Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Rusesabagina ahukumiwa kifungo cha miaka 25 jela

Mtu ambaye aliyeoneshwa katika filamu kama shujaa aliyeokoa maisha ya watu wengi wakati wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda amepatikana na hatia ya ugaidi na mahakama nchini humo.

Moja kwa moja

Ambia Hirsi

  1. Kufikia hapo tunatamatisha habari za leo, hadi kesho alamsiki

  2. Habari za hivi punde, Rusesabagina ahukumiwa kifungo cha miaka 25 jela

    Baada ya kupatikana na hatia ya kushiriki katika vitendo vya ugaidi, aliyekuwa shujaa wa filaumu ya Hotel Rwanda Paul Rusesabagina hatimaye amehukumiwa kifungo cha miaka 25 jela.

    Mahakama moja nchini Rwanda ilimpata na hatia kuhusiana na mashtaka yanayohusiana na ugaidi.

    Alisusia uamuzi wa kesi hiyo na hakutoka jela ili kuhudhuria mahakama.

    Rusesabagina alituhumiwa kwa kuwa mwanzilishi na mfadhili wa kundi moja la waasi ambalo lilitekeleza mashambulio nchini Rwanda 2018 na kuwaua watu tisa.

    Mkosoaji huyo wa Rais Paul Kagame alikiri kutuma fedha kwa kundi hilo lakini akakana kuhusika katika mashambulizi.

    Rusesabagina ametaka kesi hiyo kuwa aibu.

    Mwanawe wa kike Anaise Kanimba aliambia BBC kwamba familia yake haijaamua iwapo itakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

  3. Watu wawili wauawa kwa shambulio la guruneti Burundi

    Watu wawili wameuawa na wengine wamejeruhiwa katika shambulio la guruneti mjini Gitega nchini Burundi polisi wameeleza.

    Ripoti kutoka mjini humo zinasema kuwa shambulio hilo lilitokea kwenye kilabu cha pombe , karibu na kituo cha basi chenye pilika nyingi, Jumapili jioni wakati watu walipokusanyika kwa ajili ya kupata kinywaji.

    Mkuu wa polisi wa mjini Gitega ameiambia BBC kuwa washukiwa kadhaa wamekamatwa na uchunguzi ulikuwa ukiendelea kubaini nani hasa alihusika na shambulio hilo.

    Shambulio hilo lilitokea siku moja baada ya kuripotiwa kwa makombora katika eneo jirani na uwanja wa ndege wa kimataifa katika mji mkuu wa kibiashara, Bujumbura.

    Waasi wa RED-Tabara, ambao wanafikiriwa kufanya operesheni zao kutoka eneo la mpaka mashariki mwa DRC, walikiri kutekeleza shambulio hilo.

    Mnamo mwezi Juni, watu wawili waliuawa katika mashambulio ya guruneti huko Bujumbura katika jaribio dhahiri la kuvuruga mkutano ulioitishwa na UN kuhusu eneo la Maziwa Makuu ambao ulipaswa kufanyika jijini.

  4. DR-Congo yatuhumiwa kupuuza ubakaji uliofanyika gerezani mwaka mmoja uliopita

    Shirika la kutetea haki la Human Rights Watch linasema mamlaka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zimepuuza tahadhari za mara kwa mara zilizotangulia ghasia za gerezani mwaka jana ambapo wafungwa wa kiume waliwabaka wanzao wa kike kwa siku tatu mfululizo.

    Mwaka mmoja baadaye ripoti mpya inatoa wito kwa mamalaka za DR- Congo kuchunguza kwa kina kilichofanyika na kuwachukulia hatua waliohusika na unyanyasaji huo.

    Uchunguzi unaaminika kuanza siku moja baada ya ghasia hizo lakini, mwaka baadaye bado haujakamilika, kutokana na kile kinaripotiwa kuwa ukosefu wa rasilimali.

    Wafungwa 37 wa kike kati ya 56 miongoni mwao msichana wa miaka 16 wametoa ushahidi mbele ya mwendesha mashtaka wa jeshi wakisema wao ni wahanga wa ghasia na ubakaji.

    Baadhi ya manusura walibakwa mara kadhaa na wanaume tofauti katika ghasia hizo zilizodumu kwa siku tatu.

    Wahasiriwa saba walipachikwa mimba na wengine kuambukizwa magonjwa ya zinaa ikiwa ni pamoja na virusi vya HIV/Ukwimwa, ripoti hiyo inasmea.

    Watafiti wanataka waathirika wapatiwe huduma ya matibabu na msaada wa afya ya akili.

    Mamlaka ya DR-Congo bado hayajajibu ombi la BBC, la kutaka kauli yake kuhusiana na suala hilo.

    Mnamo Septemba 2020 wafungwa 2,000 wa gereza kuu la Kasapa walifanya ghasia na kuchoma moto majengo ya gereza hilo na kuwashambulia wafungwa wa kike.

    Mlinzi wa gereza alifariki kutokana na majeraha aliyoyapata wakati wa ghasia hizo, na vikosi vya usalama viliripotiwa kuwapiga risasi watu wasiopungua 20 katika vurugu hizo.

  5. Waghana wanasherehekea ushindi wa kihistoria wa Emmy wa Michaela Coel

    Mwigizaji wa Uingereza wa mwenye asili ya Ghana amekuwa mwanamke mweusi wa kwanza kushinda tuzo ya Emmy kwa uandishi wa hadithi fupi.

    Kipindi chake maarufu I May Destroy You kinamfuatilia mhusika mkuu Arabella, anavyokabiliana na kiwewe cha unyanyasaji wa kijinsia.

    Michaela Coel aliigiza, kuandika na kuelekeza mchezo huo wa kuigiza.

    Watumiaji wa Twitter wa Ghana wamepokea ushindi wake, kwa neno moja, "Michaela Coel ni mwaminifu sana kwa kazi yake. Anastahili ushindi huu, umechukua muda mrefu sana. ”

    Mwingine alisema nchi yet inajivunia ushindi wako: "Hakika... huu ni ushindi kwa Ghana pia ... Hongera @MichaelaCoel ... Ghana inakuenzi."

  6. Romeo Beckham: Mtoto wa nyota wa zamani wa Man Utd na England aanza kukipiga Fort Lauderdale

    Romeo Beckham, mtoto wa nahodha wa zamani wa England David Beckham, Jumapili hii amecheza mchezo wake wa kwanza akiwa na timu ya Fort Lauderdale inayoshiriki ligi daraja la tatu nchini Marekani.

    Kinda huyo mwenye umri wa miaka 19 alianza kama kiungo, nafasi aliyokuwa anaichezea baba yake kwenye mchezo wa sare ya 2-2 dhidi ya South Georgia Tormenta.

    Timu hiyo ni ya akiba iliyo chini ya timu ya Inter Miami – inayoshiriki ligi kuu ya Marekani na inayomilikiwa na baba yake.

    "Ni Baraka kucheza mchezo wangu wa kwanza wa kulipwa usiku huu," Romeo aliandika katika mtandao wake wa Instagram.

    Romeo aliyesaini mkataba wa kulipwa na klabu hiyo mapema mwezi Septemba, alionyesha mchezo mzuri na kutengeneza nafasi muhimu ya kufunga mwanzoni mwa mchezo huo.

    Katika sehemu ya kiungo kulikuwa na muunganiko mzuri akicheza sambamba na Harvey Neville, mtoto wa kocha mkuu wa Inter Miami, Phil Neville. Phil Neville alicheza pamoja na Beckham kwenye klabu ya Manchester United.

    Mtoto wa Neville alikuwa akicheza mchezo wake wa 16 akiwa na timu hiyo yenye maskani yake huko Florida, baada ya kuondoka kwenye timu ya vijana ya Manchester United na kujiunga na baba yake nchini Marekani.

    Romeo Beckham alipumzishwa katika dakika ya 79 na kusema kwa sasa "mawazo yake yote ni kwenye mchezo unaofuata".

    Baba yake Beckham alitikisa vichwa vya habari duniani baada ya mwaka 2007 kufanya uhamisho wa kushangaza wa kuhamia LA Galaxy ya Marekani akitokea kwa magwiji Real Madrid.

    Akiwa Marekani alishinda vikombe viwili mfululizo vya MLS mwaka 2011, 2012 na mwaka 2019 akajengewa sanamu nje ya uwanja wa La Galaxy ili kumpa heshima ya kuichezea klabu hiyo kwa miaka 6.

  7. Mafuriko ya Burundi: Viwango vya maji vyaongezeka Ziwa Tanganyika

    Majanga ya kiasili yamelazimisha zaidi ya watu 100,000 kutoroka makwao nchini Burundi ikatika miaka ya hivi karibuni, Shirika la watoato la Save the Children linasema.

    Baadhi yao walikua wakiishi kando ya Ziwa Tanganyika ambako viwango vya maji vimepanda kutokana na dhoruba kali, lililosababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi.

    Watu walielezea kuamka usiku na kupata nyumba na mashamba yao yamesombwa na maji ya ziwa hilo, la pili kwa ukubwa duniani.

    Save the Children lilisema ni "mzozo uliosahaulika".

    Karibu 85% ya watu 122,500 wanaoishi katika makambi nchini Burundi wamehamishwa na majanga ya asili, badala ya mizozo, shirika hilo lilisema.

    Sababu nyingi zinachangia mafuriko, lakini hali ya joto inayosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa hufchangia uwezekano wa mvua nyingi.

    Viwango vya joto duniani tayarivimefikia nyuzi 1.2 tangu enzi ya viwanda ilipoanza na joto litaendelea kuongezeka endapo serikali ulimwenguni hazittadhibiti uzalishaji wa hewa ya kaboni.

  8. Rais wa Zambia alisifiwa kwa kusafiri na maafisa 'wachache'

    Rais wa Zambia Hakainde Hichilema amekuwa akisifiwa mitandaoni kwa kusafirina “maafisa wachahche” kuhudhuria kikao cha 76 za mkutano wa baraza la kuu la umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani .

    Bwana Hichilema alisafiri kwa kutumia ndege ya Qatar Airways fkutoka mjini Lusaka, akiandamana na mawaziri wawili.

    “Kama nilivyoahidi kabala niingie madarakani, utahakikisha usimamizi mzuri wa rasilimali za umma na kwa hivyo tumesafiri na timu konda ambayo inaundwa na Mawaziri wa Mambo ya Nje na Fedha, Stanley Kakubo na Dk Situmbeko Musokotwane mtawaliwa, "alisema katika taarifa kabla ya kuondoka.

    "Huyu ni wa kwanza katika eneo ambalo [Rais wa Zimbabwe] Emmerson Mnangagwa na [Lazaro wa Malawi] Chakwera huchukua ndege zilizojaa watu wanaodandia safari", aliandika mwandishi wa habari wa Zimbabwe Hopewell Chin'ono.

    Mtumiaji mwingine wa mitandao ya kijamii aliandika: "Afrika inainuka: Rais wa Zambia Hakainde Hichilema ameondoka Zambia kwenda Mkutano Mkuu wa UN, New York kwa kutumia ndege ya kibiashara".

    Rais wa Malawi mnamo Julai alikosolewa kwa kusafiri na familia yake kwa safari ya Uingereza lakini akasema kwamba walihitajika kwa hafla hiyo.

  9. Macron awaomba msamaha mashujaa wa vita wa Algeria

    Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amewaomba msamaha Harkis -r Waalgeria waliopigania uhuru wa Algeria dhidi ya Ufaransa.

    Bwana Macron alizomewa aliposema Ufaransa ilizembea katika majukumu yake kwa mashujaa hao.

    Aliahidi ukumbusho na sheria juu ya fidia mwishoni mwa mwaka.

