Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wanafunzi wapigwa marufuku kuendelea na masomo baada ya kurekodi picha ya ngono DRC
Wanafunzi sita wa sekondari nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wamepigwa marufuku kuhudhuria shule yeyote katika taifa hilo baada ya video ya ngono waliyoshiriki kusambaa mtandaoni.
Moja kwa moja
Rais Kenyatta atangaza ukame kuwa janga la kitaifa Kenya
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta hii leo ametangaza ukame unaoathiri sehemu za nchi ya Kenya kuwa janga la kitaifa.
Bw. Kenyatta ameelekeza hazina na Wizara ya Mambo ya Ndani na kuongoza juhudi za Serikali kusaidia kaya zilizoathiriwa ikiwa ni pamoja na usambazaji wa maji na misaada ya chakula.
Uamuzi huo umetolewa baada ya mkutano wa Leo kati ya Rais na viongozi kutoka maeneo kame nchini wakiongozwa na waziri wa Fedha Ukur Yatani.
Mapinduzi ya Guinea ni kurudi hatua nyuma- Museveni
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametoa wito kwa viongozi wa mapinduzi nchini Guinea ''kuondoka'', akisema kuwa mapinduzi hayo ni ''hatua za kurudi nyuma''.
''Wanapaswa kuambiwa waondoke kwasababu wao si suluhisho la nchi,'' Bw. Museveni aliiambia France 24.
''Tulikuwa nayo mapinduzi miaka ya 1960- yalikuwa sehemu ya matatizo ya Afrika hivyo ninalaani mapinduzi (ndani ya Guinea)''.
Rais wa awamu tatu wa Guinea Alpha Conde aliondolewa madarakani Jumapili na wanajeshi wa kikosi maalumu cha jeshi.
Walimshutumu kwa matumizi mabaya ya ofisi na rushwa.
Mapinduzi yamelaaniwa nje ya taifa hilo, lakini raia wengi wa Guinea wameunga mkono kuondolewa kwa Bw. Condé, 83, huku wakilitaka jeshi kuhakikisha utawala wa kiraia unarejea.
Bwana Museveni ameiambia France 24 kuwa uamuzi wake wa kukubali wakimbizi wa Afghanistan ulikuwa sababu za ''kibinadamu''.
Makaburi ya pamoja yagunduliwa Ethiopia-Maafisa wa Amhara
Maafisa nchini Ethiopia wamewashutumu wapiganaji wa Tigray kwa kuwaua raia 119 katika mkoa wa jirani wa Amhara.
Walisema waligundua makaburi mawili ya pamoja katika wilaya ya Dabat. Maafisa wamesema mauaji yalitekelezwa katika kipindi cha siku mbili mwanzoni mwa mwezi huu.
Wakazi wa kijiji cha China, kilicho umbali wa kilomita kumi kutoka Dabat, walisema kulikuwa na mapigano makali katika eneo hilo.
Mkuu wa wilaya ya Dabat Ato Sewnet Wubalen amesema miili 119 imegundulika lakini wakazi wanasema kuna watu wengine bado hawajulikani walipo.
Miili hiyo ilizikwa tena kwenye uwanja wa kanisa.
Aliongeza kuwa walioathirika '' walikuwa wakulima wasio na hatia, mapadre, watoto na wanawake''.
Maafisa katika eneo hilo waliozungumza na BBC walisema wapiganaji waasi walitekeleza vitendo vya kikatili baada ya kushindwa kwenye mapigano makali yaliyodumu kwa siku 10.
Chama cha TPLF hakijasema lolote kuhusu shutuma dhidi yake kuwa wapiganaji wake waliwaua raia.
Uongozi wa mkoa wa Amhara sasa unadhibiti eneo la China , Gondar Kaskazini lililokuwa limechukuliwa na waasi.
Vita kati ya vikosi vya serikali ya shirikisho na TPLF vilianza mwezi Novemba mwaka jana, vita ambavyo vilisambaa katika mikoa ya jirani mwezi Juni.
Askofu ameacha kazi kwasababu ya mapenzi
Wakati askofu Xavier Novell alipoacha kazi mwezi uliopita, kanisa katoliki lilisema ni kutokana na sababu binafsi bila kutoa maelezo kamili.
Lakini sasa vyombo vya habari vya Uhispania kwasababu alimpenda mwanamke mmoja mwandishi anayeandika simulizi za kusadikika.
Mwaka 2010 akiwa na umri wa miaka 41,alikuwa askofu mdogo zaidi Uhispania kaskazini mashariki mwa mji wa Catalonia.
Aliunga mkono kile kinachoitwa tiba ya uongofu kwa watu wenye mapenzi ya jinsia moja na kutoa mapepo.
Askofu huyo alipata umaarufu katika Kanisa Katoliki la Uhispania, uamuzi wake wa kujiuzulu kwa idhini ya Vatican uliwastaajabisha watu, mwezi uliopita.
Alisema walikutana mara kadhaa na maafisa wa Vatican na vile vile Papa mwenyewe.
Xavier Novell alizoea kutoa kuzungumzia juu ya utoaji mimba na kutoa maoni mkali juu ya mapenzi ya jinsia moja.
Taarifa ya kuacha kazi yake ilishangaza wengi kuwa amempenda Silvia Caballol ambaye alikuwa ameachik.
Silvia alikuwa mwanasaikolijia na mwandishi wa vitabu vya simulizi.
Taarifa zinasema askofu huyo wa zamani sasa anatafuta ajira katika eneo la Barcelona kama mtaalamu wa kilimo.
Wabunge wakamatwa Kenya wakihusishwa na ghasia Laikipia
Wanasiasa wawili wamekamatwa wakihusishwa na ghasia zinazoendelea katika hifadhi ya mazingira ya Laikipia. William Kamket, mbunge ma mbunge wa zamani Mathew Lempurkel, wako kwenye kituo cha polisi wakihojiwa.
Serikali inafanya uchunguzi juu ya kuhusisha siasa katika ghasia hizo zilizosababisha mamia ya watu khama makazi yao.
Mamia ya watu wamekimbia makazi yao wakati ghasia zilipotokea katika hifadhi ya Laikipia iliyopo bonde la Ufa nchini Kenya.
Mamlaka imeonyesha wasiwasi juu ya watu wenye silaha ambao walikuwa wanapambana na polisi.
Zaidi ya watu 12 wameuawa, wakiwemo sita waliouawa wiki iliyopita.
Wanafunzi wapigwa marufuku kuendelea na masomo baada ya kurekodi picha ya ngono DRC
Wanafunzi sita wa sekondari nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wamepigwa marufuku kuhudhuria shule yeyote katika taifa hilo baada ya video ya ngono waliyoshiriki kusambaa mtandaoni.
Wanafunzi hao walifukuzwa shule na waziri wa elimu Tony Mwaba.
Video hiyo ilipigwa picha nje ya shule yao iliyopo mjini Kinshasa, lakini ikiwaonesha wamevaa sare za shule.
Sura tano za wavulana na moja ya msichana zilionekana kwenye video hiyo.
Waziri wa haki za binadamu bwana Albert-Fabrice Puela amesema marufuku hiyo inaminya haki za watoto.
Rais Samia aongoza sherehe za utamaduni
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametawazwa kuwa chifu mkuu wa machifu wote Tanzania na kupewa jina la Hangaya jina linalomaanisha nyota ang’avu.
Katika tamasha la kwanza utamaduni la siku mbili liloandaliwa na machifu wote wa Tanzania nzima likilenga kuhifadhi utamaduni na kuhamasisha utalii wa utamaduni.
Tamasha hilo limehudhuriwa na machifu zaidi ya 100 kutoka makabila yote ya Tanzania ambapo walishudia shughuli mbalimbali za kitamaduni zikiwemo ngoma za asili, kusaga nafaka kwa kutumia mawe, urushaji wa mikuki michezo ya nyoka na mengineyo mengi .
Wakati akifunga tamasha hilo rais Samia amesema ana anzisha rasmi kombe la chifu Hangaya ikiwa ni jitihada za kuendeleza tamasha hilo.
Rais wa Somalia ateua mkuu mpya wa ujasusi
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi "Farmajo" amemteua mkuu mpya wa ujasusi siku chache baada ya waziri mkuu kuchagua mtu mwingine kwa ajili hiyohiyo.
Hatua hiyo inazidisha mvutano kati ya rais na waziri mkuu.
Waziri mkuu Mohamed Roble alimfukuza mkuu wa intelijensia Fahad Yasin baada ya kukaidi agizo lake la kutoa ripoti kamili juu ya wakala wa kijasusi wa kike aliyepotea ndani ya saa 48.
Rais alisema waziri mkuu hakuwa na mamlaka ya kumfukuza mkuu huyo wa intelijensia na kumrudisha.
Rais Farmajo amemteua Yasin Abdullahi Mohamed kukaimu nafasi ya ukuu wa ujasusi .
