Rais wa zamani wa Afghanistan Ashraf Ghani yuko UAE huku akidaiwa kubeba dola milioni 169
Balozi wa Afghanistan nchini Tajikstan amedai kwamba rais Ghani alikuwa amebeba dola milioni 169 alipotoroka nchi yake siku ya jumapili .
Moja kwa moja
Asha Juma
Waziri wa Jinsia Uganda afanya utani kuhusu ‘Wakimbizi Warembo’ kutoka Afghanistan
Kufuatia tangazo kwamba wakimbizi wanaokimbia Taliban watakubaliwa kupata hifadhi nchini Uganda, waziri wa jinsia wa nchi hiyo ametania juu ya wanawake wenye kupendeza kuwa miongoni mwao.
"Nimewaona wanaume wetu wa Uganda wakiombea kutua salama kwa wakimbizi wa Afghanistan, na kuzisambaza picha kadhaa za wanawake kama hizi hapa chini," Betty Amongi alisema kwenye Twitter.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
"Wanaahidi kuunga mkono kikamilifu ushirikiano na serikali wakati huu kwenye mradi huu! Natumai sio [Chama] cha Wanaume wa wachoyo," akaongeza, akimaanisha utani mtandaoni juu ya mizaha kuhusu wanaume wasiotaka kutumia fedha zao katika uchumba .
Wengine mtandaoni walicheka pamoja naye lakini wengine waliona haifai, ikizingatiwa hofu kubwa wanayo jinsi wanawake na wasichana wanavyoteswa chini ya utawala wa Taliban.
Bi Amongi aliambia BBC kwamba alikuwa akijibu tu maoni ya watu wengine kwenye mitandao ya kijamii, na ujumbe wake wa twitter ulikuwa tu wa mzaha
Kanisa lamfukuza kazi Padre aliyeonekana akibusu wanafunzi

Kanisa la Anglikana nchini Ghana limemfukuza kazi padre aliyeonekana kwenye video iliyosambaa mtandaoni, akiwabusu wanafunzi.
Kanisa limemfukuza padre Balthazar Obeng Larbi siku ya Jumannne baada ya kukaa kikao na kujadili suala hilo.
Wakati uchunguzi ukiendelea, kanisa limekuja na maamuzi ya kumfukuza padre huyo wa chuo cha Mt. Monica.
Kufukuzwa kwa padre huyo kutawadhihirishia umma hatua waliyoichukua, pamoja na kuwapa ushauri nasaha mabinti watatu walioonekana kwenye video.
Padre Balthazar Obeng Larbi amezuiwa kufanya shughuli zote za utumishi wakati uchunguzi ukiwa unaendelea na kufuata ushauri kutoka kwa kamati iliyoundwa kwa ajili kushughulia suala la padre huyo.
Katika taarifa ya kanisa hilo, imeelezea kusikitishwa na tukio hilo na uchunguzi umeanza mapema.
Taarifa hiyo imeeleza wanafunzi hao watatu watapewa ushauri nasaha ili kuondoa mshtuko waliopata.
Katika mitandao ya kijamii ilisambaa video ikimuonyesha kiongozi wa dini aliyevaa nguo za kijani akiwaita wanafunzi watatu wa kike kwenye mimbari, na kisha akawavua barakoa zao kabla ya kuwabusu, huku kelele za kushangiliwa zikisikika.
"Nimechukizwa sana na hata sielewi. Inawezekanaje hili kutokea kwenye Taasisi ya elimu?," mmoja wa watumiaji wa mtandao wa Twitter aliandika. Mwingine akaandika: "Baba mchungaji anawabusu wanafunzi watatu mbele ya shule nzima. Aibu!"
Ethiopia yashinda dhahabu na Fedha katika mashindano ya Riadha ya wachezaji walio chini ya umri wa miaka 20 Kenya

Chanzo cha picha, Peter Njoroge /BBC
Waethiopia Tadese Worku na Ali Abdilmana wameshindadhahabu na fedha katika mbio za mita 3000 katika siku ya kwanza ya mashindano ya riadha kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20 nchini Kenya .
Waethiopia hao waliongoza kuanzia mwanzo hadi mwishohuku Worku akisajili rekodi ya mudabora wa kibinafsiwa dakika sab aba sekunde 42
Kenya haikuwa na budi ila kusalimu amri baada ya waakilishi wakeDaniel Kinyanjui na Bernard Yegon kumaliza katika nafasi za saba na tisa
Mueritrea Habtom Samuel alishinda medali ya shaba .
Timu ya Kenya yam bio za 4X400m ilifutiliwa nje ya mahsindano baada ya kukiuka kanuniu kwa kuruka kistari wakati wa kupokezana vijiti .

Chanzo cha picha, Peter Njoroge BBC

Chanzo cha picha, Peter Njoroge BBC

Chanzo cha picha, Peter Njoroge BBC

Chanzo cha picha, Peter Njoroge BBC

Chanzo cha picha, Peter Njoroge BBC
Uchunguzi waanzishwa kuhusu ubakaji baada ya ongezeko la idadi ya wasichana wadogo kujifungua
Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha idadi ya kutisha ya wasichana wamepata ujauzito katika mkoa wa Gauteng nchini Afrika Kusini - na visa vingine vya ubakaji bado vinachunguzwa.
Jumla ya watoto 934 walizaliwa na wasichana kati ya miaka 10 na 14 ndani ya mwaka mmoja, waziri wa afya wa Gauteng aliibua jambo hili bungeni. Umri halali wa kuzaa nchini Afrika Kusini ni miaka 16.
Ingawa Baba wa watoto hao hufikiriwa kuwa chini ya umri na wasichana wengi wa umri wa kati nchini Afrika Kusini wanawindwa zaidi na wazee wanaofahamika kama "Sugar daddies” - ambao wanawaahidi pesa na zawadi nyingi.
Walimu pia walihusishwa hapo zamani, na maafisa wa elimu wanasema wale waliopatikana na hatia ya ubakaji wa kisheria wameondolewa kwenye kazi zao.
Mengi zaidi yanahitajika kufanywa kulinda wasichana wadogo na kuwaelimisha vijana kuhusu idhini na matokeo ya ngono, Refiloe Nt’sekhe, kutoka chama cha upinzani cha Democratic Alliance, aliiambia TimesLive
Rais aliyeondolewa madarakani Afghanistan Ashraf Ghani yuko UAE huku akidaiwa kubeba dola milioni 169

Chanzo cha picha, Reuters
Rais aliyetoroka nchi yake ya Afghanistan Ashraf Ghani yupo katika Umoja wa Falme za kiarabu UAE , Wizara ya mashauri ya kigeni ya taifa hilo la Ghuba imetangaza .
" Wizara ya mashauri ya kigeni ya UAE inathibitisha kwamba taifa hili limemkaribisha rais Ashraf Ghani na familia yake kwa misingi ya kibinadamu’ msemaji wa wizara hiyo alisema kupitia taarifa .
Bw. Ghani alitoroka mji mkuu wa Kabul siku ya jumapili wakati wapiganaji wa Taliban walipoukaribia mji huo .
Huku hayo yakiarifiwa balozi wa Afghanistan nchini Tajikstan amedai kwamba rais Ghani alikuwa amebeba dola milioni 169 alipotoroka nchi yake siku ya jumapili .
Alitaja kuondoka kwa Ghani kama ‘usaliti kwa taifa lake’
Balozi Mohammad Zahir Aghbar alikuwa akizungumza na waandishi wa Habari katika mji mkuu wa Tajik Dushanbe.
Pia alitangaza kwamba ubalozi wa nchi hiyo ulipanga kumtambua aliyekuwa naibu wa Ghani Amrullah Saleh kama kaimu wa rais wa Afghanistan
Katika ujumbe wa sauti uliotolewa kwa BBC News jana usiku Bw.Saleh alidai kuwa kiongozi ‘halali wa muda wa Afghanistan’ na kuapa kwamba ‘vita havikuwa vimeisha’
Moshi wa Jenereta waua familia ya watu saba, Nigeria
Familia ya watu saba katika jimbo la Osun kusini magharibi mwa Nigeria imeripotiwa kupoteza maisha baada ya moshi wenye sumu ya hewa ya ukaa, polisi wamethibitisha kuwa ndugu hao ambao walikutwa nane kwenye chumba kimoja ni mmoja tu ndiye alikuwa anapumua.
Msemaji wa polisi,Yemesi Opalola ameiambia BBC kuwa waathirika waligunduliwa na majirani kuwa walikuwa wamefariki wakiwa usingizini.
Hatahivyo polisi bado wanachunguza zaidi kuhusu chanzo cha vifo vya ndugu hao.
Opalola anaamini kuwa hewa ya ukaa iliyotoka kwenye jenereta ndio chanzo cha vifo hivyo.
Ndugu aliyenusurika kifo amewekwa kwenye uwangalizi mkubwa.
Vifo vya aina hii vimeonekana kutokea sana hasa kwenye maeneo ambayo bado hayajaendelea nchini Nigeria kutokana na kukatika kwa umeme.
Mwezi uliopita familia ya watu wanne iliripotiwa kupoteza maisha wakiwa wamelala huko katika jimbo la Kwara mashariki ya kati mwa Nigeria.
Gavana wa Nigeria awataka wananchi kutembea na silaha

Gavana wa jimbo nchini Nigeria amewataka wananchi kununua silaha ili kuanza kujilinda dhidi ya makundi ya wahalifu ambao wameshamiri kuteka watu na kuwalizimisha kuwapa fedha.
Aminu Masari, Gavana wa jimbo la Katsina lililopo kaskazini Magharibi mwa Nigeria amewashaangaa wananchi wanaoendelea kulalamika kuhusu makundi ya wahalifu.
Amesema kuwa wanachofanya wavamizi kimekuwa kikilelewa na wananchi wenye na wala hakuna wa kulaumiwa.
Gavana ameyasema hayo siku ya Jumanne alipotembelea mji wa Jibia ikiwa ni kati ya eneo lililokuwa limeathiriwa na matukio hayo ya uvamizi.
Waziri wa ulinzi wa Nigeria alishambuliwa baada ya kutoa matamshi kama haya ya Gavana.
Raia wengi nchini humo wanasema kuwa matamshi yanayotolewa na baadhi ya viongozi wa juu wa nchi ni kama kushindwa kuweka mikakati bora ya ulinzi na wanataka kuwaachia wananchi majukumu yasiokuwa ya kwao.
Wakosoaji wamesisitiza kuwa ulazimishwaji wa raia katika kununua silaha utaongeza zaidi matukio ya kiuhalifu nchini Nigeria.
Kwa miaka ya hivi karibuni makundi ya kijambazi yanayofahamika kama ‘Bandits’ yameonekana kushamiri, watu wengi wameripotiwa kutekwa na familia zao kulazimishwa kutoa hela ili waachilie
Matukio haya yamewafanya wengi kuacha makazi yao na wengine kupoteza maisha.
Mwanamke aliyepokea fedha kwa bahati mbaya yuko hatarini kufungwa jela
Mwanamke mmoja ambaye ni mfanyabashara Kenya amekutwa na hatia baada ya kukaa na fedha zilizotumwa kwake kwa bahati mbaya, kwa njia ya huduma ya simu.
Mwezi uliopita, Elizabeth Karimi Muthoni alipokea shilingi 271,200 za Kenya ($2,400; £1,700) kutoka kwa Bakar Hussein Mohamed.
Alitoa kiasi cha fedha na alikuwa na mazungumzo na bwana Mohamed kuzirudisha zote, alisema mahakamani.
Siku ya Jumatatu, mwendesha mashtaka wa kaunti ya Kajiado, kusini mwa mji mkuu wa Nairobi, ilimtaka Muthoni kulipa faini ya dola 1,800 na yuko hatarini kufungwa gerezani kwa miaka miwili.
Mwili wa mtumwa uliohifadhiwa vizuri wapatikana Pompeii baada ya miaka 2000

Chanzo cha picha, Archaeological Park of Pompeii/University of Valencia
Mwili wa mtu mmoja aliyekuwa mtumwa ambao ulihifadhiwa vizuri na sehemu yake bado ipo katika hali nzuri umepatikana katika makabauri ya kalekatika mji wa Pompeii.
Mwili huo umekuwa kaburini tangu wakati wa mlipuko ambao uliofunika mji huo katika majivu miaka mingi iliyopita.
Kulingana na maandishi yaliyokuwa kwenye kaburi hilo, mwili huo ni wa mwanaume aliyetambuliwa kama Marcus Venerius Secundio, ambaye alikuwa na miaka 60 na aliwahi kuwa mtumwa.
Baadaye katika maisha yake baada ya kuachiwa huru, Secundio alianza kufanya kazi kama kuhani na kufanya matambiko ya kigiriki na Latini katika mji huo wa Italia .
Mwili wa Secundio' ulikuwa umehifadhiwa katika kaburi lenye michoro ya rangi ya kijani .Nywele zake na sikio lake moja bado vipo katika hali nzuri na vinaweza kuonekana kwa karibu .
Wakenya wanaofanya kazi Afghanistan wataondolewa na waajiri wao
Maelezo ya video, Mkenya azungumzia kuhamishwa kutoka Afghanistan baada ya Taliban kuwasili Wakenya wanaofanya kazi Afghanistan wataondolewa na waajiriwa wao , Wizara ya mambo ya nje imeeleza.
Kwa mujibu wa gazeti la The Standard, limenukuu mahojiano ya katibu mkuu wa mambo ya nje Balozi Macharia Kamau amesema kuwa Kenya haina ubalozi nchini Afghanistan lakini kuna raia wake nchini humo wanaofanya kazi kwenye taasisi za kimataifa .
Aidha Kamau amenukukuliwa tena na gazeti la Daily Nation amesema "Kenya haina mahusiano wa karibu wa kidplomasia na Afghanistan kutokana na kwamba nchi hiyo haijakaa sawa kiusalama kwa muda mrefu hivyo hatukutarajia kuona wakenya wakiishi huko."
Katika mchakato huo wa kuwaondoa raia wake ikiwa nchi hiyo haina ubalozi wake huko, wataalamu wanashauri raia hao kukubali maamuzi yanayokekelezwa na mataifa yao kwa kuwarudisha.
Nchi kadhaa za magharibi zimefanikiwa kurudisha raia wao huku wakiwa wamepanga kuendeleza mpango huo.
Uingereza,Marekani,Ujerumani,Uholanzi pamoja na Pakistan wameweza kuwaondoa raia wake pamoja na ofisi za mabalozi huko Kabul.
Taliban iliweza kuchukua mamlaka nchini Afghanistan baada ya kuiteka miji kadhaa ikiwemo Kabul Jumapili hii, Rais wa taifa hilo Ashraf Ghani alikimbia nchini humo na kusema kuwa asingependelea kuona umwagaji wa damu zaidi.
Siku moja baadae baada ya Taliban kuingia raia walionekana katika kiwanja cha ndege kuikimbia nchi hiyo.
Tetemeko Haiti: Vifo vyaongezeka na kufikia karibu 2,000

Chanzo cha picha, EPA
Watu wapatao 1,941 wamekufa kutokana na tetemeko lililopiga Haiti siku ya Jumamosi.
Watu wapatao 10,000 wamejeruhiwa na wengine wengi hawafahamiki walipo baada ya tetemeko lenye ukubwa wa 7.2 katika vipimo vya Ritcher.
Shughuli ya uokoaji bado inaendelea baada ya mvua kubwa iliyopiga wiki hii.
Umoja wa Mataifa umesema, watoto wapatao 500,000 wanahangaika kupata malazi, maji safi na chakula.
"Familia nyingi za Haiti ambazo zimepoteza kila kitu kutokana na tetemeko la ardhi , sasa hivi wanakaa eneo la maji kutokana na mafuriko," alisema Bruno Maes, mwakilishi wa shirika la kimataifa linaloshughulika na ufadhili kwa watoto (Unicef).

