Obasanjo: Sijakataliwa kama mpatanishi wa Ethiopia
"Waziri Mkuu [Abiy Ahmed] amenipa kila usikivu nilioomba. Amenionyesha adabu ya hali ya juu"
Moja kwa moja
Lizzy Masinga
Obasanjo: Sijakataliwa kama mpatanishi wa Ethiopia

Chanzo cha picha, AFP
Rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo, amekana uvumi kwamba hakukaribishwa nchini Ethiopia kama mpatanishi wa mgogoro huko.
"Hakuna aliyekataa upatanishi wangu," Bw Obasanjo aliambia redio ya BBC Focus on Africa kutoka Ethiopia ambako amekuwa akikutana na watu kutoka pande zote mbili za mzozo katika jukumu lake kama mjumbe wa Umoja wa Afrika.
"Waziri Mkuu [Abiy Ahmed] amenipa kila usikivu nilioomba. Amenionyesha adabu ya hali ya juu ."
Kisha, akizungumzia safari yake ya Jumapili katika mji mkuu wa jimbo la Tigray, Mekelle, Bw Obasanjo alisema: "Rais wa Tigray... alinipokea jinsi ningepokelewa na kiongozi wa Kiafrika... kwa hiyo wazo la kukwepa na kutonipokea na yote hayo sio sahihi."
"Kila mtu anasema: 'Angalia, tunashukuru kwa kuteuliwa. Tunajua hii ndiyo njia ya kufuata. Tunataka mtu ambaye ni mwaminifu... na hatuwezi kupata mtu yeyote bora kuliko wewe."
Lakini vipi kuhusu mazungumzo ya kumaliza mzozo wa mwaka mzima ambao umewaacha mamilioni ya watu wakihitaji sana msaada wa chakula?
Rais wa zamani wa Nigeria hakulizungumzia hili.
Alisema katika hatua hii "anajaribu kujua ni masuala gani yenye umuhimu kwa makundi mbalimbali" kabla ya kuzungumzia mada ya mazungumzo.
Msemaji wa chama cha Tigray People's Liberation Front Getachew Reda alituma picha ya Bw Obansanjo akiwa na kiongozi wa TPLF Debretsion Gebremichael, akisema majadiliano hayo yalikuwa "yenye ufanisi"
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Jumbe za mitandao ya kijamii zinafuatiliwa kwa wanaokwepa kodi - ripoti

Chanzo cha picha, Reuters
Watu wanaoonyesha utajiri wao kwenye mitandao ya kijamii wanaangaliwa kwa karibu na mamlaka ya utozaji ushuru nchini kenya , gazeti la Nation nchini humo linaripoti.
Machapisho yanayoonyesha magari ya kifahari, nyumba za kifahari na karamu za kifahari hufuatiliwa mara kwa mara na maafisa wa Mamlaka ya Ushuru ya Kenya wakiangalia uwezekano wa udanganyifu wa kodi, alionya Kamishna Mkuu wake Githii Mburu.
Mamlaka zinasema wale watakaobainika kukwepa kodi zao wapo katika hatari ya kupigwa marufuku kusafiri, kutozwa ushuru ambao haujalipwa kutoka kwa akaunti zao za benki, na kufunguliwa mashtaka.
Wanawake watakiwa kutotumika kwenye matangazo ya biashara Pakistan

Chanzo cha picha, Reuters
Mshauri wa Waziri mkuu wa Pakistan amehoji ni kwanini picha za wanawake bado zinatumiwa kunadi bidhaa zao za kiashara licha ya kwamba kuna wanaume wenye sura nzuri wanaoweza kunadiwa.
Tahir Ashrafi, mshauri wa Waziri mkuu Imran Khan wa masuala ya dini, amesema wanawake hawapaswi kutumia kutangaza biashara.
Amewaambia waandishi wa habari katika mji wa Lahore kwamba haungi mkono tabia hiyo.
Maulana Ashrafi pia amezungumzia kuhusu ongezeko la uhalifu wa kingono nchini Pakistan.
Amesema hukumu kali zaidi zitatolewa kwa wahusika, akisema waalimu wana jukumu katika kumaliza ponografia nchini
Ecowas yawawekea vikwazo viongozi wa Mali

