Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
KFC yaahidi kununua viazi vya Kenya baada ya malalamiko
Baadhi kwenye mitandao ya kijamii walitaka KFC isusiwe, wakihoji ni kwa nini ilihitaji kuleta viazi hivyo kutoka Misri.
Moja kwa moja
Amri ya kutotoka nje yatangazwa Lamu,pwani ya Kenya baada ya watu kukatwa vichwa
Serikali ya Kenya imeweka amri ya kutotoka nje asubuhi hadi jioni katika eneo la pwani la Lamu, kufuatia mauaji ya watu saba - wawili kati yao walikatwa vichwa - na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Kiislamu.
Waziri wa usalama wa ndani Fred Matiangi amesema amri hiyo ya kutotoka nje inalenga kusaidia vikosi vya usalama kuwasaka wanamgambo hao.
Washukiwa kadhaa tayari wamekamatwa, kwa mujibu wa msemaji wa polisi.
Licha ya kuwepo wanajeshi wa Kenya na Marekani, kundi la al-Shabab lenye uhusiano na al-Qaeda limefanya mashambulizi kadhaa katika eneo hilo na kusababisha makumi ya watu kupoteza maisha na nyumba kuchomwa moto.
Katika shambulio la hivi punde siku ya Jumatatu, watu watano waliuawa kwa kupigwa risasi na wengine wawili kukatwa vichwa.
Mlima wa volcano wa Nyiragongo watoa moshi na majivu
Mojawapo ya volcano zinazoendelea kutokota duniani - Mlima Nyiragongo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo – unatema mawingu makubwa ya moshi mweusi na majivu ya volkano angani.
Picha zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha kreta ya Mlima Nyiragongo imejaa lava moto.
Wanajiolojia kutoka Kituo cha Kuchunguza Volcano cha Goma wanasema bado hakijatiririka, lakini wameona ongezeko la shughuli za mitetemo.
Mkurugenzi wa kituo hicho, Celestin Kasereka, aliambia BBC kwamba milipuko ya hapa na pale ndiyo iliyosababisha moshi na majivu ambayo yanaweza kuonekana katika jiji lote la Goma. Pamoja na hayo, Nyiragongo huenda isilipuke tena , alisema.
Wakazi wameshauriwa kuwa watulivu, lakini hili litakuwa gumu kwa wengi, kwani athari mbaya iliyosababishwa na mlipuko wa Mei iliyopita bado ni mpya akilini mwao.
Ilisababisha vifo vya watu 32, na kuwalazimisha maelfu kutoka kwa nyumba zao.
Wengi walikimbilia nchi jirani ya Rwanda huku wengine wakiwa bado wanaishi katika kambi za muda huko Goma.
Habari za hivi punde, Mechi ya nusu fainali ya Carabao kati ya Arsenal na Liverpool yaahirishwa
Mechi ya mkondo wa kwanza ya nusu fainali ya Kombe la Carabao ya Liverpool dhidi ya Arsenal Alhamisi imeahirishwa kwa sababu ya "mlipuko mkubwa wa Covid" katika kilabu hiyo ya Anfield.
The Reds walifunga kwa muda kituo chao cha mazoezi cha kikosi cha kwanza Jumatano baada ya meneja msaidizi Pep Lijnders kuwa wa hivi punde kulazimika kujitenga.
Mechi ya kwanza sasa itakuwa Anfield Januari 13 na ya pili Uwanja wa Emirates Januari 20, saa 19:45.
Liverpool walikuwa wameomba kuahirishwa kwa mchuano huo siku ya Jumanne.
Pombe iliyotengezwa kutumia ndizi yasababisha vifo vya watu 11-ripoti
Watu 11 wameripotiwa kufariki nchini Rwanda tangu siku kuu ya Krismasi baada ya kunywa pombe ya kienyeji inayotengezwa kutumia ndizi katika wilaya ya kusini mashariki mwa nchi hiyo ya Bugesera.
Watu wanne zaidi wanaripotiwa kuwa hospitalini kwa matibabu lakini tayari wamepofuka.
