Auawa kwa kupigwa risasi kwa kumbaka binti yake
Mwanaume mmoja nchini Somalia auawa kwa kupigwa risasi mpaka kufa huko kusini mwa Somalia na serikali ya Jimbo la Jubaland baada ya kumbaka binti yake wa kambo mwenye umri wa miaka mitatu ambaye alifariki kutokana na majeraha ya kubakwa.
Moja kwa moja
Esther Namuhisa
42 Wafariki kwenye mafuriko Ujerumani

Chanzo cha picha, EPA
Takribani watu 42 wamefariki dunia na wengine kadhaa hawajulikani walipo kufuatia mafurukio makubwa yaliyosababishwa na mvua huko magharibi mwa Ujerumani, Polisi imethibitisha.
Mafuriko hayo yameathiri zaidi majimbo ya Rhineland-Palatinate na Rhine-Westphalia Kaskazini, ambapo majengo kadhaa na magari yamesombwa na maji.
Mafuriko kama hayo yameathiri pia nchi jirani ya Ubelgiji na kusababisha vifo vya watu 6, huku jiji la Liège likiwataka wakazi wake kuhama mara moja.
Mafururiko hayo yanafuatia mvua kubwa kuwahi kunyesha katika eneo la magharibi mwa Ulaya na kusababisha mito mikubwa kupasuka na kumwaga maji kwenye maeneo ya watu.
Nyumba zaidi ya 200,000 hazina umeme huku miundo mbinu kama barabara, reli na mifumo ya maji ikiharibiwa vibaya na mvua hizo zilizonyeshwa kwa zaidi ya saa 24
Mmoja wa viongozi wakubwa wa jimbo la Rhineland-Palatinate Malu Dreyer, ameyaelezea mafuriko hayo kama janga kubwa.
"Kuna vifo, waliopotea na wengine wengi wako kwenye hatari," alisema. "Watoa za dharura wanaendelea na shughuli za uokoaji licha ya kuhatarisha maisha yao."
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, ambaye yuko Marekani kukutana na Rais Joe Biden, amesema ameshitushwa na janga hilo.
Hannah Cloke, profesa kutoka chuo kikuu cha Reading, ameiambia BBC kwamba, kiwango cha vifo vilivyoripotiwa kusababishwa na mafuriko Ulaya kunaonyesha jinsi mifumo iliyopo ilivyoshindwa kufanya kazi.
Baadhi ya mawaziri wa Ujerumani akiwemo waziri wa mazingira, Svenja Schulze aliyeandika katika mtandao wa twitter kwamba: "Mabadiliko ya tabianchi yamewasili Ujerumani", wanaonekana kutoa lawama kwa mabadiliko hayo.
Waziri wa mambo ya ndani Horst Seehofer ameliambia gazeti la Bild kwamba hali ya hewa iliyopo sasa ni athari za wazi za mabadiliko ya tabia nchi, na kutaka nchi hiyo kujiandaa vizuri zaidi.
Nnamdi Kanu aliteswa Kenya-Wakili

Chanzo cha picha, AFP
Wakili wa Nnamdi Kanu, anayeongoza kundi lililopigwa marufuku na ambalo linataka kujitenga kwa jimbo la kusini -mashariki mwa Nigeria, ameiambia BBC kwamba amekutana na mteja wake kwa mara ya kwanza tangu alipokamatwa zaidi ya wiki mbili zilizopita.
Alloy Ejimako amesema kiongozi wa watu wenye asili wa Biafra (Ipob) alionekana amedhoofika akiwa na alama ya kujeruhiwa kwenye mikono na kichwa.
Amesema Bw. Kanu, ambaye anazuiliwa katika kituo kinachoendeshwa na polisi wa Nigeria wanaofanya huduma za siri, alimwambia alizuiliwa na kuteswa Kenya kabla ya kusafirishwa nymbani mwezi uliopita.
Bw. Kanu, ambaye anakabiliwa na mashtaka yanayohusiana na uhaini, alitoroka Nigeria mwaka 2017 akiwa nje kwa dhamana- lakini alizuiliwa mwezi uliopita baada ya kukamatwa na kurejeshwa kutoka nchi ambayo mamlaka imekataa kutaja.
Duru zinaashiria alikamatwa Kenya na kuzuiliwa kwa muda katika ubalozi wa Kenya Nigeria nchini wakati huo.
Bw. Ejimako anasema mteja wake amemfahamisha kuwa alizuiliwa katika kituo cha kibinafsi akiwa amefungwa nyororo kwenye sakafu baridi kwa siku kadhaa
Anadai kuwa alipigwa, kuteswa na kuzuiliwa kuwasiliana kabla ya kuwasilishwa kwa mamlaka ya Nigeria.
Serikali ya Nigeria wala mamlaka ya Kenya hazijatoa tamko lolote kuhusiana na madai hayo.
Bwana Kanu, 53, alianzisha Ipob mnamo 2014 - kundi la hivi karibuni linalotetea nchi ya jamii WaIgbo wa Nigeria.
Mwaka 1967 viongozi wa Igbo walitangaza uhuru wa jimbo la Biafra, baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha vifo vya karibu watu milioni moja, uasi wa kujitenga ulishindwa.
Kesi yake inaendelea Julai 26.
Soma zaidi:
Jinsi mafuta ya kupikia yalivyotumika kuzuia waporaji Afrika Kusini
Wafanyakazi wa maduka makubwa nchini Afrika Kusini katika miji ambayo ina ghasia za waporaji wameamua kumwaga mafuta ya kupikia katika milango ya kuingia katika maduka yao.
Katika maduka ya mji wa Tugela uliopo KwaZulu-Natal, jimbo ambalo kwa siku kadhaa kumekuwa na uporaji katika maduka , maghala na viwanda.
Video hii inaonesha jinsi wafanyakazi wa Shoprite wakimwaga mafuta ikiwa imeshirikishwa mtandaoni.
Meneja wa duka , Mduduzo Sikhakhane, amekiambia chombo cha habari nchini humo -Times Live kuwa hiyo ni mbinu ya kuzuia waporaji wasiingie dukani.
"Hakuna aliyeweza kuingia dukani mwao kwasababu waikuwa wanateleza kama wendawazimu," alisema.
Iliripotiwa kuwa hilo ndio duka pekee ambalo halikuvamiwa katika eneo hilo.
Vindeo nyingine ikiwaonesha watu wakiteleza wakati wakitembea nje ya duka hilo pia imewekwa mtandaoni , huku watu wakisifia jinsi walivyolinda biashara yao.
Uongozi wa Shoprite umesema unarekebisha maduka mengine yaliyoathirika na uporaji na kuanza kuweka bidhaa tena.
Maandamano ambayo yaianzia jimbo la KwaZulu-Natal na Gauteng baada ya rais wa zamani wa Afrika Kusini kufungwa gerezani, na ghasia zikaibuka.
Watu wapatao 72 wamefariki na zaidi ya watu 1,700 wamekamatwa Afrika Kusini katika maandamano mabaya kutokea katika miaka kadhaa.
Kwa mujibu wa kiongozi wa KwaZulu-Natal, Sihle Zikalale, jimbo hilo linakadiriwa kuwa na hasara za kiasi cha dola milioni 206.
Auawa kwa kupigwa risasi kwa kumbaka binti yake
Mwanaume mmoja nchini Somalia ameuawa kwa kupigwa risasi kusini mwa nchi hiyo na serikali ya Jimbo la Jubaland baada ya kumbaka binti yake wa kambo mwenye umri wa miaka mitatu ambaye alifariki kutokana na majeraha ya kubakwa.
Mahakama katika mji wa Dhobley imemkuta Hussein Adan Ali mwenye umri wa miaka 28 na hatia siku ya Jumatano, kama ilivyotangazwa katika kituo cha Televisheni cha eneo hilo.
Viongozi wa jadi na maofisa wa mahakama walipitia ushahidi kabla ya kutekeleza hukumu hiyo.
Kwa mujibu wa ushahidi uliowasilishwa, Ali alikuwa amekula mirungi wakati alipomfanyia unyanyasaji huo mtoto wake.
Haijaweka wazi tukio hilo lilitokea wapi lakini mahakimu wamesema mtoto amefariki Jumatano.
Matangazo ya Televisheni hayakuonesha kama mawakili walihudhuria mahakamani au mshutumiwa kama alipata fursa ya kukata rufaa.
Hukumu hiyo ya kifo ilitolewa chini ya sheria za kiislamu, mahakama ilisema.
Televisheni ya taifa ya Somalia iliweka picha ya Ali katika kurasa yake ya twitter:
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Watanzania walalamikia tozo mpya ya miamala ya simu
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Aboubakar Famau
- Nafasi, BBC News, Dodoma

Nchini Tanzania, hii leo tozo ya miamala ya simu imeanza rasmi ambapo watumiaji wa simu wamejikuta gharama za kutuma na kutolea fedha kwa njia ya simu kuongezeka kwa asilimia mia moja.
Tozo hiyo iliyopewa jina la ‘Tozo ya Uzalendo’ ilipitishwa katika bunge la bajeti mwezi uliopita, ambapo imeongeza makato kwa kila muamala utakaofanyika kupitia njia ya simu.
Hii leo, makampuni ya simu nchini humo, yameweka matangazo magazetini yanayoonyesha viwango vya tozo mpya.Huku baadhi ya viwango hivyo kuonyesha kuongezeka kwa asimilia mia moja.
Waziri wa fedha nchini Tanzania ametetea hatua hiyo kwa kusema fedha hizo zitasaidia kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa madarasa ya shule na kuendelea.
Hata hivyo, tozo hiyo, imekosolewa vikali na wananchi ambao wanahisi itawaongezea mzigo maskini.
Afrika Kusini yaongeza vikosi vya jeshi kupambana na vurugu

Chanzo cha picha, AFP
Serikali ya Afrika Kusini imeongeza vikosi vya jeshi na kufikia 25,000, ambapo ni mara 10 zaidi ya wale waliokuwa wamependekezwa awali ili kukabiliana na watu wanaofanya uporaji na ghasia katika jimbo la Gauteng na KwaZulu-Natal.
Mamlaka imewataka wananchi kutetea biashara zao kwa waporaji ili sheria ichukue mkondo wake.

Chanzo cha picha, AFP
Makumi maelfu ya biashara yameibiwa baada ya rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma kufungwa gerezani kwa makosa ya kutoiheshimu mahakama.
Baadhi ya barabara zimefungwa, majengo yamechomwa moto huku mitaa na maduka yakiwa yamejaa uchafu.

Usiku mmoja maduka makubwa 208 yameripotiwa kuvamiwa ndani ya usiku mmoja.
Hata hivyo maofisa wanasema matukio ya vurugu yamepungua tangu wanajeshi hao 25,000 walivyoanza kazi.
Amhara yaapa kufanya mashambulizi mapya Tigray

Chanzo cha picha, AFP
Mamlaka nchini Ethiopia katika eneo la Amhara imesema watafungua mashtaka dhidi ya jeshi la majirani zao wa Tigray.
Waasi wamechukua maeneo mengi ya Tigray katika wiki za hivi karibuni, na vikosi vya nchi hiyo na washirika wake kuondoka katika maeneo muhimu.
Msemaji wa serikali ya Amhara imesema uvumilivu unawashinda.
"Leo , tumefungua mashtaka".
Wajumbe wa zamani wa usalama wametakiwa kujitolea na kuhamasisha.
Vikosi vya Tigray vikiwa vinaelekea katika eneo la Amhara katika vita ya wenyewe kwa wenyewe . Huku pande zote mbili zikiona kuwa na haki .
Inaonekana kuwa na ari kubwa ambayo inaweza kusababisha damu kumwagika tena na kuanzisha awamu nyingine ya mgogoro.
Awali Ethiopia ilikuwa nchi imara katika Pembe la Afrika na mshirika muhimu wa Magharibi katika vita dhidi ya ugaidi.
Na sasa iko kwenye hatari ya kuongezeka kwa vita zidi na kuwa taifa dhaifu barani Afrika.
Virusi vya corona: Kigali yawekewa tena marufuku ya kutotoka nje

