Mwandishi wa vitabu 'aliyeteswa' atoroka Uganda - wakili

Mwandishi wa Uganda Kakwenza Rukirabashaija, ambaye ameshutumu mamlaka kwa kumtesa alipokuwa kizuizini, ametoroka nchini, wakili wake ameithibitishia BBC

Moja kwa moja

  1. Mcheshi Eric Omondi azua sintofahamu bungeni Kenya

    Ruka Instagram ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa Instagram ujumbe

    Mchekeshaji wa Kenya Eric Omondi hii leo amezua sintofahamu nje ya majengo ya bunge nchini Kenya baada ya kujifungia katika kisanduki kinachoonesha ndani.

    Kwa mujibu wa gazeti la The standard, lengo lake lilikuwa kushinikiza bunge kujadili muswada unaopatia kipaumbele asilimia 75 ya muziki wa Kenya kuchezwa katika maeneo yote nchini.

    ‘’Huu ni mgomo wa kutokula na nitasalia hapa hadi wabunge watakapojadili muswada huu’’, Omondi alinukuliwa na gazeti la The Standard akisema.

    ‘’Natangaza rasmi mgomo wa kula, iwapo nitalazimika kusalia hapa kwa miezi miwili, basi ni sawa. Iwapo nitakufa hapa kwasababu ya kutokula pia ni sawa’’, Omondi alisema.

    Tayari Mbunge wa Dagoretti nchini Kenya John Kiarie amewasilisha muswada bungeni unaosema kwamba suala linalowasilishwa na mcheshi huyo litajadiliwa.

    Miezi miwili iliopita mcheshi huyo alikamatwa alipokuwa akijaribu kuvamia bunge kwa suala hilo hilo.

    ‘’Nilipokuwa hapa siku za nyuma , nilisalia peke yangu , hakuna msanii hata mmoja wa muziki alinisaidia kupigania maslahi yao’’, Omondi alilalama.

    Lengo lake amesema kwamba ni kuhakikisha kuwa muswada huo unapitishwa kufikia machi mwezi huu ili kuwasaidia wasanii nchini kenya.

  2. Mwandishi wa vitabu 'aliyeteswa' ataoroka Uganda - wakili

    Kakwenza

    Chanzo cha picha, PEN PINTER PRIZE

    Maelezo ya picha, Muandishi Kakwenza

    Mwandishi wa Uganda Kakwenza Rukirabashaija, ambaye ameshutumu mamlaka kwa kumtesa alipokuwa kizuizini, ametoroka nchini, wakili wake ameithibitishia BBC.

    Wakili huyo hakufichua alikokwenda mwandishi huyo aliyeshinda tuzo hiyo, ambaye alikuwa amepewa dhamana na mahakama.

    Rukirabashaija alikuwa ameomba ruhusa ya kuondoka nchini kutafuta matibabu kutokana na majeraha ambayo anasema aliyapata wakati alipokuwa kizuizini hivi majusi katika eneo lisilojulikana.

    Lakini mahakama ilikataa kumpa mwandishi huyo paspoti yake.

    Rukirabashaija alikamatwa mwezi Disemba na kushtakiwa kwa mawasiliano ya kuudhi kwa kutoa matamshi yasiyofurahisha kuhusu Rais Yoweri Museveni na mwanawe kwenye Twitter.

    Katika moja alimwita mtoto wa rais - Jenerali wa jeshi Muhoozi Kainerugaba - "mnene".

    Kesi yake inatarajiwa kuanza Machi 23.

    Rukirabashaija anajulikana zaidi kwa The Greedy Barbarian, riwaya ya kejeli ambayo inaelezea ufisadi wa hali ya juu katika nchi ya kubuni, na Banana Republic: ambapo kuandika ni uhaini

    Kitabu hicho kinaelezea mateso aliyopitia akiwa kizuizini miaka miwili iliyopita.

    Mwaka jana, alijishindia Tuzo ya Pen Pinter kwa kuwa mwandishi jasiri wa kimataifa.

