Davido atimiza ahadi yake ya kutoa mamilioni ya pesa kwa yatima

Davido atimiza ahadi yake ya kutoa mamilioni ya pesa kwa yatima na kujulisha umma

Moja kwa moja

  1. Na hadi hapo tumefika mwisho wa matangazo haya ya moja kwa moja kwa leo.Tukutane kesho panapo majaaliwa

  2. Wajumbe wa amani wachukuliwa mateka DRC

    Mjumbe wa amani Thomas Lubanga alifungwa jela kwa uhalifu wa kivita

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Jaribio la kuwashawishi wanamgambo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuweka silaha chini limekamilika huku wajumbe watatu wa amani - wote waliokuwa wababe wa kivita - wakichukuliwa mateka.

    Rais Félix Tshisekedi alimtuma Thomas Lubanga, Germain Katanga na Floribert Ndjabu kujadiliana na wanamgambo wa Codeco ambao wameshutumiwa kwa ukatili katika miezi ya hivi karibuni.

    Lakini msemaji wa kundi hilo ameliambia shirika la habari la Ufaransa kwamba jeshi la Congo lilifyatua makombora wakati wa mkutano huo, na wajumbe hao wamekamatwa.

    Juhudi za kuwapata kwa njia ya simu zimeshindikana. Codeco inadai kuwakilisha maslahi ya kabila la Lendu katika mapigano ambayo yameliharibu eneo la mashariki mwa DRC kwa miaka mingi.

    Lubanga na Katanga walitumikia vifungo vya miaka 14 na 12 mtawalia baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kuwapata na hatia ya kufanya uhalifu wa kivita mashariki mwa DR Congo.

    Ndjabu alifungwa jela miaka 15 kwa mauaji ya walinda amani tisa wa Umoja wa Mataifa.

    • ADF: Lifahamu kundi la waasi kutoka Uganda linaloshirikiana na Islamic State
    • Kwanini hali ya usalama imeendelea kuwa tete nchini DRC?
  3. Habari za hivi punde, Urusi yamfukuza mwanadiplomasia wa Marekani kutoka Moscow – ripoti

    Urusi imemfukuza naibu balozi wa Marekani katika ubalozi wa Marekani mjini Moscow, kulingana na shirika la habari la serikali ya Urusi RIA.

    Haijabainika mara moja sababu ambayo Moscow imetoa ya kumfukuza mwanadiplomasia Bart Gorman. Marekani itajibu hatua hiyo, RIA inaripoti.

    • Mzozo wa Ukraine: Madai ya Urusi ya kuondoa vikosi vyake ni ya uwongo ,Marekani yasema
    • Mzozo wa Ukraine: 'Putin amenihakikishia hakutakuwa na mzozo' - Macron
  4. Jinsi ‘kikombe cha uji’ kinavyowafanya watoto kubakia shuleni

    Maelezo ya video, Francis Amonde: Kijana anayewavutia watoto kwenda shule kutumia ‘kikombe cha uji’’

    Francis Amonde kijana mwenye umri wa miaka 30 alianzishampango wa kujitolea wa“kikombe cha uji” unaotoa kiamsha kinywa na mlo wa mchana kwa watoto wa shule 5,295 katika shule tofauti nchini Kenya.

    Mpango huu umeleta matumaini kwa wavulana na wasichana wadogo ambao hawawezi kupata milo hiyo nyumbani.

    Idadi ya wanafunzi katika shule ya msingi ya Kawangware imeongezeka .

    Francis anaeleza ni kwanini alianzisha mpango huu na ni nini kilimchochea pamoja na changamoto anazopitia kupata pesa za kunua unga na sukari.

  5. Watu 13 wafa baada ya kuanguka kisimani wakiwa harusini India

    Polisi walisema waathiriwa wote ni wanawake na watoto

    Chanzo cha picha, ANI

    Takriban watu 13 wamefariki baada ya kutumbukia kisimani wakati wa sherehe ya harusi katika jimbo la kaskazini mwa India la Uttar Pradesh.

    Polisi walisema waathiriwa - wote, wanawake na watoto - walikuwa wameketi kwenye bamba la chuma lililofunika kisima hicho wakati kilipoporomoka chini kutokana na uzani wao.

    Watu wawili zaidi wamejeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea wilayani Kushinagar. Waziri Mkuu Narendra Modi alitaja vifo hivyo kuwa "vya kuhuzunisha ".

