‘Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania akubali kukutana na chama cha upinzani Chadema’

Katibu Mkuu wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Chadema John Mnyika ametangaza kuwa ombi la kukutana na rais wa nchi hiyo Samia Suluhu Hassan limekubaliwa.

Moja kwa moja

Abdalla Seif Dzungu

  1. Na hapo tumefika mwisho wa taarifa zetu za moja kwa moja hii leo, kesho tena panapo majaaliwa

  2. Sudan Kusini kuharibu dozi 60,000 za Covid-19

    Meneja wa Matukio ya Covid-19 nchini humo Richard Laku amesema serikali haitatumia chanjo 60,000 na itaziharibu.

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Wizara ya afya ya Sudan Kusini imekataa ushauri kutoka kwa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) la kutoharibu chanjo ya Oxford-AstraZeneca iliyopitwa na muda wake wa matumizi.

    Meneja wa Matukio ya Covid-19 nchini humo Richard Laku amesema serikali haitatumia chanjo 60,000 na itaziharibu.

    WHO imeziuliza serikali kusubiri mwongozo wake ikibaini kuwa chanjo hizo zinaweza kutumika hadi miezi 36 baada ya utengenezaji.

    Dk Laku alisema msimamo wa serikali ni kwamba "dozi hizo za chanjo hazitatumika, lakini hakuna cha budi ila kuziharibu ."

    Afisa wa Matayarisho na Udhibiti wa Afya wa Kimataifa wa WHO nchini humo Wamala Joseph Francis alisema kulikuwa na utaratibu kwa shirika hilo kuwafikia watengenezaji kwa mwongozo.

    "Wakati hali kama hii inatokea kwa bidhaa ya thamani kama chanjo hii ya Covid, kawaida tunamfikia mtengenezaji na kumpa sampuli - ili mtengenezaji aweze kufanya majaribio ya ziada na aamue kwa muda gani chanjo itakaa sawa - kwa hivyo hiyo itaamua kipindi cha kuongeza tarehe ya kumalizika muda wa matumizi, ”Dk Francis alisema.

  3. Mogadishu yaripotiwa kuwa shwari baada ya mapigano makali

    Mji wa Mogadishu umeripotiwa kuwa shwari baada ya mapigano makali

    Chanzo cha picha, Reuters

    Mji Mkuu wa Somalia, Mogadishu, Jumatatu hii umekuwa shwari baada ya mapigano kati ya wanaounga mkono upinzani na vikosi vya usalama vya serikali, Redio binafsi ya Risala imeripoti.

    ''Hali katika maeneo yaliyotokea mapigano yamekuwa shwari hii leo na watu walionekana wakitembea katika maeneo yao ya kazi na wengine walitoka kwa ajili ya kutathimini hali ilivyo,'' tovuti ya Redio ya Risala imeeleza.

    Mapigano makali kati ya wapiganaji watiifu wa upinzani na vikosi vya usalama vya serikali vilizuka siku ya Jumapili.

  4. Waganda washeherekea ushindi wa Kaluuya wa tuzo ya Oscar

    Raia wa uganda mitandaoni wamemshangilia muigizaji Kiingereza Daniel Kaluuya mwenye asili ya Uganda baada ya kushinda tuzo ya Oscar.

    Bw. Kaluuya alishinda tuzo ya mhusika msaidizi katika filamu ya Judas and the Black Messiah.

    Akitoa shukrani alisema anawashukuru mashabiki wake wa Londo na Kampala.

    Mama yake raia wa Uganda aliyekuwa ameketi miongoni mwa hadhira pia alimtambua kuwa na machango mkubwa katika kazi yake.

    Waganda wamempongeza kwa ushindi wake:

    ''Hongera Kaluuya . Mara zote umekuwa ukijivunia asili yako na nchi yako inajivunia wewe .

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  5. ‘Rais Samia akubali kukutana na Chadema’

    Katibu Mkuu wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Chadema John Mnyika ametangaza kuwa ombi lao la kukutana na rais wa nchi hiyo Samia Suluhu Hassan limekubaliwa.

    Kwa kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter, Mnyika ameeleza kuwa majibu ya ombi lililotumwa na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe waliyapokea Aprili 20.

    “...Rais amekubali kukutana na kushauriana na Chadema. Tunasubiri kujulishwa tarehe ya kukutana,” ameandika Mnyika katika ukurasa wake wa Twitter.

    Siku ya Alhamisi wiki iliyopita wakati akilihutubia Bunge kwa mara ya kwanza, Rais Samia alieleza azma yake ya kutaka kukutana na viongozi wa vyama vya siasa.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  6. Mradi wa gesi Msumbiji: Total yasitisha shughuli zake katika vitalu vya gesi baada ya mashambulizi

    Attacks by Islamist militants have killed thousands and displaced hundreds of thousands of people in northern Mozambique

    Chanzo cha picha, AFP

    Kampuni kubwa ya nishati ya Ufaransa Total imesimamisha shughuli katika eneo la uwanja mkubwa wa gesi kaskazini mwa Msumbiji wiki kadhaa baada ya wanamgambo wa Kiislamu kushambulia mji ulio karibu.

    Kampuni hiyo ilisema kwamba ilikuwa ikiondoa wafanyikazi wake wote kwa sababu ya hali ya usalama "inayoendelea kubadilika ".

    Makumi ya watu waliuawa katika shambulizi la mwezi Machi.

    Wanamgambo wanaohusishwa na kundi la Islamic State (IS) ndio wanaosababisha mzozo katika eneo hilo lenye Waislamu wengi.

