Rais Samia ataka muda zaidi suala la Katiba mpya
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasihi Watanzania kumpa muda wa kushughulikia masuala ya uchumi kabla ya kutazama masuala mengine ya katiba na mikutano ya kisiasa.
Moja kwa moja
Lizzy Masinga
Raia 'wahofia’ kupungua uzito ghafla kwa Kim Jong-un

Chanzo cha picha, EPA/KNCA
Maelezo ya picha, Shirika la habari la KCNA la Korea Kaskazini limetoa picha ya Kim Jong-un akiwa kwenye mkutano wa chama chake Juni 18, 2021 Korea Kaskazini imeonesha video ambayo haijawahi kuoneshwa hapo kabla ya mmoja wa raia wake akionesha wasiwasi wake kuhusiana na hatua ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kupungua uzito ghafla.
Afya ya kiongozi huyo ni nadra sana kuangaziwa na picha yake hudhibitiwa na vyombo vya habari.
Televisheni kuu nchini humo pia imemuonesha Bwana Kim akiwa amepunguza uzito ikilinganishwa na miaka ya hivi karibuni.

Chanzo cha picha, EPA/KNCA
Maelezo ya picha, ... Hii ni picha ya kiongozi wa Korea kaskazini aliyopigwa Februari mwaka huu Kumekuwa na uvumi juu ya afya ya kiongozi huyo wa Korea Kaskazini katika kipindi cha mwongo mmoja ambacho amekuwa madarakani lakini ni nadra sana kwa serikali yake yenye usiri mkubwa.
Je watazamaji wa Korea Kaskazini wameona nini?
Video mbili zilizooneshwa kwenye kituo kikuu cha televisheni cha Korea Central Television, zimesababisha wasiwasi mkubwa kuhusu afya ya kiongozi huyo mkuu wa Korea Kaskazini.
Moja ya picha hiyo imemuonesha akiwasili katika tamasha akiwa amepunguza uzito kweli.
Video ya pili ilikuwa isiyo ya kawaida iliyomuonesha raia wa Pyongyang ambaye alielezea kituo cha televisheni cha Central katika taarifa kuu za habari Ijumaa: "Kumuona [Bwana Kim] akiwa amepunguza uzito kiasi kile, sote tulihuzunika.
"Kila mmoja alianza tu kulia," alisema.
Picha za awali kutoka chama cha kiongozi huyo mapema mwezi huu, zilionesha kuwa Bwana Kim amepunguza uzito.
Rais Samia ataka muda zaidi suala la katiba mpya

Chanzo cha picha, Ikulu Tanzania
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasihi Watanzania kumpa muda wa kushughulikia masuala ya uchumi kabla ya kutazama masuala mengine ya katiba na mikutano ya kisiasa.
Rais Samia ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini Tanzania ambao amekutana nao Ikulu ya Dar es Salaam.
Amewaomba Watanzania apewe muda kwanza ili kuisimamisha nchi kiuchumi kisha atashughulikia masuala mengine.
''Naomba nipeni muda kwanza nisimamishe nchi kiuchumi, tuite wawekezaji wawekeze, ajira zipatikane, halafu tutashughulikia masuala mengine.''
''Tutashughulikia katiba, tutashughulikia mikutano ya hadhara, wakati ukifika.'' Alisema Rais Samia.
Hata hivyo amesema sasa wanaruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano na wau wao, mikutano ya ndani, kamati kuu zinakaa, Halmashauri kuu za vyama vya siasa vinakutana.
Sambamba na hilo wameruhusu pia wabunge kwenye maeneo yao kufanya mikutano ya hadhara.
''Uchumi wetu ni suala la maana zaidi kuliko mengine, sisemi kwamba katiba si ya maana, lakini ninaomba nipeni mud, niisimamishe Tanzania kiuchumi kwanza halafu tutatazama na mengine. Alifafanua Rais Samia.
Makundi ya wanamgambo wa Boko Haram, Iswap yaungana

Chanzo cha picha, AFP
Chini ya miezi miwili baada ya kuuawa kwa kingozi wa Boko Haram Abubakar Shekau katika makabiliano na kundi la IS la Iswap, ripoti zinasema makundi hayo mawili ya jihadi yameungana tena chini ya kamanda mpya.
Hatua hii imekuja wakati mawaziri wa mambo ya nje kutoka katika nchi zaidi ya 40 wanapokutana mjini Roma hii leo kujadili ongezeko la kitisho la kundi la wanamgambo wa IS barani Afrika.
Shirika la habari lenye mahusiano ya karibu na mashirika ya usalama ya Nigeria limesema kuwa kwa pamoja, Boko Haram na wapiganaji wa Iswap walionekana kwenye picha ya video wakiapa utii kwa mamlaka mpya.
Jimbo la Puntland nchini Somalia lawanyonga wapiganaji 21 wa al-Shabab
Wanaume ishirini na moja wameuawa katika jimbo lenye uhuru wa Somalia la Puntland baada ya kupatikana na hatia ya kuwa wanachama wa kundi la wanamgambo wa Kiislam la al-Shabab.
Walihukumiwa na mahakama ya kijeshi huko Galkayo na kupigwa risasi na kikosi maalum kilichojihami kwa bunduki .
Redio ya serikali ilisema kuwa 18 kati yao walikuwa wametekeleza mauaji na ulipuaji wa mabomu kwa zaidi ya muongo mmoja.
Hukumu kama hizo za kifo zilikuwa zimetolewa na mahakama katika maeneo mengine ya Somalia hapo awali.
Lakini hii inaripotiwa kuwa idadi kubwa zaidi ya mauaji ya wafuasi wa al-Shabab kuwahi kutokea Puntland.
Mamlaka huko Puntland zilikuwa zimeapa kuwafikisha mahakamani wafuasi wa al-Shabab au watu watakaopatikana wakisaidia kundi hilo katika mashambulio yake.
Mwanaharakati wa Chadema, Mdude Nyagali aachiwa huru
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Munira Hussein
- Nafasi, BBC Africa

Chanzo cha picha, MDUDE NYAGALI/ FACEBOOK
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya imemuachia huru Mdude Nyagali baada ya kutomkuta na hatia katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya kusafirisha madawa ya kulevya.
Chama cha Upinzani Chadema kimeandika katika ukurasa wake wa Twitter kuhusu kuachiwa kwa mwanaharakati huyo.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Hukumu hiyo imefikiwa hii leo baada ya kuahirishwa tarehe 14 mwezi Juni mwaka huu.
Mdude alikuwa akikabiliwa na shtaka la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin gramu 23.4 mwaka 2020.
Mdude alikuwa akikosoa utendaji kazi wa serikali ya chama tawala CCM kwenye majukwaa ya kisiasa pamoja na mitandao ya kijamii.
Pia Mdude aliwahi kushtakiwa kwa kosa la uchochezi dhidi ya serikali.
Marufuku ya kutotoka nje yatangazwa baada ya milipuko ya mabomu DRC

Chanzo cha picha, AFP
Mamlaka za mji wa Beni ulio mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo siku ya Jumapili zilitangaza amri ya kutotoka nje kufuatia milipuko miwili ya mabomu kwa siku moja.
"Sitaki kuona mtu yeyote mtaani," meya wa jiji hilo, Kanali Narcisse Muteba, alisema, akitahadharisha kuwa taarifa kuhusu mipango ya mashambulizi zaidi.
Katika tukio la hivi karibuni mtu aliyekuwa amebeba bomu alikufa wakati lilipolipuka nje ya kilabu cha pombe.
Mapema Jumapili takribani watu wawili walijeruhiwa wakati bomu kulipuka ndani ya Kanisa Katoliki katika mji huo huo.
Ilitokea muda mfupi kabla ya sherehe ya kipaimara cha watoto kuanza.
Ingawa haijulikani bado ni nani aliyehusika na milipuko hiyo, kikundi cha waasi waADF - hufanya mashambulio ya mara kwa mara katika mkoa huo na imeyalenga makanisa hapo awali.
Mnamo Mei, maimamu wawili wanaojulikana kwa kuwakosoa waasi wa ADF walipigwa risasi na kuuawa - mmoja wao ndani ya msikiti.
Watu waliojihami waua watu 15 na kuchoma moto mabasi Burundi

Takriban watu 15 wameuawa katikati mwa Burundi, ripoti za vyombo vya habari nchini humo zinaripoti.
Shambulio hilo Jumamosi jioni lilikuwa katika mkoa wa Muramvya, ambapo watu 12 walifariki katika shambulio kama hilo mwezi Mei.
Kulingana na walioshuhudia tukio hilo, watu wenye silaha walifunga barabara kwa mawe makubwa wakati wa giza kisha wakayafyatulia risasi magari hayo.
Mabasi mawili yalichomwa moto. Abiria kadhaa waliojeruhiwa walipelekwa hospitalini.
Wizara ya mambo ya ndani ya Burundi ilielezea shambulio hilo kuwa la ugaidi. Haijulikani ni nani aliyehusika
Matokeo ya Tuzo za BET yalivyopokelewa Tanzania