  3. Timu ya soka ya Senegal yazawadiwa mashamba na pesa taslimu

    Rais wa Senegal amlimbikizia sifa kocha wa timu ya taifa, Aliou Cissé

    Chanzo cha picha, Senegal Presidency

    Maelezo ya picha, Rais wa Senegal amlimbikizia sifa kocha wa timu ya taifa, Aliou Cissé

    Senegal imemzawadia kila mchezaji wa timu ya taifa ya kandanda zawadi ya pesa taslimu na mashamba kufuatia ushindi wao katika Kombe la Mataifa ya Afrika.

    Kila mchezaji wa timu alipokea zaidi ya $87,000 (£64,000) na kiwanja katika mji mkuu, Dakar, na katika mji jirani wa Diamniadio wakati wa sherehe iliyofanyika ikulu ya rais.

    Rais Macky Sall pia aliteua timu hiyo katika Tuzo ya heshima kutoka kwa Rais ambayo ni maarufu nchini Senegal, huku mashabiki wakishangilia nje ya lango.

    Rais hapo awali aliishukuru timu hiyo kwa kufika “kilele cha dimba hilo la Afrika” na kuleta ”fahari na heshima ambayo inaashiria watu wa kipekee. ”

    Pia alimsifu kocha wa timu hiyo, Aliou Cissé.

    Senegal iliishinda Misri kwa mikwaju ya penalti 4-2, na kuwa mabingwa wa michuano hiyo kwa mara ya kwanza katika historia yao.

  4. Marekani yatangaza vikwazo vya viza dhidi ya maafisa wa Somalia

    Anthony Blinken

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani, Anthony Blinken

    Marekani imetangaza vikwazo vya viza dhidi ya maafisa wa sasa au wa zamani wa Somalia wanaotuhumiwa kuhujumu michakato ya kidemokrasia.

    Hatua hiyo inawadia wakati ambapo Marekani inasukuma kufanyika kwa uchaguzi wa kuaminika nchini Somalia - ambao umechelewa kwa muda mrefu.

    Katika taarifa, Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alisema vizuizi vya visa vinatumika kwa watu “ambao wameshindwa kutekeleza majukumu yao ya kutekeleza uchaguzi kwa wakati na wazi“.

    Pia vinalenga maafisa ambao “wamewalenga waandishi wa habari na wanachama wa vyama vya upinzani kwa unyanyasaji, vitisho, kukamatwa na vurugu“.

    Somalia imeahirisha uchaguzi tangu mamlaka ya Rais Mohamed Abdullahi Farmajo yalipokamilika Februari mwaka jana.

    Uchaguzi wa wabunge usio wa moja kwa moja ulianza Novemba na ulitarajiwa kuhitimishwa ifikapo tarehe 24 Disemba lakini umekumbwa na ucheleweshaji kutokana na migogoro.

    Waziri Mkuu Mohamed Hussein Roble na viongozi wa majimbo ya kanda walifikia makubaliano tarehe 9 Januari kukamilisha uchaguzi ifikapo Februari 25.

    Wizara ya mambo ya nje ya Marekani inasema viongozi hao wa kisiasa wanapaswa kufuata ahadi zao za kukamilisha mchakato huo kufikia tarehe ya mwisho iliyowekwa.

    Vikwazo hivyo vinafuatia onyo la mwezi uliopita dhidi ya kucheleweshwa zaidi kwa uchaguzi.

  5. Diamond Platnumz awa msanii wa kwanza kutoka Tanzania kutumbuiza katika Grammy’s Global Spin

      • Author, Veronica Mapunda
      • Nafasi, BBC Dar es Salaam
    th

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Msanii wa bongo flavour nchini Tanzania Diamond Platnumz ameweka rekodi nyingine baada ya kuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania kutumbuiza katika jukwaa la mfululizo wa vipindi GLobal Spin vinavyoandaliwa na waandaji wa tuzo za Grammy

    Onesho lake limeoneshwa usiku wa tarehe 7 kupitia mitandao rasmi ya Grammy ambapo Diamond aliimba wimbo wake mpya unaoitwa Gidi pamoja na bendi na wanamitindo ambao kwa pamoja walinogesha onesho hilo

    Kwa onesho lake hilo Diamond anakuwa si tu msanii pekee kutoka Tanzania kupewa heshima hiyo bali ni kwa Afrika Mashariki yote.

    Bosi huyo wa lebo ya WCB hajawahi kupata uteuzi wa Grammy lakini kutokana onesho hilo alilofanya ni wazi kuwa ni njia nzuri ya kuweza kuwakilisha nchi katika Tuzo zijazo za 64 za kila mwaka za Grammy.

    Maonesho haya yaGlobal Spin, yalizinduliwa mwaka 2021 ambapo huangazia na kushirikisha wasanii kutoka pande zote ulimwenguni.

    Kila kipindi kinachorushwa huusisha oneshokutoka kwa msanii au kikundi maarufu kusheherekea ubunifu nan chi zao.

    Mfululizo wa kipindi hicho hurushwa kila inapofika siku ya jumannena ni mara moja kwa wikikupitia mitandao rasmi ya Grammy ambayo ni YouTube, Facebook, Instagram, na Twitter.

    Global Spin inalenga kuwaweka mashabiki wa muziki duniani pamoja kwa njia ya kusisimua zaidi.

    • Msanii nyota wa Tanzania Diamond Platnumz afikisha mashabiki milioni 5 youtube
    • Diamond Platnumz: 'Mafunzo muhimu niliyopata wakati wa janga la corona'
  6. ICJ kutoa uamuzi juu ya kesi ya DRC na Uganda

    Mahakama ya Kimataifa ya Haki mjini Hague Jumatano inatarajiwa kutoa uamuzi wa kesi ya muda mrefu kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Uganda.

    Nchi zote mbili zinadai zilipwe fidia kutokana na mizozo katika jimbo la Ituri lenye utajiri wa madini nchini DR Congo kuanzia mwaka 1998 hadi 2003.

    Mwaka 2005, mahakama iliamua kwamba Uganda lazima ilipe fidia kwa DR Congo kwa kukalia na kupora mali huko Ituri.

    Pia iligundua kuwa DR Congo ina hatia ya kushambulia ubalozi wa Uganda katika mji mkuu Kinshasa na kuuamuru ulipe fidia.

    Mahakama iliamuru majirani hao kujadiliana kuhusu fidia - lakini hawakuweza kufikia makubaliano, huku Kinshasa ikirejesha kesi hiyo mahakamani mwaka wa 2015.

    DR Congo inadai zaidi ya $11bn (£8bn) kama fidia kwa kuikalia Uganda, ambayo imekataa na kutaja hatua hiyo kama"isiyo na uwiano."

  7. EU yaiondolea Burundi vikwazo vya kifedha

    Rais Évariste Ndayishimiye afurahishwa na uamuzi wa EU wa kuondoa vikwazo

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Rais Évariste Ndayishimiye afurahishwa na uamuzi wa EU wa kuondoa vikwazo

    Umoja wa Ulaya umesema unaondoa vikwazo vyake vya kifedha dhidi ya Burundi.

    EU imetaja mazingira ya amani ya kisiasa na maendeleo ya serikali ya Burundi katika maeneo kadhaa, ikiwa ni pamoja na haki za binadamu na kurejea kwa hiari kwa wakimbizi nchini humo.

    Hata hivyo ilibainisha kuwa changamoto zinazoendelea zimesalia“katika nyanja za haki za binadamu, utawala bora, maridhiano na utawala wa sheria.“

    Kuondolewa kwa vikwazo na EU kunafuatia uamuzi kama huo wa Marekani mwaka jana.

