Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ziarani nchini Kenya
Ziara hiyo ya rais Samia ni muendelezo wa jitihada za nchi hizo mbili kuboresha na kuendeleza uhusiano wa muda mrefu
Moja kwa moja
Ambia Hirsi
Uganda yaharamisha utoaji watu kafara

Chanzo cha picha, Science Photo Library
Maelezo ya picha, Mtu yeyote atakayekutwa na viungo vya binadamu atakabiliwa na kifungo cha maisha Bunge la Uganda imepitisha mswada wa kuharamisha kutoa watu kafara na kupendekeza kifungo cha maisha kwa wale watakaovunja sheria .
Kabla ya kufikiwa kwa hatua hiyo sheri aya nchi hiyo haikuwa na sheria maalum ya kuangazia uhalifu wa kutoa watu kafara na badala yake kosa hilo lilikuwa likihukumiwa ka mauaji.
Mswada huo pia unaharamisha mtu kupatikana na viungo vya mwili wa binadamu, utumizi wa vungo hivyo kwa dawa au kuuza kwa maslahi ya kibinafsi.
Mtu atakayepatikana na hatia hiyo anakabiliwa na kifungo cha maisha gerezani.
Takwimu zinazoashiria ukubwa wa utowaji kafara wa watu unatofautiana katika maeneo tofauti nchini Uganda kwasababu visa hivyo haviripotiwi katika maeneo mengine ama hakuna hatua ya kisheria inayochukuliwa kikamilifu kuhusiana na uhalifu wa aina hiyo.
Kulingana na utafiti wa mwaka 2014 uliofanywa na Tume ya kutetea haki nchini Uganda kuhusu utoaji kafara, watoto hususan wale walio na umri wa chini ya miaka sita umeshamiri sana
Kulingana na mswada huo manusura wa utoaji kafara ya binadamu watapewa ushauri nasaha na kulipwa fidia.
Mswada huo utakuwa sheria pale Rais atakapotia saini kuuidhinisha .
BAWACHA: 'Ndugai anavunja katiba wazi wazi'
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Eagan Salla
- Nafasi, BBC Swahili, Dar es Salaam

Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Mendeleo Chadema wamemtaka spika wa bunge la Tanzania Job Ndugai kusimamia katiba na sheria kwenye swala linalowahusu wabunge 19 wa viti maalumu waliofukuzwa uanachama Chadema.
Wakiongozwa na aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Mlimba Suzan Kiwangwa wanamtaka spika Ndugai kutangazia wazi ni lini alipokea barua hiyo inayomuarifu juu ya kufukuzwa kwao uanachama.
Kumekuwa na kauli zinazo kinzana kati yake na naibu wake juu ya swala wabunge hao 19 wa viti maalum
Sakati hiyo imechukua sura mpya baada ya spika Ndugai kwa mara ya kwanza kukiri bungeni kupokoa nyaraka inayolihusu suala hilo kutoka chadema.
Akizungumza bungeni Ndugai alionya viongozi wa vyama vya siasa kutokumuandikia barua alizoziita vipeperushi kumpa maelekezo juu ya namna ya kuliendesha bunge kwani ni wajibu wake kuwalinda wabunge.

Maelezo ya picha, Wanawake hao wanamtaka spika Ndugai kutangazia wazi ni lini alipokea barua hiyo 
Bw. Ndugai walisema iwapo kuna haja ya kufanya hivyo basi wahusiska waambatanishe katiba ya yao kipengele kilicho vunjwa na muhtasari wa kikao kilichofanya maamuzi wanayotaka achukue juu ya mhusika au wahusika ili naye na wataalamu wake wajiridhishe jiwapo wanaotakiwa kufukuzwa walitendewa haki kwa kusikilizwa.
Ndugai amesema viko vyama ambavyo vimejaa udikteta na mfumo dume ambapo kundi la wanaume linakaa na kuwafukuza wanawake “kundi la wanawake tupu wabunge 19 wanafukuzwa hata kama ingekuwa ni chama changu CCM kinafukuza wanawake 19 kwa barua tu kipeperushi lazima ningewaambia wasubiri”
Kwa sasa Spika amewataka wabunge hao 19 wakiongozwa na Halima Mdee,kuendelea na kazi bila ya wasiwasi wakati wakisubiri baraza kuu la chama hicho kusikiliza rufaa yao.
- Athari za kuwafukuza wanachama 19 wa Chadema
Rais Kenyatta na Samia wafanya mazungumzo ya faragha

