Waziri Mkuu wa Ethiopia aonekana akiwa na sare za kijeshi

Serikali ya Ethiopia imetangaza mipaka ya kuripoti vita hivyo, ambapo waasi wa Tigray wanasemekana kuendelea na harakati zao kuelekea mji mkuu.

Moja kwa moja

  1. Aina mpya ya kirusi cha Corona yatua Ulaya

    Kisa cha kwanza cha maambukizi charipotiwa Ubelgiji

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Kisa cha kwanza cha maambukizi charipotiwa Ubelgiji

    Ubelgiji imeripoti kisa cha kwanza cha aina mpya ya kirusi cha Corona barani Ulaya ambacho kwanza kigunduliwa nchini Afrika Kusini - huku Shirika la Afya Duniani likifanya mkutano maalum kuangazia umuhimu wake.

    Wataalamu mjini Geneva wataamua ikiwa kirusi hicho kinahitaji kutambuliwa kama ni hatari.

    WHO inasema itatoa mwongozo mpya baada ya mazungumzo lakini imeonya kwamba itachukua wiki kadhaa kubaini ikiwe kirusi hicho kivyoweza kuambukizwa na ikiwa chanjo itasalia kuwa na ufanisi dhidi yake.

    Rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen,iliwakumbusha watengenezaji kwamba kandarasi zao na EU inamaanisha lazima wabadili chanjo zao mara moja kwa kuzingatia kirusi hiki kipya.

    Pia alisema kuwa safari zote za anga kwenda nchi zilizo na kirusi kipya cha corona zinapaswa kusitishwa.

    Soma zaidi:

  2. Chuo Kikuu cha Kenya chaomba radhi kwa tangazo tata la mavazi

    Chuo Kikuu Ushirika cha Kenya

    Chanzo cha picha, CUK

    Chuo kikuu kimoja nchini Kenya kimeomba radhi kufuatia ya picha zilizosambaa mtandaoni za bango chuoni hapo linalosema kuwa ubakaji husababishwa na jinsi wanawake wanavyochagua kuvaa.

    Chuo Kikuu cha Ushirika cha Kenya kilikiri kwamba madai kwenye bango hilo - kwamba "mavazi yasiyofaa husababisha unyanyasaji wa kijinsia na ubakaji" - yalikuwa ya uwongo.

    Ilisema bango hilo ni"la kupotosha na la kusikitisha" linalohimiza kanuni za mavazi kwa wanafunzi lilikuwa limewekwa bila idhini yake na baraza la wanafunzi.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    "Tunataka kuthibitisha dhamira yetu ya kuhakikisha kuwa aina zote za ukatili wa kijinsia na unyanyasaji zinatokomezwa," taarifa ya chuo hicho ilisema:

  3. Waziri Mkuu wa Ethiopia aonekana akiwa na sare za kijeshi

    Maelezo ya video, Waziri Mkuu wa Ethiopia aonekana akiwa kwenye mavazi ya kijeshi

    Serikali ya Ethiopia imetangaza mipaka ya kuripoti vita hivyo, ambapo waasi wa Tigray wanasemekana kuendelea na harakati zao kuelekea mji mkuu.

    Katika onyo kwa vyombo vya habari na watumiaji wa mitandao ya kijamii, imepiga marufuku kuripotiwa kwa harakati zozote za kijeshi au taarifa kutoka kwa uwanja wa vita - isipokuwa habari hiyo imeidhinishwa na serikali.

    Wakati huo huo vyombo vya habari vya serikali vimeonesha picha za Waziri Mkuu, Abiy Ahmed, akiwa katika eneo la kijijini akiwa amevalia sare za kijeshi, baada ya kusema siku zilizopita kwamba ataelekea mstari wa mbele.

    Katika mahojiano alionekana kukaidi na kusema kuwa wanajeshi wa serikali wamechukua tena baadhi ya maeneo.

