Mahakama yatengua uamuzi wa Fatma Karume kufutiwa uwakili

Hata hivyo uamuzi huo haumaanishi amerejeshewa uwakili wake uliofutwa awali, isipokuwa anapaswa kwenda mbele ya kamati ya maadili ili kujitetea.

Moja kwa moja

Dinah Gahamanyi

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo, tukutane tena kesho majaaliwa

  2. Watu kadhaa wanaswa baada ya daraja inayojengwa kuanguka Nairobi

    Daraja

    Chanzo cha picha, Hisani

    Watu kadhaa wanahofiwa kunaswa baada ya sehemu ya kivuko cha barabara kuu inayojengwa mjini Nairobi kuanguka.

    Waliyonaswa ni pamoja na wafanyikazi wa ujenzi na wauzaji wa barabarani katika soko la Kangemi jijini Nairobi.

    Vyombo vya habari vya huko vinaripoti kuwa watu wasiopungua wanne tayari wameokolewa.

    Kuna msongamano mkubwa wa magari katika eneo hilo jioni hii, kwani juhudi za uokoaji bado zinaendelea.

  3. ‘Hatumuogopi rais’ Timu ya taifa ya Gambia yasusia kukutana na rais wa nchi Adama Barrow

    Adama Barow

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Timu ya taifa ya soka nchini Gambia imesusia mkutano na Rais wa nchi hiyo Adama Barrow kufuatia mzozo kuhusu mafao yao ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.Wachezaji wameandika kwa Rais wa Shirikisho la Soka la Gambia (GFF) Lamin Kaba Bajo kukataa mwaliko wa kukutana na rais Jumatatu.

    GFF haijajibu majaribio ya BBC Sport Africa ya kupata jibu kwa barua iliyotumwa na kikosi hicho.Katika mkutano huo wachezaji walitarajia Rais Barrow atakabidhi Dalasi milioni 11 (takriban $ 215,000) kugawanywa kati ya wachezaji wote na wafanyikazi wa kitengo cha kiufundi waliohusika katika kufuzu kwa Kombe hilo.

    Kikosi hakihisi pesa zinazotolewa zinaonyesha ukubwa wa mafanikio yake na kina wasiwasi pia kwamba kukubali pesa hizo kutaweka mfano mbaya kwa siku zijazo."Timu ingependa kumshukuru Mheshimiwa kwa mwaliko huo lakini watakataa mwaliko wa kukutana na pesa zilizotolewa," barua hiyo ilisema."Kwa wachezaji, kuichezea Gambia haijawahi kuwa kuhusu pesa.

    Badala yake, mara zote ilikuwa juu ya kupeperusha bendera ya Gambia na kuwapa watu wa Gambia fahari."Wachezaji walikuwa wakifurahia wito wa kuchezea timu ya taifa bila kutarajia au kuomba malipo yoyote, bila kujali ugumu ambao wakati mwingine unajitokeza"Soka ni mchezo wa motisha. Baada ya kufuzu kushiriki kombe la Mataifa ya Afrika mwakani kwa mara ya kwanza katika historia ya Gambia.

    Timu inastahili kupewa bonasi ambayo itawatia motisha wachezaji na kila mtoto ambaye ana ndoto ya kuchezea Gambia. siku moja."Timu inahisi kwamba heshima na motisha waliyopewa wachezaji iko chini ya ile inavyotakiwa kuwa.

    Kwa sababu hiyo, wachezaji kwa kauli moja waliamua kukataa mwaliko."Tunatumahi kuwa kwenda mbele, wachezaji watapewa motisha ya kutosha wakati maandalizi ya kombe la Afrika yanaendelea."

    Gambia iliweza kufuzu kwa fainali za Kombe hilo mwezi Januari nchini Cameroon kwa kumaliza kileleni mwa kundi lao mbele ya Gabon, DR Congo na Angola.

  4. Mahakama yatengua uamuzi wa Fatma Karume kufutiwa uwakili

    Fatma karume

    Mahakama Kuu nchini Tanzania imetengua uamuzi wa kamati ya maadili ya mawakili wa kumfutia moja kwa moja uwakili mwanasheria Fatma Karume.

    Pamoja na kutengua uamuzi huo, Mahakama hiyo imeagiza uamuzi huo uliotokana na malalamiko yaliyowasilishwa na mwanasheria mkuu wa serikali yarejeshwe kwenye Kamati hiyo ya Maadili na mwanasheria huyo apewe nafasi ya kujitetea.

    Hata hivyo uamuzi huo haimaanishi amerejeshewa uwakili wake uliofutwa awali, isipokuwa anapaswa kwenda mbele ya kamati ya maadili ili kujitetea.

    kwenye ukurasa wake wa Twitter Fatma ametaja uamuzi huo wa mahakama ingawaje amesema hajarejeshewa uwakili

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Fatma Karume mtoto wa Rais mstaafu wa awamu ya sita Zanzibar, Aman Karume na mjukuu wa mtoto wa Rais wa kwanza wa nchi hiyo, Abed Karume alivuliwa uwakili mwaka 2019 kwa madai ya hatua yake ya kukosoauteuzi wa Mwanasheria Mkuu Dkt Adelarus Kilangi aliyeteuliwa na rais John Pombe Magufuli February, 2018.

    Ingawa kujihusisha kwake kwenye siasa kunahusishwa na kadhia iliyomkuta.Baada ya uamuzi huo wa Mahakama, Fatma mbali na kutoa ufafanuzi wa kuhusu uamuzi huo kupitia mtandao wake wa Twitter amewashukuru pia watu mbalimbali akiwemo wanasheria waliomsimamia kesi yake hiyo akiwemo Peter Kibatala, Profesa Issa Shivji, Rugemaleza Nshala na Mike Ngale.

    Kwa muda sasa Mwanasheria huyo amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali iliyo madarakani na amejitambulisha kama mwanamamke asiye muoga kusema chochote na popote.Kutokana na misimamo yake hiyo , ameshakutana na visa vya kuvamiwa na kuchomwa kwa ofisi yake ya uanasheria pamoja na kufukuzwa kwenye Taasisi moja ya kisheria aliyokuwa anafanya kazi.

  5. Waziri Mkuu wa Ethiopia kuendelea kufanya kazi na vikosi Eritrea

    Abiy Ahmed

    Chanzo cha picha, AFP

    Katika mahojiano ya kipekee na BBC, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema kuwa serikali yake itaendelea kufanya kazi na vikosi vya Eritrea vinavyopigana na vikosi vya jimbo la Tigray kaskazini mwa nchi.

    Wanajeshi kutoka nchi jirani ya Eritrea, ambao wanaunga mkono vikosi vya serikali, wamekuwa wakishutumiwa kwa mauaji ya kikatili, kuwabaka wanawake, na kuzuia misaada ya kibinadamu kuwafikia watu waliopo katika maeneo ya hatari ya vita.

    Eritrea imekanusha madai hayo.

    Mwezi Machi mwaka huu, Bw Abiy alikuwa ameahidi kuwa wataondoka katia jimbo la Tigrey.

    Waziri mkuu huyo ameiambia BBC pia kwamba serikali yake inashirikiana na wanajeshi wa Sudan katika Tigray – lakini hakuelezea ni kwa kiwango gani.

    Bw Abiy alikuwa ndio amemaliza kupiga kura yake katika kijiji cha nyumbani cha Beshasha ambako anagomea kiti cha ubunge katika uchaguzi nchini mumo.

  6. Watu 10,000 watakaruhusiwa kutazama michezo ya Olympiki

    Olympiki

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Takriban watazamaji 10,000 ndio watakaoruhusiwa kuhudhuria Michezo ya 2020 Olympiki mjini Tokyo Japan, licha ya tahadhariya corona kutoka kwa wataalam wa afya.

    Mashabiki kutoka nje ya nchi wamekwishazuiwa kuingia kwenye viwanja lakini waandaaji wanasema wakazi wataweza kufanya hivyo ili mradi hawazidi asilimia 50 ya idadi ya wanaopaswa kuwa uwanjani.

    Mashabiki wanazuiwa kupiga kelelena watatakiwakutekeleza masharti kila mara wawapo viwanjani.

    Michezo hiyo inatarajiwa kuanza tarehe 23 Julai huku Olympiki ya Walemavu- Paralympics ikitarajiwa -ikifuatia mwezi mmoja baadaye.

