'Tanzania hatuna wakimbizi kutoka Msumbiji'

Waziri wa mambo ya ndani nchini Tanzania, bwana George Simbachawene amekanusha uwepo wa wakimbizi kusini mwa Tanzania .

Moja kwa moja

Ambia Hirsi

  1. Na kufikia hapo tunakamilisha matangazo haya ya moja kwa moja. Kwaheri na Asante.

  2. 'Tanzania hatuna wakimbizi kutoka Msumbiji'

    msu

    Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, bwana George Simbachawene amekanusha uwepo wa wakimbizi kusini mwa Tanzania .

    Waziri Simbachawane amesema Tanzania kazi yake kama nchi ni kulinda mipaka yake na kulinda watu wake.

    Vilevile ifahamike kuwa katika jumuiya ya kimataifa Tanzania inawahifadhi wakimbizi na waomba hifadhi zaidi ya laki mbili sabini na tano elfu kutoka nchi mbalimbali zilizopata machafuko ya kisiasa au mapigano ya wenyewe kwa wenyewe au sababu nyingine mbalimbali.

    "Kazi ya taifa letu katika kulinda mipaka na nchi yake, mpaka wa kusini ambao tuapakana na Msumbiji kuna mikoa mitatu Lindi, Mtwara na Ruvuma, katika mikoa hiyo sisi hatuna wakimbizi kutoka nchi yeyote ila tunafahamu kuwa katika nchi ya Msumbiji jimbo la Cabo Delgado kuna machafuko ambayo yalifanywa na magaidi.

    Magaidi wanafanya ghasia katika eneo hilo na hivyo watu wanakimbia katika maeneo mbalimbali, na katika upande wetu sisi si rahisi kuweza kuwachuja kujua huyu mkimbizi au gaidi, maana kwa macho hatuwezi kupima au kuona tofauti yao," Simbachawene amesema.

    Aidha aliogeza kusema kuwa Tanzania haijaresha wakimbizi kwa sababu haina wakimbizi kusini mwa nchi yake.

    Amesema katika ukanda wa Afrika Mashariki na ukanda wa maziwa makuu, Tanzania inaongoza kwa kuhifadhi wakimbizi na wana uzoefu huo na vilevile wana heshimu sana sheria za kimataifa kwa wakimbizi lakini mpaka sasa hawana wakimbizi wa Msumbiji alisisitiza kwa kusema ... "Hatuna wakimbizi kusini mwa Tanzania sasa tunawafukuza vipi!".

    Awali, Mamlaka nchini Msumbiji zimesema kuwa zaidi ya raia 9,600 wa Msumbiji wanaokimbia vurugu kaskazini mwa Jimbo la Cabo Delgado "wamerudishwa kwa nguvu" kutoka Tanzania tangu Januari 2021, Diario de Noticias gazeti binafsi nchini humo limeripoti.

    Kulingana na Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa karibu watu 900 "walisukumwa kwa lazima" kuvuka mpaka kati ya tarehe 7 na 9 Juni.

    Ripoti hiyo inakuja saa chache baada ya manusura walionukuliwa na tovuti inayomilikiwa na watu binafsi O Pais, kufichua kwamba mji wa Palma kaskazini mwa Msumbiji, ulibaki ukikaliwa na wanamgambo, ambao wanachama wao wanaendelea "kuchoma nyumba, kuua na kuteka nyara watu".

    Mashambulio makubwa ya hivi karibuni ya kundi hilo dhidi ya mji wa Palma mnamo 24 Machi, yaliwahamisha zaidi ya watu 70,000, na kuongeza idadi ya watu waliohamishwa kutokana na ghasia kaskazini mwa Msumbiji hadi karibu 800,000.

    Mnamo mwezi Aprili Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania George Simbachewene alisema kuwa Ripoti ya Umoja wa mataifa juu ya Tanzania kurudisha wakimbizi wa Msumbuji haina uhalisia wowote.

