Chui aliyepotea akamatwa baada ya kuingia katika boma la mtu Kenya
Chui huyo anaaminika kupotea kutoka Mbuga ya Kitaifa ya Tsavo hadi katika mji jirani wa Voi ambako alipatikana, vyombo vya habari nchini humo viliripoti.
Moja kwa moja
Dinah Gahamanyi
UN yaamuru uchunguzi ufanywe kuhusu ukiukwaji wa haki katika vita vya Ethiopia

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Vita hivyo vimesababisha mzozo wa kibinadamu huku mamilioni wakihitaji chakula, Umoja wa Mataifa unasema Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limeamuru uchunguzi kuhusu ukiukwaji wa haki katika mzozo wa Ethiopia kuchunguzwa.
Muungano wa Ulaya ulikuwa umetoa wito wa kufanyika kwa kikao maalum cha baraza hilo mjini Geneva baaada y amashirika ya kitetea haki kusema ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ambao unaweza kuwa uhalifu wa kivita ulifanyika katika vita hivyo vya zaidi ya mwaka mmoja.
Ethiopia imepuuzilia mbali hatua hiyo na kusema imechochewa kisiasa. Baraza la haki za Umoja wa Mataifa lilionya tena kwamba pande zote katika vita vya wenyewe kwa wenyewe zinafanya ukiukaji mkubwa.
Ilisema kuna hatari kwa eneo zima na kutoa wito kwa pande zote kujiondoa.
Ramaphosa anaendelea vyema baada ya kuugua Covid-19

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Rais kwa mara nyingine tena alitoa wito kwa watu kupata chanjo Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa anaendelea kupata nafaa baada ya kupata dalili ya Covid-19 na anaendelea kupata matibabu, kulingana taarifa.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 69-alipatikana na maambukizi ya corona tarehe 12 Disemba - alipoamua kujitenga mjini Cape Town.
Hali yake inaendelea kufuatiliwa kwa karibu na kutibiwa na madaktari wa kijeshi.
Rais anaendelea vyema na anatoa wito kwa watu kuwa waangalifu wakati huu wa msimu wa Krismasi, taarifa iliendelea kusema.
Raia wa Ufaransa wahukumiwa kwa njama ya mapinduzi ya Madagascar

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, waendesha mashtaka walisema washtakiwa walikuwa wakipanga kumuua Rais Rajoelina Raia wawili wa Ufaransa wamehukumiwa vifungo vya miaka 10 na 20 gerezani kwa kupanga njama ya kumpindua Rais wa Madagascar Andry Rajoelina.
Paul Rafanoharana naPhilippe François walishakiwa kwa kuhatarisha usalama wa taifa, kujihusisha na uhalifu na njama ya kutaka kumuua rais.
Watu wengine 20 waliotuhumiwa kwa kuwa washirika wao pia wamehukumiwa vifungo gerezani.
Wakili wa raia hao wa Ufaransa anapanga kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
"Sio hukumu niliyotarajia, ni uamuzi usio wa haki... ni kesi ya kisiasa," wakili wa utetezi Solo Radson alinukuliwa akisema na shirika la habari la AFP.
Mamlaka inasema ilifichua njama ya mapinduzi, iliyopewa jina la "Apollo 21", baada ya kunasa barua pepe, silaha na pesa wakati wa uvamizi mwezi Julai.
François, kanali wa zamani wa jeshi la Ufaransa, alihukumiwa kifungo cha miaka 10.
Rafanoharana, ambaye ni Mfaransa mwenye asili ya-Madagasca aliwahi kuwa mshauri wa Rais Rajoelina, alihukumiwa kifungo cha miaka 20 huku mkewe apewa kifungo cha miaka mitano jela.
Mwingine aliyehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela ni Waziri Mkuu wa zamani wa Madagascar, Victor Ramahatra.
Madagascar imekuwa na historia ndefu ya mapinduzi na machafuko tangu ilipopata uhuru wake kutoka kwa Ufaransa mwaka 1960.
- Kifo cha Rais wa Haiti: Hawa ni marais wengine waliouawa kwa kupigwa risasi wakiwa madarakani
Pande zote katika vita vya Ethiopia zilikuka haki za binadamu-Umoja wa mataifa

