Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Jiwe Kubwa la thamani ya dola milioni 100 lapatikana kisimani

"Mtu ambaye alikuwa akichimba kisima hicho alitujulisha juu ya jiwe la kipekee. Baadaye baadaye tulipata jiwe hili la thamani kubwa," Bwana Gamage, mmiliki wa jiwe hilo, aliambia BBC.

Moja kwa moja

Lizzy Masinga

  1. Bilionea aliyeikosoa serikali ya China ahukumiwa kifungo cha miaka 18

    Bilionea mashuhuri wa China amehukumiwa kifungo cha miaka 18 gerezani, ikiwa ni adhabu ya hivi karibuni dhidi ya wamiliki wa makampuni wanaokosoa serikali.

    Sun Dawu anaongoza biashara kubwa kabisa binafsi ya masuala ya kilimo katika wilaya ya Hebei.

    Sun, mwenye miaka 67 awali alikuwa akizungumzia masuala ya haki za binadamu na mada za kisiasa.

    Mashtaka mengine dhidi yake yanahusisha kumiliki ardhi, kukusanya watu kwa ajili ya kushambulia mashirika ya kiserikali na kuwazuia wafanyakazi wa serikali kutekeleza majukumu yao. Pia alitozwa faini ya dola 478,697.

    Alikuwa mmoja wa watu wachache kuishutumu wazi serikali kwa kuficha mlipuko wa homa ya nguruwe ambayo iliathiri mashamba yake mnamo 2019, na baadaye ikaharibu sekta hiyo kwa kiasi kubwa nchini humo.

    Kampuni ya Sun ni miongoni mwa makampuni makubwa China, zikiwa zinajihusisha na usindikaji nyama na vyakula , shule na hospitali.

    Aliripotiwa kukamatwa mwaka jana sambamba na nduguze 20 na wafanyabiashara wenza, kutokana na mgogoro wa ardhi inayoendeshwa na serikali.

  2. 'Tapeli' Hushpuppi akutwa na hatia ya makosa ya utakatishaji fedha

    Mtu mashuhuri katika mtandao wa Instagram raia wa Nigeria Hushpuppi, ambaye jina lake halisi ni Ramon Abbas, amekiri kosa katika mahakama nchini Marekani la utakatishaji fedha

    Alikamatwa, sambamba na washukiwa wengine, huko Dubai mwezi Juni mwaka jana kwa shutuma za ulaghai wa kiasi cha dola milioni 1.1 za Marekani zinazohusishwa na ufadhili wa shule.

    Hushpuppi alirejeshwa Marekani ili kuyakabili mashtaka dhidi yake.

    Nyaraka zake za kujibu mashtaka zimeonesha kuwa alikiri kuhusika katika sakata ya ufadhili wa shule na vitendo vingine vya ulaghai ikiwemo kinachojulikana kama barua pepe za kibiashara na kuwahadaa watu kupitia mitego iliyohusisha dola milioni 24 taarifa ya Ofisi ya mwendesha mashtaka marekani imesema.

    Nyaraka zake za kujibu mashtaka zinaonesha kwamba alikiri kuhusika katika mpango wa fedha za shule na kama shughuli zingine za ulaghai, pamoja na ile inayojulikana kama mipango ya biashara ya barua pepe, ambayo ilifikia $ 24m, taarifa kutoka Ofisi ya Wakili wa Merika inasema.

    Taarifa imeongeza kuwa Hushpuppi alishirikiana na raia wa Kenya na Nigeria kwenye udanganyifu huo wakijifanya washauri na wafanyakazi wa benki kumtampeli mfanyabiashara wa Qatar.

    Hushpuppi alikuwa maarufu sana kwenye mtandao wa Instagram kutokana na mtindo wake wa maisha ya kifahari akimiliki magari mbalimbali ya kifahari.

  3. Kenya na Uingereza zaandaa kwa pamoja mkutano wa elimu duniani

    Mkutano wa kushughulikia mzozo wa elimu ulimwenguni uliosababishwa na janga la Corona unaendelea London.

    Kongamano hilo linaandaliwa kwa pamoja na Uingereza na Kenya, linakusudia kukusanya zaidi ya $ 5bn (£ 3.5bn) kwa mfuko wa kununua vitabu, kufundisha walimu na kujenga madarasa.

    Waziri mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, anatarajiwa kuonya kwamba janga hilo lina hatari ya kuunda "urithi wa talanta iliyopotea".

    Wakati mmoja ilikadiriwa zaidi ya watoto bilioni moja hawakuwa shuleni kwa sababu ya shule kufungwa .

    Wengi bado hawajarudi darasani, haswa katika nchi zinazoendelea.

    Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria na mwanaharakati wa elimu wa Pakistani Malala Yousafzai, ni miongoni mwa wanaohudhuria mkutano huo.

  4. Mzozo waibuka Somalia kuhoji msaada wa masanduku ya kura kutoka UN

    Mzozo umeibuka nchini Somalia juu ya kwanini baadhi ya serikali zingine za majimbo zilipokea misaada ya masanduku ya kura kutoka UN.

    Ofisi ya UN nchini Somalia (UNSOM) ilitoa vifaa vya uchaguzi kwa jimbo la Kusini-Magharibi, televisheni ya kitaifa ya Somali iliripoti.

    Hata hivyo, baadhi ya watu mtandaoni wameitaja hatua hiyo kama "ugonjwa wa utegemezi", wakisema kwamba masanduku ya kura ambayo yametengenezwa kwa plastiki, yanaweza kununuliwa ndani ya nchi.

    Wengine walisema ni aibu kwamba serikali haikuweza kufanya uchaguzi bila kupata misaada.

    Majimbo ya Somalia yanatakiwa kufanya uchaguzi wa bunge na seneti ambao ulicheleweshwa juu ya mizozo kati ya wadau.

    Majimbo hayo yako katika harakati za kuandaa uchaguzi wao wa seneti.

    Jubbaland inatarajiwa kufanya uchaguzi wake Alhamisi (leo).

    Kucheleweshwa kwa uchaguzi siku za nyuma, kulisababisha vurugu kubwa katika mji mkuu Mogadishu wakati viongozi waliposhindwa kukubaliana jinsi uchaguzi utakavyofanyika.

    Hapa kuna baadhi ya ujumbe kutoka mtandao wa Twitter unaoonesha hasira baada ya kupokea misaada ya masanduku ya kura.

  5. Idris Elba: "Sabrina Dhowre amenipa furaha ya kipekee,nampenda sana’

    Muigizaji maarufu Idris Elba na mpenzi wake Sabrina Dhowre wamesema uhusiano wao ni dhabiti sana na ndoa yao inategemea maelewano na mapenzi ya dhati .

    Katika mahojiano ya hivi karibuni na E! huko Marekani wamesema wamefurahia maisha ya ndoa na wanalenga kuishi pamoja kwa miaka mingi ijayo.

    ‘Hapo awali nilikuwa nimesema sitasikika tena kuhusu mambo ya ndoa lakini nikakutana na Sabrina .Tuliamua kuoana.watu wengi walishangaa mbona nilibadilisha mawazo’ amesema Elba

    Sabrina kwa upande wake amesema hana cha kulalamikia kuhusu ndoa yao.

    "Sabrina ni mtu mkarimu sana na ananitunza vyema . Ni yeye nimpendaye.Pia ni mtu muaminifu sana’ amesema Elba

    Idris Elba alikutana na Sabrina katika baa huko Vancouver, Canada mwaka wa 2017 na wakapendana .

    Walioona Aprili mwaka wa 2019 katika jiji la Marrakesh , Morocco.

    Uhusiano na familia ya Sabrina

    Sabrina, ni msichana wa Kisomali-Canada na amesema alimtambulisha Elba kwa familia yake ambapo walimkaribisha vizuri .

    " Kwa kweli mama yangu anamuelewa vizuri sana Elba na anampenda sana’

    Amesema hakuwasikiliza watu wengi walioikosoa ndoa yake na Elba kwa msingi wa dini na utamaduni .Alipoulizwa kuhusu watoto alisema alilenga kupata watoto na Elba .

    Idris Elba ni nani?

    Babake alitoka Sierra Leone na mamake anatoka Ghana .Walioana Sierra Leone na kuhamia London

    Idris alihitimu kutoka shule ya upili mnamo 1988 na akaanza kazi yake katika vilabu vya usiku akifanya kazi kama DJ na pia kuigiza.

    Idris anasifika kwa kuigiza filamu, kufanya kazi kama DJ na pia kufanya muziki wa kufoka.

    Idris Akuna Elba ameoa mara tatu:

    1) Mkewe wa kwanza alikuwa Kim Norgaard na walioana kutoka 1999 hadi 2003 na walikuwa na watoto wawili.

    2) Mkewe wa pili alikuwa Sony Nicole Hamlin ambaye alimuoa mnamo 2006. Walidumu miezi 4 tu.

    3) Wa tatu ni mkewe Sabrina ambaye wapo naye hadi sasa

  6. Unawezaje kumnyonyesha mwanao na pia kushiriki Olimpiki?

    Huku mashindano ya Olimpiki ya Tokyo yakiendelea nchini Japan, washiriki walio na Watoto wachanga walipewa sababu ya kutabasamu kabla ya mashindano kuanzabaada ya kukubaliwa kwamba wanaweza kwenda na wanaowanaonyonya mjini Tokyo .

    Hatua hiyo isilifiwa sana na wanariadha ambao ni wazazi wa kunyonyesha

    Tulizungumza na baadhi wa wanariadha nyota kutoka Kenya ambao pia ni wazazi kuhusu wanavyosawazisha malezi na ndoto ya kupata mafanikiokatika mashindano makubwa kama ya Olimpiki.

  7. Rais wa Tunisia amfuta kazi mkuu wa Televisheni ya Taifa

    Rais wa Tunisia Kais Saeid amemfukuza kazi mkuu wa televisheni ya kitaifa, Mohamed Lissaad Dahech, na kumteua wa kushikilia nafasi hiyo kwa muda.

    Awali, Bw.Saeid aliwafuta kazi maafisa wengi wa serikali.

    Alianza jukumu la uongozi mwishoni mwa juma baada ya kulisimamisha bunge na kumuondoa Waziri Mkuu.

    Wapinzani wa rais wamemshutumu kwa kupanga mapinduzi nchini humo.

    Lakini anasisitiza kuwa ametekeleza wajibu wake ndani ya mamlaka yake wakati wa mzozo nchini humo.

    Tunisia inakabiliwa na changamoto ya kuzorota kwa uchumi na kuongezeka kwa maambukizi ya Covid-19, na kusababisha kuongezeka kwa wasiwasi kimataifa.

  8. Jamaa atumia pikipiki kuiba vito vya thamani ya dola milioni 2.36 Paris

    Polisi huko Paris wanamtafuta mtu aliyeiba vito na mawe ya thamani katika soko la vito vya zaidi ya thamani ya € 2m (£ 1.7m; $ 2.36m).

    Mwanamume huyo anayedhaniwa kuwa na umri wa miaka ya 50 au 60, alifika na kuondoka katika duka la Chaumet kwa kutumia pikipiki inayoendeshwa mtu akiwa amesimama Jumanne alasiri.

    Alitoa silaha na kutishia kuweka bomu alilosema alikuwa ameliweka dukani humo,polisi wanasema

    Sehemu hiyo iko katika eneo linalosemekana kuwa tajiri karibu na Champs-Elysées.

    CCTV ilinasa picha za mtu huyo akiingia dukani akiwa amevaa suti ya rangi ya kijivu na barakoa ya kumziba uso.

    Polisi wanasema alilazimisha wafanyikazi kutoa vito na mawe ya thamani pamoja na funguo za duka, kabla ya kuwafungia wafanyikazi wakati anaondoka.

    Hakuna vurugu zilizotokea kipindi hicho.

    Chaumet ni eneo la vito vya thamani ya juu vilivyoko Paris na maduka kote ulimwenguni.

    Pia ni sehemu ya kikundi cha bidhaa za kifahari maarufu kama LVMH.

  9. Burundi yaridhia kupokea chanjo dhidi ya virusi vya corona

    Burundi imeridhia kupokea chanjo ya Covid , lakini serikali haitawahamasisha watu kupata chanjo hiyo, waziri wa afya nchini humo ameeleza.

    Dkt Thaddée Ndikumana amewaambia waandishi wa habari kuwa chanjo hizo zimependekezwa na Benki ya Dunia na wakachukua uamuzi wa ''kuzikaribisha''.

    Aliongeza, hatahivyo serikali haitahamasisha watu kuchoma chanjo, bali kila atakayehitaji ataifuata chanjo hiyo.

    Mamlaka ya Burundi wamekuwa na wasiwasi kuhusu kupokea chanjo hizo, na hapo awali walisema watafuatilia ufanisi wa chanjo katika maeneo mengine, kabla ya kuzikubali nchini.

    Katika mkutano na wanahabari Alhamisi jioni, waziri alithibitisha ripoti kuwa maambukizi ya virusi vya corona yameongezeka katika wilaya za kaskazini zilizo maeneo ya mpakani na Rwanda, na mji wa kibiashara wa Bujumbura.

    Kwasababu hiyo, amesema watafungua vituo vya tiba katika mikoa iliyoathirika.

    Wizara ya afya ya Burundi hadi sasa imeripoti maambulizi karibu 6,000 vya Covid tangu janga hilo lilipoingia nchini humo mwezi Machi 2020.

