Uganda kuwapokea wakimbizi 2000 wa Afghanistan

Kundi la kwanza la karibu Waafghanistan 500 linatarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe saa chache zijazo.

Moja kwa moja

Asha Juma

  1. Mpaka hapa tumefikia tamati ya matangazo yetu ya habari za moja kwa moja, tukutane tna kesho majaaliwa

  2. Makamu wa Rais Afghanistan ajitokeza na kudai yeye ndiye Rais baada ya Ghani kuwakimbia Taliban

    h

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Makamu wa Rais wa Afghanistan aliyeondolewa kijeshi yeye na Rais wake, Amrullah Saleh, amesema kwamba yeye ndiye Rais mpya akikaimu madaraka hayo kutoka kwa Ashraf Ghani, Rais aliyetimka nje ya nchi kufuatia kundi la kudhibiti nchi hiyo.

    Salehe aliandika katika mtandao wake wa twitte kwamba, yuko nchini humo na amekwa akiwasiliana na viongozi wote kuomba ridhaa na kuungwa mkono.

    Anasema kwa mujibu wa Katiba ya nchi hiyo, Asipokuwepo Rais kwa mazingira yeyote ama kwa kujiuzulu, kufariki ama kuumwa, Makamu wa Rais anashika nafasi hiyo mpaka uchaguzi.

    Ruka X ujumbe, 1
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 1

    Katika ujumbe wake wa awali alisema kwamba "hajakata tamaa" na kuwataka raia wa nchi hiyo "kuugana nae dhidi ya Taliban" katika ujumbe unaoonyesha kupinga kilichofanywa na Taiban wiki hii.

    Jumapili hii Makamu wa Rais huyo na Mkurugenzi huyo wa zamani wa shirika la ujasusi la nchi hiyo, Bwana Saleh aliapa kwamba "katika mazingira yoyote" hawezi kujisalimisha kwa Taliban.

    Ruka X ujumbe, 2
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 2

    Wakati huo huo aliban msemaji wa kundi la Taliban, Zabihullah Mujahid amezungumza kwa mara ya kwanza na vyombo vya habari na kusema: Hatutaki maadui wa ndani wala wa nje, tunataka kuhakikisha kwamba Afghanistan haiwi tena uwanja wa vita," alisema na kuongeza ' Tumewasamehe wote waliopambana dhidi yetu, tumezika uhasama. Baada ya miaka 20 ya mapambano, tumeikomboa nchi na kuwafurusha wageni, ni jambo la kujivunia kwa nchi nzima," alisema.

  3. Video ya Padri 'aliyewabusu wanafunzi' yazua hasira Ghana

    h

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Kanisa la Anglikana nchini Ghana limeiambia BBC kwamba litachunguza taarifa kuhusu Padri mmoja wa kanisa hilo kuwabusu wanafunzi watatu wa kike katika chuo kimoja nchini humo.

    Lakini pia Kanisa hilo litaangalia namna ya mabinti hao watakavyopatiwa ushauri nasaha "mara baada ya uchunguzi huo kukamilika," alisema George Dawson-Ahmoah wa Dayosisi ya Koforidua.

    Katika mitandao ya kijamii ilisambaa video ikimuonyesha kiongozi wa dini aliyevaa nguo za kijani akiwaita wanafunzi watatu wa kike kwenye mimbari, na kisha akawavua barakoa zao kabla ya kuwabusu, huku kelele za kushangiiwa zikisikika.

    "Nimechukizwa sana na hata sielewi. Inawezekanaje hili kutokea kwenye Taasisi ya elimu?," mmoja wa watumiaji wa mtandao wa Twitter aliandika.

    Mwingine akaandika: "Baba mchungaji anawabusu wanafunzi watatu mbele ya shule nzima. Aibu."

  4. Mahakama Kenya yaamuru Polisi 6 wanaotuhumiwa kwa vifo vya ndugu wawili kukaa ndani kwa siku 14 kupisha uchunguzi

    polisii

    Chanzo cha picha, The Standard Kenya

    Mahakama nchini Kenya imamuru mafisa sita wa polisi nchini humo kuzuiliwa ndani kwa siku 14 ili kutovuruga ushahidi wa kesi ya vifo vya ndugu wawili vilivyotokea mapema mwezi huu.

    Mahakama ya hakimu mkazi ya Miimani Nairobi imetoa amri hiyo ya kuwekwa ndani maafisa hayo ili kusubiri mashataka yao kuhusu vifo vya ndugu hao waliofariki Agosti 1, 2021.