Chanzo cha picha, Getty Images
Watu elfu kumi wamebaki bila makazi kutokana na tetemeko la ardhi na majengo mengi yakiwa yamebaki na nyufa.
Kusini magharibi mwa Haiti kunaonekana kuwa kumeathirika zaidi na tetemeko haswa katika mji wa Les Cayes.
"Jana [Jumanne] jioni, nilipata makazi karibu na kanisani lakini nilisikia ardhi ikitetemeka tena ,nilikimbia na kurudi hapa," mkazi mmoja wa mji wa Magalie Cadet alinukuliwa na wakala wa habari wa AFP.
Aidha baadhi ya hospitali zilikuwa zimelemewa na zilikuwa zina uhitaji wa dawa ili kuweza kutibu waliojeruhiwa.
- Haiti yakumbwa na tetemeko la ardhi la ukubwa wa 7.2
AFCON 2021: Vigogo kushangazwa?

Chanzo cha picha, Getty Images
Droo ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika AFCON 2021 imepangwa jana, huku vigogo na mabingwa watetezi Algeria wamepangwa kundi moja na bingwa wa zamani, Ivory Coast.
Katika sherehe za upangaji wa makundi hayo iliyofanyika jijini Yaounde, Cameroon timu hizo ziko kundi moja la E pamoja na mataifa ya Guinea ya Ikweta na Sierra Leone.
Magwiji wa soka la Afrika kama Didier Drogba, El Hadji Diouf na Samuel Eto'o, waikuwepo kushuhudia upangaji huo wa droo ulioongoza na Rais wa CAF,Patrice Motsepe.
Michuano hiyo inayozijumuisha timu 24 zilizopangwakatika makundi 6 itaanza Januari 9 mpaka Februari 6, 2022 nchini Cameroon.
Timu 6 zitakazoongoza makundi na 6 zitakazoshika nafasi ya pili zitaungana na zingine 4 zitakazokuwa na matokeo mazuri kwenye nafasi ya 3, kucheza hatua ya mtoano.
Je vigogo wako katika hali gani?

Chanzo cha picha, Getty Images
Ukitaja vigogo wa soka Afrika, unataja timu za Ghana, Senegal, Nigeria, Algeria, Cameroon, Tunisia na Misri, kwa kuwa zinaundwa na wachezaji wengi wakubwa wanaocheza soka Ulaya.
Nigeria – bingwa mara tatu wa michuano hiyo ya AFCON –watakutana na mtihani mgumu kwenye kundi D wakipangwa kukutana na Misri, inayoongozwa na Mohamed Salah, nyota wa kutegemewa wa Liverpool. Timu zingine kwenye kundi hilo ni Sudan na Guinea-Bissau.
Senegal, yenye mkali mwingine wa Liverpool, Sadio Mane, ambao walipoteza dhidi ya Algeria katika fainali ya AfCON ya mwaka 2019 wao watakutana na Zimbabwe, Guinea na Malawi kwenye kundi B, ambalo angalau wana haueni.
Wenyeji Cameroon, wanaotafuta taji la sita la AFCON, wako kundi A wakiwa na Ethiopia, Cape Verde na Burkina Faso, ambao watakutana nao katika mechi ya ufunguzi huko Yaounde. Cameroon hapa wana haueni angalau na anatarajiwa kuvuka kuelekea hatua ya mtoano.
Marafiki wanaocheza timu moja ya Arsenal, Thomas Partey na Pierre-Emerick Aubameyang watakutana katika kundi C, wakati Ghana ya Partey itakapokutana na Gabon ya Aubameyang katika kundi hilo lenye timu ya Comoros wanaoingia kwa mara ya kwanza pamoja na vigogo wengine Morocco.
Hapa Morocco na Ghana zinatarajiwa kuvuka hatua inayofuata, huku Gabon ikitarajiwa kuvuka kupitia kapu la mshindi wa tatu
Timu zingine zilizoingia kwa mara ya kwanza Gambia, imepangwa kundi F na kigogo Tunisia, pamoja na timu za Mali na Mauritania.
Hapa Tunisia haitarajiwi kukutana na kikwazo chochote cha kutinga hatua ya mtoano.
Fainali za AFCON 2021 zilipaswa kufanyika mwaka huu, lakini zilisogezwa mbele mara mbili mpaka mwakani kwa sababu ya athari za janga la Korona.
Cameroon ilipangwa kuwa mwenyeji wa fainali hizo mwaka 2019 lakini ilitoswa baada ya maandalizi yako kutoridhisha kabla ya Misri kufanya hivyo.
Makundi ya AFCON 2021:
Kundi A: Cameroon, Burkina Faso, Ethiopia, Cape Verde
Kundi B: Senegal, Zimbabwe, Guinea, Malawi
Kundi C: Morocco, Ghana, Comoros, Gabon
Kundi D: Nigeria, Egypt, Sudan, Guinea-Bissau
Kundi E: Algeria, Sierra Leone, Equatorial Guinea, Ivory Coast
Kundi F: Tunisia, Mali, Mauritania, Gambia
UN: Acheni kuwahamisha wakimbizi wa Afghanstani

