Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Chadema wafungua kesi kudai dhamana ya Hashim

Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimefungua kesi kudai kuachiliwa kwa dhamana kwa kiongozi wa baraza la wazee la chama hicho Hashim Issa Juma (63) ambaye anashilikiwa kwa siku ya nne sasa.

Moja kwa moja

Dinah Gahamanyi

  1. Mpaka hapo tumefikia tamati ya habari zetu za moja kwa moja kwa leo, tukutane kesho majaliwa

  2. Twiga mtoto kupewa jina la 'Njeri' huko Marekani kwaibua hisia mseto Kenya

    Hifadhi ya wanyama ya jiji la Oklahoma imesema imepata jina la twiga mtoto aliyezaliwa Septemba 15, mwaka huu.

    Kuanzia Oktoba 3, 2021 Hifadhi hiyo iliendesha shindano ya kusaka jina kwa ajili ya twiga huyo mtoto, aliyezaliwa na twiga mama anayeitwa Julu.

    Twiga huyo mtoto amepewa jina la Njeri, jina maarufu la kabila la wakikuyu nchini Kenya baada ya majina manne kushindanishwa na watu kupiga kura.

    Majina mengine yaliyopendekezwa yalikuwa ni Acacia kwa maana ya aina miti yenye asili ya Afrika anayookula twiga, Mosi jina la Kiswahili kwa maana ya mtoto wa kwanza na Najuma linalomaanisha furaha.

    Abdulshakur aliandika kwenye mtandao wake wa twitter kwamba huenda twiga huyo alitoka Kenya.

    Wengine wakakosoa tafrisi ya jina Njeri, wakisema tafsiri iliyotumika ya Njeri si sawa. Mtu anayejiita The Ecotraveller kwenye mtandao wake wa twitter alionyesha kuhoji maana ya jina hilo na mwingine Wanjoghi Githae alifafanua kuwa Njeri inaweza kumaanisha mtu anayependa kuzuru mahali.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Vyombo vya habari Marekani, jina la Njeria wamelitafsiri kama shujaa mpambanaji. Kwa mujibu wa wakenya, tafsiri isiyo rasmi ya Njeri ni mtu anayependa kufanya ziara, kuzuru ama kutembelea maeneo mbalimbali.Hata hivyo wakenya wameonekana kupokea kwa hisia tofauti wengine wakitaniana kupitia kitendho cha twiga kupewa jina la Kikenya.

    Twiga huyo Njeri ni wa pili kuzaliwa katika katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, wa kwanza kuzaliwa anaitwa Kioni, aliyezaliwa mwezi Juni na mama yake Julu, anayeitwa Ellie mwenye miaka 21.

  3. Waziri mkuu Abiy atangaza baraza lake jipya la mawaziri Ethiopia, watatu wapinzani

    Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ametangaza baraza lake jipya la mawaziri baada ya kuapishwa siku mbili zilizopita kufuatia ushindi wa chama chake kwenye uchaguzi mkuu wa utata wa mwezi Juni mwaka huu.

    Katika baraza hilo, Abiy ameteua wanasiasa watatu kutoka upinzani.

    Berhanu Nega – kiongozi wa chama cha ‘Ethiopian Citizens for Social Justice, ambaye ameshinda viti vichache katika uchaguzi huo ameteuliwa kuwa waziri wa elimu.

    Aliwahi kuanzisha kikundi cha waasi kilichopigwa marufuku, na umaarufu wake ulikuja kupitia uchaguzi tata uliomwaga damu wa mwaka 2005, wakati chama chake kilipofanikiwa kuzoa viti vingi isivyotarajiwa.

    Belete Molla – kiongozi wa NaMA – ameteuliwa kuwa waziri wa masuala ya teknolojia

    Kejela Merdasa – kutoka chama kilichowahi kupigwa marufuku cha Oromo Liberation Front (OLF) – ameteuliwa kushika nafasi ya waziri wa utamaduni na michezo.

    Uteuzi mkubwa uliogusa wengi ni ule wa Abraham Belay kutoka chama cha waziri mkuu Abiy cha Prosperity Party (PP) aliyeteuliwa kuwa waziri wa ulinzi.