    Wakati wa shambulizi la mwezi Machi tarehe 24 wafanyikazi na wenyeji walitafuta hifadhi katika Hoteli ya Amarula Palma na baadaye wakasimulia visa vya kutisha kuhusu shambulizi hilo

    Mwaka jana Total ilianzishaa mradi wa kuyeyusha gesi wa - $ 20bn (£ 14.6bn) - ambao, ukikamilika, utakuwa hifadhi ya pili ya gesi kwa ukubwa barani Afrika.

    Uasi huo wa miaka minne katika mkoa wa Cabo Delgado umeacha zaidi ya watu 2,500 wakiwa wamekufa na 700,000 wakikimbia makazi yao tangu uasi huo uanze mwaka 2017.

    Rais Felipe Nyusi ameahidi kurejesha amani katika eneo hilo.

  7. Kenya haifungi kambi za wakimbizi za Dadaab na Kakuma –Mkuu wa UNHCR

    Kamishna wa UNHCR Filippo Grand (Kushoto) akiwa ziaani nchini Rwanda

    Serikali ya Kenya haifungi kambi za wakimbizi za Dadaab na Kakuma lakini inataka suluhisho, kamishna mkuu wa shirika la wakimbizi laumoja wa mataifa amesema.

    Filippo Grandi anatembelea DR Congo, Rwanda na Burundi, ili kufahamu shida ambazo zinawakabili wakimbizi katika maeneo hayo.

    Mwezi uliopita, Kenya ilitoa makataa ya siku 14 ya kufungwa kambi za Dadaab na Kakuma, ikitoa sababu za hifu ya usalama wa kitaifa, na wizara ya mambo ya ndani ilikuwa imesema "hakuna nafasi ya mazungumzo zaidi".

    Nchini Rwanda Jumapili, Bwana Grandi aliwaambia waandishi wa habari kwamba "wamekuwa na mazungumzo mazuri sana na serikali ya Kenya".

    "Serikali ya Kenya haifungi kambi hizo, serikali ya Kenya inataka kupata suluhisho, wanataka kujua ni ipi njia bora ya kusonga mbele." Bwana Grandi alisema.

    Shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa limewasilisha kwa Kenya mipango ya baadaye ya kambi hizo mbili, pia alifichua .

    "Nadhani serikali ya Kenya itaendelea kutoa makazi… lakini inaeleweka wanataka kuwa na mkakati wa siku zijazo na mazungumzo yanaendelea."

    Mnamo Aprili, mahakama kuu ya Kenya imeripotiwa kuzuia kwa muda kufungwa kwa kambi hizo mbili za wakimbizi ambazo zinahifadhi zaidi ya watu 400,000.

  8. Idadi ya vifo kutokana na ghasia za Amhara huenda ikafikia 200

    ghasia zinazoendelea Ethiopia

    Chanzo cha picha, Reuters

    Ofisi ya afisa mkuu anayesikiliza malalamishi ya umma Ombudsman nchini Ethiopia inasema kwamba idadi ya watu waliouawa katika ghasia kati ya makabila mawili makubwa huenda imefikia watu 200.

    Ripoti za awali zilisema kwamba takriban watu 50 walifariki katika mapigano kati ya watu wa makabila ya Amharana Oromo katika jimbo la kaskazini la Amhara.

    Ofisi hiyo inasema kuwa Endale Haile alisema kwamba takriban watu 330,000 wamewachwa bila makao na ghasia hizo.

    Alisema kwamba takriban robô ya nyumba hizo katika mji wa Ataye zilikuwa zimechomwa.

    Sehemu kubwa ya vita hivyo vimefanyika katika eneo moja lililopo katika eneo la kabila la Amhara ambalo lina raia wengi wa kabila la Oromo.

    Mapema wiki hii, Ethiopia ilitangaza hali ya tahadhari katika maeneo ya jimbo hilo.

    Masuali yanaulizwa kuhusu iwapo uchaguzi unaotarajiwa mwezi Juni utafanyika.

    Maeneo kadhaa ya taifa yanakumbwa na ghasia hususan eneo la Kaskazini la Tigray ambalo limekuwa katika vita kwa kipindi cha miezi sita iliopita.

  9. Vikosi vya usalama Somalia vyapigana kuhusu muhula wa Farmajo

    vikosi vya usalama somalia

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, vikosi vya usalama Somalia

    Mapigano yamezuka katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu kati ya makundi kinzani ya vikosi vya usalama.

    Ripoti zinasema kwamba silaha kali zilitumika huku makombora yakirushwa karibu na kasri la rais.

    Baadhi ya vikosi hivyo vinamuunga rais Mohammed Abdaullahi Mohammedhuku vingine vikimpinga.

    Wiki iliopita bwana Mohammed anayejulikana kama Farmajo kwa utata alijiongezea muda wake ofisini.

    Muhula wake uliisha rasmi mwezi Februari.

    Hatua hiyo ilikosolewa naj amii ya kimataifa ikiwemo Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.

    Ripoti kutoka Mogadishu siku ya Jumapili zilisema kwamba kile kilichoanza kama ghasia zilisambaa hadi katika maeneo mengine ya mji ikiwemo maeneo ya kati.

    Vyombo vya habari nchini humo vilisema kwamba mapigano yalikuwa kati ya vikosi vya serikali na vitengo vya usalama ambavyo vinaunga mkono upinzani.

    Lakini baadhi ya wababe wa kivitana viongozi wa koo mbalimbali wanahusishwa katika ghasia hizo.

  10. Natumai hujambo . Ni siku nyengine tena ambapo tutakupasha mubashara kuhusu yale yanayoendelea ulimwenguni.Usiende mbali