    Katika mahojiano na BBC Simbachawene alisisitiza kuwa Tanzania inalinda mipaka yake na kujilinda dhidi ya magaidi ambao wakati mwingine wanaweza kujichanganya na wakimbizi na kisha kuingia nchini.

  3. Baba ajipata mashakani kwa kumruhusu mwanawe kuendesha gari

    Baba mmoja nchini Kenya amehukumiwa kifungo cha miezi mitatu gerezani au kulipa faini ya dola 185 za Kimarekani kwa kumruhusu mtoto wake wa miaka saba kuendesha gari katika barabara ya umma.

    Ayub Kinyanjui alikamatwa Jumatatu baada ya kanda ya video inayomuonesha mtoto wake wa kiume akiendesha gari karibu na mji wa Muranga, kaskazini mwa mji kuu Nairobi, kusambazwa mitandaoni mwishoni mwa wiki iliyopita.

    Mtuhumiwa alikiri mashtaka ya kumruhusu mtu asiye na leseni kuendesha gari kwa kujua.

    Kituo kimoja cha redio kimeweka katika mtandao wa Twitter picha yake akiwa mahakamani.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  4. Rais Samia awafukuza kazi maafisa wawili kwa kuwaonea wafanyabiashara

    Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewafukuza kazi Mkuu wa wilaya pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa na Sheilla Lukuba, kufuatia tukio la hivi karibuni ambapo wafanyabiashara wadogo waliondolewa kwa nguvu katika eneo hilo.

    Rais Samia ametangaza uamuzi huo mkoani Mwanza wakati wa mkutano wake na Vijana wa Tanzania.

    Rais alielezea kusikitishwa kwake na kitendo cha kuondolewa kwa nguvu kwa Wafanyabiashara hao, na kuongeza ingekuwa ni lazima Wafanyabiashara hao kuondolewa ingetumika njia nyingine na si nguvu na kuharibu bidhaa zao.

    ''Wafanyabiashara hao walitengewa eneo la mbali kwa ajili ya kufanya biashara zao na walipoona hakuna biashara waliamua kurudi maeneo ya mjini na ndipo walipoanza kuondolewa kwa nguvu'', alisema

    Amemuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu kusimamia jambo hilo.

    Wiki iliyopita Rais Samia alimfuta kazi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila aliyetaka wananchi wabebe mabango kumkaribisha.

  5. Mwanamitindo wa Marekani aomba msamaha kwa kuwadhalilisha watu mtandaoni

    Mwanamitindo

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Chrissy Teigen ameomba msamaha kwa kuwadhalilisha watu kadhaa kwenye Twitter.

    Teigen alichapisha msururu wa ujumbe kwenye Twitter mwezi Mei kumuomba radhi mtangazaji wa runinga Courtney Stodden, ambaye alimtuhumu kwa unyanyasaji.

    Stodden alikubali msamaha lakini akasema huenda ni jaribio la kusafisha sifa ya Teigen.

    Alisema hakuwa akitafuta huruma, na kuongeza kuwa "ameabadilikana sio mtu wa kuandika vitu hivyo vya kutisha" baada ya kuolewa, kupata watoto na kutafuta matibabu.

    "Sisi sote ni ztunapitia kipindi kigumu maishani," Teigen aliandika. "Sitaomba msamaha wenu, ila naomba uvumilivu wenu."

    Mwaka 2011 Teigen, ambaye alikua na miaka 25 wakati, alipotuma ujumbe huo kwa Stodden aliyekuwa na miaka16 akimtaka kujitoa uhai.

    Wakti huo Stodden alijizolea umaarufu kama bibi arusi wa mwigizaji Doug Hutchison, ambaye alikuwa na umri wa miaka 50 wakati walioa.

    Chrissy Teigen ambaye ni mwanamitindo na mwandishi wa Merekani ana wafuasi milioni 35 kwenye mtandao wa Instagram na wafuasi milioni 13.5 kwenye Twitter.

  6. TB Joshua kuzikwa 'kanisani'

    TB Joshua

    Chanzo cha picha, Twitter

    Kanisa la Mhubiri Nigeria Temitope Balogun Joshua, maarufu TB Joshua limetangaza siku na mahali atakapozikwa.

    Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu, kanisa la Sinagogi la mataifa yote SCOAN, lilisema Mhubiri TB Joshua atazikwa karibu na makao yake makuu mjini Lagos.

    Mhubiri huyo aliyekuwa na umri wa miaka 57 alifariki Juni 5,2021 siku chache kabla ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

    "Tunajiandaa kwa ibada ya kila wiki kukumbuka maisha ya Nabii TB Joshua." taarifa ilisema.

    • TB Joshua:Fahamu maneno ya mwisho aliyosema katika mahubiri yake kabla ya kifo
    • Fahamu Utabiri na utata uliomzunguka TB Joshua

    TB Joshua, alizaliwa tarehe 12 mwezi Juni 1963 katika mji wa Arigidi huko Aoko kaskazini mashariki mwa jimbo la Kusini magharibi mwa Nigeria.

    TB Joshua anajulikana kuwa muhubiri Mkristo anayehubiri katika runinga.

    Ndiye mwanzilishi wa kanisa la Sinagogi la mataifa yote SCOAN ambalo huhubiri moja kwa moja katika runinga ya Emmanuel TV mjini Lagos.

    TB Joshua ana makanisa mengi katika mataifa tofauti barani Afrika na Amerika Kusini.

  7. Tazama: Daktari wa Mifupa ambaye hajasomea taaluma hiyo lakini ni stadi

    Maelezo ya video, Ni shupavu wa tiba ya kiasili na hata hospitali za umma zinamtegemea

    (Makala hii ni maelezo ya habari na sio ushauri au maelekezo ya kutegemewa kimatibabu.Iwapo utahitaji msaada wa matibabu ,mshauri daktari au mamlaka husika ya huduma za kitaalam )

  8. Wafanyakazi wakamatwa kwa kukataa kuwapa polisi burger za bure

    Wafanyikazi hawakuruhusiwa kufunga jikoni walipokuwa wakizuiliwa, mgahawa huo umesema

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Wafanyikazi hawakuruhusiwa kufunga jikoni walipokuwa wakizuiliwa, mgahawa huo umesema

    Wafanyikazi wote 19 katika mkahawa mmoja nchini Pakistan walizuiliwa baada ya kukataa kuwapa baga (burger) za bure kundi la maafisa wa polisi wiki iliyopita.

    Wafanyikazi wa Johnny & Jugnu mjini Lahore walikamatwa Jumamosi usiku na kuzuiliwa usiku kucha.

    Maafisa tisa wa polisi waliohusika katika tukio hilo sasa wamesimamishwa kazi.

    Afisa mwandamizi wa polisi wa mkoa Inam Ghani alitangaza kusimamishwa kwao katika mtandao wa Twitter, akisema: "Hakuna mtu anayeruhusiwa kuchukua sheria mikononi mwake. Udhalimu hautavumiliwa. Wote wataadhibiwa."

    Katika taarifa iliyochapishwa kwenye Facebook, Johnny & Jugnu ilisema maafisa hao wa polisi walikuwa wamekwenda kwenye mgahawa huo siku mbili kabla ya tukio hilo na kuomba burger za bure.

  9. Mlipuko wa Somalia waua zaidi ya wanajeshi 10

    Wanawake wanalia

    Chanzo cha picha, Reuters

    Zaidi ya wanajeshi 10 wameuawa baada ya mlipuaji wa kujitoa mhanga kujilipua katika kambi moja ya kijeshi iliyopo mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, ripoti zinasema.

    Mwanahabari aliyekua katika eneo la tukio amesema mlipuaji huyo alijidai kuwa mwanajeshi, na kuingia katika kambi ya jeshi ya Wadajir na kuanza kulipua vilipuzi alivyokuwa amejifunga kiunoni, wakati wa mafunzo ya asubuhi.

    Watu wengine 10 pia wamejeruhiwa.

