Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Rais Mstaafu wa Kenya Hayati Mwai Kibaki amezikwa kijijini kwake Othaya

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameongoza taifa katika mazishi ya mtangulizi wake Hayati Mwai Kibaki huko Othaya Kaunti ya Nyeri.

Moja kwa moja

  1. Na kufikia hapo tunakamilisha matangazo haya ya moja kwa moja. Kwaheri.

  2. Rais Mstaafu wa Kenya Hayati Mwai Kibaki amezikwa kijijini kwake Othaya

    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameongoza taifa katika mazishi ya mtangulizi wake Hayati Mwai Kibaki huko Othaya Kaunti ya Nyeri.

    Mwili wa Rais huyo wa zamani ulishushwa kaburini na Wanajeshi wa Ulinzi wa Kenya muda mfupi baada ya saa kumi na moja jioni mbele ya familia yake, Rais Uhuru Kenyatta, Mke wa Rais Margaret Kenyatta na viongozi kadhaa wa kitaifa miongoni mwao DP William Ruto na Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga.

  3. Habari za hivi punde, Mino Raiola: Wakala wa soka afariki akiwa na umri wa miaka 54

    Mino Raiola, wakala aliyewakilisha baadhi ya wachezaji mashuhuri wa kandanda, amefariki akiwa na umri wa miaka 54.

    Raiola alikuwa wakala wa mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Haaland, kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba na wa AC Milan Zlatan Ibrahimovic.

    Raiola pia alikuwa rais wa Jukwaa la Soka, ambalo liliwakilisha mawakala wakuu na wachezaji wao.

    "Uwepo wake utakosekana milele," familia ya Raiola ilisema kwenye taarifa.

    Iliema "Kwa huzuni isiyo na kikomo, tunashiriki kifo cha wakala anayejali na wa kushangaza wa mpira wa miguu kuwahi kutokea.

    "Mino alipambana hadi mwisho kwa nguvu zile zile alizoziweka kwenye meza za mazungumzo kuwatetea wachezaji wetu. Kama kawaida, Mino alitufanya tujivunie na kamwe hakutambua.

    Raiola, ambaye pia alimwakilisha mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, fowadi wa Italia Mario Balotelli na beki wa kati wa Uholanzi Matthijs de Ligt, alikuwa mtu mwenye utata na ushawishi mkubwa katika soka la dunia.

  4. Urusi yaizuia ndege ya Ukraine kuingia katika anga yake

    Makombora mawili yaligonga kiwanda cha kusafisha mafuta katika eneo linalopakana na Ukraine wakati vitengo vya ulinzi wa anga vya Urusi vilipoizuia ndege ya kivita ya Ukraine iliyokuwa ikijaribu kuingia anga ya Urusi, gavana wa eneo la Bryansk amesema.

    Alexander Bogomaz alisema wimbi la mlipuko kutoka kwa tukio hilo liliharibu sehemu za kituo cha mafuta lakini hakukuwa na majeruhi.

    Urusi haijabainisha katika chapisho lake kwenye Telegram ikiwa milipuko hiyo ilitokana na moto wa ulinzi wa anga wa Urusi au ilitokana na makombora yaliyorushwa kutoka kwa ndege ya kijeshi ya Ukraine.

    Mapema wiki hii, magavana wa Bryansk na eneo jirani la Kursk walisema kwamba vituo viwili vya ukaguzi vya mpaka viligongwa na makombora "kutoka Ukraine".

    BBC haijafanikiwa kuthibitisha madai hayo.

    Unaweza pia kusoma

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
    • SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
  5. Ufaransa yaahidi kuongeza msaada wa kijeshi na kibinadamu kwa Ukraine

    Rais Emmanuel Macron anasema Ufaransa itaongeza msaada wa kijeshi na wa kibinadamu kwa Ukraine, kufuatia mazungumzo na Volodymyr Zelensky.

    Macron pia alisisitiza "wasiwasi wake mkubwa" juu ya mashambulizi ya Urusi katika miji ya Ukraine na "hali isiyoweza kufumbiwa macho" katika mji wa bandari wa kusini wa Mariupol.

    Marekani, Ufaransa na washirika wengine wameipatia Kyiv mamia ya silaha za masafa marefu ili kuisaidia kukabiliana na mashambulizi ya Moscow katika eneo la Donbas mashariki mwa Ukraine.

