Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Mamia ya watu wajipanga wakiwa watupu ufukweni mwa bahari Israeli

Mamia ya watu wamejitoalea kuvua nguo zao na kubaki watupu ili wachorwe picha zinazoelezea namna Bahari ya kifo au Dead Sea inavyoendelea kunyauika

Moja kwa moja

Ambia Hirsi

  1. Rais Samia: Ziara zangu za kigeni zinazaa matunda

    Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametetea ziara zake nje ya taifa hilo tangu alipochukua madaraka mwezi Machi akisema kwamba ziara hizo zimekuwa zikiwafaidi Watanzania.

    Kulingana na gazeti la The Citizen Online, Rais Samia ametaja ziara yake nchini Kenya mnamo mwezi Mei akisema kwamba imeimarisha biashara kati ya nchi hizo mbili.

    Rais Samia alisema hayo nchini Tanzania wakati akihutubia mkusanyiko wa watu mjini Arusha ikiwa miongoni mwa ziara zake za kikazi katika eneo hilo.

    Kwa mujibu wa gazeti la The Citizen Tanzania, Samia ambaye alichukua mamlaka kutoka kwa mtangulizi wake John Pombe Magufuli mnamo tarehe 19 Machi mwaka huu kufuatia kifo cha Magufuli tarehe 17 mwezi Machi , alisafiri nchini Uganda mwezi Aprili ambapo alikutana na mwenzake wa taifa hilo Yoweri Mjuseveni pamoja na washikadau wengine katika mradi wa bomba la Mafuta.

    Mwezi Mei , alifanya ziara ya siku mbili nchini Kenya ambapo yeye na mwenzake wa Kenya rais Uhuru Kenyatta walizungumzia kuimarisha biashara kati ya mataifa hayo mawili.

    Mwezi huohuo, alifanya ziara ya siku moja nchini Uganda ili kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa rais Museveni kufuatia ushindi wake katika uchaguzi mkuu wa Uganda wa 2021.

    Mnamo mwezi Juni Rais Samia alielekea katika mji mkuu wa Msumbiji , Maputo kwa mkutano wa viongozi wa SADC ambapo walizungumzia kuhusu masuala ya ushirikiano na maendeleo.

    Mwezi Julai alielekea Burundi kuimarisha biashara kati ya mataifa hayo mawili. Mwezi Agosti alisafiri nchini Rwanda.

    Mwezi huohuo pia alielekea nchini Malawi ambapo alishiriki mkutano wa 41 wa SADC.

    Baadaye akaelekea Zambia kuhudhuria kuapishwa kwa rais Hakainde Hichilema baada ya kiongozi huyo kuibuka mshindi wa uchaguzimkuu.

    Mwezi Septemba , rais Samia alihudhuria mkutano wa 76 wa baraza la Umoja wa mataifa {Unga} mjini New York.

    ‘’Naambiwa kwamba kiwango cha biashara katika mpaka wa Namangaimeongezeka mara sita’’, alisema.

    Kulingana na EAC , bishara ambazo tanzania inauza Kenya zimefikia $167m katika kipindi cha miezi sita kufikia mwezi Juni mwaka huu.

  2. Watu wawili wanusurika baada ya siku kadhaa ndani ya eneo lisiloweza kufikika

    Polisi nchini imesema wawili hao walikuwa hawana maji mwilini na kuumia kutokana na mchoko lakini walikuwa sawa.

    Polisi nchini Ausralia inasema kuwa ‘’ni muujiza’’ kwa wawili hao kunusurika kwa siku kadhaa bila kunywa majibaada ya kupotea njia katika eno la kaskazini mwa Australia lisilokaliwa na watu.

    Mahesh Patrick, 14, na Shaun Emitja, 21, walipatikana wakiwa maeneo tofauti karibu na chemichemi za Alice mmoja Ijumaa na mweingine Jumamosi.

    Wote walikuwa hawana maji mwilini na waliumia sana kutokana na mchokolakini viginevyo walikuwa salama, polisi ilisema.

    Gari lao lilikwama kwenye matoke siku ya Jumatatu, wiki iliyopita wakati walipokuwa katika safari ya saa nne kupitia eneo lisilokaliwa na watu.

