Urusi yaishutumu Ukraine kwa shambulio la mpakani
Wachunguzi wa Urusi wanasema kuwa Ukraine ilifanya mashambulizi ya anga kwenye eneo la makazi nchini Urusi mapema leo.
Maafisa wanasema helikopta mbili za kijeshi zinazoruka chini zikiwa na silaha nzito zilishambulia mji wa Klimovo, na kuwajeruhi watu saba akiwemo mtoto na kuharibu nyumba sita.
Ripoti za shambulio hilo - ambazo hazijathibitishwa kwa njia huru - zilikuja baada ya Moscow kutangaza kuwa itashambulia kwa mabomu maeneo ya Kyiv na maeneo mengine ya Ukraine ikiwa vikosi vya Ukraine vitaendelea kushambulia eneo lake.
Kulingana na gavana wa eneo la Belgorod la Urusi, kijiji cha Spodaryushino kilipigwa makombora na Ukraine, na kusababisha uhamishaji wa watu .
Akiandika kwenye Telegram, Vyacheslav Gladkov alisema hakuna mtu aliyejeruhiwa na hakuna majengo yaliyoharibiwa.
Madai hayo yanajiri baada ya maafisa wa Urusi kuishutumu Ukraine kwa kufanya mashambulizi ya anga kwenye eneo jingine la makazi ya watu katika mji wa Klimovo katika eneo la Bryansk.
Wiki mbili zilizopita, bohari ya mafuta pia ilichomwa moto huko Belgorod - Urusi ilidai Ukraine ilihusika na hii pia.
BBC haiwezi kuthibitisha ni nani aliyehusika na matukio haya, lakini Ukraine ilikanusha kugonga bohari ya mafuta ya Belgorod mapema mwezi huu.
Unaweza pia kusoma
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine