Kenya na Tanzania zatia saini makubaliano ya kuondoa vikwazo mipakani

Tanzania na Kenya zimetia saini makubaliano ya kuondoa vikwazo vya kibiashara ambavyo vilikuwa vikizuia ushirikiano mzuri wa kufanya biashara.

Moja kwa moja

Dinah Gahamanyi

  1. Ndugu wa kiongozi wa kidini wa Uturuki akamatwa Kenya

    Baadhi ya wasukiwa wa jaribio la mapinduzi ya Uturuki, wakiwa wamepangwa wakati wa kesi, Agosti 2017

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Baadhi ya wasukiwa wa jaribio la mapinduzi ya Uturuki, wakiwa wamepangwa wakati wa kesi, Agosti 2017

    Vyombo vya habari vya Uturuki vinasema huduma za usalama zinazofanya kazi katika nchi za kigeni zimemkamata mpwa wa kiongozi wa kidini aliyeko uhamishoni Fetullah Gulen na kumrejesha nyumbani Uturuki.

    Taarifa hizo zinasema kuwa Selahaddin Gulen ni kiongozi wa kile ambacho serikali ya Uturuki inakiita shirika la ugaidi la Fetullah Gulen.

    Mke wa Selahattin Gulen Serriye, ambaye ni mwalimu nchini Kenya, aliweka video kwenye mtandao wa kijamii siku 11 zilizopita akisema kwamba mume wake ametekwa nyara mjini Nairobi, na kwamba anahofu kuwa anapelekwa Uturuki.

    Rais Recep Tayyip Erdogan anamlaumu Fetullah Gulen kwa jaribio la mapinduzi dhidi yake lililozimwa yapata miaka mitano iliyopita. Bw Gulen, ambaye anaishi nchini Marekani, alikanusha kuhusika na jaribio hilo

  2. Msanii wa muziki wa Jerusalema atoa wimbo mpya na Akon

    BJerusalema

    Msanii wa muziki wa Afrika Kusini Master KG, ambaye amepata umaarufu kwa wimbo wake Jerusalema, amewashirikisha Akon na David Guetta katika kibao chake kipya.

    Shine Your Lighti na midundo ya sauti ya kwaito na ujumbe wa wimbo huo ni kuhusu kusambaza upendo.

    Master KG alisema alitaka mchanganyiko mpya wa wimbo wa Jerusalema lakini aliamua kubadilisha azma hiyo baada ya Guetta kukubali kufanya naye kazi, umeripoti wavuti wa habari wa IOL.

    Guetta ambaye amefanya kazi na Akon kabla kushirikiana na msanii huyo mwenye uraia wa Senegal na Marekani katika wimbo Shine Your Light

    Master KG anasema anatumai wimbo mpya utahubiri umoja na upendo kwa duniai wakati ulimwengu ukikumbwa na janga

    Sikiliza wimbo hapa chini:

    Ruka YouTube ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje Mitandao ya kijamii inaweza beba matangazo

    Mwisho wa YouTube ujumbe

  3. Nyota wa filamu ya Tarzan adhaniwa kufa

    Joe Lara alicheza filamu iliyopeperushwa katika msururu wa vipindi vya TV miaka ya 1990  kama Tarzan: The Epic Adventures

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Joe Lara alicheza filamu iliyopeperushwa katika msururu wa vipindi vya TV miaka ya 1990 kama Tarzan: The Epic Adventures

    Nyota wa filamu ya Tarzan Joe Lara, anayefahamika zaidi kama Tarzan, anadhaniwa kufa baada ya ndege kuanguka katika jimbo la Tennessee.

    Joe Lara mwenye umri wa miaka 58 - ni miongoni mwa watu wanaoaminiwa kufariki wakati ndege ndogo aina ya jet ilipoanguka karibu na mji wa Smyrna Jumamosi.

    Mkewe, Gwen Shamblin Lara, ambaye alianzisha kanisa la kupunguza uzito wa mwili, pia ni miongoni mwa wahanga wa ajali hiyo. Wafanyakazi wa uokozi walibaini vifusi na mabaki ya miili ya binadamu katika eneo la ajali.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Bw Lara aliigiza nafasi kuu ya Tarzan katika televisheni mwaka 1989 Tarzan katika Manhattan kabla ya kucheza nafasi hiyo katika msururu wa vipindi vya TV vya Tarzan: The Epic Adventures.

    Alicha kucheza filamu mwaka 2002 na kuanza kazi ya uanamuziki wa muziki wa country (country music).

  4. Mlinzi wa Crystal Palace na Ufaransa Mamadou Sakho akaribishwa na Rais wa Zanzibar

    Mamadou Sakho amekuwa katika ziara ya mapumziko nchini Tanzania pamoja na familia yake.

    Chanzo cha picha, Ikulu/Zanzibar /Twitter

    Maelezo ya picha, Mamadou Sakho amekuwa katika ziara ya mapumziko nchini Tanzania pamoja na familia yake.

    Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi amemkaribisha Mamadou Sakho mchezaji wa timu ya Taifa ya Ufaransa na Mlinzi wa timu ya Crystal Palace ya Uingereza.

    Mamadou Sakho amekuwa katika ziara ya mapumziko nchini Tanzania pamoja na familia yake.

    ‘’Nimefurahi uwepo wako na tupo tayari kushirikiana nawe kuanzisha kituo cha michezo cha watoto, tuwape vijana wetu nafasi’’, amesema Rais Dk. Hussein Mwinyi.

    Sakho ambaye alimtembelea Rais wa Zanzibar baada ya kukubali kuwa Balozi wa Utalii wa Tanzania amesema angependa kuwa mmoja kati ya watu wa mwanzo kuanzisha kituo cha michezo cha watoto:

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  5. Burundi iko tayari kwa uwekezaji kutoka Kenya

    Ndayishimiye  aliimshukuru rais Uhuru Kenyatta  kwa mchango wake katika mchakato wa  kuleta amani nchini mwake.

    Chanzo cha picha, State House/Kenya

    Maelezo ya picha, Ndayishimiye aliimshukuru rais Uhuru Kenyatta kwa mchango wake katika mchakato wa kuleta amani nchini mwake.

    Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye amesema nchi yake iko tayari kuimarisha ushirikiano wake na Kenya pamoja na jamii ya kimataifa.

    Katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta mjini Kisumu Rais Ndayishimiye aliimshukuru rais Uhuru Kenyatta kwa mchango wake katika mchakato wa kuleta amani nchini mwake.

    Ndayishimiye ameelezea jinsi Burundi ilivyofanya mageuzi ili kuvutia wawekezaji wa kigeni ikiwemo kuwezesha mtu kufungua kampuni chini ya saa 24 .

    Rais Ndayishimiye amewakaribisha wawekezaji kutoka Kenya akisema kuna fursa nyingi za uwekezaji katika sekta za Kilimo,Utalii,Kawi,madini na Benki.

    Kiongozi wa upinzani wa Kenya Raila Odinga alituma ujumbe wa Twitter ambapo alielezea kuwa Ndayishimiye atakuwa mgeni wa heshima katika sikukuu ya Madaraka, ambapo Wakenya husherehekea siku taifa lao lilipojitawala lenyewe mwaka 1963 baada ya kuwa chini ya utawala wa Muingereza tangu mwaka 1920.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye alitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kisumu mwendo wa saa 10:15 asubuhi akiwa ndani ya ndege ya Kenya Airways Dreamliner.