    Waandalizi na serikali ya Japan wataoa tangazo kuhusu michezo ya Olympiki ya walemavu tarehe 16 Julai.

    Hii inakuja baada ya wataalam wa afya kutoa ripori wakisema kuwa kuandaa shindano hiyo bila watazamaji na mashabiki "ni hatua itakayopunguza hatar "na wakatoa wito mashindano hayo yasiwe na watazamaji wala mashabiki viwanjani.

  7. Serikali ya Sweden yapinduliwa kwa kura ya kutokuwa na imani nayo

    Waziri Mkuu wa Sweden

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Stefan Lofven

    Jumla ya wabunge 181 kati ya 349 wa Sweden wamepiga kura kuunga mkono hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, huku 51 wakikosa kuchagua kwa kutokuwepo.

    Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Sweden kwamba kiongozi wa muungano Social Democratic anakuwa na wiki moja ajiuzulu au kuitisha uchaguzi.

    Uamuzi huo umekuja baada ya kuibuka kwa mzozo juu ya udhibiti wa kodi ulioongozwa na chaka cha mrengo wa Kushoto kuondoa uungaji mkono wake kwa serikali ya muungano.

    Matokeo hayo yanamaanisha kuvunjika kwa serikali ya muungano wa Social Democrat ambao ni wachache na chama cha Kijani ( Green Party).

    Kama waziri mkuu akiamua kung’atuka madarakani, Spika wa bunge atatakiwa kuanza kufanya mazungumzo na vyama mbali mbali ili kuunda serikali mpya.

  8. Wakuu wa Wilaya wapya waanza kuapishwa Tanzania

    Joshua Nassari, ni miongoni mwa wanasiasa wa upinzani walioteuliwa kuwa Wakuu wa Wilaya na Rais  Samia

    Chanzo cha picha, Millard Ayo.COM

    Maelezo ya picha, Joshua Nassari, ni miongoni mwa wanasiasa wa upinzani walioteuliwa kuwa Wakuu wa Wilaya na Rais Samia Suluhu

    Wakuu wapya wa wilaya nchini Tanzania wameanza kuapishwa katika maeneo tofauti ya mikoa nchini humo. Kwa mujibu wa sheria, Wakuu hao wa Wilaya wanakula kiapo mbele ya wakuu wa mikoa.

    Kati ya wakuu hao wa Wilaya 139 walioteuliwa na Rais Samia Suluhu, 56 ni wapya kabisa wakiwemo waaandishi wa habari, wasanii maarufu, wasomi na wanasiasa waliohama kutoka vyama vya upinzani.

    Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nickson Simon Joh (Nikk wa Pili), ni miongoni mwa walioapishwa leo akisindikizwa na kaka yake, ambaye pia ni msanii maarufu wa hip hop Afrika Mashariki, Joh Makini pamoja na kundi zima la Weusi, analotoka Nikk wa Pili.

    Aliyekuwa mshindi wa pili wa Mashindano ya urembo Tanzania mwaka 2006, Jokate Mwegelo ni miongoni mwa walioapa leo, huku aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 1998, Basila Mwanukuzi, mtangazaji wa kituo cha habari cha ITV, Abdallah Mwaipaya, Fatma Nyangasa (Azam TV) na Gabriel Zakaria wa Televisheni ya taifa ya TBC, ni miongoni mwa wanaoapa kuwa wakuu wa Wilaya.

    Jockete

    Chanzo cha picha, Jocket Mwegelo /Facebook

    Maelezo ya picha, Mshindi wa pili wa Mashindano ya urembo Tanzania mwaka 2006, Jokate Mwegelo ameteuliwa tena kuwa Mkuu wa wilaya

    Majina mengine yaliyoteuliwa na kuwa miongoni mwa wakuapishwa ni pamoja na Msanii wa siku nyingi wa maigizo na filamu nchini humo, Juma Chikoka maarufu kama Mchopanga, Afisa uhusiano wa Clouds Media, Simon Simalenga na aliyekuwa mtangazaji wa ITV, Godwin Gondwe, ambaye katika awamu iliyopita alikuwa klwenye nafasi hiyo na sasa amerejeshwa.