Chanzo cha picha, Ikulu ya Rais Kenya
Rais Samia Suluhu Hassan na mwenyeji wake Uhuru Kenyatta wa Kenya wapo katika mazungumzo ya faragha katika Ikulu ya Rais, jijini Nairobi.
Mama Samia amewasili asubuhi ya leo jijini Nairobi na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo kabla ya kuelekea Ikulu ambapo alipokelewa na Bwana Kenyatta.
Mazungumzo hayo ya ndani yanatazamiwa kuhususisha masuala mbalimbali kipaumbele kikiwa ni kukuza ushirikiano wa kibiashara na mahusiano ya kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili jirani.
Baada ya mazungumzo hayo, marais hao wawili wanatarajiwa kufanya mkutano na waandishi wa habari na kueleza baadhi ya mambo waliyokubaliana.
Rais Samia yupo Kenya kwa ziara ya siku mbili na hapo kesho mchana anatarajiwa kuhutubia Bunge la Kenya.
Soma zaidi:
- Ziara ya Samia Kenya: Biashara, Diplomasia na Jumuiya ya Afrika mashariki kupewa kipaumbele
- Samia Suluhu Hassan: Rais mpya anayekabiliana na dhana ya kutokuwepo kwa corona Tanzania
Fahamu Kwanini wastaafu wengi Nigeria wananyimwa pensheni zao
Maelezo ya video, BBC Africa Eye : Kwanini wastaafu wengi Nigeria wananyimwa pensheni zao Bunge la Uganda lapitisha sheria kuhusu uhalifu wa kijinsia

Chanzo cha picha, Getty Images
Bunge la Uganda limepitisha sheria ya kina kuhusu uhalifu wa kijinsia, ikifuta baadhi ya vifungu katika sheria ya jinai ya miongo kadhaa.
Hatua hiyo mpya inatoa nafasi ya kubuniwa kwa sajili ya kitaifa ya wahalifu wa kingono.
Mtu yeyote atakayefungwa kwa kuwa mhalifu wa kingono jina lake litaorodheshwa katika sajili hiyo ndani ya siku kumi ya mahakama kutoa hukumu yake.
Watalazimika kutoa maelezo kuhusu historia yao wakati wa kuomba nafasi ya kazi, au nafasi yoyote ambayo inawaweka hatarini watoto wanaowatunza.
Na kwa mara ya kwanza, sheria juu ya unyanyasaji mitaani, unyanyasaji wa kijinsia katika maeneo ya umma na vile vile unyanyasaji katika mazingira ya kitaalam imeanzishwa.
Sheria hiyo pia inatoa adhabu yaya kifungo cha miaka saba gerezani kwa mtu yeyeote atakayesambaza video zilizo na maudhui ya kiutuuzima katika mitandao ya kijamii.
Wanaharakati wanasema sheria hiyo itasaidia kukabiliana na visa vya watu kuvujisha video za ngono kama hatua y akumhujumu muathiriwa, katika baadhi ya visa video kama hizo zinasambazwa kutoka kwa akaunti ya muathirika.
sheria hiyo mpya pia inaharamisha utalii wa kingono unaohusisha watoto.
Pia unaweza kusoma:
- Mama wa Kiganda ambaye haoni aibu kuwa na mtoto anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja
Iraq yapiga marufuku maonyesho ya Televisheni ya ugaidi