  10. Mapigano yapamba moto Amhara wakati vita vya Ethiopia vikiendelea

    Mapigano makali yameripotiwa mkoani Amhara nchini Ethiopia- ishara kuwa vita vya Tigray vinasambaa katika mikoa ya jirani.

    Maafisa mjini Amhara wamesema majeshi ya serikali na vikosi vya Amhara vimehusika katika mapigano dhidi ya waasi wa Tigray People’s Liberation Front (TPLF).

    Hatua hii inakuja wakati mji ikiendelea kutuma vikosi vyake kupambana na TPLF.

    Pamoja na hayo, msemaji wa Waziri Mkuu Abiy Ahmed alisema makubaliano ya usitishaji mapigano uliotangazwa mwezi uliopita hayakutekelezwa.

    Serikali na waasi wa TPLF wamenyoosheana vidole kwa kuchangia kuongezeka mzozo.

    Katika hali tofauti, mamlaka katika mkoa wa magharibi wa Benishangul-Gumuz zinasema vikosi vya usalama vimewaua zaidi ya wapiganaji 100 wenye silaha ambalo limekuwa likitekeleza mashambulizi mengi ya kikabila.

  11. Sri Lanka:Jiwe la thamani ya dola milioni 100 lapatikana kisimani

    Mamlaka nchini Sri Lanka zimesema zimepata jiwe kubwa zaidi la thamani ya mamilioni ya pesa aina ya sapphire bila kutarajia .

    Mfanyabiashara wa vito alisema jiwe hilo lilipatikana na wafanyikazi wakichimba kisima nyumbani kwake katika eneo lenye utajiri wa madini la Ratnapura.

    Wataalam wanasema jiwe hilo, ambalo lina rangi ya samawati, lina thamani inayokadiriwa kufikia dola milioni 100 katika soko la kimataifa.

    Jiwe hilo lina uzani wa karibu kilo 510 au karati milioni 2.5 na limepewa jina la "Serendipity Sapphire".

    "Mtu ambaye alikuwa akichimba kisima hicho alitujulisha juu ya jiwe la kipekee. Baadaye baadaye tulipata jiwe hili la thamani kubwa," Bwana Gamage, mmiliki wa jiwe hilo, aliambia BBC.

    Hakutaka kutoa jina lake kamili au eneo kwa sababu za usalama.

    Bwana Gamage, ambaye ni mfanyabiashara wa vito wa kizazi cha tatu, alijulisha mamlaka juu ya ugunduzi huo, lakini ilichukua zaidi ya mwaka mmoja kusafisha jiwe kuondoa matope na uchafu mwingine kabla hawajalichambua na kulithibitisha.

    Wakati wa mchakato wa kusafisha, Bw Gamage alisema mawe mengine yalitoka yalidondok na yaligunduliwa kuwa yakuti ya ubora wa juu.

    Ratnapura, ambayo inamaanisha jiji la vito katika Sinhalese, unajulikana kama mji mkuu wa madini katika nchi hiyo Asia Kusini. Mawe mengine ya thamani yamepatikana huko zamani.

    Sri Lanka ni muuzaji mkuu wa vito vingine vya thamani.

    Mwaka jana, nchi hito ilipata karibu nusu bilioni ya dola kupitia uuzaji wa kigeniwa vito naalmasi

    "Sijawahi kuona jiwe kubwa la thmani kama kama hilo hapo awali. Hii labda iliundwa karibu miaka milioni 400 iliyopita," Dk Gamini Zoysa, mtaalam mashuhuri wa jiolojia aliambia BBC.

    Wataalam pia wanasema hata hivyo, kwamba ingawa jiwe holo lina thamani kubwa ya karati, mawe yote ndani yake hayawezi kuwa ya ubora wa hali ya juu .

    Utaftaji huo unakuja wakati tasnia ya vito ya Sri Lanka imepata hasara kwa sababu ya janga la Corona .

    Wale wanaofanya kazi katika sekta hiyo wanatumai "Jiwe la Serendipity" sasa litavutia wanunuzi na wataalam wa kimataifa - ingawa jiwe hilo bado halijachambuliwa na kuthibitishwa na wataalam huru wa kimataifa.

    "Ni jiwe la thamani , labda ndio kubwa zaidi ulimwenguni. Kwa ukubwa na thamani yake, tunafikiria itavutia wauzaji wa vito na madini au majumba ya kumbukumbu," Thilak Weerasinghe, Mwenyekiti wa Mamlaka ya Vito nchini Sri Lanka, anasema.

  12. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja hivi leo