  10. CPJ yamtaka Rais Samia kurekebisha sheria zinazokandamiza uhuru wa habari

    Samia

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Kamati ya kimataifa ya kulinda waandishi habari CPJ imemuandika barua ya wazi rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kumtaka arekebisha sheria mbalimbali ili kuhakikisha wanahabari wanafanya shughuli zao kwa uhuru na usalama.

    Barua hiyo ya wazi iliyosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kamati hiyo, Joel Simon imesisitiza kufanyika kwa marekebisho ya sheria ili hatua hizo ziwe na tija.

    ''Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita,CPJ imeshuhudia ukandamizwaji wa vyombo vya habari vya Tanzania, kufungiwa kwa vyombo vinavyokosoa, kukamatwa kwa wanahabari, kubughudhiwa kwa waaandishi wa mtandanoni na kulindwa kwa wale wanaowashambulia waandishi.

    ''Tunakuandikia kukutaka uchukue hatua kuhakikisha uhuru na mazingira salama kwa waandishi, kwa kurekebisha sheria ili kuendana na katiba ya Tanzania na mikataba ya kikanda na kimataifa'', ilisema sehemu ya barua hiyo.

    • Uhuru wa vyombo vya habari: Upi mustakabali Afrika Mashariki?

    CPJ imetaja baadhi ya sheria ambazo zinakinza uhuru wa habari na uhuru kujieleza nchini Tanzania ambazo zinapaswa kufanyiwa marekebisho ni pamoja na sheria makosa ya mtandao ya mwaka 2015, Sheria ya huduma za Habari za mwaka 2016, sheria ya upatikanaji wa habari ya mwaka 2016 na Marekebisho ya Sheria ya mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya mwaka 2020.

    Vinasa sauti

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Si mara ya kwanza kwa Kamati hiyo ya CPJ kuandika barua ya wazi kwa Rais wa Tanzania, mwaka 2019, iliwahi kumuandikia barua ya aina hiyo aliyekuwa rais wa Tanzania John Magufuli ikitaka serikali yake kufuta mashitaka dhidi ya mwandishi habari Erick Kabendera na itoe maelezo kuhusu aliko mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi, Azory Gwanda.

    Mara baada ya kuapishwa mwezi Machi mwaka huu kama Rais wa awamu ya sita, Rais Samia alitangaza kuvifungulia baadhi ya vyombo vya habari vilivyofungiwa kwa makosa mbalimbali.

    Hatua hiyo ilipokelewa vizuri na wadau wa habari wakiona kama ana nia njema ya kuhakikisha uhuru wa vyombo hivyo.

  11. Mamia ya nchi yapigwa marufuku kuingiza mbwa Marekani

    Mbwa

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Kituo Cha Marekani cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) kimetangaza marufuku ya mwaka mmoja ya kuagiza mbwa kutoka nchi 113 kwa kuhofia ugonjwa wa kichaa cha mbwa.

    Marufuku hiyo inahusisha mbwa wote, pamoja na wale wanaotumika kutoa msaada wa kifikra kwa wanaohitaji usaidizi wa wanyama hao na wale ambao wamekuwa katika nchi zenye hatari katika miezi sita iliyopita.

    Tangazo hilo linakuja wakati ambapo pamekuwa na ongezeko kubwa la watu wanaomiliki mbwa kati kati ya janga la Corona.

    ''Mamia ya mbwa hawa walikuwa na vyeti bandia vya kuthibitisha matibabu ya kichaa cha mbwa'', CDC imesema.

    "Hatua hii ni muhimu kuhakikisha afya na usalama wa mbwa walioingizwa Marekani na kulinda afya ya umma na kuzuia kuletwa tena kwa virusi mbali mbali vya ugonjwa wa kichaa cha mbwa," CDC ilisema katika taarifa.

    Marufuku hiyo inalenga nchi tofauti ikiwa ni pamoja na Kenya, Misri, Brazil na Urusi.