    Aliwahi kuongoza utawala wa mpito wa jimbo la Tigray ulioundwa na serikali kabla ya waasi kufanikiwa kutwaa maeneo mengi ya jimbo hilo mwezi Juni.

    Karibu viti vyote katika uchaguzi huo vilichukuliwa na chama cha PP. Chama cha OLF ni miongoni mwa vyama kadhaa vya upinzani vilivyosusia uchaguzi huo.

  4. Siku chache baada ya kutiwa hatiani YouTube yaziondoa Channeli za R. Kelly

    Mtandao wa YouTube umeziondoa Channeli za TV za R. Kelly baada ya mwanamuziki huyo kutiwa hatiani mwezi uliopita kwa makosa ya unyanyasaji wa kingono.

    Mahakama imebaini kuwa kwa miaka 20 mwanamuziki huyo alitumia umaarufu na ushawishi wake kuwanyanyasa kingono wanawake na watoto.

    Mtandao wa YouTube umeziondoa Chaneli mbili za RKellyTV na RKellyVevo, ukisema uamuzi huo "ni kwa mujibu wa miongozo ya uwajibikaji kwa mwenye maudhui ".

    Mwanamuziki huyo hataweza tena kufungua Chaneli nyingine ya Youtube, lakini nyimbo zake zitaendelea kuonekana katika mtandao wa YouTube Music.

    Pia kwa sasa nyimbo zake zitaendelea kusikilizwa kwenye mitandao mingine na mashabiki zake wataendelea kusikiliza na kutazama.

    Youtube iliwahi huko nyuma pia kuondoa Chaneli za watu waliokutwa na hatia, ikiwemo ya kocha wa timu ya Viungo na sarakasi ya Marekani Larry Nassar, ambaye aliwekwa ndani kwa makosa ya udhalilishaji wachezaji vijana wa michezo hiyo waliokuwa anawasimamia.

    Kuna kundi linaendesha Kampeni ya ‘The MuteRKelly’ inayotaka nyimbo za R. Kelly zisipigwe kabisa radioni, kwenye vituo vya TV na mitandaoni limetoa wito kwa mitandao mingine kufuata nyayo za YouTube.

    Baada ya kutiwa hatiani R. Kelly atahukumiwa mwezi Mei mwakani na anaweza kujikuta akimalizia maisha yake jela.

  5. Forbes yamuondoa Trump katika orodha ya mabilionea baada ya miaka 25

    Donald Trump ana utajiri unaokadiriwa kuwa wa dola bilioni 2.5, akiwa na upungufu wa dola milioni 400, sababu ambayo imemuondoa kwenye orodha ya mwaka huu ya Forbes ya watu 400 tajiri zaidi nchini Marekani.

    Tajiri huyo mwekezaji katika sekta ya makazi, bado ni tajiri sawa na alivyokuwa mwaka mmoja uliopita, wakati aliposhikilia nafasi ya 339 katika orodha hiyo, lakini utajiri wake umepungua kwa kiasi cha dola milioni 600, tangu mwanzoni mwa janga la Covid.

    Hisa za teknolojia, sarafu ya kidijitali na mali nyingine vimeshamiri katika enzi ya Covid.

    Lakini mali kubwa za jiji-ambazo ndio sehemu kubwa ya utajiri wa Bw Trump- zimedhoofika, na hivyo kumsukuma rais huyo wa zamani nje ya klabu hiyo ya pekee ya taifa orodha.

    Iwapo Trump anamtafuta mtu wa kumlaumu, anaweza kwa kuanza kujilaumu mwenyewe. Miaka mitano iliyopita alikuwa na fursa nzuri ya kuwa na utajiri wa aina mbali mbali.

    Mara baada ya uchaguzi wa mwaka 2016 election, maafisa wa maadili wa serikali ya shirikisho nchini humo walimshinikiza Trump kuufanya utajiri wake wa makazi kuwa utajiri mseto.

    Hiyo ingemruhusu kuwekeza tena faida katika aina nyingine za viwango vya mapato na kutoweza kuepukana na migongano ya maslahi na mamlaka yake kama rais.