    Vikwazo hivyo viliwekwa mwaka wa 2016 baada ya hayati Rais Pierre Nkurunziza kugombea muhula wa tatu madarakani, jambo ambalo lilizusha maandamano mabaya ya watu mitaani.

    Rais Évariste Ndayishimiye alikaribisha uamuzi huo na kusema kuwa nchi hiyo iko tayari kushirikiana na washirika wote.

  8. Korea Kaskazini yajigamba kuwa na uwezo wa kuitikisa dunia kwa mamkombora yanayofika Marekani

    TH

    Korea Kaskazini ilijigamba siku ya Jumanne kwamba ni mojawapo ya nchi chache tu duniani zenye uwezo wa kuweka silaha za nyuklia na makombora ya hali ya juu na ndiyo pekee iliyosimama kidete kwa "kuitikisa dunia" kwa majaribio ya makombora.

    Mvutano wa kimataifa umekuwa ukiongezeka kutokana na mfululizo wa majaribio ya hivi karibuni ya makombora ya balistiki ya Korea Kaskazini, hatua zilizopigwa marufuku kwa muda mrefu na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

    Januari ulikuwa mwezi wa rekodi wa majaribio kama haya, na takribani majaribio saba, ikiwa ni pamoja na aina mpya yakombora"hypersonic" linaloweza kwenda kwa kasi.

    Pia kati ya majaribio hayo ni kurusha kwa mara ya kwanza tangu 2017 kwa kombora la masafa ya kati la Hwasong-12, lenye uwezo wa kushambulia maeneo ya Marekani katika Bahari ya Pasifiki.

    Taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini ilisema mfululizo wa majaribio tangu mwaka mpya yanawakilisha "mafanikio ya ajabu" ambayo yaliimarisha "kuzuia vita vya Korea Kaskazini."

    Pia ilinukuu Hwasong-15, kombora la masafa marefu zaidi (ICBM) kuwahi kurushwa na Korea Kaskazini, ambalo halijarushwa tangu jaribio lake la kwanza mnamo 2017, na inaaminika kuwa na uwezo wa kufika popote nchini Marekani.

  9. DR Congo yafichua njama ya 'kuyumbisha serikali'

    th

    Chanzo cha picha, Reuters

    Wachunguzi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wana "ushahidi mkubwa" unaoonyesha hatua dhidi ya usalama wa taifa, msemaji wa rais amesema.

    Katika taarifa yake iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa Jumanne usiku, Kasongo Mwema alisema jaribio la namna hiyo la "kuvuruga taasisi za kidemokrasia" halitavumiliwa.

    Inafuatia kukamatwa Jumamosi kwa François Beya, mshauri maalum wa usalama wa Rais Félix Tshisekedi.

    Ilitokea wakati rais huyo alipokuwa akihudhuria mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.Kukamatwa huko kulizua maandamano, huku wanachama wa chama cha rais wakiingia mitaani.

    Msemaji wa rais Jumanne alisema uchunguzi unaendelea na hali imedhibitiwa.

    Kimya kutoka kwa serikali na afisi ya rais tangu kisa hicho cha Jumamosi kimechochea tetesi za ukosefu wa utulivu nchini.

    Si Bw Beya wala mawakili wake ambao wametoa taarifa yoyote kwa umma kuhusiana na kukamatwa kwake.

  10. Unaweza pia kutazama:

    TH

    Mamba mmoja wa mwitu nchini Indonesia amenasuliwa baada ya kuwa na tairi shingoni mwake kwa miaka sita.

    Mkazi wa eneo hilo Tili, ambaye ni mwokozi wa wanyama aliyejifundisha mwenyewe, alikuwa akimfuatilia mamba huyo kwa wiki tatu kabla ya kumkamata na kuondoa tairi hiyo .

    TH

    Baada ya kumkamata mamba huyo alitumia msumeno kukata tairi na kumwachilia mnyama huyo kurejea tena majini.

