Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tulia Ackson ateuliwa kuwania nafasi ya spika Tanzania
Chama Cha Mapinduzi kimemteua Dkt.Tulia Ackson kuwania nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Moja kwa moja
Kwanini kuna malumbano baina ya Davido na binamu yake?
Mwanamuziki wa Nigeria, Davido amekuwa na malumbano na binamu yake Bamidele Adeleke kwenye mitando ya kijamii, jambu lililoibua gumzo miongoni mwa Wanigeria.
Davido alituma jumbe nyingi mtandao wa Twitter akimtaka binamu yake Bamidele apambane naye katika kugombea kiti cha ugavana wa jimbo la Osun, katika uchaguzi wa 2022.
Bamidele Adeleke anagombea kiti hicho na mjomba wake, Ademola Adeleke kwa tiketi ya chama cha Peoples Democratic Party (PDP)
Mjomba wake ambaye ni seneta wa zamani awali aligombea ugavana kwa tiketi ya chama cha PDP mwaka 2018 lakini Gboyega Oyetola kutoka chama cha All Progressive Congress (APC) alimshinda.
Septemba 2021, Seneta Adeleke alirejea kutoka ng’ambo na kutangaza wazi nia yake ya kugombea ugavana katika jimbo la Osuni
Hatahivyo, hilo halikumfurahisha binamu yake Davido, ambaye Januari 18 aliamua kuweka picha ya binamu yake Bamidele Adeleke na akasema anapanga kugombea dhidi yake.
"Inashangaza! Mimi nilimaliza Chuo kikuu na pointi 2:1. Lakini binamu yangu Dele ambaye alihangaika kupata hata pointi 2: sasa ni miongoni mwa "wasomi wenye akili..." Davido aliandika kwenye twitter.
Baada ya ujumbe wa Davido, mjomba wake, Ademola Adeleke alijibu kwa Twitter akisema ; "Usiwe na wasiwasi mpwa wangu Mungu yuko nasi ❤️"
Binamu yake Davido Banidele Adeleke alimjibu pia Davido kwa twitter akisema hata kwa yote wanayokwenda kumfanyia 'bado nitaendelea kuwapenda'
Oga Bamidele alisema mashabiki wa Davido walimtishia kwenye mitandao ya kijamii
Kwa Picha: Sherehe za ubatizo wa Waethiopia
Mkanyagano katika mkutano wa injili wa Wakristo Liberia wawauwa 29
Takriban watu 29, wakiwemo watoto 11, na mwanamke mmoja mjamzito, wamekufa katika mkanyagano uliotokea katika mkutano wa injili wa Wakristo katika eneo linalokaliwa na watu wengi katika mji mkuu ,Monrovia.
Msemaji wa polisi Moses Carter ameiambia BBC kuwa mkanyagano huo ulitokea Jumatano usiku wakati makundi ya magenge, baadhi yao wakiwa wamebeba visu, kuingia katika eneo la wazi na kuwashambulia waumini.
Aliongeza kuwa mtu mmoja, ambaye alikuwa ameshika kisu, amekamatwa.
Mkutano huo wa injili-The crusade -neno ambalo kwa kawaida hutumiwa na Liberia kuelezea mkutano wa Wakristo -ulikuwa umeandaliwa na mchungaji mwenye ushawishi.
Miili ya waliokufa imepelekwa katika hifadhi ya maiti katika hospitali inayofahamika kama - Redemption Hospital, karibu na eneo ulipofanyika mkutano huo, katika mji wa mwambao wa New Kru.
Idadi ya magenge inayoendesha harakati zake kwenye mitaa ya miji ya Liberia imeongezeka katika miaka ya hivi karibuni.
Rais George Weah alitarajiwa kutembelea eneo la tukio Alhamisi, kulingana kituo cha redio -OK FM, ambacho ni cha kibinafsi kilichopo mjini Monrovia.
Tulia Ackson ateuliwa kuwania nafasi ya Uspika Tanzania
Chama Cha Mapinduzi kimemteua Dkt.Tulia Ackson kuwania nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hatua hiyo imetangazwa na katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka, punde baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM.
Kabla ya kuomba kuwania nafasi ya Spika, Dkt.Tulia alikuwa Naibu spika wa Bunge.
Kiti cha spika kwa sasa kiko wazi baada ya aliyekuwa spika wa bunge Job Ndugai kujiuzulu.
Tulia atawania nafasi hiyo na wagombea wa vyama vingine watakaopitishwa na vyama vyama vyao.
Papa Benedict alishindwa kuchukua hatua dhidi ya unyanyasaji , ripoti mpya yabaini
Papa wa zamani Papa Benedict XVI alishindwa kuchukua hatua dhidi ya visa vya watoto wanne walionyanyaswa alipokuwa askofu mkuu wa Munich, Uchunguzi wa Ujerumani kuhusiana na Kanisa Katoliki umebaini.
Papa Benedict, wakati ule akiitwa Josef Ratzinger, alikuwa na wadhifa huo kuanzia mwaka 1977 hadi mwaka 1982. Amekanusha shutuma hizo.
Lakini ripoti mpya kuhusiana na madai ya historia ya unyanyasaji yaliyochunguzwa na kampuni ya sheria ya Ujerumani inamtia hatiani papa huyo wa zamani.
Unyanyasadi uliendelea chini ya uongozi wake, imedai ripoti hiyo, na kuongeza kuwa washutiwa wa unyanyaji huo waliendelea kuwa na nyadhifa za kanisa.
Papa huyo wa zamani , ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 94, alikuwa Kiongozi wa Kanisa wa 600, mwaka 2013. Tangu wakati huo amekuwa akiishi maisha ya ukimya katika mji wa Vatcan.
Ripoti mpya, iliyoitishwa na Kanisa Katoliki, alidai aliambiwa kuhusu taarifa za unyanyasaji wa watoto wakati alipokuwa akikaimu kama Askofu mkuu, lakini hakuchukua hatua.
"Visa viwili kati ya visa hivi vya unyamyasaji, vilitekelezwa wakati wa uongozi wake," wakili Martin Pusch alisema alipokuwa akitangaza ripoti.
"Katika matukio yote mawili, washukiwa waliendelea kufanya kazi ya kuhuduu kama wachungaji." Alisema.
Miili ya watu watatu yakutwa pembezoni mwa mto Tanzania
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Alfred Lasteck
- Nafasi, BBC News, Dar es Salaam
Miili ya wanawake watatu imeokotwa pembezoni mwa mto katika eneo Nyakato-Buzuruga jijini Mwanza, Kaskazini Magharibi mwa Tanzania.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Gidion Msuya miili hiyo iligunduliwa Januari 19, 2022 na uchunguzi wa vifo hivyo inaendelea.
Msuya aliiambia BBC kuwa, “Bado tunaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na mpaka sasa bado hatujabaini taarifa za marehemu wala taarifa za waliohusika kwenye tukio hilo.
Akiilezea tukio hilo lililoshuhudiwa jana, Mwenyekiti wa mtaa wa Mecco eneo la Nyakato, Scolastica Barnabas alisema miili hiyo iliopolewa na kukutwa haina nguo ikiwa na majeraha shingoni.
Alisema maiti tatu hizo zilizokutwa kando ya mto huo ni za wanawake wanaokadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 18.
Polisi wa Kenya wachunguza kifo cha DJ
Dj wa Kenya anayefanya kazi na chombo kimoja cha habari nchini Kenya amefariki baada ya kuzimia akiwa kazini jijini Nairobi.
Polisi wanachunguza chanzo cha kifo chake baada ya wafanyakazi wenzake kuviambia vyombo vya habari kuwa alizima akaunti zake za mitandao ya kijamii, kutuma ujumbe mfupi kwa familia na marafiki na kuacha ujumbe.
DJ Lithium alipelekwa hospitalini na wenzake lakini madaktari walisema alifariki alipofika.
Wakenya mtandaoni wamekuwa wakitoa sifa na kutuma salamu za rambirambi kwa familia yake.
Mwajiri wake Capital FM alisema kuwa Dj huyo alikuwa mwenye talanta.
DJ Lithium alikuwa akifanya kazi katika kituo cha redio kwa miaka minane iliyopita.
Mkuu wa Umoja wa Mataifa apongeza juhudi za Ethiopia za kuleta amani
Katimu Mkuu wa umoja wa Mataifa António Guterres imesema kuna "jitihada kubwa za kuleta amani" nchini Ethiopia baada ya zaidi ya mwaka mmoja wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Bw Guterres alizungumza na mjumbe mkuu wa Umoja wa Afrika (AU) katika Pembe ya Afrika Olusegun Obasanjo ambaye alimweleza kuhusu juhudi za amani.
Bw Obasanjo amekuwa akikutana na maafisa wa serikali ya muungano yna kundi la waasi wa Tigray People's Liberation Front (TPLF).
Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alisema mjumbe wa AU "alionyesha matumaini kwamba sasa kuna fursa ya kweli ya utatuzi wa kisiasa na kidiplomasia wa mzozo huo".
Vikosi vya serikali vimekuwa vikipambana na waasi kaskazini mwa nchi hiyo kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, katika vita vilivyosababisha vifo vya mamia ya watu.
Mapigano kati ya pande hizo mbili yalikuwa yamesimama lakini hivi majuzi kumekuwa na ripoti za mapigano mapya.
Mamilioni ya watu wanakufa kutokana na magonjwa sugu ya dawa, ripoti
Zaidi ya watu milioni 1.2 walifariki kote duniani mnamo 2019 kutokana na maambukizo yanayosababishwa na bakteria sugu kwa viua vijasumu, kulingana na utafiti mkubwa zaidi wa suala hilo hadi sasa.
Hii ni zaidi ya idadi ya vifo vya kila mwaka kutokana na malaria au Ukimwi.
Nchi maskini ndizo zimeathirika zaidi lakini ukinzani wa dawa za kuua viini unatishia afya ya kila mtu, ripoti hiyo inasema.
Uwekezaji wa dharura katika dawa mpya na kutumia za sasa kwa busara zaidi unapendekezwa ili kulinda dhidi yake.
Matumizi ya kupita kiasi ya viuavijasumu katika miaka ya hivi karibuni kwa maambukizo madogo-madogo inamaanisha kuwa yanapungua ufanisi dhidi ya maambukizo hatari.
Watu wanafariki kutokana na maambukizi ya kawaida amabyo yalikuwa yakitibika kwasababu ya bakteria ambayo imekuwa sugu kwa matibabu.
Maafisa wa afya wa Uingereza hivi majuzi walionya upinzani dhidi ya viuavijidudu (AMR) ni "janga lililofichwa" ambalo linaweza kuibuka baada ya Covid-19 isipokuwa dawa za kuua viua vijasumu hazitaidhinishwa.
Makadirio ya vifo vya kimataifa kutoka kwa AMR, iliyochapishwa katika Lancet, yanatokana na uchambuzi wa nchi 204 na timu ya watafiti wa kimataifa, wakiongozwa na Chuo Kikuu cha Washington, Marekani.
Rais wa Burundi aonesha "vipaji vyake vya kupiga ngoma"
Watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini Burundi wamepigwa na butwaa kumuona Rais Evariste Ndayishimiye, akiwa amevalia vazi la kitamaduni la wapiga ngoma, akiimba na kucheza "ngoma za kifalme".
Ikulu ya Burundi, Ntare Rushatsi House, ilishirikisha picha hizo kwenye mtandao wa Twitter kueleza kuwa Rais alikuwa akimalizia rasmi kipindi cha likizo ya serikali na alichukua fursa ya kutembelea hifadhi ya ngoma huko Gishora, Gitega.
Chapisho hilo pia lilisema kuwa Rais, ambaye amekuwa mpiga ngoma tangu akiwa na umri mdogo, hangeweza kujizuia kuvaa vazi hilo na kujiunga na wapiga ngoma wa Gishora.
