Maafisa wa polisi saba wafikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji Tanzania
Polisi Mkoani Mtwara limewakamata na kuwafikisha mahakamani Maafisa wa Polisi saba kwa tuhuma za mauaji ya mfanyabiashara Mkoani Lindi, kusini mwa Tanzania.
Moja kwa moja
Msaada wa kwanza wa Msalaba Mwekundu wafika Tigray katika muda wa miezi mitano

Chanzo cha picha, AFP
Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) inasema kwamba, kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miezi mitano, imepeleka msaada wa matibabu katika eneo la Tigray lililokumbwa na vita nchini Ethiopia
Taarifa hiyo ni mwanga adimu wa matumaini kwa Tigray, ambayo anaendelea kuteseka kutokana na uhaba wa vifaa muhimu, miezi 15 katika mzozo huo.
Mratibu wa afya wa ICRC nchini alisema hatua hiyo ni "afueni kubwa".
Ndege hizo - zilizokuwa dawa muhimu - ziliwasili katika mji mkuu wa Tigray Mekelle, siku ya Jumatano na ICRC inapanga safari zaidi katika siku zijazo, pamoja na kutuma misafara kwa barabara.
Hii inafuatia ahadi ya serikali mjini Addis Ababa kuwezesha usafirishaji wa ndege wa chakula na vifaa muhimu vya matibabu katika eneo linalodhibitiwa na waasi.
Ingawa mapigano mapya kwenye mpaka kati ya maeneo ya Tigray na Afar huenda yakatatiza utoaji wa msaada kwa njia ya barabara.
ICRC hapo awali ilisema uhaba wa vifaa vya msingi umewalazimu madaktari huko Tigray kurejelea tena kutumia glavu na vifaa vya upasuaji.
Shirika la Afya Duniani(WHO) hivi majuzi lilisema halijaruhusiwa kutuma vifaa vya matibabu kwa Tigray tangu Mei mwaka jana.
- Mzozo wa Tigray, Ethiopia: Kwa nini ulimwengu mzima una wasiwasi na mzozo huu?
- Ethiopia: Mzozo wa Tigray ulivyogeuka vita vya wenyewe kwa wenyewe
- Mzozo wa Tigray: Waziri Mkuu wa Ethiopia Ahmed Abiy akiri kuwa vikosi vya Eritrea viko ndani ya Tigray
- Mzozo wa Ethiopia wa Tigray: Lalibela yachukuliwa tena - serikali
Orodha ya viumbe wapya 224 waliogunduliwa eneo Mekong yachapishwa

Chanzo cha picha, PRESS ASSOCIATION
Maelezo ya picha, Tumbili aina ya Popa langur aliye na duara nyeupe kwenye macho yake Kundi la uhifadhi la Mfuko wa Wanyamapori Ulimwenguni (WWF) limechapisha orodha ya viumbe wapya 224 waliogunduliwa eneo Mekong.
Viumbe hao ni pamoja na tumbili aliye na duara nyeupe kwenye macho yake, vyura, nyati na aina pekee ya mianzi michanga inayojulikana, ripoti ya WWF inasema.
Baadhi ya viumbe vilivyo hatarini kutoweka duniani katika eneo hilo wanakabiliwa na tisho la kuangamia hata kabla ya kutambuliwa.
Eneo la Mekong linajumuisha Cambodia, Laos, Myanmar, Thailand na Vietnam.