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Vita ambavyo vilianza katika eneo la kaskazinila Tigray mwaka jana vimesambaa katika maeneo mengine ya nchi Umoja wa Mataifa (UN) kwa mara nyingine tena wamesema kwamba pande zote katika vita vya wenyewe kwa wenyewe zimekiuka haki za binadamu kwa kiwango cha juu.
Kuna hatari katika jimbo lote na pande zote zinapaswa kurudi nyuma, Umoja wa Mataifa ulisema katika mkutano wake wa baraza la usalama la haki za binadamu mjini Geneva.
Kufuatia ombi la Muungano wa Ulaya, kikao hicho kitaamua iwapo kutateua timu ya kimataifa ya kuchunguza ukiukaji wa haki za binadamu, ambao makundi hayo yanasema unaweza kuwa uhalifu wa kivita.
Ethiopia imepuuzilia mbali hatua hiyo na kuitaja kuwa ni uchochezi wa kisasa.Mkutano huo utajadili suala la waasi wa Tigray kupitia.
Serikali ya Ethiopia inaendelea kuwakamata watu, na watu kati ya 5000 na 7,000 wameshikiliwa, wakiwemo wafanyakazi wa Umoja wa mataiafa, yanasema mashirika ya kimataifa.
Wapiganaji wamchinja mchungaji Msumbiji

Chanzo cha picha, afp
Maelezo ya picha, Maelfu wamewachwa bila makao katika eneo hilo kutokana na ghasia kaskazini mwa Msumbiji Wanamgambo wa Kiislamu wamemuua mchungaji mmoja wa kanisa katika wilaya ya Macomia, ilio na gesi nyingi katika mkoa wa kaskazini wa Cabo Delgabo , kulingana na ripoti.
Jumatano iliopita, mkaazi wa kijiji cha Nova Zambezia alienda katika kituo kikuu cha polisi , akibeba mfuko uliokuwa na kichwa cha mchungaji huyo , chanzo kimoja cha kijeshi kimesema.
Wapiganaji hao wanaodaiwa kuhusika na Islamc state walimkamata mchungaji huyo katika uwanja mmoja, wakamkata kichwa na kumpatia mkewe kichwa hichona kumuagiza kuwaelezea polisi.
Hili ni shambulio la hivi karibuni kutekelezwa na Wanajihad ambao wamekuwa wakilenga wilaya kadhaa za mkoa wa Cabo Delgado tangu mwezi Oktoba 2017.
Wanamgambo hao hivi majuzi wamehamia mkoa wa Niassa , kufuatia wanajeshi waliopelekewa nchini humo na Rwanda, Msumbiji Pamoja na mataifa ya SADC.
Ndege ya Uingereza yaidungua 'droni ndogo ya adui ' Syria

Chanzo cha picha, Getty Images
Ndege ya jet ya kikosi cha anga cha Uingrereza Royal Air Force Typhoon imeitungua "droni ndogo hatari"juu ya anga la Syria, imesema Wizara ya ulinzi.
Ni mara ya kwanza kwa jeshi la Uingereza kuiangusha ndege yay a adui mwingine tangu vilipotokea vita vyaFalklands War karibu miaka 40 iliyopita.
Wizara ya ulinzi imesema kuwa droni hiyo-ambayo ilidunguliwa tarehe 14 Disemba - "ilisababisha tisho" kwa vikosi vya muungano vinavyopigana dhidi ya kundi la Islamic State kusini mwa Syria.
Haikusema ni kundi gani hatari kilichokuwa kinaendesha droni hiyo.
Waziri wa ulinzi wa Uingereza Ben Wallace alisema shambulio lilikuwa"tukio la kuvutia la kuonyesha uwezo wa vya RAF wa kuwatimua maadui angani".
Mwanafunzi Nigeria aliyechomwa moto na wenzake wanaoabudu miungu

