Mwanaharakati, Dkt.Cyrilo aachiwa kwa dhamana Tanzania
Mwanaharakati wa kimtandao nchini Tanzania anayefahamika kwa jina la Dkt.Cyrilo Christopher ambaye ni Daktari wa binadamu pia mwandishi wa vitabu aliyekuwa akishikiliwa katika kituo cha polisi cha Kati Jijini Dar es salaam leo Jumatano ameachiwa kwa dhamana.
Moja kwa moja
Mwanaharakati, Dkt.Cyrilo aachiwa kwa dhamana Tanzania
Mwanaharakati wa kimtandao nchini Tanzania anayefahamika kwa jina la Dkt.Cyrilo Christopher ambaye ni Daktari wa binadamu pia mwandishi wa vitabu aliyekuwa akishikiliwa katika kituo cha polisi cha Kati Jijini Dar es salaam leo Jumatano ameachiwa kwa dhamana.
Hata hivyo hapo awali kuliibuka sintofahamu ya ni wapi alipo.
Hata hivyo Hakukua na taarifa za wazi kutoka kwa Polisi nchini Tanzania kukiri kwamba inamshikilia isipokua tu kwa watu wake wa karibu.
Hata hivyo watu wake wa karibu walithibitisha kuwepo kwake katika kituo kikuu cha polisi kwa siku tatu na leo amepatiwa dhamana
Scolar Kisanga amezungumza na wakili wake, Dickson Matata.
Maelezo ya sauti, Dkt.Cyrilo aachiwa kwa dhamana Mzee mmoja Eritrea afariki akiwa na miaka 127, familia yake yataka awekwe kwenye kitabu cha Guinness

Chanzo cha picha, Zere Natabay
Mzee mmoja huko nchini Eritrea amefariki akiwa na umri wa miaka 127, familia yake imesema.
Aidha familia hiyo imesema ina matumaini kwamba Natabay Tinsiew atapata nafasi ya kuandikwa kwenye kitabu cha Guinness World Records kama mtu aliyewahi kuishi miaka mingi zaidi.
"Uvumilivu, ukarimu na maisha ya furaha" ndio siri ya mzee huyo kuishi kwa muda mrefu, mjukuu wake Zere Natabay aliiambia BBC Tigrinya.
Bwana Natabay alifariki siku ya Jumatatu akiwa na amani katika kijiji chake, Azefa - ambacho kina idadi ya watu takribani 300 na kipo kwenye korongo lililozungukwa na milima.
Mjukuu wake amesema rekodi za kanisa - pamoja na cheti chake cha kuzaliwa - kinaonesha kuwa alizaliwa mnamo mwaka 1894 - na ndio mwaka ambao alibatizwa - na hivyo kumfanya awe amefariki akiwa na miaka 127.
Lakini familia ya Bw. Natabay inaamini kuwa mzee huyo alizaliwa mnamo mwaka 1884, lakini alibatizwa miaka 10 baadaye, wakati mapadre walipokuja karibu na kijijini kwao.Kulikuwa na mapadre wachache wakati huo, na watu walikuwa wakiwasubiri watembelee kijiji chao.
Padre Mentay, wa kanisa katoliki ambaye alihudumu katika kijiji hicho kwa miaka saba, alithibitisha kwamba rekodi zilionesha kwamba Bwana Natabay alizaliwa mnamo 1894. Alisema alikuwepo wakati wanakijiji wakisherehekea alipotimiza miaka 120 mnamo 2014.
Bwana Zere aliiambia BBC kuwa tayari alikuwa amewasiliana na Guinness World Record ili kuthibitisha hati rasmi za kuzaliwa kwa babu yake, na alikuwa akingojea kusikia kutoka kwao.
Katika kitabu cha Guinness World Records kimemrekodi mwanamke wa Ufaransa Jeanne Calment, aliyekufariki mnamo 1997 akiwa na miaka 122, kama mtu aliyeishi miaka mingi zaidi.
Bwana Natabay alioa mnamo mwaka 1934, mke wake alifariki mwaka 2019 akiwa na umri wa miaka 99.
Wakati wa maisha yake, Bwana Natabay alikuwa mfugaji, mwenye ng'ombe wengi, mbuzi na nyuki.
Vilevile alifanikiwa kuishi na kuona vizazi vitano vya familia yake vikikua.
