Washukiwa katika shambulio la risasi dhidi ya Jenerali wa Uganda waoneshwa kwenye CCTV

Polisi nchini Uganda wametoa picha za mtaa za CCTV za wanaume wawili wanaoaminiwa kuhusika na jaribio la kumuua Waziri wa uchukuzi nchini humo.

Moja kwa moja

Dinah Gahamanyi

  1. Na mpaka hapa ndio tunafikia mwisho wa matangazo haya ya moja kwa moja kwa leo, tukutane tena kesho majaaliwa.

  2. Kenya inamshikilia Mghana anayeshutumiwa kwa utapeli akitumia mapenzi

    Mghana anayedaiwa kuwalaghai wanawake, anadaiwa kukutwa na vifaa vinavyohusishwa na uchawi

    Chanzo cha picha, DCI/KENYA

    Maelezo ya picha, Mghana anayedaiwa kuwalaghai wanawake, anadaiwa kukutwa na vifaa vinavyohusishwa imani za kishirikina

    Maafisa nchini Kenya wamemkamata raia wa Ghana anayedaiwa kufanya ulaghai kupata dola 83,000 (£58,490) kutoka kwa mwanamke katika kwa njia ya utapeli wa mapenzi.

    Idara yapolisi ya Upelelezi wa makasa ya jinai (DCI) imesema kuwa mwanamke ambaye ni meneja katika kampuni ya Tala, ambayo hutoa inayotoa mikopo midogo midogo kwa njia ya mtandao kwa Wakenya, alikutana Mghana anayeitwa Victor Anane kupitia mtandao wa kuchumbiana.

    "Mshukiwa... aaliyejitambulisha kama muhubiri, aliwasiliana na wanawake ambao walitaka wapenzi na kupendwa kupitia mtandao kwa kuwaahidi kuwa angeyafanya maisha yao kuwa bora zaidi kabla ya kuwatapeli pesa zao."

    Mwanamke huyo alimshuku Bw Anane tu pale alipotembelea nyumba yake iliyopo katika mji mkuu, Nairobi, polisi imesema.

    “Alishituka kumkuta vifaa vinavyohusishwa na uchawi na Imani za kichawi. Siku iliyotarajiwa kuwa ya tarehe ya kwanza ya mapenzi kati yao iligeuka kuwa mbaya,”ilisema idara ya DCI, huku ikituma picha za vitu vya ajabu kwenye Twitter vinavyodaiwa kuhusishwa na uchawi vilivyopatikana kutoka katika nyumba ya Bw Anane wakati maafisa walipoivamia:

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Maafisa pia walipata pesa bandia na vifaa vilivyotumiwa kutengeneza pesa bandia.

    Maafisa wa usalama wanasema baadhi ya pesa alizopewa mwanaume huyo zilichukuliwa kutoka kwenye akaunti za Tala.

    Mshukiwa, ambaye hajatoa kauli juu ya madai dhidi yake, anatarajiwa kufikishwa mahakamani kukabiliana na mashitaka ya kupata fedha kwa udanganyifu.

  3. Washukiwa katika shambulio la risasi dhidi ya Jenerali wa Uganda waoneshwa kwenye CCTV

    Gari la Jenerali Katumba Wamala lilinyunyiziwa risasi

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, Gari la Jenerali Katumba Wamala lilinyunyiziwa risasi

    Polisi nchini Uganda wametoa picha za mtaani za CCTV za wanaume wawili wanaoaminiwa kuhusika na jaribio la kumuua Waziri wa uchukuzi nchini humo.

    Gari la Jenerali Katumba Wamala lilinyunyiziwa risasi na watu wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki, na kumuua binti yake pamoja na dereva.

    Inadhaniwa kuwa alikuwa akifuatwa na washambuliaji kwa mbali kabla ya shambulio la Jumanne.

    Picha za video za CCTV zinawaonesha watu wawili. Mmoja wao amevalia fulana ya blu yenye mistari.

    Moja ya pikipiki hizo iligeuza eneo ambalo sio mbali kutoka eneo la tukio la shambulio, kabla ya kutoweka ndani ya kituo cha petroli.

    Jenerali Katumba Wamala alikuwa na mtoto wake wa kike, dereva na mlinzi aliposhambuliwa

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Jenerali Katumba Wamala alikuwa na mtoto wake wa kike, dereva na mlinzi aliposhambuliwa

    Hakuna hata sura ya mmoja wao inayoweza kutambulika.