Watu watano walikamatwa siku ya Jumatatu kuhusiana na tukio hilo, akiwemo mmiliki wa kiwanda cha kutengeneza pombe hiyo nchini humo, Ofisi ya Upelelezi ya Rwanda imethibitisha.
Viwango vya juu vya methanoli vilivyopatikana katika moja ya bia hiyo kwa jina Umuneza, vinaweza kuhusishwa na vifo hivyo, kulingana na Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Rwanda.
Kiwanda cha bia kinachojulikana kama Rwandabev kilikuwa kikifanya kazi bila leseni.
Kampeni ya nchi nzima imezinduliwa ili kubana pombe za kienyeji ambazo hazijaidhinishwa.
KFC yaahidi kununua viazi vya Kenya baada ya malalamiko
Kampuni ya vyakula ya KFC, imewaahidi wateja wa Kenya kwamba itavinunua viazi vya nchini humo kufuatia lalama kwamba huwa inaagiza viazo kutoka nje.
Migahawa yake nchini Kenya ilikuwa imeacha kutoa vibanzi au chipsi kwa sababu ya changamoto za usafirishaji zilizosababishwa na Covid.
Lakini Wakenya walieleza kuwa wakulima wa eneo hilo walikuwa na akiba ya kutosha ya viazi.
Baadhi kwenye mitandao ya kijamii walitaka KFC isusiwe, wakihoji ni kwa nini ilihitaji kuleta viazi hivyo kutoka Misri.
Mwakilishi wa kampuni hiyo alisema wasambazaji walilazimika kupitia uhakikisho wa ubora.
KFC ndio kampuni ya hivi punde zaidi kukumbwa na usumbufu wa Covid.
Mwalimu wa sayansi Marekani akamatwa kwa kumchanja mwanafunzi mwenye umri wa miaka 17
Mwalimu wa shule moja ya New York ambaye hana uhitimu rasmi kufanya matibabu amekamatwa kwa madai ya kutoa chanjo ya Covid kwa mwanafunzi, maafisa wanasema.
Polisi wanasema Laura Russo alitoa dozi hiyo nyumbani kwake licha ya kuwa hakuwa na kibali cha kisheria cha kutoa chanjo au idhini kutoka kwa wazazi wa mvulana huyo.
Bi Russo, 54, ambaye anafundisha biolojia, alizuiliwa mkesha wa mwaka mpya na anaweza kufungwa jela miaka minne iwapo atapatikana na hatia.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 17 aliripotiwa kutaka chanjo hiyo.
Sindano ya chanjo inaweza kuwa hatari ikiwa inafanya vibaya. Madaktari na wafanyikazi wa matibabu walio na leseni wanapaswa kuthibitisha kuwa chanjo sio ghushi au imeisha muda wake. Wagonjwa wanapaswa pia kuulizwa kuhusu historia yao ya matibabu wafuatiliwe kuona hali zao baada ya kuchanjwa .
Polisi wanasema haijulikani jinsi Bi Russo alipata chanjo inayodaiwa kuwa ya Covid, au ni chanjo gani. Hivi sasa, chanjo ya Pfizer-BioNTech ndio pekeelililoidhinishwa kwa Wamarekani walio chini ya umri wa miaka 18.
Video ya tukio hilo katika Long Island inaonekana kumwonyesha Bi Russo akimwambia kijana: "Utakuwa sawa, natumai."
"Haya nenda. Chanjo ya nyumbani," anasema.
Arsenal yashtakiwa na shirikisho la soka FA
Klabu ya Arsenal imeshtakiwa na Shirikisho la soka Uingereza FA kwa kushindwa kuhakikisha wachezaji wao wanajiendesha kwa utaratibu ufaao wakati wa mechi ya Jumamosi dhidi ya Manchester City.
Tukio hilo lilitokea dakika ya 59 baada ya beki wa Gunners, Gabriel kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kupokea kadi ya pili ya njano.