    Ofisi ya rais wa Ufaransa pia inasema msaada kwa Ukraine ni sawa na "zaidi ya tani 615 za vifaa, ikiwa ni pamoja na vifaa vya matibabu, jenereta kwa hospitali, chakula cha msaada, malazi na magari ya dharura".

  6. Ukraine yaishutumu Urusi kwa kuiba nafaka

    Naibu waziri wa kilimo wa Ukraine ameishutumu Urusi kwa kuiba tani laki kadhaa za nafaka kutoka katika eneo linalokaliwa na vikosi vyake.

    Akizungumza kwenye televisheni ya taifa ya Ukraine Taras Vysotskyi, alisema anahofia kwamba Urusi inaweza kuiba tani nyingi za tani milioni 1.5 za nafaka katika maeneo ambayo sasa inadhibitiwa.

    Urusi haijazungumzia madai hayo, lakini jeshi lake limekumbwa na hasara kubwa kiuchumi.

    Mashambulio ya makombora ya Urusi na hatua yake ya kuziba bandari ya Bahari Nyeusi ya upande wa Ukraine yametatiza uzalishaji wa nafaka, na kuzua wasiwasi wa kimataifa juu ya kupanda kwa bei ya vyakula.

    Ukraine ni mojawapo ya wauzaji wa juu wa mafuta ya nafaka na mboga duniani. Imepewa jina la utani "ghala la mkate" la Uropa.

    Vysotskyi amewahakikishia wananchi wa Ukraine kwamba hawatakabiliwa na uhaba wa chakula kwa sababu ya usumbufu huo.

    Meli ya mizigo iliyobeba zaidi ya tani 71,000 za mahindi ya Ukraine iliondoka kwenye bandari ya Romania ya Constanta siku ya Alhamisi - ya kwanza tangu Urusi ilipoivamia Ukraine tarehe 24 Februari.

    Constanta inashughulikia mauzo ya nje ya Ukraine kwa ushirikiano wa Romania ya mshikamano, kwani jeshi la wanamaji la Urusi inashikilia bandari Odesa, kitovu kikuu cha usafirishaji wa Ukraine.

    Nafaka ni suala nyeti sana nchini Ukraine, na familia nyingi zina kumbukumbu za njaa ya miaka ya 1930 ("Holodomor"), iliyosababishwa na uhamisho wa Sovieti wa wakulima matajiri ("kulaks") na unyakuzi wa mashamba.

  7. Urusi yajibu kauli ya 'ukatili' iliyotolewa na Marekani dhidi yake

    Balozi wa Urusi nchini Marekani Anatoly Antonov amepinga shutuma za msemaji wa Pentagon John Kirby kwamba Rais wa Urusi Vladimir Putin alitenda kwa "ukatili" katika uvamizi wake nchini Ukraine.

    Hapo jana, Kirby alionekana kuwa na hisia kali alipouliza jinsi mtu yeyote "mwenye maadili" angeweza kuhalalisha ukatili unaofanywa na Urusi.

    Lakini katika chapisho la mtandao wa kijamii, Bw Antonov alielezea kauli ya Kirby kama "ya kuudhi na isiyokubalika".

    "Imekuwa kawaida maafisa wa utawala huweka maamuzi yao juu ya uwongo chafu wa mamlaka ya Ukraine," Bw Antonov alisema.

    Balozi wa Urusi aliongeza kuwa Marekani haitaki uhasama nchini Ukraine ukomeshwe.

    "Kilicho muhimu kwa John Kirby na wenzake ni kwamba tata ya kijeshi na viwanda vya Amerika inapokea mapato ya ziada kwa kuondoa silaha za kizamani kutoka kwa maghala yao.

    "Alimalizia kwa kusema Bw Kirby "amepoteza heshima ya afisa wa Marekani, kwa kutumia matusi ya mitaani".

  8. Kwa picha: Ibada ya mwisho za Rais wa zamani wa Kenya Mwai Kibaki

    Misa ya Mazishi ya Rais Mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki ilihudhiriwa na wakenya wa tabaka mbali mbali

  9. Ibada ya mazishi ya Mwai Kibaki inaendelea muda huu

    Ibada ya mazishi ya Rais wa zamani wa Kenya Mwai Kibaki anaendelea huko Othaya, Nyeri.

    Ibada hiyo inaongozwa na Kanisa Katoliki ambalo marehemu alikuwa mshirika.

    Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wanahudhudia ibada hiyo.

  10. Marekani yaishtumu Urusi kwa 'kufanya ukatili' nchini Ukraine

    Wizara ya Ulinzi ulinzi ya Marekani imemshutumu Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa kutekeleza"ukatili" katika uvamizi wake nchini Ukraine.

    Msemaji wa Pentagon John Kirby alionekana mwenye hisia kali alipoelezea "ukatili" wa Urusi nchini Ukraine.

    Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky siku ya Ijumaa alisema kuwa bado yuko tayari kufanya mazungumzo ya amani na Bw Putin.

    Lakini alisema anahofia huenda mazungumzo ya amani yasifanyike huku na Urusi ikiendelea na uvamizi wake.

    Akizungumza na vyombo vya habari vya Poland, Bw Zelensky alisema alitaka kukutana na Bw Putin kwa sababu "mtu mmoja ndiye anayeamua kila kitu" nchini Urusi.

    Lakini uharibifu ulioachwa na vikosi vya Urusi katika maeneo yaliyokaliwa umefanya majadiliano yoyote kuwa magumu, alisema.

    "Baada ya Bucha na Mariupol watu wanataka kuwaua tu. Wakati kuna hisia kali kama hiyo, ni vigumu kujadili chochote.

    Siku ya Alhamisi, Ukraine ilitangaza kuwasaka wanajeshi 10 wa Urusi wanaotuhumiwa kwa uhalifu wa kivita huko Bucha - kitongoji kilicho kaskazini mwa Kyiv ambapo takriban raia 400 waliuawa.

    Unaweza pia kusoma

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
    • SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
  11. Wakazi wa Othaya wajitokeza kumuaga Hayati Mwai Kibaki

    Wakazi wa Othaya, eneo la kati mwa Kenya wamejitokeza kumuaga aliyekuwa Rais wa Kenya Mwai Kibaki.

    Msafara huo wa mazishi uliondoka Nairobi leo asubuhi kwa barabara.

    Ibada ya mazishi itafanyika katika uwanja wa Shule ya Approved yaOthaya, kabla ya Kibaki kuzikwa nyumbani kwake Othaya.

  12. Mzozo ya Ukraine: Mukhatasari wa habari za hivi punde

    Ikiwa ndio mwanzo unajiunga nasi haya ndio yanayojiri nchini Ukraine

    • Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky asema kuwa yuko tayari kufanya mazungumzo ya amani na Rais wa Urusi Vladimir Putin licha ya ukatili wa Urusi dhidi ya nchi yake.
    • Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov anasema kuwa nchi yake haioni kuwa iko vitani na Nato, shirika la habari la serikali Ria limeripoti.
    • Afisa mkuu wa ulinzi amesema Marekani haiamini kuwa Urusi itatumia silaha za nyuklia, Reuters inaripoti.
    • Pentagon imemshutumu rais wa Urusi kwa "kufanya ukatili" katika uvamizi wake Ukraine.
    • Urusi imejaribu kubadilishana raia wa Ukraine na wanajeshi wa Urusi waliokamatwa kinyume na Mkataba wa Geneva, kulingana na naibu waziri mkuu wa Ukraine.
    • Balozi wa Uingereza amerejea Kyiv, akijiunga na balozi 27 za kigeni zinazofanya kazi nchini humo kwa sasa.
  13. Rais Mstaafu wa Kenya Hayati Mwai Kibaki kuzikwa leo

    Msafara wa mazishi ya Hayati Rais Mstaafu wa Kenya Emilio Mwai Kibaki umeondoka makafani ya Lee Jijini Nairobi kuelekea nyumbani kwake Kaunti ya Nyeri.

    Mwili wa Rais huyo wa Tatu wa Kenya utapitia Kaunti za Kiambu, Murang'a, Kirinyaga na Nyeri ili kuwapa wakazi wa eneo la Kati mwa Kenya fursa ya kumuaga kiongozi wao mpendwa na aliyehudumu kwa muda mrefu.

    Mara baada ya Ibada ya Mazishi ya Kiserikali katika Uwanja wa Shule ya Othaya, mwili wa hayati Mwai Kibaki, aliyefariki Ijumaa wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 90, utazikwa nyumbani kwake Munyange viungani mwa mji wa Othaya.

  14. Karibu kwa matangazo ya moja kwa moja leo Jumamosi 30.04.2022.