    Awali Mwendesha mashtaka msaidizi wa serikali, Jacinta Nyamosi aliitaka mahakama hiyo kuwaweka ndani maafisa hayo sita ili wasiweze kuingilia ama kuvura ushahidi wa kesi hiyo.

    Hapo jana Mkurugenzi wa mashitaka (DPP) Noordin Haji alimuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi kuwakamata maafisa hao ili kuhojiwa na kujibu tuhuma zinazowakabili.

    Poisi hao wanaoshikiliwa katika kituo cha Polisi cha Nairobi Capito Hill, ni Bension Mputhia, Consolata Kariuki, Nicholas Cheruiyot, Martin Wanyama, Lilian Chemuna na James Mwanki wanaotokea katika kituo cha Polisi cha Manyatta, Embu.

    Ndugu hao Benson Ndwiga na Emanuel Mutura walifariki wakiwa mikononi mwa Polisi huko Kianjakoma katika kaunti ya Embu, muda mfupi baada ya kukamatwa kwa kosa la kukiuka masharti ya Korona.

    Awali taarifa iliyotolewa na maafisa wa Polisi ilieleza kwamba kati ya watu waliokamatwa kutokana na kukiuka masharti ya korona, wawili waliruka wakati gari likienda kwenye barabara ya Kiriare-Buvori na walikuja kubaini hilo baada ya kufika kituo cha polisi.

    Baada ya zoezi la kuwasaka kufanyika walipatikana wakiwa wamekufa na miili yao ilipatika umbali wa mita 35 kati yao. Wamezikwa Ijumaa iliyopita.

  5. Kisa kimoja tu cha Corona chasababisha New Zealand: kufunga shughuli zote nchi nzima

    h

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, New Zeeland ni moja kati ya mataifa machache duniani yaliyoweza kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona.

    New Zealand imetangaza sharti la kutotoka nje kwa nchi nzima na kufunga shughuli mbalimbali baada ya mtu mmoja kubainika kuwa na virusi vya Korona.

    Hicho ni kisa cha kwanza cha korona kubainika katika kipindi cha miezi sita iliyopita. Kisa hicho kimebainika huko Auckland, ambayo sharti la kutotoka nje litakwenda kwa wiki moja, wakati maeneo mengine ya nchi hiyo yatatekeleza sharti hilo la kutotoka nje kwa muda wa siku tatu.

    Mamlaka zinasema zinafanyia kazi kubaini kama kisa hicho kipya ni cha kirusi kipya cha Delta ama la.

    Karibu 20% ya watu nchini humo wamepatiwa chanjo.

    Coromandel, mji uliopo pwani ambapo aliyebainika kuwa na virusi hivyo aliutembelea, nao umekumbana na sharti la kutotoka nje kwa siku saba.

    Waziri mkuu Jacinda Ardern alisema masharti magumu yanapaswa kuwekwa ikiwemo kufungwa kwa shule, maofisi na shughuli za biashara na kuacha huduma muhimu tu ili kujikinga na maambukizi.

    "Nataka kuwahakikishia kuwa New Zealand tumejipanga kkukabiliana na jambo hili.

    Mgonjwa huyo aliyembukizwa ana umri wa miaka 58, ambaye anaelezwa kubainika na maambukizi hayo tangu alhamisi wiki iliyopita.

  6. Waziri Gwajima amtaka Askofu Gwajima athibitishe tuhuma za hongo ya chanjo au akamatwe

    Gwajima

    Chanzo cha picha, MWANANCHI

    Waziri wa afya wa Tanzania, Dk Doroth Gwajima amemtaka Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima nchini humo, Josephat Gwajima kuthibitisha tuhuma alizotoa dhidi yake kuhusu 'kupokea hongo' ili apokee chanjo ya Covid-19.

    Kwa mujibu wa ukurasa wa twitter wa wizara ya afya ya nchi hiyo, Askofu huyo anapaswa kuthibitisha tuhuma hizo alizozitoa hivi karibuni na kuagiza kuviagiza vyombo vya dola kumchukulia hatua mara moja endapo atashindwa kuthibitisha tuhuma hizo.

    Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi la Tanzania, Waziri huyo alitoa agizo la kuhojiwa kwa Askofu Gwajima na vyombo vya dola leo Agosti 17, 2021 akiwa katika kijiji cha Kyatunge, Butiama, mkoani Mara, na kueleza kuwa Askofu Gwajima amekuwa akitoa taarifa za kupotosha kwa makusudi kuhusu chanjo ya corona.

    Waziri Gwajima alisema Askofu Gwajima amekuwa akitoa kauli hizo zinazoivuruga serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Covid 19.

    Siku moja baada ya Tanzania kupokea msaada wa dozi zaidi ya milioni 1 ya chanjo aina ya Johnson Johnson mwezi uliopita kutoka Marekani, Askofu Gwajima aliwaeleza waumini wake wakati wa ibada ya Jumapili iliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba daktari atakaye’shadadia’ suala la chanjo bila kufanya utafiti wa kina ikiwemo madhara yake ya muda mrefu na muda mfupi atakufa.

    Tunalazimisha tena, na mnajiuliza mnalazimishia nini? kama ni hela kiasi gani? kwa ajili yta roho za watu? alihoji Askofu Gwajima na kuongeza ‘Sitamnyamazia mjinga yeyote atakayejibu haya maswali bila kufikiri, ntakusemesha mpaka utatafuta taulo ya kuvaa, unachanja watanzania milioni 60 kwa majaribio?‘ Alihoji Gwajima kwenye ibada kuhusu chanjo kutofanyiwa utafiti wa kutosha.

    Mbali na kauli hizo, Gwajima ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kawe, jijini Dar es Salaaam, ameeendelea kusisitiza mara kadhaa kwenye ibada za Kanisa lake jijini Dar es Salaam kwamba yeye hatochanjwa na waumini wake hawatachanjwa kwa imani kuwa chanjo hizo si salama, kauli ambazo zimekosolewa vikali na wanaounga mkono chanjo wakiwemo viongozi.

    Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba, aliandika kupitia ukurasa wake wa Twitter kwamba kauli ya Askofu Gwajima haikubali na ni hatari.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Aliyekuwa mbunge wa Iringa kutoka chama cha upinzani cha CHADEMA mchungaji Peter Msigwa aliitaka Serikali kumchukulia hatua Askofu Gwajima kwani kauli zake zinaweza kusababisha watanzania wengi zaidi kupoteza maisha.

    Mara kadhaa Serikali ya nchi hiyo hasa baada ya kuingia madarakani kwa Rais Samia Suluhu mwezi Machi mwaka huu, imekuwa ikisisitiza kuwa chanjo zote ilizoziruhusu kutumika nchini humo zimetafitiwa na kwamba ni salama kwa matumuzi ya wananchi wake.

    Mpaka Agosti 15, 2021, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na katibu mkuu wa wizara ya afya ya nchi hiyo,Profesa Abel Makubi watanzania 207,391 walikuwa wameshapatiwa chanjo ya corona.

  7. Uganda kuwapokea wakimbizi 2000 wa Afghanistan

    Wakimbizi wa Afghanistan

    Chanzo cha picha, AFP

    Uganda imesema kuwa itawachukua wakimbizi 2000 wa Afghanistan wanaokimbia mzozo nchini mwao – kufuatia ombi la Marekani.

    Hii inafuatia hatua ya wanamgambo wa Taliban kuchukua uongozi wa nchini hiyo wikendi iliyopita baada ya serikali iliyokuwa madarakani kuanguka.

    Uganda imepongezwa kimataifa kutokana na sera yake ya kuwakaribisha wakimbizi.

    Kundi la kwanza la karibu Waafghanistan 500 linatarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe saa chache zijazo.

    Waziri wa Wakimbizi wa Esther Anyakun ameiambia BBC kwamba Rais Museveni amekubali kuwachukua jumla ya wakimbizi 2000 raia wa Afghanistan – kufuatia ombi la Marekani.

    Aliongeza kuwa watakapofika watafanyiwa vipimo vya corona na kuwekwa karantini. Vifaa na gharama zote zitashughulikiwa na Serikali ya Marekani.

    Uganda itakuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuwapokea watu wanaotoroka ghasia nchini Afghanistan.

    Uganda ambayo imekuwa na historia ya muda mrefu ya kuwakaribisha wakimbizi - kwa sasa ni nyumbani kwa zaidi ya watu milioni moja waliokimbia mzozo na majanga.

    Wakimbizi nchi humo wanaoishi katika makazi au vijijini na wenyeji. Baadhi yao wamepewa kipande cha ardhi na kuruhusiwa kufnaya kazi.