  6. Makumi wanaoshukiwa kuwa watekaji nyara wakamatwa Nigeria

    Polisi nchini Nigeria inasema imewakamata watu 20 wanaoshukiwa kuwa ni watekaji nyara wenye silaha kaskazini –magharibi mwa nchi ambako utekeji kwa ajili ya kikombozi umeshamiri.

    Maafisa wamesema kuwa watu hao wanatoka katika magenge mawili ambayo yamekuwa yakiendesha harakati zao zaidi kwenye pikipiki katika kanda hiyo.

    Katika taarifa yake msemaji wa polisi Frank Mba amesema silaha za "kisasa" zikiwemo gurunedi za kiwango cha juu 11 na bunduki 11 zimepatikana.

    Washukiwa hao bado hawajafikishwa mahakamani.

    Kwa mujibu wa taarifa hiyo, washukiwa wakuu wakati mwingine hujifanya kama madereva wa mabasi ya kibiashara

    Inasema wasafiri kutoka kwenye vituo vya magari hutoka na kuwafahamisha wajumbe wa magenge hayo ambao huwashambulia kwa kuwavizia kwenye barabara na kuwateka nyara wasafirikwa ajili ya kudai kikombozi.

    Nigeria imekuwa ikihangaika kukabiliana na ongezeko la wimbi la mauaji na utekaji nyara kwa ajili ya kikombozi unaofanywa na magenge ya wahalifu yenye silaha yanayowalenga watoto wa shule, jamii na wasafiri.

  7. Urusi kuanza mpango wake wa filamu katika anga za mbali

    Baadhi ya watengenezaji wa filamu nchini Urusi wamewasili katika kituo cha kimataifa cha anga za mbali kuanza kuchukua filamu kwa mara ya kwanza katika anga za mbali.

    Yulia Peresild ma muelekezaji wa filamu Klim Shipenko watashiriki katika filamu itakayoitwa "The Challenge".

    Ni filamu ya vichekesho inayoelezea hadithi ya mpasuaji aliyetumwa duniani kunusuru maisha ya mwanaanga Mrusi.

    Mwandishi wa BBC Yuria Peresil anaarifu kuwa hakuna muda uliobaki wa kuogopa.

    Mradoi huo wa anga za mbali unatarajiwa kufuatiwa na mradi kama huo uliopangwa na baadhi ya wapanda farasi wa Marekani hivi karibuni.

    Unaweza pia kusoma:

    • Yuri Gagarin:Hatari fiche zilizomkabili mwanadamu wa kwanza kwenda anga za mbali
    • China na Urusi zimetangaza mpango wa kujenga kituo cha anga za mbali mwezini
  8. Missouri yamuua mwanaume kwa kuwauwa watu watatu katika tukio la ujambazi

    Mwanaume mmoja kutoka jimbo la Missouri nchini Marekani ameuawa kutokana na mauaji aliyoyatekeleza, licha ya mawakili wake kumuombea msamaha wakisema kuwa alikuwa na ulemavu wa kiakili.

    Ernest Johnson alichomwa sindano ya sumu Jumanne baada ya Mahakama ya juu zaidi ya Marekani kukataa kuangalia uwezekano wa kuacha kumuua baadaye siku hiyo.

    Mwanaume huyo aliyekuwa na umri wa miaka 61, ambaye aliomba kuhurumiwa, alikuwa amepata uungaji mkono kutoka kwa Papa Francis na wajumbe wawili wa baraza la Congress.

    Johnson aliwauwa wahudumu watatu wa duka dogo la bidhaa mbali mbali katika tukio la ujambazi lilizofanyika mwaka 1994.

    Mawakili wa Bw Johnson walidai kuwa hakupaswa kuhukumiwa kifo kwasababu vipimo mbali mbali vya uwezo wake wa kiakili vimeonyesha kuwa ana uwezo wa kiakili wa mtoto nab ado alikuwa anasoma katika darasa la tatu.

