Joe Biden awataka raia wa Marekani kuondoka Ukraine mara moja

Bw Biden alisema hatatuma wanajeshi kuwaokoa Wamarekani ikiwa Moscow itavamia Ukraine.

Moja kwa moja

  1. Idadi ya waliofariki kutokana na kimbunga yafikia 111 Msumbiji

    Kimbunga Batsirai

    Chanzo cha picha, afp

    Maelezo ya picha, Kimbunga Batsirai

    Takriban watu 111 nchini Madagascar sasa wanadaiwa kufariki tangu Kimbunga Batsirai kilipopiga kisiwa kimoja cha Bahari Hindi karibu wiki moja iliyopita.

    Nyumba nyingi zilibomoka kutokana na upepo mkali, na kuwaacha takriban watu 30,000 wakiishi katika makazi ya dharura, kulingana na shirika moja la kukabiliana na za kitaifa.

    Mataifa ya Kusini mwa Afrika hivi majuzi yamekuwa yakikabiliana kimbuga Ana.

    Vimbunga vimekuwa jambo la kawaida kawaida katika sehemu hii ya lakini tatizo la mabadiliko ya tabia nchini yamechochea ya hali ya hewa na kuvifanya vimbunga hivyo kuwa hatari zaidi.

    Hali hiyo imechangia kuwepo kwa ukame, ambao umeathiri sana kusini mwa Madagascar, na hivyo kusababisha wito wa misaada ya kibinadamukwa haraka.

    Nchini Madagascar, vifo 87 kati ya 111 vilivyotokana na Kimbunga Batsirai vilikuwa katika wilaya ya kusini-mashariki ya Ikongo.

    Watu wote 55 waliouawa kutokana na kimbunga Ana walikuwa wanatoka sehemu nyingine ya Madagascar iliopo kaskazini reuters inaripoti.

  2. Kaka yake Kurt Zouma ajipata mashakani baada ya nduguye kumpiga paka

    Yoan Zouma

    Chanzo cha picha, Rex Features

    Maelezo ya picha, Yoan Zouma alikuwa mchezaji huru kabla ya kujiunga na Dagenham & Redbridge mnamo mwezi Desemba

    Dagenham & Redbridge imesema Yoan Zouma hataichezea klabu hiyo hadi kukamilika kwa uchunguzi wa shirika la kufuatilia ustawi na kuzuia ukatili dhidi ya wanyama (RSPCA) kuhusu video ya kaka yake akimpiga teke paka.

    Zouma, 23, aliripotiwa kuchukua video ya mlinzi wa West Ham Kurt Zouma akimpiga teke na kofi mmoja wa wanyama wake wa nyumbani.

    Shirika la RSPCA tangu wakati huo limechukua paka wawili na wanawasiliana na Polisi wa Essex kuhusu tukio hilo.

    Yoan Zouma alikuwa ameomba msamaha na kusema anajutia kuhusika kwake kwenye video hiyo.

    Dagenham ilisema Zouma alitafutwa na shirika hilo wiki hii ili kusaidia katika uchunguzi wao na "alishirikiana nao kikamilifu."

    Beki huyo wa kati wa Ufaransa alijiunga na timu ya Ligi ya Taifa mnamo mwezi Desemba na ameshiriki michuano sita.

    "Dagenham & Redbridge FC ingependa tena kusisitiza kwamba inalaani aina yoyote ya ukatili dhidi ya wanyama na inaelewa kikamilifu hisia za wafuasi wake wengi," taarifa ya klabu ilisema.

    "Kwa hivyo klabu imeamua kwamba hadi shirika la RSPCA likamilishe uchunguzi wake, Yoan hataichezea Dagenham & Redbridge katika mechi yoyote ile. "Hatua zaidi itakayoonekana inafaa kuchukuliwa itachukuliwa baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa RSPCA."

    Kurt Zouma alitajwa katika kikosi cha kwanza cha West Ham dhidi ya Watford siku ya Jumanne, siku moja baada ya video hiyo kubainika.

