Waziri mkuu wa Sudan aliyepinduliwa 'anaishi' katika nyumba ya kiongozi wa mapinduzi
Jenerali wa ngazi ya juu zaidi wa Sudan anasema jeshi lilichukua mamlaka Jumatatu ili kuepusha vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Moja kwa moja
Dinah Gahamanyi
Waziri mkuu wa Sudan aliyepinduliwa 'anaishi katika nyumba ‘ya kiongozi wa mapinduzi’

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Bw Hamdock hajaonekana tangu Jumapili Jenerali wa ngazi ya juu zaidi wa Sudan anasema jeshi lilichukua mamlaka Jumatatu ili kuepusha vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Jenerali Abdel Fattah al-Burhan alisema kuwa makundi ya kisiasa yalikuwa yamewachochea raia dhidi ya vikosi vya usalama.
Alisema kuwa amekuwa akimtunza Waziri mkuu aliyeondolewa madarakani , Abdalla Hamdok, ndani ya nyumba yake "kwa usalama wake" lakini kwamba atamrejesha nyumbani kwake Jumanne.
Maandamano yanaendelea kwa siku ya pili katika mji mkuu, Khartoum, huku barabara nyingi, madaraja na maduka vikiwa vimefungwa.
Mawasiliano ya simu na intaneti yamevurugika kwa kiasi kikubwa. Takriban watu kumi wameripotiwa kuuawa tangu ghasia zilipoanza.
Unaweza pia kusoma:
- Mapinduzi ya Sudan: Waandamanaji wauawa na makumi wengine kujeruhiwa
- Viongozi Sudan wakamatwa, huku kukiwa na ripoti za mapinduzi ya Kijeshi
Jeshi la Mali lamfukuza mjumbe wa ECOWAS

Chanzo cha picha, GHANA PRESIDENCY
Mali imemfukuza mjumbe maalumu wa Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za magharibi mwa Afrika (ECOWAS).
Taarifa iliyotolewa na serikali ya mpito ya kijeshi imesema: "Mienendo ya Hamidou Bolyhaikuambatana na kazi yake."
Serikali ya Mali imemshutumu mjumbe maalum ECOWAS kwa kushirikiana na makundi ya upinzani.
Kufukuzwa kwa mjumbe huyo kumekuja wakati serikali ya Mali ikikabiliwa na shinikizo kubwa kutoka kwa jamii ya kimataifa, ECOWAS ikiwemo, linaloitaka ikabidhi mamlaka kwa raia.
Hatahivyo, jeshi limesema kuwa litaendesha uchaguzi baada ya mkutano wa kitaifa, na kujadili matatizo ya kiusalama.
Waumini kumi na wanane wauawa katika shambulio la Msikiti Nigeria

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Polisi imesema mshambuliaji mmoja aliuawa Taarifa kutoka katika jimbo la Nigeria la Niger zinasema kuwa watu takriban 18 waliuawa Jumatatu baada ya watu wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki waliposhambulia Msikiti katika jamii ya Maza-Kuka.
Waumini wengine wengi walijeruhiwa.
Wanavijiji walisema kuwa kundi kubwa la washambuliaji liliuvamia Msikiti na kuwafyatulia risasi watu ambao walikuwa katika sala ya alfajiri.
Polisi wa eneo hilo wanasema mmoja wa washambuliaji aliuawa na vikosi vya usalama.
Tukio hilo ni la hivi tu karibuni katika jimbo la Niger ambalo limeshuhudia ongezeko la ghasia.
Tarehe 30 Mei majambaziwaliwateka nyara wanafunzi 136 katika shule ya Kiislamu katika mji wa Tegina.
Mwezi Februari, mamia ya watoto walitekwa nyara katika jimbo hilo.

Unaweza pia kutazama:
Maelezo ya video, Africa Eye: Watoto wa Nigeria wanaotekwa nyara Azma ya Zuma ya kumkataa mwendeshamashitaka katika kesi yake yakataliwa

Chanzo cha picha, EPA
Mahakama ya juu zaidi nchini Afrika Kusini imepuuzilia mbali ombi la rais wa zamani wa nchi hiyo Jacob Zuma la kutaka Mwendesha mashitaka mkuu katika kesi ya ufisadi dhidi yake aondolewe.
Katika ombilake Bw Zuma alikuwa amemshutumu mwendesha mashitaka huyo wa serikali kwa kuwa na upendeleo dhidi yake na kutoa kwa siri rekodi zake za kibinafisi za afya yake kwa vyombo vya habari – madai ambayo hayakuthibitishwa.
Bw Zuma alikuwa amekwepa kushitakiwa kwa karibu miongo miwili kuhusiana na mashitaka ya madai ya kupokea rushwa kutoka kwa kampuni ya silaha ya Ufaransa -Thales, iliyohusiana na mkataba wa silaha wa dola bilioni 2.
Rais huyo wa zamani anakabiliwa na mashitaka makubwa, ikiwa ni pamoja na ufisadi, rushwa, kukosa uaminifu katika mkataba wa abilioni ya fedha ya silaha.
Jaji alilalamika juu ya kucheleweshwa kwa mara kwa mara kwa kesi, akisema kuwa kwa maslahi ya haki sula hilo linapaswa kusikilizwa mapema iwezekanavyo.
Jopo la mawakili wa Bw Zuma limesema limeazimia kukata rufaa dhidi ya uamuzi uliotolewa na mahakama ya juu nchini humo.
Unaweza pia kusoma:
- Jacob Zuma: Rais wa zamani wa Afrika Kusini ambaye uongozi wake ulikumbwa na utata mwingi
- Jacob Zuma: Rais wa zamani wa Afrika Kusini ajisalimisha mwenyewe polisi
- Aliyekuwa Rais Afrika Kusini Jacob Zuma anakabiliwa na 'kosa la kuidharau mahakama '
Ethiopia yasema imefanya shambulio jipya la anga katika mji mkuu wa Tigray Mekelle

Maelezo ya picha, Vikosi vya Tigray Kulinga na taarifa kutoka ofisi ya mawasiliano ya serikali , kambi ya mazoezi iliyopo viungani mwa mji huo imelengwa na uvamizi huo uliofanyika Jumanne.
Televisheni ya Tigray, inayodhibitiwa na vikosi vya waasi, imethibitisha mashambulio hayo ya anga lakini haikusema iwapomadai ya serikali ya kuilenga kambi ya mazoezi yalikuwa ni sahihi.

Tangu wiki iliyopita, kumekuwa na mashambulio kadhaa ya anga katika mji huo pamoja na maeneo mengine ya magharibi na kaskazini mwa Tigray. Vikosi vya waasi vinaishutumu serikali kwa kuwalenga na kuwauwa raia huku ikishindwa katika mapambano. Lakini maafisa mjini Adis Ababa wanasema mashambulio yao yanalega wanajeshi.
Hii inakuja huku vita vikiendelea kuimarika baina ya serikali na waasi hususan katika jimbo jirani la Amhara ambako vikosi vya Tigray vinadhibiti maeneo muhimu.
Unaweza pia kusoma:
- Uchumi wa Ethiopia waathiriwa na mzozo wa Tigray
- Mzozo wa Tigray: Kufufuka kwa uasi kunamaanisha nini kwa Waziri Mkuu wa Ethiopia?
- Mzozo wa Tigray: Waziri Mkuu wa Ethiopia Ahmed Abiy akiri kuwa vikosi vya Eritrea viko ndani ya Tigray
Mlipuaji mabomu ya kujitoa muhanga ndiye aliyeshambulia basi Kampala