  8. Barcelona ina deni la £1.15bn

    Barcelona

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Barcelona

    Rais wa klabu ya Barcelona Joan Laporta amefichua kwamba klabu hiyo ya Uhispania ina deni la £1.15bn, akiitaja hali hiyo kuwa ya wasiwasi sana.

    Deni la kulipa mishahara ya klabu hiyo kwa sasa ni asilimia 103 ya jumla ya pato lote la klabu.

    Laporta amemlaumu mtangulizi wake Josep Maria Bartomeu kwa deni hilo, akimshutumu kwa kuiwacha klabu hiyo katika hali mbaya.

    ‘’Iwapo tungemuongezea kandarasi Lionel Messi, deni la mishahara lingefikia asilimia 110 ya pato lote, suala ambalo ligi ya La Liga ilikataa kukubali’’.

    Messi alitangaza kuondoka katika klabu hiyo katika hotuba iliojawa na hisia wiki iliopita na kuingia katika kandarasi ya miaka miwili na klabu ya PSG.

    ‘’Mishahara yetu inawakilisha asilimia 103 ya pato la jumla la klabu hii , hiyo ni sawa na kati ya asilimia 20-25 zaidi ya washindani wetu’’, alisema Laporta, akiwa katika kipindi cha pili cha uongozi wake tangu aliposhinda uchaguzi wa mwezi Machi.

    ‘’Kitu cha kwanza tulichofanya tulipowasili tulilazimika kuomba mkopo wa Yuro milioni 80 , la sivyo tungeshindwa kulipa mishahara. Utawala uliopita ulikuwa na udanganyifu chungu nzima’’.

    ‘’Barcelona ina upungufu wa Yuro milioni 451 – ni urithi mbaya sana . Kile ambacho kimekuwa kikifanyika kinatia wasiwasi’’.

    Bartomeu alijitetea katika barua ya wazisiku ya Jumamosi , akidai kwamba mikakati ya kifedha ambayo angeweka iwapo asingelazimishwa kujiuzulumwezi Oktoba ingemruhusu Messi kusalia Barcelona.

  9. Polisi wanaohusishwa na mauaji ya kaka 2 wafikishwa mahakamani Kenya

    Maafisa sita wa polisi wanaohusishwa na vifo vya kaka wawili kutoka eneo la Embu nchini Kenya wamefikishwa mahakamani mjini Nairobi, kulingana na vyombo vya habari nchini humo.

    Jumatatu, mwendesha mashitaka mkuu wa serikali ya Kenya Noordin Haji aliagiza kukamatwa mara moja na kufunguliwa mashitaka mjini Nairobi kwa maafisa wote wa polisi waliohusika na vifo vya kaka hao kutoka kijiji cha Kianjokoma.

    Awali, maafisa hao walikuwa wamesimamishwa kazi baada ya kukamilishwa kwa uchunguzi wa vifo vya kaka hao wawili Benson Njiru, 22, na Emmanuel Mutura, 19. Wawili hao walipatikana wamefariki mapema mwezi huu baada ya kukamatwa na polisi wakati wa saa za kutotoka nje.

    DPP Haji alitoa agizo kwa Jenerali Inspekta wa polisi Hillary Mutyambai katika taarifa ya Jumatatu.

    Alisema kwamba kuhamishwa kwao "kutasaidia kuzuia muingilio wowote wa ushahidi na au kutishwa kwa washukiwa" huku Mamlaka Huru ya Utendakazi wa polisi nchini (IPOA) ikichunguza tukio hilo.

    "Kwasababu hiyo na kwa kutilia maanani umuhimu wa suala hili, tunatarajia kupokea matokea ya uchunguzi wote kuhusu suala hili mwisho wa siku ya leo," DPP alisema.

    DPP aliongeza kuwa maagizo yake yametokana na uchunguzi wa awali uliowasilishwa na kitengo cha masuala ya ndani (IAU).

  10. Mashambulizi ya kijeshi Msumbiji 'yanayokabiliwa na changamoto'

    Mwezi uliopita Rwanda ilituma wanajeshi wake 1,000 kwenda Msumbiji kupigana na wanamgambo

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Mwezi uliopita Rwanda ilituma wanajeshi wake 1,000 kwenda Msumbiji kupigana na wanamgambo

    Mkuu wa jeshi la Msumbiji amesema shambulio linaloendelea katika mkoa wa kaskazini wa Cabo Delgado limekabiliwa na upinzani kidogo kwasababu wapiganaji walioko huko labda huenda walitupilia mbali silaha zao na kujifanya kama raia.

