Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Mauaji ya raia wa Bucha ni mauaji ya kiholela- Ukraine

Wakati majeshi ya Moscow yakiondoka maeneo karibu na Kyiv, kuna ushahidi unaoongezeka wa mauaji ya kiholela.

Moja kwa moja

  1. Na kufikia hapo tunakamilisha matangazo haya ya moja kwa moja. Hadi kesho Kwaheri.

  2. Hii ndio sababu tunashambuliwa na kuangamizwa - Zelensky

    Raia wa Ukraine hawataki kutawaliwa na Urusi na wanashambuliwa na kuangamizwa kutokana na hilo, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema.

    Akizungumza na CBS News kupitia mfasiri siku ya Jumapili, Zelensky alielezea uvamizi huo wa Urusi kuwa unahusisha "mateso ya taifa zima".

    Alipoulizwa moja kwa moja ikiwa vitendo vya Urusi vilijumuisha mauaji ya halaiki, alisema: "Kwa hakika, haya ni mauaji ya kimbari.

    Kuondolewa kwa taifa zima na watu. Sisi ni raia wa Ukraine. Tuna zaidi ya mataifa 100. "

    Hii ni kuhusu uharibifu na kuangamizwa kwa mataifa haya yote.

    Sisi ni raia wa Ukraine na hatutaki kutishwa kwa sera ya Shirikisho la Urusi.

    "Hii ndiyo sababu tunashambuliwa na kuangamizwa, na hili inafanyika katika Ulaya ya Karne ya 21."

    Unaweza pia kusoma

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Vita vya Ukraine:Kwa nini Urusi inajaribu kuzingira mashariki ya Ukraine
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
    • SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
  3. Mkuu wa Nato anataja vifo vya raia wa Bucha kuwa ni ukatili

    Katibu Mkuu wa Nato Jens Stoltenberg amese,a vifo vya raia katika mji wa Bucha "havikubaliki".

    Akizungumza na CNN, alisema vifo hivyo ni "ukatili dhidi ya raia ambao hatujaona Ulaya kwa miongo kadhaa" na kwamba "hii inasisitiza umuhimu wa vita hivi kukomeshwa".

    Stoltenberg anaungana na viongozi wengine dunia kulaani matukio katika maeneo yaliyoachwa nyuma na majeshi ya Urusi waliondoka miji kadhaa inayozunguka Kyiv.

    Kufuatia kujiondoa kwa Urusi kutoka Bucha, kumekuwa na ripoti nyingi za maiti zilizopatikana zimevaa nguo za kiraia.

    Unaweza pia kusoma

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Vita vya Ukraine:Kwa nini Urusi inajaribu kuzingira mashariki ya Ukraine
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
    • SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
  4. Wanajeshi wa Urusi wafariki baada ya wenyeji wa Kharkiv kuwapa mikate yenye sumu, Ukraine inasema

    Wanajeshi wawili wa Urusi walikufa na na wengine 28 kulazwa hospitali baada ya wenyeji katika mkoa wa Kharkiv nchini Ukraine kuwapa mikate iliyotiwa sumu - kulingana na Wizara ya Ulinzi ya Ukraine.

    Katika taarifa yake ya kijasusi, Ukraine liwaelezea raia hao kama "wapinga wavamizi kwa njia zote zinazopatikana" na kudai kuwa wanajeshi walioathiriwa walikuwa wanatoka Kitengo cha 3 cha Rifle cha Urusi.

    Wizara hiyo pia ilisema wanajeshi wengine 500 wa Urusi walilazwa hospitalini wakiwa na "sumu kali ya pombe isiyojulikana asili yake".

    BBC haijaweza kudhibitisha madai hayo kikamilifu.

    Unaweza pia kusoma

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Vita vya Ukraine:Kwa nini Urusi inajaribu kuzingira mashariki ya Ukraine
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
    • SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
  5. Watu sita wauawa katikati mwa mji mkuu wa jimbo la California

    Takriban watu sita wameuawa na wengine 10 kujeruhiwa kwa kupigwa risasi katikati mtaa wa Sacramento, polisi katika mji mkuu wa jimbo la California wanasema.

    Watu walikimbia barabarani baada ya milio ya risasi kusikika katika eneo lililojaa mikahawa na baa.

    Maafisa wa polisi walifunga eneo kati ya barabara ya 9 na 13 baada ya ufyatuaji risasi asubuhi ya Jumapili.

    Wamewataka wananchi kujitokeza na kutoa taarifa zozote zitakazosaidia kuwabaini watuhumiwa.

    Mkuu wa polisi wa Sacramento Katherine Lester aliwaambia waandishi wa habari kwamba maafisa karibu na umati mkubwa sana katika eneo hilo walikuwa wamesikia milio ya risasi mwendo wa 02:00 (09:00 GMT).

    "Hii ni hali ya kusikitisha sana," alisema.

  6. Vita vya Ukraine: Matukio ya hivi punde kwa ufupi

    Ikiwa ndio mwanzo unajiunga nasi - haya ndiyo matukio ya hivi punde kwa mukhtasari.

    Mauaji ya Bucha

    • Wakati majeshi ya Urusi yakirudi nyuma, Ukraine inadai kuchukua tena udhibiti wa eneo la karibu na mji mkuu wa Kyiv, huku hofu ya kile kilichoachwa nyuma ikiibuka.
    • Tukio la uharibifu liliwakumba wanajeshi wa Ukraine baada ya kuuteka tena mji wa Bucha, mwandishi wa BBC Jeremy Bowen anaripoti.
    • ''Takriban maiti 20 ilikuwa imetapakaa barabarani wakati wanajeshi wa Ukraine walipoingia mjini humo.
    • Baadhi yao walikuwa wamefungwa mikono nyuma ya migongo yao," mwandishi wetu anasema.
    • Uingereza imeahidi kuunga mkono uchunguzi wa uhalifu wa kimataifa kuhusu uhalifu wowote wa kivita

    Odesa yashambuliwa

    • Moshi mweusi umefunika anga juu ya mji wa bandari wa Odesa, baada ya mashambulizi ya anga ya Urusi.
    • Urusi inadai ililenga vituo vya mafuta katika eneo ambalo Ukraine ilikuwa ikitumia kuwasafirisha wanajeshi wake.
    • Afisa wa Ukraine alisema makombora yamelipua "miundombinu muhimu" na hakukuwa na majeruhi.
  7. Mfungwa wa Guantanamo arejeshwa Algeria baada ya takriban miaka 20

    Mfungwa wa Guantanamo Bay Sufiyan Barhoumi amerejeshwa nchini Algeria, maafisa wa Marekani wanasema, baada ya kukaa karibu miaka 20 katika kituo hicho.

    Alikamatwa katika nyumba moja nchini Pakistan akiwa na mwanachama mkuu wa al-Qaeda mwaka 2002, na kushutumiwa kushiriki katika mpango wa kuishambulia Marekani kwa mabomu.

    Lakini Wizara ya Ulinzi ya Marekani ilisema kuzuiliwa kwake hakukuzingatiwa tena kuwa muhimu.

    Ilisema Algeria imetoa hakikisho kwamba atatendewa ubinadamu.

    Katika taarifa, idara hiyo iliongeza kuwa mamlaka ya Marekani ilipendekeza kwamba Bw Barhoumi anaweza kurejeshwa katika nchi yake ya asili "chini ya hakikisho la kiusalama".

    Idara hiyo haikutoa maelezo zaidi kuhusu Bw Barhoumi.

    Algeria pia haijatoa hadharani tamko lolote kuhusiana na suala hilo.

  8. Vita vya Ukraine: Barabara ya Bucha imejaa mizinga na maiti zilizoteketea

    Vikosi vya Urusi huenda vinaacha ushahidi wa uhalifu wa kivita wakati vinaporejea kutoka maeneo karibu na Kyiv, mshauri wa rais wa Ukraine Volodmyr Zelensky amesema katika mahojiano na BBC.

    Sergey Nikiforov alielezea picha zinazotoka katika miji ya Bucha, Hostomel, na Irpin - karibu na Kyiv - kuwa ya "kuvunja moyo".

    Anasema vikosi vya Ukraine vimekuta makaburi ya halaiki, watu wakiwa wamefungwa mikono na miguu, na miili ya raia waliouawa kwa risasi nyuma ya vichwa vyao.

    "Ni vigumu sana kuelewa kwa nini hii inafanyika," alisema. "Ni ukatili mtupu. Hakuna ulazima wa kijeshi kufanya haya yote."

    Mwandishi wa BBC Jeremy Bowen amekuwa chini mjini Bucha, mitaa ambayo anaripoti kuwa imejaa maiti na mizinga iliyoteketea.

  9. Katika picha: Moshi ukifuka kutoka kwa vituo vya mafuta vya Odesa

    Picha kutoka Odesa zinaonyesha athari za mashambulizi kadhaa ya anga yaliyofanywa na Urusi dhdi ya mji huo wa bandari mapema leo asubuhi.

    Urusi inasema ililenga vituo vya mafuta katika eneo ambalo Ukraine ilikuwa ikitumia kuwasafirisha wanajeshi wake.

    Maafisa wa Ukraine wanasema hakuna majeruhi walioripotiwa kufikia sasa.