    Waliposhindwa kulivuta gari lao, walikaa ndani yake usiku mzima kabla ya kuondoka siku iliyofuata kutafuta maji ya kunywa.

    Iliwalazimu kutembea umbali wa kilomita 5 (maili 3.1) kwenye mlima kabla ya kugundua kuwa walikuwa wamepotea njia, walisema maafisa.

    "Walidhani walikuwa wanaelekea mwelekeo wa barabara yaSandover Highway," alisema polisi wa eneo la Kaskazini, akimaanisha barabara kuu moja inayoelekea kaskazini – hadi kusini inayopitia kwenye kanda.

    Waliripoti kupotea baada ya kushindwa kurejea siku ile katika Hermannsburg, wanakoishi jamii ya wazawa yapata kilomita 120(maili 7) kusini -magaharibi mwa chemichemi za Alice

    Wawili hao walipiga kambi kwenye mlima mmoja usiku mzima, ambako polisi wanaamini walipata chanzo cha maji na kuweza kunywa.

  3. Mamia ya watu wajipanga wakiwa watupu ufukweni mwa bahari Israeli

    Mamia ya watu wamejitoalea kuvua nguo zao na kubaki watupu ili wachorwe picha zinazoelezea namna Bahari ya Dead Sea inavyoendelea kunyauka.

    Watu hao wake kwa waume wapatao 300, walikuwa wamevaa nguo za ndani nyeupe na hivyo kuacha sehemu nyingine za mwili wao wazi ili kutoa fursa kwa mpiga picha Mmarekani Spencer Tunick, ambaye amefanya sanaa hiyo katika maeneo mengine ya fukwe za bahari duniani kama njia ya kuhamasisha watu kutunza bahari.

    Mpiga picha huyo amewahi kuendesha kampeni hiyo katika maeneo kama eneo la barafu la Uswiss na ufukwe wa Afrika Kusini. Upigaji picha huo ulihamasishwa na Wizara ya utalii ya Israeli.

    “Matembezi yangu nchini Israeli yamenipa uzoefu wa kipekee na ninafurahi wakati wote kurejea hapa na kupiga picha katika nchi pekee ya Mashariki ya Kati inayoruhusu sanaa ya aina hii,” alisema Tunick.

  4. Kiongozi wa upinzani ajitangaza mshindi wa uchaguzi wa Cape Verde

    Baada ya kupata chini ya asilimia 52 ya kura katika uchaguzi wa urais wa Jumapili nchini Cape Verde, mgombea wa upinzani Jose Maria Neves amejitangaza mshindi .

    Matokeo ya awali ambayo yametangazwa kutoka asilimia 99.4 ya vituo vya kupiga kura pia zilionesha hasimu wake mkuu, Carlos Alberta Veiga, amepata 42% ya kura.

    Bwana Veiga alikua mgombe wa chama cha rais anayeondoka was thetJorge Carlos Fonseca.

    Alikubali kushindwa katika mkutano na waandishi wa habari na kumpongeza Bw. Neves.

    Bw. Neves, 61, aliwai kuwa waziri mkuu kuanzia 2001 hadi 2016. Alikuwa mgombe wa cha kikubwa cha siasa cha African Party for the Independence of Cabo Verde (PAICV) nchini Cape Verde.

    Wakati wa kampeni alisema kuwa akichaguliwa, atashughulikia mgawanyiko unaoshuhudiwa nchini, kufufua uchumi na kusuluhisha mzozo wa afya ulisababishwa na janga la coronavirus.

    Katika hotuba yake ya kwanza rasmi baada ya uchaguzi, alisema atakuwa "rais wa raia wote wa Cape Verde".

    Aliambia BBC kwamba "amefurahishwa sana na ushindi wake".

    Wagomba saba walishiriki uchaguzi huo wa urais. Mshindi alihitajika kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura zilizopigwa ili kuepuka duru ya pili ya uchaguzi. Matokeo ya awali ya uchaguzi yanastahili kuidhinishwa na Tume ya Uchaguzi katika siku chache zijazo.