  4. Kenya yaweka masharti kwa wasafiri kutoka kusini mwa Afrika

      • Author, Rhoda Odhiambo
      • Nafasi, BBC health reporter, Nairobi
    Vituo vya afya vinaonywa kujiandaa kwa ongezeko la visa vipya vya corona

    Chanzo cha picha, Reuters

    Wasafiri watakaoingia Kenya kutoka mataifa ya kusini mwa Afrika lazima waoneshe uthibitisho wa kipimo cha PCR kinachoonesha kutokuwa na maambukizi mapema, kisha wakae karantini wanapowasili na kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara baada ya hapo, wizara ya afya ya nchi hiyo imetangaza.

    Hatua hiyo imekuja baada ya kuthibishwa kuwepo kwa aina mpya ya virusi vya corona, inayojulikana kama B.1.1.529, nchini Afrika Kusini, Botswana na Hong Kong.

    Kenya haijatangaza mipango ya haraka ya kupiga marufuku safari za ndege kutoka Afrika Kusini.

    Shirika la ndege la Kenya Airways kwa sasa linafanya safari mbili za ndege kila siku hadi Johannesburg na tatu kwenda Cape Town.

    Mkurugenzi Mkuu wa Afya wa nchi hiyo Patrick Amoth anasema kwamba ingawa idadi ya abiria inaweza isiwe kubwa kutoka Namibia, Lesotho, Botswana, Eswatini na Zimbabwe, itifaki zilizoimarishwa za ufuatiliaji zitaanzishwa.

  5. Ufaransa yasitisha safari za ndege kutoka baadhi ya mataifa ya kusini mwa Afrika

    Ufaransa imesitisha safari za ndege kutoka mataifa kadhaa ya kusini mwa Afrika ili kukabiliana na aina mpya ya virusi vya corona.

    Hatua hiyo ambayo ni sawa na ile iliyotangazwa na Uingereza, inahusu Afrika Kusini, Lesotho, Botswana, Zimbabwe, Msumbiji, Namibia na Eswatini.

    Safari za ndege kutoka nchi hizi zimesitishwa mara moja kwa takribani saa 48, Ofisi ya Waziri Mkuu wa Ufaransa imesema katika taarifa.

    "Watu ambao wamesafiri katika siku 14 zilizopita katika mojawapo ya nchi hizi wanaalikwa kuripoti kwa mamlaka na kufanya vipimo vya RT-PCR haraka iwezekanavyo," taarifa hiyo inaongeza, kwa mujibu wa Le Figaro.

  6. Wanamgambo wamezuia rufaa ya mtoto wa Gaddafi nchini Libya - wakili

    Saif al-Islam Gaddafi anasakwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa tuhuma za uhalifu wa kivita

    Chanzo cha picha, AFP

    Wanamgambo wamevamia mahakama ya Libya na kuwazuia majaji kushughulikia rufaa ya Saif al-Islam Gaddafi dhidi ya uamuzi wa kumtenga kwenye kinyang'anyiro cha urais, kwa mujibu wa wakili wake.

    Khaled Zaidi aliwaambia waandishi wa habari katika jiji la Sebha kwamba kesi hiyo haikuweza kufanyika kwa sababu "wafanyakazi wa mahakama na majaji walilazimishwa kutoka nje wakiwa wamenyooshewa bunduki".

    Alitaja hatua hiyo kuwa "isiyokubalika na isiyostaarabika" na kuonya kuwa itakuwa na "madhara katika mchakato wa uchaguzi".

    Tume ya uchaguzi ilikuwa imezua kugombea kwa wagombea kadhaa wa kinyang'anyiro cha urais akiwemo Bw Gaddafi - mtoto wa marehemu kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi - ikitaja sababu za kisheria.

    Bw.Gaddafi anasakwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita wakati wa maandamano ya wananchi dhidi ya utawala wa marehemu baba yake.

    Waendesha mashtaka wa kijeshi wa Libya walikuwa wameitaka tume ya uchaguzi kusitisha kutayarisha makaratasi ya bwana Gaddafi na mbabe wa kivita Khalifa Haftar hadi watakapohojiwa kuhusu mashtaka ya uhalifu yanayoletwa dhidi yao.

    Siku ya Alhamisi, mahakama ya Misrata ilitoa hukumu ya kifo bila kuwepo mahakamani dhidi ya Bw Haftar kwa kulipua chuo cha kijeshi cha Misrata mwaka wa 2019 na kuua wanajeshi wa Libya wakati wa uasi wake dhidi ya serikali ya umoja wa kitaifa.

    Ugombea wa Bw Haftar kwa uchaguzi wa urais unaonekana kuthibitishwa na tume ya uchaguzi.

  7. Dkt.John Nkengasong: Kupiga marufuku safari za ndege hakutadhibiti Covid-19

    Dkt. John Nkengasong

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mkuu wa wakala anayeshughulikia janga la virusi vya corona Afrika anasema kuweka vizuizi kama vile kupiga marufuku safari za ndege hakuna uwezekano wa kupunguza kuenea kwa virusi vipya.

    "Vikwazo vinavyowekwa kila mara hufanya iwe vigumu kushughulikia janga hilo,"

    Dkt. John Nkengasong, Mkurugenzi wa Vituo vya Afrika vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa, aliiambia BBC Newsday.

    "Haisaidii... haijawahi kusaidia kupunguza kuenea kwa janga la corona," anasema, akimaanisha uamuzi wa Uingereza kusimamisha safari za ndege kutoka nchi sita za kusini mwa Afrika.

    Anapendekeza kufuata hatua za afya ya umma kama vile kuvaa barakoa, haswa kwenye mikusanyiko wakati wa sherehe za msimu wa baridi, na kunawa mikono.

    "Epuka mikusanyiko ya watu na utekeleze hatua za kimsingi za afya ya umma na kijamii ambazo zinafaa dhidi ya anuwai zote. Nadhani hiyo ndiyo tunapaswa kuidumisha." Alisema.

  8. WHO yaitisha kikao cha dharura leo kujadili kirusi kipya cha Corona cha Afrika Kusini

    Corona

    Chanzo cha picha, AFP

    Shirika la Afya Duniani (WHO) linatazamiwa kufanya mkutano maalum leo Ijumaa kuhusu aina mpya ya virusi vinavyoenea kwa kasi nchini Afrika Kusini.

    Wataalamu huko Geneva wataamua ikiwa kuna haja ya kuweka mkazo kuhusu wasiwasi wa virusi hivyo. Afisa mkuu wa WHO alisema inaweza kuchukua mpaka wiki kubaini ikiwa idadi kubwa ya mabadiliko ya chembe za urithi za kirusi hicho ina athari kwa ufanisi wa chanjo zilizopo.

    Hilo linakuja wakati Uingereza imeweka marufuku ya muda kwa safari zote za ndege kutoka Afrika Kusini na nchi tano jirani. Hakuna visa vilivyogunduliwa nchini Uingereza. Wataalamu wa Afrika Kusini wanasema kirusi hicho kipya kimeenea kwa kasi miongoni mwa wanafunzi mjini Pretoria.

  9. Tangazo la mavazi chuoni lazua 'balaa' Kenya

    CUK

    Chanzo cha picha, CUK

    Chuo kikuu kimoja nchini Kenya kimeshutumiwa kufuatia tangazo lake chuoni hapo linalohusisha ubakaji na uvaaji wa mavazi yasiyo ya heshima.

    Tangazo lililowekwa katika lango kuu la Chuo Kikuu cha Ushirika cha Kenya linaonyesha kanuni ya mavazi inayokubalika - na mifano ya wanawake wanaovaa mavazi kama hayo.

    Ujumbe mmoja kwenye bango hilo unasema kuwa "mavazi yasiyofaa husababisha unyanyasaji wa kijinsia na ubakaji". Baadhi ya Wakenya kwenye Twitter wameonekana kuwa na mtazamo tofauti na taasisi hiyo:

    Ruka X ujumbe, 1
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 1

    Ruka X ujumbe, 2
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 2

    Ruka X ujumbe, 3
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 3

    Chuo chenyewe hakijazungumzia bado ukosoaji huo.

  10. Watu 43 wauawa katika mapigano ya kikabila Sudan

    Darfur

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Tangu mizozo ya wenyewe kwa wenyewe itamalaki kuanzia mwaka 2003 zaidi ya watu 300,000 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya milioni 2 walilazimika kuyakimbia makazi yao huko, Darfur, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

    Umoja wa Mataifa umethibitisha kuwa katika siku kadhaa za mapigano ya jamii katika jimbo la Darfur nchini Sudan yamesababisha takriban watu 43 kupoteza maisha na maelfu kuyahama makazi yao.