Chanzo cha picha, RASLAN’S SHOOTING
Vipindi viwili vya televisheni ambavyo vimezua ghadhabu nchini Iraqi kwa kuwafanyia mzaha watu maarufu kwa kutumia vilipuzi bandia na kuiga visa vya utekaji vimesitishwa.
Mmalaka ya mawasiliano imesema vipindi hivyo - Tony's Bullet na Raslan's Shooting - vimekiuka kanuni za mawasiliano.
Kipindi kimoja cha Risasi ya Raslan, mwigizaji alizimia kwa hofu baada ya kufungwa vilipuzi bandia.
Watazamaji walikosoa vipindi hivyo kwa kuendekeza ukatili hasa ikizingatiwa vitisho vya mara kwa mara kutokana na mashambulio yanayofanywa na wanamgambo nchini Iraq.
Islamic State imetimuliwa katika ngome yake Iraq lakini kundi hilo limeendelea kuwashambulia raia na wanajeshi.
EU yafuta mpango wa kutuma waangalizi wa uchaguzi wa Ethiopia
Umoja wa Ulaya EU, umefuta mpango wa kuwatuma waangalizi wake katika uchaguzi wa Ethiopia utakaofanyika mwezi Juni kwa "kutoafikiana kuhusu masuala kadhaa muhimu".
Mwakilishi Mkuu wa Muungano huo Josep Borrell amesema viwango vinavyohitajika kama vile uhuru wa waangalizi na kuingiza nchini humo vifaa vya mawasiliano kwa ajili ya usalama wao umezuiliwa.
"Inasikitisha kwamba EU haujapewa hakikisho kuhusu kwamba watu wa Ethiopia watapata nafasi ya kushiriki uchaguzi huo kwa njia ya kidemokrasia," aliandika katika taarifa iliyowekwa mtandaoni:
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
EU imetoa wito kwa serikali ya Ethiopia kuendesha uchaguzi huru na wa haki.
Muungano huo umesema utaunga mkono kwa bodi ya uchaguzi kwa euro milioni 20 ($24m; £17m).
Ethiopia inajiandaa kufanya uchaguzi mkuu Juni 5. Uchaguzi huo uliahirishwa kutokana na janga la corona.
Jimbo la Tigray lilipuuza hatua ya serikali na kufanya uchaguzi wake.
Félix Verdejo: Bondia ashtakiwa kwa kumuua mpenzi wake mjamzito

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Bw. Verdejo (kulia) alipigana katika Olimpiki ya mwaka 2012 Bondia wa Puerto Rico aliyepigana katika michezo ya Olimpiki ya London mwaka 2012 ameshtakiwa kwa kumteka na kumuua mpenzi wake aliyekuwa mjamzito.
Félix Verdejo anatuhumiwa kwa kumshambulia na kumuua Keishla Rodríguez kisha kuutupa mwili wake chini ya daraja karibu na San Juan,mji mkuu wa eneo hilo la kisiwani lilipo chini ya himaya ya Marekani.
Alijisalimisha kwa polisi siku ya Jumapili baada ya kukataa kushirikiana na wachunguzi, polisi imesema.
Kifo hicho kiibua maandamano kupinga mauji dhidi ya wanawake huko Puerto Rico.
Mwezi Januari, kisiwa hicho kilitangaza hali ya hatari kufuatia dhulma dhidi ya wanawake. Puerto Rico huripoti angala kisa kimoja cha mauji ya mwanamke kila wiki, kwa mujibu wa kundi la kutetea haki nchini, huku visa vingine 60 vy auhalifu wa aina hiyo vikiripotiwa mwaka jana.
Bondia huyo mwenye umri wa miaka 27- anakabiliwa na mashtaka ya utekaji, wizi wa gari ulisababisha kifo na kuua kwa kukusudia mtoto ambaye hajazaliwa.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan awasili Kenya

Chanzo cha picha, Wizara ya Mambo ya Nje Tanzania
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasili nchini Kenya kwa ziara rasmi ya ya siku mbili.
Ziara hii ya rais Samia ni muendelezo wa jitihada za nchi hizo mbili kuboresha na kuendeleza uhusiano wa muda mrefu na itakuwa ndio ziara ya pili nje ya taifa lake kwa rais Samia tangu alipochukua madaraka kutoka kwa hayati Dkt John Magufuli.
Rais Samia anatarajia atafanya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Uhuru Kenyatta kisha atalihutubia Bunge la Kenya litakalojumuisha Wabunge wa Mabunge yote mawili.

Chanzo cha picha, Wizara ya Mambo ya Nje Tanzania
Aidha, Rais Samia atahudhuria na kuhutubia mkutano wa jukwaa la wafanyabiashara wa Kenya na Tanzania utakaofanyika jijini Nairobi.
Alifanya safari yake ya kwanza akiwa Rais nchini Uganda mnamo Aprili 11 na Rais Yoweri Museveni akielezea kuwa lengo la ziara yake ni kuimarisha uhusiano wa nchi mbili na kumaliza makubaliano ya mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka nchini Uganda
Rais huyo ameonekana kutopendelea kulinganishwa na Magufuli na amewashutumu wabunge wa Tanzania kwa kufanya hivyo.
Soma zaidi:
- Rais Samia kuzuru Kenya: Biashara, Diplomasia na Jumuiya ya Afrika mashariki kupewa kipaumbele
- Samia Suluhu Hassan: Rais mpya anayekabiliana na dhana ya kutokuwepo kwa corona Tanzania
Hujambo na karibu katika matangazo mubashara leo Jumanne 04.05.2021.