Hisia mbalimbali zimeanza kutolewa mitandaoni nchini Tanzania baada ya ushindi wa mwanamuziki wa Nigeria Burna boy katika tuzo za BET .
Damini Ebunoluwa Ogulu maarufu Burna boy aliwashinda wapinzani wake wakuu katika tuzo hiyo ya kimataifa wanamuziki Naseeb Abdul Juma wa Tanzania maarufu Diamond Platinumz na Wizkid kutoka Nigeria.
Na punde tu baada ya tuzo hizo kutangazwa baadhi ya Watanzania waliokuwa wakiendesha kampeni ya pingamizi dhidi ya Diamond mtandaoni wakiwa na lengo la mwanamuziki huyo kuondolewa katika tuzo hizo walifurahi.
Mmoja ya waanzilishi wa kampeni hiyo na wanaharakati wa haki za kibinadamu nchini humo Maria Sarungi aliandika :
‘’Asanteni sana ❤️ wapendwa!
Mtu asikwambie kuwa sauti yako haina nguvu!
Wakati tunaanza najua watawala walitubeza, kama kutukana tumetukanwa lakini hamkukata tamaa
Sasa tuendelee kudai HAKI na Uwajibikaji kwa enablers and collaborators wote ✊’’
Ruka X ujumbe, 1Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Badala yake Bi Sarungi alimpongeza mshindi wa Tuzo hiyo Burnaboy.
Ruka X ujumbe, 2Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
hatahivyo kuna wale waliokuwa wakimpigia Debe Diamond Platinumz kushinda tuzo hiyo, waliodai kwamba wale walioanzisha kampeni hiyo hawakuwa na uzalendo.
Ruka X ujumbe, 3Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 3
Msemaji wa serikali ya Tanzania Gerison Msigwa hakuwachwa nyuma katika mjadala huo ambapo amempongeza Diamond kwa kuwakilisha taifa hilo, akisema kwamba licha ya msanii huyo kutofauti alileta heshima kubwa kwa Tanzania.
Aliandika katika mtandao wa Twitter akisema: ‘’Watanzania tunajua wewe ni Mshindi, Mpambanaji, Mzalendo wa kweli na Mwanamuziki bora sana Afrika na Duniani. Tutaipata wakati mwingine’’.
Ruka X ujumbe, 4Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 4
Diamond akitoa shukran zake za dhati kwa wale waliomuunga mkono kwa dhati akisema kwamba kupitia tuzo hiyo ameoana upendo na umoja wa Watanzania.
Ruka Instagram ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa Instagram ujumbe
Aliongezea kwamba ni faraja kuona Dunia inapotaja nchi zenye Wanamuziki bora Tanzania inatajwa.
Waliopokea Chanjo ya AstraZeneca ya India kunyimwa pasi maalum ya kuingia Ulaya

Chanzo cha picha, Reuters
Pasi maalumu ya Umoja wa Ulaya, itakayoanza kutumika tarehe 1 mwezi Julai kurahisisha safari kwenda Ulaya kwa wale waliopata chanjo itaanza kufanya kazi lakini ikiwa na sharti moja muhimu
Mtu yeyote aliyepewa chanjo ya AstraZeneca inayozalishwa na Taasisi ya Serum ya India hatastahiki kupata pasi hiyo- na hiyo inajumuisha raia wengi wa nchi za kipato cha chini na cha kati ambao walipatiwa chanjo zilizosambazwa na mpango wa COVAX uliofadhiliwa na WHO.
Hii ni kwasababu pasi maalumu ya Umoja wa Ulaya itatambua tu toleo la Vaxzevria la chanjo ya AstraZeneca ambayo ilitengenezwa nchini Uingereza au maeneo mengine ya Ulaya, na hivyo kupitishwa na Wakala wa Dawa wa Ulaya (EMA).Kwa upande mwingine, ununuzi na usambazaji mkubwa wa chanjo chini ya mpango wa COVAX unahusisha chanjo ya AstraZeneca, iliyotengenezwa na Taasisi ya Serum ya India.
Wakati hayo yakijiri, Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametahadharisha uwepo "ubinafsi wa chanjo" ulimwenguni lakini akasema "itawaamsha" Waafrika kujitosheleza.
Rais Museveni amesema kuwa Afrika wanahitaji malighafi kuzalisha chanjo zao wenyewe na sio michango ya chanjo kutoka nchi zilizoendelea.
‘’Ni aibu kwetu sisi Waafrika. Kwanini tutegemee kila kitu kutoka nje. Hii ni aibu kwa Afrika, ‘’ aliwaambia wajumbe waliohudhuria mkutano wa Shirika la Afya duniani, Jumapili.
Rais Museveni alisema kuwa nchi za bara la Afrika zinapaswa kuacha kusubiri chanjo za misaada na kutengeneza zao wenyewe.
‘’Ubinafsi duniani ni mbaya, lakini ni vizuri. Ninaupenda kwa kuwa unawaamsha Waafrika. Ni aibu kwa bara zima la Afrika limelala, likisubiri kuokolewa na wengine kama ilivyotokea wakatu wa biashara ya utumwa,’’ alisema.
Rais Museveni amesema Uganda ilikuwa kwenye mchakato wa kutengeneza Chanjo yake yenyewe na ilikuwa inahitaji tu msaada wa malighafi akisema,‘’Msiwe na shaka tutanunua. Hatuhitaji msaada.’’
Habari za asubuhi na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja

