Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Moto waibuka katika ibada ya mazishi ya Mchungaji TB Joshua
Moto umewaka Katika ghala lililopo ndani ya kanisa la mhubiri aliyekuwa na ushawishi mkubwa nchini Nigeria TB Joshua mjini Lagos.
Moja kwa moja
Dinah Gahamanyi
Mzozo waibuka kuhusu mazishi ya rais wa zamani wa Zambia Kenneth Kaunda
Baadhi ya wanafamilia ya Rais wa zamani wa Zambia Kenneth Kaunda wamekwenda kortini kujaribu kuzuia mazishi yake katika uwanja wa kitaifa wa Embassy Park katika mji mkuu Lusaka.
Kaunda - rais wa kwanza wa nchi hiyo ambaye alikuwa afisini kutoka 1964 hadi 1991 – aliaga dunia mnamo 17 Juni akiwa na umri wa miaka 97.
Serikali baadaye iliamuru kwamba atazikwa katika eneo la Embassy Park ambapo marais wengine wa zamani wamelazwa. Mazishi hayo yanapaswa kufanyika siku ya Jumatano.
Lakini sasa baadhi ya watoto, wajukuu na vitukuu wa Kaunda wanaomba korti iruhusu kiongozi huyo wa zamani kuzikwa mahali pengine, karibu na mkewe Mama Betty Mutinkhe Kaunda.
Wanasema hii itakuwa kulingana na matakwa yake ya mwisho.
Haijulikani ni wangapi katika familia ya Kaunda wanaounga mkono msimamo huu na ikiwa mazishi yataahirishwa sasa.
Serikali ya Zambia haijatoa tamko juu ya suala hilo.
Ramla Ali aweka historia kwa kuwa Bondia wa kwanza wa kike wa Olimpiki kuiwakilisha Somalia
Ramla Ali, mwanamke wa Kisomali, ameandikisha historia kwa nchi yake kwa mara nyingine, na kuwa mwanamke wa kwanza wa Somali kushriki mashindnao ya Olimpiki.
Ramla ametangaza kwenye Twitter leo kwamba amefuzu kwa Michezo hiyo.
Atakuwa mwanamke wa kwanza kuwahi kushindana kitaalam kwenye Olimpiki akiwakilisha Somalia.
Wakati mashindano ya Olimpiki yakianza mwezi huu, Somalia ina wanariadha wanaowakilisha nchi kwenye mashindano hayo mwaka huu.
Ramla Ali, atajiunga na katika Olimpiki na Munirah Warsame, ambaye pia anawakilisha Somalia uwanjani .
Ramla hatasafiri na timu yake, kulingana na taarifa kwenye Twitter. Walakini, mumewe atakuwa naye.
Watoto milioni 4.5 wanahitaji msaada wadharura Sudan Kusini-UN
Umoja wa Mataifa umeonya kuwa takriban watoto milioni nne na laki tano nchini Sudan Kusini wanahitaji msaada wa dharura kutokana na mzozo wa muda mrefu nchini humo na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Shirika la Umoja wa Mataifa la watoto UNICEF limesema taifa hilo changa zaidi duniani linakabiliwa na mojawapo ya mizozo mibaya zaidi ya kibinadamu duniani.
Ijumaa wiki hii Sudan Kusini inaadhimisha miaka kumi tangu kujinyakulia uhuru lakini Umoja wa Mataifa unasema matumaini ya mwanzo mpya kwa Wasudan Kusini yanadidimia.
Umoja huo umeongeza kusema kuwa maisha ya watoto wengi nchini humo ni ya tabu mno kwani bado wanakumbwa na ghasia, utapia mlo na madhila mengine huku kupunguzwa kwa ufadhili kukifanya hali kuwa mbaya zaidi.
Viongozi wa Sudan Kusini wanajaribu kutekeleza kikamilifu makubaliano ya amani yanayolenga kumaliza mzozo wa miaka mingi.
Serikali mpya ya Israeli yashindwa kurefusha sheria ya utata ya uraia
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Caro Robi
- Nafasi, BBC Swahili
Bunge la Israel limeshindwa kurefusha sheria tata inayowazuia Wapalestina walioolewa na Waisraeli wanaoishi katika ukingo wa Magharibi na ukanda wa Gaza kupata haki ya uraia wa Israel .
Badaa ya kikao cha bunge kilichodumu usiku kucha jana, bunge la Israel lilipiga kura sare ya 59 kwa 59 kuhusu sheria hiyo yenye utata.