  10. Urusi yadai kuwa shambulizi la Odesa lililenga miundombinu

    Wizara ya ulinzi ya Urusi sasa inasema kwamba vikosi vyake viliharibu kinu cha kusafisha mafuta na hifadhi tatu za mafuta zenye usahihi wa juu wa makombora ya baharini na angani katika eneo la Odesa, shirika la habari la Interfax linaripoti.

    Ilisema kuwa vifaa hivyo vilikuwa vinatumiwa na Ukraine kuwasafirisha wanajeshi wake karibu na mji wa Mykolaiv.

    Kama tulivyoripoti katika taarifa yetu ya awali, maafisa wa Ukraine wanasema kuwa hakuna majeruhi walioripotiwa kutokana na shambulio hilo la asubuhi ya leo.

  11. Vita vya Ukraine: Je, Odesa imejiandaa vipi?

    Macho yote yamegeukia mji wa bandari wa kusini, ambapo milipuko ilisikika Jumapili asubuhi.

    Odesa imekuwa ikijiandaa kwa mashambulio kwa wiki kadhaa sasa, huku meli za kivita za Urusi zikizunguka pwani ya Bahari Nyeusi.

    Wakazi waliondoka, na mikahawa na tramu zikiwa tupu huku mitaa ikifunikwa na mitego ya tanki na makaburi maarufu yaliyozungukwa na mifuko ya mchanga ya kinga.

    Lakini jiji hilo lilikuwa limeanza kufunguliwa tena kwa tahadhari, licha ya ving'ora vya mashambulizi ya anga, doria za vitongoji na hofu ya shambulio la Urusi, mwandishi wa BBC Andrew Harding aliripoti wiki iliyopita.

    Kujiamini huko kwa kiasi fulani kulitokana na hatua ya kusonga mbele kwa Urusi kwenye pwani ya Bahari Nyeusi.

    Lakini hatimaye Urusi ilifanya mashambulizi dhidi ya mji huo wa kimkakati mapema Jumapili.

    Katika taarifa ilyochapishwa katik mtandao wa Telegram, afisa wa kijeshi wa Ukraine Vladislav Nazarov anasema kuwa hadi sasa hakuna majeruhi walioripotiwa kufuatia shambulio hilo.

    Nazarov anaongeza kuwa miundombinu muhimu iliharibiwa lakini hakutoa maelezo zaidi juu ya lengo.

    Unaweza pia kusoma

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Vita vya Ukraine:Kwa nini Urusi inajaribu kuzingira mashariki ya Ukraine
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
    • SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
  12. Milipuko mikubwa yasikika katika bandari ya Odesa ya Ukraine - ripoti

    Milipuko mikuwabwa imeripotiwa katika bandari ya Odesa kusini mwa Ukraine Usiku wa kuamkia leo Jumapili.

    Moshi ilionekana ukitanda mji huo wa kimkakati katika pwani ya Bahari Nyeusi Jumapili asubuhi, mashuhuda aliambia shirkala la habari la Reuters.

    Anton Herashchenko, mshauri wa waziri wa mambo ya ndani wa Ukraine, amethibitisha kwenye chaneli yake ya Telegram kwamba "Odesa alishambuliwa kutoka angani" kwa makombora, ambayo baadhi anasema "yalidunguliwa na ulinzi wa anga".

    Awali mwandishi wa Washington Post Isabelle Khurshudyan,ambaye yupo mjini Odesa, aliandika ujumbe katika mtandao wa Twitter: "Tunasikia milipuko mikubwa viungani mwa Odessa muda huu. Dirisha la chumba cha hoteli ninayoishi imetingisihka. Sian uhakiki ni nini hasa kilichotokea ."

    Serhiy Bratchuk, msemaji wa utawala wa kijeshi wa eneo la Odesa, aliwataka wakaazi wa jiji hilo kusalia kwenye makazi ya kujikinga dhidi ya mabomu.

    "Tutashinda maadui wataenda kuzimu!" aliandika katika chapisho la Facebook.

    Unaweza pia kusoma

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Vita vya Ukraine:Kwa nini Urusi inajaribu kuzingira mashariki ya Ukraine
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
    • SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
  13. Uwezekano wa mazungumzo kati ya Putin na Zelensky upo- Mpatanisi wa Ukraine

    Huku ushahidi mpya ukiibuka wa mauaji ya raia katika eneo la Kyiv na kuendelea kwa mapigano kwingineko nchini Ukrainia, je kuna matumaini ya kuwepo kwa makubaliano ya amani?

    Mpatanishi mkuu wa Ukraine alisema Jumamosi kwamba mazungumzo hayo yameendelea vya matumanini kwamba Rais Volodymyr Zelensky anaweza kuzungumza na mwenzake wa Urusi, Vladimir Putin.