Chanzo cha picha, Osun State University.
Mwanafunzi katika Chuo kikuu cha Nigeria kilichopo katika Osogbo, mji mkuu wa jimbo la Osun alichomwa moto na wanafunzi wenzake.
Msemaji wa polisi katika jimbo Osun Yemisi Opalola ameithibitishia BBC tukio hilo.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Chuo kikuu kwa vyombo vya habari, mwanafunzi huyo alikuwa katika kiwango cha juu cha masomo katika Chuo kikuu cha jimbo la Osun.
Shule hiyo imesema kuwa tukio hilo lilitokea tarehe 11 Disemba.
Msemaji wa Chuo hicho Ademola Adesoji amesama tukio hilo lilifahamika baada ya mwanafunzi huyo kwa jinaVictor Oke kukosa kuhudhiria mitihani yake ya masomo, na ndipo walipowasiliana na wazazi wake waliowafahamisha kuwa alishambuliwa na wanafunzi waliomlazimisha kujiunga na ibada za miungu, jambo ambalo hakulitaka.
"Walimpiga kwa mawe, wakapasua mwamba na kumchoma kwa moto kabla ya kuondolewa kwenye moto huo na watu ,"ilisema taarifa.
Katika mitandao ya kijamii nchini Nigeria watu wanashirikisha umma picha inayoonyesha Victor akipigwa.
Anaonekana kwenye picha moja akiwa ameketi ndani ya maji huku watu wakimpiga, na baadaye kumtupa kwenye moto uliokuwa umewashwa.
Victor anasikika akipiga mayowe akisema sitaki kuabudu miungu!.
Chuo kikuu kimesema kiliongea na wazazi waliokifahamisha kuwa alikuwa anapokea matibabu.
Umati washerehekea kifo cha mke wa dikteta wa Chile Augusto Pinochet

Chanzo cha picha, Reuters
Umati umekusanyika katika mji mkuu, Santiago,muda mfupi baada ya taarifa ya kifo kutangazwa
Lucia Hiriart, mjane wa dikteta wa zamaniwa Chile Augusto Pinochet amefariki akiwa na umri wa miaka 99.
Katika kipindi cha dakika chache baada ya kutangazwa kwa taarifa hiyo, umati mkubwa wa watu walikusanyika katika mji mkuu ,Santiago, kusherehekea kila walichokiona kama mwisho wa utawala wakurithishana.
Kwa baadhi, Hiriart alikuwa mfadhili aliyewasaidia wasiojieweza. Lakini kwa wengine alionekana alijulikana kutokana na ushawishi wa mume wake Pinochet.
Pinochet aliiongoza Chile kati ya mwaka 1973 na 1990, wakati watu zaidi ya 3,000 waliuliwa na taifa au kutoweka
Kifo chake kinakuja huku uchaguzi wa urais ulioigawanya nchi ukitarajiwa kufanyika Jumapili.
Wapiga kura watachagua baina ya kiongozi wa zamani wa wanafunzi Gabriel Boric, na mgombea wa mrengo wa kushoto aliyelaani utawala wa kijeshi uliopita wa Chile, na mgombea mwenye itikadi za mrengo wa kulia , José Antonio Kast.

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Waandamanaji wengi wanaona kifo cha Hiriart kama mwisho wa utawala kwa kurithi 
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Pinochet, anayeonekana hapa pamoja na mke wake mwaka 2000,aliongoza utawala uliowauwa na kuwatesa maelfu ya watu 
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Kifo hiki kimekuja siku kadhaa kabla ya uchaguzi wa rais ulioligawanya taifa 
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Muandamanaji huyu amea fulana inayosema: "hakuna ufashisti kamwe" Unaweza pia kusoma:
- Chile: Raia washangilia kifo cha jemedari
Umoja wa Mataifa kufanya kikao cha dharura kuihusu Ethiopia

