Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Mfahamu bilionea kijana asiye na ofisi wala makazi ya kudumu

Katika kipindi cha miaka miwili tu Johnny Boufarhat, ameweza kutengeneza mabilioni ya pesa na kuwa kijana mwenye umri mdogo mwenye utajiri wa kibinafsi aliojitafutia mwenyewe.

Moja kwa moja

Dinah Gahamanyi

  1. Tokyo 2020: Mtu wa pili wa timu ya Olimpiki ya Uganda athibitishwa kuwa na corona Japani

    Raia wa pili wa timu ya Uganda amethibitishwa kuwa na virusi vya corona nchini Japani, siku tatu baada ya raia mwingine wa nchi hiyo hiyo kuthibitishwa kuwa na virusi hivyo baada ya kuwasili tu nchini humo kwa ajili ya michezo ya Olimpiki itakayofanyika mwezi ujao.

    Michezo ya Olimpiki iliahirishwa kwa mara ya kwanza katika historia mwaka jana kwsababu ya janga hilo lakini imepangiwa kuanza Julai 2 licha ya kuibuka kwa wimbi jingine la virusi hivyo nchini Japani.

    Uganda, ambayo imekuwa ikishuhudia kuongezeka kwa maambukizi siku za hivi karibuni, imetuma kikosi cha watu 9 katika mashindano hayo ambao wote wamepata chanjo.

    "Mtu wa pili wa timu yetu Uganda amethibitishwa kuwa na virusi vya corona," Kamati ya Olimpiki ya Uganda imesema kupitia taarifa iliyotoa.

    "Mwanariadha huyo haoneshi dalili za moja kwa moja na anafuatiliwa kwa karibu na mamlaka ya afya katika mji wa Izumisano. Wengine katika timu wako sawa na wanaendelea kuzoea hali ilivyo katika mji wa Izumisano."

    Wajumbe wote wa Uganda waliokwenda kwenye mashindano hayo ikiwa ni pamoja na wanamasumbwi, mwogeleaji na mnyanyuaji uzani walithibitishwa kutokuwa na virusi hivyo kabla ya kuondoka nchini Uganda wiki jana.

    Hata hivyo, Patrick Lihanda alithibitishwa kuwa na virusi vya corona baada tu ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Tokyo huko Narita Jumamosi, na aliwekwa karantini katika kituo kilichotengwa na serikali, maafisa wa Japani walinikuliwa na vyombo vya habari.

    Kuendelea kuthibitishwa kwa maambukizi ya virusi vya corona kutazua maswali zaidi kuhusu ikiwa michezo hiyo ya Olimpiki inastahili kuendelea huko Japani ambako wenyeji wengi wanapinga wazo hilo.

    Hata hivyo, mafisa husika wamekataa kuahirisha tena michezo hiyo ambayo inatarajiwa kuanza Julai 23 hadi Agosti 8, wakisema kwamba watakuwa salama wa salmin.

    Uganda imekuwa na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona tangu mwanzoni mwa mwezi Juni, huku idadi ya watu wanaothibitishwa kuwa na virusi hivyo ikiongezeka kutoka chini ya 100 hadi zaidi ya 1,700.

    Wajumbe kutoka Afrika ndio waliokuwa kundi la pili la wanariadha wa kigeni kuwasili kwa ajili ya mazoezi kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.

  2. SADC kupambana na Ugaidi mpakani mwa Tanzania na Msumbiji

    Rais wa Msumbiji, Phillipe Nyusi amesema Jumuia ya Kiuchumi ya Kusini mwa Afrika, SADC itakuwa mdau mkubwa katika mapambano dhidi ya ugaidi, ambao unashamiri kaskazini mwa nchi hiyo.

    Akifungua mkutano wa dharura wa jumuia hiyo ya SADC mjini Maputo, Rais wa Msumbiji ambaye ndiye mwenyekiti wake kwa sasa ameelezea mikakati ya Jumuia hiyo kusaidia kupambana na magaidi ambao kwa sasa wamejikita katika jimbo la Cabo Delgado nchini humo.

    Katibu Mtendaji SADC, Stergomena Tax, alisema ingawa kwa sasa juhudi kubwa zimepigwa kuhusu ugaidi kwenye eneo hilo , bado hali ya baadaye ni ya kutilisha wasiwasi.

