Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Baba mbaroni kwa kuwabaka binti zake watatu

Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 57, mkoani Manyara Kaskazini mwa Tanzania anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini Tanzania kwa tuhuma za kuwabaka watoto wake watatu wa kike alhamisi ya juma lililopita.

Moja kwa moja

  1. Kim Kardashian awashitaki wawekeza wa sarafu za kidigitali

    Nyota wa mitandao ya kijamii na televisheni Kim Kardashian ni miongoni mwa watu watatu maarufu waliotajwa katika mashitaka yanayoendelea ya watu waliowekeza pesa zao katika Kampuni ya sarafu za kidigitali inayofahamika kama- Itrium Max cryptocurrency na kupoteza pesa zao.

    Watu wengine wanaoshitaki ni pamoja na mwanandondi Floyd Mayweather Jr., mchezaji wa mpira wa kikapu, Paul Pierce na wabunifu wa mfumo wa malipo ya pesa za kidigitali - cryptocurrency.

    Nyaraka za kesi hiyo zinadai kwamba watu maarufu walishirikiana na Idrium Max "kuwawakilisha vibaya na kuuza pesa zao za kidigitali ".

    Itriyam Max ilikana madai hayo na inasubiri ukweli ujulikane.

    Idrium Max Cryptocurrency haina uhusiano wowote wa kisheria au kibiashara na pesa zilizouzwa katika mfumo wa pesa za kidigitali chini ya jina Ethereum.

  2. Baba mbaroni kwa kuwabaka binti zake watatu Tanzania

      • Author, Alfred Lasteck
      • Nafasi, BBC News, Dar es Salaam

    Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 57, mkoani Manyara Kaskazini mwa Tanzania anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini Tanzania kwa tuhuma za kuwabaka watoto wake watatu wa kike alhamisi ya juma lililopita.

    Akitoa taarifa jijini Dodoma mapema leo, Mkuu wa Mawasiliano katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Prudence Constantine amesema kuwa baba huyo anadaiwa kuwafanyia tendo hilo la kikatili mabinti zake hao wenye umri wa miaka 15, 17 na 18.

    Constantine alisema kuwa wizara imesikitishwa na taarifa za tukio hilo na inapenda kutoa taarifa kuwa tayari mtuhumiwa yupo mikononi mwa polisi kwa taratibu zaidi za kisheria.

    Aidha, amesema kuwa watoto wameshapatiwa huduma za kiafya na wanaendelea kupatiwa huduma za msaada wa kisaikolojia na kijamii.

    Mkuu huyo alisema kuwa hivi karibuni kwenye jamii kumekuwa na ongezeko la vitendo vya ukatili kwenye makundi yote ya jamii ikiwemo watoto.

    Hivyo alisema kuwa Wizara inawaomba wananchi kuungana kupinga ukatili wa makundi yote kwa ujumla wake na kutoa taarifa mapema kwenye vyombo vya serikali na vyombo vya kijamii vinavyoweza kutoa msaada wa haraka pale tukio linapotokea.

  3. Mwanaume akatwa kichwa Msumbiji katika shambulio la imani za kishirikina

    Polisi nchini Msumbiji wanasema kichwa cha mwanaume mwenye upara kimekatwa na kuondolewa na wahalifu waliotaka kukiuza kwa mteja wao nchini Mali.

    Wakati mteja wao alipotoweka, walikiacha kichwa hicho katika mji wa kati wa Muandiwa.

    Baadhi ya watu wa Msumbiji wanaamini kuwa kichwa cha mwanaume mwenye upara huwa kina dhahabu ndani yake.

    Ripoti ya kwanza kuhusu kuuawa kwa wanaume wenye upara kwa ajili ya kuchukua vichwa vyao ziliripotiwa mwa 2017.

    Biashara ya viungo vya binadamu ni jambo la kawaida katika nchi za Msumbiji, Malawi na Tanzania ambako vinaaminiwa kuleta utajiri na bahati katika mapenzi.

    Sehemu za miili ya watu wenye ulemavu wa ngozi (ualbino) huuzwa kwa bei ghali.

  4. Nigeria imeshindwa kusimamia sheria za kuzuia ndoa za utotoni - Wanaharakati

    Wanaharakati Nigeria wameshutumu mamlaka ya Nigeria kwa kushindwa kutekeleza ipasavyo sheria zake ili kuzuia ndoa za utotoni, katika ripoti iliyotolewa Jumatatu.

    "Inasikitisha kwamba karibu miongo miwili baada ya Sheria ya Haki za Mtoto kupitishwa, wasichana wa Nigeria bado wanalazimishwa kuingia kwenye ndoa za utotoni" Mkurugenzi wa Human Rights Watch Afrika Mausi Segun alisema.