    Tume itaundwa kusikiza madai kutoka kwa wapiganaji walionusurika na watoto wao, ambao waliolelewa kwenye uzio wa sing'eng'e katika kambi za Ufaransa.

    Maelfu ya watu walipelekwa Ufaransa baada ya nchi hiyo kushindwa mwaka 1962, lakini wengine wengi wengi zaidi waliachwa nyuma na kuteswa kwa kuwa washirika.

    Marais waliopita waliomba msamaha, lakini viongozi Harki walisema mfuko wa ugumu wa dola milioni 50 (£36.5m) uliotangazwa miaka mitatu iliyopita haikidhi mahitaji.

  10. Habari za hivi punde, Rusesabagina apatikana na hatia ya ugaidi

    Mtu ambaye alioneshwa katika filamu ya ''Hotel Rwanda'' kama shujaa aliyeokoa maisha ya watu wengi wakati wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda amepatikana na hatia ya ugaidi katika mahakama nchini Rwanda.

    Paul Rusesabagina alipatikana na hatia ya kulifadhili kundi moja la waasi akiwa mafichoni ambalo liliwauawa raia katika shambulio la 2018.

    Familia yake imedai kwamba alichukuliwa na kupelekwa nchini Rwanda kwa nguvu.

    Pia inasema kwamba mpendwa wao hakushtakiwa na mahakama huru.

    Safari ya Rusesabagina kutoka mtu aliyekuwa na sifa chungu nzima hadi kuwa adui wa serikali ilianza wakati alipokuwa akiikosoa sana serikali.

    • Utata juu kukamatwa kwa 'shujaa' wa filamu ya mauaji ya Rwanda.
    • Paul Rusesabagina: Rwanda yakiri kuwa 'iliilipa ' ndege iliyomtoa Dubai na kumpeleka Kigali, bila kujua
    • Watoto wa Rusesabagina wadai baba yao anaamriwa cha kuzungumza na kuwa alikataliwa kuwa na wanasheria huru
  11. Jeneral Muhoozi: Uganda kufanya kazi na Misri kwa ustawi wa bonde la mto Nile

    Mwana wa Rais wa Uganda Jeneral Muhoozi Kainerugaba ameelezea jinsi anavyounga mkono Misri katika msururu wa ujumbe katika mtandao wake rasmi wa Twitter siku ya Jumapili.

    Jeneral Muhoozi, ambaye alimuangazia rais wa Misri Jenerali Fatah el-Sisi kama bosi wake wa zamani, akisema Uganda itaendelewa kufanya kazi na Misri ili kuhakikisha ustawi katika katika bonde la mto Nile.

    Jenerali, ambaye ni kamanda wa vikosi vya ardhinikatika jeshi la Uganda, alisema alihudumiwa vyema katika mafunzo yake ya miezi sita nchini Misri miaka 10 iliyopita.

    Aliongeza kuwa mtu yeyote atakayepigana na Misri atakuwa vitani na Uganda pia.

    Ujumbe huo ulikosolewa vikali na Waithiopia kupitia kwenye Twitter.

    Uhusiano kati ya Ethiopia na Misri umekumbwa na mvutano kwa miaka kadhaa, kufuatia hatua ya nchi hiyo ya kujenga bwawa kubwa la kuzalisha kawi, katika mto Nile.

    Jenerali Muhoozi aliandika ujumbe mwingine kwenye Twitter kusema kuwa anasikitika kushambuliwa katika mtandao huo.

    Aliikosoa Ethiopia kwa vita katika eneo la Tigray kaskazini mwa nchi hiyo, akisema Watigray ni jamii yake.

    Soma zaidi:

  12. Wanajeshi nchini Guinea wamzuia kwa muda waziri wa zamani

    Utawala mpya wa kijeshi nchini Guineaumemkamata waziri wa zamani siku ya Jumapili na kupekua nyumba yake kabla ya kumuachia saa kadhaa baadye.

    Wanaume waliokuwa wamevalia sara walivamia nyumba ya Tibou Kamara katika mji mkuu wa Conakry wakati wa asubuhi, kumkamata na kumpeleka mahali pasipojulikana. Aliachiliwa huru mwendo wa mchana.

    Vitu kadhaa ikiwemo simu zilichukuliwakutoka kwake.

    Kukamatwa kwake kunaashiria kulithibitishwa na Kamati ya kitaifa ya maridhiano na (CNRD) Pamoja na timu yake.

    Viongozi wa mapinduzi wanamtuhumu kwa kukiuka ahadi ya kutokua na upande wowote katika usimamizi wa jeshi.

    Bw. Kamara alikuwa waziri wa viwanda na mshauri war ais wa zamani Alpha Condé, ambaye alifurushwa madarakani mapema mwezi huu.

    Maelezo zaidi:

  13. Uteuzi wa kocha mpya wa timu ya taifa ya soka Kenya wazua gumzo mitandaoni

    Uteuzi wa kocha mpya wa timu ya taifa ya soka Kenya umezua gumzo mitandaoni.

    Wakenya wamekuwa wakitumia mitandao wa kijamii ya Twitter kuelezea kutoridhishwa kwao na uteuzi wa mkufunzi mpya wa timu ya taifa ya soka Harambe stars Mturuki Engin Farat.

    Shirikisho la Soka la nchini Kenya (FKF) lilitangaza uteuzi wake Siku ya Jumapili kwa kandarasi ya miezi miwili.

    Baadhi ya wakenya wamekuwa wakihoji jinsi Mkuu wa FKF Nick Mwendwa alivyoafikia uteuzi huo.

    Danny Akala aliuliza ni vipi Nick Mwendwa na FKF walivyomteua kocha ambaye hajawahi kushinda mechi yoyote.

    Firat anachukua nafasi ya Jacob 'Ghost' Mulee ambaye alijiuzulu wadhifa huo siku chache zilizopita.

    Mtumiaji mwingine wa mtandao huo JG anamtetea Nick Mwendwa akisema amejitahidi kadri ya uwezo wake kutatua matatizo ambayi yamekua yakiikabili Harambee Stars kwa miaka kadhaa.

  14. Mauaji ya Urusi:Mtu aliyejihami kwa bunduki awaua watu kadhaa katika chuo kikuu cha Perm

    Takriban watu wanane wameuawa wakati mtu mwenye bunduki alipofyatua risasi katika chuo kikuu katika mji wa Perm nchini Urusi, maafisa wanasema.

    Mshambuliaji huyo alitembea hadi chuoni humo Jumatatu asubuhi na kuanza kufyatua risasi.

    Wanafunzi na walimu walijifungia ndani ya jengo la chuo kikuu; wengine walionekana wakiruka kutoka madirisha.

    Haijulikani ni watu wangapi walijeruhiwa. Polisi wa Urusi wanasema kuwa mshambuliaji huyo amezuiliwa.

    Kamati rasmi ya Uchunguzi ya Urusi inasema mshambuliaji huyo alikuwa mwanafunzi katika chuo hicho kikuu.

    Tukio hilo lilitokea katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Perm, kilichoko karibu kilomita 1,300 (maili 800) mashariki mwa mji mkuu, Moscow.

    Video zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha wanafunzi wakirusha vitu vyao kutoka kwa madirisha kwenye majengo ya chuo kikuu kabla ya kuruka kumtoroka mshambuliaji huyo .

    Sehemu hii ya video ya wanafunzi wanaoruka nje ya madirisha ilitangazwa kwenye Runinga ya Urusi:

  15. Mauji ya Wakili wa Kenya Willie Kimani - washtakiwa wote wana kesi ya kujibu

    Mahakama Kuu nchini Kenya imeamua kuwa watuhumiwa wote watano- maafisa wanne wa polisi na raia mmoja- wana kesi ya kujibu kuhusiana na mauaji ya Willie Kimani, wakili aliyetekwa nyara na kuuawa Juni, 2016 akiwa na mteja wake Josephat Mwenda na dereva Joseph Muiruri.