Kamishina wa wakimbizi, Filippo Grandi, ameyataka mataifa ya magharibi kuacha kuwaondoa watu Afghanstan kufuatia, uvamizi wa Taliban.
Mataifa kadhaa ya ulaya - ikiwemo Ujerumani na Uholanzi-ambao tayari walitangaza wiki iliyopita kuwa watasitisha zoezi la kuwaondoa watu, mara baada ya Taliban kudhibiti eneo kubwa la nchi nzima ya Afghanstani.
Lakini mataifa kadhaa ya Ulaya yamesema yataendelea kuwaondoa watu. Wiki iliyopita Austria ilitoa onyo kwa tume ya ulaya dhidi ya kuweka zuio la kuwaondoa wakimbizi ambao wanatafuta makazi ulaya.
Bwana Grandi alisema ni muhimu pia kwa mataifa ya jirani ya Afghanistan, haswa Iran na Pakistan,kuacha mipaka yao wazi ili kuweza kuwaruhsu raia wa Afghanstan ambao wana hofu ya usalama wao dhidi ya utawala wa Taliban.Mpango wa muda mrefu unahitajika alisema , bwana Grandi alisema.
Inakadiriwa kuwa raia wa Afghanstan wapatao 550,000 wameondoka nchini kwao tangu Januari, licha ya kuvuka mipaka ya kimataifa kukiwa na vizuizi mpaka sasa.
Mpiga picha anasa picha za Taliban wakitoa kipigo kwa raia
Onyo: Yaliyomo kwenye picha huenda yakakuogopesha
Marcus Yam, mpiga picha na mwandishi wa kigeni wa gazeti LA Times, amekuwa akisimulia tukio aliloshuhudia karibu na uwanja wa ndege wa Kabul Jumanne.
Yam amesema alishuhudia makumi ya watu wa Taliban wakipiga risasi hewani, na silaha zao zikilenga umati wa watu. Aidha walitumia vitu kama vile fimbo, kamba na njia zingine kuwapiga raia.
Picha za ugofya (‘Graphic images he captured’ ) zilizonaswa zinaonyesha angalau mwanamke mmoja aliumizwa na mtoto mdogo akaachwa akiwa anatoka damu kutokana na kile kinachoonekana kuwa jeraha la kichwa.
Yam pia aliandika kwamba yeye mwenyewe alichapwa mguuni wakati anapiga picha matukio yanayoendelea eneo hilo.