  12. Mamia wazidi kukimbilia kijiji kimoja Kwa-Zulu-Natal kuchimba 'almasi'

    Afrika Kusini

    Polisi nchini Afrika Kusini wanapata wakati mgumu kuwazuia mamia ya watu wanazidi kukimbilia kijiji kimoja katika eneo la Kwa Zulu-Natala kuchimba kinachoshukiwa kuwa madini ya almasi.

    Mamia ya watu walianza kwenda kijiji humo baada ya mchungaji mmoja wa ng'ombe kugundua kile alidhani ni almasi zaidi ya wiki moja iliyopita.

    aFRIKA kUSINI

    Ugunduzi wake umesababisha watu kutoka mikoa mingine kufanya safari ya kujiunga na utafutaji wa madini hayo ya thamani.

    Badhi ya wanaosaka madini hayo ni wanawake wasio na kazi ambao walikuwa wamekusanyika karibu na moto wakiota baada ya kutumia usiku mzima kuchimba kile wanachotarajia ni almasi.

    Afrika Kusini
    Afrika Kusini

    Serikali inatuma timu ya wataalam wa jiolojia na madini kudhibitisha ikiwa almasi imepatikana katika eneo hilo. Wakati huo huo polisi pia wako katika eneo la tukio lakini wanaonekana kuwa wanajitahidi kuzuia watu kuendelea kuchimba.

    Serikali ya mkoa imeelezea shughuli hii kama uchimbaji haramu wa madini.

  13. Kwanini bango hili linazua gumzo Nairobi

    Bango

    Chanzo cha picha, Facebook

    Maelezo ya picha, Tangu lilipobomolewa mara ya kwanza lilimekuwa likichungwa

    Utata unaozunguka hatua ya serikali ya kaunti ya Nairobi kuipatia barabara moja jijini humo ya jina la katibu wa muungano wa wafanyakazi humu nchini Farncis Atwoli unaendelea kufukuta.

    Katika hatua ya hivi punde bango hilo lililowekwa katika barabara ya Dik Dik na kupewa jina la Farncis Atwoli limechomwa moto.

    Tangu lilipobomolewa mara ya kwanza mwishoni mwa mwezi Mei limekuwa likilindwa lisibomolewe tena.

    Bango

    Chanzo cha picha, TWITTER

    Atwoli alikerwa na waliotekeleza shughuli hiyo na kutaka polisi kuazisha uchunguzi mara moja ili wawajibishwe kisheria.

    "Katika nchi ambapo watu wanaheshimu sheria, kuna utaratibu wa kufuata iwapo unapinga barabara hiyo kupewa jina langu.Naomba polisi kufanya uchunguzi,"Atwoli alisema.

    Wanaopinga kuwekwa kwa bango hilo wamekuwa wakitumia mtandao wa Twitter kuelezea malalamiko yao huku baadhi wakisema ni ukiukaji wa sheria.

    Akijibu hatua ya bango hilo kubomolewa kwa mara nyingine Bw. Atwoli amesema: Hilo halimuumizi. Badala yake amewauliza wanaofanya kitendo hicho wanajisikiaje. ''Unapata vipi usingizi ukifahamu fika kwamba wewe ni mharibifu''

    Ruka X ujumbe, 1
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 1

    Saa chache baadaye bango hilo lilirudishwa tena na picha zake kusambzwa mitandaoni

    Ruka X ujumbe, 2
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 2

  14. Tanzania yawarejesha nyumbani wakimbizi wanaotoroka ghasia Msumbiji

    Thousands have been forced to flee their homes

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Maelfu ya watu wamelazimika kutoroka makwao

    Mamlaka nchini Msumbiji zimesema kuwa zaidi ya raia 9,600 wa Msumbiji wanaokimbia vurugu kaskazini mwa Jimbo la Cabo Delgado "wamerudishwa kwa nguvu" kutoka Tanzania tangu Januari 2021, Diario de Noticias gazeti binafsi nchini humo limeripoti.

    Kulingana na Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa karibu watu 900 "walisukumwa kwa lazima" kuvuka mpaka kati ya tarehe 7 na 9 Juni.

    Ripoti hiyo inakuja saa chache baada ya manusura walionukuliwa na tovuti inayomilikiwa na watu binafsi O Pais, kufichua kwamba mji wa Palma kaskazini mwa Msumbiji, ulibaki ukikaliwa na wanamgambo, ambao wanachama wao wanaendelea "kuchoma nyumba, kuua na kuteka nyara watu".

    Mashambulio makubwa ya hivi karibuni ya kundi hilo dhidi ya mji wa Palma mnamo 24 Machi, yaliwahamisha zaidi ya watu 70,000, na kuongeza idadi ya watu waliohamishwa kutokana na ghasia kaskazini mwa Msumbiji hadi karibu 800,000.

    Mnamo mwezi Aprli Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania George Simbachewene alisema kuwa Ripoti ya Umoja wa mataifa juu ya Tanzania kurudisha wakimbizi wa Msumbuji haina uhalisia wowote.

    Katika mahojiano na BBC Simbachawene alisisitiza kuwa Tanzania inalinda mipaka yake na kujilinda dhidi ya magaidi ambao wakati mwingine wanaweza kujichanganya na wakimbizi na kisha kuingia nchini.

    Maelezo zaidi:

    • Tanzania: 'Tunapolinda mipaka yetu tusitafsiriwe kama tunawazuia wakimbizi'
    • Shambulizi la Palma Msumbiji: Kwanini kujihusisha kwa kundi la IS kunatiliwa chumvi
  15. Diamond na Tuzo za BET: Naheshimu mawazo ya kila mtu

    Diamond

    Chanzo cha picha, Diamond Platnumz

    Msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, Diamond Platnumz amewajibu wanaotaka aondolewe kwenye tuzo za BET, akisema ni mawazo yao na anayaheshimu.

    Diamond amezungumza hayo wakati akihudhuria mualiko wa tukio la sherehe ya mtoto wa muigizaji nyota wa filamu za Tanzania maarufu kama Bongo movie, Irene Uwoya, Krish.

    'Mimi naheshimu mawazo ya kila mtu, mtu akinifurahia, akinitukana akinisema mimi nashukuru', alisema Diamond kupitia kituo cha TV cha Wasafi, anachokimiliki.

    Diamond ambaye hajatoa nyimbo kwa zaidi ya miezi sita sasa, tangu jina lake litajwe mwezi Mei mwaka huu kuwania tuzo hizo za BET kumeanzishwa harakati za kumpinga msanii huyo mitandaoni ili aondolewe au asishinde tuzo hizo za mwaka huu za BET.

    Ni tuzo kubwa duniani, zinazohusisha wasaniii weusi duniani wenye asili ya Afrika.

    Wanaompinga msanii huyo kupitia mitandao ya kijamii wanadaiwa kufanya hivyo ili kuonesha hisia zao kutokana na msanii huyo 'kushiriki siasa akikiunga mkono chama tawala cha CCM' nchini humo, kilichoshinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 unaolalamikiwa kuwa na ulikuwa wa udanganyifu licha ya Tume ya taifa ya uchaguzi Tanzania kusema ulikuwa huru na wa haki.

    Lakini pia wanadai kwamba msanii huyo yuko karibu na wanasiasa, wanaodaiwa kukiuka haki za binadamu.

    Diamond anayetamba na wimbo 'Waa!' aliomshirikisha gwiji la muziki kutoka DRC, Koffi Olomide, licha ya kuhaidi kulizungumzia rasmi suala hili la kupingwa kwake kwenye tuzo hizo siku chache zijazo, alisema hatachukia mtu anayemsema vibaya.

    'Epuka sana kumchukia mtu anayezungumza kitu kibaya juu yako, huwezi kujua, kaamka leo kavurugwa hasira zake kakumalizia wewe, kesho mwenyewe akikaa atajuta na kukuomba msamaha', alisema.

    Soma zaidi:

    • Hamis Tale, asema harakati za kumpinga Diamond kushinda tuzo za BET hazitafanikiwa
  16. Karibu katika matangazo ya moja kwa moja leo Jumanne 15.06.2020.