Wanigeria wakimbilia kanisa la TB Joshua kumuomboleza

Taarifa za kifo cha mhubiri maarufu, Temitope Balogun Joshua, maarufu kwa jina la T.B Joshua zimeendelea kupokelewa kwa mshangao na raia wengi wa Nigeria na dunia kwa ujumla.

Moja kwa moja

Ambia Hirsi

  1. Tumefika mwisho wa taarifa zetu za moja kwa moja mpaka kesho panapo majaaliwa

  2. Tajiri mkubwa duniani kusafiri kwenda anga ya mbali

    Mwanzilishi wa kampuni ya Amazon Jeff Bezos

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mwanzilishi wa kampuni ya Amazon Jeff Bezos amesema atasafiri hadi anga la mbali na kaka yake katika safari ya kwanza kwa binadamu kuzinduliwa na kampuni yake, Blue Origin.

    Katika ujumbe kwenye mtandao wake wa Instagram, Bwana Bezos alisema safari ya anga la mbali ni kitu ambacho alikitamani sana "katika maisha yake yote".

    Kampuni ya Blue Origin ina nadi kiti kimoja katika chombo watakachotumia, kwa mtu mmoja kujiunga na wawili hao katika safari yao ya kwanza ya anga za mbali.

    Jeff Bezos ni mmoja kati ya matajiri wakubwa duniani.

    Thamani ya utajiri wake ni dola bilioni 186.2 sawa na (£131.5bn), kulingana na jarida la Forbes.

    "Julai 20, tunakwenda safari hiyo na kaka yangu," aliandika kwenye mtandao wake wa Instagram. "Safari ya kipekee na rafiki yangu.

    Kaka yake Bezos, Mark ameitaja kuwa "fursa ya kipekee" katika video hiyo.

    Akinadi kiti cha kwenda anga la mbali - jina gari la Blue Origin – lilikuwa limefika dola milioni 2.8 pale Bwana Bezos alipotangaza mpango wake wa kwenda anga la mbali. Mnada huo utakamilika Juni 12.

    Safari hiyo yenye kuongozwa na binadamu inawadia wiki mbili tu baada ya Bwana Bezos kujiuzulu kama mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Amazon.

    Na badala yake, atakuwa mwenyekiti mtendaji wa kampuni yake ya manunuzi mtandaoni iliyoanzishwa miaka 30 iliyopita ili kumuwezesha kuwa na "muda na nguvu" ya kuangazia biashara nyingine.

  3. Hali ya kawaida yarejea tena katika wilaya iliyokumbwa na volkano nchini Rwanda

    Rubavu

    Hali ya kawaida inarejea katika wilaya ya Rwanda iliyoathiriwa na volkano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wiki mbili zilizopita.

    Mlipuko wa volkano katika Mlima Nyiragogo uliua watu 32 na kuharibu mamia ya nyumba katika eneo la Goma nchini DR Congo. Baadaye kulikuwa na msururu wa mitetemeko ya ardhi katika mikoa ya jirani ikiwa ni pamoja na wilaya ya Rubavu nchini Rwanda.

    Wakazi wengi walitoroka baada ya nyumba na mali zao - pamoja na miundombinu - kuharibiwa.

    Huko Rubavu, biashara sasa zimeanza kufunguliwa. Shule na hospitali - ambazo pia zilikuwa zimefungwa kufuatia shughuli za volkano - zimeanza tena shughuli.

    Baadhi ya wakaazi wamekuwa wakilalamika juu ya ukosefu wa msaada wa serikali kujenga upya maisha yao.

    rUBAVU

    Sibomana Ibrahim aliambia BBC kwamba alilazimishwa kuhamisha wazazi wake baada ya nyumba zao kubomoka.

    "Tulikodisha nyumba huko Amakoro baada ya nyumba zetu nne kubomoka. Ilibidi nibaki hapa kulinda mali zetu, sasa ninaondoa udongo na uchafu kwenye nyumba.

