Nyota wa PSG Mauro Icardi awasili Tanzania

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina na Klabu ya PSG inayoshiriki ligi kuu ya Ufaransa, Mauro Icard amewasili nchini Tanzania.
Nyota huyo aliwasili na mkewe Wanda Icardi nchini humo kwa likizo ya siku kadhaa.
Wawili hao wanadaiwa kuwa katika hifadhi moja ya wanyamapori ambapo wanajivinjari.
Wakati Icardi akiendelea na mapumziko yake nchini Tanzania, timu yake ya Taifa ilienda sare ya 1-1 wiki hii na mahasimu wao Chile, mchexzo wa kufuzu fainali za kombe la dunia mwakani.
Kwa sasa Icardi amepoteza nafasi katika timu ya taifa, ambapo kocha Leonel Scaloni amekuwa akiwatumia zaidi Lionel Messi, Lautaro Martinez na Sergio Aguero.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa Instagram ujumbe