Chanzo cha picha, PRESS ASSOCIATION
Maelezo ya picha, Chura mwenye kichwa vikubwa ni miongoni mwa spishi mpya zilizogunduliwa 
Chanzo cha picha, PRESS ASSOCIATION
Maelezo ya picha, Viumbe hawa wanakabiliwa na tisho la kuangamia hata kabla ya kutambuliwa Kifo cha mwathiriwa wa ubakaji wa miaka 13 chazua ghadhabu Liberia
Kifo cha msichana wa umri wa miaka 13 kilichotokea baada ya kudaiwa kubakwa na mwanamume mwenye umri wa miaka 47 katika mji mkuu, Monrovia kimezua hisia kali nchini Liberia.
Kisa hicho cha unyanyasaji wa kingono unaohusisha mtoto ni cha tatu katika kipindi cha mwezi mmoja - na kusababisha maandamano.
Blessing Molton alikufa siku ya Jumatatu, wiki moja baada ya kushambuliwa - na siku moja kabla ya kufanyiwa upasuaji, kulingana na gazeti la Frontpage la Liberia.
Waandamanaji walikusanyika nje ya bunge siku ya Jumanne kutaka juhudi zaidi kufanywa kukomesha unyanyasaji wa kingono.
Walishikilia mabango ya kutaka kukomesha ubakaji na haki kwa Blessing Molton
Katika ujumbe wake wa kila mwaka siku ya Jumatatu, Rais George Weah alisema serikali yake inafanya kila iwezalo kukabiliana na tishio hilo.
Msafara wa watu mashuhuri wasombwa na mto Msumbiji

Chanzo cha picha, Opais
Msafara wa watu mashuhuri nchini Msumbiji ulisombwa na maji kwenye mto magharibi mwa Msumbiji baada ya kimbunga Ana kukumba nchi hiyo.
Gavana wa mkoa wa Tete na Meya wa Mji wa Tete walikuwa wakirejea kutoka kwa shughuli ya kutathmini uharibifu ulisababishwa na kimbuka hicho wakati msafara wao uliposombwa na maji ya Mto Rovubwe - Ijapokuwa waliokolewa pamoja na abiria wengine
Hata hivyo, watu watatu akiwemo mwandishi wa habari bado hawajulikani waliko.
Mkoa wa umeathiriwa vibaya na kimbunga hicho. Watu sita miongoni mwao watoto wamefariki - wengi wao baada ya kuangukiwa na kuta.
Mji wa Tete umetenganishwa na wilaya ya Moatise baada ya daraja Mto Rovubwe, unaotokana na Mto Zambezi, kuanguka.
Kimbunga Ana kiligonga kaskazini mwa nchi siku ya Jumatatu na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ikiwemo nyumba, hospitali, shule, nguzo za umeme na madaraja.
Ijapokuwa kimbunga hicho kimetulia, watabiri wa hali ya hewa nawasema mvua kubwa ikiandamana na upepo mkali na ngurumo za radi itaendelea kushuhudiwa katika maeneo ya kati na kaskazini.
Uganda yamuondoa mkuu wa ujasusi wa jeshi anayekabiliwa na vikwazo vya Marekani
Mkuu wa ujasusi wa jeshi la Uganda Meja Jenerali Abel Kandiho ameondolewa kwenye wadhifa wake wiki kadhaa baada ya Marekani kumuwekea vikwazo vya kifedha kwa madai ya ukiukaji wa haki za binadamu.
Meja Jenerali Kandiho, ambaye alibadilishwa kama mkuu wa Utawala wa Ujasusi wa Kijeshi (CMI) na Meja Jenerali James Birungi, ametumwa Sudan Kusini kuongoza Mchakato wa Ufuatiliaji wa Usalama, kulingana na taarifa ya jeshi la Uganda.
Uhamisho huo unakuja siku chache baada ya mwana wa kiume wa Rais Yoweri Museveni, Luteni Jenerali Kainerugaba Muhoozi, kuzuru Rwanda kwa mazungumzo na Rais Paul Kagame - safari ambayo iliashiria uhusiano mzuri kati ya nchi hizo jirani baada ya miaka kadhaa ya mvutano.
Awali Rwanda ilimshutumu Meja Jenerali Kandiho kwa kufanya kazi na wapinzani wake.
Waziri mkuu wa Ethiopian akubali ombi la waasi wa TPLF