    Rais Samia alimteua pia aliyekuwa katibu mkuu wa chama kikuu cha upinzani cha CHADEMA, Vicent Mashinji na wapinzani wengine waliojiunga na chama tawala katika kipindi cha hivi karibuni kama Joshua Nassari, Peter Lijualikali kutoka CHADEMA walioapishwa leo.

    Wnasiasa hao wanaungana na orodha ya wapinzani wengine walioteuliwa kuwa wakuu wa wilaya akiwemo Kalisti Lazaro (aliyekuwa meya wa jiji la Arusha (CHADEMA), Moses Machali aliyekuwa NCCR Mageuzi na ACT-Wazalendo, Julius Mtatiro aliyetoka (CUF) na Albert Msando aliyekuwa mwanasheria, CHADEMA.

    Rais Samia amewaacha baadhi ya wakuu wa Wilaya waliokuwa na tuhuma mbalimbali zikiwemo za kunyanyasa akiwemo Lengai Sabaya ambaye kwa sasa yuko jela kwa tuhuma mbalimbali, Samwel Odunga na Richard Kasesera. Ingawa kwa nyakati tofauti viongozi hao wamekana tuhuma zozote zinazoelekezwa kwao.

    Msanii Juma Chikoka maarufu kama Mchopanga ameapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rorya

    Chanzo cha picha, Millard Ayo.COM

    Maelezo ya picha, Msanii Juma Chikoka maarufu kama Mchopanga ameapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rorya

    Msanii Juma Chikoka maarufu kama Mchopanga ameapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rorya,

    Joshua Nassari ameapa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda,

    Katibu mkuu wa zamani wa CHADEMA, Dkt. Viccent Mashinji ameapa kuwa mkuu wa wilaya ya Serengeti.

  9. Mwanariadha maarufu Usain Bolt apata mapacha

    Bolt

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Usain Bolt alipata umaarufu kukimbia mwendo wa kasi zaidi kwa mbio fupi na kuitwa Mwanaume mwenye kasi kubwa zaidi dunaini

    Mwanariadha maarufu wa Jamaica Usain Bolt ameitangazia dunia kuwa yeye na mpenzi wake wamefanikiwa kupata watoto mapacha wa kiume.

    Bw Bolt, ambaye maarufu kwa mbio za masafa mafupi mwenye umri wa miaka 34 amesema amewapatia watoto wake majina Thunder Bolt na Saint Leo Bolt.

    Ametoa tangazo hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram katika kusherehekea siku ya kimataifa ya akina baba- ujumbe ulioambatana na picha ya mpenzi wake -Kasi Bennett, wakiwa na mapacha hao pamoja na mtoto wao mkubwa msichana Olympia Lightning mweye umri wa mwaka mmoja.

    Ruka Instagram ujumbe, 1
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa Instagram ujumbe, 1

    Mpenzi wake Usain Bolt, Bennett pia ametuma ujumbe kwenye mtandao wa Instagramakisema, Bolt ni " Mwamba wa familia na baba bora wa watoto wetu"

    Ruka Instagram ujumbe, 2
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa Instagram ujumbe, 2

  10. Mbwa wa Ufaransa anayesaidia waathiriwa wa uhalifu mahakamani

    Mbwa
    Maelezo ya picha, Lol, hapa akiwa na Mwendesha mashitaka Frédéric Almendros, ni wa kwanza rasmi barani Ulaya kutoa usaidizi rasmi kwa waathiriwa wa uhalifu

    Mahakama moja nchini Ufaransa ina Mbwa anayekuwa mahakamani kwa ajili ya kusaidia waathiriwa wa uhalifu kuondoa wasiwasi.

    Mbwa huyu kwa jina Lol mwenye umri wa miaka mitano, amekuwa mahakamani kwa muda wa miaka miwili sasa akifanya kazi hiyo.

    Mbwa huyu mweusi hutembea na waendesha mashitaka, huku akitoa usaidizi wa kisheriakwa waathiriwa wa uhalifu, hususan wale ambao waliathiriwa na unayanyasaji wa kingono na unyanyasaji mwingine.