    Mbali na ugaidi mkutano huo wa dharura pia unajadili masuala mbalimbali ikiwemo usalama, migogoro na uchumi wa ukanda huo ambao umeathiriwa kwa kiasi kikubwa vibaya na janga la Corona linalokabili ulimwengu kwa sasa.

    Katika Mkutano huo wa dharura, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alitambulishwa rasmi na Mwenyekiti wa SADC, ikiwa ni mkutano wake wa kwanza kuhudhuruia kama Rais tangu ashike madaraka mwezi Machi mwaka huu kufuatia kifo cha mtangulizi wake, John Magufuli.

    SADC ina meno ya kukabiliana na ugaidi?

    Bado kuna wasiwasi na uwezo wa SADC katika mapambano ya ugaidi katika eneo Cabo Delgado, Kaskazini mwa Msumbiji. Licha ya dhamira yake na nia, huenda ikakabiliwa na upinzani mkali kutokana na nyenzo, mbinu na rasilimali za Jumuia hiyo.

    Wengi wanaitazama kama Jumuia inayoweza kushirikiana zaidi kibiashara na kijamii kuliko kwenye masuala ya usalama hasa ugaidi.

    Suala la ugaidi nchini Msumbiji halijaanza leo, limeanza tangu mwaka 2017 baada ya wanamgambo wanaodaiwa kuwa ni wakiislam kushambulia mji huo wenye utajiri wa mafuta na gesi wa Cabo Delgado na kusababisha makumi ya watu kuuawa na maelfu kuukimbia mji huo unaokadiriwa kuwa na wakazi 75,000.

    Unaweza kujiuliza kwani SADC ilikuwa wapi tangu wakati huo? Au kwa sababu mwenyekiti wake sasa ni Rais wa Msumbiji, maslahi yanafanya suala hilo lishughulikiwe kwa nguvu inayotajwa?

    Kuna wakati Umoja wa Mataifa ulisema ulikuwa umepokea taarifa za kuogofya kwamba Tanzania iliwakatalia watu zaidi ya 1,000 waliokuwa wanakimbia mashambulizi ya wanamgambo kaskazini mwa Msumbiji, lichaya kwamba Tanzania ni jirani na mwanachama wa Msumbiji

    Tanzania ilijibu mapigo kupitia kwa Waziri wake wa mambo ya ndani, George Simbachawene kwamba, taarifa ya Umoja wa Mataifa haina uhalisia wowote.

    'Hakuna uhalisia wowote wa ripoti hii Je unawezaje kuwajua wanapotaka kuvuka kuja upande wa pili, je unawezaje kuwajua kama humo hakuna magaidi, sisi tunaogopa hawa magaidi, tunalinda mipaka yetu na tunapolinda tusitafsiriwe kama tunawazuia wakimbizi'' anasema Waziri Simbachawene.

    Utofauti wa namna hii, unazidi kuleta maswali kwamba SADC iko pamoja kushughulikia usalama katika eneo hilo? Lakini wapo wanaoona kuna matumaini hasa kufuatia kuingia madarakani kwa Rais Samia Suluhu, ambaye ujirani na Msumbiji unafanya nafasi yake kuwa muhimu zaidi na leo amehudhuria kikao cha kwanza muhimu cha SADC kuhusu Usalama na masuala ya ugaidi Kaskazini mwa Msumbiji.

  3. Ukosefu wa iPad ya Ramaphosa wawasisimua watumiaji wa mtandao wa kijamii

    Video ya Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa iliyomuonesha akiuliza ni wapi iPad ilikopotelea imesambazwa sana kwenye mtandao.

    Ramaphosa ambaye alionekana akiwa amefadhaika alikuwa akirudia mara kwa mara kusema imeibiwa, akiongeza kuwa " hili ni tatizo la kila mara kuwapatia kifaa chako watu wengine".

    "Wameeiba…Nilikuwa na iPad yangu, Nilikuwa nayo mikononi mwangu, Imeenda " alisema.

    Alikuwa amesimama kuhutubia katika tukio lakini hakuwa na hotuba yake.

    Hii ni video ya dakika mbili ya rais wakati wa tukio hilo.

    Rais aliombwa kuketi chini na kusubiri huku maafisa wakijaribu kutafuta kifaa hicho.

    Baadaye alitoa hotuba-na Mkuu wa mawasiliano ya kidigitali wa rais alituma ujumbe wa Twitter kwamba"ipad ya rais imepatikana ".

    Baadaye ofisi ya rais ilisema kuwa alikuwa "anatoa mzaha huku akisubiri iPad yake ".