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, takriban mtu mmoja alifariki na wengine kadhaa walijeruhiwa katika lipuko Maafisa nchini Uganda wanasema kuwa mlipuaji bomu la kujitoa muhanga alisababisha mlipuko uliotokea kwenye basi, mjini Kampala Uganda Jumatatu.
"Mshambuliaji alikufa katika mlipuko huo ," alisema Msemaji wa polisi Fred Enanga Jumanne.
Aliongeza kuwa mshambuliaji huyo alikuwa katika ‘’orodha ya wanaotafutwa’’ na alikuwa mjumbe wa kikundi cha Kiislamu chenye uhusiano na Allied Democratic Forces (ADF), wanaoendesha harakati zao katika nchi jirani ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Wasafiri kadhaa walijeruhiwa katika mlipuko huo wa Jumatatu.
Jumamosi mlipuko mwingine ulitokea katika mgahawa mjini Kampala na kumuua mtu mmoja na kuwajeruhi wengine watatu.
Polisi ilisema kuwa kuwa mlipuko wa Jumamosi ulisababishwa na kifaa cha vilipuzi kilichokuwa na misumari pamoja na vipande vya vyuma, kilichokuwa kimefunikwa na mfuko wa plastiki.
Bw Enanga alisema kuwa wachunguzi walibaini kuwa kulikuwa na "uhusiano wa hali ya juu"baina ya mashambulio mawili.
"Kuna watu binafsi au makundi ya watu wanaoandaa hivi vilipuzi vya kutengenezwa ambao ni washirika wa makundi ya washambuliaji hao," Alisema Bw Enanga.
Klabu ya Simba yaridhia ombi la kuondoka kwa kocha Gomes

Chanzo cha picha, Simba Insatgram
Klabu ya Simba imesema kuwa imeridhia ombi la Kocha Mkuu, Didier Gomes da Rosa la kuachana na Simba kuanzia leo Jumanne.
Taarifa ya klabu hiyo imesema baada ya tathimini na majadiliano ya kina pande zote zimeafikiana kwa mujibu wa mkataba kwa manufaa ya wote.
Kutokana na hatua hiyo, aliyekuwa kocha msaidizi Thierry Hitimana, ndiye atakuwa kocha Mkuu wa Simba katika kipindi cha mpito akisaidiwa na Selemani Matola.
Aidha, Klabu pia imefanya mabadiliko madogo katika benchi la ufundi kwa kusitisha mikataba ya aliyekuwa kocha wa makipa, Milton Nienov na mwalimu wa viungo, Adel Zrane.
Mbowe apata jaji mpya
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Eagan Salla
- Nafasi, BBC Swahili, Dar es Salaam

Chanzo cha picha, NMG
Kesi inayomkabili kiongozi mkuu wa upinzani nchini Tanzania Freeman Mbowe na wenzake watatu imechua sura mpya baada ya kupata Jaji mpya
Jaji Joachim Tiganga amejitambulisha hii leo katika mahakama kuu divisheni ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi mbele ya washitakiwa na waendesha mashitaka.
Jaji Tiganga anakuwa Jaji wa tatu kusikiliza shauri hili.
Hii ni baada ya Jaji Kiongozi Mustapha Siyani aliyekuwa akisikiliza shauri hilo kuteuliwa kuwa Jaji kiongozi, na hivyo kuomba kujiweka kando kutokana na ongezeko la majukumu.
Jaji wa kwanza alikataliwa na upande wa washitakiwa kwa kile walichodai hawakuwa na imani naye.

Chanzo cha picha, CHADEMA
Maelezo ya picha, Bw mbowe anashitakiwa pamoja na watu wengine watatu Mbowe na wenzake watatu wana kabiliwa na tuhuma kadhaa ikiwa ni pamoja na ugaidi, kupanga njama za kuwadhuru viongozi wa serikali, rushwa na kuhujumu uchumi.
Tangu kushikiliwa kwa Mwenyekiti huyo wa CHADEMA zaidi ya miezi miwili iliyopita, kumekuwa na ukosoaji mkubwa juu ya tuhuma zinazomkabili, huku wakosoaji wa ndani na nje wakitafsiri hali hii kama ukandamizaji wa demokrasia.
Bw Mbowe alikamatwa alipokuwa akiendelea na makongamano ya kudai katiba mpya nchi nzima.
Unaweza pia kusoma:
- Freeman Mbowe: Polisi Tanzania wathibitisha mwenyekiti wa Chadema amefikishwa mahakamani leo
- Freeman Mbowe: LHRC, Amnesty International wataka Mbowe aachiwe na uhuru wa kisiasa uheshemiwe Tanzania
- Freeman Mbowe: Bingwa wa mikakati ya siasa za upinzani anayewanyima usingizi watawala
Maandamano yaendelea Sudan kwa siku ya pili baada ya mapinduzi

