Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ukraine haiko tayari kusalimisha eneo lake lolote kwa Urusi- mshauri wa Zelensky
Akizungumza katika mkesha wa mazungumzo zaidi kati ya Urusi na Ukraine, Alexander Rodnyansky alisema "sasa shinikizo ni kwa Urusi".
Moja kwa moja
Urusi inapanga kuwazuia watu kutoka nchi "zisizo rafiki"kuingia nchini humo- Lavrov
Moscow inaandaa hatua za kuzuia kuingia nchini Urusi kwa raia wa nchi "zisizo rafiki", Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema.
"Rasimu ya amri ya rais inaandaliwa kuhusu hatua za visa ili kulipiza kisasi katika kukabiliana na vitendo visivyo vya kirafiki vya mataifa kadhaa ya kigeni," alisema katika hotuba ya televisheni.
Shirika la habari la serikali Tass lilimnukuu akisema hatua hizo "zitajibu hatua zisizo za kirafiki za Marekani na washirika wake", ikiwa ni pamoja na "vikwazo visivyo halali" na "maamuzi ambayo yanakiuka haki za raia wa Urusi na vyombo vya kisheria".
Haijabainishwa hatua hizo zitatumika kwa nchi zipi, lakini serikali hapo awali iliidhinisha orodha ya nchi na maeneo "yanayofanya vitendo visivyo vya kirafiki dhidi ya Urusi, kampuni zake na raia".
Orodha hiyo inajumuisha Marekani na Kanada, mataifa ya Umoja wa Ulaya, Uingereza, Ukraine, Uswizi, Norway, Japan, Korea Kusini, Australia, New Zealand, Singapore na nyingine kadhaa.
Ukraine imechukua tena udhibiti wa Irpin, asema meya
Meya wa Irpin, mji ulioko kaskazini-magharibi mwa Kyiv, alisema vikosi vya Ukraine vimetwaa udhibiti kamili wa mji huo siku ya Jumatatu.
Mji huo, ambao upo kilomita 20 tu (maili 12) nje ya mji mkuu, umeshuhudia mapigano muhimu zaidi kwa mustakabali wa Kyiv.
"Tuna habari njema leo - Irpin amekombolewa," Meya Oleksandr Markushyn alisema katika chapisho la video kwenye mtandao wa kijamii.
"Tunaelewa kuwa kutakuwa na mashambulizi zaidi katika mji wetu na tutaulinda kwa ujasiri," aliongeza.
Habari hii haikuweza kuthibitishwa mara moja na BBC.
Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Madereva 16 wa bodaboda waachiwa huru baada ya kuhusishwa na video ya kudhalilishwa kwa mwanadiplomasia
Mahakama nchini Kenya imewaachilia huru waendesha bodaboda kumi na sita waliokamatwa kufuatia shambulio dhidi ya mwanadiplomasia wa kike, mapema mwezi huu katika mji mkuu wa Nairobi.
Hii ni baada ya waendesha mashtaka kukosa kutoa ushahidi wowote dhidi yao.
Lakini mwanaume anayeaminika kuwa ndiye aliyepanga kisa hicho kilichozua hasira nchini Kenya si miongoni mwa walioachiliwa na atafunguliwa mashtaka Jumatatu.
Video hiyo inayowaonesha wanaume wakimpapasa mwanamke huyo huku akipiga kelele kuomba msaada kutoka ndani ya gari, ilisambaa mitandaoni nchini Kenya na kupelekea kukamatwa kwa makumi ya waendesha pikipiki kadhaa jijini Nairobi. Lakini baada ya karibu wiki mbili kizuizini, waendesha mashtaka walisema hawakuwa na ushahidi wa kutosha kuwahusisha washukiwa kumi na sita na kesi ya unyanyasaji wa kijinsia.
Mshukiwa mkuu wa shambulio hilo Zachariah Nyaore Obadiah, bado yuko kizuizini na atafunguliwa mashtaka Jumatatu. Alikamatwa na mamlaka katika mpaka wa Kenya na Tanzania alipokuwa akijaribu kutoroka.Msako mkubwa ulifanyika kufuatia tukio hilo dhidi ya madereva wa bodaboda.
- Boda-Boda: Tishio la kudumu la teksi za pikipiki,boda boda nchini Kenya
- Je neno Boda Boda limetokea wapi Afrika?
Ukraine haiko tayari kusalimisha eneo lake lolote kwa Urusi- mshauri wa Zelensky
Mshauri mkuu wa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameambia kipindi cha BBC Radio 4's World at One kwamba Ukraine "haiko tayari kuacha eneo lolote".
Akizungumza katika mkesha wa mazungumzo zaidi kati ya Urusi na Ukraine, Alexander Rodnyansky alisema "sasa shinikizo ni kwa Urusi".
"Ni wazi, hawawezi kuendeleza vita hivi kwa miaka mingi na ari yao iko chini sana hata hawawezi kuendelea kuviopa vikosi vyao vifaa kuendelea na mapigano," alisema.
Bw Rodnyansky, ambaye pia ni profesa msaidizi wa uchumi katika Chuo Kikuu cha Cambridge, alisema Ukraine haitasilimisha "uadilifu wa kieneo".
Alipendekeza toleo "halisi zaidi" la "mkataba wa Budapest" - ambalo liliipa Ukraine hakikisho la usalama - lingekuwa muhimu kufikia amani.
"Mkataba wa Budapest ulipaswa kuhakikisha usalama wetu kwa malipo ya kuacha silaha za nyuklia katika miaka ya 90.
"Inabidi iwe kitu kama hicho ambapo hatua zingebainishwa, ni nchi gani hasa zingechukua hatua kwa njia gani ikiwa usalama wako unatishiwa."
Lakini alionya kwamba uwezekano wa kuhusika kwa nchi za Nato katika mapatano kama hayo itakuwa "suala tete".
"Ndio maana mazungumzo sio rahisi, kwa sababu haungependa kuanzisha Kifungu cha 5, kimsingi, kuvuta Nato yote kwenye mzozo na Urusi.
"Hiyo ndiyo [ambayo] nchi za Nato hazitaki kutokea na ndiyo maana mazungumzo bado yanaendelea."
Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Kenya na Jersey zatia saini makubaliano ya kurejesha mamilioni yaliyopotea
Serikali za Kenya na Jersey zimetia saini mkataba wa kihistoria ambao utashuhudia mamilioni ya dola za fedha za umma zinazodaiwa kuibwa na matajiri wawili wa Kenya kurudishwa nchini kununua vifaa vya kuokoa maisha vya katika pambano dhidi ya janga la Covid 19 .
Makubaliano hayo na Jersey, kisiwa kinachojitawala katikaEnglish Channel yametajwa kuwa "ushindi kwa watu wa Kenya" na Kamishna Mkuu wake nchini Uingereza, Manoah Esipisu.
Alitia saini mkataba huo huko London na Mwanasheria Mkuu wa Jersey Mark Temple.
Mwanamuziki wa Nigeria adhulumiwa kingono jukwaani
Video imeibuka ya unyanyasaji wa kingono wa mwimbaji wa Afrobeats wa Nigeria akiwa jukwaani.
Msanii Ruger mwenye umri wa miaka 22, ambaye jina lake halisi ni Michael Adebayo, anaonekana akicheza wimbo wake wa kwanza, Dior, wakati shabiki anafika kutoka kwa umati na kumshika sehemu zake za siri.
Huku akionekana kushtuka, anasimamisha onyesho lake kwa sekunde chache kisha akapanda jukwaani.
Video hiyo, ambayo sasa inavuma, imezua gumzo mtandaoni kuhusu wahasiriwa wa kiume wa unyanyasaji wa kijinsia.
Ruger bado hajazungumza lolote kuhusu tukio hilo linalodaiwa kufanywa na shabiki mmoja wa kike siku ya Jumapili.