Chanzo cha picha, AFP
Viongozi wa jumuiya ya kiuchumi yan chi zilizoko magharibi mwa Afrika ECOWAS, ECOWAS, wameweka vikwazao dhidi ya wajumbe wa serikali ya mpito ya Mali na familia zao.
Vikwazo hivyo ni pamoja na marufuku ya kusafiri pamoja na kufujwa kwa mali zao.
Hatua hiyo inafuatia kushindwa kwa viongozi hao kufuata ratiba ya kurejesha utawala wa kiraia kufikia mwezi wa Februari mwaka ujao.
Katika mkutano maalum mjini Accra, Ghana, Viongozi wa mataifa ya Afrika Magharibi wametoa wito kwa jamii ya kimataifa kutekeleza vikwazo hivyo.
Ecowas itachukua hatua zaidi mwezi ujao kama hapatakuwa na hatua zozote za utekelezwaji ya raiba hiyo zitakazochukuliwa na viongozi wa serikali ya mpito ya Mali
Mapinduzi yamefanyika mara mbili katika kipindi cha mwaka mmoja, huku nchi hiyo ikikabiliwa na uasi unaoelendelea kuongezeka.
Obama anasema "Marekani imerejea" katika mapambano ya mabadiliko ya tabia nchi

Chanzo cha picha, PA MEDIA
Anasema baraza la Congress limepitisha muswada miundo mbili wa Biden uliokubaliwa na pande mbili za kisiasa, ambao anasema utabuni kazi sisizokuwa na uchafuzi wa hali ya hewa na kuongeza kuwa ana imani kwamba toleo hilo la muswada bora litaidhinishwa katika kipindi cha wiki mbili zijazo.
Anasema hilo litaiweka Marekani katika utayari wa kufanikiwa malengo yake ya kufikia asilimia 50-52 ya punguzo la gesi chafu kufikia mwaka 2030.
Na anasema kwamba Marekani sio nchi pekee iliyochukua hatua za ujasiri , huku akielezea ahadi zilizotolewa na Uingereza, Muungano wa Ulaya, Korea Kusini na Canada.
Obama anasema kwamba makubaliano ya Paris yalionyesha kuwa inawezekana nakazi muhimu imefanyika katika Glasgow pia.
Lakini anasema "tuko bado mbali sana na kule tunakotaka kuwa".
Unaweza pia kusoma:
- Mabadiliko ya tabia nchi: Nchi masikini zaidi duniani zinataka nini kutoka katika mkutano wa mabadiliko yatabia nchi wa Glasgow ?
- Mabadiliko ya tabia nchi yataleta mzozo wa kimataifa, ripoti ya kiintelijensia ya Marekani inasema
- Cop 26: Wanaharakati vijana kutoka Afrika wataka dunia ifanye maamuzi sahihi
Astroworld: Travis Scott na Drake washtakiwa kuhusu mkanyagano mkubwa katika tamasha la muziki

Chanzo cha picha, Getty Images
Rapa wa Marekani Travis Scott anakabiliwa na hatua za kisheria baada ya takriban watu wanane kuuawa na mamia kujeruhiwa kwenye mkanyagano kwenye tamasha lake la Texas Astroworld.
Mshiriki mmoja aliyejeruhiwa amemshutumu Scott na mtumbuizaji wa kushtukiza Drake kwa kuchochea umati, na anadai kulipwa $1m (£741,000) kama fidia.
Wote wawili hawajatoa tamko kuhusu kesi hiyo.
Katika taarifa kufuatia tukio hilo , Scott alisema alikuwa akichukua hatua kusaidia familia za wahasiriwa - mdogo zaidi ambaye alikuwa na umri wa miaka 14 tu.
Wakati huo huo, risala zimetolewa kwenye mitandao ya kijamii kwa waliouawa.
"Kucheza dansi ilikuwa ni tamanio lake na sasa anacheza akielekea kwenye malango ya mbinguni," familia ya Brianna Rodriguez mwenye umri wa miaka 16 ilisema katika taarifa.
Benki ya Dunia yafanya tathmini maandalizi ya Tanzania ya Kidijitali
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Aboubakar Famau
- Nafasi, BBC News, Dodoma

