Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uharibifu wa Borodynka ni wa ‘kutisha zaidi’ kuliko wa Bucha
"Miili ishirini na sita yatolewa kutoka kwa vifusi huko Borodyanka"
Moja kwa moja
'Yasiyoweza kufikirika yamefanyika hapa ': Mkuu wa EU aitembelea Bucha Ukraine
Ursula von der Leyen, rais wa Tume ya muungano wa Ulaya, amekuwa akiutembelea mji wa Bucha uliopo kaskazini mwa mji mkuu wa Ukraine Kyiv . Bucha ulikuwa ni mji ambapo miili ya raia ilipatikana iliwa imetapaa kwenye mtaa baada ya Urusi kuondoka mjini humo.
Urusi inakanusha kuwauwa rai ana imeishutumu Ukraine kwa kupanga mauaji kwa ajili ya kuviharibia sifa vikosi vyake. Hatahivyo kuna Ushahidi thabiti na unaoendelea kujitokeza kwamba uhalifu wa kivita ulitekelezwa na Urusi.
"INi jambo lisiloweza kufikirika ambalo limetokea hapa ," alisema von der Leyen wakati wa zaiara yake. "Tumeshuhudia sura katili ya jeshi la Putin."
Unaweza pia kusoma
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Wito wa kuwalinda raia katika mapambano dhidi ya Majihad wa Sahe
Muungano wa watu kwa ajili ya Sahel (People’s Coalition for the Sahel) umezitolea wito serikali za mali, Niger na Burkina Faso kuwalinda raia wakati wa mapigano dhidi ya wanamgambo wa Kiislam.
Muungano huo umetaja mapambano ya hivi karibunikatika kati mwa mali ambako wakazi walisema watu 300 waliuawa na wanajeshi pamoja na mamluki wa Urusi.
Baadhi ya wale waliokamatwa katika kijiji cha Moura waliamrishwa kuchimba makaburi kabla ya kupigwa risasi na kuuawa.
Muungano huo wa mashirika yasiyo ya kiserikali unataka hili na maasi mengine yachunguzwe.
Ulisema kutowaadhibi wahusika kunafanya watu kutokuwa na imani na taifa na kuchochea watu wengi kujiunga na makundi yenye silaha.
Misri yaanzisha uchunguzi juu ya mauji ya ufukweni ya kasisi wa Kanisa la Coptic
Mwendesha mashitaka mkuu wa Misri ameanza upelelezi juu ya mauaji yakasisi Mkristo wa dhehebu la Coptic yaliyofayika katika jiji la Alexandria kwenye bahari ya Mediterranean.
Father Arsanios Wadid, wa kanisa la Virgin Mary ( Bikra Maria), alidungwa kisu siku ya Alhamisi nje ya klabu moja iliyoko ufukweni.
Mwanaume mmoja mkongwe baadaye alikamatwa na polisi.
Wakristo wa dhehebu la Coptic – ambao ni 10% ya raia wa Misri ambao ni milioni 95-wamekuwa wakilalamika kwa muda mrefu kwa kuwa waathiriwa wa mara kwa mara wa ghasia za uhalifu wenye misingi ya chuki.
Kramatorsk: Takriban watu 1,000 walikuwa katika kituo cha treni roketi zilipopigwa - shahidi
Zaidi ya watu 1,000 walikuwa wamekusanyika katika stesheni ya reli mashariki mwa Ukraine ilipopigwa na roketi siku ya Ijumaa, mtu aliyeshuhudia ameambia BBC.
Watu 40 wamefariki dunia wakiwemo watoto 10 wakati makombora yalipolipuka katika kituo cha Kramatorsk wakati raia walipokuwa wakipanga foleni kuhamia eneo salama, kulingana na meya wa eneo hilo.
Picha kutoka eneo la tukio zinaonyesha miili na mifuko iliyotelekezwa ikiwa kwenye jukwaa lakusubiria treni. Ukraine ilisema Urusi ililenga raia, lakini Urusi imekanusha shambulio hilo.
Nathan Mook, mfanyakazi wa kutoa misaada ambaye aliona watu wakisongamana kwenye kituo hicho, alihesabu kati ya milipuko mitano hadi 10: "Dakika mbili baada ya sisi kupita, unaihisi kabla ya kuisikia: boom, mlipuko".
Bw Mook alisema aliona zaidi ya watu 1,000 katika kituo hicho muda mfupi kabla ya shambulio hilo kutokea, na ofisi ya mwendesha mashtaka wa eneo hilo ilisema karibu watu 4,000 walikuwepo wakati huo, hasa wanawake na watoto.
Zaidi ya watu 80 walijeruhiwa, maafisa walisema.
Uingereza yawawekea vikwazo mabinti zake Putin
Uingereza imewawekea vikwazo mabinti wawili watu wazima wa Rais wa Urusi Vladimir Putin.
Majina ya binti zake - Katerina Vladimirovna Tikhonova na Maria Vladimirovna Vorontsova - sasa yameongezwa kwenye orodha ya vikwazo vya Uingereza.
Ni sehemu ya juhudi "zilizoratibiwa" na Marekani, ambayo tayari imeweka vikwazo kwa wanawake hao wawili.
Serikali ya Uingereza pia imemuwekea vikwazo bintiye waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov, Yekaterina Sergeyevna Vinokurova.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari ya ofisi ya Mambo ya Nje, serikali ya Uingereza ilisema inalenga zaidi "maisha ya kifahari ya watu wa karibu wa Kremlin", na marufuku ya kusafiri na kufungia mali kwa watatu hao.
Kwa mujibu wa serikali ya Uingereza, zaidi ya £275bn ya kitengo cha vita cha Putin sasa imehifadhiwa na vikwazo vilivyoratibiwa vya Uingereza na kimataifa katika wiki za hivi karibuni.
Imeongeza kuwa Urusi inaelekea kwenye mdororo mkubwa zaidi wa uchumi tangu kuporomoka kwa Umoja wa Kisovieti huku vikwazo vikiathiri uwezo wa Rais Putin wa kuanzisha vita nchini Ukraine.
Soma zaidi:
Zaidi ya watu 30 wauawa katika shambulizi la kombora kwenye kituo cha treni – Ukraine
Kampuni ya reli inayomilikiwa na serikali imesema zaidi ya watu 30 wameuawa na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa katika shambulio la roketi la Urusi kwenye kituo cha treni cha Kramatorsk.
Kramatorsk kilikuwa mojawapo ya stesheni za mashariki kabisa ambazo bado zinaendelea kufanya kazi nchini Ukraine, na gavana wa Donetsk alisema maelfu ya watu walikuwa pale wakati huo, wakijaribu kupanda treni nje ya eneo hilo.
Mkuu wa reli ya Ukraine alisema roketi mbili zilipiga kituo hicho.
Katika ujumbe kwenye Telegram, mwenyekiti wa Shirika la Reli la Ukraine, Oleksandr Kamyshin, aliandika kwamba kituo cha treni katika jiji la Kramatorsk huko Donetsk imepigwa kwa makombora.
Aliongeza, "kuna waathirika".
Halmashauri ya jiji la Kramatorsk imewaonya watu kukaa kwenye makazi.
Kramatorsk ilijulikana sana kuwa mojawapo ya njia kuu za uokoaji kutoka mashariki mwa Ukrainia.
Maelezo ya treni zinazoondoka jijini yalikuwa yakitumwa na mamlaka za mitaa.
Soma zaidi:
Dmitry Peskov asema hasara ya wanajeshi wa Urusi ni "janga kubwa"
Urusi imekiri kupata "hasara kubwa" ya wanajeshi nchini Ukraine, huku uvamizi huo ukiingia siku yake ya 44.
Msemaji wa rais Dmitry Peskov aliambia kituo cha Uingereza cha Sky News kuwa waliopoteza maisha ni "janga kubwa kwetu".
Alisema anatumai Moscow itafikia malengo yake ya vita "katika siku zijazo".
Maoni ya Bw Peskov yalifuatia kutimuliwa kwa Urusi katika baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatano.
Baadhi ya wajumbe 93 kati ya 193 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa walipiga kura kuunga mkono karipio hilo la kidiplomasia, lililofuatia madai ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na wanajeshi wa Urusi katika mji uliokuwa unakaliwa kwa mabavu wa Bucha kaskazini mwa Ukraine.
Moscow ilitangaza kujiuzulu kutoka kwa baraza hilo wakati inajibu.
Chombo hicho kilionyesha "wasiwasi wake mkubwa juu ya mzozo unaoendelea wa haki na mzozo wa binadamu", na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliishutumu Urusi kwa ukatili zaidi huko Borodyanka, mji ulio karibu na mji mkuu wa Kyiv.
Bw Peskov alikanusha pendekezo lolote kwamba wanajeshi wa Urusi walihusika na mauaji katika mji wa Bucha na kuliambia shirika la utangazaji kwamba "tunaishi katika siku za kughushi na uwongo".
Alidai bila msingi wowote kuwa picha za raia waliouawa katika mji huo zilizoonyeshwa ni za kughushi.
Walakini, kukiri kwake kwamba Urusi imepata hasara kubwa ni ya kushangaza.
Mnamo tarehe 25 Machi, Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilisema wanajeshi wake 1,351 waliuawa katika mapigano.
Ukraine imekadiria vifo vya Warusi kuwa karibu 19,000.
Hata hivyo, si Urusi wala Ukraine makadirio ya hasara ya Urusi yanaweza kuthibitishwa kwa kujitegemea - na wachambuzi wametahadharisha kuwa Urusi inaweza kuwa inapunguza kiwango chake cha wahasiriwa, wakati Ukraine inaweza kuiongeza ili kuongeza ari yake.
Viongozi wa nchi za Magharibi wanaamini kuwa kati ya wanajeshi 7,000 na 15,000 wa Urusi wameuawa.
Soma zaidi:
Kondoo azaa watoto 10 kwa wakati mmoja, Uingereza
Katika hali isiyo ya kawaida kondoo amezaa watoto 10 kwa wakati mmoja , mfugaji amesema.
Mmiliki wa mifugo hiyo Rupert Burr alielezea kuwa tukio hilo ni "la ajabu sana" kwa watoto wa kondoo kuzaliwa wengi kwa wakati mmoja mwishoni mwa mwezi Machi.
Tukio hilo la nadra lilitokea kwenye shamba la Roves ambapo ni kituo cha wageni cha huko Sevenhampton, Swindon.
Mkulima Megan Priest alisema kuwa alitarajia watoto wa kondoo watatu tu lakini alishtuka kuona wengine wawili walipozaliwa.
Bw Burr alisema: "Uwezekano wa hili ni mdogo sana, wanasema inawezekana kuwa moja kati ya milioni kwa kondoo kupata watoto watano kwa wakati mmoja,na baada ya muda mfupi kuzaa wengine hivyo kuwa kumi katika siku chache ni jambo la ajabu sana." Bibi Priest aliongeza:
"Yule kondoo alizaa watoto watatu ambao tuliwaweka kwenye zizi ili kuwaosha, kisha tukarudi na kuwakuta wengine wawili wamezaliwa.
"Ni nadra sana, haswa kwa idadi ya kondoo tulio nao, unaweza kutarajia labda kupata kondoo watano, na sio wote walio hai, lakini kuwa kumi na wote kuwa hai inashangaza sana."
Bw Burr anafanya biashara ya familia katika shamba ambalo baba yake alilianza mwaka 1951.
Ameishi kwenye shamba hilo maisha yake yote, akifanya biashara hiyo tangu mwaka 1970.
Binti yake, Pippa Burr, alisema walikuwa na bahati sana na wana-kondoo wao. "Nilinunua kondoo wangu miaka kumi na moja iliyopita na wamenifanya nijivunie," alisema.