Chanzo cha picha, Reuters
Umati wa raia wa Sudan umeingia kwenye mitaa ya mji mkuu wa Sudan, Khartoum kufanya maandamano ya kupinga mapinduzi ya Jumatatu ya kijeshi.
Takriban watu 10 waliripotiwa kuuawa na wengine makumi kadhaa kujeruhiwa, wengi wao ikiwa ni kutokana na risasi zilizofyatuliwa na wanajeshi kwenye makundi ya waandamanaji.

Maelezo ya picha, Watu wengi wakikufa baada ya wanajeshi kufyatua risasi kwenye umati wa waandamanaji Kuna idadi kubwa ya wanajeshi waliopelekwa mitaani na wengine wamefunga mitaa inayounganisha mji huo na maeneo mengine ya nchi.
Unaweza pia kusoma:
- Mapinduzi ya Sudan: Waandamanaji wauawa na makumi wengine kujeruhiwa
- Viongozi Sudan wakamatwa, huku kukiwa na ripoti za mapinduzi ya Kijeshi
Bintimfalme wa Japan Mako aolewa na mpenzi wake wa kiume wa 'kawaida'

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Wawili hawa walizungumzia uhusiano wao katika mkutano na waandishi wa habari Jumanne Bintimfalme wa Japan Mako ameolewa na mpenzi wake aliyesoma naye chuo Kei Komuro – na hivyo kupoteza hadhi zake za Ufalme
Chini ya sheria ya Japan, mwana familia ya ufalme hunyang’anywa mamlaka na hadhi za kifalme anapoolewa na "mtu wa kawaida" ingawa wanafamilia wa kiume hawapotezi hadhi hizo.
Alivuka taratibu za kawaida za harusi ya kifalme na kukataa malipo ambayo kwa kawaida hutolewa kwa wanafamilia wa kike wanapoondoka kutoka familia hiyo.
Ni mjumbe wa kwanza wa familia ya ufalme huo wa Japan kukataa yote.
Wawili hao wanatarajia kuhamia nchini Marekani-ambako Bw Komuro anafanya kazi kama wakili-baada ya ndoa. Hatua hiyo imepelekea watu wengi kumlinganisha na wanafamilia ya ufalme wa Uigereza Meghan Markle na Mwanamfalme Harry, na kupewa majina bandia ya "Japan's Harry and Meghan".
Saw ana Bi Markle, Bw Komuro amekuwa akichunguzwa sana tangu uhusiano wake na Bi Muko ulipotangazwa. Hivi karibuni zaidi alikosolewa kwa kufuga nywele zake nyuma kama mwanamichezo aliporejea nchini Japan.
Watekaji wadai mamilioni ya pesa ili wawaachilie watu watatu waliotekwa kutoka Kanisani