Serikali ya Rwanda imetangaza marufuku ya kutoka nje ya muda wa siku 10 katika mji mkuu wa Kigali na wilaya nane baada ya ripoti za vifo na wagonjwa wa corona kuongezeka.
Watu wametakiwa kutotoka nje ya nyumba zao kuanzia Jumamosi tarehe 17 mpaka tarehe 26 Julai, ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.
Biashara, shughuli za umma na usafiri, shule, michezo na burudani vyote vimefungwa na mazishi yanatakiwa kuhudhuriwa na watu 15 tu.
Watu wanaweza kutoka nje ya nyumba zao kwa ajili ya huduma muhimu pekee au wafanyakazi muhimu.
Wiki nne zilizopita, taifa hilo limerekodi watu elfu moja waliopata maambukizi ya corona kwa siku na siku saba zilizopita hali ilikuwa mbaya zaidi.
Maofisa wa afya wamesema kusambaa kwa wimbi la tatu la kirusi kipya cha Delta ndio kinafanya taifa hilo kuwa na hali mbaya zaidi.
Rwanda imerekodi visa zaidi ya 50,000 vya covid , na zaidi ya waathirika 600 na huku zaidi ya watu mia nne wamepata chanjo.
‘Mshukiwa akiri jinsi alivyowaua watoto 10 asimulia jinsi alivyowafyonza damu waathiriwa'

Chanzo cha picha, twitter
Polisi nchini Kenya wamemkamata mshukiwa wa mauaji mwenye umri wa miaka 20 anayedai kwamba amewaua watoto takribani kumi katika msururu wa visa vya utekaji nyara na mauaji .
Mshukiwa huyo aliyetambuliwa kama Masten Milimu Wanjala aliwaelekeza maafisa wa polisi katika sehemu mbalimbali alikoitupa miili ya waathiriwa wake baada ya kuwaua katika tukio ambalo limewashangaza wengi.
Idara ya jinai kupitia twitter imechapisha taarifa ya simulizi ya mshukiwa huyo na jinsi alivyokuwa akitekeleza mauaji ya kikatili ya watoto ka kuwahadaa wanapokuwa wakicheza.
Polisi wamesema mbinu zake za kutekeleza mauaji ni za kuogofya na amekiri kwamba amekuwa akitumia kemikali inayofanana na unga kwa wathiriwa wake kabla ya kuwaua kwa kuwanyonga au kuwafyonza damu kupitia mishipa .
Miili ya waathiriwa wake wawili ilipatikana katika eneo la Kabete,viungani mwa jiji la Nairobi kisha mwili mwingine ulipatikana jana karibu na eneo hilo hilo pembezoni mwa mto.
Polisi wanasema mshukiwa alianza kutekeleza mauaji ya watoto akiwa na umri wa miaka 16,alipomuua msichana mwenye umri wa miaka 12 aliyetoweka katika Kaunti ya Machakos ,kilomita takriban 54 magharibi mwa mji mkuu Nairobi .
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Polisi wamesema wanaendelea kumhoji mshukiwa ili kutambua sehemu nyingine alikoweka miili ya waathiriwa wake . Wachunguzi wamesema mwanaume huyo aliwaambia kwamba alikuwa akiwafuata watoto hao baada ya kucheza nao kwa muda .
Alikamatwa katika mtaa wa Kitengela mjini Nairobi baada ya uchunguzi kubaini kwamba alikuwa katika sehemu moja ambako watoto wawili walitoweka .
Visa vya kutekwa nyara kwa watoto vimeongezeka mjini Nairobi na polisi wamefanikiwa kuwaokoa watoto kadhaa lakini wengi wamekuwa wakipatikana wameuawa . Polisi maajuzi wameunda kikosi maalum cha kuchunguza na kusuluhisha kei za utekaji nyara jambo ambalo wanasema linatishia usalama wa taifa .
Habari...Karibu katika taarifa zetu za moja kwa moja leo ikiwa ni Alhamisi 15/07/2021.