    "Ndiyo sababu tunaendelea kuwafuata na kufanya uchunguzi kwa yeyote anayewasili haswa wale wanaodai wanatoka Palma, ambako kwa muda mrefu hadi hivi karibuni eneo hilo lilikuwa halina watu," Brigedia Chongo Vidgal aliiambia televisheni inayomilikiwa na serikali Jumapili usiku.

    Alisema "asilimia 95 ya wanamgambo walikuwa Msumbiji.

    Mwaka jana kikundi hicho kiliteka mji wenye kuongoza kwa gesi wa Palma na mji wa bandari wa kimkakati wa Mocímboa da Praia.

    Eneo la Mocímboa da Praia lilitekwa tena wiki iliyopita baada ya kampeni iliyoongozwa na wanajeshi wa Rwanda ambao walipelekwa mkoa huo mwezi uliopita kama sehemu ya makubaliano ya nchi mbili.

    Brigedia Vidgal alisema wanajeshi wa Rwanda walikuwa na vifaa bora na kuongeza kuwa wanajeshi wa Msumbiji "wana hisia kubwa ya uzalendo" na walikuwa wakifanya kazi kwa karibu na wenzao.

    Alisema pia kwamba wanajeshi wa Rwanda walikuwa wepesi kutoa taarifa kuhusu ujumbe huo, ikiwemo kushirikishana picha za wanajeshi kwasababu walikuwa na waandishi wa habari ndani ya jeshi.

    "Sisi pia tuko tunakaribisha waandishi wa habari wa kitaifa kufuata mfano huo," alisema.

    Nchi wanachama katika kambi ya ukanda wa kusini mwa Afrika, Sadc, pia wamejiunga na juhudi za kupambana na wanamgambo wa Kiislam kaskazini mwa Msumbiji.

    Zaidi ya watu 3,000 wameuawa huku wengine 820,000 wakitoroka makazi yao tangu kuanza kwa uasi huko Cabo Delgado mnamo mwaka 2017.

  11. Afghanistan: ‘UK na Marekani lazima zilinde Waafghanistan’ – Malala Yousafzai

    Malala Yousafzai
    Maelezo ya picha, Malala Yousafzai

    Rais wa Marekani Joe Biden "ana mengi ya kufanya" na lazima "achukue hatua ya ujasiri" kuwalinda watu wa Afghanistan, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Malala Yousafzai amesema.

    Mwanaharakati huyo wa haki za wanawake wa Pakistani alipata hifadhi nchini Uingereza baada ya kupigwa risasi kichwani na Taliban mnamo 2012.

    Aliiambia kipindi cha BBC cha Newsnight kwamba wakati umewadia kwa viongozi wa ulimwengu - haswa Uingereza na Marekani - kuchukua hatua na kulinda raia na wakimbizi nchini humo.

    "Nchi zinahitaji kufungua mipaka yao kwa wakimbizi wa Afghanistan", alisema.

    Yousafzai, sasa akiwa na umri wa miaka 24, alikuwa na miaka 15 wakati alipolengwa na Taliban kwa kuzungumza juu ya haki ya wasichana kuelimishwa.

    Alinusurika shambulio hilo ambapo mwanamgambo alipanda basi lake la shule kaskazini-magharibi mwa bonde la Swat na akafyatua risasi, akijeruhi marafiki zake wawili wa shule pia.

    Baada ya kupona majeraha mabaya aliyokuwa amepata, yeye na familia yake walihamia Birmingham.

    Akiwa na umri wa miaka 17, baadaye alikua mtu mwenye umri mdogo zaidi kushinda Tuzo ya Amani ya Nobel.

    Alisoma katika Chuo Kikuu cha Oxford, na amekuwa mwanaharakati anayeoongoza wa haki za binadamu.

    "Sio ushindi wa Marekani", Yousafzai amesema hivyo katika mahojiano maalum na BBC Newsnight juu ya shida zinazokumba Afghanistan kipindi hiki.

    Aliongeza: "Ombi langu kwa nchi zote, haswa Marekani, Uingereza, na nchi za magharibi, ni kwamba lazima walinde binadamu wote, wanawake na watetezi wa haki za binadamu. "Na unajua kilichotokea, unajua, tunaweza kubishana juu ya hilo. Lakini tunahitajika pia kuzungumza juu ya hatua tunazohitaji kuchukua. Tunahitaji kuzungumza zaidi juu ya suluhisho hivi sasa."

    Aidha, aliishutumu Marekani kwa kutoa taarifa zisizowajibika wakati Taliban inateka Afghanistan.