Chanzo cha picha, FACEBOOK: OLATUNJI BLESSING
Wanakijiji wa Obada Oko katika eneo la Ewekoro katika jimbo la Ogun nchini Nigeria Jumapili walipigwa na butwaa baada ya watu wenye silaha kuvamia kanisa lililopo karibu na barabara na kuwateka nyara waumini watatu.
Kwa mujibu wa gazeti la Vanguard nchini humo, watu waliotekwa walijulikana kwa majina kama Alani-Bello, Adebare Oduntan na Mary Oliyide.
Watu hao walikuwa katika ibada ya usiku kabla ya ibada ya siku ya Sabato ambayo hufanyika Jumamosi kwa waumini wa thehebu la Wasabato(SDA), ndipo watu wenye silaha walipowavamia na kuwachukua.
Taarifa hiyo inasema, sasa watekaji wanadai kikombozi cha pesa za Nigeria au Naira milioni 6 kutoka kwa familia za mateka kabla ya kuwaachilia.
Akithibitisha tukio hilo, Msemaji wa polisi wa jimbo la, Abimbola Oyeyemi alisema kuwa kituo cha polisi kimewapeleka maafisa wakekusaidia kituo cha polisi cha Obada Ok ambako watu hao walitekwa.
Polisi imesema kuwa iliwaonya awali waumini kuacha maombi ya usiku katika maeneo yaliyoathiriwa na utekaji nyara, na kuwataka kuifahamisha polisi iwapo wangetaka kufanya hivyo ili wapewe usalama wa kutosha.
Serikali ya Tanzania yaazimia kuwachanja watu 100,000 kila siku

Serikali ya Tanzania imesema itatumia lugha za kikabila kutoa elimu ili kuhakikisha lengo la kutoa chanjo ya watu 100,000 kwa siku inatimia.
Chanjo zinazolengwa kwenye mpango huo ni dozi 1,065,000 za Sinopharm ambazo ziliingia nchini Oktoba 8, 2021 katika mpango wa msaada wa Covax.
Kabla ya dozi hizo, tayari Tanzania ilishapokea dozi 1,058,400 za chanjo ya Johnson & Johnson ambazo Katibu amesema kuwa zilishaisha.
Kauli hii imetolewa leo na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais -Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt Grace Magembe alipozungumza na BBC ambapo amesema uamuzi wa kushirikisha wadau mbalimbali ikiwemo viongozi wa kimila na kidini katika kutoa taarifa za uhamasishaji kuhusu uchanjwaji.
Dkt Grace ambaye anashughulikia masuala ya afya wizarani hapo amesema kuwa ushirikishwaji wa makundi mbalimbali yamekuwa na mchango mkubwa kwani jamii haswa vijijini wanazungumza zaidi ya lugha za kikabila licha ya Watanzania kuunganishwa na lugha ya Kiswahili.
“Zoezi la utoaji chanjo za Uviko 19 ulivyoanza ulikumbwa na changamoto kuu mbili, vituo vilikuwa 100 lakini sasa vipo 6000 kote nchini, na hii imerahisisha upatikanaji wa huduma sambamba na sasa watu kupitia lugha mama wanapata uelewa mzuri wa umuhimu wa chanjo.”
Kwa mujibu wa Dkt Grace, wamefanya utafiti katika mikoa ya Manyara na Arusha na kugundua kuwa kuna baadhi ya taasisi na vyombo vya habari wanapelekea elimu k akutumia lugha za asili na kuwafanya watu waelewe mapema zaidi.
Unaweza pia kusoma:
- Rais Samia Suluhu wa Tanzania apokea chanjo ya Corona
- Virusi vya Corona: Rais Samia Suluhu na Changamoto ya Corona na Chanjo
- Rais Samia Suluhu Hassan aruhusu balozi na taasisi kuingiza chanjo nchini humo
Marekani yatoa wito wa 'kurejea bila masharti ' kwa utawala wa kiraia Sudan
Waziri wa mambo yan je wa Mrakani Antony Blinken ametoa wito wa"urejeshwaji wa mara moja" wa utawala wa kiraia "bila masharti".
Jeshi la Sudan lilichukua mamlaka Jumatatu na wanajeshi wameripotiwa kuwauwa wata takriban saba na kuwajeruhi wengine 80 baada ya kufyatua risasi kwenye umati wa waandamanaji.
"Marekani inapinga kuvunjwa kwa serikali ya mpito Jumapili kulikofanywa a vikosi vya usalama ," alisema kwenye ujumbe wake wa Twitter:
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Marekani imezuia msaada wake wa moja kwa moja wa dola milioni 700 kwa serikali ya Sudan na inatoa wito wa kuachiliwa kwa viongozi wa kiraia wanaoshikiliwa – ambao miongoni mwao ni pamoja na Waziri Mkuu Abdalla Hamdok.
- Taarifa zaidi kuhusu mzozo wa Sudan:
- Mapinduzi ya Sudan: Waandamanaji wauawa na makumi wengine kujeruhiwa
- Viongozi Sudan wakamatwa, huku kukiwa na ripoti za mapinduzi ya KijeshiSudan: Je mapinduzi ya kijeshi yanaongezeka Afrika?
- Omar al-Bashir: Mapinduzi ya kijeshi yamng'oa mtawala baada ya maandamano
Watu 2 wafariki katika mlipuko wa basi la abiria Uganda