    Upande wa mashtaka ulifunga kesi yake wiki iliyopita baada ya kuwasilisha mashahidi 46. Upande wa utetezi utaanza kuwasilisha hoja zake wiki ijayo.

    Wakili wa utetezi, Cliff Ombeta anasema atawasilisha mashahidi 16. Jaji kisha ataamua ikiwa watano hao wana hatia au la.

    Watatu hao walitoweka baada ya Kimani kuwasilisha kesi dhidi ya afisa wa polisikwa niaba ya Mwenda.

    Wiki moja baadaye, miili ya watatu hao iliyokuwa imeanza kuoza ilipatikana katika mto, viungani mwa mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

    Mauaji yao yalizua ghadhabu kali miongoni mwa wanasheria na Wakenya nchini.

    Kikosi cha polisi kinatuhumiwa kwa msururu wa mauaji ya kiholela katika miaka ya hivi karibuni

  16. Korea Kaskazini:Aukus inaweza kuchochea 'nchi kukimbilia kujihami na zana za kinyuklia

    "Korea Kaskazini imekosoa mkataba mpya wa usalama kati ya Marekani, Uingereza na Australia, ikisema unaweza kusababisha "nchi kukimbilia kujihami na zana za kinyuklia."

    Afisa wa wizara ya mambo ya nje alisema makubaliano ya Aukus "yatasumbua usawa wa kimkakati katika eneo la Asia-Pasifik."

    Mkataba huo utajumuisha Marekani na Uingereza zikiipa Australia teknolojia ya kujenga nyambizi zinazotumia nyuklia.

    Inatazamwa sana kama juhudi ya kukabiliana na ushawishi wa China katika Bahari ya China Kusini inayozozaniwa.

    Mkataba wa Aukus ulitangazwa wiki iliyopita na pia utajumuisha makombora ya meli, akili ya bandia na teknolojia zingine.

    "Hivi ni vitendo visivyofaa na vya hatari ambavyo vitasumbua usawa wa kimkakati katika eneo la Asia-Pasifiki na kusababisha kila nchi kukimbilia kuwa na silaha za nyuklia," amesema afisa wa wizara ya mambo ya nje ya DPRK akirejelea makubaliano ya usalama.

    Wiki iliyopita, Korea Kaskazini ilifanya majaribio mawili makubwa ya silaha - lile la kombora la masafa marefu na kombora la balistiki.

    China pia imekosoa makubaliano hayo na msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Beijing Zhao Lijian amesema muungano huo unahatarisha "kuharibu kabisa amani ya eneo ... na kuimarisha juhudi za kujihami kwa silaha za nyuklia.

    Pyongyang ilisema ni "kawaida kabisa kwa nchi jirani [kama] China kulaani vitendo hivi kama kutowajibika kwa kuharibu amani na utulivu wa eneo hilo."

    Matarajio ya mkataba huo ni kuona Marekani ikishirikisha wengine teknolojia yake ya nyambizi kwa mara ya kwanza katika miaka 60, hapo awali ikiwa ilishirikisha Uingereza mara moja tu.

    Ni nchi gani zilizo na nyambizi?

    Inamaanisha Australia itaweza kujenga nyambizi zenye nguvu za nyuklia ambazo ni haraka mno na ngumu kuzigundua kuliko meli za kawaida.

    Zinaweza kukaa ndani ya maji kwa miezi kadhaa na kudungua makombora ya umbali mrefu - ingawa Australia inasema haina nia ya kuweka silaha za nyuklia ndani yake.

    China haikutajwa moja kwa moja wakati wa tangazo la mpangilio wa usalama.

    Hata hivyo, viongozi wa nchi hizo tatu walitaja mara kwa mara masuala ya usalama wa kikanda ambayo "yameongezeka sana".