Kura hiyo inaonekana mtihani wa kwanza mkubwa kisiasa kwa waziri mkuu Naftali Bennet tangu aingie madarakani mwezi uliopita. Sheria hiyo ambayo wakereketwa wanaitaja kuwa ubaguzi inatarajiwa kuacha kufanya kazi leo Jumanne.
Bwana Bennet alikuwa amewasilisha kura hiyo kuhusu sheria ya uraia kama kipimo cha kura ya imani na serikali yake inayojumuisha chama chake cha kizalendo, vyama vya mrengo wa kushoto, kulia na vya Kiarabu.
Lakini baada ya kikao hicho cha bunge kilichokesha kupiga kura, wabunge hamsini na tisa waliunga mkono hoja ya upande wa serikali, wengine 59 wakapinga na wawili wakasusia kura hiyo wakiwa wabunge kutoka chama cha Waarabu kinachowakilisha Waarabu Waisraeli walio wachache ambao wamo katika serikali ya muungano.
Wanasiasa wa mrengo wa kulia ambao katika kipindi cha nyuma waliunga mkono sheria hiyo wakiongozwa na aliyekuwa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu walipiga kura kuipinga sheria hiyo, hatua inayoonekana ni kumfedhehesha bwana Bennet anayekiongoza chama cha Yamina.
Bwana Netanyahu ambaye sasa ni kiongozi wa upinzani amesema sio kazi ya upinzani kuisaidia serikali kukabiliana na magumu inayokabiliwa nayo.
Sheria hiyo kuhusu uraia na kibali cha kuishi Israel ilipitishwa mwaka 2003 wakati wa wimbi la maandamano ya Wapalestina yaliyoghubikwa na mashambulizi yaliyoilenga Israel kutoka kwa wanamgambo wa Kipalestina .Viongozi wa Israel wamekuwa wakiirefusha kila mwaka tangu wakati huo wakihoji ni kwa sababu za kiusalama.
Maelfu ya Wapalestina walioolewa na raia wa Israel ambao walikuwa hawawezi kupata uraia kuanzia leo sasa wanaweza kufanya hivyo.
Jimbo la Nigeria lafunga shule kutokana na utekeji nyara
Maafisa katika jimbo la kaskazini mwa Nigeria la Kaduna wameamrisha kufungwa mara moja kwa shule katika maeneo yanayokabiliwa na hatari ya mashambulio.
Hii inakuja simu moja baada ya watu wenye silaha kuwateka nyara wanafunzi 150 kutoka shule ya sekondari katika jimbo hilo. Katika tukio jingine tofauti mama mmoja na mtoto mchanga walichukuliwa kutoka hospitali.
Vikosi vya usalama kwa sasa vinawasaka watekaji nyara ili kuwaokoa wahanga.
Kamishna wa jimbo laKaduna wa elimu, Shehu Usman Muhammad, ameiambia BBC kwamba shule zote zilizopo zaidi yaumbali wa dakika 30 kwa gari kutoka kwenye kituo cha usalama zimeamrishwa kufungwa hadi mipango mingineya usalamaitakapofanywa.
Haiko wazi ni hatua gani mpya zitakazochukuliwa huku serikali ikionekana kulemewa na hali mbaya ya usalama inayoendelea kuenea nchini humo.
Awali, majimbo kadhaa kaskazini mwa Nigeria yalifunga shule zake lakini hilo halikutatua mzozo wa utekeji nyara.
Bintimfalme akana baba yake hakuutoroka msukosuko wa Eswatini
Binti wa Mfalme Muswati 11 wa Eswatini amekanusha tetesi kuwa ametoroka nchi kufuatia maandamano ya kuunga mkono demokrasia, yaliyokabiliwa na ghasia na za kukamatwa kwa watu.
Sikhanyiso Dlamini, ambaye anahudumu kama waziri wa Eswatini wa habari na teknolojia, ameiambia BBC kwamba : "Ndio, sisi ni ufalme".
Aliongeza kuwa: Mfalme Muswati ni mchungaji. ‘’Mfalme ni mfalme kwa watu wake. Na hawezi kuwa mfalme kama ataiacha nchi yake nyuma kwa sababu yoyote ile."
Katika siku za hivi karibuni picha za uchomaji na wizi wa mali zimekuwa zikichukuliwa kutoka Eswatini, ambao ndio ufalme wa mwisho uliosalia wenye mamlaka kamili barani Afrika.