Chanzo cha picha, AFP
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed anasema serikali yake iko katika mazungumzo na waasi wa TPLF.
Taarifa ya Shirika la habari la Associated Press inaripoti kuwa Bw Abiy Ahmed alitoa kauli hiyo wakati wa mkutano na Waethiopia wanaoishi katika mataifa ya kigeni.
"Kutakuw ana mazungumzo, na makubaliano yataweka maslahi ya umma kwanza," alisema Bw Abiy.
Lakini bado hajatangaza rasmi makubaliano ya serikali yake na TPLF.
Muungano wa Afrika na Marekani wamekuwa wakishirikiana kuzileta pande hizo mbili pamoja ili kumaliza uhasama, lakini bado hawajaweza kufanya hivyo.
Unaweza pia kusoma:
- Mzozo wa Tigray, Ethiopia: Kwa nini ulimwengu mzima una wasiwasi na mzozo huu?
- Ethiopia: Mzozo wa Tigray ulivyogeuka vita vya wenyewe kwa wenyewe
- Mzozo wa Tigray: Waziri Mkuu wa Ethiopia Ahmed Abiy akiri kuwa vikosi vya Eritrea viko ndani ya Tigray
- Mzozo wa Ethiopia wa Tigray: Lalibela yachukuliwa tena - serikali
Gari linalopaa lashinda cheti cha idhini ya kupaa

Maelezo ya picha, AirCar: 'gari linalopaa ' likipaa angani Gari linalopaa lenye uwezo wa kusafiri kilomita zaidi ya 160 kwa saa kwa na urefu wa zaidi ya mita 2,500 imepewa kibali kinachofaa kupaa na mamlaka ya usafiri ya Slovakia.
Ikiwa kama gari na ndege, AirCar ina injini ya BMW na hutumia petroli ya kawaida.
Kampuni hiyo inasema kuwa imefanya safari za za majaribio za saa 70 ili kupata cheti hicho, pamoja na zaidi ya safari za angani 200 na kutua.

Cheti cha "AirCar' kinafungua milango ya uzalishaji mwingi wa magari yenye ufanisi wa juu zaidi yanayosafiri ," alisema muasisi wake, Profesa Stephen Klein.
"Huu ni uthibitisho rasmi na wa mwisho wa uwezo wetu wa kubadilisha njia tunayosafiri safari za urefu wa masafa ya kati."
Ni ndege gani za kijeshi ambazo Marekani inaiuzia Misri?

Chanzo cha picha, Getty Images
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imeidhinisha mauzo ya ndege 12 za kijeshi kwa Misri .
Ndege hizo ziliuzwa kwa dola bilioni 2 za Kimarekani.
Mifumo ya uongozaji wa ndege za ulinzi pamoja na vifaa vingine vya kijeshi pia vitauzwa kwa serikali ay Misri kwa dola milioni 300.
Mauzo ya silaha hizi kwa Misri yanakuja baada ya utawala wa Rais wa Marekani Joe Biden kuikosoa hivi karibuni Misri kwa ukiukaji wa haki za binadamu
Mafuriko yawauwa watu tisa Uganda

Chanzo cha picha, Uganda Red Cross/Twitter
Takriban watu tisa, akiwemo mtoto mmoja, wamefariki kufuatia mafuriko na maporomoko ya udongo katika wilaya ya Kisoro kusini-magharibi ma Uganda.
Miili minane kati ya miili hiyo ilikuwa imefukuliwa kufikia Jumanne asubuhi, limesema Shrika la msalaba mwekundu la Uganda.
"Wa tisa ni mtoto ambaye aliangukiwa na udongo wakati alipokuwa akikimbia. Kwahiyo hakuna anayejua ni wapi hasa pa kuchimba ,"lilisema.
Mvua kubwa imeharibu nyumba, barabara, na miundo mbinu.
Jumatano, shirika la msalaba mwekundu lilisema kuwa linatoa msaada wa dharura kwa ajili ya familia 300 zilizoathiriwa na mkasa huo.
Awali shirika hilo lilituma picha kwenye Twitter , zilizoonyesha baadhi ya uharibifu:
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Maafisa wa polisi saba wafikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji Tanzania
Polisi Mkoani Mtwara wamethibitisha kuwakamata na kuwafikisha mahakamani Maafisa wa Polisi saba kwa tuhuma za mauaji ya mfanyabiashara Mkoani Lindi, kusini mwa Tanzania.
Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Marck Njera imesema mauaji hayo yalifanyika Januari 5, 2022 na mwili wa marehemu ulitupwa kitongoji cha Majengo kijiji cha Hiari Wilayani Mtwara.
Mfanyabiashara huyo, Mussa Hamisi mkazi wa Kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea Mkoani Lindi.
Maafisa wanaoshikiriwa ni Mrakibu wa Polisi Gilbert Kalanje ,Mkuu wa Upelelezi wa wilaya ya Mtwara, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Charles Onyango.
Wengine ni Mrakibu wa Polisi Msaidizi Nicholaus Kisinza ,Mkuu wa Kikosi cha Intelejensia ya Jinai mkoa wa Mtwara, Mkaguzi wa Polisi John Msuya Mganga, Mkuu wa Zahanati ya Polisi Mtwara, Mkaguzi wa Polisi Msaidizi Marco Mbuta, Mkaguzi wa Polisi Shirazi Mkupa na Koplo Salimu Juma Mbalu.Uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.
Mwanaume aliyekataa chanjo anyimwa tiba ya kupandikizwa moyo Marekani