  5. Mashambulio ya angani yagonga mji mkuu wa Tigray - waasi na mashahidi

    Mashambulio ya angani yamefanywa dhidi ya mji mkuu wa jimbo la Tigray, Mekelle, kaskazini mwa Ethiopia, waasi na wakazi wameambia BBC.

    Vikosi vya muungano vimekua vikipikabiliana na wapiganaji wa Tigray People's Liberation Front (TPLF) kaskazini mwa nchi kwa karibu mwaka mmoja.

    Kindeya Geberehiwot, mwanachama wakamati kuu ya TPLF, ameambia BBC Tigrinya kwamba mashambulio ya Jumatatu asubuhi yalilenga sehemu mbili za mji huo.

    Shambulio la kwanza, lilitokea viungani mwa mji wa Mekelle, karibu saa 09:30 (06:30 GMT) ambapo raia watatu waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa, Bw. Kindeya alisema.

    Shambulio la pili lilitokea katika soko lenye shughuli nyingi ambapo makumi ya watu walijeruhiwa, aliongeza kusuma.

    Wakazi pia wameambia BBC kuhusu mashambulio hayo huku watumiaji wa mitandao ya kijamii wakishirikisha picha zinazoonesha uharibifu uliosababishwa.

  6. Mshukiwa wa mauaji wa mwanariadha ya Kenya afikishwa mahakamani

    Mpenzi wa mwanariadha wa Kenya Agnes Tirop, amefikishwa mahakamani kama mshukiwa wa mauaji.

    Hakimu amesema atawaruhusu polisi kumzuilia Ibrahim Rotich kwa siku 20, wakati ambao pia atafanyiwa uchunguzi wa kiakili kubaini ikiwa anaweza kufunguliwa mashtaka.

    Bw. Rotich alikamatwa wiki iliyopita mjini Mombasa pwani ya Kenya.

    Polisi wanasema alikuwa akijaribu kutorka nchini.

    Agnes Tirop alipatikana akiwa ameuawa kuwa kuchomwa kisu nyumbani kwake magharibi mwa Kenya.

  7. Olunga aendelea kung'aa katika Ligi ya Qatar

    Mchezaji soka wa kimataifa wa Kenya, Michael Olunga ameendeleza msururu wa ufungaji mabao katika Ligi ya Qatar baada ya kuiwezesha klabu yake Al Duhail kupata ushindi wa nyumbani.

    Mchambuliaji huyo alifunga 3-0 katika mechi ya Jumapili ya Al Duhail dhidi ya Al Rayyan iliyochezwa katika uwanja wa Thani Bin Jassim maarufu (Al-Gharafah Stadium).

    Olunga mwenye umri wa miaka 27 sasa amefunga mabao manane tangu msimu ulipoanza katika mechi tatu alizocheza.

  8. China yafanya jaribio la kombora kutoka angani

    China imefanyia majaribio kombora lake jipya lenye uwezo wa nyuklia kutoka angani, ripoti zinasema.

    Kulingana na gazeti la Financial Times, China ilifanya jaribio hilo mwezi Agosti lakini haikutaka kujulikana.

    Kulingana na ripoti hiyo, shirika la kijasusi la Marekani limeshangazwa na hatua iliyopigwa na China kiteknolojia.

    Kando na China kuna nchi zingine tatu ikiwemo Marekani, Urusi na Korea Kaskazini zinazofanyia kazi teknolojia ya hypersonic.

    Kama na makombora ya balistiki, makombora ya hypersonic yana vifaa vya nyuklia na yana uwezo wa kuyabeba.

    Kombora hili linaweza kuruka kwa kasi mara tano kuliko kasi ya sauti.

    Tofauti na makombora ya balistiki, makombora ya kusafiri kwa ndege huruka chini na polepole kuelekea shabaha yao.

  9. Mwanamke ajifungua watoto saba nchini Pakistan

    Mwanamke mmoja amejifungua watoto saba mjini Abbottabad huko Pakistan.

    "Mungu ametujaalia watoto wanne wa kiume na watatu wa kike. Tunafuraha sana."Alisema mume wake,Yar Mohammad

    Kulingana na vyanzo vya habari katika hospitali hiyo, hali ya watoto hao na mama yao imeimarika.