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Mzoz wa Tigray uliibuka Novemba mwaka jana Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa litafanya kikao cha dharura juu ya Ethiopia, huku kukiwa na taarifa za maafa zaidi katika jimbo la Tigray.
Kikao hicho cha Ijumaa, ambacho kiliombwa na Muungano wa Ulaya, kitaamua iwapo utateuliwa ujumbe wa kimataifa kuchunguza ukiukaji wa haki za binadamu ambao makundi ya haki za binadamu yanasema unaweza kuwa uhalifu wa kivita.
Mzozo katka jimbo la Tigyar uliibuka mwezi Novemba mwaka jana, wakati serikali ya Eritrea ilipotuma vikosi vyake ndani ya jimbo hilo kuzima mashambulio yaTigray People’s Liberation Front – baada ya wapiganaji wake kuteka ngome za jeshi la serikali kuu.
Ni mwezi uliopita tu Umoja wa Mataifa ulitoa ripoti ya kurasa 100 iliyoelezea kwa kila ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu katika Tigray, ikiwa ni pamoja na kufyatua makombora katika miji, kuwauwa raia, na kusambaa kwa vitendo vya unyanyasaji wa kingono.
Wiki hii, mahsirika ya haki za binadamu ya kimataifa, Amnesty International na Human Rights Watch yaliainisha maafa zaidi ikiwa ni pamoja na kuwafunga mahabusu watu wengi, ukatili, kuwalazimisha watu wengi wa jamii ya Watigrayan kuhama makwao.
Mashirika ya Umoja wa Mataifa hayana uwezo kwa kiasi kikubwa wa kuzifikia jamii nyingi ambazo zinakabiliwa na njaa kubwa.
Muungani wa Ulaya unasema baraza la Umoja wa Mataifa la haki za binadamu lina jukumu la kuzuwia ukiukaji zaidi wa haki za binadamu, na kuhakikisha haki inapatikana kwa waathiriwa-nchi wanachama zinataka baraza hilo liwateuwe wachunguzi wa kimataifa.
Ethiopia imepuuzilia mbali hatua hiyo ikiitaja kuwa yenye uchochezi wa kisiasa.
Unaweza pia kusoma:
- Vita vya Ethiopia: Kwanini kujua kinachoendelea Tigray ni muhimu?
- Ethiopia: Mzozo wa Tigray ulivyogeuka vita vya wenyewe kwa wenyewe
- Mgogoro wa Ethiopia wa Tigray: Jinsi TPLF ilivyolizidi maarifa jeshi la Ethiopia
- Mzozo wa Ethiopia wa Tigray: Lalibela yachukuliwa tena - serikali
Kuanguka kwa Bouncy castle : Australia yaomboleza 'mkasa mbaya ' baada ya watoto kuuawa

Chanzo cha picha, TASMANIA POLICE
Maelezo ya picha, Watoto watano walioukufa walikuwa ni: (kutoka kushoto) Zane Mellor, Addison Stewart, Peter Dodt, Jalailah Jayne-Maree Jones na Jye Sheehan Australia inaomboleza kifo cha "kutisha" na mkasa wa kitaifa baada ya watoto watano kufariki walipokuwa wakicheza katika kifaa cha kuchezea kinachoitwa bouncy castle , amesema waziri mkuu wa nchi hiyo Scott Morrison.
Watoto hao walianguka kutoka kimo cha mita 10 juu (futi 32) baada ya upepo kuipeperusha bouncy castle angani katika shule ya Tasmania siku ya Alhamisi.

Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Wakazi wa Davenport rwameacha maua, wanasesere na rambi rambi nyingine mbele ya shule Polisi waliyatambua majina ya watoto waliokufa kama Addison Stewart aliyekuwa na umri wa miaka 11, na Zane Mellor-miaka 12, Jye Sheehan, Jalailah Jayne-Maree Jones, na Peter Dodt.
Watoto wengine watatu bado wako katika hali mahtuti.
Mtoto mwingine aliyejeruhiwa ameruhusiwa kutoka hospitali.
Polisi inasema wazazi wa watoto waliofariki katika ajali hiyo hawakutaka kuongea wazi, lakini wametoa rambirambi zao kupitia mtandao.
Chui aliyepotea akamatwa baada ya kuingia katika boma la mtu Kenya

Chanzo cha picha, Getty Images
Chui mmoja amekamatwa na maafisa wa wanyamapori nchini Kenya baada ya kupotea na kwenda katika nyumba moja kusini-mashariki mwa Kenya.
Video ya askari wa wanyamapori wakiwa wamembeba chui huyo ambaye kichwa chake kilikuwa kimefunikwa, ilichapishwa na gazeti la Daily Nation:
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Chui huyo anaaminika kupotea kutoka Mbuga ya Kitaifa ya Tsavo hadi katika mji jirani wa Voi ambako alipatikana, vyombo vya habari nchini humo viliripoti.
Wakati wa kunaswa kwa chui huyo, wananchi waliizingira nyumba hiyo huku wakirekodi kwa simu zao.
Visa vya wanyama pori kupotea katika maeneo yaliyojengwa si jambo nadra nchini Kenya.
Shirika la Huduma ya Wanyamapori nchini Kenya hapo awali lilihimiza umma kuwa waangalifu na kuripoti wanyama wowote wanaozurura kupitia nambari isiyolipishwa.
Mnamo Julai, maafisa walimkamata simba ambaye alipatikana katika eneo la makazi karibu na jiji kuu la Nairobi.
Chris Noth: Wanawake wawili wanamtuhumu mwigizaji wa Sex And The City kwa unyanyasaji wa kingono

