walipoingia mamlakani miaka ya 1990.

    Lakini walikuwa hawajatekeleza sheria hii katika miji ya Afghanstan tangu wachukue mamlaka ya nchi mwaka jana.

    Burqa

    Chanzo cha picha, Reuters

    Wanawake wengi nchini Afghanistan tayari wanavaa burka lakini baadhi, hususan katika maeneo ya mijini huvaa tu vilemba vya kawaida vinavyofunika nywele zao.

  3. Saratoga Hotel: Watu 22 wafariki baada ya mlipuko mkubwa Havana

    Search and rescue operations are underway at the Saratoga Hotel

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Shughuli ya za msako na uokoaji azinaendelea katika Saratoga Hotel

    Takriban watu 22 wamefariki na wengine zaidi ya 60 wamelazwa hospitalini baada ya mlipuko mkubwa kuikumba moja ya hoteli za kipekee na kifahari zaidi nchini Cuba.

    Inaaminiwa kuwa tanki la gesi ambalo lilikuwa limeegeshwa nje ya Saratoga Hotel iliyopo katika eneo la Old Havana liliwaka na kusababisha mlipuko ambao uliharibu magorofa kadhaa ya jengo.

    Hoteli hiyo ya kihistoria ilikuwa imejiandaa kwa ajili ya kufunguliwa baada ya janga la Covid katika kipindi cha siku nne. Kwa sasa imebakia kuwa magofu, huku sehemu kubwa ya kuta zake za nje zikiwa zimepasuka.

    Operesheni ya msako na uokoaji inaendelea kuwasaka watu waliokwama chini ya vifusi vya jengo.

    Rais wa Cuba amesema miongoni mwa watu waliokufa ni pamoja na mwanamke mmoja mjamzito pamoja na mtoto.

    Majeruhi wanatibiwa katika hospitali moja iliyopo karibu.

  4. Chelsea yakubali masharti ya mauzo na mmiliki wa LA Dodgers, Todd Boehly

    Todd Boehly ana hisa katika timu tatu za Los Angeles

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Todd Boehly ana hisa katika timu tatu za Los Angeles

    Klabu ya Chelsea imekubadili masharti kuhusu mauzo ya pauni bilioni 4.25 ($5.2bn) ya klabu kwa muungano wa makampuni unaoongozwa na Todd Boehly, mmiliki mwenza wa timu ya LA Dodgers ya baseball.

    Klabu ya Chelsea ilitangazwa kuuzwa kabla ya mmiliki wake Roman Abramovich kuwekewa vikwazo kwa madai ya uhusiano wake na rais wa Urusi Vladimir Putin kufuatia uvamizi wa Ukraine.

    Taarifa ya Chelsea imesema kuwa mmiliki mpya atalipa pauni bilioni 2.5 kwa ajili ya hisa za klabu. Pesa hizo zitawekwa kwenye akaunti za benki zilizofujwa kwa ajili ya kutolewa kama msaada kwa mashirika ya misaada.

    Muungano huo wa makampuni unaongozwa na Boehly lakini Clearlake Capital, kampuni ya kibinafsi yenye makao yake California, itamiliki hisa nyingi za Chelsea.

    Wawekezaji wengine ni pamoja na bilionea wa Marekani Mark Walter, ambaye pia ni mmiliki mwenza wa LA Dodgers, na bilionea Mswizi Hansjoerg Wyss.

  5. Hujuma za Wabelarus ‘zilichangia kuifanya Urusi ikate tamaa kuuteka mji mkuu Kyiv’

    Baadhi ya vijiji vilivyo  vya Belarus viko karibu na maeneo ya vita baina ya Urusi na Ukraine, na baadhi vimeshuhudia makombora yakianguka kwenye ardhi yake

    Wahujumu katika Belarus walikuwa na mchango mkubwa katika kuilazimisha Urusi kuachana na jaribio lake la kuuteka mji mkuu wa Ukraine Kyiv, kulingana na kiongozi wa upinzani wa Belarus Svetlana Tikhanovskaya.

    Ameiambia BBC kwamba kulikuwa na vitendo 80 vya njama za hujuma dhidi ya leri ambayo inatumiwa kuwapelekea wanajeshi Warusi huduma na silaha kabla ya wao kuondoka kutoka kaskazini mwa Ukraine mwezi mmoja uliopita.

    Amesema kuwa wanaharakati walikuwa wanatoa ujasusi kuhusu matembezi ya wanajeshina ufyatuaji wa makombora.

    Wabelarus wengi - 86% - kati yao walikuwa hawaungi mkono vita, alisema.

    Bi Tikhanovskaya ameema hatma ya Ukraine na Belarus inaunganishwa na ushindi wa Ukraine unaweza kuisaidia Belarus kuwa huru na utawala wa kiimla wa Alexander Lukashenko.

    Baadhi ya vikosi vya Urusi viliingia nchini Ukraine vikitokea Belarus, ambayo inaonekana kama taifa lenye ushirika na Moscow.

    Unaweza pia kusoma:

    • ‘Usiwe kijana wa madhabahu ya Putin’ - Ukosoaji usio wa kawaida wa Papa Francis kwa Patriaki Cyril kwa msaada wake kwa vita vya Ukraine
    • Mfahamu Jenerali wa Putin anayeaminika zaidi mashariki mwa Ukraine
    • Vikwazo vya magharibi vyawakimbiza matajiri wa Urusi kwenda Dubai
  6. Vita vya Ukraine: Kiongozi wa Ukraine achora mstari mwekundu kwa ajili ya mkataba na Urusi

    Zelensky

    Chanzo cha picha, Reuters

    Raia hamsini hawakuweza kuondoka kwenye mji wa shuguli za viwanda vya chuma wa Mauripol Ijumaa.

    Mpango wowote wa amani na Urusi utategemea kurudi nyuma kwenye maeneo vilipokuwa vikosi vya Urusi kabla ya uvamizi, Rais wa Ukraine anasema

    Akizungumza na bodi ya washauri wa masuala ya kisiasa na uchumi mjini London, rais Volodymyr Zelensky alisema kwamba haya hicho ndiokigezo cha chini anachoweza kukubali.

    Amesema amekuwa kiongozi wa ‘’Ukraine, na sio Ukraine nusu ". Lakini hakuitaja Crimea, jimbo lililotwaliwa na Urusi katika mwaka2014.

    Urusi kwa sasa inapigana kuchukua udhibiti kamili wa mji wa Mariupol.

    Bado kuna vikosi vya Ukraine pamoja na baadhi ya raia kusini -mashariki mwa mji wa Azovstal , ambao umekumbwa na mashambulizi makali ya Urusi.

    Kwa hatimayekuuteka mji wa Mauripol yatakuwa ni mafanikio makubwa zaidi katika kipindi cha miezi miwili ya vita na itampa Rais wa Urusi Vladimir Putin kitu fulani cha kusherehekea tarehe 9 Mei ambayo ni siku ya ushindi nchini Urusi-siku ambayo taifa hilo linaadhimisha ushindi wa Usovietidhidi ya Wanazi katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

    Unaweza pia kusoma:

    • ‘Usiwe kijana wa madhabahu ya Putin’ - Ukosoaji usio wa kawaida wa Papa Francis kwa Patriaki Cyril kwa msaada wake kwa vita vya Ukraine
    • Mfahamu Jenerali wa Putin anayeaminika zaidi mashariki mwa Ukraine
    • Vikwazo vya magharibi vyawakimbiza matajiri wa Urusi kwenda Dubai
  7. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mubashara leo Jumamosi tarehe 07.05.2022