    Bw. Mohammed anasema uchunguzi wa awali ulipobaini mke wake amebeba watoto kadhaa tumboni walishauriwa waende hospitali kuu kwa uangaalizi wa karibu.

    Madaktari waliomhudumia walishangazwa sana na hali ya mwanamke huyo.

    Kulingana na Dkt Hina Fayaz, daktari bingwa wa wanawake katika Hospitali ya Jinnah huko Abbottabad, mwanamke huyo alikuja kwake kwa mara ya kwanza Jumamosi.

    Anasema, "Baada ya uchunguzi wa ultrasound na ripoti zingine, tuligundua kuwa ana watoto watano ndani ya tumbo lake na ujauzito wake ulikua zaidi ya miezi minane"

    Dk Hina Fayaz anasema kwamba alishtuka sana kuona ripoti ya matibabu ya mwanamke huyo.

    Madaktari waliomhudumia walishangazwa sana na hali ya mwanamke huyo.

    "Alikuwa na shinikizo la damu iliyotajwa kuwa ya kiwango hatari. Tumbo lake lilikuwa limevimba. Kabla ya hapo, alikuwa amejifungua na watoto wawili kwa nja ya upasuaji. Alikuwa na maumivu makali kwenye kovu la upasuaji wa kwanza.''

    Hata hivyo madaktari walifanikiwa kuwatenganisha watoto hao kabla ya kuwatoa tumboni.

    "Tulijitahidi sana kuhakikisha mama asipoteze damu nyingi wakatiwa kuwatenganisha."

    Watoto hao kwa sasa wanapewa uangalizi maalum.

    Baba yao anasema kuwatunza haitakuwa kazi ngumu kwa sababu anaishi na jamaa zake.

  10. Msaidizi wa karibu wa Rais wa Venezuela ashtakiwa Marekani

    Mmoja wa wasaidizi wa karibu wa Rais wa Venezuela Nicolás Maduro amesafirishwa kutoka Cape Verde kwenda Marekani, ambapo ameshtakiwa kwa utakatishaji fedha.

    Hazina ya Marekani inasema Alex Saab alifkuwa kiungo muhimu wa serikali ya Bwana Maduro.

    Serikali ya Venezuela imesitisha mazungumzo yake na mrengo na upinzani ambao unaungwa mkono na Marekani.

    Mazungumzo hayo yalikuwa ya kutatua mgogoro wa kisiasa ambao umesababisha vurugu na kuporomoka kwa uchumi.

    Majadiliano hayo yalipaswa kuanza tena wikendi hii huko Mexico.

    Marekani inamshutumu Bwana Saab - mfanyabiashara mzaliwa wa Colombia na mjumbe wa Venezuela - kwa kutumia akaunti zake katika benki za Marekani ili kupata mapato ya ufisadi.

  11. Abiy: Ethiopia lazima isimamishe msaada wa chakula ili kuepuka shinikizo

    Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed anasema nchi hiyo inahitaji kukoma kupokea msaada wa chakula ili kuepuka shinikizo za kigeni dhidi ya serikali, Kituo cha televisheni cha kinachomilikiwa na serikali ETV) kimeripoti.

    "Tukihakikisha vitu hivi vinavyoitwa ngano [msaada wa chakula] haviingii Ethiopia, asilimia 70 ya matatizo ya Ethiopia yatasuluhishwa.

    "Tatizo la Ethiopia ni msaasa wa ngano. Kutokana na msaaada wa ngano kunakuja magonjwa. Kutokana na masaada wa ngano kunakuja mambo mengi, athari nyingi. Tukisimamisha, baadhi ya matatizo yatasuluhishwa ," Bwana Abiy alisema.

    Waziri Mkuu alisema hayo alipozuru mashamba ya ngano katika eneo la Oromia.

    Ethiopia, ambayo ni miongoni mwa nchi ambazo zinapokea misaada ya kigeni, inakabiliwa na shinikizo kutoka kwa nchi kadhaa za magharibi kutokana mzozo wa Tigray kaskazini mwa nchi, ambako ambapo mamilioni wako katika hatari ya njaa.