Video tofauti kwenye mitandao ya kijamii inaonekana kumuonyesha mwanamke yuleyule wakati mwingine wa onyesho jukwaani akicheza dansi
Ruger anamgonga kwa upole begani anapocheza, lakini hajishughulishi naye zaidi kwenye klipu hiyo.
Tukio hilo limezua hasira na mshtuko mtandaoni.
"Nilitazama video ya unyanyasaji wa kijinsia ya Ruger na mimi pia tunahisi kuwa na kiwewe. Inatisha sana, mtu huyo alikuwa akifanya ufundi wake na mtu akamwondoa furaha na amani. Hebu fikiria wanaume wengine ambao wanapitia hali mbaya kila siku lakini huwezi kusema kwa sababu ulimwengu utakudhihaki," mtu mmoja aliandika kwenye Twitter.
"Dunia ina dhuluma dhidi ya wanaume linapokuja suala la mambo ya ngono tunadhani siku zote yanaanzishwa na wanaume na wasingeweza kudhulumiwa. Wanaume wengi walipoteza utu wao kwa wanawake wakubwa lakini wanaendelea kuishi nao kwa sababu hakuna anayewasikiliza. ," mwingine alisema.
Akitajwa na vyombo vya habari vya nchini kuwa nyota anayechipukia, baadhi ya nyimbo bora za Ruger ni pamoja na Bounce na Dior, ambao ulikuwa wimbo namba moja kwenye Apple Music nchini Nigeria, Uganda, Kenya na Gambia mwanzoni mwa mwaka. .
Vita vya Urusi vimeigharimu Ukraine $564.9bn kufikia sasa - Ukraine
Vita vya Urusi dhidi ya Ukraine vimeigharimu Ukraine $564.9bn (£429.3bn) kufikia sasa katika uharibifu wa miundombinu, kupoteza ukuaji wa uchumi na mambo mengine, kulingana na waziri wa uchumi wa Ukraine.
Mapigano hayo yameharibu kilomita 8,000 (maili 4,970) za barabara na mita za mraba milioni 10 za makazi, Yulia Svyrydenko alisema katika chapisho la mtandao wa kijamii.
Urusi inaendelea kusema kuwa inaendesha "operesheni maalum ya kijeshi" nchini Ukraine kwa lengo la kuipokonya silaha nchi hiyo.
Ukraine na washirika wake wa Magharibi wamesema msimamo huo ni kisingizio cha uvamizi usio na msingi.
Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Walioshinda tuzo za Oscars 2022
Tuzo za Oscar za mwaka huu zimetolewa huko Los Angeles, kuwapa tuzo wasanii bora zaidi wa tasnia ya filamu katoka miezi 12 iliyopita.
Hii hapa orodha ya washindi wa Tuzo za 94 za Academy.
- Filamu iliyoshinda picha bora: Coda
- Muigizaji bora wa kike • Jessica Chastain - The Eyes of Tammy Faye
- Muigizaji bora wa kiume •Will Smith - King Richard
- Muongozaji bora •Jane Campion - The Power of the Dog
- Uigizaji bora wa asili • Belfast - Sir Kenneth Branagh
- Filamu iliyogeuzwa kutoka kwa sanaa ya kwanza • Coda - Sian Heder
- Simulizi bora za katuni • Encanto
- Riwaya bora ya simulizi • Summer of Soul
- Simulizi bora ya kimataifa • Drive My Car (Japan)
- Wimbo bora: No Time to Die - No Time to Die
- Mpiga picha za video: Dune - Greig Fraser
- Uhariri bora wa filamu • Dune - Joe Walker
- Ubunifu bora wa mavazi • Cruella - Jenny Beavan
- Sauti bora • Dune - Mac Ruth, Mark Mangini, Theo Green, Doug Hemphill na Ron Bartlett
- Mfumo bora wa uzalishaji filamu • Dune - Patrice Vermette na Zsuzsanna Sipos
- Filamu fupi bora ya katuni : The Windshield Wiper
- Makala bora fupi : The Queen of Basketball
Soma zaidi
- Tuzo za Oscars 2022: Will Smith aomba radhi kwa kumzaba kibao mchekeshaji Rock jukwaani
- Oscars 2022: Zifahamu filamu bora 16 zilizoingia kwenye mashindano ya tuzo za Oscars
Mamia ya watu wamekimbilia Uganda baada ya mashambulizi ya waasi wa DR Congo
Mamia ya raia wa Kongo wamekimbilia nchini Uganda kufuatia mashambulizi ya waasi dhidi ya makazi yao.