    Johnson, ambaye ni Mmareknani mweusi, alizaliwa na hali ya kasoro ya kiakili ya vilevi baada ya mama yake kunywa vilevi kupindukia wakati alipokuwa na ujauzito wake.

  9. Mali yamuita mjumbe wa Ufaransa kuhusiana na kauli za Macron

    Waziri wa mambo ya nje wa Mali amemuita balozi wa Ufaransa Jumanne kupinga kauli zilizotolewa na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kuhusu serikali inayoongozwa na jeshi.

    Wizara ya mambo ya nje ilisema kuwa ilikuwa imemuita balozi wa Ufaransa kumfahamisha juu ya ' 'ghadhabu na kutokubali'', kwa kauli zilizonukuliwa na mashirika ya habari.

    Jumanne Rais Macron aliwashutumu maafisa wa kijeshi wa Mali kwa kuacha kutekeleza majukumu yao.

    Aliviambia vyombo vya habari kuwa sio jukumu la jeshi la Ufaransa kujazi kile alichokielezea kama "mambo yasiyo ya kazi ‘’ ya taifa la Mali.

    "Waziri huyoaliwataka maafisa wa Ufaransa kuwa na subira, kuepuka kutoa kuhukumu," imesema Wizara ya mambo ya nje ya Mali.

    Mwezi uliopita, waziri mkuu wa mpito wa Mali, Choguel Maïga, iliishutumu Ufaransa kwa "kulitelekeza" taifa katika kile alichosema "katikati ya safari ya angani" baada ya nchi hiyo ya Ulaya kuamua kupunguza nusu ya vikosi vyake nchini Mali.

    Uhusiano baina ya nchi mbili umeharibika tangu yalipofanyika mapinduzi ya kijeshi nchini Mali mwaka jana.

  10. SADC yakubali kuongeza muda wa vikosi vyake Msumbiji

    Jumuiya ya nchi zilizoko kusini mwa Afrika, SADC, imekubali kuongeza zaidi uwepo wa vikosi vya kikanda vinavyopambana na waasi kaskazini mwa Msumbiji.

    Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi amethibitisha kurefushwa zaidi kwa muda wa vikosi hivyo Jumanne jioni katika mwisho wa kikao kisicho cha kawaida.

    Awamu ya kwanza ya upelekaji wa vikosi hivyo ilipangwa kukamilika tarehe 15 Oktobar.

    Kikao hicho kiliitishwa kutathmini utendaji wa vikosi vya kikanda.

    Rais Nyusi alisema kuwa Msumbiji iliridhishwa na tathmini iliyofanywa sasa na kwamba hali imeimarika kwa kiasi kikubwa katika maeneo yaliyoathiriwa.

    Kikao hicho kilitoa heshima kwa wanajeshi waliofariki wakiwa kazini nchini Msumbiji. Watatu hao walikuwa ni kutoka mataifa ya Tanzania na Botswana.

    Unaweza pia kusoma:

    • Viongozi wa mataifa jirani waahidi kusaidia Msumbiji katika mkutano wa SADC
    • Mzozo wa Msumbiji: Wanajeshi wa Rwanda waongoza vita dhidi ya wapiganaji Msumbiji
    • Tanzania kupeleka vikosi vyake vya kijeshi Msumbiji
  11. ‘China huenda ikawa na uwezo wa kuishambulia Taiwan kufikia 2025’ Waziri wa Ulinzi

    Uhusiano wa kijeshi na China ni mbaya zaidi katika miaka 40, waziri wa ulinzi wa Taiwan amesema.

    Chiu Kuo-cheng pia alionya China itakuwa na uwezo wa kukivamia kisiwa hicho ifikapo 2025.

    Maoni yake yalikuja baada ya China kutuma "idadi kubwa " ya ndege za kijeshi katika eneo la ulinzi wa anga la Taiwan kwa siku nne mfululizo.

    Taiwan inajiona kuwa nchi huru. Beijing, hata hivyo, inaiona Taiwan kama jimbo lake lililojitenga.

    Haijafutilia mbali uwezekano wa matumizi ya nguvu kufanikisha kuungana na kisiwa hicho.