    Ndayishimiye aliyeandamana na Mke wa Rais Angeline Ndayubaha (aliyeketi ), pembeni ni Bi Magreth Kenyatta

    Chanzo cha picha, State House/Kenya

    Maelezo ya picha, Rais Ndayishimiye ameambatana na mkewe Bi Angeline Ndayubaha (aliyeketi ), pembeni ni Bi Magreth Kenyatta

    Ndayishimiye aliyeandamana na Mke wa Rais Angeline Ndayubaha alipokelewa na kiongozi wa ODM Raila Odinga, waziri Raychelle Omamo Omamo na maafisa wengine wakuu wa serikali.

    Rais wa Burundi atakuwa mgeni wa heshima katika sherehe za Siku ya Madaraka zitakazofanyika Kisumu Jumanne.

  6. China yakomesha sera ya watu kuwa na watoto wawili pekee

    Mimba

    Chanzo cha picha, Getty Images

    China sasa imewaruhusu watu kuwa na hadi watoto watatu baada ya kupungua kwa kiwango cha watoto wanaozaliwa nchini humo.Hatua hiyo ni mabadiliko makubwa ya kisera kwa serikali ya nchi hiyo.

    Shirika la habari linalomilikiwa na serikali Xinhua, limesema uamuzi huo ulitangazwa siku ya Jumatatu katika mkutano wa viongozi wakuu wa chama cha kikomunisti .

    Tangazo hilo linajiri baada ya matokeo ya hesabu ya watu inayofanyika kila baada ya miaka kumi kuonesha kwamba idadi ya Wachina ilisajili ukuaji mdogo sana katika miongo iliyopita.

    Hatua hiyo imeishinikiza Beijing kubadilisha sera ili kuwauhusu watu kuwa na watoto watatu.

    China ilifutilia mbali sera yake ya mtoto mmoja mnamo 2016, na kuibadilisha na kikomo cha watoto wawili ambacho kimeshindwa kusababisha kuongezeka kwa idadi ya watu .

    Gharama ya kulea watoto katika miji imezuia wanandoa wengi wa China kuza watoto zaidi.Hatua hiyo ya hivi karibuni iliidhinishwa na Rais Xi Jinping katika mkutano wa viongoziwakuu wa kisiasa shirika la habari la serikali limesema Kutakuwa na "hatua za kuunga mkono, ambazo zitasaidia kuboresha muundo wa idadi ya watu wa nchi yetu, kutimiza mkakati wa nchi kukabiliana kikamilifu na idadi ya watu waliozeeka na kudumisha faida na utoaji wa nguvu azi ", Xinhua ilisema.

    Lakini wataalam wengine walikuwa na wasiwasi juu ya athari ya sera hiyo"Ikiwa kulegeza sera ya idadi ya watoto kungekuwa na ufanisi, sera ya sasa ya watoto wawili inapaswa kudhibitishwa kuwa na ufanisi pia," Hao Zhou, mchumi mwandamizi huko Commerzbank, aliambia Reuters."Lakini ni nani anataka kuwa na watoto watatu? Vijana wanaweza kuwa na watoto wawiliiwapo ni wengi. Suala la msingi ni gharama ya maisha ni kubwa sana na shinikizo za maisha ni kubwa sana."

  7. Kenya naTanzania zatia saini makubaliano ya kuondoa vikwazo mipakani

    Namanga
    Maelezo ya picha, Kusainiwa kwa makubaliano haya kunatarajiwa kurahisisha biashara kati ya Tanzania na Kenya

    Tanzania na Kenya zimetia saini makubaliano ya kuondoa vikwazo vya kibiashara ambavyo vilikuwa vikizuia ushirikiano mzuri wa kufanya biashara.

    Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania, Profesa Kitila Mkumbo alisema kuwa utiaji wa makubaliano hayo ni mojawapo ya jitihada za kuwezesha mahusiano ya biashara na nchi jirani kufuatia ziara iliyofanywa nchini Kenya

    Alisema jumla ya vikwazo 37 vilijadiliwa katika mkutano wa pande zote hapo awali na kati ya hivyo vikwazo 19 viliondolewa na pande zote mbili zilikubaliana na kuweka mpango maalumu wa kutatua masuala yaliyobaki

    Katika mkutano wa tano walijadili masuala ya kibiashara katika sekta za kilimo, forodha, uhamiaji na usafirishaji ambapo masuala 30 kati ya 64 na mengine yaliyobaki yamewekewa mkakati maalumu na muda wa utekelezaji.