    "Nadhani jinsi Marekani ilivyoelezea vita hivi na jinsi ilivyotangazwa kama mshindi, nafikiri hii inatuma picha isiyo ya kweli," alisema.

    "Taliban walingoja kwa miaka ishirini na wao [Marekani] wanadai kile wanachokiita ushindi baada ya hapo."

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, hivi karibuni alisema kwamba ujumbe ulioongozwa na Marekani huko Afghanistan umekuwa wa mafanikio.

  12. Facebook yathibitisha kupiga marufuku maudhui yenye kujihusisha na Taliban

    Kampuni zinazoendeleza teknolojia zakabiliwa na changamoto ya namna ya kushughulikia maudhui ya Taliban

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Kampuni zinazoendeleza teknolojia zakabiliwa na changamoto ya namna ya kushughulikia maudhui ya Taliban

    Mtandao wa kijamii wa Facebook inachukulia Taliban kama kundi la kigaidi na hivyobasi, inapiga marufuku maudhui yote yanayounga mkono Taliban katika majukwaa yao.

    Kampuni ya Facebook imesema timu ya wataalam wa Afghan inafuatilia na kuondoa maudhui yote yenye kufungamana na kundi hilo.

    Facebook imegusia kwamba sera hiyo inatumika kwa majukwaa mengine yote ya mitandao yao ikiwemo Instagram and WhatsApp.

    Hata hivyo, kuna taarifa kwamba Taliban inatumia jukwaa la mawasiliano la Whatsapp kuwasiliana.

    Facebook imeiambia BBC kwamba itachukua hatua ikiwa itabaini akaunti kwenye programu za simu yenye kijihusisha na kundi hilo.

    Majukwaa pinzani ya mitandao ya kijamii kama vile Twitter na Youtube pia nayo yameanza kufuatilia kwa karibu namna ya kushughulikia maudhui ya kundi la Taliban.

  13. "Wamarekani hawastahili kufariki dunia katika vita ambavyo Waafghan wenyewe hawako tayari kujipigania"

    Rais Biden wa Marekani

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, Rais Biden wa Marekani

    Rais wa Marekani Joe Biden ametetea uamuzi wake wa kuondoa majeshi yake nchini Afghanistan licha ya nchi hiyo kutekwa na Taliban haraka mno.

    Hata hivyo, Biden amekubali kuwa matokeo yaliyochangia Taliban kupindua serikali ya Afghan na kuchukua madaraka yalitendeka kwa "haraka sana kuliko ilivyotarajiwa".

    "Wamarekani hawawezi na hawastahili kupigana vita au kufariki dunia katika vita ambavyo Waafghan wenyewe hawako tayari kujipigania," Biden amesema kutoka Ikulu ya Marekani.

    "Nasalia kuwa thabiti na uamuzi wangu," ametoa hakikisho.

    Jumapili, Taliban walitangaza ushindi baada ya rais wa Afghan Ashraf Ghani kutoroka nchi na serikali yake ikaporomoka.

    Wanamgambo wenye msimamo mkali wanarejea serikalini baada ya karibu miaka 20 ya uwepo wa muuungano ulioongozwa na Marekani ambao umeshindwa.

    Uwanja wa ndege wa Kabul

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Picha za vurugu katika uwanja wa ndege wa Kabul kabla ya kuwasili kwa Taliban

    "Marekani haikudhamiria kujenga taifa"

    Biden anakabiliwa na ukosoaji mkubwa kisiasa kutokana na uamuzi wake wa Aprili kuagiza wanajeshi wote wa Marekani kuondoka Afghanistan kufikia Septemba 11, maadhimisho ya miaka 20 tangu kutokea kwa shambulizi lililochochea Marekani kuvamia nchi hiyo.

    Rais alisema kuwa lengo la miaka 20 halikuwa "kujenga nchi," bali kuzuia mashambulizi ya kigaidi katika ardhi ya Marekani.

    "Sitapitisha jukumu hili kwa rais wa tano," ameelezea, akirejelea jambo ambalo amekuwa akilisema tangu alipofanya uamuzi wake wa kuondoka Afghanistan mnamo mwezi Septemba.

    "Nimesikitishwa sana na matukio tunayokabiliana nayo sasa hivi lakini sijutiii uamuzi wangu wa kumaliza vita vya Marekani nchini Afghanistan.

  14. Hujambo na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja hii leo ikiwa ni tarehe 17/08/2021.