Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Waziri mkuu wa Tanzania Majaliwa awasimamisha kazi Watendaji wa wizara ya Fedha

Taarifa hiyo imemnukuu Majaliwa akisema Sh155 milioni zililipwa kwa baadhi ya watumishi zikiwa ni posho yakuandaa miongozo wakazi.

Moja kwa moja

  1. Na kufikia hapo tumefikisha mwisho matangazo yetu ya moja kwa moja.Kwaheri

  2. Zimbabwe yamkamata mwizi anayevalia kama ‘shetani’

    Mtuhumiwa wa wizi amekamatwa katika wilaya ya kusini mwa Zimbabwe ya Gutu kwa madai ya kutumia vazi la "shetani " kuwatisha waathiriwawake kabla ya kuwaibia, vyombo vya habari vinaripoti.

    Paul Nyathi, msemaji wa polisi wa kitaifa, alisema kuwa uchunguzi umethibitisha kwamba mtu huyo - aliyejulikana kama Norman Chagwiza - alikuwa ameiba katika nyumba mbili.

    "Angejifanya kama shetani kwa kuvalia nguo za kutishana wakati watu wanakimbia, angeiba mali zao," Bw Nyathi alinukuliwa akisema katika tovuti ya News Day.

    "Aliiba ngazi katika nyumba fulani, kisha katika tukio lingine, alifunga mlango kutoka nje wakati akijaribu kuiba paneli za kawi ya jua , lakini mmiliki wa nyumba hiyo alivunja mlango na kumfukuza hadi akamkamata," ameongeza.

    Bw Chagwiza, 27, bado hajatoa tamko juu ya madai hayo.

  3. Kenya sasa itawachanja waliopewa dozi ya kwanza pekee -Waziri wa Afya

    Wizara ya afya ya Kenya imeshauri hospitali kuacha kutoa dozi ya kwanza ya chanjo ya AstraZeneca COVID-19. Waziri wa Afya Mutahi Kagwe anasema shehena ya chanjo inayowasilinchini humo hivi leokutoka Covax imemekusudiwa wale wanaostahili dozi ya pili ya chanjo hiyo.

    Zaidi ya Wakenya 950,000 ambao waliopokea dozi yao ya kwanza ya chanjo ya Covid-19 katikati ya Machi watapokea dozi ya pili kutoka leo.

    Waziri wa afya wa nchi hiyo anasema chini ya hali ya sasa itakuwa bora kuhakikisha kuwa watu hawa wamepewa chanjo kamili.

    Dozi moja ya chanjo ya Oxford-AstraZeneca inatoa karibu 70% ya kinga kwa angalau wiki 12 na asilimia 81 baada ya dozi kamili.

    Waziri alisema wale ambao bado hawajachanjwa watapewa chanjo zingine kama vile Johnson na Johnson. Walakini, bado haijulikani ni lini itawasili

  4. Mamia ya maelfu watoroka mlipuko wa Volkano DR Congo

    Umoja wa Mataifa umeonya kwamba zaidi ya watu 400,000 wametoroka mji wa Goma nchini DR Congo kutokana na hofu ya kuzuka kwa mlipuko mwengine wa Volkano karibu na mto Nyiragongo.

    Siku ya Alhamisi , maafisa waliagiza watu waondoke katika mji huo, kwa madai kwamba lava ya Volkano inayoingia ziwa Kivu inaweza kusababisha tsunami na wingu la gesi ya sumu.

    Nusu ya mji huo umesalia mahame.

    Kuondoka huko kwa watu kulisababishwa na kuongezeka kwa matetemeko ya ardhiyaliokuwa yakitoka katika mlima Nyarigongo na hofu huenda ukalipuka tena.

    Mamia ya maelfu ya wakaazi wametoroka.

    Mji wa Sake umefurika watu na sasa wanaelekea nchi jirani ya Rwanda , hifadhi ya wanyamapori ya Virunga na hata Ziwa Kivu.

    Mashirika yá misaada yameanza kutoa msaada huku watu walioachwa bila makao wakitafuta chakula na maji .

    Mitetemeko ilikuwa michachesiku ya Alhamisi usiku – hali iliosababisha wengine kuwa na matumaini kwamba hali huenda ikawa shwari.

    Lakini sauti kadhaa zimekuwa zikisikikakutoka kwa mlima huo.

  5. Waziri mkuu wa Tanzania Majaliwa awasimamisha kazi Watendaji wa wizara ya Fedha

    Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi mkaguzi mkuu, mkaguzi msaidizi na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Fedha na Mipango kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma zinazowakabili.

    Majaliwa amemuagiza mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru), Salum Hamdun kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma hizona endapo itabainika kwamba si kweli wahusika warejeshwe kazini.

    Majaliwa amezitaja tuhuma hizo kuwa ni malipo yaliyofanyika Machi 31, 2021 kupitia vocha 30 ya Sh251 milioni yakielezwa kuwa ni malipo maalum bila kutaja kazi iliyofanywa na waliofanya kazi hizo

    Taarifa hiyo imemnukuu Majaliwa akisema Sh155 milioni zililipwa kwa baadhi ya watumishi zikiwa ni posho yakuandaa miongozo wakazi.

  6. Magugu yanavyohatarisha maisha ya wanyama pori na mifugo hifadhi ya Ngorongoro

      • Author, Aboubakar Famau
      • Nafasi, BBC News, Dodoma

    Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro nchini Tanzania-NCCA imeanzisha kampeni maalumu ya kuondoa magugu vamizi kwa kutumia mapanga na matrekta.

    Mamlaka hiyo, imeamua kuchukua hatua hiyo, baada ya tafiti zilizofanywa kubaini kwamba, magugu hayo ambayo ni vamizi na hatari kwa ekolojia ya Bonde la Hifadhi ya Ngorongoro yameenea kwa asilimia 22 katika eneo ambalo linaaminika kuwa na idadi kubwa ya wanyama pori hivyo kuhatarisha maisha yao pamoja na mifugo.

    Hifadhi ya Ngorongoro ni moja wapo ya vivutio muhimu kabisa vya utalii nchini Tanzania, lakini pia ni ya sehemu kihistoria inayotumiwa kufanya tafiti mbalimbali.

    Elia Kimat, ni kijana wa kimasai ambae ni mzaliwa katika eneo la Ngorongoro lakini pia ni mfugaji, anakiri kuwepo kwa magugu haya tangu miaka ya nyuma, lakini yamekuwa yakionekana juu ya milima.

    “Miaka iliyopita, ilikuwa haijazidi hivi. Sasa mwaka 2020, kulikuwa na mvua kubwa, ndio ilizidisha kuleta mbegu za mimea hii, ndio maana imezidi ndani ya kreta,” anasema Kimat, mwenye umri wa miaka 36.

    Kreta, au kwa jina jengine kaldera, ndio kivutio kikubwa cha Hifadhi ya Ngorongoro hivyo wenyeji wanasema, ndio kitovu cha utalii wa eneo hilo.

    Watalii kutoka ndani na nje ya nchi wamekuwa wakifurika katika eneo hili, kwa sababu, ndio eneo pekee mtalii analoweza kuwaona wanyama pori kama vile simba, tembo, punda milia, twiga na wengine kwa uharaka na katika eneo moja.

    Hata hivyo, kusambaa kwa magugu vamizi kwa asilimia ishirini na mbili katika eneo hili, kunahatarisha uwepo wa kreta katika siku za usoni.

    Dk Freddy Manongi, ambae ni Kamishna wa Uhifadhi wa NCCA ameiambia BBC kuwa hatua zinaendelea kuchukuliwa:

    “Kwanza tumegundua, kuagiza udongo kwa ajili ya ujenzi wa barabara kuna madhara, hivyo tumeamua, kwanza kutumia mchanga wa ndani lakini pia kuzipandisha hadhi barabara kuu kutoka kuwa za udongo ziwe za barabara ngumu.”

    Kuhusu njia za kibaiolojia au kikemikali kupambana na magugu vamizi amesema: “Hizi njia zina madhara yake kama hazitatumika vizuri, kwa hiyo, bado tunafanya utafiti kujua ni njia gani tunaweza kuzitumia.”

  7. Vikosi vya kigeni kuisaidia Msumbiji dhidi ya Magaidi

    Viongozi wa baadhi ya mataifa ya kusini mwa Afrika wamekubali kuanzisha jeshi la pamoja la dharura ambalo litakabiliana na wanamgambo wa kiislamu katika mkoa wa kaskazini wa Cabo Delgado nchini Msumbiji.

    Viongozi wa SADCwamekubaliana katika mkutanosiku ya Alhamisi kwamba jeshi hilo litaongozwa na Msumbiji.

    Litashirikisha wanajeshi kutoka mataifa ya SADCijapokuwa hakuna idadi ya wanajeshi iliotajwa.

    Kuna hofu kwamba mashambulizi ya Msumbiji huenda yakatapakaa jadi mataifa Jirani.

    Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi, ambaye pia ndiye kaimu mwenyekiti wa SADC amesema kuwa hatua hiyo itasaidia katika kuwapunguza nguvu wanamgambo hao mbali na kuharibu vyanzo vyao vya silaha na mikakati.

    Alitetea ushirikiano huo aliodai kwamba unaweza kwa urahisi kukabiliana na ugaidikaskazini mwa Msumbiji bila kukatiza tamaa za mataifa mengine yanayotoa usaidizi, ndugu na mashirika ya kimataifa.

    Marekani Ufaransa na Ureno iliotawala eneo hilo tayari zilikuwa zimeonesha hamu ya kutaka kutoa usaidizi wa kiufundi na mafunzo kwa wanajeshi wa Msumbiji.

  8. Diamond platinumz kuwania tuzo za BET

    Wasanii watatu wa Afrika wameteuliwa kuwania tuzo za BET nchini Marekani.

    Diamond Platinumz wa Tanzania, Wizkid na Burnaboykutoka Nigeria pamoja na wasanii wa Ufaransa .

    Burnaboy aliibuka mshindi wa orodha hiyo mwaka uliopita .

    Wasanii hao watawania tuzo ya mwanamuziki bora wa kimataifa.

    Tuzo za BET zitafanyika tarehe 27 mwezi Juni na watu watahudhuria tamasha lake baada ya kufanyika kwa video mwaka uliopita kwasababu ya mipuko wa virusi vya corona.

    Wanamuziki wa Marekani Megan Thee Stallion na DaBaby wameteuliwa mara saba kila mmoja kuwania tuzo tofauti .

    Card B na Drake pia wametueliwa kuwania tuzo tano.

  9. Natumai hujambo