Chanzo cha picha, LA Times via Getty
Maelezo ya picha, Mwanahabari alinasa picha za mwanamke na watoto wakiwa wanatiririka damu 
Chanzo cha picha, LA Times via Getty
Maelezo ya picha, Baadhi ya raia kwenye umati walionekana kutamaushwa na vurugu hizo Biden alivunja makubaliano yetu na Taliban: Pence

Maelezo ya picha, Rais Joe Biden wa Marekani Aliyekuwa makamu wa rais wa zamani wa Marekani Mike Pence amejiunga na wale wanaokosoa jinsi Marekani ilivyoondoa majeshi yake Afghanistan, huku maoni yake yakichapishwa katika Jarida la Wall Street.
Akiita kilichotokea kuwa "udhalilishaji wa sera za kigeni tofauti na kitu chochote nchi yetu imevumilia tangu mgogoro wa mateka wa Iran", Bw. Pence alidai Rais Joe Biden alikuwa amevunja mpango wa makubaliano ambao utawala uliopita ulikuwa umekubaliana na Taliban.
Mkataba huo, Bwana Pence alisema, ulikuwa ni kuondoka wanajeshi wa Marekani hatua kwa hatua kutoka Afghanistan maadamu Taliban ilisitishe mashambulizi dhidi ya wafanyikazi wa Marekani, ikatae kuwa eneo salama kwa magaidi na kujadiliana na viongozi wa Afghanistan juu ya kuunda serikali mpya.
Bwana Pence alidai kwamba Rais Biden alivunja mpango huo kwa kutangaza kwamba vikosi vya Marekani vitasalia Afghanistan kwa miezi kadhaa zaidi, na kwamba hii ilichochea Taliban kuanza mashambulizi yao.
Lakini wengine tayari wameanza kukataa tabia iliyojitokeza ya utendaji matukio namna hii.
Msomi na mwandishi wa habari Thomas Joscelyn ameelezea kuwa Taliban walishindwa kutimiza masharti kadhaa vile vile, ingawa alikubali kwamba wapiganaji wengi walijizuia kuwashambulia Wamarekani.
Mkenya ashtakiwa Uingereza kwa kuuza kile alichokiita dawa ya corona

Chanzo cha picha, Google
Maelezo ya picha, Askofu Wiseman anaendesha kanisa la Bishop Climate Ministries ambalo ni sehemu ya Kingdom Church Mhubiri mzaliwa wa Kenya anayeishi Uingereza amefikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kuuza kile alichokiita 'dawa' ya Covid-19.
Askofu Irungu Wiseman wa kanisa la Bishop Climate aliuza chupa zenye mchanganyiko wa mafuta moja ikiwa ni pauni 91.
Alishtakiwa katika mahakama moja mjini London kwa udanganyifu na makosa ya ukosefu wa utendaji haki katika biashara.
Hata hivyo, alikanusha mashitaka hayo.
Bwana Wiseman alitengeneza video na kuzisambaza mtandaoni akidai mafuta hayo ni tiba ya Covid-19.
Hadi kufikia sasa, hakuna tiba ya Covid-19, kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO).
Bwana Wiseman anaendesha kanisa la Bishop Climate Ministries ambalo ni sehemu ya Kanisa la Kingdom Church lililoko London Kusini.
Chatu ashangaza wafanyakazi kwa kujitokeza kwenye rafu za viungo