Maafisa katika jimbo la Kivu Kaskazini walisema wapiganaji wa M23 walivamia vijiji vya Tchanzu na Runyoni.
Kambi ya jeshi la Kongo pia iliripotiwa kushambuliwa.
Walioshuhudia wanasema kumekuwa na mapigano makali kati ya waasi na wanajeshi wa serikali.
Kundi la M23, ambalo lina wanachama wengi kutoka kabila la Watutsi, lilikuwa jeshi kuu la mapigano mashariki mwa Kongo, na kuuteka mji mkuu wa mkoa wa Goma mnamo 2012.
Baadaye lilifanya mazungumzo na serikali ya Kongo lakini linasema matakwa yake hayajawahi kutekelezwa.
Hapo awali Umoja wa Mataifa ulishutumu Uganda na Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23.
Matokeo ya KCPE: Magata Bruce aibuka wa kwanza katika mtihani wa kitaifa wa shule za msingi Kenya
Matokeo ya mtihani wa kitaifa wa shule za msingi nchini Kenya yametolewa .
Magata Bruce Mackenzie kutoka Gilgil Academy ndiye mtahiniwa bora wa KCPE mwaka huu akiwa na alama 428 kati ya alama 500.
Alifuatwa na Momanyi Ashley wa Shule ya Makini aliyepata 427, huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Muteti Shabtell wa Shule ya Kimataifa ya Kitengela aliyepata alama 426.
Alipokuwa akitoa matokeo hayo, Waziri wa Elimu Prof George Magoha alisema kuwa mtihani wa KCPE wa 2021 haukuvuja zaidi kwa sababu ya udhibiti mkali uliowekwa.
“Jumla ya watahiniwa 315,275 walipata kati ya 300-399, huku 578,197 wakipata kati ya alama 200 hadi 299,” alisema.
Waziri pia alifichua kuwa tathmini ya kwanza ya kitaifa ya mtaala mpya wa elimu - CBC kwa Darasa la 6 iko tayari na itafanyika mnamo Novemba.
"Watahiniwa watapata alama 40 kutokana na tathmini na alama nyingine 60 zitatokana na upimaji endelevu kutoka kwa darasa la 3, 4 na 5," Magoha alisema.
Watahiniwa 1,214, 031 walifanya mtihani wa KCPE 2021.
Ukraine iko tayari kujadili pendekezo la kutoegemea upande wowote – Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anasema kuwa kama sehemu ya makubaliano ya amani na Urusi, Ukraine iko tayari kujadili kupitisha hoja ya kutoegemea upande wowote, lakini itabidi ihakikishwe na pande tatu na kupigiwa kura ya maoni, Reuters inaripoti.
"Dhamana ya usalama na kutoegemea upande wowote, kutojihami kwa nyukilia kwa nchi yetu. Tuko tayari kuishughulikia. Hili ndilo jambo muhimu zaidi," anasema kwenye simu ya video.
Kiongozi huyo wa Ukraine - akizungumza kwa Kirusi - anaongeza uvamizi wa Urusi umesababisha uharibifu wa miji inayozungumza Kirusi nchini Ukraine.
Matumizi ya lugha ya Kirusi nchini Ukraine ni jambo ambalo limejadiliwa wakati wa mazungumzo ya amani kati ya Ukraine na Urusi, Reuters inaripoti Zelensky akisema. Lakini anaongeza Ukraine imekataa kujadili matakwa mengine ya Urusi, kama vile kuondolewa kijeshi kwa Ukraine.
Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Rwanda yataka fedha zaidi ili vikosi vyake viendelee kusalia Msumbiji
Rwanda inataka fedha zaidi ili kuhakikisha vikosi vyake katika mkoa wa Cabo Delgado Kaskazini mwa Msumbiji vinavyombana na wanamgambo wa Kiislamu, viendelee kusalia huko.
Vikosi vya wanajeshi 1,000 wa Rwanda vilipelekwa katika eneo hilo mwaka jana na tangu wakati huo kimeteka vijiji na miji mingi kutoka kwa wanamgambo hao.
Balozi wa Rwanda nchini Msumbiji amesema wameuomba Umoja wa Ulaya msaada wa kifedha kwa wanajeshi hao ili kuimarisha hali ya usalama katika eneo hilo.
"Tumeimarisha maeneo ya wilaya kama ya Palma na Mocímboa da Praia. Tunasubiri serikali [Msumbiji] ifanye uamuzi kuona kama watu wanaweza kurejea," alisema Nikobisanzwe.
Hata hivyo alisema hakuna muda wa mwisho wa kuwepo kwa wanajeshi wa Rwanda nchini humo.
Mshangao wa Lupita juu ya kofi la Will Smith kwa Rock wawa gumzo mtandaoni
Video ya mshangao ikimuonyesha msanii wa filamu nchini Kenya Lupita Nyong'o juu ya hatua ya Will Smith kumzaba kofi mchekeshaji Chris Rock katika sherehe za tuzo za Oscars Jumapili usiku imetapakaa katika mitandao ya kijamii.
Smith alimzaba kofi Rock baada ya mzaha wake kuhusu mke wa mwigizaji Jada Pinkett Smith, akisema "Jada, anasubiri kwa hamu GI Jane 2."
Jada aliwahi kuzungumzia huko nyuma kuhusu matatizo yake ya nywele.
Alisema: "Nimekuwa na matatizo ya kupoteza nywele. Wakati inaanza (hali hii) ilikuwa ya kutisha."
Lupita kama ilivyo kwa wengine walipigwa na butwaa, lakini kwa namna yake, namna alivyoshangaa kukadakwa na kamera.
Idara ya Polisi ya Los Angeles baadaye ilieleza kwamba Rock "alikataa kuwasilisha ripoti ya polisi" kufuatia tukio hilo.
Chuo cha Sanaa na Sayansi, ambacho kinaandaa tuzo za Oscars, kilituma ujumbe twitter kwamba "haingu mkono vurugu za aina yoyote".
Namna watoto 'njiti' wanavyopigania maisha yao kwenye miji iliyozingirwa na mabomu Ukraine
Katika mji uliozingirwa wa Kharkiv, Polina anapigania maisha yake.
Ana umri wa siku tano tu, na alikuwa na uzito wa chini ya pauni moja na nusu [zaidi ya gramu 600] wakati alipozaliwa.
Watoto waliozaliwa kabla ya wakati kama Polina wameshambuliwa tangu vita vilipoanza, kwa mujibu wa Iryna Kondratova, mkurugenzi katika kliniki ambako Polina alizaliwa.
"Maambukizi, ukosefu wa msaada wa matibabu, lishe mbaya: vita vinasababisha hatari ya kuzaliwa mapema," alisema.
Kwa sasa watoto ‘njiti’ wamefikia asilimia 50% ya watoto wote wanaozaliwa katika kliniki yake.
Sio hospitali zote nchini Ukraine zinaripoti ongezeko la watoto njiti, lakini katika hospitali ya uzazi huko Lviv, ambayo imeshuhudia ongezeko kubwa hivi karibuni kwa kina mama wanaojifungua mapema kwenye maeneo ya migogoro. Kujifungua mapema kumeongezeka mara mbili, kutoka mtoto mmoja kati ya kumi, hadi mtoto mmoja kati ya watano.
Hospitali imeanza kujenga hifadhi maalum ya chini ya ardhi ili kuwalinda watoto hao katika chumba maalumu cha wagonjwa mahututi, dhidi ya mashambulizi ya anga.
Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Njaa yawakutanisha wanafunzi wa vyuo vikuu Afrika Mashariki huko Zanzibar
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Aboubakar Famau
- Nafasi, BBC News, Zanzibar
Zaidi ya wanafunzi 50 kutoka vyuo vikuu kadhaa vya Afrika Mashariki wanakutana mjini Unguja, Zanzibar nchini Tanzania kwenye kongamano maalumu la siku nne.
Shughuli hiyo ina lengo la kuwajengea uwezo wanafunzi wa vyuo vikuu kutatua matatizo halisia yanayoikabili jamii ya kila siku kama vile usalama wa chakula, njaa na utapiamlo.
Kilele cha kongamano hili kinatarajiwa kuibua washindi watatu ambao watakuwa wamefanikiwa kuja na suluhisho ya moja wapo ya changamoto hizo.
Mwaka huu, changamoto kubwa wanayotakiwa kujadili na kuipatia suluhisho ni tatizo la utapiamlo kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.
Mradi huu uko chini ya udhamini wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Denmak-Danida na umeandaliwa na Chuo Kikuu cha Serikali ya Zanzibar-SUZA.
Hii ni mara ya kwanza kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Afrika Mashariki kukutanishwa na kushindanishwa.
Patricia Nachibule, kutoka Chuo Kikuu cha Gulu nchini Uganda, anasema yeye amefurahi kuwa sehemu ya jukwaa hili kwa sababu itampa fursa ya kujifunza ambavyo hakuwa na uelewa navyo, hasa katika masuala ya utatuzi wa changamoto.
Nae Jeniffer Tairo, kutoka Chuo Kikuu cha SUA, anasema kuna haja kubwa ya wanafunzi wa vyuo vikuu kupewa fursa na mafunzo ya jinsi ya kutatua changamoto za jamii, kwa sababu wao ni sehemu muhimu ya jamii.
Tatizo la utapiamlo linaonekana kushamiri katika jamii nyingi za kiafrika licha ya sehemu kubwa kujishughulisha na kilimo.
Hivyo, nchini Tanzania, Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa-FAO kwa kushirikiana na serikali na wadau wengine, wameandaa mpango wa miaka mitano wenye lengo la kuoanisha shughuli za kilimo na lishe ili kukabiliana na utapiamlo.
Spika wa zamani Burkina Faso akamatwa
Vikosi vya usalama nchini Burkina Faso vimemkamata spika wa zamani wa nchi hiyo , siku chache baada ya kutoa wito wa kuachiwa mara moja kwa rais aliyeondolewa madarakani Roch Kaboré.
Alassane Bala Sakandé, ambaye pia ni kiongozi wa chama tawala cha zamani, alikamatwa na polisi nyumbani kwake mapema Jumapili asubuhi.
Aliachiwa bila ya kufunguliwa mashtaka jioni baada ya saa kadhaa za mahojiano katika mji mkuu Ouagadougou, kituo cha utangazaji cha Redio Omega kiliripoti.
"Ameshutumiwa kwa matamshi aliyoyatoa katika mkutano na waandishi wa habari wa chama chake, Movement for Progress uliofanyika Machi 24," shirika la habari la AFP awali liliwanukuu mawakili wake wakisema.
Bwana Sakandé alisema kuwa rais huyo wa zamani hakuwa kwenye kifungo cha kawaida cha nyumbani bali uko kizuizini kutokana na hali ngumu aliyodaiwa kukumbana nayo.
Rais huyo wa zamani aliondolewa madarakani mwezi Januari na amekuwa akizuiliwa chini ya kifungo cha nyumbani tangu wakati huo.
Jumuiya ya kikanda ya Afrika Magharibi Ecowas, ambayo imetishia kuiwekea Burkina Faso vikwazo zaidi, imetaka aachiliwe bila masharti.
Makazi ya makamu wa Rais Sudan Kusini, Machar yazingirwa na Jeshi
Vikosi vya serikali ya Sudan Kusini vimeripotiwa kuzingira makazi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Riek Machar katika mji mkuu Juba.
Haijulikani iwapo Bw Machar yuko katika nyumba hiyo ama la.
Hatua hiyo inajiri siku moja tu baada ya kiongozi huyo wa zamani wa waasi kuwataka viongozi wa kikanda na kimataifa kuingilia kati kumaliza mapigano mapya katika majimbo ya Unity na Upper Nile - ambayo yanachukuliwa kuwa ni ngome zake.
Kwa wiki kadhaa sasa, mapigano kati ya jeshi la Sudan Kusini na vikosi tiifu kwa Bw. Machar vimeripotiwa katika maeneo mbalimbali, na kutishia makubaliano tete ya amani kati yake na Rais Salva Kiir.
Serikali haijatoa tamko lolote kuhusu iwapo wanajeshi wake wamezingira majengo hayo.
Mkataba wa amani uliotiwa saini mwaka 2018 kumaliza karibu miaka sita ya umwagaji damu unaonekana uko nyuma ya utekelezaji wa masuala muhimu kama vile kuundwa kwa jeshi la umoja.
Haya ndio matukio ya hivi punde:
Zelensky anasisitiza juu ya uhuru: Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anasema vipaumbele vyake ni uhuru na uadilifu wa eneo katika duru inayofuata ya mazungumzo ya amani na Urusi.
Mazungumzo ya ana kwa ana yanatarajiwa kufanyika nchini Uturuki wiki hii.
Hapo awali alisema yuko tayari kujadili Ukraine katika hali ya kutoegemea upande wowote - jambo kuu la mzozo na Urusi.
Biden anakanusha wito wa mabadiliko ya utawala: “Hapana“ - ndivyo Rais wa Marekani Joe Biden alisema kwa waandishi wa habari alipoulizwa kama alikuwa akitoa wito wa mabadiliko ya utawala nchini Urusi.
Siku ya Jumamosi, katika hotuba yake katika mji mkuu wa Poland Warsaw, alisema Putin “hawezi kubaki madarakani”. Tangu wakati huo utawala wa Biden umekuwa ukipuuza matamshi ya nje, ukisema Biden alimaanisha Putin hapaswi kuwa na mamlaka juu ya majirani.
Ukraine yadai Urusi kuondoa baadhi ya wanajeshi: Urusi imepata hasara kubwa katika eneo la Kyiv na kulazimika kuondoa wanajeshi wake, Jenerali wa jeshi la Ukraine amesema.
Alisema vikundi viwili vya jeshi la Urusi vimeondolewa katika nchi jirani ya Belarus, ambayo ni mshirika wa Urusi.
Onyesho la tuzo za Oscar: Nyota wa Hollywood wameunga mkono Ukraine kwenye tuzo za Oscar.
Watu kadhaa mashuhuri walitoa heshima na kuka kimya kwa muda kuonyesha kuunga mkono watu wa Ukraine.
Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Wanafunzi kuanza masomo leo huko Kyiv licha ya vita kuendelea
Wanafunzi katika mji mkuu Kyiv wanatarajiwa kuanza masomo yao leo- kupitia njia ya mtandao.
Jumapili Meya wa Kyiv alitangaza masomo kuanza tena, akisema masomo hayo "yatatumia njia mbalimbali kulingana na hali ya sasa".
"Kazi muhimu leo ni kuhakikisha mji unaendelea kuwepo na kazi zinaendelea hata katika hali ngumu ya sasa ya sheria za kijeshi," alisema Vitali Klitschko katika chapisho lake la Telegram.
"Wanajaribu kututisha. Hii haiwezi kufanya kazi!" alisema.
Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa zaidi ya nusu ya watoto wa nchi hiyo wameikimbia nchi hiyo wakati wa vita.