    Unaweza pia kutazama:

    Maelezo ya video, Jinsi mamba alivyoondolewa tairi iliyokuwa imemkaba shingoni kwa miaka sita
  11. Milionea wa Czech aliyeendesha gari kwa kasi ya kilomita 417 kwa saa Ujerumani sasa anakabiliwa na mashtaka

    th

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Milionea kutoka Jamhuri ya Czech Radim Passer anakumbwa na uchunguzi wa ofisi ya mwendesha mashtaka wa Ujerumani.

    Mmiliki huyo wa gari aina ya Bugatti Chiron alichapisha video ya jinsi alivyoongeza kasi hadi 417 km / h kwenye gari lake kwenye barabara moja katika eneo la Saxony-Anhalt huko Ujerumani msimu uliopita wa joto .

    Hakuna kikomo rasmi cha kasi kwa magari ya Ujerumani, lakini ikiwa ofisi ya mwendesha mashitaka wa jiji la Stendal atapata uhalifu katika vitendo vyake, anaweza kufungwa jela miaka miwili, au angalau faini kubwa.

    Hali hiyo imezidishwa kuwa mbaya baada ya kugundulika kwamba mnamo 2015 Passer tayari alikuwa akiongeza kasi kwenye barabara moja ya nchi hiyo hadi 400 km / h katika Bugatti Veyron.

    Mara zote mbili alichapisha video kwenye YouTube, na zimetazamnwa zaidi ya mara milioni 10.

    Waziri wa Uchukuzi wa Ujerumani Volker Wissing alilaani tabia ya dereva huyo akibainisha kuwa ingawa hakuna vizuizi vya mwendo kasi kwenye barabara za magari, gari lazima liwe na udhibiti kila wakati.

  12. Kiasi cha juu zaidi cha Bitcoin zenye thamani ya $5bn zilizoibwa chanaswa

    yh

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Sarafu za Bitcoin iliyoibiwa yenye thamani ya zaidi ya $5bn (£3.7bn) imekamatwa na Idara ya Haki ya Marekani – ukamataji mkubwa zaidi kuwahi wa aina yake kuwahi kutokea

    Maafisa pia waliwakamata na kuwafungulia mashtaka watu wawili siku ya Jumanne kwa kujaribu kutakatisha pesa hizo, ambazo ni sawa na karibu 120,000 Bitcoin.

    Fedha hizo, zilizoibiwa na mdukuzi ambaye alikiuka ubadilishanaji wa sarafu fiche mwaka wa 2016, zilikuwa na thamani ya takriban $71m.

    Lakini, pamoja na kupanda kwa thamani ya Bitcoin, sasa ina thamani ya zaidi ya $5bn.

    Msaidizi wa Mwanasheria Mkuu Kenneth Polite Jr alisema kunaswa huko kulikuwa dhibitisho kwamba serikali "haitaruhusu sarafu fiche kuwa mahali salama pa ufujaji wa pesa au eneo la uvunjaji sheria ndani ya mfumo wetu wa kifedha".

    Pesa hizo zilitokana na udukuzi wa mwaka wa 2016 wa ubadilishanaji wa crypto unaojulikana kama Bitfinex.

    Kulingana na maafisa wa Idara ya Haki, mdukuzi alivunja jukwaa, akafanya zaidi ya miamala 2,000 ambayo haijaidhinishwa na kisha kuingiza pesa hizo kwenye pochi ya kidijitali inayodaiwa kuendeshwa na Ilya Lichtenstein, 34, wa New York.

  13. Mwanaharakati Malala akemea hatua ya wasichana kuzuiwa kuvaa hijab India.

    th

    Chanzo cha picha, UMESH MARPALLY

    Maelezo ya picha, Wanafunzi hao wanasema hawaruhusiwi kuhudhuria darasani

    Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Malala Yousafzai amezungumza kuunga mkono wanafunzi sita wa India wanaopigania haki yao ya kuvaa hijabu darasani.