    Korea Kaskazini pia ilirejelea taarifa ya hapo awali iliyotolewa na Ufaransa, ambayo ilitaja makubaliano hayo kuwa "usaliti," na kusema kwamba mkataba huo umesababisha "mgogoro mkubwa" kati ya washirika.

    Ufaransa imekuwa ikikosoa mkataba wa Aukus kwasababu ilifikisha ukomo wa makubaliano yenye thamani ya $ 37bn (£ 27bn) yaliyosainiwa na Australia mnamo mwaka 2016 kwa Ufaransa kujenga nyambizi 12 za kawaida.

    Ufaransa inasema iliarifiwa juu ya makubaliano hayo saa chache kabla ya tangazo rasmi kwa umma kutolewa.

    • Ufaransa yajiondoa kutoka mazungumzo ya mkataba wa Ulinzi na Uingereza huku mzozo ukitokota
    • Uingereza, Marekani, Australia kuzindua jeshi kwa jina Aukus kuikabili China
    • Aukus: China yalaani Muungano mpya wa kijeshi kati ya Marekani ,Uingereza na Australia
  17. Rais Samia kulihutubia baraza kuu la UN kuna umuhimu gani kwa Tanzania?

    Wadadisi wa masuala ya kisiasa na kiuchumiwamesifu hatua ya rais wa Tanzania Samua Suluhu kwa uamuzi wake wa kuhudhuria kikao cha 76 za mkutano wa baraza la kuu la umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani .

    Wengi wanahisi hatua hiyo itakuwa na manufaa kwa Tanzania na sio tu kiuchumi bali pia katika kuboresha uhusiano wake wa kidiplomasia .

    Tanzania haijaweza kuhudhuria vikao hivyo vya UN kwa takribani miaka sita na mchambuzi wa masuala ya kisiasa Mohammed AbdulRahman anasema hatua ya rais Samia kwenda katika kikao hicho ni ishara ya kubadilika kwa sera ya taifa hilo kuhusu masuala ya kigeni .

    Anasema rais wa awamu ya tano hayati John Magufuli aliangazia sana maendeleo ya ndani ya nchi lakini mrithi wake anafahamu fika umuhimu pia wa kukuuza ushirikiano na nchi nyingine pamoja na viongozi mbali mbali kupitia vikao kama hivyo .

    Burundi pia ni nchi ambayo inahudhuria kikao hicho baada ya muda mrefu bila viongozi wake kufanya hivyo .

    Rais Samia atahutubia baraza kuu la umoja wa mataifa siku ya Alhamisi ,Septemba tarehe 23 .

  18. Hukumu dhidi ya Rusesabagina kutolewa leo Rwanda

    Mahakama mjini Kigali leo inataraji kutoa hukumu yake dhidi ya Paul Rusesabagina, mkosoaji mkuu wa serikali ya Rwanda.

    Yeye na washirika wenzake 20, watuhumiwa kwa ugaidi ambao unaunahusiana wa mashambulio yaliyofanywa na kundi la waasi la MRCD- FLN dhidi ya Rwanda miaka ya 2018 na 2019.

    Waendesha mashtaka waliomba hukumu ya kifungo cha maisha jela dhidi ya Rusesabagina aliyejitoa katika kesi hiyo mara tu ilipoanza kusikilizwa kwa madai kuwa hawezi kupata haki katika mahakama za Rwanda.

    Juhudi za Bwana Paul Rusesabagina ambaye ni mwanahotelia wa zamani zilisaidia kuwaokoa zaidi ya watu 1200 wakati wa mauaji ya kimbari nchini humo ziliangaziwa katika filamu ya Marekani, Baadaye alikuwa mkosoaji wa serikali ya Rais Paul Kagame.

    Aliishia kushtakiwa na kufungwa nchini Rwanda baada ya kudaiwa kutekwa mjini Dubai. Rwanda imekanusha kumteka.

    Binti yake Carine Karimba ameiambia BBC kwamba hawatarajii haki yoyote kutoka kwa mfumo wa haki wa Rwanda.