Arsenal wana hadi Januari 7 kujibu
Korea Kaskazini yarusha kombora la balestiki baharini
Korea Kaskazini imeyatua kombora la balistiki baharini ,waziri wa ulinzi wa Korea Kusini amesema.
Kombora hilo liliripotiwa mara ya kwanza na walinzi wa pwani ya Japan mapema Jumatano, kabla ya kuthibitishwa na mamlaka za Seoul baadaye.
Umoja wa Mataifa unapiga marufuku Korea Kaskazini kufanya majaribio ya silaha za balestiki na nyuklia.
Hii ni mara ya kwanza kurusha kombora kufanywa na Pyongyang baada ya kiongozi Kim Jong-un kuahidi kuimarisha uwezo wa ulinzi wa nchi hiyo mwezi uliopita.
Hii ni mara ya kwanza kurusha kombora kufanywa na Pyongyang baada ya kiongozi Kim Jong-un kuahidi kuimarisha uwezo wa ulinzi wa nchi hiyo mwezi uliopita.
Hii ni mara ya kwanza kurusha kombora kufanywa na Pyongyang baada ya kiongozi Kim Jong-un kuahidi kuimarisha uwezo wa ulinzi wa nchi hiyo mwezi uliopita.
"Ujasusi wa Korea Kusini na Marekani wanachambua kwa karibu kwa undani zaidi," Mkuu wa Pamoja wa Wafanyakazi wa Kusini (JCS) walisema katika taarifa.
Waziri wa ulinzi wa Japan Nobuo Kishi alisema kuwa kombora hilo la balestiki liliruka takriban kilomita 500 (maili 310), Reuters iliripoti.
Kulingana na mtaalam mmoja hata hivyo, hapakuwa na njia ya kuthibitisha safu kamili ya shambulio la kombora hilo.
Tembo awaua mama na mtoto nchini Zimbabwe
Mama na mtoto wake wa miezi kadhaa walikanyagwa hadi kufa na tembo kusini-mashariki mwa Zimbabwe.
Mwanamke huyo, ambaye alikuwa amewatembelea jamaa zake katika wilaya ya Chipinge vijijini wakati wa Sikukuu ya Mwaka Mpya, alikuwa njiani kurudi nyumbani wakati tembo alipowashambulia.
Msemaji wa Mamlaka ya Hifadhi za Zimbabwe Tinashe Farawo alisema kuwa tembo huyo aliwashambulia ghafla na kuwaua wawili hao papo hapo.
Tembo huyo ameuawa.
Migogoro kati ya binadamu na wanyamapori ni ya kawaida katika baadhi ya maeneo ya vijijini nchini Zimbabwe.
Waziri wa mambo ya nje wa China kufanya ziara Eritrea, Kenya na Comoro
Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi amewasili Eritrea mnamo Jumanne katika kituo cha kwanza katika ziara ya mataifa matatu ya Afrika ambayo pia itampeleka Kenya na Comoro.
Waziri wa Habari wa Eritrea Yemane Meskel, katika chapisho kwenye Twitter, alisema kuwa Bw Wang alipokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje Osman Saleh na maafisa wengine wakuu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Asmara
Yemane alisema Wang atakuwa nchini humo kwa siku mbili, na atafanya mazungumzo na waziri wa mambo ya nje na baadaye rais Isaias Afwerki.
China imeongeza juhudi za kutumia misaada ya chanjo ya Covid-19 ili kuimarisha ushawishi wake barani Afrika, huku kukiwa na onyo mpya kutoka Marekani kwa washirika wa Kiafrika kuhusu kile kinachoitwa diplomasia ya mtego wa deni.
Watangazaji maarufu wa TV ya Ufaransa wafariki kutokana na covid siku 6 tofauti
Grichka na Igor Bogdanoff ,mapacha mashuhuri wa Ufaransa, watangazaji wa kipindi cha televisheni cha hadithi za kufikirika katika miaka ya 1980 kuhusu anga za juu.
Watangazaji hao wlikufa kwa ugonjwa wa coronavirus ndani ya siku chache.