    "Baada ya kumhoji muathiriwa huwa ninamuita mbwa kusaidia kama ninaaminiuwepo wake utasaidia kumliwazaili aweze kufunguka na kusema kilichotokea, au hata wanapolazimika kutoa ushahidi wakati mahakamani ," anasema Mwendesha mashitaka Frédéric Almendros. "Mbwa huketi kando ya waathiriwa mahakamani na mara nyingi huwasaidia kuhimili wasi wasi mahakamani."

    Lol anadhaniwa kuwa ndiye mbwa wa kwanza baraniUlaya kutoa usaidizi wa aina hii mahakamani na anaamimiwa kuifahamu mahakama kuliko mhalifu yeyote sugu.

    Lol amethihirika kuwa maarufu miongoni mwa mawakili katika mahakama ya  Cahors
    Maelezo ya picha, Lol amethihirika kuwa maarufu miongoni mwa mawakili katika mahakama ya Cahors

    Amefundishwa kuwa mtulivu

    Mbwa huyu aina yaLabrador amefundishwa kuwa mtulivu anapowaona watu asio wafahamu, wakiwemo watoto. Anaweza kutulia hata wakati wa wasiwasi ,hali zinazowafanya watu mahakamani kupaza sauti za juu na hali za kihisia kama vile hoja za waathiriwa mahakamani, ambapo waathiriwa wa ubakaji wanapokutana ana kwa ana na washambuliaji wao.

    Hadi sasa Mbwa Lol amekuwa katika kesi 80 za uchunguzi wa uhalifu tofauti zilizowahusisha waathiriwa kuanzia miaka mitatu hadi wa miaka 90.

  11. Baadhi ya picha za uchaguzi wa Waziri Mkuu nchini Ethiopia

    uchaguzi Ethiopia

    Raia wa Ethiopia wanapiga kura hii leo kumchagua Waziri Mkuu, huku Waziri Mkuu anayeondoka madarakani Abiy Ahmed akitarajia kupata kiti hicho tena.

    Uchaguzi huu unafanyika huku taifa hilo likiwa katika zozo wa kivita katika jimbo la Tigrey.

    Bw Abiy anatazamiwa kupiga kura katika wilaya Beshaha iliyopo kusini- magharibi mwa Ethiopia alikozaliwa.

    Wandishi wa BBC wametuma picha za watu wakipiga kura katika maeneo yaBeshaha na Agaro.

    Agaro ni mjiuliopo katika jimbo ambako Bw Abiy anagombea dhidi ya wagombea wawili wa upinzani kuchaguliwa kama mbunge katikabunge la wawakilishi la Ethiopia.

    Uchaguzi huu ni jaribio la kwanza kwa Waziri Mkuu tangu alipoingia madarakani mwaka 2018.

    Soma zaidi juu ya uchaguzi wa Waziri Mkuu wa Ethiopia

    • Uchaguzi mkuu Ethiopia: Je ni Fursa ya kuzaliwa upya kwa demokrasia au kuendelea kwa mizozo?
    uchaguzi Ethiopia
    uchaguzi Ethiopia

    Chanzo cha picha, BB

    uchaguzi Ethiopia
    uchaguzi Ethiopia
  12. Mawe yaliyokimbiliwa Afrika Kusini yagundulika kuwa hayakuwa Almasi

    Almasi

    Wataalam wa machimbo ya migodi wamebaini kuwa mawe yaliyopatikana KwaHlati katika Ladysmith, KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini ni vipande vya madini ya quartz na, sio Almasi.

    Jopo la wataalamu lilitoa tangazo Jumapili.

    Zaidi ya watu 1,000 walikimbilia katika kijiji cha KwaHlatikusaka kuyasaka mawe hayo ambayo waliamini yalikuwa ni Almasi.

    Watu walisafiri kutoka maeneo mbali mbali kote nchini Afrika Kusini kujiunga na wanavijiji ambao walikuwa wakiyachimba tangu Jumamosi , baada ya kusikia kuwa vipande hivyo vya mawe vilikuwa ni Almasi ambayo ingewatajirisha.

    Uvumbuzi wa mawe haya utabadilisha maisha, alisema mchimbaji mmoja Mendo Sabelo aliyekuwa amebeba vipande vya mawe hayo.

  13. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mubashara leo Jumatatu tarehe 21.06.2021