  12. Misri kuwazuia wafanyikazi ambao hawajachanjwa kwenda kazini

    Misri itawazuia wafanyikazi wa umma ambao hawajachanjwa dhidi ya kuingia katika majengo ya serikali kutoka katikati ya mwezi ujao.

    Ilani ya baraza la mawaziri Jumapili ilisema wafanyikazi watalazimika kupewa chanjo au kufanyiwa vipimo vya Covid kila wiki ili waruhusiwe kuingia kwenye majengo ya serikali kutoka 15 Novemba.

    Baraza la mawaziri pia liliruhusu kufunguliwa kwa bafu katika misikiti kutoka Jumatano.

    Bafu zilifungwa mnamo Machi mwaka jana kama sehemu ya hatua za kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona Serikali pia imetenga pauni bilioni Moja za Misri ($ 64m; £ 47m) kushughulikia janga hilo.

    Misri imetoa chanjo zaidi ya milioni 30 kwa raia wake dhidi ya idadi ya watu zaidi ya milioni 100, kulingana na data kutoka kwa wizara yake ya afya.

  13. Mafuriko yasababisha vifo vya takriban watu 24 India

    Watu wasiopungua 24 wamefariki katika mafuriko kusini mwa India baada ya mvua kubwa kusababisha mito kufurika, kukata usafiri katika miji na vijiji.

    Watoto watano ni kati ya waliokufa.

    Kuna hofu idadi ya waliofariki inaweza kuongezeka zaidi kwani watu wengi hawajulikani waliko.

    Nyumba kadhaa zilisombwa na maji na watu walinaswa katika wilaya ya Kottayam katika jimbo la Kerala.

    Video kutoka eneo hilo ilionyesha abiria wa basi wakiokolewa baada ya gari lao kujaa maji ya mafuriko. Kottayam na Idukki ni wilaya mbili zilizoathirika zaidi katika jimbo hilo.

    Siku kadhaa za mvua kubwa pia zimesababisha maporomoko hatari ya ardhi.

  14. Waandamanaji wanadai mapinduzi ya kijeshi Sudan mgogoro ukizidi kuongezeka

    Wapinzani wa serikali ya mpito ya Sudan waliandamana katika barabaraza mji mkuu wa Khartoum Jumamosi kushinikiza jeshi kudhibiti nchi hiyo.

    Maelfu ya watu kadhaa walikusanyika nje ya ikulu ya rais huku mgogoro wa kisiasa ukiendelea kuongezeka.

    Jeshi na makundi ya kiraia yamekuwa yakigawana madaraka tangu Rais Omar al-Bashir alipong'olewa madarakani mwaka 2019.

    Tangu wakati huo, viongozi wa jeshi wamekuwa wakidai mageuzi ya Umoja wa Vikosi vya Uhuru na Mabadiliko (FFC), muungano wa raia ambao uliongoza maandamano ya kumpinga Bashir na kuunda sehemu muhimu ya serikali ya mpito.

    Vikosi vya wanajeshi pia vimetaka kubadilishwa kwa baraza la mawaziri.

    Hata hivyo, viongozi wa raia wanasema kuwa madai hayo ni njama ya kutaka kunyakua mamlaka kutoka kwa wanajeshi.

    "Tunahitaji serikali ya kijeshi, serikali ya sasa imeshindwa kutuletea haki na usawa," mwandamanaji mmoja aliiambia AFP.

    Tofauti na maandamano ya hapo awali nchini, waandamanaji waliruhusiwa kufika kwenye majengo ya ikulu ya rais na kulikuwa na polisi wachache.

    • Kiongozi wa baraza la kijeshi la mpito nchini Sudan ameapa ''kuung'oa utawala
    • Omar al-Bashir: Namna kiongozi mwenye mamlaka makubwa ya kijeshi alivyodumu mamlakani
    • Mapinduzi Mali: Je mapinduzi ya kijeshi yanaongezeka Afrika?
  15. Karibu katika matangazo ya moja kwa moja leo Jumatatu 18.10.2021