    Mkasa huo ulitokea Jumatano jioni wakati wa sherehe ya kitamaduni ya "haldi", ambapo jamaa hupaka uso wa bi harusi na bwana harusi kama alama ya ustawi.

    Bamba hilo lilipovunjika, wageni wengine walikimbia kuwaokoa na kuwapeleka katika hospitali iliyo karibu.

    Wakati watu 11 walitangazwa kupoteza maisha, wengine wawili walifariki baadaye wakati wa matibabu, polisi walisema.

    Waziri mkuu wa Uttar Pradesh Yogi Adityanath amewataka wakuu wa wilaya kusaidia familia za walioathirika, huku hakimu wa wilaya S Rajalingam akisema watalipwa fidia.

  6. Saudi Arabia: Wanawake 28,000 wawania nafasi 30 za kazi za udereva wa treni

    Kutokana na mabadiliko, ushiriki wa wanawake katika nguvu kazi umeongezeka karibu maradufu

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Kampuni ya reli inayowaajiri madereva 30 wa treni wanawake nchini Saudi Arabia inasema imepokea maombi 28,000.

    Waombaji waliofaulu wataendesha treni za mwendo kasi kati ya miji mitakatifu ya Makka na Madina baada ya mwaka wa mafunzo.

    Ni mara ya kwanza majukumu kama haya kutangazwa kwa wanawake nchini humo.

    Kwa miongo kadhaa, Saudi Arabia ilikuwa na mojawapo ya viwango vya chini zaidi vya ushiriki wa wafanyakazi wa kike duniani.

    Lakini katika miaka ya hivi karibuni serikali imefanya jitihada za kuongeza idadi ya wanawake kazini kama sehemu ya mpango wa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa kuleta mseto wa uchumi unaotegemea mafuta.

    Pia imesukuma mageuzi kadhaa ya kijamii, ikiwa ni pamoja na kukomesha marufuku ya wanawake kuendesha gari na kurahisisha sheria za usimamizi wa wanaume ili kuruhusu wanawake kusafiri kwa uhuru.

    Kutokana na mabadiliko hayo, ushiriki wa wanawake katika nguvu kazi umeongezeka karibu maradufu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita hadi 33%, na wanawake wengi zaidi kuliko wanaume waliingia kazini katika nusu ya kwanza ya mwaka jana.

    Hata hivyo, wanaume bado wanashikilia nafasi nyingi za kazi, hasa katika sekta ya umma, kulingana na utafiti uliochapishwa mwaka jana na taasisi ya Marekani,Brookings.

    Msukumo wa kuajiri wa kampuni ya reli ya Uhispania Renfe kwa hivyo una uwezekano wa kutosheleza sehemu ndogo tu ya wanawake wanaotaka kufanya kazi katika sekta ya umma.

    Licha ya mageuzi makubwa ya kijamii, wanawake wa Saudia bado lazima wapate kibali cha mlezi wa kiume ili kuolewa, kuondoka gerezani, au kupata huduma fulani za afya.

    Wanaharakati wa haki za binadamu wanasema wanawake pia wanaendelea kukabiliwa na ubaguzi kuhusiana na ndoa, familia, talaka na maamuzi yanayohusiana na watoto.

    • Jinsi somo la 'mwanaume anavyoweza kuoa mara nyingine' lilivyoibua utata nchini Saudi Arabia
    • Wakati Tanzania, Kenya zikihaha kuandika Katiba, kuna mataifa yasiyokuwa na katiba ya kuandika
  7. Upandikizaji wa kwanza wa uume wafanywa na Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan

    Inakadiriwa kuwa asilimia 15-20 ya wanaume wana matatizo ya Erectile dysfunction (ED) na mshindo wa mapema(Premature Ejaculation)

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Hospitali ya Chuo Kiku cha Aga Khan imesema imefanikisha upandikizaji wa kwanza wa uume katikakanda ya Afrika mashariki na kati .

    Upasuaji huo maalum umefanyiwa kwa mwanaume katika umri wa miaka ya 40 ambaye alikuwa na hali ya maumbile nyeti kushindwa kuwa tayari, kwa kitaalamu Erectile dysfunction (ED) tatizo ambalo limemsumbua kwa miaka kadhaa kulingana na taarifa ya hospitali hiyo .

    Tatizo hilo hutokea wakati ambapo mwanaume hawezi kushiriki katika tendo la ndoa kwa dakika 15 mfululizo na mgonjwa huyo alikuwa amepokea aina nyingine za matibabu bila hali yake kuboreka .