Serikali ya Tanzania hii leo imekutana na ujumbe wa Benki ya Dunia kwa lengo la kufanya tathimini ya maandalizi ya uboreshwaji wa mifumo ya Elimu Teknologia Habari na Mawasiliano-Tehama.
Mkutano huu unafuatia makubaliano ya mwezi wa nane mwaka huu ambapo Benki ya Dunia iliipa Tanzania kiasi cha fedha bilioni 349 ambazo ni sawa na dola milioni 150 za kimarekani. Lengo la fedha hizo ni kufanya maboresho ya minara ya simu ipatayo 488 nchi nzima, pamoja na kujenga mengine mipya zaidi ya 300.
Iwapo uboreshwaji huu utafanyika kwa kipindi cha miaka mitano kuanza sasa, utasaidia ufanisi wa upatikanaji wa mtandao kwa wananchi wa mijini na vijijini. Vilevile, itaongeza kasi ya upatikanaji wa mtandao kutoka teknolojia ya 2G mpaka teknolojia wezeshi ya 3G.
Akizungumza mara tu baada ya kukutana na ujumbe huo, muhandisi Mathew Kundo ambae ni Naibu Waziri Mawasiliano ameihakikishia Benki ya Dunia kwamba fedha walizokopeshwa zitatumika katika malengo yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake, Honest Njau ambae ni mratibu wa mradi wa Tanzania ya Kidigitali, amesema mradi huo ni mradi wa kimapinduzi ambao umegawanyika katika sehemu tatu.
‘Mradi huu ni mradi wa kimapinduzi. Ni mradi ambao unaenda kuleta mapinduzi upande wa Tehama. Umegawanyika katika sehemu tatu. Sehemu ya kwanza inaangalia mazingira wezeshi kwa ajili ya kuratibu matumizi ya Tehama, vile vile inaangalia maeneo ya biashara mtandao, anuani za makazi, na kuboresha au kupeleka huduma mbalimbali za serikali. Sehemu ya pili tunaangalia maunganisho ambapo tunaenda kuweka misingi kwa ajili ya kufikisha huduma. Vile vile tunaenda kuangalia mawasiliano ya simu.”
Serikali ya Tanzania kwa muda mrefu imekuwa ikitilia mkazo ukuaji wa TEHAMA kwa kusema kuwa imerahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii.
Akizungumza mwezi jana katika kilele cha Mbio za Mwenge, huko wilayani Chato, Mkoani Geita, rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali inatarajia kujenga chuo cha kisasa cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ili kuongeza kasi, ubunifu na ufanisi katika matumizi ya TEHAMA.
Oscar Pistorius kuachiwa kwa msamaha