    Vijana hao wamekuwa wakiandamana katika jimbo la Karnataka kwa wiki kadhaa, wakitoa kupinga katazo la chuo kuhusu vazi la hijab - lililoelezewa na Malala kuwa "la kuogofya".

    Mzozo huo umeenea na kuzusha mivutano ya kidini ndani ya jimbo hilo, huku mapigano yakiripotiwa kuzuka.

    Shule zimefungwa kwa siku tatu kutokana na suala hilo.

    Mzozo huo pia umegonga vichwa vya habari nchini India, na sasa umefika katika mahakama kuu ya jimbo hilo.

    Shauri lililowasilishwa mahakamani na mmoja wa wanafunzi hao linasema kuwa kuvaa hijabu ni haki ya kimsingi ya dini iliyohakikishwa na katiba.

    Siku ya Jumanne, Malala - ambaye alipokuwa na umri wa miaka 15 aliponusurika kushambuliwa na Taliban nchini Pakistani kwa kutetea haki ya wasichana kuelimishwa - alitoa wito kwa viongozi wa India kufanya kitu "kukomesha kutengwa kwa wanawake wa Kiislamu".

    "Kukataa kuwaruhusu wasichana kwenda shuleni wakiwa wamevalia hijabu ni jambo la kutisha," mwanaharakati huyo mwenye umri wa miaka 24 aliandika kwenye mtandao wa . "Lengo la wanawake linaendelea - kwa kuvaa kidogo au zaidi."Alisema.

  14. Israel yaishambulia Syria kujibu mashambulio ya angani

    th

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Jeshi la Israel limesema lilishambulia betri za makombora nchini Syria siku ya Jumatano baada ya kombora la kutungulia ndege kurushwa kuelekea Israel wakati ambapo televisheni ya taifa ya Syria iliripoti kuwa ni shambulio la awali karibu na Damascus Shirika la Reuters linaripoti .

    Msemaji wa jeshi alikataa kuzungumzia ripoti ya Syria ya shambulio la awali la Israel karibu na mji mkuu wa Syria ambalo liliripotiwa kumuua mwanajeshi mmoja na kujeruhi watano.

    Lakini jeshi lilisema lilifanya shambulio la kujibu Syria baada ya kurusha kombora la kutungua ndege.

    Ilisema kuwa kombora hilo lilifyatua ving'ora katika maeneo ya Israel na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, na kulipuka angani.

    "Kufuatia kurushwa kombora la kutungulia ndege mapema usiku wa kuamkia leo, Vikosi vya Ulinzi vya Israel vilishambulia betri za makombora ya kutoka ardhini hadi angani na rada ambazo zilirusha ndege za jeshi la anga la Israeli," jeshi lilisema kwenye Twitter.

    Televisheni ya serikali ya Syria ilisema hapo awali kwamba Kikosi cha ulinzi wa anga cha Syria kilidungua idadi ya makombora ya Israeli juu ya Damascus.

    Israel ilirusha makombora kutoka kwa Miinuko ya Golan inayokaliwa na Israel na ulinzi wa anga wa Syria ukaangusha baadhi yao, televisheni ya taifa ya Syria ilisema.

    "Uchokozi wa Israel" pia ulifanya shambulio la anga mapema Jumatano kwa makombora kutoka kusini mashariki mwa mji mkuu wa Lebanon Beirut, TV ya serikali iliongeza.

    Mwanajeshi mmoja wa Syria aliuawa na watano kujeruhiwa katika mashambulizi hayo, televisheni ya taifa iliripoti, ikitoa mfano wa chanzo cha kijeshi.

    Israel imekuwa ikiendeleza mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya kile inachosema kuwa ni walengwa wa Iran nchini Syria, ambapo majeshi yanayoungwa mkono na Tehran yakiongozwa na Hezbollah ya Lebanon yamemuunga mkono Rais Bashar al-Assad katika muongo mmoja uliopita katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria.

  15. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja hii leo Jumatano tarehe 9 Februari 2022