    Kikosi cha pamoja cha ujasusi cha polisi, na jeshi kinachunguza tukio hilo la ufyatuaji risasi.

    Jeshi linasema linachunguza simu ambazo zinaonekana kuwa zilitumiwa kufanya mpango wa jaribio la mauaji.

    Uganda imeshuhudia mashambulio kadhaa ya aina hiyo ya watu maarufu katika kipindi cha miaka michache iliyopita.

    Huduma za ujasusi hazijaweza kutatua kisa chochote.

  4. Majaji saba kusikia na kuamua kesi ya rufaa juu ya BBI Kenya

    Martha Koome,  Jaji mkuu wa Kenya

    Chanzo cha picha, ZAKHEEM RAJAN

    Maelezo ya picha, Martha Koome, Jaji mkuu wa Kenya

    Majaji saba wataisikiza na kuamua juu ya kesi ya rufaa iliyowasilishwa dhidi ya uamuzi wa hivi karibuni wa Mahakama ya juu zaidi nchini Kenya kuhusu mchakato wa kuleta amani na maridhiano nchini humo (BBI).

    Hii imetangazwa na Rais wa Mahakama ya rufaa, Daniel Musinga, ambaye pamoja na mahakimu Roselyn Nambuye na Anne Okwengu, walikuwa wamekutana na mawakili Jumatano kwa ajili ya kutoa miongozo juu ya rufaa.

    Mawakili walikubaliana na mahakama kwamba rufaa inapaswa kusikilizwa kwa ukamilifu badala ya kusikiliza uamuzi wa awali wa mahakama pekee.

    Wakili James Orengo, ambaye amekata rufaa kwa niaba ya BBI na kiongozi wa Chama cha upinzani ODM Raila Odinga, amesema kuwa rufaa ambayo wameiwasilisha ni ya dharura sana na inahitaji kushughulikiwa haraka.

    Viongozi wanaounga mkono mchakato wa BBI, ikiwa ni pamoja na Rais Uhuru Kenyatta na Bw Odinga, wameitaka Mahakama ya rufaa kuingilia kati na kuzuia uamuzi wa Mahakama ya juu ambao ulizuia azma ya BBI inayolenga kufanya marekebisho katika katiba.

    Katika uamuzi wake Mahakama kuu ilibaini kuwa rais alitumia mamlaka yake kuzidi kiasi na kukiuka sura ya sita ya katiba, wakati alipoanzisha na kupigia debe mabadiliko ya katiba.

    Kikundi cha mawakili kilitahadharisha kuwa hiyo inaweza kuwa sababu ya kumshitaki rais.

  5. Jimbo la Florida lazuia michezo ya wasichana waliobadili jinsia

    Gavana wa Florida Mrepublican Ron DeSantis

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Gavana wa Florida Mrepublican Ron DeSantis alisema kwamba ni muhimu kwamba maadili ya mashindano ya shule za umma yanapaswa kulindwa

    Florida limekuwa jimbo la kwanza mwaka huu kupiga marufuku wanawake na wasichana waliobadili jinsia zao kushiriki michezo katika shule za umma ya kike.

    Gavana wa jimbo hilo Mrepublican, Ron DeSantis amesaini sheria ya marufuku hiyo Jumanne.

    Sheria hiyo inasema wanawake na wasichana wanapaswa kucheza katika timu za "jinsia ya kibaiolojia" iliyoandikwa kwenye cheti chao cha kuzaliwa.

    Wanaharakati kutoka makundi ya wapenzi wa jinsia moja, na waliobadili jinsia -LGBT wamepinga hatua hiyo ambayo wameitaja kama "kibaguzi", huku kundi moja kikiapa kupinga sheria hiyo kisheria.

    "Tunaamini kwamba ni muhimu kwamba maadili ya mashindano haya yanapaswa kulindwa," Bw DeSantis alisema alipokuwa akisaini sheria hiyo katika Shule ya Kikristo iliyopo katika mji wa Jacksonville.

    "Tutaenda kwa misingi ya kibaiolojia, sio kwa misingi ya itikadi wakati tunapofanya michezo."

    Mwakilishi wa jimbo la Florida Carlos Smith, Mdemocrat ambaye anatambuliwa kama Latino na anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja, alipinga muswada huo ambao ameutaja kama "wa kutisha".