    Miongoni mwa masuala makuu manne waliyotatua upande wa Tanzania ni:

    • Kuwezesha upitishaji wa bidhaa mpakani hususani vinjwaji baridi kama juisi kutoka Tanzania kwenda Kenya.
    • Kuondolewa kwa tozo za ukaguzi zilizokuwa zinatozwa na mamlaka ya Kenya kwenye bidhaa za Tanzania ikiwemo unga wa ngano wenye alama ya ubora kutoka mamlaka husika Tanzania.
    • Kuwezesha upitishaji wa mahindi kutoka Tanzania kwenda Kenya
    • Kuondoa ushuru wa asilimia 25 kwenye bidhaa za kioo kutoka Tanzania kwenda Kenya.
    Utiwaji saini wa makubaliano hayo umefuatia ziara ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu nchini Kenya  mapema mwezi Mei

    Chanzo cha picha, IKULU KENYA

    Maelezo ya picha, Utiwaji saini wa makubaliano hayo umefuatia ziara ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu nchini Kenya mapema mwezi Mei

    Waziri alisema kwa upande wa Kenya, mambo ambayo wameweza kukubaliana ni pamoja na kutoa upendeleo kwa bidhaa za saruji zinazozalishwa nchini Kenya ambazo zinakidhi matakwa ya vigezo vya uasili wa bidhaa za jumuiya ya Afrika Mashariki.

    Alisema kuwa jambo lingine ni kutoa upendeleo maalumu kwa vinywaji kutoka Kenya ikiwemo juisi za nanasi baada ya kukidhi vigezo vya bidhaa vya jumuiya ya Afrika Mashariki.

    Jambo lingine ni kuhakikisha bidhaa zinazoharibika haraka kama vile maziwa zinapewa kipaumbele zinapovuka mipaka kutoka Kenya kuingia Tanzania kwa kuzingatia taratibu za sheria ya forodha, huku jambo lingine likiwa ni kuongeza muda wa kibali cha kuingiza bidhaa za mifugo kutoka siku 15 hadi siku 30.

    Kwa upande wake Waziri wa Kenya wa Viwanda na Biashara Betty Maina amesema hatua hiyo ni nzuri ili kuimarisha biashara kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi wa Tanzania na Kenya.

  8. Mshukiwa wa utapeli wa mamilioni ya pesa akiwa Marekani kufikishwa mahakamani Kenya

    Stacey Marie Parker anatuhumia kuwatapelli Wakenya mamilioni ya fedha huku akidai watapata  faida zaidi

    Chanzo cha picha, DCI Kenya Twitter

    Maelezo ya picha, Stacey Marie Parker anatuhumia kuwatapelli Wakenya mamilioni ya fedha huku akidai watapata faida zaidi

    Mwanamke anayeshukiwa kuwa ndiye msimamizi wa mpango wa utapeli ambao ulitumiwa kuwalaghai Wakenya mamia ya mamilioni ya pesa amekamatwa mwishoni mwa wiki na atafikishwa mahakamani leo.

    Stacey Marie Parker mwenye umri wa miaka 50, alikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jumamosi alipowasili kutoka Marekani.

    Mshukiwa alikamatwa kufuatia uchunguzi ulioendeshwa na idara ya makosa ya Jinai nchini Kenya baada ya kuhusishwa na sakata hiyo ya ulaghai iliyopora pesa za wawekezaji ambao hawakujua kwamba wanahadaiwa.