Mkuu wa intelijensia wa zamani alikuwa anatajwa kuwa mshauri wa rais katika masuala ya usalama.
Hii sio mara ya kwanza kwa rais na waziri mkuu kutofautiana kwa umma.
Mwezi wa nane, waziri mkuu alitembelea Kenya na kusaini mkataba licha ya kwamba rais alikuwa amepiga marufuku mkataba wa kigeni mpaka baada ya uchaguzi.
IMF yatoa mkopo wa dharura wa $567.25,Tanzania
Shirika la Fedha Duniani (IMF) limethibitisha kutoa dola milioni 567.25 kwa ajili ya kusaidia masuala ya dharura ya kifedha nchini Tanzania.
Fedha hiyo itashughulikia gharama za haraka za kiafya, kibinadamu, na masuala ya kiuchumi yanayotokana na athari za janga la COVID-19.
Ufadhili huu umetangazwa baada ya mazungumzo kati ya IMF na Tanzania, chini ya utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kukabiliana na Covid 19.
Hatahivyo IMF ilitoa taarifa juu ya janga la COVID-19 kuathiri vibaya uchumi wa Tanzania, sekta ya afya na ustawi wa idadi ya watu.
Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa ukuaji wa taifa ulipungua mnamo 2020 na unatarajiwa kubaki chini kwa mwaka 2021, ikiongeza kueleza juu ya umasikini na athari katika ajira.
Wakati huo huo mamlaka imejitolea kuimarisha utawala na uwazi ili kuhakikisha kuwa rasilimali za kifedha zinatumiwa vyema kushughulikia mgogoro huo.
Mwezi Machi 2020 Serikali ya Tanzania iliiomba IMF mkopo huo wa dharura kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huo bila mafanikio, kufuatia mazungumzo hayo kuishia njiani. Mwezi Machi mwaka huu, serikali ya Tanzania iliwasilisha tena ombi hilo.
Hata hivyo, mwakilishi huyo wa IMF, Reinke alisema bado mchakato ni mrefu kabla ya kuidhinishwa kwa mkopo huo kwa Tanzania, akisema yapo mambo mengi ya kuzingatiwa mbali na utoaji wa takwimu.
- Virusi vya Corona: IMF yathibitisha itatoa mkopo Tanzania ikitoa takwimu za hali ya corona
Maafisa wafukuzwa kazi Afrika Kusini baada ya Mchungaji Bushiri kutoroka
Maofisa watano wa wizara ya mambo ya ndani nchini Afrika Kusini wamesimamishwa kazi kwa kuwa walishiriki katika kumsaidia mchungaji wa Malawi kwenye nakala za makazi.
Mchungaji Shepherd Bushiri alipata kibali cha makazi cha kudumu jambo ambalo lilizua maswali mengi.
Alikimbia nchi hiyo baada kukwepa kulipa dhamana ya madai udanganyifu na utakatishaji fedha.
Waziri wa mambo ya ndani Aaron Motsoaledi alisema maofisa watano waliadhibiwa baada ya uchunguzi kumalizika.
Waziri alikanusha madai kuhusu idara ya mambo ya ndani na maofisa wake walimsaidia kurahisisha mambo ya mchungaji huyo.
Bwana Bushiri yupo Malawi na kesi yake bado haijaisha.
Mamia wakimbia makazi yao Laikipia, Kenya
Mamia ya watu wamekimbia makazi yao wakati ghasia zilipotokea katika hifadhi ya Laikipia iliyopo bonde la Ufa nchini Kenya.
Mamlaka imeonyesha wasiwasi juu ya watu wenye silaha ambao walikuwa wanapambana na polisi.
Zaidi ya watu 12 wameuawa, wakiwemo sita waliouawa wiki jana
Milio ya risasi ilisikika majira ya mchana, moshi ukionekana huku polisi wakisema ghala la shule moja liliteketea na wanafanya uchunguzi kuhusu tukio hilo .Kupitia taarifa polisi wamesema wanafunzi hawakuwa katika shule hiyo ya Merigwiti iliyodaiwa kuchomwa katika ripoti za vyombo vya habari hapo awali nchini humo .
Wakazi wamekuwa wanakimbia makazi yao ambayo wamekaa kwa miongo kadhaa.
Washambuliaji katika hifadhi binafsi ya Laikipia pia wanalisha mifugo yao kwa jeuri kwenye mashamba ya mahindi ya wakulima wasio na ulinzi.
Kamishna wa eneo la Bonde la Ufa,George Natembeya amedai wavamizi hao wana bunduki aina ya M16 , ambazo haziuzwi nchini humo.