Chanzo cha picha, AFP
Mwanamichezo aliyekutwa na hatia na nyota wa zamani wa olimpiki ya walemavu Oscar Pistorius anapaswa kuachiwa huru kwa msamaha baada ya kuhukumiwa kwa mauaji ya mpenzi wake Reeva Steenkamp mwaka 2013.
Hilo ni kutokana na kutumikia nusu ya muda wa kifungo chake.
Lakini kabla ya msamaha huyo atapaswa kushiriki katika programu ya ''mazungumzo ya waathiriwa''-maafisa wameiambia BBC.
Mpango huo ni sehemu ya mpango wa kurejesha haki nchini -ambao unafanya kazi ya kuwaunganisha tena wakosaji katika jamii zao.
Pistorius ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 13 na miezi 5 kwa mauaji ya mwanamitindo Reeva Steenkamp - anatumikia kifungo chake katika gereza moja mjini Pretoria.
Bodi ya parole itaamua iwapo itaruhusu kuachiliwa kwa Pistorius mapema.
Kabla ya hilo kutokea - yeye na familia ya Reeva Steenkamp watakutana mara kadhaa ili kujua miongoni mwa mambo mengine - kwamba amerekebishwa.
Mchakato huo utaongozwa na timu ya wataalamu wakiwemo wanasaikolojia.
Maafisa wanasema hii inaweza kuchukua miezi au hata miaka kukamilika. Iwapo ataachiliwa atatumikia kifungo chake kilichosalia nyumbani na atahitaji kuripoti kwa maafisa wa magereza mara kwa mara.
Mawakili kutoka Rwanda, Burundi wazuiwa kuhudumu Kenya
Bunge la Kenya limewazuia mawakili wa Rwanda na Burundi kufanya kazi zao nchini Kenya hadi mawakili wa nchi hiyo waruhusiwe kufanya kazi katika nchi hizo mbili kwa misingi ya maelewano.
Kamati ya Bunge ya Kitaifa ya Haki na Masuala ya Kisheria inataka nchi zote wanachama wa Afrika Mashariki kushughulikia suala hilo kabla ya Kenya kufungua biashara ya huduma za kisheria kwa Rwanda, Burundi na Sudan Kusini.
Wanasheria wa Tanzania na Uganda kwa sasa wanaruhusiwa kufanya kazi za sheria nchini Kenya kwa mujibu wa vifungu vya 12 na 13 vya Sheria ya Mawakili.
Mawakili 13 wa Kenya ambao kwa sasa ni mawakili wa Chama cha Wanasheria wa Rwanda (RBA) wameliomba Bunge kuharakisha kuingizwa kwa Rwanda na Burundi katika Sheria ya Mawakili ili kumwezesha Jaji Mkuu kuwaapisha na kuwaandikisha mawakili wa nchi hizo mbili kufanya kazi nchini Kenya.
Waasi wavamia vijiji vya Chanzu,Runyoni, wakazi wakimbia makazi yao DRC

Chanzo cha picha, social Media
Kundi lisilojulikana lenye silaha limeshambulia vijiji vya mashariki mwa jimbo la Kivu kaskazini mwa DR Congo karibu na mpaka na Uganda na kusababisha mamia ya raia kuyaacha makazi yao.
Wenyeji wanasema kuwa washambuliaji waliwakimbiza idadi ndogo ya jeshi la taifa ili kukalia Chanzu, Runyoni, Ndiza, na vijiji zaidi katika eneo la Rutshuru.
Shirika la kiraia huko Rutshuru linashuku waasi wa M23 ambalo mnamo 2013 lilitia saini makubaliano na serikali ya kuwaondoa na kumaliza uasi, halijasema chochote kuhusu shambulio hilo.
Mamia wamefunga mpaka wa Bunagana wa nchi hiyo na Uganda asubuhi ya leo'', Bw. Ayobangira Safari mbunge wa mkoa huo ameiambia BBC Idhaa ya maziwa makuu.
Vijiji vilivyoshambuliwa "vilikuwa ngome ya waasi wa M23 kabla ya kushindwa vita na jeshi " na kuhamishwa, mbunge huyo alisema.
Wiki iliyopita waasi walishambulia na kuudhibiti mji wa Bukavu Kusini kwa saa kadhaa.
Wajumbe watembelea Tigray kujadili mgogoro - Ripoti
Mkuu wa misaada wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths na mjumbe wa Umoja wa Afrika katika Pembe ya Afrika, Olusegun Obasanjo, walitembelea eneo la kaskazini la Tigray nchini Ethiopia siku ya Jumapili kujadili upatikanaji wa misaada ya kibinadamu na uwezekano wa kusitishwa kwa mapigano katika mzozo huo uliodumu kwa mwaka mzima.
Bw Griffiths na Bw Obasanjo, rais wa zamani wa Nigeria, walikuwa katika mji mkuu wa eneo la Mekelle kwa wakati mmoja, kwa mujibu wa ripoti.
Hatahivyo, haijulikani ikiwa wawili hao walikuwa kwenye safari moja. Televisheni ya Tigray iliripoti kwamba wawili hao walikutana na "rais wa serikali ya Tigray, Dk Debretsion Gebremichael" katika ofisi yake kwa ajili ya mazungumzo juu ya "mgogoro nchini Ethiopia na njia za kutoa misaada ya kibinadamu na masuala ya kikanda".
Ilisema Bw Griffiths na Bw Obasanjo baadaye walirejea Addis Ababa. Msemaji wa Umoja wa Mataifa alinukuliwa na shirika la habari la AFP akisema kuwa Bw Griffiths alikutana na "mamlaka zisizo na ukweli" za Tigray na kusisitiza "haja ya upatikanaji wa huduma za kibinadamu na ulinzi wa raia kupitia maeneo yote chini ya udhibiti wao".
Msemaji wa TPLF, Getachew Reda, alichapisha picha kwenye ukurasa wa twitter inayoonesha mkutano kati ya Bw Obasanjo na viongozi wa TPLF.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Google yasheherekea kuzaliwa kwa mwanzilishi wa masomo ya lugha za ishara barani Afrika.