    Katika mpango ulioratibiwa na kupangwa vizuri, wawekezaji walidanganywa kuwekeza pesa zao katika programu ya mtandaoni inayojulikana kama Amazon Web Worker, kwa kudhani kuwa watapata faida kubwa ya hadi 38% kwa amana inayodumu kwa siku 7 tu.

    Kumbi za mitandao ya kijamii zilikuwa zimejaa matangazo yaliyowashawishi Wakenya kujiunga na mpango huo ili wapate faida .

    Wakenya wasio ambao hawakujua kwamba mpango huo ulikuwa utapeli walipakua programu kwa wingi na wakasajiliwa huku wengi wakiweka amana zao. Wengine waliwapeleka wapendwa wao , watoto na marafiki wa karibu kwenye mpango huo, kwa nia ya kupata utajiri wa haraka.

    Hadi wakati programu hiyo ilipofutwa kutoka mtandaoni bila taarifa kwa wawekezaji , ndipo wawekezaji walipogundua walikuwa wamedanganywa.

    Walishtuka kujua kwamba programu hiyo haikuhusishwa kwa njia yoyote na Amazon, kampuni ya teknolojia ya kimataifa iliyo nchini Marekani Programu hiyo ilizama na amana zenye thamani ya mamia ya mamilioni ya pesa .

  9. Jumuiya ya AfriKa Magharibi (ECOWAS) yaivua Mali uanachama

    Kanali Goïta  aliambiwa aendeshe uchaguzi mwezi Februari mwaka ujao

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Kanali Goïta aliambiwa aendeshe uchaguzi mwezi Februari mwaka ujao

    Jumuiya ya Afrika Magharibi Ecowas wameiondoa Mali katika uanachama wa Jumuiya hiyo kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika nchini humo wiki iliyopita -yakiwa ni ya pili katika kipindi cha miezi tisa.

    Kiongozi wa mapinduzi na ambaye sasa ni Kanali Assimi Goïta, alihudhuria mkutano katika mji mkuu wa Ghana, Accra.

    Waziri wa mambo ya nje wa Ghana Shirley Ayorkor Botchwey aliwambia waandishi wa habari kwamba jumuiya hiyo imeitolea wito Mali kumteua Waziri Mkuu mpya ambaye anafaa kuwa raia mara moja, ili kuheshimu kipindi cha mpito cha miezi 18 na kufanya uchaguzi wa urais mwezi Februari.

    Ghana ilisema utulivu wa Mali ni muhimu ili Afrika Magharibi iweze kudhibiti harakati za ugaidi katika kanda hiyo.

    Kanali Goïta alinyakua mamlaka baada ya kuamuru kukamatwa kwa Rais Bah Ndaw na waziri mkuu Moctar Ouane.

  10. Mchezaji wa Crystal Palace ya na Ufaransa Mamadou Sakho, akubali kuwa balozi wa Utalii Tanzania

    Mamadou Sakho

    Chanzo cha picha, Mamadou Mamadou Sakho /Twitter

    Mchezaji wa timu ya mpira wa miguu wa klabu ya Crystal Palace inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza (EPL) na Mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa amekubali ombi la Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kuwa Balozi wa hiyari wa utalii wa Tanzania.

    Mamadou Sakho amekubali ombi hili wakati alipokutana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TTB, Betrita Lyimo katika Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro.

    mekuwa nchini Tanzania tarehe kwa mapumziko ya siku 10 akiwa ameambatana na familia yake

    Chanzo cha picha, Mamadou Sakho/Twitter

    Maelezo ya picha, Mamadou Sakho amekuwa Tanzania kwa ziara ya mapumziko pamoja na familia yake

    Mamadou ambaye ni raia wa Ufaransa amekuwa nchini Tanzania tarehe kwa mapumziko ya siku 10 akiwa ameambatana na familia yake ambapo alitemebelea maeneo ya utalii nchini humo ikiwa ni pamoja na Hifadhi ya wanyama ya Serengeti.

  11. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mubashara leo tarehe 31.05.2021