Maelezo ya picha, Nyoka ajitokeza kwenye rafu Duka la kuuza vyakula liligeuka kuwa hali ya mshike mshike Australia wakati mmiliki wa duka hilo alipoona chatu anayetoka kwenye rafu ya duka.
Helaina Alati, 25, alikuwa katika duka lake huko Sydney siku ya Jumatatu wakati nyoka huyo asiye na sumu mwenye urefu wa mita 3 alipojitokeza.
Duka hilo kubwa lipo pembezoni mwa mji wa viunga vya kaskazini magharibi.
Lakini kuona nyoka kwenye rafu yenye viungo sicho kile Bi Alati alichokitarajia.
Kwa bahati nzuri kwa pande zote mbili, Bi Alati ni mwokoaji wa wanyama pori na anaufahamu uzuri wa nyoka.
"Niligeuza kichwa changu tu na tayari alikuwa karibu sentimita 20 kutoka usoni mwangu, akiniangalia tu moja kwa moja, " aliiambia BBC.
Alifanya uamuzi mara mbili mbili lakini alibaki mtulivu.
Hakuna mtu mwingine aliyekuwa karibu.
Mara moja akagundua ni chatu wa almasi. Bi Alati alijua kwamba nyoka huyo hana sumu hasa baada ya kutoa ulimi wake na kuusimamisha.
"Alikuwa akiniangalia moja kwa moja wakati wote, ni kama alikuwa akisema: "Unaweza kunipeleka nje tafadhali?", amesema.
Baada ya kupiga picha ya nyoka, Bi Alati alitahadharisha wafanyikazi na akasema anaweza kuwasaidia kumtoa.
Alichukua begi la nyoka kutoka nyumbani kwake, akarudi dukani, "akampiga mkia na akaanguka ndani yake."
Kisha alimuacha katika msitu ulio mbali na nyumba hizo,
Msemaji wa Taliban mwenye mazungumzo ya kutisha aliyeamua kuonesha uso wake

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Msemaji wa Taliban Kwa miaka mingi amefanya kazi nyuma ya pazia, sauti tu kupitia simu ndio ilikuwa inasikika.
Lakini siku ya Jumanne, hilo lilibadilika wakati msemaji wa Taliban Zabihullah Majahid alipojitokeza kwenye mkutano wa kwanza na waandishi wa habari wa Taliban.
"Yalda Hakim wa BBC anasema "alishtuka", kuona sura ya mwanamume ambaye alikuwa akiongea naye kwa zaidi ya muongo mmoja, akijibu swali la kwanza kutoka kwa mwandishi wa habari wa kike.
Hakim anaongeza kuwa hilo lililikuwa tofauti na ujumbe mwingine aliokuwa akipokea kutoka kwake.
"Baadhi ya ujumbe ulikuwa ni wenye msimamo mkali Kiisilamu. Wale ambao munafikiri: Mtu huyu ni mwenye kiu ya damu kwa Wamarekani, yeye ni mwenye kiu ya damu kwa mtu yeyote katika serikali ya Afghanistan. "
"Halafu leo amekaa hapo na kusema hakutakuwa na kisasi," Hakim anasema.
"Kwa miaka mingi ametuma ujumbe wa umwagaji damu na sasa ghafla, anataka amani? Ni vugumu sana kuunganisha hilo".
Trump amkosoa Biden jinsi alivyoshughulikia suala la Afghanistan

Maelezo ya picha, Donald Trump Trump amkosoa Biden jinsi alivyoshughulikia suala la Afghanistan katika mahojiano na kituo cha habari cha Fox News.
Rais huyo wa zamani wa Marekani pia alikosoa kujiondoa kwa Joe Biden kutoka Afghanistan, na vile alivyoshughulikia suala la wanaovuka mpaka wa Mexico ambayo idadi yake hivi karibuni imepita ile iliyorekodiwa kwa kipindi cha miongo miwili.
"Angalia kile alichokifanya Biden katika mpaka wa kusini... [hali ilivyo nchini Afghanistan] ni kama mpaka wa kusini lakini imeshughulikiwa vibaya zaidi.
Hakuna mtu aliyeshughulikia suala la mpaka wa kusini vibaya zaidi kuliko yeye, Afghanistan vivyo hivyo", amesema.
Bwana Trump pia alidai kwamba angeshughulikia uondoaji wa majeshi kwa njia tofauti.
"Nilipunguza [jeshi la Marekani nchini Afghanistan] kutoka karibu 20,000 hadi wanajeshi 2,500 - na [sasa wanaondoa] tena wanajeshi kabla hatujatoa raia wetu na wakalimani na watu wengine ... waliotusaidia.
"Sasa basi, tulichokuwa tunatakiwa kufanya ni kuchukua wanajeshi wetu mwisho - watu walikuwa ni wawe wa [kwanza] kuondoka", amesema.