    "Hii inachochea chuki dhidi ya waliobadili jinsia na kuwaweka watoto hatarinibila sababu yoyote ," aliandika kwenye Twitter.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  6. Mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari Félicien Kabuga ataka muda zaidi kuandaa kesi

      • Author, Yves Bucyana
      • Nafasi, BBC Swahili
    Kabuga anazuiliwa The Hague nchini Uholanzi tangu Oktoba kufuatia kukamatwa kwake nchini Ufaransa mnamo Mei

    Chanzo cha picha, IRMCT LIVE

    Maelezo ya picha, Kabuga anazuiliwa The Hague nchini Uholanzi tangu Oktoba kufuatia kukamatwa kwake nchini Ufaransa mnamo Mei

    Wakili wa Mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari ya Rwanda, Félicien Kabuga ameiomba mahakama ya kimataifa ya jinai (ICC) mjini The Hague kumpa muda zaidi ili kuandaa kesi kabla ya kuanza kusikilizwa kwa undani.

    Kabuga anazuiliwa The Hague nchini Uholanzi tangu Oktoba kufuatia kukamatwa kwake nchini Ufaransa mnamo Mei 2020, kwa tuhuma za mauaji ya kimbari.

    Kesi hiyo iliendelea tena Jumanne jioni, miezi sita baada ya kuahirishwa kwa ombi la pande zote mbili kujiandaa kwa kesi hiyo.

    Jaji alitangaza Jumanne kwamba mahakama ilikataa ombi la Kabuga, mwenye umri wa miaka 86, la kuachiliwa kwa muda kwa sababu za kiafya. Mahakama imesema kuwa madai hayo hayana msingi kwa sababu afya yake inafuatiliwa kwa karibu.

    Kesi hiyo iliendeshwa kwa njia ya video lakini Kabuga hakuonyeshwa kwenye picha hizo, lakini alisikika akijibu swali kwa lugha yake ya Kinyarwanda . Kabuga alisikika kwa sauti ya uzee na akionekana kuchoka.

    Wakili wa Kabuga, Emmanuel Altit, alisema wanahitaji muda wa ziada kuandaa kesi yenye faili kubwa, kwani kuna maombi waliyowasilisha mahakamani ambayo hayajapatiwa majibu na kulikuwa na ugumu katika uchunguzi wao.

    Alisisitiza kwamba upande wa utetezi bado unakabiliwa na tatizo la kulinda usalama wa mashahidi wao walioko nchini Rwanda na pia matatizo ya utendajikazi katika kipindi kigumu cha Covid 19.

    "Upande wetu uko katika wakati mgumu wa kufanyia kazi, wakati upande wa mashitaka ulipata muda wa miaka mingi wa kujiandaa kwa kesi hiyo,sisi tuna shida ya kuwa na timu ndogo," alisema Altit.

  7. AU yaondoa kwa muda uanachama wa Mali na kuonya kuiwekea vikwazo

    AU himetoa wito wa kurejea kwa utawala wa kiraia nchini Mali

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, AU himetoa wito wa kurejea kwa utawala wa kiraia nchini Mali

    Mali imeondolewa kwa muda uanachama wa Muungano wa Afrika kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya wiki iliyopita, yakiwa ni ya pili katika kipindi cha miezi tisa.

    Mapinduzi ya kwanza yalifanyika mwezi Agosti mwaka 2020 yaliyofuatiwa na mapinduzi ya kijeshi, lakini nchi hiyo ilirejea katika hali ya utulivu baada ya kutangazwa kwa viongoziwa kiraia kuongoza serikali ya mpito.

    Sasa kwasababu utawala umepinduliwa, kwasababu kwa mara nyingine tena utawala umepinduliwa na Mali inajipata ikiwa imetengwa.

    Katika taarifa yake AU imetoa wito wa kurejeshwa mamlakani kwa serikali ya kiraia ikisema kuwa haitasita kuiwekea vikwazo na hatua nyingine za adhabu iwapo wanajeshi hawataamrishwa kurudi katika kambi zao.

    Jumatatu, viongozi wa Jumuiya ya Afrika Magharibi - Ecowas pia waliiondoa kwa muda Mali katika uanachama wa jumuiya hiyo, na kuitolea wito serikali ya kijeshi kuheshimu kipindi cha mpito cha miezi 18 kuelekea uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika mwezi februari mwaka ujao.