Mnamo Disemba 28, Grichka na kaka yake wakiwa na umri wa miaka 72, ndugu hao wawili ambao hawakuwa wamechanjwa dhidi ya Covid-19.
Marafiki zao walisema walikuwa na uhakika kwamba mtindo wao wa maisha ungeweza kuwafanya afya zao kuimarika licha ya kuwa walikuwa wamelazwa hospitalini katikati ya mwezi Disemba.
Lakini familia yao hazikueleza sababu ya kifo chao, wakili wao Edouard de Lamaze alithibitisha kwamba wote walikuwa wameambukizwa virusi hivyo.
Bobi Wine amhutubia Museveni katika wimbo mpya
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda na mwanamuziki Bobi Wine ameachia wimbo mpya kwa jina Ogenda, neno la Kiganda linalomaanisha "Utaanguka".
Wimbo huo unamlenga Rais Yoweri Museveni moja kwa moja kwa sababu amekiuka ahadi yake kuleta demokrasia nchini, anasema.
Bobi Wine ameambia BBC kwamba kwamba alilazimika kufichua uhalifu uliofanywa chini ya utawala wa rais ndio sababu picha zilizotumika kwenye video zinatisha.
"Utawala nchini Uganda umewekeza pesa nyingi kuficha ukatili huo," alisema.
Bobi Wine alisema vyombo vya habari nchini Uganda vimezimwa na njia pekee ya kufichua uozo huo ni kupitia muziki.
"Haki inaweza kupatikana pale tu tunapofichua uhalifu, ndiyo maana tunaendelea kuuibua, hiyo ndiyo njia pekee tunayoweza kupambana nayo," alisema.
- Bobi Wine: Mfahamu mwanasiasa mwiba anayeikosesha usingizi serikali ya rais Museveni Uganda
Mjumbe maalum wa Marekani kuzuru Ethiopia wiki hii
Mjumbe maalum wa Marekani katika Pembe ya Afrika, Jeffrey Feltman, atasafiri hadi Ethiopia wiki hii ili kufanya mazungumzo na mamlaka kuhusu vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema kuwa Bw Feltman "alikuwa ajadiliane na maafisa wakuu kuhusu matarajio ya kupatikana kwa amani mpakani".
Katika siku za hivi karibuni waasi wamerejea katika ngome yao katika jimbo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia.
Serikali ya Ethiopia ilisema wanajeshi wake hawatawafuata waasi katika eneo hilo.
"Tunaamini hii inatoa fursa kwa pande zote mbili kusitisha operesheni za mapigano na kuja kwenye meza ya mazungumzo," msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Ned Price alisema.
Ziara ya mjumbe huyo maalum inakuja baada ya Marekani kuondolea Ethiopia upendeleo wa kibiashara kutokana na madai ya ukiukwaji wa haki.
Marekani na EU waonya wanajeshi wa Sudan dhidi ya kumtaja Waziri Mkuu
Marekani, Norway, Uingereza na Umoja wa Ulaya zimeonya jeshi la Sudan dhidi ya kumteua waziri wao mkuu, zikisema kuwa hatua hiyo inaweza kulitumbukiza taifa hilo kwenye mzozo.
Nchi hizo zilisema hazitaunga mkono waziri mkuu au serikali iliyoteuliwa bila kushirikisha wadau mbalimbali wa kiraia.
Waziri mkuu wa zamani, Abdalla Hamdok, alijiuzulu siku ya Jumapili huku kukiwa na mkwamo wa kisiasa na maandamano makubwa yaliyotokana na mapinduzi ya kijeshi ya Oktoba.
Kwa mara nyingine tena nchi za Magharibi zimekemea hatua za jeshi dhidi ya waandamanaji - zaidi ya 50 wameuawa tangu mapinduzi.
Siku ya Jumanne, vikosi vya usalama vilirusha gesi ya kutoa machozi katika miji kadhaa kutawanya umati mkubwa wa watu waliokuwa wakiandamana kupinga utawala wa kijeshi.
Karibu katika matangazo ya moja kwa moja leo Jumatano 05.01.2022.