Lakini Bi Dlamini ametoa picha tofauti ya matukio ya hivi karibuni, akisema:
"Sisi ni ufalme wa amani na tunaamini katika mazungumzo ya amani. Hakuna sababu yoyote ambayo itafanya haki za watu wetu ziingiliwe kuzuia maombi yao.’’
Ingawa hali ya utulivu imerejea sasa kwenye mitaa ya Eswatini, muungano wenye makao yake ng’ambo unatoa wito wa kufanyika kwa mazungumzo ya upatanishi ya jumuiya ya kikanda ya Afrika , Sadc –pamoja na katiba mpya ya kidemokrasia, kutopigwa marufuku kwa vyama vya kisiasa na mamlaka ya mpito.
Wakati hayo yakijiri Shirika la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limeelezea kuwa na "hofu kubwa" juu ya ghasia za mauaji zilizofuatia maandamano ya kuunga mkono demokrasia katika Eswatini.
"Tumepokea madai ya matumizi ya nguvu yasiyofaa na yasiyo muhimu, unyanyasaji, katika kuzuia maandamano yakiwemo matumizi ya risasi ya polisi ," ilisema taarifa ya Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja huo.
Norway yatoa sheria ya udhibiti wa picha zinazowekwa mitandaoni
‘Kiuno cha nyigu’’, nyonga na makalio makubwa, ngozi nyororo... unapotizama picha kwenye mitandao ya kijamii, wakati mwingine ni vigumu kufahamu ni picha ipi imehaririwa na ile ambayo ni halisi.
Lakini je mtuma picha angekuwa anatoa maelezo kwamba picha hii imefanyiwa uhariri na hii ni halisi ingewasaidia watumiaji kujiamini?.
Sheria mpya nchini Norway sasa inaanza kutekelezwa ambayo itamaanisha kuwa watumiaji wa mitandao ya kijamii wenye ushawishi hawatatuma picha zazo zilizohaririwa bila kusema ni nini wamezifanyia picha zao.
Sheria hii itazihusu jumbe zote za picha zilizplipiwa kwenye majukwa yote ya mitandao ya kijamii, kama sehemu ya juhudi za"kupunguza shinikizo za miili yao’’ambazo watumiaji wa mitandao vijana wanazipata wanapowatazama watu wenye ushawishi kwenye mitandao hiyo.
Madeleine Pedersen, 26, ni mshawishi katika mtandao wa Instagram kutoka Moss nchini Norway.
Anasema "umefika wakati " sheria zibadilishwa na anatumaini sheria hiyo itawazuia vijana kujilinganisha na picha ambazo sio halisi.
"Kuna watu wengi sana ambao wameshindwa kujiamini kutokana na miili yao au uso wao,"anasema.
Obasanjo ajitetea juu ya propaganda za kisiasa dhidi yake
Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo amekanusha ripoti zinazosema kuwa ataunda chama chake cha kisiasa kabl aya uchaguzi mkuu unaotarajiw akufanyika nchini Nigeria mwaka 2023.
Mwishoni mwa juma, magazeti ya Nigeria yaliripoti kwamba rais huyu wa zamani atatekeleza mpango wake wa kuanzisha chama kipya cha kisiasa.
Katika taarifa, yake kwa vyombo vya habari Makamu wa rais Kehinde Akinyemi ameseam kuwa Obasanjo hana mipango ya kubuni chama kipya sasa au "katika siku za zijazo".
Obasanjo alisema wanaopiga propaganda wanapaswa kwenda kwenye hospitali ya magonjwa ya akili kwa ajili ya kufanyiwa kipimo cha skani.
"Nimemaliza suala la siasa lakini kwa nafasi yangu katika Nigeria na katika Afrika kwa ujumla, hupaswi kuzungumzia nafasi yangu duniani. Mlango wangu uko wazi wakati wote kwa wale wanaotaka kunsikiliza. Matendo yangu, nafasi yangu au ushauri wangu juu ya kitu fulani ambacho kinaendelea , ninaweza kufanya mambo yangu, bila kuungwa mkono na mtu yeyote au shirika lolote.
"Kama kungekuwa na chama ambacho Obasanjo angekiunda leo ambacho ni cha usalama, ukosefu wa ajira, njaa na umasikini, na changamoto nyingine zinazoikabiri nchi yangu, kingekuwa chama cha kuwaokoa watu wa Nigeria, kuunganisha nchi , kubuni amani na usalama na uthabiti pamoja na maendeleo , ”amesema Obasanjo.