Ngoma za Burundi sasa ni sehemu ya orodha ya urithi wa kitamaduni usioshikika wa Unesco.
Wapalestina wafurushwa mashariki mwa Jerusalem
Maafisa wa polisi nchini Israel wameifurusha familia moja ya Kipalestinana kuvunja nyumba yao katika eneo la makazi ya mashariki mwa Jerusalem la Sheikh Jarrah.
Maafisa walivamia makazi ya familia ya Salhiya alfajiri na kuwakamata watu kadhaa kabla ya tingatinga kuwasili .
Kumekuwa na makabiliano ya siku mbili baada ya mkuu wa nyumba hiyo kutishia kuilipua badala ya kuondoka.
Maafisa wa Israel walisema kwamba nyumba hiyo ilikuwa haramu – kitu ambacho familia hiyo ilikana na kwamba ardhi hiyo ilihitajika kujenga shule.
Tukio hilo lilivutia jamii ya kimataifa , huku Muungano wa Ulaya na Uingereza ukionya kwamba ufurushaji wa Wapalestina katika ardhi inayokaliwa na Israel ni haramuchini ya sheria za kimataifana kusababisha hali ya wasiwasi mjini Jerusalem.
Wote Waisraeli na Wapalestina wanadai kumiliki mji huo wa zamani.
Israel ambayo ilikalia eneo la mji huo lililokuwa chini ya Jordan1967na kufanikiwa kulivamia na kulinyakua 1980 katika mpango usiotambulika na jamii ya kimataifa – inatambua mji wote wa Jarusalem kama mji wake mkuu.
Hatahivyo viongozi wa Palestina wanataka mashariki mwa Jerusalem – eneo ambalo lina makaazi ya Wapalestina 350,000 na Wayahudi 200,000 kuwa mji wake mkuu wa taifa huru la Palestina.
Wafungwa 10 DRC wahukumiwa kwa ubakaji gerezani
Wafungwa kumiwamepatikana na hatia ya kuwabaka makumi ya wafungwa wa kikewakati wa ghasia katika jela moja iliojaa wafungwa kupitia kiasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.
Wanawake 37 na msichana mmoja walitoa ushahidi kwamba walibakwa mara kadhaa wakati wa ghasia za siku tatu katika jela ya Kasapa Central Prison karibu na mji wa Lubumbashi 2020.
Baadhi ya wafungwa wa kike walipata uja uzitona kuambukizwa maradhi ikiwemo HIV
Wanaume hao 10 walipigwa faini na kuagizwa kuhudumia miaka mingine 15 jela kila mmoja wao.
Ijapokuwa baadhi ya wafungwa waliogopa kutoa ushahidi , makumi walitoa ushahidi mbele ya kiongozi wa mashtaka wa jeshi kwamba walibakwa wakat iwa ghasia hizo.
Melania Mumbo ambaye ni wakili wa waathiriwa, aliambia AFP News ‘’Tumeridhika na uamuzi baada ya kupigania haki kwa muda mrefu.
Gereza hilo lilitekwa na wafungwa wa kiume kwa siku kadhaa mwezi Septemba 2020. Walichoma eneo la wafungwa wa kike- ikiwemo msichana wa miaka 16- na hivyobasi kuwalazimisha wanawake hao kulała katika eneo jingine la jela hiyo ambapo walibakwa.
Takriban wafungwa 20 na askari jela waliripotiwa kuuawa wakat wa ghasia hizokabla maafisa wa usalama kuchukua udhibiti.
Ubakaji huo uliangaziwa na shirika la haki za kibinadamu la Human Rights Watch , ambao waliarifu watawala kuchunguza unyanyasaji huona kuwahudumia walioathiriwa.
Shirika hilo linasema kwamba jela hiyo iliojengwa kumiliki wafungwa 800 , ilikuwa na karibia wafungwa 2000 wakati wa ghasia hizo.
Natumai hujambo. Kama ilivyo ada tutakupasha kuhusu habari tofauti duniani