    "Kufikia mwaka 2025, China itasongesha karibu uwezekano wa mzozo kamili. Ina uwezo sasa, lakini haitaanzisha vita kwa urahisi, ikizingatia mambo mengine mengi," Chiu Kuo-cheng alisema wakati kamati ya bunge Taipei ikiingatia muswada wa matumizi ya ulinzi wa mabilioni ya dola kujenga makombora na meli za kivita.

    Taiwan ilijitenga na China bara wakati wakomunisti walipochukua madaraka mnamo 1949.

    Wachambuzi wameonya kuwa Beijing inazidi kuwa na wasiwasi kuwa serikali ya Taiwan inaelekea kuafikia azimio rasmi la kujitangazia uhuru na inataka kumzuia Rais wake Tsai Ing-wen kuchukua hatua zozote katika mwelekeo huo.

    Washirika kadhaa wa Magharibi wa Taiwan wameelezea wasiwasi wao juu ya onyesho wazi la China la nguvu zake za kijeshi katika siku za hivi karibuni.

    Hata hivyo, Rais wa Marekani Joe Biden alisema mwenzake wa China Xi Jinping amekubali kutii "makubaliano ya Taiwan".

    Bwana Biden alionekana kuashiria sera ya muda mrefu ya Washington ya "China moja" ambayo inaitambua China badala ya Taiwan.

  12. Facebook inawadhuru watoto na kudhoofisha Demokrasia, asema mfanyakazi wake wa zamani

    Mfanyakazi wa zamani wa Facebook amewaambia wabunge nchini Marekani kwamba tovuti na programu za kampuni hiyo ’’zinawadhuru watoto, zinasababisha mgawanyiko na kuthoofisha demokrasia yetu ".

    Frances Haugen, mwenye umri wa miaka 37, meneja wa zamani wa bidhaa katika kampuni ya Facebook aligeuka kuwa mfichua siri, ambaye ameikosoa sana kampuni katika bunge la congress la Marekani.

    Facebook imekuwa ikikabiliwa na uchunguzi na ongezeko la miito inayoitaka idhibiti mtandao huo.

    Facebook imesema nini?

    Muasisi wa Facebook Mark Zuckerberg amejibu, akisema, maelezo ya hivi karibuni yalitoa "picha ya uongo" kuihusu kampuni.

    Katika barua yake kwa wafanyakazi, amesema kuwa mengi kati ya madai ‘’hayana maana yoyote’’ huku akielezea juhudi zao katika kupambana na maudhui yenye madhara, kuanzishwa kwa uwazi na kubuni " mpango wa tafiti unaoongozwa na kampuni hiyo kushugulikia masuala haya ".

    ’’Tunajali sana kuhus masuala kama usalma, maisha bora na afya ya akili’’, amesema Bw Zuckerberg, katika barua yake iliyowekwa kweney ukurasa wake wa Facebook.

    "Ni vigumu kusikia maelezo ambayo hayawakilishi kazi yetu na nia zetu’’

    Facebook ni mtandao maarufu zaidi wa kijamii duniani. Kampuni inasema ina watumiaji bilioni 2.7 wanaotembelea ukurasa huo kila.

    Mamia ya mamilioni ya watu pia hutumia mitando mingine ya kamouni hiyo, ikiwa ni pamoja na WhatsApp na Instagram.

    Lakini imekuwa ikikosolewa kwa kila kitu kuanzia kushindwa kulinda usiri wa watumiaji hadi kutofanya juhudi za kutosha kuzuwia usambaaji wa taarifa potofu.

    Unaweza pia kusoma:

    • Mark Zuckerberg akiri kampuni yake inakabiliana na Urusi
    • Mark Zuckerberg amezitaka serikali kusaidia kuweka sheria za udhibiti wa taarifa za intaneti
    • Kurasa za Mark Zuckerberg zimedukuliwa
  13. Chadema wafungua kesi kudai dhamana ya Hashim

    Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimefungua kesi kudai kuachiliwa kwa dhamana kwa kiongozi wa baraza la wazee la chama hicho Hashim Issa Juma (63) ambaye anashilikiwa kwa siku ya nne sasa.

    Kupitia taarifa yao kwa vyombo vya habari chadema wanasema licha ya kufanya utaratibu wote kumuombea dhamana kiongozi huyo bado polisi wameendelea kumshikilia.

    Kufuatia hayo, timu ya wanasheria wa chama hicho wamefungua shauri mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini Dar es salaam, wakitaka jeshi la polisi kueleza kwa nini hawataki kumpatia dhamana mtuhumiwa huyo wakati ni haki yake ya kikatiba.

    Akizungumzia sakata hilo Jumanne, Kamanda wa kanda maalumu ya jeshi la polisi Dar es salaam Jumanne .

    Muliro alisema jeshi hilo bado linamshikilia mwenyekiti wa baraza la wazee wa Chadema Hashimu Issa Juma kwa tuhuma za kutoa kauli za kichochezi

    Kamanda Muliro anasema wanamhoji kwa kina baada ya tarehe 01/10/2021 akiwa eneo la ufipa kinondoni kutoa kauli za kichochezi zilizokuwa na nia ya kujenga chuki kati wananchi na serikali.

    Bwana Hashim alikamatiwa visiwani Zanzibar na baadae kurejeshwa Dar es salaam ambako alitolea kauli zinazodawa kuwa ni za kichochezi.

    Jeshi la polisi linaendela kukusanya ushahidi ili kuhakikisha hatua zinachukuliwa kwa mujibu wa sheria‘’.

    Jeshi la polisi linakusanya ushahidi wote kwa kadiri inavyowezekana na litahakikisha hatua za kisheria dhidi ya mtuhumiwa huyu zinafanyika kwa kufuata mtiririko wa kisheria’’ Alisema kamanda Muliro.

    Unaweza pia kusoma:

    • Nini maana ya mwisho wa Uenyekiti wa Mbowe Chadema?
    • Chadema yataka kuonana na Rais Samia
    • Chadema yamjibu Rais Samia, yasema amepotoshwa
  14. Michoro nadra ya mwanamasumbwi Muhammad Ali yauzwa kwa takriban $1m

    Mkusanyiko nadra wa kazi za michoro ya mwanamasumbwi gwiji Muhammad Ali imeuzwa kwenye mnada kwa karibu dola milioni 1 (£733,760).

    Kazi zake 26 za usanii zilipelekwa katika jumba la mnada la Bonhams mjini New York.Mojawapo ya kazi zilizosubiriwa ni ule wa mfano wa nyuki, uliouzwa kwa dola 425,000 (£311,853), kiasi hicho kikiwa ni mara 10 ya makadirio ya awali ya mauzo yake.

    Ali alisifiwa kwa kuwa mmoja wa wanariadha bora zaidi, mwanaharakati na mshairi, lakini usanii wake wa kuchora haukujulikana.

    Kituo cha manada cha Bonhams kilisema alichora katika maisha yake –akitiwa moyo na baba yake ambaye alikuwa mchoraji aliyesomea taaluma hiyo na hatimaye alifanya masomo kutoka kwa msanii wa michezo LeRoy Neiman.

    "Muhammad Ali alijitolea kuendeleza utamaduni kwa vizazi Kazi zake za usanii zilionyesha mambo hayo yalikuwa moyoni mwake: Mwanamasumbwi, Mtetezi wa haki za binadamu, Dini na Amani ya dunia na Mtu aliyejali utu ," alisemaHelen Hall, Bonhams Mkurugenzi wa taasisi ya Popular Culture, kabla ya mauzo.

    Michoro hio iliwekwa kwenye mnada na mkusanyaji wa sanaa na rafiki wa Mohammad AliRodney Hilton Brown, ambaye alisemaAlisema picha zake tatu za kwanza alizichora baada ya mpambano wa Boston mwaka . Jumla ya mauzo ya michoro hiyo ilikuwa ni dola 945,524 (£693,788) kiwango ambacho kilikuwa ni mara tatu zaidi ya bei iliyotarajiwa

  15. Habari...Karibu katika matangazo ya moja kwa moja ya ukurasa wa BBC Swahili, leo ikiwa Jumatano 06/10/2021