    Davyd Arakhamia aliripoti kuwa hatua zimepigwa katika mazungumzo kati ya wajumbe kwa njia ya video siku ya Ijumaa, akisema Urusi imekubali mapendekezo ya Ukraine kuhusu masuala yote isipokuwa Crimea, eneo ambalo Urusi ilinyakua kutoka Ukraine mwaka 2014.

    Nyaraka za rasimu katika hatua hiyo, zilisema, kwamba marais hao wawili wangeweza kufanya mashauriano moja kwa moja, lakini kazi ilikuwa ikiendelea katika masuala kadhaa mbali na waraka wenyewe.

    Urusi haijatoa tamko lolote kuhusiana na suala hili. Mpatanishi wake mkuu, Vladimir Medinsky, alisema baada ya mazungumzo ya Ijumaa kwamba misimamo ya Urusi kuhusu Crimea na Donbas haijabadilika.

    Urusi inasisitiza kwamba Ukraine itambue Crimea kama Urusi, na kutambua uhuru wa Donbas, ambapo waasi wanaoungwa mkono na Urusi wanadhibiti sehemu kubwa ya eneo.

    Unaweza pia kusoma

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Vita vya Ukraine:Kwa nini Urusi inajaribu kuzingira mashariki ya Ukraine
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
    • SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
  14. Kwa nini Urusi inajaribu kuzingira mashariki ya Ukraine

    Urusi imeelekeza zaidi nguvu zake za kivita kuelekea mashariki mwa Ukraine, baada ya msururu wa vikwazo hasa karibu na mji mkuu wa Kyiv.

    Msukumo huu katika eneo linalojulikana kama Donbas unaweza kuashiria mgogoro wa muda mrefu zaidi, inasema Marekani.Soma hapa

  15. Je, huu ni mwanzo wa enzi mpya ya usalama barani Ulaya?

    Ndi na La

    Nato imepata nguvu tena, Muungano wa Ulaya, EU imeinuliwa na kuwa mshirika anayeaminika wa kijiografia, na mwanachama wake tajiri na mwenye nguvu zaidi, Ujerumani, ghafla aliaga hisia za Vita vya Pili vya Dunia na kutangaza uwekezaji mkubwa katika jeshi lake.

    Lakini katika mazungumzo yote ya Brussels ya kujenga EU "uhuru wa kimkakati", inaonekana na Washington wakati inakabiliwa na vitisho vya Urusi.

    Mipango ya ulinzi ya EU, iliyoundwa ili kukamilisha - au kuchukua nafasi - Nato, sio jambo jipya. Na hadi sasa, hawajawahi kufanya kazi.

    Nchi zote zinakubali kwamba inaleta maana kukusanya rasilimali na ujuzi. Hata hivyo, hakuna taifa linalotaka kutanguliza.

    Lakini EU ina raison d'être yake nyuma. Iliyoundwa awali kama mradi wa amani, maono yake yalitetereka katika siku za hivi karibuni.

    Unaweza pia kusoma

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Vita vya Ukraine:Kwa nini Urusi inajaribu kuzingira mashariki ya Ukraine
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
    • SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
  16. Urusi inataka kunyakua mashariki na kusini mwa Ukraine - Rais Zelensky

    Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameonya kwamba Urusi inataka kuteka maeneo ya mashariki na kusini mwa Ukraine,

    Katika hotuba ya video usiku wa Jumamosi, alisema: "Je, lengo la wanajeshi wa Urusi ni nini? Wanataka kunyakua Donbas [mashariki] na kusini mwa Ukraine.

    "Lengo letu ni nini? Tujilinde, tulinde uhuru wetu, ardhi yetu na watu wetu."Zelensky pia alipongeza vikosi vya Ukraine vinavyolinda bandari ya kusini ya Mariupol iliyozingirwa, ambayo imeaharibiwa kutokana na majuma kadhaa ya mashambulizi makombora ya Urusi.

    Upinzani wa Ukraine huko Mariupol na miji mingine ya Ukrane uliruhusu Kyiv "kupata wakati kujiimarisha", na kusaidia kudhoofisha uwezo wa kijeshi wa Urusi, rais alisema.

    Mapema wiki hii, Urusi ilitangaza kwamba "itapunguza kwa kiasi kikubwa" operesheni za mapigano karibu na mji mkuu wa Kyiv na mji wa kaskazini wa Chernihiv, na badala yake kuzingatia maeneo ya mashariki mwa Ukraine.

    Unaweza pia kusoma

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Vita vya Ukraine:Kwa nini Urusi inajaribu kuzingira mashariki ya Ukraine
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
    • SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
  17. Hujambo na karibu kwa matangazo ya moja kwa moja leo Jumapili 03.04.2022.