    "Hatukuwa na msaada kutoka kwa serikali, isipokuwa chakula. Walituambia tungoje, sijui tutasubiri kwa muda gani," alisema.

    Niyoyita Zakia alisema alihamia mji mkuu Kigali na baadaye alirudi Rubavu na sasa alikuwa akiishi katika nyumba ya rafiki yake . Alisema ilikuwa nvigumu kukimu mahitaji yake na watoto wake wanane.

    Mamlaka huko Rubavu zimesema wale wote walioathirika watapata msaada lakini hawajaonyesha hii itakuwa kwa njia gani

    rUBAVU
  4. Kiongozi wa mapinduzi ya Mali kuapishwa kuwa rais

    Kanali Assimi Goita

    Chanzo cha picha, AFP

    Kanali Assimi Goïta leo anatarajiwa kuapishwa kuwa rais wa mpito wa Mali.

    Ni wiki mbili tangu amuondoe rais wa mpito na waziri mkuu katika mapinduzi - ya pili ndani ya miezi tisa.

    Wiki iliyopita, viongozi wa Jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika Magharibi, Ecowas, waliungana na Muungana wa Afrika kufutilia mbali uanachama wa Mali, kutoa wito kwa serikali ya jeshi kuzingatia kipindi cha mpito cha miezi 18 kuelekea uchaguzi mkuu wa urais mwezi Februari.

    Ufaransa na nchi zingine za Magharibi zinataka kurejeshwa kwa utawala wa kiraia.

    Mali ni kiungo ni muhimu katika uthabiti wa eneo la Sahel ambalo linakabiliwa na visa vya mara kwa mara vya uvamizi wa kijihadi.

    Maelezo zaidi:

    • Mapinduzi Mali: Jinsi ya kutatua kitendawili cha mapinduzi ya Mali
    • Mali: Kwa nini mapinduzi yanashangiliwa nyumbani, majirani wakilalamika
  5. Watu 36 wafariki katika ajali ya treni Pakistan

    At least 30 people have died in the crash, and several more are in a critical condition

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Watu kadhaa pia wameripotiwa kuwa katika hali mahututi

    Treni mbili za abiria zimegongana kusini mwa Pakistan, na kuua watu takriban 36 na wengine kadhaa kujeruhiwa.

    Maafisa walisema kuwa gari moshi moja lililokuwa likisafiri kwenda mkoa wa Sindh lilikuwa limepoteza mkondo na kuanguka katika njia ya reli. Treni ya pili iliyokuwa na abiria kisha iligongana nayo na kupinduka.

    Timu za uokoaji ziliwapeleka majeruhi katika hospitali za karibu na inadhaniwa kuwa watu kadhaa wako katika hali mbaya.

    Pakistan imeshuhudia msururu wa ajali mbaya za treni katika miaka iliyopita.

    Kati ya 2013 na 2019, watu 150 walikufa katika ajali kama hizo, kulingana na ripoti za vyombo vya habari nchini humo.

    Afisa mwandamizi katika wilaya ya Ghokti, Usman Abdullah, aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba ni vigumu kujua ni watu wangapi bado wamenaswa katika treni hizo.

  6. Wafuasi wa SCOAN: 'TB Joshua amesinzia atarudi'

    Maelezo ya sauti, Kifo cha TB Joshua chapokelewa kwa simanzi

    Habari za kifo cha Mhubiri maarufu, Temitope Balogun Joshua, maarufu kwa jina la T.B Joshua zimewashangaza raia wengi wa Nigeria na dunia kwa ujumla.

    Kanisa la Sinagogi kwa mataifa yote SCOAN ambalo lilianzishwa na mhubiri huyo lilithibitisha habari za kifo chake Jumapili alfajiri, huku chanzo kikiwa bado hakijawekwa bayana.

    Lakini ni kwa namna gani raia nchini humo waliopokea taarifa za kifo hicho?

    Mwandishi wa BBC Scolar Kisanga amezungumza na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria DKT. Benson Bana.

    Maelezo zaidi:

    • Mfahamu Temitope Balogun maarufu TB Joshua
    • Temitope Balogun Joshua: Fahamu Utabiri na utata uliomzunguka TB Joshua
  7. Uganda yafunga shule siku 42 kudhibiti maambukizi ya Covid 19

    Nchi hiyo imekuwa ikiripoti ongezeko la maambukizi

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Nchi hiyo imekuwa ikiripoti ongezeko la maambukizi

    Uganda imefunga shule zote pamoja na taasisi za elimu ya juu kwa siku 42 kufuatia wimbi jipya la maambukizi ya virusi vya corona.

    Nchi hiyo ilifunga shule zote mwezi Machi 2020, na kuzifungua kwa awamu tangu mwezi Oktoba. Lakini wanafunzi wa shule za msingi na upili walikuwa hawajarejea wote shuleni.

    Katika hotuba yake kwa taifa siku ya Jumapili, Rais Yoweri Museveni alisema waalimu wote sasa watahitajika kuchanjwa kabla ya kuruhusiwa kurejea kazini.

    Walikuwa wamejumuishwa katika kundi la kwanza la watu walioshtahili kuchanjwa wakati nchi hiyo ilipozindua kampeni ya chanjo ya corona mwezi Machi mwaka huu.

    Mikusanyiko yote ya kisiasa imesitishwa isipokuwa mikutano ya bunge na mahakama.

    Mikusanyiko ya umma pia imesitishwa kwa siku 42. Ni watu 20 watakaoruhusiwa kuhudhuria harusi au mazishi.

    Usafiri wa umma na wa kibinafsi kutoka kutika wilayani kuingia jiji kuu la Kampala zitapigwa marufuku kuanzia tarehe 10 mwezi Juni. Magari ya kusafirisha mizigo hayataathiriwa na marufuku hiyo.

    Shughuli nyingi za kiuchumi zitaendelea kama kawaida lakini hatua za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona zitaimarishwa.

    Nchi hiyo imethibitisha ongezekola hali ya juu ya maambukizi ya corona katika wiki mbili zilizopita ikilinganishwa na miezi iliopita.

    Jumla ya watu 1,259 wamethibitishwa kuambukizwa, kiwango cha juu zaidi kurekodiwa tarehe 4 Juni tangu janga la corona lilipoatangazwa.

  8. Pigano la Mayweather na Logan Paul lamalizika bila mshindi

    Floyd Mayweather Jr V Logan Paul

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mbabe wa masumbwi Floyd Mayweather Jr amekutana na kisiki asichokitarajia cha Logan Paul katika pambano la ndondi la kujiburudisha lililomalizika bila kupatikana mshindi.

    Paul, ambaye ni maarufu kwenye mtandao wa YouTube ameonyesha upinzani mkali katika pambano hilo la raundi nane dhidi ya Mayweather ambaye hajawahi kupoteza mchezo wowote kati ya michezo yake 50 ya ndondi aliyopigana.

    Kabla ya pambano hilo, Mayweather na Paul walieleza kwamba wanataka kutoa burudani ya kweli kwa wote wataotazama.

    Floyd Mayweather Jr V Logan Paul

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Utofauti wa uzoefu na uwezo katika masumbwi kati ya Mayweather na Paul, uliwafanya wengi kuamini kwamba Paul angegaragazwa mapema tu kwa Knock out, lakini Paul alioyesha kwamba si mshawishi tu bali hata kwenye ulingo wa masumbwi.

    Mayweather ambaye kama angetumia nguvu zake na uwezo wake wa kawaida basi angemshinda kirahisi Paul mapema tu, lakini alimsukumia makonde ya kawaida mpinzani wake huyo.

    Pambano hilo halikuwa la ushindani, lilikuwa la maonyesho na hakutangazwa mshindi kwa kuwa halikuwa na jaji.

  9. Mwanamfalme Harry na Meghan watangaza kuzaliwa kwa mtoto wao wa pili

    Mergan na Harry

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mwanamfalme Harry Mtawala wa Sussex na mke wake Meghan wametangaza kuzaliwa kwa mtoto wao wa pili, msichana.

    Lilibet "Lili" Diana Mountbatten-Windsor alizaliwa Ijumaa asubuhi katika hospitali ya Santa Barbara, California.

    Mama na mtoto wako katika hali nzuri ya kiafya, ilisema taarifa ya wanandoa hao.

    Kasri la Buckingham Palace limesema: "Malkia, Mwanamfalme wa Wales na Duchess wa Cornwall, na mtawala wa Cambridge na mkewe wamefahamishwa na wamefurahishwa na taarifa hizo."

    Mwanamfalme Harry na Meghan wamesema wamempatia mtoto wao wa pili jina la Lilibet ambalo ni jina la utani la Familia ya Kifalme kwa Malkia.

    Jina lake la kati, Diana, lilichaguliwa kumuenzi "bibi yake mpendwa", Malkia wa Wales.

  10. Kifo cha TB Joshua: Wanigeria wakimbilia kanisa lake kumuomboleza

    Mama huyu alishindwa kuhimili majonzi
    Maelezo ya picha, Mama huyu aliyeshindwa kuhimili majonzi anaonekana akilia

    Wafuasi wa Mhubiri wa Nigeria Temitope Balogun Joshua, maarufu TB Joshua wamekusanyinka katika makao makuu ya kanisa la Synagogue Church of All Nations [SCOAN] mjini Lagos kuomboleza kifo chake.

    Kifo cha TB Joshua kilichotokea Jumapili Alfajiri kumeiibua maswali mengi huku baadhi ya watu wakitaka kujua kilitokana na nini.

    Kanisa la SCOAN halikuthibitisha chanzo cha kifo cha ghafla cha mhubiri huyo.

    Dis woman outside di church break down begin cry as she hear di news
    Maelezo ya picha, Waumini walikusanyika katika ukumbi wakanisa hilo baada yakupokea taarifa za kifo cha TB Joshua

    Waumini na watu wanaoishi karibu na kanisa hilo walikusanyika kumuomboleza.

    "Alikuwa mtu wa Mungu. ISijawahi kuona mhubiri mkarimu anayewasaidia watu hata kama sio wafuasi wa kanisa lake," Saidat ambaye ni muumini wa dini ya Kiislamu aliiambia BBC.

    Nkiru, mmoja wa waombolezaji alisema"Nitamkosa sana. Sijui hili kanisa litaendele vipi baada ya kifo chake."

    Di church environment full wit pipo wey dey cry and lament di death of dia Prophet.
    Maelezo ya picha, Kina mama hao wanaonekana wakiwa na majonzi makubwa baada yakupokea taarifa za kifo cha TB Joshua

    Mke wake Evelyn Joshua, mmoja wa wahubiri wakuu wa kanisa la SCOANalielezea kugutushwa na kifo cha ‘'ghafla'' cha muwe wake.

    "Kumpoteza mwenza sio jambo rahisi; iwe ghafla ua la, inavunja moyo.

    "Majonzi huharibu ustawi wetu kwa ujumla. Lakini cha msingi ni kumtumainia Mungu." Mke wa TB Joshua aliongeza kusema.

    Prohpet TB Joshua and im wife, Evelyn Joshua
    Maelezo ya picha, Mhubiri TB Joshua na mke wake , Evelyn Joshua

    "Ni yeye tu [akiashiria Mungu] anaweza kutufariji wakati huu mgumu," alisema mke wa mhubiri huyo.

    Taarifa iliotolewa na kanisa lake la SCOAN siku ya Jumapili alfajiri ilithibitisha TB Joshua alifariki akiwa na umri wa miaka 57.

    Maelezo zaidi:

    • Mfahamu Temitope Balogun maarufu TB Joshua
    • Temitope Balogun Joshua: Fahamu Utabiri na utata uliomzunguka TB Joshua
  11. Hujambo na karibu katika matangazo mubashara leo Jumatatu 07.06.2021.