    "Tunajua kwamba baba yangu atapatikana na hatia... Hatuna matumaini yoyotekatika mfumo wa haki wa Rwanda...Matumaini yetu yako katika haki ya kimataifa, jamii ya kimataifa," alisema.

    "Baba yangu hakutendewa haki. Haki zote za kimsingi za babangu yangu...Tulijua kuwa hakutakuwa na kesi ya haki kwa baba yangu na sasa ulimwengu unajua pia, "aliongeza.

    • Paul Rusesabagina: Rwanda yakiri kuwa 'iliilipa ' ndege iliyomtoa Dubai na kumpeleka Kigali, bila kujua
    • Watoto wa Rusesabagina wadai baba yao anaamriwa cha kuzungumza na kuwa alikataliwa kuwa na wanasheria huru
  19. Nyuki waua pinguini zaidi ya 60 wa Afrika Kusini walio hatarini

    Pinguini 63 wa Afrika wanaokabiliwa na tishio la kuangamia wameuawa na nyuki katika tukio ambalo sio la kawaida karibu na mji wa Cape Town, wahifadhi wa ndege nchini Afriks Kusini wanasema.

    Ndege hao wanaolindwa, kutoka jamii ya ndege wa Simonstown,walipatikana katika ufukwe wakiwa wameumwa na nyuki.

    Afisa kutoka wakfu wa Afrika Kusini unaohifadhi ndege wa pwaniumelalamikia vifo vya pinguini hao akisema spishi yao tayari inakabiliwa na tisho la kuangamia.

    Nyuki wa asali wa Cape pia ni sehemu ya ekolojia ya mitaaambayo ina maeneo kadhaa ya uhifadhi.

    Pinguini wa Afrika wako kwenye orodha ya Jumuiya ya Kimataifa uhifadhi wa asili.

  20. Uchaguzi Urusi : Chama cha Putin chaongoza wakati kukiwa na madai ya wizi wa kura

    Chama cha Rais Vladimir Putin cha United Russia party kinaonekana kupata ushindi mkubwa wa wabunge, huku kukiwa madai ya wizi wa kura.

    Kura za awali zinatoa utabiri mkubwa wa ushindi kwa chama tawala.

    Wakosoaji wengi wa Kremlin walizuiwa kushiriki katika uchaguzi huo, na kumekuwa na ripoti kadhaa za kura kuibwa na wengine kulazimishwa kupiga kura.

    Tume ya uchaguzi ilikataa madai hayo . Kura zilichagua wabunge 450 kwa bunge la Duma huko Moscow. Jumla ya vyama 14 vilikuwa sehemu ya kura hiyo.

    Katika matokeo ya awali , tume ilisema kwamba 50% ya kura zilizohesabiwa, chama cha United Russia kimepata zaidi ya kura 46%, kikifuatiwa na Chama cha Communist party kwa 21%

    United Russia ilidai kushinda saa chache baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa Jumapili jioni. Televisheni ya taifa ilionesha ofisa wa juu wa United Russia , Andrei Turchak, akiwapongeza wafuasi wake huko Moscow kwa kile alichokuwa akikifafanua kuwa ushindi wa haki na kweli .

    Matokeo ya awali yanaonesha kuwa licha ya kwamba chama cha Putin kinaweza kuwa na viti vingi bungeni , ambapo imepoteza kama moja ya tano ya wafuasi wake.

    Mwaka 2016, chama hicho kilipata ushindi wa 54% ya kura. Chama cha Communists kiliona wafuasi wao waliongezeka kwa 8%.

    Wasiwasi kuhusu hali ya maisha na madai ya rushwa na kufungwa kwa mkosoaji wa Kremlin Alexei Navalny kumeathiri chama cha bwana Putin kuungwa mkono.

    • Uchaguzi wa Urusi: Mambo matano unayohitaji kujua
    • Alexei Navalny: Kwanini kumfunga Navalny kutampa taabu Rais Putin?