    ‘Upandikazaji huu huchukua takribai saa moja na unahusisha kuweka kifaa maalumu (Prosthesis) ambacho kinapachikwa kwenye uume na kumwezesha mtu kufanya tendo la ndoa wakati wowote bila kuhitajika kutumia dawa nyingine’ amesema Dkt.Ahmed Yousef aliyeongoza upasuaji huo .

    Upasuaji huo umefanyika kwa mara ya kwanza katika ukanda huu kwa sababu unahitaji utaalamu wa kipekee na ufahamu wa kitengo cha tiba ya Urolojia.

    Inakadiriwa kuwa asilimia 15-20 ya wanaume wana matatizo ya Erectile dysfunction (ED) na mshindo wa mapema(Premature Ejaculation) na wengi wanateseka kimya kimya kwa sababu ya hali hizo .

  8. Mzozo mbaya Mali: Macron atangaza wanajeshi kuondoka baada ya miaka

    Wanajeshi wa Ufaransa wamekuwa wakipigana nchini Mali tangu 2013

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Ufaransa wamekuwa wakipigana nchini Mali tangu 2013

    Ufaransa na washirika wake katika kikosi cha Umoja wa Ulaya wataondoa wanajeshi wao kutoka Mali baada ya takriban muongo mmoja, rais Emmanuel Macron ametangaza.

    Wanajeshi hao wamehusika katika vita dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu nchini humo.

    Bw Macron alisema uamuzi wa kuondoka ulifuatia kuvunjika kwa uhusiano wa kidiplomasia, huku kukiwa na ongezeko la uhasama kutoka kwa watawala wa kijeshi wa Mali.

    Vikosi hivyo vitatumwa tena katika eneo la Sahel barani Afrika.

    "Hatuwezi kubaki katika shughuli za kijeshi pamoja na mamlaka ambazo mikakati na malengo yaliyofichika hatushirikishani," Bw Macron aliambia mkutano wa wanahabari mjini Paris siku ya Alhamisi.

    Alikanusha madai kuwa kujiondoa huko ni kukubali kushindwa na kusisitiza kuwa Ufaransa inasalia na nia ya kupambana na waasi wa Kiislamu katika eneo hilo.

    Aliongeza kuwa Niger imekubali kuwa mwenyeji wa baadhi ya vikosi vinavyoondoka.

    "Ufaransa imekuwa na jukumu muhimu la katika uhamasishaji huu wa kimataifa kwa ajili ya Sahel", alisema.

    "Tutaendelea kuhakikisha jukumu hili la kuunganisha."

    Soma zaidi:

  9. Malawi: Wabunge walikosolewa kwa kudai kupewa makoti ya mvua

    Raia wa Malawi wanawakosoa wabunge wao baada ya mbunge kuliomba bunge kuwanunulia makoti ya mvua.

    Mbunge wa Lilongwe Kusini Steven Kamsiyamo alitoa ombi hilo Jumatano akisema walihitaji kujikinga na mvua wakati wakitembea hadi chumbani kutoka kwa maegesho ya magari.

    Inasemekana kwamba kiongozi huyo wa bunge aliwahakikishia wabunge kuwa suala hilo litapelekwa kwa kamati ya tume ya bunge ili kuzingatiwa.

    Inasemekana Bw Kamsiyamo aliondoa ombi lake saa chache baadaye:

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Baadhi ya Wamalawi wamekasirishwa na hatua hiyo wakisema wabunge hao walikuwa wabinafsi na wasio na hisia wakati ambapo mafuriko yameharibu familia nyingi kote nchini.

    “Tuna waathiriwa wa mafuriko huko Salima na Lower Shire ambao wanahitaji msaada. Kwa nini upoteze pesa kwenye makoti ya mvua?”

    Bright Malenga aliuliza kwenye Twitter.

    “Kiwango hiki cha haki hakiwezi kufikirika,” mtumiaji mwingine wa Twitter alisema.

    Mafuriko yaliyosababishwa na dhoruba ya hivi majuzi ya kitropiki ya Ana yaliua makumi ya watu na kuharibu mashamba, nyumba na barabara.

    Wiki iliyopita, mamlaka ya hali ya hewa ilitoa tahadhari ya mafuriko katika maeneo ya kati na kaskazini mwa Malawi.