    Serikali haijajibu ukosoaji wa ripoti hiyo. Ikiangalia jimbo la Kano katika jimbo lenye Waislamu wengi kaskazini na lmo katika eneo la kusini lenye Wakristo wengi, shirika la kutetea haki za binadamu lilisema liligundua kuwa wasichana walioolewa katika majimbo yote mawili walinyimwa haki zao za kimsingi za elimu, mahali salama pa kuishi na uhuru kutoka kwa ghasia.

    Human Rights Watch inadai kuchukuliwa hatua kwa mamlaka za kitaifa na kikanda nchini humo kwa mujibu wa katiba yake yenyewe, pamoja na Mkataba wa Afrika wa Haki na Ustawi wa Mtoto na Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Mtoto.

  5. Kisiwa cha Piel: Utafutaji wa leseni ya kuendesha baa ya miaka 300 waanza

    Utafutaji wa kumpata "mfalme" wa kuendesha kisiwa cha mbali na baa ya miaka 300 karibu na pwani ya Cumbria.

    Shirika mojalimejiunga na harakati za kuendesha Kisiwa cha Piel mnamo Julai baada ya watoza ushuru wa awali kuondoka.

    Watusasa wanaweza kutuma maombi ya ukodishaji wa miaka 10 ili kuendesha baa na kusimamia kisiwa hicho, ambacho kina jumba lililoharibiwa la Karne ya 14 na kambi.

    Baraza la Barrow Borough lilisema mtu huyo "atavikwa taji" kwa kumwagiwa pombe kichwani.

    Baraza ni mlinzi wa kisiwa - kinachoweza kufikiwa tu kwa feri - na inataka mwendesha mpya awepo kwa msimu wa kiangazi.

    Lisema majukumu ya mwombaji aliyefanikiwa yatajumuisha "utunzaji wa nyumba ya wageni, matengenezo ya uwanja wa eneo linalozunguka na usimamizi wa kambi na choo na bafu".

    Aidha baraza hilo lilielezea Kisiwa cha Piel kama "mali kuu kwa Cumbria", lakini likaonya kuwa "mahali pa kipekee na mwendeshaji yeyote anahitaji kufahamu vikwazo vinavyotolewa na nguvu na hali ya hewa".

  6. Watu 10 wauawa ndani ya wiki moja Kaskazini mwa bonde la ufa Kenya

    Hali ya taharuki imepanda katika eneo la kaskazini mwa bonde la Ufa nchini Kenya ambako kumeshuhudiwa msururu wa mashambulio kwa miezi kadhaa.

    Katika majimbo yaPokot Magharibi, Baringo na Elgeyo Marakwet mamaia ya familia zimesambaratishwa kutokana na wizi wamaa kwa mara wa mifugo na mizozo ya mipaka.

    Ripoti zinasema zaidi ya watu 60 wameuawa ndani ya miezi mitano.

    Viongozi wa eneo hilo wanasema hali inaendelea kuwa mbaya baada ya watu 10 kuawa wiki iliyopita.

    Shule kadhaa pia zimeshambuliwa na badhi ya wanafunzi kujeruhiwa , zikiwa zimesalia miezi miwili kabla ya kufanyika kwa mitihani ya kitaifa.

    Video iliyosambazwa katika mitandao ya kijamiinchini humo, inaonesha wanafunziwakijificha kwa hofu chini ya madawati, meza na viti huku milio ya risasi ilitawala angani.

    Viongozi wa usalama katika eneo hilo hata hivyo wameambia vyombo vya Habari vya ndani kwa video hiyo hiyo ni ya uchochezi kwani shambulio lilikuwa likitokea zaidi ya kilomita moja kutoka shuleni.

  7. Uhaba wa mafuta wakumba Uganda kufuatia msongamano mpakani

    Uganda inakabiliwa na tatizo la mafuta kufuatia kujengwa kwa wasafirishaji mafuta katika maeneo ya mpakani mwa Malaba na Busia mashariki mwa nchi hiyo.

    Foleni za lori zinazongoja, zenye urefu wa kilomita 70 (maili 43), zimeripotiwa.

    Madereva wa malori katika eneo hilo wamekuwa wakiandamana kupinga hitaji la serikali ya Uganda kwamba wapime Covid-19 katika maeneo ya mpakani, bila kujali kama waliwasilisha kipimo cha PCR hasi au la.

    Agizo la vipimo mpakani lilitolewa mwanzoni mwa mwezi. Baadaye Uganda ilisitisha lakini tayari kulikuwa na mkusanyiko wa lori katika maeneo ya mpakani.

    Nchi hiyo inaagiza mafuta yake yote na bidhaa nyingine za petroli na hutumia takriban lita 6.5m (galoni 1.7m) kwa siku.

    Bei ya mafuta imekuwa ikipanda kwa kasi tangu mwaka jana, lakini ongezeko kubwa limeonekana katika wiki iliyopita.

    Katika mji mkuu wa Kampala, baadhi ya vituo vya mafuta vimekuwa vikiuza petroli, inayojulikana kama V-power na baadhi ya wasambazaji, ambayo inagharimu shilingi 5,200 za Uganda ($1.5: £1.0) kwa lita katika baadhi ya maduka.

  8. 71 wajitokeza Tanzania kumrithi Job Ndugai kama Spika

    Mchakato wa kumtafuta spika wa Tanzania kuchukua nafasi ya Jacob Ndugai ndani ya chama cha mapinduzi CCM unaanza leo ukiwa na wagombea 71 watakao chujwa.

    Sekretarieti ya Halmashauri kuu ya taifa inakutana leo kujadili wagombea na kuishauri kamati kuu ya halmashauri kuu juu ya wagombea waliojitokeza kuwania kiti hicho cha Uspika.

    Mchakato huo utadumu kwa muda wa siku tatu ambapo siku inayofuata na tarehe 19 itakuwa kazi ya kuchuja na kufanya uteuzi wa mwisho utakaofanywa na Kamati kuu ya halmashauri kuu.

    Majina yatakayopatikana hapo yatapelekwa kwa cocus ya chama ya wabunge wa CCM kwa ajili ya kupiga kura ili kumpata mgombea mmoja akayekwenda bungeni kwa ajili ya kupigiwa kura.

    Mgombea huyo wa CCM ataungana na wagombea wa vyama vingine ili kupigiwa kura ambapo mpaka sasa chama kilichoanza mchakato wa kutafuta mgombea wa Uspika ni chama cha Alliance For Democratic Change ADC ambapo mwanachama wake Maimuna Said amechukua fomu tayari.

    Wagombea kadhaa wanatajwa kuwa mstari wa mbele kumrithi Mbunge wa Kongwa Job Ndugai aliyejiuzulu Januari 6 kufuatia shinikizo kutoka kwa wafuasi wa chama tawala dhidi ya matamshi yake ya kukopa taifa.

    Mchakato wa uchukuaji fomu za kugombea nafasi hiyo ndani ya CCM ulioanza Januari 10, ulifungwa Jumamosi Januari 15, ambapo kila fomu ilitolewa kwa kiasi cha shilingi million moja.

  9. Rafael Benitez: 'Sikujua uzito wa jukumu nililopewa Everton'

    Everton inatarajiwa kumuajiri Dancun Fergusonna Leighton Baines kuwa kaimu wakufunzibaada ya kumfuta kazi Rafael Benitez.

    Hapo jana muda mfupi baada ya kupigwa kalamu Benitez alisema kwamba hakujua uzito wa jukumu alilopewa katika klabu hiyo baada ya kufutwa chini ya miezi saba ya kuhudumu.

    The Toffees waliamuajiri kocha huyo wa zamani wa Liverpoolkuwa mrithi wa Carlo Ancelotti.

    Everton imeshinda mechi moja kati ya 13 za ligi ya Premiana wako katika nafasi ya 16 katika jedwali la ligi , alama sita juu ya eneo la kushushwa daraja.

    ‘’Tulijua haitakuwa rahisi’’, Benitez alisema alipokuwa akiondoka.

    ‘’Ilikuwa changamoto kubwa, kihisia na kimichezo. Upendo wangu wa mji huu , na watu wakeulinifanya kukubali changamoto hii, lakini ni wakati unapokuwa ndani ndiposa unapogundua uzito wa jukumu ulilopewa’’.

    ‘’Kuanzia siku ya kwanza , wafanyakazi wangu na mimi mwenyewe tulifanya kazi kama kawaida, kwa kujizatiti . Hatukuweza kupata matokoe mazuri lakini tulivutia nyoyo za wengi’’.

  10. Rais wa Mali aliyepinduliwa madarakani aaga dunia

    Rais wa Mali aliyeondolewa madarakani Ibrahim Boubacr Keita amefariki akiwa na umri wa miaka 76 , familia yake na rafiki zake wamesema.

    Miaka miwili iliopita aliugua kiharusi lakini chanzo cha kifo chake siku ya Jumapili hakikuwekwa wazi.

    Alifariki mwendo wa saa tatu saa za Uingereza nyumbani kwake mjini Bamako , mmoja wa ndugu zake alikiambia chombo cha Habari cha AFP.

    Bwana Keita aliiongoza Mali kwa miaka saba hadi 2020, wakati alipopinduliwa baada ya maandamano makubwa dhidi ya serikali kutokana na jinsi alivyolishughulikia suala la Wanajihad.

    Mgogoro wa kiuchumi na uchaguzi ulio huru pia ulisababisha maandamano hayo dhidi ya utawala wake.

    Bwana Keita alihusika katika siasa kwa zaidi ya miongo mitatu, akihudumu kama Waziri Mkuu kutoka 1994 hadi 2000.

  11. Natumai hujambo. Tutakupasha kuhusu habari tofauti duniani