Bwana Zere alisema babu yake atakumbukwa kama "mtu wa kushangaza", ambaye alikuwa mwema, anayejali na mchapa kazi.
Kundi jipya la Jihadi ladai kuua wapelelezi wa Sudan
Kundi hilo la jihadi ambalo halijulikani hapo awali limesema liliwaua maafisa sita wa ujasusi wa Sudan wakati wa majibizano ya risasi Jumanne.
Serikali imeonesha kuchukizwa na mashambulizi hilo na kudai kuwa wanaohusika ni wanamgambo kutoka kundi la Dola la kiislamu (IS).
Lakini kundi la wanajihadi linalojiita Movement for Preaching and Combat lilitoa taarifa ya kuwaona maafisa wa Sudan na pia limekataa uhusiano wowote na IS.
Bado hakuna anaweza kuthibitisha kuwa hawa wameamasishwa na nani kufanya hivyo.
Mamlaka nchini humo zilikiri kupoteza maafisa watano katika uvamizi wa Jumanne na kusema wapiganaji 11 walikamatwa.
Wiki iliyopita jeshi la Sudan lilifanikiwa kukwamisha jaribio la mapinduzi.
Mashirika ya ndege ya Kenya na Afrika Kusini yasaini mkataba wa ushirikiano

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Shirika la ndege la Afrika Kusini lilirejelea shughuli zake wiki iliopita Shirika la ndege la Afrika Kusini( SAA) na shirika la ndege la Kenya(KQ) zimetia saini mkataba wa muda mrefu ushirikiano wa kuunda shirika la ndege la Afrika.
SAA na KQ, ambazo zimekuwa zikikabiliwa na mizozo ya kifedha na usimamizi, zinasema ushirikiano wao utafanya sekta ya usafiri wa angaga kuwa na ushindani zaidi.
Walitia saini hati ya makubaliano ili kuongeza uwezo wao wa ukuaji wa pande zote.
Ushirikiano huo unajumuisha kutumia Pamoja huduma kama njia ya usafiri na, ukarabati, na pia kutafuta fursa za kufikia uchumi wa kiwango ha juu.
Mashirika yote mawaili yamesisitiza kwamba yataendelea kuwa huru kushirikiana na mashirika mengine.
SAAilirejelea shughuli zake wiki iliopita baada ya kusitishwa kwa zaidi ya mwaka mmoja kwa sababu ya kufilisika.
KQ iliathiriwa vibaya na janga la Covid-19,na imekuwa ikitegemea usafirishaji wa mizigo ili kupunguza hasara.
Nigeria yafungia zaidi ya pasipoti 2,000 kwa ukiukaji wa kanuni za Covid
Serikali ya Nigeria inasema imesimamisha pasipoti zaidi ya 2,000 ya Wanigeria 2,000 wanaotuhumiwa kukiuka kanuni za kuzuia Covid baada ya kurudi kutoka nje.
Dkt Mukhtar Mohammed, ambaye ni Rais wa kamati ya Rais ya kushughulikia janga la Covid amesemapasipoti hizo zitafungiwa kwa mwaka mmoja.
Wakati inapojiandaa kwa wimbi la tatu la maambukizi, Nigeria imeimarisha mfumo wake wa ufuatiliaji katika viwanja vya ndege, bandari na mipaka ya ardhini.
Tahadhari sasa inazingatia wasafiri, haswa wale wanaowasili kutoka nchi ambazo wasafiri wake wanaweza kujaribu kukwepa maagizo ya kujitenga.
Watu wanaowasili kutoka mataifa kama India, Afrika Kusini, Brazil na Uturuki wanatarajiwa kukaa karantini kwa siku 14 katika vituo vilivyoidhinishwa na serikali.
Habari za hivi punde, Mo Dewji ajiuzulu nafasi ya mwenyekiti wa klabu ya Simba Tanzania
Ruka Instagram ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa Instagram ujumbe
Mwenyekiti wa bodi ya Simba ya Tanzania, Mohamed Dewji maarufu kama Mo Dewji amejiuzulu nafasi hiyo.
Mo Dewji amesema uamuzi huo umeafikiwa kutokana na kutingwa na majukumu ya biashara zake zinazomfanya kuwa nje ya nchi muda mwingi.
‘Tumekubaliana kwamba kwa kuwa mimi muda mwingi sipo nchini na ninasafiri sana, tunahitaji mwenyekti wa bodi ambaye anaweza kuingoza klabu na uwepo wake ni muhimu sana’, alisema Mo Dewji kwenye taarifa yake video fupi.