  10. Viti vya magurudumu vyatolewa kwa eneo lililoathiriwa na wanajihadi Msumbiji

    Zaidi ya watu 120,000 waliolazimika kukimbia makazi yao kwa sababu ya mashambulizi ya wapiganaji wa jihadi kaskazini mwa Msumbiji wanaishi na ulemavu, Umoja wa Mataifa unasema.

    Hii inachangia asilimia 15 ya watu waliokimbia makazi yao katika ghasia ambazo zimeharibu jimbo la Cabo Delgado tangu 2017.

    Tathmini hii ilifanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) kwani viti 35 vya magurudumu, fimbo 70 na fimbo nyeupe 35 vilipewa wenye mahitaji husika katika eneo la Cabo Delgado kwa ushirikiano na shirika la Kibinadamu.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    “Wengi wanategemea msaada wa jamaa, majirani au watu wasiowafahamu”, na bila vifaa muhimu kama vile fimbo au magongo walikuwa wakipata ugumu wa kujenga upya maisha yao, ofisi ya UNHCR huko Cabo Delgado ilisema.

    Soma zaidi:

  11. Maporomoko ya udongo yasababisha vifo takriban 100 Brazil

    Maporomoko ya ardhi Petrópolis, Brazil
    Maelezo ya picha, Mafuriko ya mvua yasababisha maporomoko ya ardhi huko Petrópolis, Brazil

    Takriban watu 100 wamefariki kutokana na maporomoko ya udongo na mafuriko katika mji wa Petrópolis nchini Brazil, maafisa wanasema.

    Jiji hilo, ambalo liko kwenye milima kaskazini mwa Rio de Janeiro, lilikumbwa na mvua kubwa.

    Nyumba katika vitongoji vya milimani ziliharibiwa na magari kusombwa na maji huku mafuriko yakipita katika mitaa ya jiji hilo.

    Timu za utafutaji na uokoaji zinakabiliana na tope kutafuta walionusurika.

    Jeshi la Ulinzi la Kitaifa la Brazil lilisema kwenye Twitter watu 24 wameokolewa wakiwa hai hadi sasa, na vifo 94 vilivyothibitishwa.

    Video zilizoshirikiwa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha uharibifu mkubwa na magari yakielea mitaani.

    "Hali inakaribiana na kama vita... Magari yanayoninginia kwenye nguzo, magari yamepinduka, matope mengi na maji bado yapo," Gavana wa Rio de Janeiro Claudio Castro aliwaambia waandishi wa habari.

  12. Charles Yohane: Mwanasoka wa zamani wa Zimbabwe auawa Afrika Kusini

    Charles Yohane

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Charles Yohane alishiriki mechi 23 kwa Zimbabwe

    Mwanasoka wa zamani wa Zimbabwe Charles Yohane amefariki dunia nchini Afrika Kusini akiwa na umri wa miaka 48 katika tukio linaloonekana kuwa la wizi wa gari.

    Beki Yohane alikuwa kwenye kikosi cha Warriors kwa mechi yao ya kwanza ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka wa 2004.

    Kufuatia kustaafu kucheza alikuwa akifanya kazi Johannesburg kama mkufunzi wa kandanda na dereva wa teksi.

    Mwili wake ulipatikana Soweto siku ya Jumatatu, ingawa inaaminika alifariki Jumamosi usiku.

    "Alitekwa nyara, walichukua gari lake na kumpiga risasi kichwani," kaka yake Lewis aliambia BBC Sport.

    Yohane alihamia Afrika Kusini kutoka Zimbabwe mwaka 1996 na kuichezea timu ya Wits inayoshiriki ligi ya daraja la kwanza, na kuwa nahodha na kuweka rekodi ya kucheza mechi 268 kutoka 1997 hadi 2006.

    Baadaye alikua kocha wa kikosi cha Wits, lakini aliachiliwa kutoka kazini. klabu hiyo ilipouza umiliki wake kwa Tshakhuma Tsha Madzivhandila mwaka wa 2020.

    Yohane aliichezea Zimbabwe mara 23, na kujiimarisha haraka kama chaguo la kwanza la beki wa kushoto wa nchi yake mwaka 1996, alipokuwa akichezea klabu ya Harare, CAPS United.

    Rafiki yake mkubwa Innocent Chikoya alicheza naye katika klabu ya Fire Batteries FC na wakahamia pamoja kwenda African Wanderers ya Afrika Kusini, na Yohane alirejea Zimbabwe kwa muda mfupi mwaka wa 1996 kwa ajili ya kuitumikia Caps United.

    "Hakuwa rafiki, alikuwa kaka, na tumempoteza katika hali mbaya," Chikoya aliambia BBC Sport.

    "Alikuwa mwerevu, mwanasoka mwenye akili, alikuwa na njia za kufanya mambo. Alikuwa kiongozi, mwenye nidhamu na kujitolea.

    "Nitauchukua mwili wake kutoka kwenye chumba cha kuhifadhi maiti siku ya Alhamisi na nitampeleka nyumbani."

    Soma zaidi:

  13. Makamu wa rais wa Kenya ajitetea kuhusu ukosefu wa ng'ombe DR Congo

    DRC

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, DRC

    Naibu rais wa Kenya amejitetea baada ya kuibua hasira katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutokana na matamshi yake ya awali yaliyoashiria kuwa hakuna ng'ombe nchini humo.

    William Ruto alisema wakati wa mkutano wa kisiasa kwamba kuna soko kubwa la mazao ya maziwa ya Kenya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa sababu "watu hawa ambao ni waimbaji tu…hawana ngombe yoyote."

    Hata hivyo kauli hiyo haikuwaendea vyema watu wengi wa Congo, ambao baadhi yao walimshutumu Bw Ruto kwa kukosa heshima.

    Mnamo Jumatano jioni, Bw Ruto alisema anajutia “kutoelewana ambako kunaweza kuwa kumetokea kwasababu ya hotuba yangu“.

    Alisema hotuba yake haikuwa rasmi na haikukusudiwi kudharau lakini ilikuwa ikisisitiza ‘’ukubwa wa fursa” nchini DR Congo.

    Balozi wa Kenya nchini DR Congo alisema maoni hayo yamesababisha “maoni hasi miongoni mwa jumuiya ya wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla”.

    “Ubalozi wa Kenya ungependa kusisitiza kwamba serikali na watu wana uhusiano wa kina na wa heshima; uhusiano wa kihistoria na serikali na watu wa [DRC],” George Masafu alisema katika taarifa yake.

    Soma zaidi:

  14. Davido atimiza ahadi yake ya kutoa mamilioni ya pesa kwa yatima

    Davido

    Chanzo cha picha, ROGER KISBY

    Maelezo ya picha, Davido

    Mwandishi na muimbaji wa muziki mwenye uraia wa Nigeria na Marekani David Adedeji Adeleke, al maarufu Davido ametoa orodha ya vituo vya yatima kote nchini Nigeria ambavyo alivipatia jumla ya naira 250 million (US $600,814.25).

    Kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa kwenye ukurasa wa Twitter, muimbaji huyo - alifichua kuwa alitimiza ahadi yake ya mwaka 2021, alipopokea mamilioni ya naira katika kipindi cha saa72 baada ya kuushirikisha umma maelezo ya akaunti yake ya benki kwenye mitandao ya kijamii wakati wa maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa.

    “Kama nilivyoahidi, kamati ya wanaume watano ya usamabazaji wa pesa iliwekwa. Tangu ilipozinduliwa, wajumbe wa kamati hii wamefanya kazi bila kuchoka kuhakikisha wanakusanya majina na taarifa zilizopo na kuhakikisha vituo vya yatima. Ninafuraha kutangaza kuwa utoaji wa pesa umekamilika ,” ilieleza sehemu ya taarifa yake.

    Kulingana na Davido, alifikiria kuushirikisha umma rekodi hiyo ili kuonyesha uwazi wa malengo yake ya awali.

    “Hadi sasa jumla ya Naira 250,000,000 zimetolewa katika vituo 292 vya yatima,” ilifichua taarifa yjake, na kuongeza kuwa, “Katika moyo wa kuwa na uwazi nilidhani ni busara kuwafahamisha wanaoniunga mkono, mashabiki, marafiki na familia yaliyofikiwa kuhusiana na hili.”

    Davido

    Chanzo cha picha, INSTAGRAM/DAVIDO

    Maelezo ya picha, Davido

    Davido alitumia fursa hiyo kutoa shukrani kwa marafiki ambao aliwaelezea kama wenye maadili ya juu na misimamo.

    “Ningependa kusema asante sana kwa kila mmoja ambaye alifanikisha hili, kamati ya watu wenye maadili memana msimamo ambao walijitolea muda wao kuhakikisha jukumu hili linafanyika, familia yangu nzuri, marafikina wengine wanaotakamema,”alisema.

    Soma:

  15. Hujambo na karibu katika matango yetu ya moja kwa moja