Vikosi vya Ukraine vinavyoulinda mji wa Mauripol vyatakiwa na Urusi kujisalimisha
Urusi imesema kuwa itahakikisha kunakuwa na usalama wa maisha ya wanajeshi wa Ukraine katika Mariupol wanaojisalimisha watakaojisalimisha katika kipindi cha saa kadhaa zijazo.
Moja kwa moja
Papa azungumzia 'vita vya Pasaka'

Chanzo cha picha, Reuters
Papa Francis amewataka viongozi kusikiliza kilio cha watu kwa ajili ya amani nchini Ukraine na kuikosoa Urusi kwa kuivuta nchi katika mzozo "katili na usio namaana ".
Akizungumza wakati wa ibada yake ya Misa ya Pasaka ya Jumapili, iliyohudhuliwa na watu wapatao 50,000 katika uwanja wa St Peter's Square, Papa Francis amesema : "Macho yetu, pia, hayaamini katika vita vya Pasaka. Tumeona damu nyingi, ghasia nyingi sana.
Mioyo yetu, pia imejawa na hofu na uchungu, kwasababu wengi wa makaka zetu na madada zetu wamelazimika kujifungia mbali ili kuwa salama kutokana na mashambulio ya mabomu."
Ukraine "imechoshwa kabisa na ghasia na uharibufu wa vita vya kikatili visivyo na maana ambavyo imevutwa ndani yake", aliongeza katika Misa yake ya kwanza ya Pasaka tangu mwaka 2019 ambayo umma uliruhusiwa kuhudhuria kufuatia miaka miwili ya sheria za udhibiti wa Covid.
Habari za hivi punde, Vita vya Ukraine: Kombora lapiga Kharkiv na kusababisha mauaji
Watu watano wameuawa na wengine 13 wamejeruhiwa katika ufyatuaji wa makombora yaliyopiga katika mji wa Kharkiv, maafisa wa eneo hilo wamesema.
"Waokoaji wanatoa huduma katika eneo la tukio ," shirika la utangazaji la umma la Ukraine Suspilne limeripoti.
Tutatoa maelezo zaidi kadri tunavyoyapokea.
Vita vya Ukraine: Jenerali mwingine wa Urusi auawa
Naibu kamanda wa kikosi cha 8 cha Urusi , Vladimir Petrovich Frolov, amefariki katika vita vya Ukraine, limeripoti shirika la habari la UrusiTASS.
Taarifa hiyo ilithibitishwa na gavana wa St Petersburg Alexander Beglov. Beglov alisema: "Vladimir Petrovich Frolov amekufa kifo cha kishujaa katika mapambano na wanaopendelea utaifa wa Ukraine."
Gavana alisema Frolov "alijitolea maisha yake ili Watoto , wanawake na wazee katika Donbas wasiweze kusikiliza tena milipuko ya mabomu. Kuacha kusubiri kifo na kuishi nyumbani, kusema kwaheri utadhani ulikuwa muda wa mwisho ".
Lakini ufyatuaji mwingi wa mabomu unaofanyika katika Ukraine hufaywa na Urusi.
Kipindi chote cha vita majenerali kadhaa na wanajeshi wengine wa vyeo vya juu wameripotiwa kuuawa. Sio jambo la kawaida kwa maafisa wa ngazi ya juu wa jeshi kujiweka katia hatari kwa kuwa karibu sana na maeneo ya mapigano, na vyanzo vya magharibi vinaamini kuwa wamefanya hivyoili kupata udhibiti wa operesheni walizonazo, katika baadhi ya maeneo, ambako wamekwama vibaya.
Vita vya Ukraine: Urusi yapiga kombora kwenye kiwanda cha silaha karibu na Kyiv, Urusi yasema Russia

Chanzo cha picha, Getty Images
Msemaji wa w izara ya ulinzi ya Urusi Igor Konashenkov amesema kuwa vikosi vya kijeshi vya Urusi vimeangamiza kiwanda cha silaha karibu na Kyiv, kulingana na shirika la habari la Reuters.
Awali, kulikuwa na ripoti kuwa milipuko katika mji mkuuwa Ukraine Kyiv. Lakini kuna taarifa chache juu ya ni wapi shambulio hilo lilifanyika.
Konashenkov alisema: "Usiku mzima, mashambulio ya hali ya juu ya makombora ya anga yaliharibu kiwanda karibu na mji wa Brovary katika mji wa Kyiv".
Vikosi vya Ukraine vinavyoulinda mji wa Mauripol vyatakiwa na Urusi kujisalimisha

Chanzo cha picha, Maxar via Reuters
Maelezo ya picha, Vikosi vya Ukraine vinafikiriwa kuwa ndio vikosi vyenye upweke na vilivyo katika eneo lenye viwanda vingi na vikubwa la Azovstal vya chuma Urusi imesema kuwa itahakikisha kunakuwa na usalama wa maisha ya wanajeshi wa Ukraine katika Mariupol wanaojisalimisha watakaojisalimisha katika kipindi cha saa kadhaa zijazo.
Kuanzia saa kumi na mbili za Urusi au saa tisa alasiri kwa saa za Afrika mashariki, na baada ya hapo vikosi vya Urusi vimesema vitawaruhusu wanajeshi kuondoka kutoka katika eneo lenye viwanda vya chuma la Azovstal - ili mradi waache silaha zao na zana nyinginezo za kijeshi nyuma.
Wale ambao watafanya hivyo watatendewa kulingana na mkataba wa Geneva kuhusu wafungwa wavita, taarifa kutoka Wizara ya ulinzi ilisema.
Taarifa iliyotolewa saa kadhaa zilizopita imekuwa ikitangazwa kwa kina maelezo ya mkataba kwa wanajeshi wa Ukraine kila baada ya dakika 30 usiku mzima.
Kama watakubali, Urusi inasema, vikosi vya Urusivitapandisha bendera nyekundu saa kumi na mbili alfajiri na Ukraine inapaswa kupandisha bendera nyeupe kuzingira ukuta wote wa kiwanda cha chuma.
Maafisa wa Ukraine hawajatoa ishara yoyote kwamba wanapanga kukubali ofay a kuondoka eneo hilo wala kujisalimisha.
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mubashara leo Jumapili tarehe 17.04.2022