    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alipigwa faini ya "kiasi cha juu iwezekanavyov na West Ham siku ya Jumatano, na ada hiyo itapelekwa kwa mashirika ya kutoa misaada ya ustawi wa wanyama.

    Soma:

  3. Wabunge wa Tanzania walalamikia ongezeko la matumizi ya vidonge vya kuzuia mimba

    Wabunge wanataka kuhimiza matumizi makubwa ya kondomu

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Wabunge wanataka kuhimiza matumizi makubwa ya kondomu

    Wabunge wa Tanzania wamesema matumizi ya dawa za dharura za uzazi wa mpango zinazojulikana kwa jina la P2 kuzuia mimba kwa wasichana wenye umri wa miaka 14-24 yanaongezeka.

    Wabunge katika kamati ya afya walikuwa wakiwasilisha ripoti kuhusu ongezeko la maambukizi ya VVU ambayo ilibainisha kwamba wasichana walikuwa wakizuia mimba zaidi ya maambukizi.

    Kondomu za mpira za kiume hutoa kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa na zinafaa kwa 98% katika kukomesha mimba.

    Kamati ilipendekeza kuwa wanaouza tembe hizo za dharura wajumuishe kondomu za ziada na kuwashauri wateja kuzitumia ili kuzuia maambukizi ya VVU.

    Takriban watu milioni 1.7 nchini Tanzania wanaishi na VVU.

  4. Baraza la mawaziri wa EAC laidhinisha DR Congo kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki

    th

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) iko hatua moja karibu na kujiunga rasmi na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), baada ya baraza la mawaziri la eneo hilo kupitisha kujiunga kwake

    Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki walipiga kura ya kuunga mkono DRC baada ya kumalizika kwa mazungumzo makali jijini Nairobi. DRC inaonekana kama soko muhimu kwa eneo hilo kutokana na maliasili yake kubwa.

    Baada ya wiki kadhaa za mazungumzo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo sasa inasubiri tu idhini ya Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao watakutana baada ya wiki chache.

    TH

    Chanzo cha picha, EAC

    Kuidhinishwa kwa baraza la mawaziri ni hatua kubwa kwa DRC ambayo iliomba uanachama mwaka 2019. Inakuja baada ya kumalizika kwa majadiliano ambayo yalilenga kuanisha sera za nchi hiyo za kijamii na kiuchumi na zile za EAC na utayari wake na uwezo wake wa kuzingatia sheria za EAC.

    Hii ni pamoja na hadhi ya mfumo wa kodi wa DRC na sheria za kimataifa. Kujumuishwa kwa soko la DRC la karibu watu milioni 90 kutapanua soko la EAC kufikia zaidi ya watu milioni 300 na kufungua umoja huo kwa uchumi wa DRC ambao una utajiri mkubwa wa maliasili.

    Kukubaliwa kwa DRC kutaifanya kuwa mwanachama wa saba wa kanda hiyo inayojumuisha Burundi, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Tanzania na Uganda.

  5. Wafungwa wa zamani wa dawa za kulevya walaumiwa kwa mapinduzi yalioshindwa Guinea-Bissau

    Watu 11 waliuawa wakati wa mapinduzi yaliyoshindwa

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Watu 11 waliuawa wakati wa mapinduzi yaliyoshindwa

    Rais wa Guinea-Bissau anasema waliopanga jaribio la mapinduzi ya wiki jana walitumikia jela za Marekani kwa ulanguzi wa dawa za kulevya.

    Umaro Sissoko Embaló alisema amiri wa zamani wa jeshi la wanamaji na wasaidizi wake wawili walihusika katika njama iliyofadhiliwa vizuri ya kumuua yeye, waziri mkuu wake na maafisa wengine wakuu.

    Alisema aliwaona wanaume wawili katika ikulu wakati wa jaribio la mapinduzi.

    Bw Embaló alikuwa akiongoza kikao cha baraza la mawaziri wakati watu wenye silaha walipovamia eneo hilo.

    Watu 11 waliuawa, wengi wao wakiwa wanajeshi.

  6. Uganda yazingatia kuwafunga jela wale wanaokataa chanjo ya COVID-19

    TH

    Chanzo cha picha, Reuters

    Mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Uganda yanakosoa sheria inayopendekezwa ambayo itawaadhibu watu wanaokataa chanjo wakati wa mlipuko wa maradhi wa hadi miezi sita jela.

    Wiki iliyopita, waziri wa serikali wa Uganda anayehusika na biashara alipendekeza marekebisho ya Sheria ya Afya ya Umma ambayo itafini a faini na vifungo vya jela kwa wale wanaokwepa hatua zilizokusudiwa kupunguza kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza.

    Muswada huo hautaji COVID-19 haswa, lakini bila shaka, COVID-19 ndio ugonjwa ambao nchi na ulimwengu unashughulika nao hivi sasa. Mswada huo unasema kwamba yeyote anayeficha ugonjwa wa kuambukiza anaweza kukabiliwa na faini ya $850 au kifungo cha hadi mwaka mmoja jela.

    Wasimamizi wa shule wanaopokea wanafunzi bila ushahidi wa chanjo, au mzazi ambaye atashindwa kuwasilisha mtoto wake kwa ajili ya chanjo, anaweza kufungwa jela hadi miezi sita, faini ya takriban $1,100 au zote mbili.

  7. Chuo kikuu cha Ethiopia kuanza kufundisha Kiswahili

    th

    Chuo Kikuu cha Addis Ababa nchini Ethiopia kitaanza kufundisha lugha ya Kiswahili baada ya kutia saini makubaliano na chuo kimoja kikuu cha Tanzania.

    Masomo hayo ya lugha yatafanikishwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

    Hatua hiyo inajiri siku chache baada ya Umoja wa Afrika kupitisha Kiswahili kama lugha rasmi ya kazi.

    Kiswahili kinazungumzwa katika nchi kadhaa za Kiafrika.

    Unesco mwaka jana ilitangaza tarehe 7 Julai kuwa siku rasmi duniani ya kuadhimisha lugha ya Kiswahili.

  8. Pendekezo latolewa la tiba ya sindano kwa watu wanaopunguza uzito Uingereza

    TH

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Watu wazima wanaohangaika kupunguza uzito wao hivi karibuni wanaweza kuchomwa sindano ya kila wiki ili kusaidia kuondoa mafuta yasiyofaa.

    Matibabu hayo, kitaalamu semaglutide, yenye jina la Wegovy, huwafanya watu wajihisi wameshiba, hivyo wanakula kidogo, na sio kama wenye njaa.

    Katika majaribio, yaliyotumiwa pamoja na lishe bora na mazoezi, ilisaidia watu wanene kupoteza sehemu ya 10 ya uzani wao - karibu wastani wa kilo 13kg.

    Na Taasisi ya Kitaifa ya Afya na Ubora wa Huduma (NICE) inapendekeza huduma hiyo ipatikane kwenye huduma za afya Uingereza, NHS.

    Uzito kupita kiasi huathiri takriban mtu mzima mmoja kati ya wanne nchini Uingereza na huongeza hatari ya hali nyingine mbaya za kiafya.

    Mnamo mwaka 2018-19, waliolazwa hospitalini nchini Uingereza walihusishwa moja kwa moja na ugonjwa wa uzito mkubwa.

    Helen Knight, kutoka NICE, alisema: "Tunajua kuwa kudhibiti uzito kupita kiasi na unene ni moja ya changamoto kubwa ambayo huduma yetu ya afya inakabili.

    "Ni hali ya maisha yote ambayo inahitaji matibabu, ina athari za kisaikolojia na kimwili, na inaweza kuathiri ubora wa maisha."

  9. Ni muujiza kurejea katika soka-Christian Eriksen

    th

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Christian Eriksen anasema ni muujiza kuweza kuanza tena soka akiwa na Brentford baada ya kuzimia alipokuwa akiichezea Denmark kwenye Euro 2020 msimu uliopita wa joto.

    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amefungwa kifaa cha maalum cha kuwezesha moyo wake kupiga cardioverter-defibrillator (ICD), baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo.

    Amejiunga na The Bees kwa mkataba wa miezi sita baada ya kuachiliwa na Inter Milan.

    "Jambo la kwanza ni kuonesha shukrani," Eriksen aliiambia BBC Sport. "Kwa watu wanaonizunguka, wachezaji wenzangu, madaktari kwanza uwanjani, madaktari wa timu na wahudumu wa afya na kisha hospitalini, kufanya kila kitu na kuangalia kila kitu.

    "Halafu ujumbe wote kutoka kwa watu kwa kuniunga mkono kwa yale ambayo familia yangu imepitia.

    Imekuwa vizuri sana kuona ujumbe wa shukrani. "Nina bahati sana na nimewaambia ana kwa ana, nimefurahi sana wamefanya walichofanya vinginevyo nisingekuwa hapa."

  10. Polisi wa Sharia wa Nigeria waharibu chupa milioni nne za bia huko Kano

    th

    Chanzo cha picha, AFP

    Polisi wa kidini nchini Nigeria wameteketeza karibu chupa milioni nne za bia katika msako mkali wa pombe.

    Chupa hizo zilisagwa ardhini na tingatinga katika mji wa kaskazini wa Kano mbele ya umati wa watu waliokuwa wakishangilia "Allahu Akbar" (Mungu ni Mkuu).

    Mji huo wenye Waislamu wengi uko katika mojawapo ya majimbo kadhaa ya kaskazini mwa Nigeria ambayo yamepiga marufuku pombe chini ya sheria ya Sharia.

    Bia hizo zilikuwa zimenaswa kutoka kwa malori yaliyokuwa yakitoka eneo la kusini lenye Wakristo wengi, maafisa wameliambia shirika la habari la AFP.

    Polisi wa Shariah, wanaojulikana kama Hisbah, mara kwa mara huharibu pombe na dawa za kulevya zilizotwaliwa lakini uchukuzi huo wa Jumatano ulikuwa mkubwa zaidi katika msako mkali unaoendelea.

    Maafisa wanasema waliviringisha chupa 3,873,163 za bia na aina nyingine za pombe kwenye tingatinga kwenye eneo la wazi kama sehemu ya vita dhidi ya vileo. Maafisa kisha waliwasha mabaki yaliyopondwa kwa moto na kuruhusu moto huo kuwaka hadi usiku, kulingana na wanakijiji waliotazama.

  11. Joe Biden awataka raia wa Marekani kuondoka Ukraine mara moja

    th

    Chanzo cha picha, AFP VIA GETTY IMAGES

    Rais wa Marekani Joe Biden ametoa wito kwa raia wote wa Marekani waliosalia nchini Ukraine kuondoka nchini humo mara moja kutokana na kuongezeka kwa vitisho vya kuchukuliwa hatua za kijeshi za Urusi.

    Bw Biden alisema hatatuma wanajeshi kuwaokoa Wamarekani ikiwa Moscow itavamia Ukraine.

    Alionya kwamba "mambo yanaweza kutokea haraka" katika eneo hilo.

    Urusi imekanusha mara kwa mara mpango wowote wa kuivamia Ukraine licha ya kuwa na wanajeshi zaidi ya 100,000 kwenye mpaka.

    Lakini ndiyo kwanza imeanza mazoezi makubwa ya kijeshi na nchi jirani ya Belarus, na Ukraine imeishutumu Urusi kwa kuizuia kuingia baharini.

    Kremlin inasema inataka kutekeleza "mistari nyekundu" ili kuhakikisha kuwa jirani yake wa zamani wa Soviet haingii NATO.

    Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson alisema Alhamisi kwamba Ulaya inakabiliwa na mzozo mkubwa zaidi wa usalama katika miongo kadhaa huku kukiwa na mvutano.

  12. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja leo Ijumaa tarehe 11 Februari 2022