Chanzo cha picha, Google
Tovuti ya google leo imeadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa na kutimiza miaka 71 ya alieyekuwa profesa na mwandishi mashuhuri nchini Kenya Okoth Okombo kwa kuweka picha yake kama nembo katika ukurasa wa mbele wa google (Doodle)
Profesa Okoth Okombo, ambaye ametoa zaidi ya machapisho 30 kuhusu Muundo na misamiati ya lugha za watu wasiosikia (Viziwi), anatajwa kama mwanzilishi wa masomo ya lugha za ishara barani Afrika.
Katika maisha yake Okombo, alifanya kazi kwa bidi ili kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu wa kusikia (Viziwi) na anatambuliwa kimataifa kama mmoja wa viongozi wasomi wa lugha ya ishara duniani.
Okombo alifanya utafiti kuhusu lugha ya ishara kenya (Kenyan Sign Language) mwaka 1991, Utafiti uliosababisha kupitishwa kwa matumizi ya lugha ya ishara nchini Kenya na kuruhusu jumuiya ya viziwi kupata fursa mpya katika jamii.
Kwa mafanikio yake, Shirikisho la viziwi ulimwenguni (World Federation of the Deaf) lilimchagua Okombo kuwa rais wa shirikisho hilo kimataifa kuanzia mwaka 1992 hadi 1995.
Msanii wa Kenya Joe Impressions ndiye aliyepata fursa ya kuchora picha hiyo anasema alifurahishwa kufanya kazi ya kuchora nembo hiyo ya Okombo iliyotumika katika ukurasa wa mbele wa kutafuta wa google
“Baada ya kufanya utafiti mtandaoni, nikafiria kuwa ni lazima nimuoneshe Profesa akifanya kile kilichomuunganisha na wanafunzi wake wengi zaidi na hicho ni kufundisha, nilitaka kupata kitendo muhimu ambacho unaweza kupata wakati wa kufundisha” alisema Impressions.
Okombo alifariki November 1mwaka 2017, katika Hospitali ya Aga Khan Hospital iliyopo Nairobi, Kenya alipokuwa akipatiwa matibabu.
Moto wachoma upande mmoja wa soko la Gikomba Nairobi

Maelezo ya picha, Soko la Gikomba Nairobi Moto umechoma upande mmoja wa soko la Gikomba jijini Nairobi na kuharibu mali ya thamani isiojulikana mapema Jumatatu.
Saa 48 kabla, wafanyabishara walipata pigo baada ya huduma ya jiji la Nairobi kupatiwa ruhusa na mahakama kuwaondoa baadhi ya wauzaji mitumba ili kutoa nafasi ya upanuzi wa kituo cha afya cha Pumwani Majengo Health Center.
Eneo la soko lililochomeka lilikuwa lile la mitumba ambapo wafanyabiashara wengi uhifadhi mali yao.
Wafanyabiashara waliowasili walikuwa tayari wamechelewa kuokoa mali yao huku ikiwa ni mabati yaliochomeka pekee ndio yaliosalia.
Gari la huduma ya Zima moto la jiji la Nairobi liliwasili katika eneo la tukio lakini moto huo tayari ulikuwa umesambaa kutokana na vibanda vya mbao vilivyotengenezwa .
Wanafunzi wawili kufikishwa mahakamani kwa shutuma za kuchoma moto shule Kenya