Polisi wa Kenya huwa wanatumia bunduki za G3 na AK47, ambapo mara nyingine watu wasiokuwa na vibali hutumia kufanya ujambazi.Wamesema wanaendelea na oparesheni ya kurejesha utulivu
Bitcoin yapingwa siku ya kwanza baada ya kuhalalishwa El Salvador
Waandamanaji wenye hasira nchini El Salvador, wanapinga kuhalalishwa kwa teknolojia ya fedha ya kidigitali.
Gharama ya Bitcoin siku ya Jumanne, ilishuka katika kiwango cha chini zaidi katika mwezi, ilishuka kutoka $52,000 (£37,730) mpaka $43,000 .
Mwanasiasa mmoja wa upinzani alisema kushuka kwa sarafu hiyo ya kidigitali kumesababisha taifa hilo kupoteza kiasi cha dola milioni tatu ($3m).
Uzinduzi wa Bitcoin nchini El Salvador umekuwa tofauti na kile ambacho Rais Nayib Bukele alikuwa anatarajia wakati akianza jaribio hilo.
Makampuni kama ya Apple na Huawei hayakuiunga mkono serikali katika mpango wake uliofahamika kama 'Chivo', na watumiaji walikuwa wanajitoa baada ya kuona kuwa hawawezi kuendelea na usajili katika makampuni hayo.
Lakini mfumo huo wa Chivo ulianza kupokelewa na majukwaa zaidi na ulikuwa unakubaliwa na kampuni kama Starbucks na McDonald's.
Serikali ilikuwa imetoa $30 ya Bitcoin kwa kila raia ili kuwahamasisha kukubali mfumo huo.
Ilidaiwa kuwa bitcoin ingeweza kukomboa $400m kwa mwaka katika malipo ya kutuma fedha nje ya nchi.
Hata hivyo kwa kutumia takwimu za benki ya dunia na serikali , BBC ilipiga hesabu na kupata kukaribia $170m.
Ed Hernandez anauza duka la familia huko San Salvador ambapo wateja wanaweza kununua mchele maharage na bidhaa za usafi.
"Wakati huu wa janga la corona ni sawa kutumia fedha ya digitali ," aliiambia BBC, anasema inamsaidia kupata hela halali na sio feki.
Moto wateketeza wafungwa 41 gerezani
Watu wapatao 41 wamekufa baada ya moto kutokea katika gereza katika gereza la Indonesia lililopo pembezoni mwa mji mkuu wa Jakarta.
Moto huo ulitokea majira ya asubuhi sana siku ya Jumatano katika gereza la Tangerang wakati wafungwa wengi wakiwa wamelala.
Kulikuwa na wafungwa 122 katika gereza C ambalo liliathiriwa na moto.
Ila gereza lote lina wafungwa 2,000 idadi iliyozidi kiwango cha gereza hilo ambacho ni watu 600.
Wafungwa hao wengi walikuwa wanashikiliwa kwa makosa ya kujihusisha na dawa za kulevya.
Watu kadhaa wanadaiwa kujeruiwa wengine wakiwa kitengo cha mahututi.
Hitilafu ya umeme inadaiwa kuwa chanzo cha moto huo, amesema msemaji wa gereza hilo ingawa amesema pia uchunguzi zaidi unafanyika.
Tazama picha za tamasha la kwanza la utamaduni Tanzania
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Eagan Salla
- Nafasi, BBC Swahili, Dar es Salaam
Tamasha la kwanza la Utamduni wa makabila yote Tanzania limefanyika jijini Mwanza.
Tamasha hilo la siku mbili limeandaliwa na viongozi wa Jadi kutoka kote Tanzania lengo likiwa ni kuuhifadhi utamaduni wao na kuhamasisha Utalii wa Utamaduni Michezo mbalimbali kama vile kucheza na nyoka.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi ambaye pia ndio atalifunga Tamasha hilo kwa kutoa tuzo kwa washindi mbalimbali wa shughuli za kiutamaduni.
Tamasha hili ni tofauti na lile lililozoeleka na wakazi wa Mwanza, Bulabo ambalo ni maalumu kwa kabila la Wasukuma pekee.
Zimbabwe yawataka wafanyakazi wa serikali kupokea chanjo au kujiuzulu
Serikali nchini Zimbabwe imewataka wafanyakazi wake kupata chanjo dhidi ya Covid-19 au wajiuzulu.
Inasema hatua hiyo inalenga kupunguza hatari ya kueneza virusi.
Katika mahojiano na kituo cha redio cha eneo hilo, Waziri wa Sheria Ziyambi Ziyambi anasema kuwa wafanyikazi ambao wanafikiria wana haki ya kuchagua ikiwa wanaweza kupewa chanjo au la wamekosea
Serikali mapema ilianzisha kanuni mpya kwa makanisa na mikahawa ili kuruhusu tu watu walio na kadi ya chanjo ndani ya majengo yao.
Lengo ni kukabiliana na changamoto ya watu kusita kuchanjwa .
Nchi hiyo ya kusini mwa Afrika imeweza kutoa chanjo kamili kwa watu milioni 1.7 pekee
Babake Britney Spears awasilisha rasmi ombi la kujiondoa kama msimamizi wa mali ya binti yake
Baba yake Britney Spears amewasilisha ombi katika mahamaka ya Los Angeles la kusitisha hadhi yake kama mtunzaji au msimamizi wa mali za binti yake aliyokuwa nayo kwa kipindi cha miaka 13 ambayo ilimpa fursa ya kusimamia maisha ya binti yake na fedha zake .
Jamie Spears aliandika kwamba binti yake "ana haki ya kufuatilia na kuhakikisha mahakama sasa inafikiria kwa uzito mkubwa ikiwa hadhi yake ya kumsimamia haihitajiki tena."
Britney Spears amekuwa akitafuta kumwondoa baba yake kwenye jukumu hilo mara mbili katika miaka miwili iliyopita.
Nyota huyo wa muziki aina ya pop ameelezea uhusiano wao kama "unyanyasaji" kiasi cha kukataa kufanya maonyesho chini ya usimamizi wa baba yake.
Hatua ya baba yake kuwasilisha ombi hilo mahakamani inawadia miezi miwili baada ya mwimbaji huyo kutoa ushahidi wa kushtusha mahakamani, akitaka hadhi ya kumtunza aliyo nayo baba yake kusitishwamara moja.
"Matukio ya hivi karibuni yanayohusiana na hadhi ya baba yake yametiliwa shaka ikiwa hali zimebadilika kiasi kwamba sababu za kuanzishwa kwake inawezekana hazipo tena" kulingana na ombi lililowasilishwa kwa mahakama kuu ya Los Angeles Jumanne.
"Bi Spears ameiambia mahakama kwamba anataka kudhibiti maisha yake mwenyewe bila ya msimamizi mtunzaji wake", ombi hilo linasema nakuongeza kuwa Spears ameelezea matumaini yake ya kujisimamia huduma zake za matibabu na kifedha.
Kombe la dunia : Penalti iliyopewa Tanzania baada ya sekunde 5 yaipa ushindidhidi ya Madagascar
Tanzania ilipata moja ya penalti ya haraka zaidi katika historia ya mpira wa miguu wakati Simon Msuva alipochezewa visivyo baada ya sekunde nne tu dhidi ya Madagascar, na matokeo yake ikawa kifua mbele na hatimaye kupata ushindi wa mabao 3-2.
Msuva iliipatia Tanzania matarajio zaidi baada ya kuanza kwa mkwaju maridadi kabisa uliompa kibarua kigumu kipa wa Madagascar, Melvin Adrien aliyejaribu kuuokoa bila mafanikio .
Kwa sekunde tano, mwamuzi alielekeza mpira ili kupigwa penalti hukuErasto Edward Nyoni akibadilisha hali dakika moja baadaye ili kuipa timu yake uongozi wa mapema.
Penalti ya Tanzania inaweza kuwa penalti ya haraka zaidi kutolewa wakati wote, ingawa hii bado haijathibitishwa rasmi.
Mnamo mwaka 2014, Montenegro walipewa penalti baada ya sekunde 10 tu katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Ghana wakati pia kumekuwa na tuzo kwa penalti za chini ya sekunde 10 kwenye mpira wa miguu katika kilabu.
Wenyeji waliendelea kuwa kifua mbele mara mbili zaidi kabla ya mapumziko ya nusu saa ya kwanza kupitia Novatus Dismas Miroshi, lakini Madagascar walijitokeza na kusawazisha hadi 2-2 kufikia wakati wa mapumziko huko Dar es Salaam shukrani kwa Njiva Rakotomarimalala na Thomas Fontaine.
Muda mfupi baada ya mapumziko, Feisal Salum Abdallah alifunga bao jingine na kupa timu hiyo alama za kufuzu kwa Kombe la Dunia kwa kuipeleka Tanzania kileleni mwa Kundi J na alama nne, mbele ya Benin kwa mabao ya kufunga.
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja hivi leo