Mo Dewji ametangaza pia nafasi yake itashikiliwa na Salim Abdallah 'try again' aliyekuwa makamu mwenyekiti wa bodi hiyo
‘Kwa makubaliano tuliyo nayo kati yangu mimi mwekezaji na Simba Sports Club, nachukua fursa hii kumteua Salim Abdallah ‘Try Again, kuwa Mwenyekiti wa Simba Sports Club’, alisema.
Kwa mujibu wa Mo Dewji uamuzi wa yeye kujiuzulu umefikiwa kwenye mkutano wa bodi hiyo uliofanyika Septemba 21, 2021.
Hata hivyo amewatoa hofu wana Simba kwamba amejiuzulu tu nafasi ya mwenyekiti wa bodi lakini bado ataendelea kuwa sehemu ya Simba.
‘Nawaomba wanasimba msifikirie kwamba mimi nimeondoka kwenye simba bali mimi bado ni mwekezaji kwenye Simba bado mwanahisa kwenye Simba, ninaipenda Simba na nitaendelea kuipenda Simba mpaka siku yagu ya mwisho.
Huenda ikawa wiki ngumu kwa wapenzi na mashabiki wa Simba, ambapo kabla ya leo Mwenyekiti wao kujiuzulu mwishoni mwa wiki wametoka kufungwa bao 1-0 na mahasimu wao Yanga kwenye kombe la ngao ya jamii kuashiria kufunguliwa kwa pazia la ligi kuu, kabla ya jana kwenda tasa ya 0-0 na Biashara United katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya nchi hiyo.
Mo Dewji mmoja wa mabilionea wa Afrika, amekuwa mwenyekiti wa Bodi ya Simba kwa miaka minne na chini ya uongozi wake amesaidia timu hiyo kushinda makombe manne mfululizo ya ligi kuu Tanzania na kuisadia timu hiyo kuingia robo fainali mbili za ligi ya mabingwa Afrika.
Wabunge wa upinzani waliokamatwa Uganda baada ya kuachiwa kufikishwa mahakamani leo

Maelezo ya picha, Mbunge Allan Sewanyana(aliyebeba kiti) anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya Masaka Wabunge wawili walio na ufungamano na mwanasiasa wa upinzani wanatarajiwa kufikishwa mahakama leo kwa madai ya kupanga mashambulio mabaya katika mkoa wa Masaka kusini mashariki.
Muhammad Ssegirinya na Allan Sewanyana wa chama cha National Unity wamekanusha mashataka dhidi yao na kuishtumu serikali kwa kuwatesa.
Kulingana na kituo cha NTV Uganda, siku ya Jumanne wabunge wa upinzani walitoka nje ya bunge kulalamikia hatua ya vyombo vya usalama kuwakamata tena wabunge wenzao wawili ambao walikuwa wameachiliwa kwa dhamana.
Karibu watu 30 waliuawa kwa kukatwa mapanga na magenge ya uhalifu mjini Masaka katika shambulio lililoanza mwezi Julai.
Sudan yaomboleza maafisa waliouawa katika oparesheni dhidi ya seli ya IS
Viongozi wa Sudan wametoa heshima zao za mwisho kwa maafisa watano wa usalama waliouawa jana katika oparesheni iliyolenga "seli inayohusishwa na kundi la Islamic State" katika mji mkuu, Khartoum, kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya serikali.
Kiongozi wa nchi hiyo, Luteni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, naibu wake, Luteni Jenerali Mohamed Hamdan Daglo (maarufu Hemeti) na Waziri Mkuu Abdallah Hamduk waliwatambua “maafisa hao watano” kama mashuhuda.
Burhan alisema waliuawa “wakitekeleza majukumu yao ya kulinda nchi dhidi ya vitendo vya kigaidi”, Shirika la habari la Sudan linaloendeshwa na serikali liliripoti.
Shirika la ujasusi lilisema maafisa hao walifanya msako katika jumba la ghorofa mbili viungani mwa mji wa Jabra baada ya kupata taarifa ya uwepo wa seli ya ugaidi inayohusishwa na kundi la Islamic State, Suna iliripoti.
Habari za hivi punde, Bondia Manny Pacquiao astaafu katika ndondi

Chanzo cha picha, Getty Images
Bondia wa Ufilipino Manny Pacquiao ametangaza kustaafu mchezo huo ili kuangazia kazi yake ya siasa.