    Watu wa Afrika Kusini kwenye mtandao walizungumzia kuhusu wakati wa kupotea kwa iPad :

    Simon Grindrod alisema: “Katika nchi nyingi, marais na mawaziri wakuu husafiri na alama za siri wa ajili ya mifumo yao ya makombora . Nchini Afrika Kusini, timu ya rais wetu hawewezi hata kulinga iPad yake binafsi .”

    “Rais alikuwa na hisia za kukata tamaa swan a wengi wetu ambao vitu vyetu hupotea kila siku ,” alituma ujumbe wa Twitter.

  4. Habari za hivi punde, Uingereza yakanusha ripoti za Urusi kwamba imefyatua risasi za ‘onyo’ kwa meli yake ya kivita

    Uingereza imekanusha ripoti za Urusi kwamba jeshi lake lilifyatua risasi za onyo kwa meli yake ya kivita katika Bahari Nyeusi.

    Ripoti nchini Urusi zilisema meli ya doria ya Urusi na ndege ya kivita zimefyatulia risasi za onyo meli ya kivita ya Uingereza katika Bahari Nyeusi,

    Shirika la habari la Interfax lilinukuu wizara ya ulinzi ikisema kwamba meli hiyo kwa jina HMS Defender iliingia katika maji ya Urusi karibu na Crimea.

    Wizara ya Ulinzi ya Uingereza bado haijatoa maoni.

    Urusi ililitwaa eneo la Crimea kutoka Ukraine mnamo 2014 lakini hatua hiyo haijatambuliwa kimataifa.

    Meli hiyo ya kivita ilikuwa katika pwani ya Ukraine ya Odessa mapema wiki hii kulingana na ubalozi wa Uingereza nchini Ukraine. Ubalozi huo ulisema Uingereza na Ukraine zilisaini makubaliano ya kujenga kwa pamoja ngome mbili za jeshi la majini kwa pamoja meli za kivita na vituo viwili vya jeshi la majini

    HMS Defender ilibadilisha mkondo wake baada ya risasi za onyo, Moscow ilisema. Ilisema kuwa tukio hilo lilitokea karibu na Cape Fiolent kusini mwa Crimea.

    Meli ya doria ilifyatua risasi mara mbili na ndege aina ya Su24-M iliangusha mabomu manne katika njia ya meli hiyo ya Uingereza .

    Baozi mdogo wa Ulinzi wa Uingereza ameitwa kwenda katika wizara ya ulinzi ya Urusi, Interfax ilinukuu wizara hiyo ikisema.

    Meli ya HMS Defender ni sehemu Kikundi cha Meli za kivita za uingereza kwa jina Carrier Strike Group . Meli hizo zinafanya misheni katika bahari nyeusi kulingana na tovuti ya Jeshi la majini la Uingereza

  5. Familia ya Uingereza inayosema ina undugu wa damu na rais wa Marekani

    Wiki iliyopita, BBC ilichunguza madai kuwa Rais wa Marekani Joe Biden ana uhusiano kijeni na England. Tangu wakati huo, familia moja ya England imejitokeza na kusema ni ndugu wa rais Biden.

    Kwa miaka 20 Paul Harris, amekua akifanya uchunguzi wa historia yake. Aliweza kukusanya taarifa kuhusu nasaba.

    Alijifunza mengi kutoka kwa bibi (nyanya)yake , Kathleen Mary Brooks, na mama yake Ann Maria Davies.

    Ilijitokeza kwamba jina la Biden lilitoka kwenye familia yake . Lakini hakulitilia maanani sana suala hilo hadi siku moja mwaka jana ambapo binti yake Rose Patton ghafla aliposema.

    "Si itakuwa jambo zuri kama tukiwa ndugu wa Joe Biden?" alisema Rose, akimaanisha rais mpya aliyechaguliwa Marekani.

    Harris alishangazwa na kauli hiyo na ndipo alipoanza kufuatilia suala hilo. Uchunguzi wake ulibaini uhusiano wa nguvu baina ya rais Biden na ndugu zake walioishi Westbourne, kijiji kilichopo West Sussex, England.

    Harris, mwenye umri wa miaka a 60 – mtengenezaji wa programu za kompyuta, anadai rais wa Marekani ana undugu na bibi yake wa tatu Emily Biden.

    Aliishi katika Westbourne, ambako vizazi kadhaa vya familia yake viliishi . Watu wa famialia yake walikuwa ni pamoja na mjomba wake William Biden,ambaye anaaminiwa kuwa alihamia nchini Marekani katika miaka ya mwanzoni 1800.