Chanzo cha picha, bbc/twitter
Maelezo ya picha, basi la abiria Kumekuwa na mlipuko ndani ya basi moja karibu na mji mkuu wa Uganda Kampala .
Maafisa wa polisi wamesema kwamba takriban watu wawili wamefariki , huku wengine kadhaa wakijeruhiwa.
Tukio hilo linajirisiku mbili baada ya bomu kulipuka ndani ya baa moja kaskazini mwa mji huo, na kumuua mtu mmojana kuwajeruhi wengine watatu.
Kwa mujibu wa mwanahabari wa BBC Patience Atuhaire haijulikani ni nini haswa kilichosababisha mlipuko huo.
Maafisa wa polisi walilizingira eneo hilo lililopo bararabani ili kuimarisha usalama.
Basi hilo lilidaiwa kusafiri katika barabara kuu ambayo inaelekea katika taifa jirani la Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Hatua hiyo inajiri huku maafisa wa polisi wakifanya uchunguzi kuhusu shambulio la Jumamosi katika mkahawa mmoja wa kampala.
Awali walikuwa wakisema kwamba kilikuwa kitendo cha ugaidi wa nchini humo , lakini kundi la Islamic State linasema lilihusika na mlipuko huo.
Uganda awali imelishutumu kundi la waasi la DRC,ADF kwa kupanga mashambulizi hayo.
Bilionea Jeff Bezos kujenga kituo cha 'kibiashara' angani

Chanzo cha picha, Blue Origin
Maelezo ya picha, Kituo cha kibiashara angani Blue Origin, kampuni inayosimamia utalii wa angani na inayomilikiwa na mwanzilishi wa kampuni ya Amazon Jeff Bezos , imetangaza mipango ya kuzindua kituo cha biashara cha angani.
Bezos alisema siku ya Jumatatu kwamba wanatumai kuendesha kituo hicho , kwa jina Orbital Reef kufikia mwisho wa muongo huu.
Nyenzo za ukuzaji zilizotolewa na kampuni hiyo zinadai kwamba kituo hicho kitachanganya mambo tofauti ya kibiasharana kitakuwa na hadi watu 10.
Kampuni hiyo itashirikiana na kituo cha angani cha Sierra na Boeing ili kujenga kituo hicho.
Blue Origin ilisema kwamba kituo hicho chenye ukubwa wa futi 32,000 zenye ujazokitawapatia wateja fursa ya kuzalisha filamu katika eneo hilo ama hata kufanya utafiti na anasema kwamba kitashirikisha hoteli ya angani.
Katika mkutano na wanahabari kuzindua mpango huo, maafisa wakuu wa Blue Originna kituo cha angani cha Sierra walikataa kutoa gharama ya ujenzi wa kituo hicho , ijapokuwa inadaiwa wanahakika kupata ufadhili wa kitita kikubwa kutoka kwa bwana Bezos, ambaye amejitolea kutumia $1bn (£726m) kwa mwaka katika kampuni ya Blue Origin.
Tangazo hilo linajiri huku Nasa ikitafuta mapendekezo ya kuunda kituo mbadala ili kuchukua mahala pake majengo ya kituo hicho yalio angani kwa miaka 20.
Natumai Hujambo na karibu katika taarifa zetu za moja kwa moja