Bondia huyo anayeshikilia mataji ya uzani tofauti ni seneta nchini humo na tayari ametangaza nia yake ya kuwania urais katika uchaguzi wa mwaka 2022.
Katika pigano lake la mwisho bondia huyu mwenye umri wa miaka 42-alishindwa na bondia wa Cuba Yordenis Ugas mjini Las Vegas mwezi uliopita.
"Nilisikia kengele ya mwisho tu. Mchezo ulikua umeisha," alisema Pacquiao.
Katika video iliyowekwa katika mitandao ya kijamii, Pacquiao alielezea kustaafu kwake kama "uamuzi mgumu" katika Maisha yake, akiongeza kuwa ndondi ilimpatia "nafasi ya kupigana na umaskini" na "ujasiri wa kubadilisha maisha zaidi".
Pia aliwashukuru mashabiki wake, marafiki na wale wote waliomuunga mkono katika mchezo huo,hususan Mkufunzi wake wa muda mrefu Freddie Roach, ambaye alimtaja kama "familia yangu, kaka na rafiki".
"Sitasahau kile nilichofanya na kufanikisha maishani mwangu," alisema.
Pacquiao anatambulika kama bondia bora wa kulipwa duniani, akishinda mataji 12 katika mikanda minane tofauti na ni bondia wa pekee kushikilia ubingwa wa dunia kwa miongo minne.
Soma:
Shambulio la angani la Nigeria lawaua raia karibu na ziwa Chad

Chanzo cha picha, AFP
Raia kadhaa wameuawa katika shambulio la angani la Nigeria lililokua likiwalenga washukiwa wa makundi ya kijihadi karibu na ziwa Chad, ambayo inapita kaskazini-mashariki mwa Nigeria na nchi tatu jirani.
Tukio hilo linakuja chini ya wiki mbili baada ya shambulio lingine dhidi ya kijiji kuwaua raia kaskazini -mashariki mwa Nigeria, ambako majeshi yanakabiliana na wanamgambo wa kijihadi.
Maelezo bado yanaibuka kutoka eneo la Kwantan Daban Masara, ambapo shambulio hilo lilifanyika Jumapili asubuhi.
Haijabainika ni raia wangapi waliuawa katika shambulio hilo, au ikiwa walikuwa na uhusiano na kundi la Wanamgambo Islamic State katika eneo la Afrika Magharibi (Iswap), ambalo linahudumu katika eneo hilo.
Shirika la Habari la AFP linasema karibu wavuvi 20 waliuawa. Shirika la Habari la Reuters liliwanukuu watu wawili- mkazi na mhasiriwa alijyeruhiwa- wakisema karibu watu 50waliuawa baada ya Jeshi la Anga la Nigeria kuwafyatulia risasi raia kadhaa.
Korea Kaskazini yarusha kombora la pili chini ya saa 24

Chanzo cha picha, Reuters
Korea Kaskazini imedai kuwa ilifanikiwa kujaribu kombora lake jipya linaloitwa Hwasong-8, siku ya Jumanne.
Vyombo vya habari vya serikali vilisema kombora hilo jipya lilikuwa moja wapo ya mifumo "mitano muhimu zaidi" ya silaha iliyowekwa katika mpango wake wa maendeleo ya kijeshi wa miaka mitano.
Walilsema kombora hilo jipya ni "silaha ya kimkakati", ambayo kwa kawaida inamaanisha uwezo wa nyuklia.
Uzinduzi wa Jumanne ni dalili nyingine ya teknolojia ya silaha iliyo nayo Pyongyang, licha ya kukabiliwa na vikwazo vikali.
Uendelezaji wa mfumo huu wa silaha ... [umeongeza] uwezo wa taifa wa kujilinda kwa kila njia," kituo cha habari cha serikali ya Korea Kaskazini KCNA kilisema.
Uzinduzi wa hivi karibuni pia uliashiria jaribio la tatu la kombora nchini humo mwezi huu.
Makombora ya Hypersonic yana kasi zaidi na wepesi zaidi kuliko yale ya kawaida, na kuifanya iwe ngumu sana kwa mifumo ya ulinzi wa makombora kuyazuia, kulingana na shirika la habari la AFP.
Karibu katika matangazo ya moja kwa moja leo Jumatano 29.09.2021