  6. Bunge la Uganda kufungwa kwa wiki mbili kutokana na corona

    Taarifa iliyotolewa na Bunge inasema bunge hilo litafungwa kuanzia wiki ijayo tarehe 28 Juni , Jumapili hadi tarehe 11 Julai ili kusafisha majengo ya bunge.

    Mkurugenzi wa mawasiliano na masuala ya umma katika bunge hilo, Chris Obore anasema uamuzi ulichukuliwa ili kuzuia jingo hilo kuwa kitovu cha maambukizi kwasababu ya idadi kubwa ya watu wanaolitembelea.

    Bunge la sasa la Uganda lina jumla ya wabunge 529, ukiondoa wahudumuwa bunge, maafisa wa usalama, waandishi wa habari, na watoaji wa huduma mbalimbali.

    Taasisi hiyo ilikuwa na matukio muhimu makuutangu mwezi Mei miongoni mwake ikiwa ni kusomwa kwa bajeti, na Hotubaya hali ya taifaambayo hutolewa na rais.

    Mamia ambao walihudhuria matukio hayo wametakiwa kufanya vipimo vya corona. Waliopatikana na maambukizi wametakiwa kujitenga wenyewe.

    Takriban watu 180 walipatikana na maambukizi ya corona kabla ya matukio haya mawili tofauti . 14 kati yao walikuwa ni wabunge na 10 walikuwa ni wafanyakazi wa bunge.

  7. Mashambulio ya anga yarindima Tigray Ethiopia

    Watu kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa na wengine kuuawa katisha shambulio la ndege za kijeshi katika mji Togoga katika jimbo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia.

    Serikali ya Ethiopia imekuwa ikipigana na waasi katika jimbo hilo kwa miezi 8.

    Mapigano yameongezeka katika kipindi cha wiki mbili zilizopita huku wapiganaji wa Tigray People’s Liberation Front wakiiteka miji na vijiji.

    Madaktari katika hospitali kuu ya Tigray Mekelle wanasema kuwa wanawatibu makumi ya watu akiwemo mtoto mwenye umri wa miaka 2 aliyejeruhiwa katika shambulio la anga siku ya Jumanne.

    Lakini wahudumu wa matibabu wanasema wamezuia kufikia eneo la shambulio ili kuwasaidi walioachwa nyuma.

    Walioshuhudia shambulio hilo wameiambia BBC kuwa ndege za vikosi vya serikali ya Ethiopia zilipiga makombora yake kwenye soko moja lililopo kilomita 25 kutoka Mekelle.

    Jeshi la Ethiopia hata hivyo limenanusha madai ya kuwalenga raia.

  8. Familia za madagascar 'zinakula matope'' kutokana na ukame mbaya

    Shirika la mpango wa chakula duniani linaonya kuwa unaolikumba eneo la kusini mwaMadagascar kwa miongo minne unasababisha njaa na ukame mkubwa

    Mkurugenzi wake, David Beasley, ambaye ndio ametembelea kanda hiyo, amesema bila msaada wa haraka kwa watu zaidi ya nusu milioni itakuwa ni "kubisha mlango kwa familia zinazokabiliwa na ukame ", huku watu wengine 800,000 wakielekea kupatwa natatizo hilo.

    Amesema kuwa alishitushwa na kile alichokiona Kusini mwa Madagascar – ambako watoto walikuwa wamebakia tu na mifupa yenye ngozi, na familia zilikuwa zikila matope na matunda pori kwasababu hapakuwa na kitu kingine.

    Beasley ameiita hali inayoendelea katika kusini mwa Madagascar ‘’janga la kimya lililo katika eneo lilililosahahulika.

    Mzozo huo unasababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa, ambapo ukame umeendelea kuwepo na kuzilazimisha familia kuzihama nyumba zao, amesema Bw Beasley.

    Amesema kuwa mataifa tajiri hayana maadili ya uwajibikaji ya kusaidia.

  9. Bilionea kijana asiye asiye na ofisi wala makazi ya kudumu

    Katika kipindi cha miaka miwili tu Johnny Boufarhat amegeuza jukwaa lake la mtandao la kupokea mikutano linalofahamika kama Hopin, kuwa kampuni yenye thamani ya zaidi ya pauni bilioni nne.

    Anawaajiri watu 500, lakini baadhi yao hajawahi hata kukutana nao, kutoka ofisi kuu.

    Kulingana na porodha ya jarida la The Sunday Times la watu tajiri linalochapishwa nchini Uingereza, kijana huyu mwenye umri wa miaka 27 tu kwa sasa ndiye tajiri kijana zaidi aliyejiwezesha mwenyewe kuwa bilionea .

    Aidha mchango aliouchangisha hivi karibuni kupitia kampuni yake Hopin ulifikia pauni milioni 400 kutoka kwa wawekezaji binafsi, na hivyo kumfanya kuwana utajiri wenye thamani ya dolabilioni $5.65 (£4.05bn).

    Lakini hupenda kufanya mambo tofauti

    ."Kuwa kampuni inayofanya kazi yote kwa njia ya mtandao inatusaidia kufanya mambo mengine ambayo kampuni nyingine hazijaweza kuyafanya kabla ," anaeleza Johnny Boufarhat, kutoka katika nyumba zake alizonunua hivi karibuni za kupangisha zilizpo katika jiji la Barcelona, Uhispania.

    Licha ya kutokuwa na ofisi ya kudumu, mjasiliamali huyu wala hana nyumba au makazi ya kudumu .

    Ni mtumiaji wa Digital/ mtandao wa kuhama hama kutoka mojawapo ya nyumba zake za kupangisha kwenye eneo moja na kuhamia kwenye nyumba moja nyingine kati ya nyumba zake za kupangisha , akiendesha kampuni yake kutoka pale alipo kwa wakati huo.

    Hana mpango wa kubadilisha mtindo wake wa kufanya kazi bila ofisi ambao ulimuwezesha kuanza biashara yake vyema.

    Na hata ameanzisha kampuni ya kipekee ya kidigitali ya kuisaidia kazi yake.

    Utakua muongozo unaoonesha ni kwa kamuni gani zilizozinduliwa na kufanya kazi kwa siku zijazo.

    Ameweza kuwakutanisha watu mtandaoni sasa na ' "ukumbi wa mikutano wa mji" kwa njia ya video kufanya mkutano wa wafanyakazi wake 500 anaouitisha mara moja kila mwezi kwenye jukwaa lake la Hoin, ambalo Boufarhat analielezea kama "mchezo wa onyesho la zaidi".

  10. Fahamu Abdala, chanjo mpya ya corona inayotajwa kuwa ya ufanisi mkubwa

    Cuba imesema kuwa dozi tatu za chanjo yake dhidi ya virusi vya corona kwa jina Abdala imethibitishwa kuwa na ufanisi wa 92.28% katika awamu ya tatu ya majaribio yake.

    Tangazo hilo limekuja siku kadhaa tu baada ya serikali kusem kuwa chanjo nyingine iliyotengenezwa nchini humo inayoitwa , Soberana 2, ilikuwa na ufanisi wa 62% kwa dozi mbili tu kati ya tatu.

    “Kwa kuathiriwa vibaya na janga la corona, wanasayansi wetu, katika Taasisi yaFinlay na kituo cha uhandisi wa Jeni na teknolojia ya kibaiolojia wameweza kupita vikwazo vyote na kutupatia chanjo zenye ufanisi mkubwa ,” Rais Miguel Diaz-Canel aliandika kwenye ujumbe wa Twitter.

    Tangazo hilo limetolewa baada ya lile la Shirika la madawa la taifa hiloBioCubaFarma, linalosimamia Finlay, ambao ni watengenezaji wa Soberana 2, na Kituo cha uhandisi wa Jeni na teknolojia ya kibaiolojia (Center for Genetic Engineering and Biotechnology, ambao ni wazalishaji wa chanjo ya Abdala.

    Chanjo zote zinatarajiwa kupewa mamalaka ya kuwa za dharura na taasisi ya usimamizi wa viwango muda mfupi.

    Cuba, ambayo sekta yake ya teknolojia ya baiolojia imekuwa ikituma nje ya nchi chanjo kwa miongo kadhaa, ina chanjo tano za corona zinazofanyiwa majaribio.

    Uaweza pia kusoma:

    • Hivi ndivyo mabilionea na mamilionea wanavyotumia fedha zao
    • Beijing ina mabilionea wengi zaidi kuliko miji mingine duniani
    • Aliko Dangote na Mohammed Dewji miongoni mwa mabilionea wa Afrika 2021
  11. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mubashara leo tarehe 23.06.2021