Chanzo cha picha, Getty Images
Wanawake wawili wamemshutumu mwigizaji wa Sex And The City Chris Noth kwa kuwanyanyasa kingono mwaka wa 2004 na 2015.
Wanawake hao walitoa maelezo ya kina ya madai ya kushambuliwa kwa The Hollywood Reporter, iliyochapishwa kwa kutumia majina ya bandia Zoe na Lily.
Gazeti hilo linasema wanawake hao hawajuani.
Katika taarifa, Bw Noth, 67, alisema "mahusiano hayo yalikuwa ya maelewano" na kwamba mashtaka ya dhulma za kingono "ni ya uwongo kabisa".
Zoe, ambaye sasa ana umri wa miaka 40, anasema alikuwa na umri wa miaka 22 wakati mwigizaji huyo alipodaiwa kumbaka katika nyumba moja huko West Hollywood mnamo 2004.
Lily, ambaye sasa ana umri wa miaka 31, anasema alibakwa katika nyumba yake ya Greenwich Village huko New York mnamo 2015 alipokuwa na umri wa miaka 25 na yeye alikuwa na miaka 60.
Nakala ya kina ya mwanahabari Kim Masters pia inawahoji watu kama vile bosi wa Zoe wakati huo, kituo cha matibabu ya ubakaji na rafiki wa Lily ambao simulizi zao zote zinaonekana kuunga mkono madai ya wanawake wote wawili. Nakala hiyo pia inanukuu jumbe za maandishi kati ya Bw Noth na Lily wakati wa madai ya kushambuliwa.
Chris Noth anajulikana kwa majukumu yake ya uigizaji katika Law & Order na Sex And The City, ambapo aliigiza mhusika mkuu, Mr Big.
.
Tania Mendoza: Mwigizaji maarufu wa Mexico auawa kwa kupigwa risasi akimngoja mwanawe

Chanzo cha picha, INSTAGRAM
Mwigizaji na mwimbaji wa Mexico amepigwa risasi na kufa alipokuwa akisubiri kumchukua mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 11 kutoka chuo cha soka katika jimbo la Morelos, ripoti zinasema.
Tania Mendoza alikuwa nje ya jumba la michezo katika jiji la Cuernavaca pamoja na wazazi wengine wakati wanaume wawili waliokuwa wamejihami walipofika kwa pikipiki siku ya Jumanne na kummiminia risasi
Mmoja wao alimpiga risasi mara nyingi kabla ya kutoroka na mwandani wake.
Takriban wanawake 10 waliuawa nchini humo kila siku mwaka jana, kulingana na data rasmi.
Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International lilisema karibu theluthi moja ya wahasiriwa - 940 - walikuwa kesi za mauaji ya wanawake, au mauaji ya kukusudia ya wanawake kwa sababu ya jinsia zao, na kuliita "janga la kushangaza".
Mendoza, ambaye alikuwa na umri wa miaka 42, alipata umaarufu mwaka wa 2005 baada ya kuigiza katika filamu ya La Mera Reyna del Sur. Alikuwa pia ametokea katika michezo kadhaa ya kuigiza lakini katika miaka ya hivi karibuni alijitolea kwa kazi yake kama mwimbaji, na kurekodi albamu tano.
Mnamo 2010, alitekwa nyara na mumewe na mtoto wake, ambaye alikuwa na umri wa miezi sita, kutoka kwa biashara yao ya kuosha magari. Tangu wakati huo, alikuwa ameripoti kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Jimbo la Morelos vitisho kadhaa vya kuuawa.
Bado haijabainika ni nani aliyehusika na mauaji ya Mendoza, au sababu yoyote iliyiosababisha mauaji yake . Baada ya ufyatulianaji risasi huo, polisi walifanya operesheni ya kuwasaka washukiwa hao, lakini hakuna aliyekamatwa.
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja leo Ijumaa tarehe 17 Disemba 2021