    Mzozo huo ulizuka wiki iliyopita kati ya wafugaji wahamaji wa Kiarabu na wakulima kutoka kabila la Misseriya Jebel, huko Jebel Moon, magharibi mwa Darfur.

    Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya vijiji 40 vilichomwa moto na kuporwa katika mapigano hayo.

    Watu kadhaa wameripotiwa kupotea wakiwemo watoto.

    Kumekuwa na milipuko ya mara kwa mara ya ghasia huko Darfur tangu kusainiwa kwa mkataba wa amani mwishoni mwa mwaka jana ambao ulisababisha kuondolewa kwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa.

  11. 52 wafariki kwenye ajali ya mgodi wa makaa ya mawe Urusi

    Mawe

    Chanzo cha picha, AFP

    Takriban watu 52 wameripotiwa kufariki katika maafa mabaya zaidi kuwahi kutokea kwenye shughuli za uchimbaji madini nchini Urusi kwenye kipindi cha muongo mmoja uliopita.

    Tukio hilo lilianza wakati vumbi la makaa ya mawe kwenye shimo la uingizaji hewa kushika moto siku ya Alhamisi, na kusababisha moshi mkubwa kwenye mgodi wa Siberia na kuua watu 11.

    Kufikia usiku, operesheni iliyoshindwa ya kuwafikia wachimba migodi kadhaa waliotoweka iligeuka kuwa janga baada ya waokoaji kadhaa kuripotiwa kukosa hewa.

    Chanzo cha huduma za dharura kiliambia shirika moja la habari kwamba "hakuna aliyeachwa hai".

    Wengi wa watu 285 katika mgodi wa Listvyazhnaya, katika eneo la Kemerovo kilomita 3,500 (maili 2,175) mashariki mwa Moscow, walitoroka baada ya tukio hilo.

    Maafisa walisema majeruhi 49 wamefikishwa hospitalini kwa matibabu. Baadhi yao wana sumu ya moshi, na wanne wanasemekana kuwa katika hali mbaya.

    Makumi ya wachimba migodi hawakuweza kukimbia baada ya tukio la awali, lakini shughuli za uokoaji zililazimika kusitishwa baada ya kiwango cha hatari cha methane kugunduliwa kwenye mgodi huo, na hivyo kusababisha hofu ya kutokea kwa milipuko.

    Moja ya timu ya uokoaji ilishindwa kutoka mgodini. Miili ya waokoaji watatu ilipatikana baadaye, na kufanya idadi rasmi ya waliokufa kufikia 14.

    Siku ya Alhamisi, vyanzo kadhaa viliambia vyombo vya habari vya Urusi kwamba hakuna manusura zaidi waliotarajiwa kupatikana na idadi ya vifo imeongezeka hadi zaidi ya 50, wakiwemo waokoaji sita kwa jumla.

  12. Maelfu waandamana Sudan kupinga uongozi wa kijeshi

    Sudan

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelfu ya watu katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum na miji mingine wameandamana kushinikiza viongozi wa kijeshi wa nchi hiyo kuachia mamlaka kwa utawala wa kiraia.

    Katika mji wa Omdurman, vikosi vya usalama viliwarushia gesi ya kutoa machozi waandamanaji waliokuwa wakipinga mapinduzi ya mwezi uliopita.

    Waandamanaji walikuwa wamekusanyika kutoa heshima za mwisho kwa makumi ya wenzao waliouawa na vikosi vya usalama vya Sudan katika wiki za hivi karibuni.

    Waandamanaji hao pia walishutumu makubaliano ya hivi karibuni ya jeshi ambayo yalishuhudia Waziri Mkuu Abdalla Hamdok akirejeshwa kwenye wadhifa wake.

    Vyama vikubwa vya siasa na vuguvugu la waandamanaji wenye nguvu nchini Sudan wamepinga uamuzi wa Bw Hamdok kutia saini mkataba huo na jeshi.

    Wengine wametaja kuwa ni usaliti au ni kuficha mapinduzi ya kijeshi kwa koti la kisiasa.