"Saa zake ndefu sana na kazi ngumu lakini unapowaona wakirukaruka inafurahisha sana."
Israel: Mshambuliaji wa kipalestina auawa baada ya shambulio baya katika baa ya Tel Aviv
Vikosi vya usalama vya Israel vimemuua Mpalestina mmoja ambaye alifyatua risasi kwenye baa moja mjini Tel Aviv na kuwaua watu wawili na kuwajeruhi wengine 12, polisi wamesema.
Mwanamume huyo, kutoka Jenin katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, alifuatiliwa hadi karibu na Jaffa na alifariki katika ufyatulianaji wa risasi.
Saa kadhaa mapema alikuwa amewashambulia watu kwenye baa kwenye Mtaa wa Dizengoff, mojawapo ya mitaa yenye shughuli nyingi zaidi mjini Tel Aviv, na kusababisha msako mkali wa usiku mzima.
Hilo lilikuwa ni tukio la hivi punde zaidi katika msururu wa mashambulizi nchini Israel ambayo yamesababisha vifo vya watu 13.
Mshambuliaji huyo, aliyetambulika kama Raad Hazem, 29, alipatikana akijificha karibu na msikiti takriban maili nne (6km) kutoka eneo la tukio. Aliuawa baada ya makabiliano mafupi ya risasi na maafisa wa kukabiliana na ugaidi na usalama.
Maafisa walisema zaidi ya maafisa 1,000 wa polisi wa Israel, vikosi maalum vya jeshi na idara ya ujasusi ya Shin Bet walihusika katika msako huo.
Waziri Mkuu wa Israel Naftali Bennett, ambaye alikuwa katika makao makuu ya ulinzi huko Tel Aviv karibu na eneo la ufyatuaji risasi wakati ulitokea, anakutana na wakuu wa usalama Ijumaa asubuhi.
Rais Tshisekedi kusaini mkataba wa kujiunga EAC
Rais wa Jamhuri ya Demikrasia ya Kongo Felix Tshisekedi amewasili mjini Nairobi amefanya ziara ya kitaifa ambapo anatarajiwa kusaini makubaliano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Wakati wa ziara yake, Rais Tshisekedi atasaini mkataba wa kujiunga na jumuiya hiyo mbele ya mwenyekiti wa jumuiya hiyo Uhuru Kenyatta.
DRC ilikubaliwa kuwa mwanachama wa saba wa jumuiya hiyo tarehe 29 Machi, baada ya wakuu wa nchi za EAC kupitisha pendekezo la baraza la mawaziri wakati wa mkutano wa 19..
Viongozi kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanatarajiwa pia katika sherehe hizo ambapo watazindua ramani mpya ya jumuiya hiyo itakayojumuisha DRC.
Rais Kenyatta na Tshisekedi pia wanatarajiwa kuweka saini mikataba ya ushirikiano.
- DRC ndani ya EAC: Nini maana yake?
- DRC inaweza kukubaliwa kuwa sehemu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki?
Uingereza: Wanajeshi wa Urusi wametoka kaskazini mwa Ukraine
Wanajeshi wa Urusi sasa "wamejiondoa kikamilifu" kutoka kaskazini mwa Ukraine, wakirejea kaskazini mwa Belarus na Urusi imesema Wizara ya Ulinzi ya Uingereza.
Baadhi ya vitengo hivyo vitahamishiwa mashariki mwa Ukraine kupigana huko Donbas. Lakini vikosi vingi vitahitaji "kuletwa tena" kabla ya kutumwa.
"Usafirishaji wowote wa wanajeshi wengi kutoka kaskazini [una uwezekano] kuchukua angalau wiki moja," wizara ilisema katika taarifa yake ya asubuhi.
Imeongeza kuwa mashambulizi ya makombora ya Urusi katika miji ya mashariki na kusini mwa Ukraine yanaendelea na wanajeshi wa Urusi wamesonga mbele kusini kutoka mji muhimu wa kimkakati wa Izyum.
Unaweza pia kusoma
KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
Takriban watu sita wauawa katika mlipuko DRC
Takriban watu sita waliuawa na wengine 15 kujeruhiwa baada ya mlipuko katika baa katika kambi ya kijeshi ya Katindo huko Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Wizara ya mawasiliano ilituma ujumbe wa Twitter siku ya Alhamisi usiku kuwa idadi ya waathiriwa ilikuwa ya awali, huku ikirekebisha idadi kubwa ya vifo iliyotangazwa na msemaji wa serikali Patrick Muyaya.
Miongoni mwa wahasiriwa ni kanali luteni na mkewe, kapteni, mmiliki wa baa hiyo na rafiki yake, pamoja na kijana wa miaka 12.
Uchunguzi umeanzishwa kuhusu mlipuko huo .
Mwishoni mwa 2020, serikali ilitangaza kwamba kambi ya kijeshi ya Katindo itahamishwa nje ya jiji ili kupunguza ukaribu wake na wakazi wa Goma wa watu milioni mbili. Hili hata hivyo bado halijatekelezwa.
Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo linapambana na makundi mengi ya waasi mashariki mwa nchi hiyo - lakini bado haijabainika kama mlipuko huo ulitokana na shambulizi.
Gavana wa kijeshi wa jimbo la Kivu Kaskazini ametoa wito kwa watu kuwa watulivu na kuepuka uvumi wakisubiri uchunguzi.
- DR Congo: FARDC yaishtumu Rwanda kwa kuisaidia M23
- Kwanini vikosi vya Uganda vimeingia DRC kwa mara nyingine?
Australia yatuma magari ya kivita Ukraine
Australia imetuma lori tatu za kwanza kati ya 20 za kijeshi zenye silaha inazotoa kwa Ukraine, kufuatia ombi la Rais wa Ukraine Zelensky wiki iliyopita.
Magari ya Bushmaster yaliyoimarishwa sana yatatumika kusafirisha wanajeshi na raia katika eneo la vita - hayatatumika kwa mashambulizi .
Zelensky alitoa hotuba ya video kwa bunge la Australia wiki iliyopita - taifa la 20 alilozungumza nalo - akiishukuru nchi hiyo kwa usaidizi wake thabiti hadi sasa.
Australia imeahidi kutoa zaidi ya A$190m (£108m; $142m) katika usaidizi wa kijeshi na kibinadamu na kuweka vikwazo kadhaa kwa watu wa Urusi na uagizaji wa mafuta.
"Mheshimiwa Rais, watu wa Australia wanasimama na Ukraine katika vita vyako vya kuishi," alisema Waziri Mkuu Scott Morrison akimjibu Zelensky wiki iliyopita.
Kiongozi wa Australia ametangaza mara kwa mara kwamba demokrasia huria lazima ziungane ili kutetea uhuru na "haki ya kuishi bila kulazimishwa, vitisho na ukatili ".
Alisema Australia ilimheshimu Zelensky kama "Simba wa demokrasia".
Unaweza pia kusoma
KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
"Miili ishirini na sita yatolewa kutoka kwa vifusi huko Borodyanka"
Miili 26 imeopolewa kutoka chini ya vifusi vya majengo mawili ya ghorofa yaliyoharibiwa huko Borodyanka, kaskazini-magharibi mwa Kyiv, kulingana na mwendesha mashtaka mkuu wa Ukraine.
Iryna Venediktova aliishutumu Moscow kwa kulenga maeneo ya raia kimakusudi, katika chapisho kwenye Facebook.
"Hakuna eneo la kijeshi hapa," alisema, akiongeza kuwa vikosi vya Urusi "viliweka makombora miundombinu ya makazi nyakati za jioni, wakati kulikuwa na idadi kubwa ya watu nyumbani".
Venediktova alidai kulikuwa na "ushahidi wa uhalifu wa kivita wa vikosi vya Urusi kila upande".
Unaweza pia kusoma
KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja leo Ijumaa tarehe 8 Aprili 2022