Chanzo cha picha, CBS
Hospitali ya Marekani imemkataa kata kata mgonjwa aliyetaka kupewa matibabu ya kupandikiziwa moyo, kwasababu hakuchanjwa chanjo dhidi yaCovid-19.
DJ Ferguson, mwenye umri wa miaka 31, anahitaji sana moyo mpya, lakini hospitali ya Brigham and Women Hospital iliyoko Boston ilimuondoa kwenye orodha ya wagonjwa waliopangwa kufanyiwa upasuaji huo, alisema baba yake, David.
Alisema kuwa chanjo ya Covidinakwenda kinyume na"kanuni za kimsingi za kijana wake, haiamini ".
Hospitali ilisema inafuata sera.
Hospitali ya Brigham and Womeniliiambia BBCkatika taarifa yake kwamba : "Ikizingatiwa upungufu uliopo wa viungo, tunafanya kila liwezekanalo kwamba mgonjwa anayepokea huduma ya kupandikizwa kiungo ana fursa kubwa ya kuishi."
Msemaji wake alisema hospitali inahitaji"Chanjo ya Covid-19, na mabadiliko ya mtindo wa maisha kwa wagonjwa wanaotarajiwa kupandikiziwa viungo vya mwili ili kuwa na uwezekano bora zaidi wa kufanikiwa kwa upasuaji na kunusurika kwa mgonjwa baada ya upandikizwaji, ikizingatiwa kuwa mfumo wa kinga mwili huwa unadhoofika haraka baada ya upasuaji ".
Hospitali hiyo iliongeza kuwa wengi wa watu 100,000 walioko katika orodha ya wale wanaosubiri kufanyiwa upandikizaji wa kiungo hawatapokea kiungo hicho katika kipindi cha miaka mitano kwasababu ya upungufu wa viungo vilivyopo.
Familia ya wahamiaji haramu yakutwa imekufa katika theruji Canada

Chanzo cha picha, KARTIK JANI
Maelezo ya picha, Jagdish Patel na familia yake Polisi ya Canada imeipata miili ya watu wanne akiwemo mtoto mchanga, katika eneo la uwanja mkubwa uliopo kwenye mpaka wa Canada na Marekani.
Watu hao walipatikana wakiwa wamekufa katika theruji walipokuwa wakijaribu kuingia nchini Marekani kinyume cha sheria.
Imetambuliwa kuwa familia iliyoangamia kwenye theruji ilikuwa ni ya Dingucha, raia wa India kutoka Gujarat Kaskazini iliyokuwa imekwenda ng;ambo na kupotea.Serikali ya India haijatoa kauli bado kuhusiana na tukio hilo.
Hatahivyo Waziri wa mambo ya nje wa India alituma ujumbe wa Twitter akielezea kusikitishwa kwake na tukio lililotokea kwenye mpaka wa Canada:
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Habari za asubuhi, karibu kwenye taarifa zetu za moja kwa moja