Wanafunzi wawili wa Shule ya sekondari ya Wasichana ya Buruburu nchini Kenya wanatazamiwa kufikishwa mahakamani Jumatatu kuhusiana na kisa cha moto katika shule hiyo kilichotokea wiki jana, na kusababisha wanafunzi 59 kulazwa hospitalini.
Wawili hao wanadaiwa kupanga na kuchoma moja ya matao mnamo Oktoba 31 kabla ya kutoroka na kuwaacha wenzao, Citizen Digital imeripoti
Katika kisa hicho, video za zilinasa wanafunzi wakiruka kutoka juu hadi ghorofa ya tatu kukimbia moto huo.
Wakati huo huo, Waziri wa Elimu George Magoha ameonya kwamba wanafunzi wote wanaohusika katika tukio la uchomaji shule watakabiliwa na mkono wa sheria.
Wanafunzi wa kidato cha nne na tatu wanatarajiwa kurejea shuleni Jumatatu huku wenzao wa kidato cha kwanza na cha pili wakitarajiwa kurejea siku ya Jumanne.
Kikao kati ya Bodi ya Menejimenti na Jumuiya ya Wazazi na Wa yalimu Alhamisi iliyopita kiliibuka na maazimio kadhaa ambayo ni pamoja na uwekaji wa kamera za CCTV shuleni hapo, milango ya kutokea ya dharura iliyofunguliwa moja kwa moja kwenda nje ili ifanye kazi na kukaguliwa mara kwa mara, taa ili kusakinishwa ili kuimarisha ulinzi na usalama.
Baadhi ya wazazi katika shule hiyo wamelalamikia uamuzi uliofikiwa na uongozi wa shule kuwataka wanafunzi wote kulipa shilingi 1,500 kwa uharibifu uliotokea wakati wa moto huo.
Je ushindi wa Westham dhidi ya Liverpool wikendi unaipa matumaini kushinda taji la ligi ya Premia?

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Mechi kati ya WestHam na Liverpool West Ham iliilaza Liverpool baada ya kupata ushindi mkubwa ambao uliwasaidia kupanda hadi nafasi ya tatu katika jedwali la ligi ya premia mbali na kutia doa matumaini ya klabu hiyo kushinda taji la ligi.
Liverpool ilianza mechi hii ikiwa na lengo la kuimarisha rekodi yake ya kutofungwa kufikia mechi 26, mbali na kupata ushindiambao ungewapeleka hadi katika katika nafasi ya pili wakiwa pointi moja nyuma ya viongozi Chelsea
Lakini walijipata nyuma mapema , wakati Alisson , akiwa chini ya shinikizo kutoka kwa Angelo Ogbonna, alipangua kona iliopigwa na Pablo Fornal na kujifunga.
Pande zote mbili baadaye ziliipuka kadi nyekundu katika kipindi cha kwanza huku Aaron Cresswell akimchezea visivyo Jordan Henderson kabla ya Ogbonna kupigwa kisukusuku na Diogo Jota – suala lililomfanya beki huyo wa Westham kutolewa nje.
Mechi hiyo ilikamilika huku West Ham wakiilaza Liverpool 3-2.
Na walipoulizwa iwapo wanaweza kushinda taji , walijibu
‘’Hatujui , ni mapema mno . lakini iwapo tutapigania ushindi katika kila mechi kama tulivyofanya hii leo kwanini tusiwe na ndoto ya kushinda’?
Kamanda wa kijeshi wa Sudan, Hemeti amuunga mkono kiongozi wa mapinduzi

Chanzo cha picha, Getty Images
Kamanda wa kijeshi wa Sudan, Mohamed Hamdan Dagalo, anayejulikana kwa jina la Hemeti, ameunga mkono hatua ya Jenerali Abdel Fattah al-Burhan kuchukua madaraka.
Hemeti, ambaye alikuwa naibu kiongozi katika Baraza la Utawala lililovunjwa sasa, alisema Jenerali Burhan "alikuja kusahihisha mwenendo wa mapinduzi, na kulinda usalama na utulivu wa nchi".
Maandamano ya kupinga mapinduzi hayo yamekuwa yakiendelea, ingawa ushiriki wa Jumapili uliripotiwa kuwa mdogo kwa sababu ya kukatika kwa mtandao.
Maafisa wa usalama waliwarushia vitoa machozi waandamanaji na baadhi ya walimu waliokuwa wakiandamana walizuiliwa.
Waandamanaji wanataka kukomeshwa kwa utawala wa kijeshi baada ya Jenerali Burhan kuvunja utawala kiraia wa serikali.
Viongozi wa Mali wawekewa vikwazo kutokana na kukwama kwa uchaguzi

Chanzo cha picha, AFP
Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za magharibi mwa Afrika, Ecowas imeweka vikwazo dhidi ya viongozi wa mpito wa Mali na familia zao.
Vikwazo vinaanzia marufuku ya kusafiri hadi kufungia mali zao za kifedha.
Hatua hii imekuja baada ya kushindwa kwao kuzingatia ratiba ya kurejesha nchi kwenye utawala wa kikatiba ifikapo Februari mwaka ujao.
Ecowas ilisema kuwa mamlaka ya Mali iliwafahamisha kuhusu kutoweza kwao kufikia makataa ya mpito ya kufanya uchaguzi.
Jumuiya hiyo ilikuwa imeondoa vikwazo vya kiuchumi vilivyowekewa nchi hiyo kutokana na mapinduzi ya mwaka jana baada ya jeshi kuahidi mchakato wa mpito wa miezi 18.
''Ecowas itazingatia vikwazo zaidi mwezi ujao ikiwa bado hakuna maendeleo kuelekea uchaguzi nchini Mali'', ilisema.
Mali imeshuhudia mapinduzi mara mbili tangu mwaka jana na iko katika mtego wa waasi wa kijihadi.
Waandamanaji warushiwa vitoa machozi Khartoum Sudan

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Maandamano Sudan Vikosi vya usalama nchini Sudan vimerusha vitoa machozi kwa waandamanaji ambao wanapigania demokrasia katika mji mkuu wa Khartoum.
Walimu waliokuwa wakishiriki katika mojawapo ya maandamano hayo walikamatwa na vikosi vya usalama.
Usiku kucha , waandamanaji waliweka vizuizi kwa siku mbili za kwanza za maandamano ili kupinga mapinduzi ya kijeshi ya mwezi uliopita.
Wanataka serikali ya kijeshi kujiuzulu na kuruhusu mabadiliko ya amani.
Maandamano hayo yanafanyika huku wapatanishi wa Muungano wa mataifa ya Kiarabu {Arab League} wakiwasili mjini Khartoum kwa mazungumzo ili kujaribu kusitisha tatizo hilo.
Waziri mkuu Abdalla Hamdok, bado amewekwa katika kifungo cha nyumbani na anakabiliwa na shinikizo kutoka kwa wanajeshi hao kushirikiana nao, mwandishi wa BBC Andrew Herding amesema kutoka mji huo mkuu.
Mwezi uliopita , kiongozi wa mapinduzi hayo Jenerali Abdel Fattah al – Burhan , alifutilia mbali utawala unaoongozwa na raia , kuwakamata viongozi wa kiraia na kutangaza hali hatari.
Habari...Karibu katika matangazo ya moja kwa moja ya kurasa ya BBC Swahili kupata taarifa za yanayojiri kutoka kila kona ya ulimwengu, leo ikiwa Jumatatu,Novema 08.