Mtoto wa rais wa zamani wa Mali asakwa na Interpol
Mmoja wa watoto wa kiume wa rais wa zamani wa Mali Ibrahim Keïta's, Karim, anasakwa na polisi ya kimataifaInterpol kuhusiana na kutoweka kwa mwandishi wa habari mwaka 2016.
Mwandishi wa habari wa Mali, Birama Touré, alipotea baada ya kukutana na Karim akimtaka atoe kauli yake katika katika taarifa aliyokuwa akiifuatilia ambayo ingemuharibia sifa.
Bw Karim alimshitaki muajiri wa mwandishi huyo, Le Sphinx, kwa kumuhusisha na kutoweka kwa mwandishi huo.
Mahakama nchini Mali ilipuuzilia mbali kesi hiyo lakini mhariri wa gazeti alikimbilia uhamishoni.
Bw Karim alikwepa kukamatwa na wanajeshi ambao walimpindua baba yake Agosti 2020.
Inasemekana anaishi katika nchi ya Ivory Coast.
Moto waibuka katika ibada ya mazishi ya Mchungaji TB Joshua
Moto umewaka usiku wa Jumatatu katika ghala lililopo ndani ya kanisa la mhubiri aliyekuwa na ushawishi mkubwa nchini Nigeria TB Joshua mjini Lagos.
Moto huo ulitokea wakati wa mchakato wa mazishi yake ulioanza jana kwa kuwashwa mishumaa kwa ajili ya kumuenzi Nabii TB Joshua aliyefariki mwezi uliopita akiwa na umri wa miaka 57.
Waombolezaji na waumini waliokusanyika katika kanisa lake la Synagogue Church of All Nations kwa ibada ambayo iliongozwa na mjane wa TB Joshua Evelyn Joshua walikanyagana walipokuwa wakitimua mbio kuokoa maisha yao.
Kanisa hilo limesema moto huo ulitokana na hitilafu ndogo ya umeme. Limesema moto huo umezimwa na hapakuwa na mtu yeyote aliyeathiriwa na moto huo.
TB Joshua atazikwa katika eneo la kanisa hilo Ijumaa.
Unaweza pia kusoma:
- Evelyn Joshua: Mfahamu mke wa muhubiri maarufu wa Nigeria TB Joshua
- Temitope Balogun Joshua: Fahamu Utabiri na utata uliomzunguka TB Joshua
- TB Joshua: Haya ndio mambo sita ambayo hukuyajua kumhusu TB Joshua
Sheria za kuvaa barakoa na kukaa mbali hazitakuwa lazima Uingereza
Waziri mkuu, Boris Johnson, alisema alitarajia kupunguza sheria za Covid kumi na tisa katika wiki mbili kutokana na kufanikiwa kwa mpango wa chanjo.
Uvaaji wa barakoa na kukaa mbali zitaondolewa miongoni mwa sheria za lazima katika mwisho wa mpango wa ''lockdown'' ya corona, amethibitisha Waziri Mkuu Boris Johnson.
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Labour, Sir Keir Starmer, aliishutumu serikali kwa kile alichodai ni kuzembea uongozini.
Sheria ya watu sita ndani ya nyumba itaondolewa na muongozo wa watu kufanya kazi nyumbani kwa miezi 16 itaondolewa.
Wazir Mkuu Boris Johnson amesema anatarajia hatua za mwisho zitaendelea kuanzia tarehe 19 Julai kama ilivyopangwa.
Hii itathibitishwa tarehe 12 Julai baada ya tathmini ya data za hivi karibuni kuhusu corona.
Wakati huo huo chama kikuu cha upinzani cha Uingereza kimeishutumu serikali kwa kutowajibika, baada ya kuthibitisha mipango ya kuondoa masharti mengi dhidi ya Corona nchini Uingereza.
Uingereza ni nchi ya kwanza kufanya hivyo wakati maambukizi yakizidi kuongezeka.
Bw Johnson amesema hata baada ya kuondolewa kwa sheria ya kuvaa barakoa binafsi ataendelea kuvaa yake katika maeneo yenye watu wengi kama " adabu’’ .
Hujambo na karibu tena kwa matangazo yetu mubashara leo Jumanne tarehe 06.07.2021