    Kanali Assimi Goita, ambaye aliongoza mapinduzi, aliteuliwa kama rais wa mpito na mahakama ya kikatiba ya nchi hiyo siku nne zilizopita.

  8. Mlima Nyiragongo: Watu nusu milioni hawana maji safi huko DR Congo

    Wakazi waliokimbia nyumba zao, wakiwemo watoto wamekuwa wakipanga misururu mirefu kupata maji

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Wakazi waliokimbia nyumba zao, wakiwemo watoto wamekuwa wakipanga misururu mirefu kupata maji

    Karibu watu 500,000 huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameachwa bila maji safi ya kunywa baada ya mlipuko wa volkeno wiki mbili zilizopita Shirika la Médecins Sans Frontières (MSF) limeonya.

    Shirika hilo limesema kuwa ugonjwa wa kuhara ni janga na umekuwa tishio kubwa hivyo basi, kuna haja ya kuhakikisha watu wa mji wa Goma wamepata maji safi ya kunywa.

    Hifadhi na mabomba yaliharibiwa pale mlima Nyiragongo ulipolipuka Mei 22.

    Aidha, mamia ya maelfu ya watu bado hawajaweza kurejea katika nyumba zao.

    "Tunasaidia kutoa mahitaji ya dharura kwa watu waliolazimika kuhama makazi yao, lakini haitoshi," amesema Magali Roudaun, mkuu wa MSF anayeongoza shughuli za utoaji msaada huko DRC.

    "Tunahitaji msaada wa dharura kutoka kwa mashirika mengine ya kutoa misaada ili kusaidia watu."

    Shirika la MSF limesema timu yake ilikuwa inatoa huduma za matibabu katika mji ulio karibu wa Sake, "ambapo kati ya watu 100,000 na 180,000 wamekusanyika makanisani, shuleni, misikitini na mitaani".

    Mlima Nyiragongo, kilomita 10 (maili sita) kutoka mji wa Goma, ulilipuka na kusababisha mtirirko lava siku 10 zilizopita, na kupelekea mauaji ya watu 32, UN imesema.

    Kumekuwa na mitetemeko mingi nchini humo tangu tukio hilo .

    Katika juhudi za kutathmini kiwango cha hatari, wataalam wamepeleka ndege zisizokuwa na rubani katika kreta inayofuka moshi ambapo lava inayoyeyuka imekuwa ikimwagika.

  9. Nimenusurika, namshukuru Mungu, Jenerali wa Uganda aliyepigwa risasi azungumza

    shambulio dhidi ya jenerali katumba Wamala lilifanywa na wanaume wanne ambao walikuwa kwenye pikipiki.

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, shambulio dhidi ya Jenerali katumba Wamala lilifanywa na wanaume wanne ambao walikuwa kwenye pikipiki.

    Waziri na Jenerali wa Uganda Katumba Wamala ametoa shukran zake kufuatia shambulio lililomlenga Jumanne asubuhi, akimshukuru Mungu kwa kunusurika na shambulio hilo.

    Katika ujumbe alioutoa katika video fupi iliyorekodiwa kutoka katika Hospitali ya Medipal Katumba ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi amesema: ‘’Mungu amenipa nafasi ya pili. Nitakuwa vyema tena msiwe na wasiwasi, Sina majeraha mabaya, ni mikono tu, lakini nitakuwa sawa. Niko na madaktari na wanafanya kila liwezekanalo. Nawapenda nyie watu. Tafadhali muombeeni mama. Yuko katika hali mbaya’’.

    Binti yake Wamala Brenda Nantongo, na dereva waliuawa katika shambulio lililofanywa na wanaume wanne ambao walikuwa kwenye pikipiki.

    ‘’Nimenusurika, lakini binti yangu Brenda Nantongo Katumba na dereva wangu Haruna walikufa katika eneo la tukio. Sijui sababu ya shambulio hili. Hapakuwa na sababu ya kumaliza maisha ya watu wasio na hatia. Roho zao zipumzike kwa amani’’, Ujumbe wa Twitter wa Jenerali Wamala ulisema.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Mkuu wa majeshi ya Uganda David Muhoozi alikuwa mmoja wa maafisa wa jeshi waliofika kwenye eneo la tukio mara baada ya kutokea kwa shambulio hilo, ambalo limelaaniwa vikali na Rais Yoweri Museveni.

  10. Natumai hujambo na karibu tena kwa matangazo yetu mubashara ya leo tarehe 02.06.2021